60. ELISHA NA MWANAMKE WA SHUNEMU
''Panapo wakati huu mwakani ,utamkumbatia mwana''
Shabaha
Nikuonyesha jinsi Mungu alivyombariki mwanamke wa Shunemu ambaye kwa upendo alimtunza Elisha. Elisha alikuwa akisafiri ktika nchi yote ya Ufalme wa kaskazini wa Israeli,akiwafundisha watu na akitenda miujiza mingi.Siyo tu kwamba miujiza yake ilikuwa ni kuwaonyesha Israeli ukuu wa Mungu wa Elisha,bali pia miujiza hyo iliwafundisha mafundisho ya ajabu ambayo yaliimarisha imani yao.Katika somo hili Elisha lionyesha kuwa hakuna lisilowezekana kwa Mungu-Mungu aliweza hata kuwafufua watu waliokuwa wamefariki. 2Wafalme 4:8-37
IMANI NA WEMA VINAPEWA THAWABU:2Wafalme 4:8-17
Basi Elisha kila alipokuwa akisafiri mji hadi mji alikuwa akipitia Shunemu. Siku moja mwanake mmoja tajiri aliyekuwa anaishi huko akamkaribisha Elisha ili ale chakula na apumzike (ajipumzishe). Kuanzia wkati huo na kuendelea, ikiwa kila mara Elisha alipopita, mwanamke huyu alimsihi aingie nyumbani kwake ili ashiriki chakula pamoja na mme wake.Huyu mwanamke alimtambua Elisha kuwa “ni mtu mtakatifu wa Mungu” na alijadiliana na mme wake kuhusu mpango aliokuwa nao wa kumjengea yule mtu wa Mungu chumba kidogo, kwa kuwa mara kwa mara hupita njia ile. Akamwambia mme wake, “Nakuomba tumfanyie chumba kidogo ukutani; na ndani yake tumwekee kitanda, na meza, na kiti, na mshumaa” (yaani kinara cha taa). Siyo kuwa ni wazo baya, bali ni chumba kidogo tu ambacho kitakuwa na vitu mhimu anavyohitaji. Hatimaye chumba kikawa kimekamilika na nabii akafurahi sana kila alipokuwa akisrfiri alipofika pale alipumzika pale.
Elisha alifurahi sana. Alimwita mwanamke huyu wa Shunemu akamwuliza nikutendee nini kwa ajili ya wema wako. Hata hivyo yule mwanamke alikuwa ametosheka na vitu. Hakuhitaji aina yoyote ya cheo ambayo yule mwanamke angepewa, kwa kuwa yeye alifurahia san kumsaidia nabii wa Mungu. Kwa hiyo Elisha akamwambia Gehazi, mtumishi wake, “Basi, atendewe nini mwanamke huyu?” ( mstari 14 )
Gehazi alifahamu kuwa kulikuwa na kitu kimoja tu ambacho yule mwanamke mwema alikuwa hana na kama angekipata angekuwa na furaha iliyo kamili. Akasema, “Hana mwana na mumewe ni mzee”
Ndipo mara moja Elisha alijua lipi lifanyike. Yule mwanamke hakuwa mwema tu bali alikuwa mwanamke mwaminifu pia, ambaye alipenda kumhudumia nabii wa Mungu. Elisha alimwita akamwambia kuwa Mungu atakupatia mwana. Na kwa kweli hili lilikuwa ni hitaji la moyo wake,lakini kwa shida aliweza kuamini kama kweli itafanyika hivyo. Yule alisema kwa kusisitiza, La!, bwana wangu, usimwambie mjakazi wako uongo”( mstari 16 ). Lakini kama Elisha alivyokuwa asema, muda ukafika akazaa mtoto wa kiume. Thawabu hii bila shaka ilikuwa ya thamani sana kuliko ule wema aliomtendea nabii, lakini Mungu alijua kwamba moyo wake ulikuwa ni mwaminifu; kwa hiyo Mungu akambariki yule mwanamke.
FURAHA YAKE INAGEUKA KUWA HUZUNI:2Wafalme 4:8-17
Kijana huyo wa kiume alipendwa sana. Alipokua ilikuwa desturi yake kumfuata baba yake shambani. Siku moja alienda shambani akiwa pamoja na wavunaji, ghdfla akajisikia kuumwa akamwambia baba yake, “Kichwa changu, kichwa changu!” Baba yake alikuwa na kazi ya kuvuna akamwagiza mtumishi wake ampeleke kijana kwa mama yake.Mama yake akamweka yule kijana magotini kwake akiendelea kumhudumia, hali ya afya ya kijana ikawa mbaya sana, kisha ilipofika mchana saa sita akafariki.
Akamchukua kijana wake wa kiume akapanda juu, akamlaza kwenye kitanda katika chumba cha Elisha kisha akafunga mlango. Kisha yule mwanamke akamtumia mume wake ujumbe, akasema, “Tafadhari, uniletee mtu mmoja wa watumishi, na punda mmoja, ili nimwendee yule mtu wa Mungu kwa haraka, kisha nikarudi tena” (mstari 22). Yule mwanaume alishtushwa sana; lilikuwa ni tukio ambalo kamwe hakulitegemea. Bado hakuweza kutambua, kama mtoto wake amefariki. Mke wake alisema kwa ufupi tu, “Siyo neon” (mstari 23)
Akatandika punda, akamwambia mtumishi wake, mwendeshe kwa kasi sana kuelekea Mlima Karmeli. Na alipokaribia, Elisha akamwona kwa mbali yule mwanamke akija akamtuma Gehazi kwenda kumlaki ili amwulize kama wote hawajambo. Alipomwuliza mwanamke kama wote hawajambo, naye alijibu, “kuwa wote hawajambo”, lakini hakunyamaza wala hakusema mpaka alipomfikia Elisha. Akaanguka chini na kushika miguu ya Elisha, lakini Gehazi akajaribu ili amwondoe. Elisha akamwambia Gehazi mwache.Elisha akasema kuna jambo ambalo limetokea lisilo kuwa la kawaida.
Huyu mwanamke masikini alikuwa amefiwa na msaada wa haraka wa Elisha ulihitajika. Mungu alikuwa hakumjulisha Elisha tatizo la yule mwanamke.
Na hatimaye yule mwanamke akafichua uchungu wake, “Je/naliomba mwans kws bwana wangu? Mimi sikusema, Usinidnganye?” (mstari 28). Ghafla Elisha aklifahamu tatizo la yule mwanamke. Yule kijana wa kiume amefariki. Elisha akampatia fimbo yake Gehazi na akimbie haraka kenda nyumbani kwa yule mwanamke wa Shunemu. Gehazi alitakiwa akimbie na wala asisimame njiani wala asimsalimie mtu yeyote.Na kisha ilikuwa ni lazima aiweke fimbo ya Elisha juu ya uso wa mtoto.
Elisha alitazamia kuwa yule mwanamke wa Shunemu atamfuata mtumishi wa Elisha, lakini yule mwanamke hakukubali kumwacha Elisha. Maana alifahamu kuwa nguvu za Mungu zilikuwa ndani yake.Elisha alikuwa ndiye aliyekuwa amefuatwa na yule mwanamke.
Kwa hiyo Elisha akainuka akaondoka pamoja na yule mwanamke.
ANAFUFUKA KUTOKA WAFU:2Wafalme 4:31-37
Gehazi alikimbia haraka akatangulia mbele na akafanya kama bwana wake alivyomwagiza, “wala hapakuwa na sauti walamajibu” (mstari 31)
Kwa hiyo Gehazi akarudi kwa Elisha akiwa na ujumbe, akasema. “Mtoto hakuamka”(mstari 31). Hatimaye Elisha akafika katika nyumba akapanda juu katika chumba chake ambapo alimkuta yule mtoto akiwa amelala kwenye kitanda chake. Gehazi alikuwa ameshindwa kumwamsha (kumfufua) mtoto; mtoto likuwa amekufa hakika.
Elisha alifunga mlango, akamwaacha nje Gehazi, mtumishi wake na mama wa mtoto. Alimwomba Mungu, maana alijua kuwayeye hana nguvu ambazo ni za kwake mwenyewe, bali ni Mungu mwenyewe peke yake anaweza kusaidia. Kisha akapanda kitandani kwake akalla juu ya mtoto, akaweka mdomo wake juu ya mdomo wa mtoto, akaweka macho yake juu ya macho ya mtoto, na akaweka mikono yake juu ya mikono ya mtoto.
Elisha alivyoendelea kumlalia yule mtoto, basi yule mtoto akapata joto. Elisha akaamka akaanza kutembea tembea mle chumbani. Kisha akarudi na kulala tena juu ya mtoto.Ghafla mtoto akapiga chafya mara saba na kishekafungu mcho yake!
Mungu alisikia maombi ya Elisha na akamrudishia uzima yule mtoto. Akawa hai kutoka katika wafu Elisha akamwambia Gehazi amwite mwanamke wa Shunemu. Ikawa mwanamke wa Shunemu alipoingia ndani ya chumba, Elisha akasema, “Mchukue mwana wako” (mstari 36).
Ghafla yule mwanamke nguvu zikamwishia akaanguka miguuni pa Elisha.Jishi alivyofurahi kwa ajili ya huu mwujiza wa pili wa kuwa kufufuka kwa mototo! Kabla ya kumchukua mwana wake, akainama mbele ya Elisha akashukuru na kumtukuza Mungu
FUNDISHO KWETU
Mungu haijali sana yote tunayoyatenda.Yeye anaijua mioyo yetu na atatupatia thawabu kutokana na uaminifu wetu.
Basi mwanamke wa Shunemu hakutegemea kupata thawabu yoyote. Yeye aliamua kumsaidia Elisha kwa sababu aliona ni manufaa kwake kumsaidia mtumishi wa Mungu.Mwanamke wa Shunemu alikuwa ameridhika na alikuwa na furaha.Ni lazima tuwe na tabia hiyo. Ni lazima tumtumikie Mungu kwa sababu tunampenda yeye na tunamshukuru kwa baraka zake anazotubariki kila siku.Haijalishi yal tuyatendayo ni machache vipi hatuwezi kupata uzima katika wafu, lakini Mungu atatupatia uzima wa milele kama tuna imani sawasawa na mwanamke wa Shunemu.
MASWALI
Majibu Mafupi
1. Yule mwanamke wa Shunemu alikuwa akimtendea nini Elisha?
2. Ni jinsi gani Mungu alivyompatia thawabu yule mwanamke wa Shunemu?
3. Siku moja ilitokea nini kwa mwana wa mwanamke wa Shunemu?
4. Mwana alipofariki mwanamke wa Shunemu alimweka wapi?
5. Mwanamke wa Shunemu alikwenda wapi mwana wake alipofariki?
6. Elisha alimwambia Gehazi afanye nini?
7. Ni habari gani Gehazi alimrudishia Elisha
8. Ni tendo gani mtoto alifanya alipokuwa amerudishwa tena kwenye uzima
9. Je!Mungu atatupatia nini ikiwa tutakuwa na tabia ya imani sawasawa na mwanamke wa Shunemu?
Majibu ya Kina
10. Eleza jinsi mwanamke wa Shunemu alivyoonyesha wema kwa Elisha, na jinsi Mungu Alivyombariki
11. (a) Mwanamke wa Shunemu alifanya nini mwana wake alipofariki?
(b) Ni kwa namna gani yule mwana alivyorudishwa tena katika uzima?