67. UFALME UNAPINDULIWA
''Hiki nacho hakitakuwa mpaka atakapokuja mwenye haki wangu nami nitampa''
Shabaha
Ni kuonyesha jinsi Yuda walivyokataa kuwasikiliza manabii wa Mungu na matokeo yake Yerusalemu ikatekwa na watu wakapelekwa utumwani. Mungu alikuwa ameshasema katika siku za Yosia, “Nitawahamisha Yuda pia mbali nami, kama nilivyowshamisha Israeli, nami nitautupa mji huu noliouchagua, naam, Yerusalemu, na nyumba ile niliyoinena, Jina langu litakuwa humo” (2 Wafalme 23:27). Yosia mwenyewe alikuwa ni mwenye haki, na Mungu alimwonyesha rehema kwa kutoyaleta mabaya katika siku zake. Ilikuwa ni siku ya huzuni sana kwa Yuda wakati Yosia alipofariki haikuchukua mmuda mrefu hukumu ya Mungu ikaanguka katika nchi.
2 Mambo ya Nyakati 36;2 Wafalme 23:31-37; Yeremia 36
MFALME WA MWISHO WA YUDA: 2 Mambo ya Nyakati 36:1-10
Yosia alikuwa na wana watatu, na baada yake kila mmoja alitawala. Hakuna hata mmoja miongoni mwao aliyefuata njia nzuri kama baba yake na wala hakuna hata mmoja aliyejiweka mwenyewe wakfu ili amtumikie Mungu kama Yosia alivyofanya. Wote watatu “walifanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA” (2 Wafalme 23:32, 37; 24:9, 19)
Yehoahazi, ndiye alikuwa wa kwanza.Alitawala kwa muda wa miezi mitatu tu. Farao, mfalme wa Misri, alimfunga gerezani na akawafanya watu wa Yuda walipe kodi ya dhahabu na fedha. Hatimaye Farao akmchukua moja kwa moja mpaka Misri ambapo alifia huko.
Na badala yake akamweka Yehoyakimu kuwa mfalme wa Yuda.Alipaswa kutoza kodi kubwa watu wake ili aendelee kulipa kodi kwa Misri. Na yeye mwenyewe aliishi maisha ya anasa Yerusalemu. Yeremia alimkemea mbele ya watu kwa ajili ya tamaa. Baba yake, Yosia, hakuwa na tabia kama hii.
Baba yake alikuwa mtu wa haki na mkweli: Aliwajali sana: “maskini na wahitaji” katika Yuda alijulikana sana kwa ajili ya wema wake na matendo yake mema (Yeremia 22:13-19).
Yehoyakimu alitawala kwa miaka kumi na moja.Na katika mwaka watatu wa kutawala kwake,Nebukadneza,mfalme wa Babeli alipigana na Farao katika vita iliyokuwa kubwa.Babeli ilishinda,na kwa hiyo Yehoyakimu akalipa kodi Babeli badala ya Misri.Na kama agemsikiliza Yeremia angeyaokoa maisha yake. Yeremia alijua kuwa Mungu alikuwa amewatuma Babeli kuja kuingamiza Yerusalemu. Aliwaambia watu waziwazi kuwa watachukuliwa mateka Babeli na watakuwa huko kwa muda wa miaka sabini.Jambo lililokuwa la mana ilikuwa ni kuuamini unabii huu na chochote abacho mfalme wa Babeli angetaka.
Yehoyakimu alikuwa mpumbavu,alikuwa na kiburi sana wakati wa kumskiliza Yeremia na akamwasi Nebukadneza.
YEHOYAKIMU ANACHOMA GOMBO: Yeremia 36
Mungu alikuwa amejaribu mara nyingi kupitia manabii kuwageuza watu mioyo, maana Mungu alikuwa amewahurumia na akiwa yu tayari kuwarehemu. Katika utawala wa Yehoyakimu, Mungu alimwambia Yeremia aandike unabii wote katika gombo ambao Mungu alikuwa ameshamwambia na ambao atamwambia siku hiyo. “Huenda nyumba ya Yuda watasokis mabaya yote niliyokusudia kuwatenda; wapte kurudi, kila mtu akaiache njia yake mbaya; nsmi nikawasamehe uovu wao na dhambi yao” (mstari3)
Kwa hiyo Yeremia alimwita mwandishi aliyeitwa Baruku, mtu mwaminifu na rafiki wakaribu na nabii.Alimsikiliza Yeremia akaandika katika gombo yote ambayo Mungu aliyomwambia Yeremia.Na kisha alikwenda akawa akimsomea mtu yeyote aliyesimama kusikiliza. Watu wakakusanyika kuomboleza kwa ajili ya mambo mabaya yaliyowapata. Maneno ya Mungu yaliyokuwa katika gombo yalikuwa ni maneno ya hasira ya Mungu, lakini yaliyojaa matumaini kwa mtu yeyote aliyeyasikiliza kwa makini. Mtu mmoja alisimama akasikiliza, kisha alikwenda kuwaambia wakuu.
Walikwenda wakamwambia Baruku ili wao wenyewe waweze kuyasikiliza maneno Yeremia. Ikawa Baruku alipomaliza kuyasoma maneno hayo yote “wakahofu sana” Na kisha walimwuliza Bauku, “Ulipataje kuyaandika maneno haya yote kinywani mwake?” (mstari 17)
Na Baruku aliwajibu, “Alinitamkia maneno haya yote kwa kinywa chake, nami nikayaandika kwa wino kitabuni” (mstari 19)
Walimjua Yehoyakimu ni mtu wa namna gani na walijua kuwa Yeremia na Baruku wangepoteza maisha yao mara mfalme atakapoyasikia maneno hayo.Kwa hiyo wakamshauri aende kujificha. “Enenda ukajifiche, wewe na Yeremia, wala mtu asipajue mlipo” (mstari 19)
Kwa hiyo wakuu wakaelewa umhimu wa yale waliyoyasikia, wakaenda kwa mfalme ambaye alikuwa akiota moto katika nyumba yake anayoitumia wakati wa baridi.Walipomweleza ni kwanini wamekwenda kwake.
Yehoyakimu akamwambia mmoja wao asome gombo. Alikuwa hajasoma mistari mingi, Yehoyakimu akatambua kuwa ni ujumbe wa aina moja aliowahi kuusikia kabla kwa Yeremia mara nyingi.
Alionyesha ni jinsi gani alivyofikiria yale maneno ya vitisho! Akachukua jembe ambalo lilikuwa mezani mbele yake, akalikata kata gombo na akavitupa vipande katika moto.
Na wakuu wengi sasa wakapata ahueni katika mawazo yao na hawakuyajali tena maneno yale. Kama mfalme alikuwa haogopi, hata wao piawasingeogopa.
Lakini, yalikuwa ni maneno ya Mungu! Watatu kati ya wale wakuu walitishwa sana na kitendo kile cha mfalme, lakini mfalme hakujali.Alimtuma watumishi wake kwenda kuwaita Yeremia na Baruku “lakini BWANA aliwaficha” (mstari 26)
Kwa hiyo neno la Mungu likawa limedharauliwa. Ni jinsi gani Yuda wangeokoka wakiwa na viongozi waovu namna hii, watu wasiomcha Mungu ambao ndiyo viongozi wao. Kitendo kile cha Yehoyakimu akajiletea mwenyewe juu yake hukumu ya Mungu.
“Hatakuwa na mtu wa kukaa katika kiti cha enzi cha Daudi; na mzoga wake utatupwa nje wakati wa mchana upigwe kwa hali na wakati wa usiku upigwe kwa baridi” (mstari 30)
Wakati Nebukadneza alipokuja tena Yerusalemu alimfunga pingu Yehoyakimu ili ampeleka Babeli, lakini akabadilisha mawazo. Akamwua pale Yerusalemu na akautupa mwili wake ukutani. Ili ni fundishoi kwa mtu yeyote atakaye pita na kumwona maiti yake kuwa ndivyo itakavyokuwa kwa mtu yeyote anayemwasi mfalme wa Babeli.
MANENO YA YEREMIA HAYAKUSIKILIZWA:
2 Mambo ya Nyakati 36:9-16; Yeremia 38:10-13
Yekonia, mwana wa Yehoyakimu, akatawala. Alikuwa ametawala miezi mitatu tu, Nebukadreza akaja akauzingira Yerusalemu na akamchukua mateka hadi Babeli. Kisha Nebukadreza akamweka Sedekia, mwana mwingine wa Yosia kuwa mfalme wa Yerusalemu. Wakati wa utawala wake Yeremia aliendelea kumwonya mfalme na watu pia, wao wakajitafutia manabii wa uongo waliosema yale ambayo watu walipenda kuyasikiliza kwa masikio yao.
Katika tukio moja Yeremia alishitakiwa kuwa aliisaliti nchi yake kwa mfalme wa Babeli kwa sababu alisema, “Bali yeye atokaye kwenda kwa Wakaldayo ataishi” (Yeremia 38:2). Wakuu wakamwambia mfalme, “Twakuomba, mtu huyu auawe, kwa kuwa aiodhofisha mikono ya watu wa vita” (Yeremia 38:4). Walimchukua wakamtupa katika shimo la tope la mavi likiwa na harufu kali mno ya chooni. Walimwacha hapo ili afe, maana kwa wakati huo mji ulikuwa umezingirwa pande zote na Nebukadreza.
Lakini Mkushi ambaye alikuwa towashi akamsihi mfalme ili amwokoe Yeremia, mfalme akakubali. Yule Mkushi akaenda kumwokoa.
Lakini bado Sedekia “hakujinyenyekesha mbele ya Yeremia nabii aliponena kwa kinywa cha BWANA” (2 Mambo ya Nyakati 36:12)
YERUSALEMU INAANGUKA: 2 Mambo ya Nyakati 37:17-21
Ikawa, katika mwaka wa kumi na moja wa kutawala kwa Sedekia, mji ambao ulizungukwa, na sasa wakiwa dhaifu kwa njaa na kwa hofu kwa muda wa miezi kumi na minane, mji ukaanguka mikononi mwa Nebukadreza (2 Wafalme25:1-2). Sedekia, bado liendelea kuyapuuza maneno ya Yeremia, akajaribu kukimbia wakati wa usiku, lakini maaskri wa Nebukadreza wakmkamata wakampeleka kwa mfalme wao.Wakawaua wana wa Sedekia mbele ya macho yake.Na kisha wakaondoa macho yake na wakampeleka Babeli, akafia huko.
(2 Wafalme25:4-7).
Na ikawa mji wa Yerusalemu, mji ambao Mungu aliuchagua ili aliweke Jina lake humo, ukaharibiwa kabisa. Wababeri wakangusha kuta za mji wa Yerusalemu na wakaiteketeza nyumba zote za mfalme, na hata wakaiteketeza kwa moto nyumba tukufu ya BWANA ambayo Selemani aliijenga kwa ajili ya kumwabudu Mungu. Walizichukua hazina zote, wakapeleka Babeli pamoja na watu waliosalia ambao hawakuawa kwa upanga. Walikuwapo huko Babeli mpaka miaka sabini ilipotimia.
Mungu hawezi kudhihakiwa, analitunza Neno lake na kuwaadhibu wasiotii na waasi kama alivyokwisha kusema.
FUNDISHO KWETU
Kutokana na somo hili tunajifunza mambo mawili kuhusu tabia ya Mungu ambayo ni ya ajabu kabisa-Mungu ni mwenye rehema na si mwepesi wa hasira, mwenye haki, na mwenye kusamehe uovu (Kutoka 34:6-7).
Mungu anataka tumtii-ni lazima tumtii Mungu. Kama tukifanya makosa, Mungu atafanya haraka kutusaidia ikiwa tutakubali kubadili tabia zetu. Lakini, kama tukikataa kulisikia Neno lake na tuzifuata njia zetu wenyewe atatuadhibiwa kama tunavyositahili. Na tabia zetu kwa wazazi wetu ni lazima iwe ya kuwatii pia.
Ni lazima tuwatii au tukubali adhabu wanayouambia kutupatia. Kama tukiwa watiifu kwa wazazi wetu tunakuwa tukijifunza kuwa watiifu kwa Mungu pia.
MAELEZO YA NYONGEZA
Wakati wa kuanguka Yerusalemu, muda ambao Yeremia alikuwa akijitahidi kwa mara ya mwisho kuwafanya watu wamsikie Mungu, manabii wakubwa wawili tayari walikuwa Babeli. Danieli alichukuliwa mateka wakati wa kutawa kwa Yehoyakimu (Danieli 1:1-3,6) na Ezekieli alichukuliwa wakati wa kutawala kwa Yehoyakini (Ezekieli 1:2). Akiwa yuko Babeli maneno ya Ezekieli yanapatana na maneno ya Yeremia.
Alimsema Sedekia kuwa “Ewe mtu wa uovu mkuu wa Israeli, ambaye siku yako imekuja, kaika wakati wa uovu wa mwisho” (Ezekieli 21:25) na haya yakatimia ambapo mwisho Yerusalemu ilipoanguka. Mungu alikuwa amesema kuwa itakubakia katika hali hiyo iliyotokea, pasipo kuwa na mfalme wa kutoka katika nyumba ya Daudi, “hata atakapokuja yeye ambaye ni haki yake; nami nitampa” (mstari 27). Huu ni unabii wa unaosisimua sana, maana mmoja aliye na haki ya kukaa katika kiti cha Daudi katika Yerusalemu ni Bwana Yesu Kristo. Bado hajatawala akiwa ni mfalme, lakinihata alipozaliwa unabii huu ulithibitishwa, maana malaika Gabrieli alimwambia Mariamu kuwa: “BWANA Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake. Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele na ufalme wake utakuwa hauna mwisho” (Luka 1:32-33)
Tunaamini kuwa Bwana Yesu Kristo atarudi upesi kutoka mbinguni, ambapo sasa anaisubiri saa iliyowekwa na Mungu ambaye atamtuma kuja kuuweka ufalme wa Mungu. (Soma Hatua ya 4 Somo la 5, Maelezo ya Nyongeza). Ni hapo Yerusalemu utakuwa ni mji wa mfalme mkuu. Mara hii tena Hekalu lenye utukufu zaidi litajengwa ambapo mataifa yote yatakuja kumwabudu na Jina la Mungu litawekwa hapo milele. Tunaomba unabii huu wa mzuri ajabu utimizwe upesi na tunaomba sisi kwa njia ya imani yetu na utii wetu kwa Mungu tushiriki furaha wakati huo wa ufalme.
MASWALI
Majibu Mafupi
1. Majina ya wana 3 waYosia ni yapi?
2. Ni jinsi gani walitofautiana na baba yao?
3. Ni nabii yupi katika Yerusalemu aliyeendelea kujaribu kuwafanya watu wasikie Neno la Mungu?
4. Baruku aliandika nini kwenye gombo?
5. Mfalme Yehoyakimu alifanya nini walipomsomea maneno ya kwenye gombo?
6. Ni nani aliyekuwa mfalme wa mwisho wa Yuda?
7. Yeremia walimtupa wapi?
8. Ni nani aliyemwokoa Yeremi?
9. Ilikuwaje wakati Sedekia alipojaribu kukimbia?
10. Hekalu lilikuwaje wakati Nebukadrza alipoingia katika mji?
11. Nini jambo gani liliwapata watu wa Yerusalemu mji ulipoharibiwa?
12. Ni kwa muda gani Israeli walikaa utumwani?
Majibu ya Kina
13. Eleza jinsi Mungu alimweleza kuandika kwenye gombo na unabii wote wa Mungu na nini kilichotokea kwa ajili ya gombo hilo?
14. Maneno ya Yeremia yalikuwa ya kuwaelekeza watu wajue Mungu anataka nini.Je,watu walipaswa wajifunze nini?
Majibu ya Nyongeza
15. (a) Je,atakuwepo mfalme atakaye keti katika kiti cha Daudi tena?
(b) Atakuwa ni nani?
(c) Itatokea lini?
|
WAFALME WA ISRAELI NA YUDA |
||||
|
YUDA |
MUDA WA KUTAWALA |
ISRAELI
|
MUDA WA KUTAWALA |
MANABII |
|
Rehoboamu |
Miaka 17 |
Yeroboamu |
Miaka 12 |
Shemaya |
|
|
|
|
|
Ahiya |
|
Abiya |
Miaka 3 |
Nadabu |
Miaka 2 |
|
|
Asa |
Miaka 41 |
|
|
Hanani |
|
|
|
Baasha |
Miaka 24 |
Odedi |
|
|
|
|
|
Azaria |
|
|
|
Ela |
Miaka 2 |
|
|
|
|
Zimri Juma 1 |
|
|
|
|
|
Omri |
Miaka 12 |
|
|
|
|
Ahabu |
Miaka 22 |
Eliya |
|
Yehoshaphati |
Miaka 25 |
|
|
Mikaya |
|
|
|
Ahazia |
Miaka 2 |
Yehu |
|
|
|
Yehoramu |
Miaka 12 |
Elisha |
|
Yehoramu |
Miaka 8 |
|
|
Eliezeri |
|
Ahazia |
Mwaka 1 |
|
|
Yahazieli |
|
Athalia |
Miaka 6 |
Yehu |
Miaka 28 |
|
|
Yoashi |
Miaka 40 |
|
|
|
|
|
|
Yehoahazi |
Miaka 17 |
|
|
|
|
Yehoashi |
Miaka 16 |
|
|
Amazia |
Miaka 29 |
|
|
Yona |
|
|
|
Yeroboamu 2 |
Miaka 41 |
Hosea |
|
Uzia |
Miaka 52 |
|
|
Isaya |
|
(Azaria) |
|
|
|
Amosi |
|
|
|
Zekaria |
Miezi 6 |
|
|
|
|
Shalumu |
Mwezi 1 |
|
|
|
|
Menahemu |
Miaka 10 |
|
|
|
|
Pekahia |
Miaka 2 |
|
|
Yothamu |
Miaka 16 |
|
|
Mika |
|
|
|
Peka |
Miaka 20 |
|
|
Ahazi |
Miaka 16 |
|
|
|
|
|
|
Hoshea |
Miaka 9 |
|
|
WALIPELEKWA UTUMWANI |
||||
|
WAFALME WA ISRAELI NA YUDA |
||||
|
YUDA |
MUDA WA KUTAWALA |
ISRAELI
|
MUDA WA KUTAWALA |
MANABII |
|
Hezekia |
Miaka 29 |
|
|
Nahumu |
|
Manase |
Miaka 55 |
|
|
|
|
Amoni |
Miaka 2 |
|
|
|
|
Yosia |
Miaka 31 |
|
|
Sephania |
|
Yehoahazi |
Miezi 3 |
|
|
Yoeli |
|
Yehoyakimu |
Miaka 11 |
|
|
Yeremia |
|
Yehoyakini |
Miezi 3 |
|
|
Habakuki |
|
Zedekia |
Miaka 11 |
|
|
Obadia |
|
WALIPELEKWA UTUMWANI BAADHI YA MANABII WALIOHUDUMU WAKATI WA WATAWALA
|
||||