CSSA 1-3-20 - DANIEL IN THE LIONS' DEN

Swahili

70. DANIELI KATIKA TUNDU LA SIMBA

“Mungu wako unayemtumikia daima, yeye atakuponya”

 

Shabaha

Kuonyeosha jinsi Mungu alivyomponya Danieli asiliwe na simba-kwa sababu alimwamini Mungu.

 

Mungu alikuwa amemwosha Nebukadreza katika ndoto kuwa ufalme wake utapinduliwa na Wamedi na Waajemi,waliowakilishwa katika sanamu hiyo na kifua na mikono ilikuwa ni fedha. Kwa hiyo ikatimia Dario Mmedi akatawala Babeli na wakati huo Danieli alikuwa anaishi huko. Ufalme wa Wamedi na Waajemi ulikuwa na maliwali mia na ishirini waliokuwa juu ya ufalme wote; kati yao walichaguliwa wakubwa watatu wawe juu yao na Danieli alikuwa ndiye wa kwanza katika hao watatu “kwa kuwa roho bora ilikuwa ndani yake” (mstari 6)

 

MAWAZI HAWAKUONA KOSA KATIKA DANIELI: Danieli 6:1-5

Mawaziri na wakuu hawakona aliowaweka mfalme juu ya ufalme wake wote walimwonea wivu Danieli. Walipenda kumtafuta kosa maana walichukia kwenda kwa Myahudi kutoa hesabu. Na katika yote aliyoyafanya, Danieli alitenda kwa uaminifu na bidii maana alifuta kanuni: “Lolote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu” (Wakolosai 3:23). Walikuwa wanajua mfalme alimwona Danieli kuwa ni mtu mwaminifu kabisa. Maana ilionekana kuwa haiwezekani kabisa kuweza kuondoa tumaini la mfalme alilokuwa nalo kwa Danieli. Walisema wao kwa wao, “hatutapata sababu ya kumsitaki Danieli huyu, isipokuwa katika mambo ya sheria ya Mungu wake” (mstari 5). Ukweli kuwa Danieli alisimama imara katika kumwabudu Mungu wake, hata pale Babeli, liliwapatia wazo.Kwa hiyo wakamwekea Danieli mtego.

 

DANIELI ANAFANYIWA NJAMA: Danieli 6:1-9

Mawaziri na wakuu waliungana wote katika kumchukia Danieli. Walimpelekea mfame mpango wao wa akili. Walimwambia mfalme, “Mfalme Dario, uishi milele. Mawaziri wote wa ufalme, na manaibu, na maamiri, na madiwani, na maliwali, wamefanya shauri pamoja ili kuwka amri ya kifalme; na kuiga marufuku, ya kwamba mtu yeyote atakayeomba dua kwa Mungu awaye yote, au kwa mtu awaye yote, katika muda wa siku thelathini, ila kwako, Ee mfalme, atatupwa katika tundu la samba”.

 

Mpango huu wa akili usingeweza kushindwa kabisa. Mpango huu ulikuwa wa hila na wakujipendekeza kwa mfalme na ungewampatia heshima na sifa nyingi kwa watu aliokuwa anawatawala. Mfalme kwa kweli hakujuwa kuwa Danieli hakuhusishwa; walikuwa wamedanganya katika hili. Mfalme aliliona kuwa ni wazo zuri na kwa hiyo akashawishika na kutia sahihi maandiko hao, na akayafanya kuwa sheria isiyoweza kubadilika, “kama ilivyo sheria ya Wamedi na Waajemi, isiyowezakubadilika” (mstari 8)

 

DANIELI ALITUPWA KATIKA TUNDU LA SIMBA: Danieli:6:10-17

Ikawa Danieli alipopata taarifa kuwa yale maandiko yametiwa sahihi, alifahamu kuwa huo ulikuwa ni mpango wa kumwua yeye. Na wakati huo alikuwa ni mzee, umri wake ulikuwa kama miaka tisini. Mungu alikuwa amembariki na kumfanikisha kwa muda wa miaka yote aliyokuwa mtumwa katika Babeli. Mungu alikuwa amemlinda na kumwokoa yeye na rafiki zake waaminifu katika taabu nyingi nyingi. Danieli alimwamini Mungu kuwa atamwokoa katika mambo yote na hata sasa aliendelea kumtumaini Mungu hata katika hili.

 

Aliingia nyumbani mwake akapiga magoti akamwomba Mungu na mbele yake madirisha yalikuwa yamefunguliwa kuelekea Yerusalemu. Kwa upande wa maghribi mbali sana kutoka hapo ndiko mji wa Yerusalemu, ambako ndiko alikochukuliwa kuwa mateka wakati alipokuwa kijana. Na sasa mji huo ambao aliupenda ukawa ni magofu; lakini Mungu aliyesema kuwa ataliweka Jina lake hapo ni Mungu aliye hai.

 

Selemani wakati akiliweka wakfu Hekalu alimwomba Mungu kuwa asikie maombi ya watumwa wake, watakapoomba wakiwa wamelekea mji wa Yerusalemu katika imani (Mambo ya Nyakati 6:36-39). Mara tatu kila siku Danieli alimomba Mungu, akiwa mbele ya madirisha yakiwa yamefunguliwa kueleka Yerusalemu na hakuacha kumwomba na kumshukuru Mungu, ingawaje maisha yake yalikuwa hatarini.Danieli alijuwa kuwa alitakiwa kumtii Mungu, kuliko kumtii mwanadamu.

 

Na ilikuwa sababu hii ya imani yake thabiti iliyosababisha mawaziri wengine na maamiri wawe na uhakika wa kumtega Danieli. Walikutanika pamoja na kumpeleleza na wakawa wamefanikiwa kumkuta akiwa haitii sheria ya mfalme kwa kuwa Danieli alimwabudu Mungu wake. Walikwenda kwa mfalme haraka. Je! hukuweka sahihi kuwa sheria, ya kwamba mtu yeyete awaye atakayemwomba Mungu mwingine au mtu yeyote isipokuwa mfalme, lazima atatupwa katika tundu la simba? Mfalme akajibu, neno hili ni kweli, “kama ilivyo sheria ya Wamedi na Waajemi isiyoweza kubadilika” (mstari 12). Mpango wao wa uovu ulikuwa umefanikiwa. “Yule Danieli, aliye mmoja wa wale wana wa wale waliohamishwa wa Yuda, hakujali wewe, Ee mfalme, wala ile marufuku uliyoiti sahihi, bali anaomba dua mara tatu kila siku.

 

Mfalme aliweza kutambua mpango wao, lakini alikuwa ameshachelewa. Alikuwa amekwisha kutia sahihi kuwa sheria pasipo kumjulisha Danieli, maana alikuwa anajuwa kuwa Danieli alikuwa ni mwaminifu sana kwa Mungu wa Israeli. Mfalme alikuwa amejifunza kuwaamini mzee na alimpenda sana Danieli, lakini sasa, kwa ajili ya kiburi chake, aliweka sahihi iliyokuwa inamaanisha kifo cha Danieli. Mfalme alihanhangaika sana akitafuta na kufanya kila njia ili aibadilishe ile sheria, ili Danieli aweze kuokoka. Kwa siku nzima alitafuta ukweli na kutafuta ukweli wa mpango huo uliofanywa kuwa sheria, mwisho hakuwa na namna nyingine ila kuitii sheria. Hatimaye washauri wake waovu wakamtaka “kwa ajili ya kufanikisha mpango wao wa kikatili.”

 

Kwa huzuni mfalme akaamuru Danieli aletwe na atupwe katika tundu la simba.Maneno ya mwisho ya mfalme kwa Danieli yalikuwa ni ya kumtia moyo. “Mungu wako unayemtumikia daima, yeye atakuponya”

 

Kisha wakaleta jiwe, likawekwa mdomoni mwa lile tundu; naye mfalme akalitia mhuri kwa mhuri wake mwenyewe na kwa mhuri wa wakuu wake.

 

DANIELI ANAOKOLEWA: Danieli 6:18-23

Mfalme akahangaika sana usiku ule akafunga na usingizi ukampaa.Hakuweza kula chakula siku hiyo, na wala na vinanda havikuletwa mbele yake.Mazingira yote ya siku hiyo hayakuwa na matumaini yoyote,lakini imani ya Danieli na ujasiri wake vilimvutia sana mfalme.Mungu wa Danieli tangu mwanzo alijulikana kwa kutenda miujiza mikubwa sana.Akili ya mfalme haikutulia kabisa usiku na hakuweza kulala usingizi.

 

Ili ajue ukweli kama Danieli ni mzima au ameliwa na simba mfalme alisubiri mpaka asubuhi.Mara kulipopambazuka alikwenda haraka sana kule penye tundu la simba.

 

Jinsi gani hakuwa na furaha kwa kujua kuwa hakufikiria mapema kabla ya kuweka sahihi na jinsi matokea yake yalivyokuwa. Kwa huzuni alimlilia Danieli, “Ee Danieli, mtumishi wa Mungu aliye hai, je! Mungu wako, unayemtumikia daima, aweza kukuokoa na simba hawa” (mstari 20). Ilikuwa ni faraja kubwa sana kwa mfalme aliposikia sauti ya Danieli, “Mungu wangu amemtuma malaika wake, naye ameyafumba makanwa ya simba, nao hawakunidhuru, kwa kuwa mbele zake mimi nilionekana sina hatia; tena mbele yako, Ee mfalme, sikukosa neon” (mstari wa 22). Danieli alipata neema kwa Mungu kwa ajili ya uelekevu wake na tabia yake ya uaminifu na Mungu akamwokoa kutoka katika tundu na kama Danieli alivyosema kuwa yeye hakuwa na kosa “kwa sababu alikuwa anamtumani Mungu wake” (mstari 23). Ilikuwa ni imani yake ambayo ”ilifunga vinywa vya samba” (mstari 11:33)

 

MFALME DARIO ANAWEKA AMRI MPYA: Danieli 6:24-28

Mfalme Dario hakupoteza muda kwa kuwaadhabu wale waovu waliokuwa wamemdanganya Mfalme kwa mpango wao.Walipaswa kupata hukumu ile ile waliyokuwa wamempangia Danieli. Walitupwa ndani ya tundu la simba, wakiwa pamoja na wake zao na watoto wao, “na wale simba wakawashinda wakaivunja mifupa yao vipande vipande, kabla hawajafika ndani ya tundu” (mstari 24).

 

Kisha mfalme akaweka amri mpya na ikapelekwa katika ufalme wake wote.

 

“Mimi naweka amri, ya kwamba katika mamlaka yote ya ufalme wangu watu watetemeke na kuogopa mbele za Mungu wa Danieli; maana yeye ndiye Mungu aliye hai, adumuye milele, na ufalme wake ni ufalme usioharibika, na mamlaka yake itadumu hata mwisho” (mstari 26). Basi mfalme alitambua kuwa siyo tu kwamba Mungu wa Danieli angemponya na kumlinda asiliwe na simba bali pia Mungu wa Danieli ni Mungu aliye hai na adumuye milele.Amri hii ya Dario inafanana na maneno yaliyo katika Danieli 2:44 ambapo Danieli alimfahamisha Nebukadreza, mfalme wa Babeli, tafsiri ya ndoto yake.Danieli aliweza kumwonyesha kuwa Dario yale aliyowahikumwosha mara moja Nebukadreza, kuwa siku moja Ufalme wa Mungu ndiyo utakaotawala badala ya falme hizi za wanadamu zinazitawala. Ufalme wa Mungu utakuwa ni Ufalme utakaodumu milele na ni wa haki na amani. Kwa hiyo Danieli alitumia nafasi hii ya kuponywa kwake asiliwe na simba kuihubiri habari njema za Ufalme wa Mungu kwa wafalme (wa mataifa) ambao hawakuwa Wayahudi.

 

MAFUNDISHO KWETU

Kwa mara nyingine tena tunapata mfano mzuri sana wa imani na utiifu. Tunaweza kamwe tusiitwe kukabiliana na changa moto hii ya tundu lililojaa simba, lakini Mungu anataka tuonyeshe imani moja kama ya Danieli. Kama imani ya Danieli na tumaini lake kwa Mungu viliweza kufunga vinywa vya simba, na sisi tunaweza kuwa na uhakika kwamba Mungu atatusaidia katika majaribu yetu kama tutakuwa waaminifu pia.

 

Hakuna kinachotuzuia kumwomba na kumshukuru Mungu kama vile Danieli alivyofanya.Kumbuka pia kuwa Mungu asingemtuma malaika wake kumwokoa Danieli, kama Danieli asingekuwa mwaminifu na imani katika shughuli zake za kila siku.Ni lazima mwenendo wetu uwe ni wa uelekevu kila wakati ili mtu asipate kosa lolote katika maneno yetu na matendo. Kwa njia ya mwenendo mzuri tunaweza kuwaonyesha wale wanaotuzunguka, kwamba tunamwamini Mungu na tunatazamia kuwa katika ufalme wa Mungu.

 

MAELEZO YA NYONGEZA

Tabia ya chukia ya mawaziri na wakuu waliyomfanyia Danieli, watu wa Mungu wametendewa hivyo hivyo katika vizazi vyote. Tabia hii huitwa “wasiowapenda Wayahudi” (anti-semitism). Wayahudi wanatoka katika uzao wa Shemu (Mwanzo 11:10-26  Shemu alikuwa ni babu wa Ibrahimu) na kwa hiyo wanaitwa “Wenye chuki dhidiyaWayahudi (Semitic). Anti-semitism maana yake wanaowachukia Wayahudi.” Katika ahadi za Mungu kwa Ibrahimu, Mungu alisema, “Nitawabriki wakubariki o, naye akulaaniye nitamlaani” (Mwanzo 12:3). Wale waliowabariki Wayahudi, uzao wa Ibrahimu, Mungu amewabariki.

 

Kuna mifano mingi sana katika Biblia kuhusu watu ambao Mungu aiwalaani kwa sababu waliwachukia watu wa Mungu. (Katika somo la 22 tutajifunza kuhusu ('Hamani adui wa Wayahudi”).Mawaziri na wakuu wa Umedi walimwonea wivu Danieli kwa mara ya kwanza kwa sababu hawakupata kosa kwake.Wivu ukageuka kuwa chuki, na ndivyo kila mara inavyo kuwa. Na kwa hiyo wakaishia kumchukia kwa sababu Danieli alikuwa ni Myahudi (Danieli 6:18) na wake zao na watoto walikuwa wana hisia zenye chuki pia kwa Wayahudi.Na ndiyo sababu Mungu akawaadhibu na wao pia.

 

Katika siku zetu, aliinuka mtu aliyeitwa Hitler aliyekuwa na mpango wa hila sawa na mpango wa watu hawa, alikusudia kuwaangamiza Wayahudi wote. Aliwaua Wayahudi milioni sita, ni idadi kubwa sana ya watu waliouawa na kitendo hiki kilisababisha Wayahudi wengine kukimbilia katika nchi ya Israeli. Na hili Mungu alikuwa ameshalisema kwamba kabla ya kurudi kwa Yesu Kristo Wayahudi watarudi katika nchi yao. Kwa hiyo wivu wa Hitler ikatimiza sehemu ya kusudi kubwa la Mungu na Israeli. Mungu atamtuma upesi Bwana Yesu Kristo kuwaokoa watu wake kutoka katika uvamizi wa jeshi kubwa la Urusi ambao utafanyika katika nchi ya Israeli. Na hata itakuwa baada ya hayo Wayahudi hawatachukiwa tena wala kudharauliwa, bali Mungu atawafanya Wayahudi kuwa kichwa cha mataifa yote (Kumbu kumbu la Torati 28:13; Yeremia 3:17).

 

Na ndipo hapo watu wote watona kwamba kusudi la Mungu kwa Ibrahimu, na Isaka na Yakobo likiwa limetimizwa: “Na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa” (Mwanzo 12:3).

 

Inatupasa tuwapende Wayahudi, kwa sababu ni uzao wa Ibrahimu, na ndiyo sababu Mungu anawapenda Wayahudi (Warumi 11:26).

 

MASWALI

Majibu Mafupi.

1. Ni kwa nini wakuu na mawaziri walimwonea wivu Danieli?

2. Ni amri ipi ambayo wakuu na mawaziri walimwomba mfalme Dario aweke sahihi?

3. Je Danieli alifanya nini aliposikia kuhusu amri?

4. Je wakuu na mawaziri walimwambia nini kuhusu Danieli?

5. Je mfalme Dario alifurahi aliposikia kuwa Danieli amevunja amri yake?

6. Je mfalme Dario alifanya usiku ule wakati Danieli alipokuwa ndani ya tundu la simba?

7. Danieli alimwambia nini mfalme alipokwenda kule kwenye tundu la simba asubuhi?

8. Je Danieli aliumizwa popote na simba?

9. Walifanywaje wale mawaziri na-wakuu waovu?

10. Amri mpya Mfalme Dario ilikuwa ipi?

 

Majibu ya Kina

 

11. Eleze habari jinsi Danieli alivyotupwa katika tundu lasimba na namna alivyookoka?

12. Mfalme Dario alijifunza nini kuhusu:

      (a) Mungu wa Danieli?

      (b) Ufalme wa Mungu?

13. Katika somo hili ni kwa vipi Danieli anakuwa ni mfano mzuri kwetu?

 

Majibu ya Nyongeza

14. (a) Ni kwa nini mawaziri na wakuu walimchukia Danieli?

      (b) Mungu katika yake kwa Ibrahimu aliahidi kuwa atawafanyaje wale wanaolaani Wayahudi?

      (c) Katika habari hii Mungu aliwafanya nini watu waliomchukia Danieli?

      (d) Ni kwanini tuwapende Wayahudi?

 

Swahili Title
070 DANIELI KATIKA TUNDU LA SIMBA
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type