65. HEZEKIA-CHANGAMOTO KUTOKA ASHURU
''Nitaulinda mji huu ,niuokoe, kwa ajili yangu mwenyewe, na kwa jili ya
Daudi, mtumishi wangu''
Shabaha
Kuonyesha jinsi Hezekia alivyomwamini Mungu kuwa atokoa mji wa Yerusalemu kutokana na uvamizi wa Ashuru. Katika mwaka wa nne wa kutawala kwa Hezekia adui katili wa Israeli, Ashuru, vikosi vyao wakitokea kaskazini wakashuka na kwa muda wa miaka mitatu wakautwaa ufalme wa Israeli. Na huu ndiyo ukawa mwisho wa ufalme wa kaskazini.Katika kusini, wanaume wa Yuda waliogopa sana lakini Hezekia aliweza kuwarudisha nyuma askari wa Ashuru kwa muda kwa kuwaahidi kulipa kodi.
Hata hivyo Hezekia alifahamu kuwa hilo lisingedumu milele.Alitakiwa ajiandae yeye mwenyewe na watu wake wajiandae kwa ajili ya kupambana na uvamizi wa Ashuru.
2 Mambo ya Nyakati 32; 2 Wafalme18:13-16; 19
HEZEKIA ANALIPA KODI: 2 Wafalme 18:13-16
Katika mwaka kumi na nne wa kutawala kwake Hezekia, Senakeribu, mfalme wa Ashuru, akaazimia kuvamia kusini dhidi ya ufalme wa Yuda na akaushinda. Akaitwaa miji Yuda mmoja baada mmoja na Hezekia alitambua kuwa mji wa Yerusalemu ulikuwa katika hatari kubwa ya kutwaliwa. Akamtumia waraka mfalme wa Ashuru ambaye alikuwa katika mji wa Lakishi uliokuwa mji mkuu, ambao ulikuwa kusini magharibi mwa Yerusalemu. Katika waraka huu Hezekia alimsihi Senakeribu arudi kwake asiingie Yerusalemu na kwamba atalipa chochote ambacho Senakeribu angehitaji.
Kodi ambayo Senakeribu aliihitaji ilikuwa ni talanta za fedha mia tatu na talanta za dhhabu thelathini.Ilikuwa ni mali nyingi .Njia peke ambayo Hezekia angefanya ilikuwa ni kuiondoa fedha yote iliyokuwa katika Hekalu la BWANA na kutoka katika hazina yake mwenyewe. Na kisha Hezekia akaiondoa dhahabu juu ya milango na kwenye nguzo za Hekalu. Ilikuwa ni huzuni iliyoje siku hiyo katika Yerusalemu, lakini hata hivyo ilimpatia muda Hezekia kuweza kuimarisha mji na kuwaandaa watu kwa vita
HEZEKIA ANAJIANDAA KWA VITA: 2 Mambo ya Nyakati 32:1-8
Wakati huu Hezekia alikuwa amemaliza kuukarabati ukuta. Baadhi ya nyumba katika mji zilibomolewa ili mawe yatumike kuuimarisha ukuta na pia kwa kujengea mnara(Isaya 22:10).
Maadui waliuzingira mji wakati mji ulipokuwa umebomolewa, na hakuna mtu aliyeweza kutoka au kuingia. Kwa hiyo ilikuwa ni lazima mji kuwa na maji mengi sana. Nje kidogo ya mji wa Yerusalemu upande wa mashariki kulikuwa na chemchemi ya mto ulioitwa Gihoni.
Mfalme Hezekia kakutana na wakuu na watu mashujaa wa vita kubuni mpango aliokuwa nao wa kuyaleta maji haya ndani ya mji.Ndipo watu wengi wakafanya kazi ya uchimba mfereji kuanzia kwenye chemchemi ya maji na wakapitisha maji chini ya mwamba hadi katika birika (kisima) ndani ya mji. Kisha wakawa wameizuia chemchemi ile ya maji nje ya mji ili maaskari wa Ashuru wakija wasiyaone maji. Walisema, “Kwa nini, wakifika wafalme wa Ashuru, waone maji mengi?” (mstari 4).
Na wengine walikuwa wakitengeneza siraha na ngao. Hezekia akafanya juhudi zote nzuri kabisa za kuuweka mji na kuwaandaa watu wake kwa jili ya vita na jeshi la Ashuru. Mfalme Hezekia alijua, hata hivyo, aliwaambia watu wasipomwamini Mungu, maandalizi hayo yote waliyokuwa wameyafanya yangekuwa bure. Alipokuwa amewateua wakuu (maakida) wa jeshi lake, aliwata na akawatia moyo. “Iweni hodari, na wa moyo mkuu, msiogope, wa msifadhaike kwa sababu ya mfalme wa Ashuru, wala kwa majeshi yote walio pamoja naye; kwa maana yupo mkuu pamoja nasi kuliko aliye pamoja naye; kwake upo mkono wa mwili; ila kwetu yupo BWANA, Mungu wetu kutusaidia, na kutupigania mapigano yetu.” (mstari 7,8).
Mfalme aliongea kwa ujasiri sana na wakuu wa jeshi lake wakamwamini na wakafurahishwa mioyo yategemea maneno yake.
ASHURU WANAKUJA YERUSALEMU: 2 Mambo ya Nyakati 32:9:20
Wakati ieshi la Ashuru walipokwisha iteka Lakishi, Senakeribu akatuma watumishi wake watatu kwenda Yerusalemu, wakiwa na jeshi kubwa. Walikwenda kuwadhoofisha watu ambao tayari walikuwa wameshaogopa jeshi la Ashuru. Akiwa amesimama karibu sana na mahali ambapo Hezekia aliyazuia chemchemi ya maji, Rabshake, mkuu kati ya hao waliotumwa, alianza kusema kwa sauti kuu kwa kiburi akamtukana mfalme na wenyeji wa mji.Akasema, “Senakeribu, mfalme wa Ashuru, asema hivi mwatumainia nini” (mstari10).
Labda walikuwa wakiitumainia Misri, na kama ndivyo, Misri ilikuwa kama fimbo ya mwanzi; Misri isingeweza kuwasaidia. Yamkini walimtumani BWANA, Mungu wa Israeli; lakini hakuna miungu ya mataifa iliyoweza kuwaokoa watu wao na mfalme mkuu wa Ashuru. “Ni nani miongoni mwa miungu ya mataifa wale walioharibiwa kabisa na baba zangu, aliyeweza kuwaokoa watu wake na mkono wangu, hata Mungu aweze kuokoa ninyi na mkono wangu?” (mstari 14). Kwa hiyo Rabshake akamkufuru BWANA, Mungu wa Israeli, lakini katika hili kwa kweli alikosea kabisa. Maana miungu ya mataifa yote haikuwa kitu chochote. Zilikuwa ni sanamu tu; hazikuwa na uwezo wa kusaidia. Lakini, Munngu wa Israeli alikuwa ni Mungu aliye hai.Munngu wa Israeli aliyasikia maneno haya ya kufuru na akawa tayari kutumia nguvu zake kumpiga mfalme wa Ashuru.
Wakati huo jeshi la Ashuru walipokuwa wanajivuna kwa namna hiyo,watu waliokuwa katika Yerusalemu walikuwa wamenyikia ndani kwa hofu wakiangalia yanayotendeka. Rabshake akapaza sauti kuu kwa lugha ya Kiebrania ili watu wote waliokuwa wanasikiliza wajue alikuwa na maanisha nini. Akamsema, “Munguu wa Yerusalemu, kana kwamba kuitaja miungu ya mataifa wa nchi, iliyo kazi mikono ya watu” (mstari 19).
MAOMBI YA HEZEKIA YA MSAADA: 2 Wafalme 19:1-7
Wakati Hezekia mfalme, aliposikia maneno hayo, alizirarua nguo zake akaingia katika nyumba ya BWANA kuomba. Akamtumia ujumbe Isaya nabii, akamwomba aombe kwa ajili ya watu wake. Isaya akamrudishia ujumbe wa maneno ya faraja: “Usiyaogope maneno hayo uliyoyasikia” (mstari 6). Mungu alikuwa anakwenda kumrudisha Senakeribu: “Naye...na kuirudia nchi yake mwenyewe; nami nitamwangusha kwa upanga katika nchi yake mwenyewe” (mstari 7)
WARAKA KUTOKA KWA RABSHAKE: 2 Wafalme 19:14-19
Ndipo baada ya haya Rabshake akaondoka na kwenda kwa Senakeribu na kwa maaskari wa Ashuru waliokuwa wamebakia huko. Hata, alipoondoka watu Yerusalemu walitarajia kupata ahueni kidogo badala yake alimwandikia mfalme Hezekia waraka wa kutisha sana, akimtukana Mungu wa Israeli. Wakati huu Hezekia akaingia na ule waraka katika nyumba ya BWANA, akaukunjua mbele ya BWANA, akaomba. “Ee BWANA, Mungu wetu, utuokoe na mkono wake, nakusihi, ili kwamba falme zote za dunia zipate kujua ya kuwa wewe ndiwe BWANA Mungu, wewe peke yako.” (mstari 19)
KIBURI CHA ASHURU CHA ANGAMIZWA:2Wafalme 19:32-37
Mungu akayasikia maombi ya Hezekia, akalituma neno kwake kupitia kwa nabii Isaya kuhusu mfalme wa Ashuru. “Yeye hatauingia mji huu, wala hatapiga mshale hapa... Njia ile ile aliyojia, kwa njia hiyo hiyo atarudi zake, wala hataingi ndani ya mji huu, asema BWANA. Maana nitaulinda mji huu, niuokoe, kwa ajili yangu mwenyewe, na kwa jili ya Daudi, mtumishi wangu” (mstari 32-34)
Jinsi Mungu alivyomwaminifu kwa wale wanaompenda.Aliuchagua mji huu kuliweka Jina lake hapo. Israeli wamekuwa walitukanisha jina lake kwa ajili ya maovu yao, lakini alikuwepo mfalme wa Yuda ambaye alipenda na kuliheshimu jina la Mungu na alichukia sana alipowasikia maadui wa Mungu wakilikufuru jina lake. Hata ikawa usiku huo huo malaika wa Mungu akatoka, akaingia kambi ya maaskari wa Ashuru akawaua kati yao maaskari mia moja na themanini na tano elfu.Asubuhi na mapema wengine walipoamka, kumbe! hao walikuwa wamekufa. Mungu alitenda kitendo ambacho Hezekia na jeshi lake hawakuwakuwa na nguvu wala uwezo wa kukifanya.Kwa pigo moja tu Mungu akkishusha kiburi cha taifa hili hodari na lenye nguvu.
Senakeribu mwenyewe hakufa wakati huu. Akarudi katikanchi yake kama Isaya alivyokuwa ametabiri (2 Wafalme 19:7) na hatimaye wana wake wawili wakamwua, alipokuwa akiabudu mungu wake.
Habari ya ushindi huu wa BWANA kulipiga jeshi la Ashuru zikaenea haraka sana na mataifa yaliyo pakana na Yuda yakaletea zawadi za shukrani kwa sababu ya mwujiza huu mkuu (2 Mambo ya Nyakati 32:23).
FUNDISHO KWETU
Fundisho hili linaonyesha kuwa Hezekia ni mfano mzuri wa kielezo cha imani. Hezekia aliamwamini kwamba BWANA ni Mungu aliye hai na kuwa anaweza yote.Alimwomba Mungu msaada, kwa sababu alijua kuwa Mungu atasikia maombi ya mtu mwaminifu na mnyenyekevu.Yeye mwenyewe alijiandaa kukabilianana na maadui uso kwa uso na akawahimiza watu wake waweke tumaini lao kwa Mungu. Na pia aliupenda mji wa Sayuni (Yerusalemu) na Zaburi 125, ambayo kuna uwezekano ni Hezekia ndiye aliyeiandika, inatufundisha kumtumaini BWANA na kuipenda Yerusalemu, mji wake aliouchagua.
“Wamtumainio BWANA ni kama mlima Sayuni, ambao hautatikisika, wakaa milele. Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, ndivyo BWANA anavyowazunguka watu wake, tangu sasa na hata milele”
MASWALI
Majibu Mafupi
1. Ni nani alituma majeshi kuipiga Israeli?
2. Ili mfalme wa Ashuru arude wake Hezekia alimlipa nini?
3. Ni jinsi gani Hezekia alivyohakikisha kuwa wanakuwa na maji ya kutosha katika mji?
4. Ni nani aliyepigana upande wa Hezekia?
5. Ni kwa nini miungu ya mataifa haikuweza kuwaokoa watu kutoka katika mkono wa Waashuru?
6. Je Rabshake alimdhania BWANA kuwa ni nani?
7. Hezekia alifanya nini aliposoma waraka kutoka shuru?
8. Ni kwa ajili ya nani Mungu aliuokoa Yerusalemu?
9. Ni nani aliye waua Waashuru?
10. Je Senakeribu aliuawa vipi?
Majibu ya Kina
11. Eleza jinsi Hezekia alivyounda Yerusalemu na kuwatayarisha watu kwa vita
12. Eleza jinsi Rabshake alivyokuja na kuwahofisha mioyo watu wa Yerusalemu
13. (a)Mungu alisema atafanya nini wakati Senakeribu alipokuja kuipiga Yerusalemu?
(b) Majeshi ya Ashuru yaliangamizwaje?