CSSA 1-3-16 - JOSIAH'S STAND FOR THE TRUTH

Swahili

66. YOSIA ANAISIMAMIA KWELI

''Nitaleta mabaya juu ya mahali hapa...wala macho yako hayataona mabaya yote nitakayoyaleta''

 

Shabaha

Kuonyesha jinsi Yosia alivyosimama imara kumfuata BWANA katika maisha yake yote na akajaribu kuwahimiza watu wake wamtumikie Mungu kama alivyofanya yeye.

 

Mfalme Hezekia alikuwa amefariki na Yuda wakabakia katika mikono ya mwana wake, Manase, mfalme mwovu. Mfalme huyu mwovu alikusudia kutofuata kazi njema ambayo Hezekia alikuwa imeifanya ya kuigeuza mioyo ya watu kumgeukia Mungu.Akamjengea Baali madhabahu, akaliabudu jua, mwezi na nyota; hata akajenga madhabahu katika nyumba ya BWANA katika Yerusalemu; na Manase akafanya hata mambo mengine ya kutisha kwa utawala wake wa muda mrefu wa miaka 55.

Na katika mwisho wa siku zake Manase akajinyenyekeza akajaribu kuzibadili njia zake, lakini alikuwa ameshafanya madhara mengi sana. Mwana wake, Amoni, akatawala baada yake naye akatenda mabaya sawasawan baba yake.Alitawala miaka miwili tu, akauawa na watumishi wake akiwa katika ikulu. Yuda walikuwa katika hali ya kusikitisha.

 

Walikuwa wamegeuka wakarudi nyuma wakamsahau Mungu wao. Walichokuwa wnahitaji sasa ni kumpata mtawala mwenye busara ambye atawarejesha kumwabudu BWANA Mungu aliye hai. Mfalme aliyefuata angekuwa ndiye ambaye angekuwa alikuwa wa haki, lakini kwa wakati huu alikuwa ni kijana kabisa.

 

2 Mambo ya Nyakati 34:1-19

 

YOSIA ANAANZA KUTAWALA: 2 Mambo ya Nyakati 34:17

Yosia akiwa kijana mdogo, alikuwa na umri wa miaka minane alipoanza kutawala, lakini alipokuwa na miaka kumi na sita tunaambiwa kwamba “alianza kumtafuta Mungu wa Daudi, baba yake” (mstari 3).

 

Inaonekana kama mama yake alikuwa ni mwalimu wake, mama yake alimlea Yosia ampende Mungu kwa kuwa Yosia “akaenda katika njia yote ya Daudi baba yake, wala hakugeuka upande wa kuume wala wa kushoto” (Wafalme 22:2). Na alipokuwa na umri wa miaka ishirini alianza kuisafisha nchi yote kwa kuondoa sanamu zote na wakazibomoa madhahu za mabaali. Akazivunjavunja na akazipondaponda kuwa mavumbi na akayamwaga mavumbi hayo juu ya makaburi ya manabii wa uongo. Alikwenda katika Yuda yote hadi katika miji yote iliyokuwaa imeizunguka Yuda, akazibomoa madhabahu na kuziponda ziponda sanamu mpaka alipokuwa amemaliza sanamu zote. Watu walifurahishwa na juhudi yake ya kulirudisha taifa kwa Mungu.

 

YEREMIA ANATABIRI: Yeremia1:14-16

Ni karibu na wakati huo huo, wakati watu wa Yuda walipokuwa wanamsaidia mfalme kijana wao kuzivunjavuja sanamu na kubomoa madhbahu ya mabaali, Yeremia nabii alianza kufundisha. Alitabiri hukumu ya kutisha kutoka kaskazini ambayo Mungu angeileta juu ya watu wake. Kama vile Ashuru walivyokuja kutoka kaskazini katika siku za mfalme Hezekia, kwa hiyo mfalme wa Babeli angekuja na kuitwaa Yerusalemu kabisa. Hapa tunamwona Yosia akiweka mfano mzuri kwa watu na kwa hiari yao walimfuata. Hata hivyo, hali hiyo tu kwa bahati mbaya ilikuwa haitoshi. Watu walimtii mfalme kijana wao kwa sababu walimpenda na walifurahishwa na juhudi yake hiyo, lakini Mungu ajuaye mioyo ya wanadamu, alifahamu kuwaa mioyo yao ilikuwa mbali naye. Yeremia alisema, “Yuda hajanirudia mimi kwa moyo wake wote” (Yeremia 3:10)

 

YOSIA ANAITAKASA NYUMBA YA BWANA: 2 Mambo ya Nyakati 34:8-19

Yosia alikuwa akifanya bidii yote ili kumtumikia BWANA Mungu wake.Kisha alikusudia kukarabati nyumba ya BWANA. Maana Walawi walikwenda nchi wakakusanya fedha kwa watu ili zisaidae kazi ya ujenzi. Walichaguliwa watu wa kufanya kazi ya kukarabati, kazi ya ujenzi, kazi ya maseremala, waashi na walipewa fedha za kununulia mbao na mawe yaliyochongwa. Matumizi ya jinsi walivyonunua vifaa hayakutunzwa maana watu “walifanya kazi kwa uaminifu” (mstari 12).

 

Siku moja walipokuwa wakileta fedha ambazo zililetwa kwa ajili ya kufanya kazi katika nyumba ya BWANA, Hilkia, kuhani mkuu, akakiona kitabu kikubwa. Alipokitazama akagundua kuwa kilikuwa ni nakala ya kitabu cha Torati ya Musa. Akamwonyesha kitabu hicho Shafani, mwandishi, na akamwambia, “Kitabu cha torati nimekiona nyumbani mwa BWANA” (mstari 15). Shafani alikuwa mtu mwenye hekima na rafiki mwaminifu wa mfalme.Alitambua umhimu wa kuonekana kwa kitabu hicho, na alijua pia,jinsi mfalme Yosia atakavyourahia kusikia habari hii.Aliingia ndani kwa mfalme kumpatia taarifa kuhusu matengenezo kuwa yote yamekwisha na wafanyakazi wote wamelipwa. Kisha akamwonyesha kitabu akamwambia kuwa Kuhani Mkuu Hilkia ndiye aliyekiona.

 

Torati ya Musa inapatikana katika vitabu vitano vya kwanza vya Biblia. Kitabu kiitwacho Mwanzo kinaelezea kuhusu uumbaji na jinsi dhambi ya Adamu na Eva ambayo ilibadilisha kila kitu; kinatueleza pia kuhusu ahadi za Mungu kwa Ibrahimu, Isaka na Yakobo; Kitabu cha Kutoka kinaelezea kutoroka kwa wana wa Israeli kutoka Misri; Kitabu cha Mambo ya Walawi, Hesabu, Kumbu kumbu la Torati vinaelezea kuhusu kuzunguka zunguka katika jangwa kabla wana wa Israeli hawajaingia katika nchi na torati ambayo Mungu aliwapa.Kama tulivyosoma katika somo la 5, kulikuwa na amri maalumu kwa ajili ya wafalme, ikiwaambia kuiandika nakala ya sheria za Mungu kutoka katika kitabu cha torati. “Na awe nayo, asome humo siku zote atakazoishi; ili apate kujifunza kumcha BWANA, Mungu wake, ayashike maneno yote ya torati hii na amri hizi, kwa kuyafanya” (Kumbu kumbu la Torati 17:19)

 

Ikawa Shafani alipomaliza kusoma, mfalme Yosia alifadhaika sana kwa kujua kwamba wamekuwa hawatii sheria ya Mungu kwa miaka mingi, “aliyararua mvazi yake” (mstari 17)

 

Siyo tu kwamba mfalme alitakiwa asome kutoka humo katika kitabu cha torati kila siku, bali pia watu wote wasomewe kwa sauti kila baada ya miaka saba wakati wa sikukuu ya vibanda. Kitabu kiliwekwa ndani ya sanduku la BWANA katika Patakatifu pa Patakatifu katika Hekalu, lakini kilipotea wakati wa utawala wa wafalme wawili wa mwisho. Na sasa akawa amesomewa baraka na laana kutoka katika Kumbu kumbu la Torati sura 28, Yosia aliweza kuelewa ujumbe huu wa haraka wa Yeremia. Kwa miaka mingi Israeli hawaku wakimtii Mungu. Isingeshangaza Mungu kuwatuma Babeli kutoka kaskazini kuja kuwaadhibu Israeli na kuwapeleka mbali utumwani.

 

MUNGU AKAMRIDHIA YOSIA: 2 Mambo ya Nyakati 34:20-28

Yosia alifadhaika sana. Nikweli kabisa Mungu ataleta mabaya haya ya kutisha juu watu wake ambayo ameyasoma katika Torati KIULIZO. Ilikuwepo njia moja tu ambayo angefanya. Aliwatuma Hilkia, Shafani na watumishi wengi ne waaminifu kwenda kwa Hulda nabii mke aliyekuwa akiishi Yerusalemu, akawaambia; “Nendeni, mkamwuliza BWANA kwa ajili yangu” (mstari 21). Kwa hiyo walikwenda wakamwambia mfalme alivyosema na hofu aliyokuwa kuhusu mambo yanayokuja baadaye. Kwa huzuni nabii alijibu kuwa ni kweli kabisa Mungu atawaadhibu watu wake. Mungu aliwaonya sana kwa miaka mingi kupitia manabii, bali ni wachche walioweza kuwasikiliza manabii hao au kubadilisha njia zao. Hata hivyo Yosia alikuwa ameuelekeza moyo wake kumtii Mungu tangu alipokuwa mtoto. Mungu alikuwa na ujumbe maalum kwa ajili yake. “Kwa kuwa moyo wako ulikuwa mwororo, nawe umejinyenyekeza mbele ya Mungu, uliposikia maneno yake juu ya mahali hapa...na kuyararua mavazi yako, na kulia mbele zangu, mimi nami nimekusikia, asema BWANA” (mstari 27). Mungu hataleta mabaya juu ya Yerusalemu katika siku za Yosia. Kwa ajili ya uaminifu wake aliwaokoa watu wa nchi kwa muda mfupi na akawapatia nafasi ya kutubu na wakazibadili njia zao.

 

Kwa hiyo walirudi kutoka kwa nabii mke na wakamwambia mfalme yote waliyoambiwa na nabii.

 

PASAKA KUBWA SANA: 2 Mambo ya Nyakati 34:29-33; 35:1-19

Wakati Yosia alipotambua rehema ya Mungu aliyomwosha, aliona kuwa hata wengine pia wanapaswa kuipokea rehema hiyo kama watafundishwa jinsi ya kumtumikia Mungu katika kweli.

 

Kwa hiyo aliwaita Yuda na watu wa Yerusalemu, makuhani na Walawi, na watu wote wakubwa na wadogo, naye akawasomea masikioni mwao maneno yote ya kitabu hicho cha agano kilichopatikana katika nyumba ya BWANA. Akafanya agano na Mungu, akaahidi kuwa atafuata njia za Mungu na kuzishika amri zake kwa moyo wake wote na kwa nguvu zake zote.

 

Na akawafanya watu wote waliokuwepo pamoja naye kuahidi kumfuata Mungu. Na sasa ikakaribia siku ya pasaka. Na Yosia akaamua kuifanya sikukuu ya pasaka kubwa sana. Alisoma kwa makini maagizo yaliyoandikwa katika torati ya Musa kuhakikisha kuwa anamtii Mungu katika mambo yote. Aliitazama historia ya maisha ya Daudi na Selemani na akajifunza kutoka kwao kuhusu utaratibu wa makuhani na Walawi kwa ajili ya huduma katika nyumba ya BWANA. Maelfu ya wanyama walikusanywa na wakachinjwa kwa ajili ya dhabihu.

 

Alikuwa amekusudia kufanya kila jema ili kwamba “wala haikufanyika pasaka kama ile katika Israeli tangu siku za nabii Samweli” (mstari 18)

 

Yosia aliyaondoa machukizo yote katika nchi, sanamu, na makuhani walioabudu vinyago; sanamu, madhabahu zote na mhali pa juu-na kila kilichokuwa chukizo katika torati ya Musa. Na hii ndiyo sababu Mungu anamsema Yosia: “Kabla ya huyo hapakuwa mfalme mfano wake, aliyemwelekea BWANA kwa moyo wake wote,na kwa roho yake yote,na kwa nguvu zake zote, sawasawa na sheria zote za Musa” (2 Wafalme 23:25)

     

FUNDISHO KWETU

Jinsi mafundisho ya mama zetu ya awali yalivyo mhimu kwa watoto.Ikiwa tutajifunza kumpenda Mungu na neno lake la kweli tuapokuwa watoto, tutaweza kukua tukiwa na bidii ya kumpendeza Mungu.Yosia ni mfano mzuri kwetu sisi wa mtu ambaye hakugeuka mkono wa kulia au mkono wa kushoto kutoyaacha yote ambayo mama yake alimfundisha.Alikuwa imara-maana yake, hakubadili nia yake au hakugeuka. Alilichunguza Neno la Mungu ili kujua kweli na kuyatenda.Kwa sababu hiyo Mungu alimbariki na atatubariki sisi pia ikiwa tutaendelea kumtii Mungu kama alivyombariki Yosia.

 

MASWALI

Majibu Mafupi

1. Yosia alikuwa na miaka mingapi alipoanza kutawala?

2. Yosia alimfuata nani kama mfano?

3. Yosia alipokuwa na miaka 20 alifanya nini?

4. Ni hukumu gani ya kutisha ambayo Yeremia alisema Mungu angeleta juu ya watu wake?

5..Ni kwa nini Yeremia alisema kuwa Mungu angewaadhibu Yuda?

6. Wakati Hekalu lilipotakaswa Hilkia aliona nini?

7. Ni kwa nini Yosia alirarua mavazi yake?

8. Hulda nabii mke alisema Mungu angefanya nini?

9. Ni kwa nini Mungu alisema kuwa hataleta mabaya juu ya Yerusalemu katika siku za Yosia?

10. Ni kwa nini Pasaka ya Yosia ndiyo iliyokuwa kubwa sana tangu siku za nabii Samweli?

 

Majibu ya Kina

11. Eleza kilichotokea wakati Hilkia alipokiona kitabu?

12. Eleza fundisho mhimu tunalojifunza kutokana na maisha ya Yosia?

 

 

Swahili Title
066 YOSIA ANAISIMAMIA KWELI
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type