59. ELISHA ANAENDELEZA KAZI YA MUNGU
''Roho ya Eliya iko juu ya Elisha''
Shabaha
Kuonyesha jinsi Elisha alivyotiwa mfuta ili kuendeleza kazi ya kuongoza watu wa Mungu wa Israeli na Eliya akatwaliwa.
Katika somo la 8 tuliona jinsi Yezebeli alivyomchukia Eliya na hata akakusudia kumwua Eliya.Alikuwa amewaua baadhi ya manabii wakati wa ukame na wengi walijificha katika mapango ili Yezebeli asiwaone.(1 Wafalme 18:3-4,13).Kwa hiyo Mungu akamwambia Eliya arudi tena kuwatia moyo wanaume na wanawake waaminifu ambao walikuwa wamebakia Israeli,ili waweze kuwatayari kuwafundisha watu jinsi ya kumtumikia Mungu wa kweli na aliye hai.Hawa ''wana hao wa manabii'' kama walivyokuwa wakijulikana,walihitaji kiongozi.Eliya alikuwa amekuwa kiongozi lakini muda ukawa umefika kwa kijana kuchukua nafasi ya Eliya,mwana wa Shafati,kuwa nabii atakayefuata ili kuwaongoza watu.
1Wafalme 19:19-12; 2Wafalme 2:1-18
ELISHA ANACHAGULIWA:1Wafalme 19:19-21
Eliya akarudi Israeli ili kumtafuta Elisha, kama Mungu alivyomwagiza.Eliya alimkuta Elisha akilima shamba kwa kutumia ngo'ombe akiwa na watumishi wake.Ikawa Eliya alipopita mbele yake,akavua vazi lake nakuliweka juu ya Elisha.Huyu kijana alifahamu moja kwa moja maana ya kitendo kile-maana Eliya alikuwa akimwonyesha Elisha ili kwamba amfuate na aifanye kazi ya nabii wa Mungu ambayo alikuwa akiifanya. Ghfla Elisha akawaacha ng'ombe na kumkimbilia Eliya,ambaye alikuwa akiendelea kutembea.Elisha akasema “Nipe ruhusa, nakuomba, uniruhusu, nikambusu baba yangu na mama yangu, kisha mimi nitakufuata'' ( mstari 20).
Kwa hiyo Elisha akarudi akuchinja maksai (ng'ombe)wawili na akafanya sherehe na watu wote pale katika lake.Kazi yake ya kulima ilikuwa imekwisha. Na sasa alitakiwa amfuate Eliya ili ajifunze kwa bidii kuhusu kazi ya kuwafundisha watu wa Mungu.
ELIYA ANAONDOKA: 2Wafalme 2:1-7
Watu wawili wakawa marafiki wa karibu hasa.Kila mtu alikuwa amezoea kumwona Eliya akiwa na mtumishi , lakini muda wake ukawa umefika ambapo Eliya ni lazima achukuliwe. Ikawa walipokuwa wanaondoka Gilgali, Eliya akamwambia Elisha, Tafadhali, kaa hapa; maana BWANA amenituma niende mpaka Betheli. Elisha alifahamu kuwa siku hiyo Mungu atamtwaa Eliya naye alikuwa amekusudia kuwa ni lazima awe pamoja naye siku hiyo.''Kama BWANA aishivyo, na roho yako iishivyo, sitakuacha'' (mstari 2 ). Kwa muda ambao Elisha alikuwa akiishi, asingemwacha Eliya.
Kisha wote wawili wakashuka hadi Betheli.Basi ''wana wa manabii'' waliokuwako Betheli wakaja kuonana na Elisha, wakamwambia, “Je/unajua kuwa BWANA atamwondoa bwana wako leo, asiwe mkubwa wako?” (mstari 3). Kwa masikitiko sana Elisha aliwajibu kuwa alikuwaanajua.''Naam, najua; nyamazeni''
Kisha BWANA akamtuma Eliya Yeriko.Eliya akamwambia Elisha abakie Betheli,lakini Elisha hakukubali kumwacha Eliya.Basi “wana wa manabii waliokuwako Yeriko pia hata ao walijua kuwa Eliya atatwaliwa siku hiyo. Elisha akajibu tena, “ninajua,nyamazeni”. Elisha hakutaka kuzungumza nao kuhusu jambo hili. Kisha Eliya akamwambia,BWANA amenituma, niende mpaka Yordani.Ndipo tena Elisha akamwambia Eliya,
“Kama BWANA aishivyo, na roho yako iishivyo, sitakuacha” (mstari 6). Ndipo wote wawili wakashuka katika mto Yordani,wakati huo watu hamsini wa “wana wa manabii” wakafika na wakawatazama kwa mbali ili kuona yatakayotokea (mstari ).
MUNGU ANAMTWAA ELIYA:2 Wafalme 2:8-11
Hata ikawa walipofika kwnye kindo za mto Yordani, ndipo Eliya “akalitwaa vazi lake la juu, akalikunja akayapiga maji” kwa kutumia vazi lile (mstari 8). Basi maji ya mto Yordani yakagawanyika huku na huku,na hao wawili wakavuka pakavu. Walipokwisha vuka hadi upande wa pili, ndipo Eliya akamgeukia Elisha na kumwambia, “Omba kwangu lolote utakalo nikutendee, kabla sijaondolewa kwako” ( mstari 9 )
Ndipo sasa Elisha akampenda sana Eliya kama vile kumpenda baba yake maana ilikuwa ni sheria katika Israeli kuwa mwana ambaye ni kifungua mimba ambaye anakuwa mkuu wa nyumba wakati baba yak anapofariki, “alipata mara mbili” au alipokea mali za baba yake mara mbili kuliko wana wengine.Ilikuwa ni ishara kuwa yeye ndiye mkuu mpya wa familia hiyo. Elisha alitaka kuendelea na kazi kubwa ya nabii,akiwa ni mkuu wa manabii wa Mungu.Kwa hiyo Elisha alimwambia Eliya, “Nakuomba mara ,sehemu maradufu ya roho yako na iwe juu yako” (mstari 9), Elisha hakuomba mara mbili ya nguvu alizokuwa nazo Eliya bali aweze kuwa ndiye wa kuchukua nafasi ya huyu nabii anayeondoka,ili kwamba kazi ya kuwafundisha watu wa Mungu iweze kufanikiwa. Hata hivyo hilo lilikuwa jambo ambalo asingeweza kulifanya.Alikuwa ameomba jambo gumu, ni Mungu peke yake ambaye angeweza kutenda jambo hilo.”Lakini, ukiniona nitakapoondolewa kwako, utalipata; la hukuniona, hulipati”.( mstari 10 ).
Kwa hiyo watu hawa wawili wakawa wakiendelea mbele huku wakiongea, ghafla, ''tazama / kukatokea gari la moto, na farasi wa moto, likawatenga wale wawili; naye Eliya akapanda mbinguni kwa upepo wa kisulisuli”. (mstari 11).
Elisha hakuweza kushangazwa, bali liyakumbuka maneno ya Eliya na akamwona akichukuliwa bele ya macho yake. “Akalia, akisema, Baba yangu, baba yangu, gari la Israeli na wapanda farasi wake!'' (mstari 12).
Mungu alimbariki Elisha kwa kumruhusu amwone bwana wake mpendwa alipokuwa akitwaliwa juu na upepo wa kisuli-suli na akaona gari la moto wakati malaika wa Mungu alipokwenda katikati yao nr kuwatenganisha.Basi Elisha asimwone Eliya tena kabisa.
ELISHA AKAWA MKUU WA MANABII:2Wafalme 2:12-15
Elisha akabakia peke yake ng'ambo ya Yordani.Ndipo akayashika mavazi yake akayararua vipande viwili.Na kisha akalichukua lile vazi la Eliya wakati alipokuwa akitwaliwa kwa upepo wa kisulisuli lililomwangukia Elisha.
Kumbuka jinsi Eliya alivyoliweka vazi lake juu ya Elisha alipokuwa akilima,ikiwa ni ishara kwamba atamfuata Eliya.Na akalichukua vazi hilo na akarudi tena kwenye kingo za mto.Ndipo akalikunja lile vazi la Eliya kama alivyomwona Eliya akifanya.Kisha akasema “Yuko wapi, BWANA, Mungu wa Eliya” (mstari 14).
Kisha maji yakagawanyika kama yalivyogawanyika wakati wa Eliya,na Elisha akavuka pakiwa pakavu. Kwa hiyo Elisha akarudi Yeriko,sehemu aliyokutana na manabii.Walimwona wakati alipovuka.Walikuwa wamemwona alipovuka mto pakiwa pakavu ndipo wakaja kukutana naye..Wakainama mbele yake wakasema, “Roho ya Eliya iko juu ya Elisha” (mstari 15). Mungu alikuwa amesikia ombi la Elisha na akajibu sala yake.Maana alikuwa na uhakika, na “wana wa manabii” walikuwa na uhakika,kwamba Mungu amempatia roho ya Eliya mara mbili.
FUNDISHO KWETU
Basi “wana wa manabii” walikuwa ni wale wanaume waaminifu katika Israeli waliokuwa wamejifunza sheria ya Mungu na waliwaonyesha wenzao jinsi ya kumwabudu Mungu wa Kweli na aliye hai.Tunapaswa kuwa kama wao.Tunapaswa kujifunza neno la Mungu kila siku na kufanya yale Mungu anayotaka sisi tutende.Kama tunalipenda neno la Mungu tutaweza kuwa na umoja na wale wote anaoipenda ile Kweli.Tunakuwa na bidii kujifunza kutoka kwa wale wanaofundisha Kweli kwa uaminifu.
MASWALI
Majibu Mafupi.
1. Katika siku za Eliya,vikundi vya wanaume waaminifu katika Israeli waliitwaje?
2. Elisha alikuwa akifanya nini wakati Eliya alipomwona ?
3. Eliya alifanya nini alipomwona Elisha kwa mara ya kwanza?
4. Ni kwa nini Elisha alikuwa na huzuni alipokuwa akimfuata Eliya Betheli na Yeriko na kisha Yordani?
5.Ni mwujiza gani wa kushangaza alioufanya alipofika mto Yordani ?
6. Elisha alimwomba Eliya ampe nini kabla Eliya hajachukuliwa ?
7. Ni kitu gani kilichokuja katikati ya Eliya na Elisha walipokuwa wanatembea ng'ambo ya Yordani?
8. Ni kwa namna gani Eliya alitwaliwa?
9 Elisha alilia ninialipomwona Eliya akitwaliwa?
10. Elisha aliwezaje kuvuka kurudi upande wa pili wa Yordani?
11. Elisha alisema nini alipoyapiga maji ya Yordani?
12. ''Wana wa manabii'' walipomwona Elisha anarudi walisemaje?
Majibu ya Kina
13. Eleza ni kwa njia gani Eliya alimchagua Elisha amfuate;
14. Eleza kilichotokea wakati Eliya na Elisha walipoondoka Gilgali pamoja na ni jinsi gani
walivuka Yordani pamoja?
15. Elezea jinsi Eliya alivyochukuliwa kwenda mbinguni
Majibu ya Nyongeza
16.(a) Watu hawa wawili walipovuka mto Yordani Elisha alimwomba Eliya nini ?
(b) Elisha aliomba apewe nini?
(c) Je!ni kwa njia gani ''wana wa manabii'' walifahamu kuwa roho ya Eliya iko juu ya Elisha ?