71. WAYAHUDI WANARUDI YERUSALEMU
“Kuijenga nyumba ya BWANA, Mungu wa Israeli iliyoko Yerusalem”
Shabaha
Kuonyesha kuwa Koreshi aliweka amri ya kuwaruhusu Wayahudi warudi Yerusalemu kuijenga tena nyumba ya BWANA huko. Ni wakati ambao Danieli alipokuwa mtumwa katika Babeli,ndipo Yerusalemu ukateketezwa na kubakia magofu. Nyumba ya BWANA yenye kuwa na uzuri wa wa ajabu iliyojengwa na Selemani ikateketezwa kwa moto hadi chini. Hata ikawa kinara cha taa cha dhahabu, vikombe vya dhahabu na mabakuli ambavyo vilikuwa ni vitakatifu kwa BWANA, vikapelekwa kuwa mapambo ya wafalme wa Babeli. Milango na kuta za mji zilibomolewa ili kuwa njia wakati wa maadui walipoingia ndani ya mji. Watu wengi, wakimemo wazee wanaume, na wanawake na watoto, waliuawa kwa upanga kinyama. Na waliokuwa wamesalia wakafungwa na kupelekwa wakiwa mateka nchi ya mbali. Baada ya kuchoka sana kutokana na kutembea muda mrefu, waliomboleza wakati walipoukumbuka mji ule walioupenda, mji wa Sayuni ambao walifikiri kuwa hautaangamizwa. Manabii wa Mungu walikuwa wameshawaonya juu ya jambo hili mapema la kuaangamizwa kwa Sayuni. Mara nyingi aliwatuma manabii wake, kwa maana alikuwa amewahurumia watu wake, lakini hawakuwasikiliza.
Iliwapasa kuivumilia adhabu ya dhambi yao. Na Yeremia alikuwa amesema kuwa watakuwa Babeli muda wa miaka sabini (Yeremia 25:11). Na sasa ikawa muda wa miaka sabini unakaribia kuisha. Wale, kama Danieli, waliochukuliwa mateka wakiwa vijana, sasa walikuwa wazee. Baadhi yao waliyakumbuka maneno na walianza kuwa na matumaini kuwa ya kurudi tena Yerusalemu. Ezra 1;3; 4:1-6; 17-23; 5:1-26
AMRI YA KORESHI: Ezra 1
“Babeli utakapotimiziwa miaka sabini, nitawajilia”, Mungu alikuwa ameshasema kupitia Yeremia, “na kulitimiza neno langu njema kwenu, kwa kuwarudisha mahali hapa” (Yeremia 29:10). Wanaume na wanawake waaminifu walikuwa wamehesabu na kujua kuwa tangu Nebukadreza aharibu Yerusalemu ilikuwa imetimia miaka sabini (9:2,16-19) na wakawa wakifikiria jinsi Mungu atakavyitimiza ahadi yake. Na siyo tu Yeremia peke yake aliyetabiri habari ya mambo, bali pia nabii Isaya miaka mia mbili kabla alikuwa amemtaja jina la mfalme ambaye angeitawala Babeli wakati muda utakapofika wa kutimizwa kwa mambo hayo.
Dario alikuwa amekufa na Koreshi, mfalme wa Uajemi, akatawala. Alikuwa ndiye aliyetajwa na nabii Isaya, maana Mungu amwambia Koreshi: “Naye atayatenda mapenzi yangu; hata atanena Yerusalemu, Utajengwa; na hilo hekalu, Msingi wako utawekwa” (Isaya 44:28). Ni unabii wa ajabu namna gani ambao ulisema miaka hiyo yote kabla.Kuna uwezekno kuwa Danieli katika siku hizo alipokuwa na cheo cha heshima huko Babeli ndiye aliyemwonyesha Koreshi maneno haya; kwa kuwa ni kweli ni ndiye aliyeweka sheria na kuituma mapema alipoanza kutawala na akawapatia uhuru Wayahudi warudi Yerusalemu. Unabii huu wa kushangaza ulimfanya Koreshi kuamini kuwa hakika Mungu ndiye anayetawala katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, na huwaweka wafalme na huwaondoa kwa ajili ya hekima yake (Danieli 4:17). Kwa hiyo Koreshi akaweka tangazo katika nchi yake yote: Koreshi mfalme wa Uajemi asema hivi; “BWANA, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote za dunia, naye meniagiza nimjengee nyumba katika Yerusalemu, ulioko Yuda. Basi kila mtu miongoni mwenunyote mlio watu wake, Mungu wake na awe pamoja naye, na akwee mpaka Yerusalemu, ulioko Yuda, kaijenge nyumba ya BWANA, Mungu wa Israeli, (yeye ndiye Mungu), iliyoko Yerusalemu. Na mtu awaye yote mahali popote aliyesalia akaapo hali ya ugeni, na asaidiwe na watu wa mahali pake, kwa fedha, na dhahabu, na mali, na wanyama zaidi ya vitu vitolewavyo kwa hiari ya mtu, kwa ajili ya nyumba ya Mungu, iliyoko Yerusalemu.” (Ezra 1:2-3)
Wayahudi wengi sana walikaa kwa raha mstarehe katika nchi ambayo iliwateka na wao na watoto wao wakachagua kuendelea kuishi huko. Amri ya Koreshi iliwataka wachangie kazi ya kuujenga tena mji wa Yerusalemu, kwa kuwapatia walewaliokuwa wanarudi, fedha, dhahabu, wanyama na vifa vingine vya ujenzi.
Koreshi, mfalme akawapatia vikombe na vyombo vyote vya fedha na vya fedha ambavyo Nebukadreza alikuwa amevichukua wakati alipoliharibu Hekalula miaka sabini iliyokuwa imepita. Na vyombo hivi vilikuwa ni hazina ya thamani kwa kuvirudisha Yerusalemu. Zerubabeli, alikuwa mkuu wa Yuda, ndiye aliyewekwa kuwa msimamizi mkuu wa ujenzi na ndiye akawa liwali wa mji. Na watu zaidi ya arobaini na mbili elfu walifuatana naye kutoka makabila ya Yuda na Benyamini na pia makuhani na Walawi. Watu hawa wote majina yao yaliandikwa katika kitabu cha orodha.
Hii ilikuwa ni idadi ndogo sana ya watu, tukifikiria kwa kuwa watu wote waliondoka katika nchi ya Israeli miaka hiyo sabini kabla. Na hata hivyo palikuwa na kazi kubwa ya kufanya na walikuwa na shauku sana ya kurudi katika mji wao waupendao ili kupanga mkakati wa kuujenga tena.
MADHABAHU INAJENGWA KWANZA: Ezra 3:1-7
Hawa Wayahudi waaminifu wakasafiri safiri ndefu ya kurudi nyumbani,kundi hilo lilikuwa na furaha sana kuliko wakati wa kwenda uhamishoni. Waliporudi katika miji yao na wakaanza tena shughuli za kilimo na kazi ya kutunza mizabibu ambayo ilikuwa imetelekezwa kwa miaka mingi sana. Wasamaria walioishi upande wa kaskazini na Wamoabi na Waedomu kwa upande wa mashariki, hawakufurahishwa kuwaona Wayahudi wakiwa wanarudi. Kwa hiyo wakayafanya maisha Wayahudi yasiwe ya furaha na Wayahudi wakahofia usalama wao.
Na Yohana, Kuhani Mkuu, na Zerubabeli liwali, wakajenga madhabahu, ili waweze kuanza kumtolea Mungu dhabihu zinazotakiwa. Walifahamu kabisa kuwa Mungu alikuwa ndiye nguvu yao. Mungu aliwawezesha kurudi kwao na angewalinda na kuifanikisha kazi waliyokuwa wanafanya, ikiwa tu watamtumainia.
Watu wakatok katika miji wakakusanyikia Yerusalemu ili kuishika Sikukuu ya vibanda na makuhani wakaendelea na kazi zao za kila siku za kuabudu, “kama ilivyoandikwa katika torati ya Musa, mtu wa Mungu” (mstari 2). Wisraeli waliishika Sikukuu ya vibanda kwa mara ya kwanza wakati Mungu alipowatoa katika Misri. Sasa walipaswa kuishika Sikukuu hiyo kuufurahia kwa kuwa Mungu alikuwa amewatoa Babeli.
MSINGI WA HEKALU UNAWEKWA: Ezra 3:8-13
Mfalme Koreshi, aliwapatia fedha kwa ajili kulijenga tena Hekalu(Ezra 6:4). Walawi wakapanga utaratibu ili kuhakikisha kazi inafanyika. Wakawalipa “ili kuanza msingi” wakaleta miti kutoka Lebanoni kwa ajili ya kujenga Hekalu; kama vile Selemani alivyokuwa amelijenga. Katika wa pili wa kufika kwao ndipo msingi ulipojengwa na watu wakakusanyikia Yerusalemu kusherehekea. Makuhani, wakavaa mavazi yao, wakazipiga baragumu za fedha na Walawi wakayapiga matoazi na wakamshukuru BWANA, “kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake kwa Israeli ni za milele” (mstari 11). Watu walimshukuru Mungu kwa kuwalinda na wakafurahi sana kwa kuona tena Hekalu likijengwa katika Yerusalemu. Uimbaji ulipokwisha, “Kisha watu wote wakapaza sauti zao, na kupiga kelele, walipomhimidi BWANA kwa sababu msingi wa nyumba ya BWANA umekwisha kuwekwa” (mstari 11)
Miongoni mwa watu waliokusanyika wengi walikuwa ni wazee sana, makuhni na Walawi na wakuu wa nyumba za mababa. Walikuwa wakiukumbuka utukufu ule na fahari ya Hekalu la Selemani,ambalo lilikuwa ni kitovu cha Israeli kwa ajili ya kuabudu.Walikuwepo siku za wa utawala wa Sedekia na wakati Nebukadreza alipokuja na jeshi kuharibu vyote viwili Hekalu na mji wa Yerusalemu.Kuonekana kwa msingi huu mpya kuliwakumbusha kile walichokuwa wamekipoteza.Walilia sana walipozikumbuka siku zile za zamani.Lakini baadhi ya watu wakapaza sauti za furaha.Walikuwa na matumaini sana kuwa kuanzia wakati huo na kuendelea Mungu angewabariki.Sauti yao ya furaha ilichanganyikana na sauti ya kukilia kwa wale waliokuwa wakiomboleza, kwa mbali sauti ilisikika.
KAZI INASIMAMA: Ezra 4:1-6, 17-23
Maadui wa Israeli hawakupenda kuona Wayahudi wakianza kazi ya kujenga kuta za mji.Haikuwafurahisha kabisa kuona watu hawa wakiwa wamerudi hapa tena, watu wanaojitenga na majirani zao. Mwanzo maadui hawa walishirikiana nao katika kazi ya kujenga. Walimwambia Zerubabeli, “Na tujenge sisi pamoja nanyi, kwa maana tunamtafuta Mungu wenu kama ninyi” (mstari 2).
Hawa walikuwa ni Wasamaria ulikuwa ni mchanganyiko wa watu ambao Waashuru waliachwa katika nchi Israeli walipouchukua ufalme wa kaskazini yaani mabila kumi ambayo yalikuwa mateka. Ibada yao ilikuwa ni ya uongo. Ingawaje baadhi yao walisikia habari za BWANA na wakajua torati kidogo ya BWANA, lakini walikuwa wanaabudu sanamu. Ndipo Zerubabeli na Yoshua wakalifahamu hilo haraka na wakaiona hatari iliyokuwapo kwa kukubali kushirikiana na watu wa namna hiyo. “Ninyi haiwahusu kushirikiana nasi katika kumjengea Mungu wetu nyumba, bali sisi wenyewe peke yetu tumjengee BWANA, Mungu wa Israeli nyumba, kama mfalme Koreshi, mfalme wa Uajemi, alivyotuamuru” (mstari 3). Wasamalia hawa waliposhidwa kupata walichokuwa wanahitaji, wakajaribu kudhoofisha mikono ya watu kwa kuingilia kazi. Na hatimaye waliandika waraka kwa mfalme wa Waajemi wakiwashitaki kwa uongo Wayahudi. Koreshi alikuwa ameshafariki na mfalme mpya wa Waajemi akakubaliana na maneno ya uongo wao naye akajibu waraka akiwaamuru Wayahudi kusimama kazi za kujenga tena nyumba ya Mungu mara moja. Kwa hiyo kazi ambayo ilikuwa imeanza kwa uaminifu na kwa hamasa kubwa ikasitishwa, mpaka Mungu alipomtuma nabii wake Hagai na Zekaria kuwatia moyo kuendelea na kazi ya kujenga.
KAZI INAKAMILIKA: Ezra 5:1-2:6
Miaka kumi na tatu ikaisha pasipo kazi kufanyika. Kwa muda huu watu wakakataa kuruhu kitu chochote kuwazuia. Na manabii wawili wakawahimiza kuendelea na kazi, Zerubabeli na Yoshua wakaweka mfano mzuri ajabu wa imani na bidii ya kazi. Waliweza kuona kuwa walivunjwa moyo upesi, lakini Mungu angeibariki kazi yao kama wangemtumaini. Maadui wao wakajaribu kuingilia tena waaandika waraka kwa mfalme wa Waajemi. Hata hivyo, safari hii, mfalme alifanya uchunguzi katika kumbukumbu za historia ya Waajemi na ndipo akaipata amri ya Koreshi. Kwa hiyo akawaandikia Wasamaria uamzi wake kwamba kazi ya kujenga tena ambayo Koreshi aliamuru ni lazima iendelee, aliandika, iacheni kazi hii ya nyumba ya Mungu iendelee, msiizuie; waacheni liwali wa Wayahudi, na wazee wa Wayahudi, waijenge nyumba ya Mungu mahali pake (mstari7). Siyo hiyo tu, lakini pia akawaagiza maadui wa Wayahudi ni lazima wachangie mchango wa ngombe, kondoo, ngano, chumvi, mvinyo na mafuta, kama makuhani wa Mungu walivyokuwa wahitaji. Akasema “a wapewe vitu hivyo vyote siku kwa siku, msikose kuwapa” Na kama mtu yeyote atabadili amri hii boriti na itolewe katika nyumba yake, akainuliwe na kutungikwa juu yake tena nyumba yake ikaangushwe chini na kuwa kama kichuguu. Na kwa maneno haya yenye nguvu, mmfalme wa Waajeshi aliwajibu maadui wa Wayahudi. Hawakujaribu kupinga tena.
Mungu aliwasaidia kwa namna ya kushangaza sana.Na miaka mingine minne iliyofuata kazi ya ujenzi ikakamilika. Huu haukuwa wakati wamaombolezo tena, “kwa kuwa BWANA amewafurahisha, na kumgeuza moyo mfalme wa Ashuru, awaeleker, ili awatie nguvu mikono yao katika kazi hiyo ya nyumba ya Mungu, Mungu wa Israeli”
(mstari 22).
FUNDISHO KWETU
Wayahudi waaminifu walipokuwa Babeli walisoma torati ya Musa na manabii kwa makini sana wakafahamu namna ambayo Mungu atakavyoleta baraka kwa watu wake na kwa Yerusalemu. Tunapoisoma Biblia kila siku, tunajifunza unabii ulioandikwa mingi miaka sana, kuwa siku moja Mungu ataleta amani Yerusalemu na kuufanya kuwa mji mkuu wa dunia nzima. Atalijenga Hekalu lenye utukufu zaidi kupita ule uliokuwapo wakati wa Hekalu lililojengwa na Selemani, na wakati huo mataifa yote watakuja Yerusalemu, ili wamwabudu mfalme, Bwana Yesu Kristo. Njia peke ya kuwa na uhakika kuwapo pale na kushiriki utukufu huu na furaha itakayokuwepo wakati huo, ni kwa kujifunza njia ya Mungu na kwa kutii amri zake kila siku.
MAELEZO YA ZIADA
Myahudi mwingine pia alipata kibali kwa mfalme wa Waajemi. Huyu alikuwa ni Ezra, mwana wa Haruni, ambaye pia alikuwa ni mwandishi na mwenye ufahamu mkubwa katika torati ya Musa. Mungu ndiye aliyemwondoa Ezra huko na kumpeleka Yerusalemu na sasa Hekalu likawa limejengwa tena, kuwaongoza watu katika njia sahihi ya kumwabudu Mungu. Jukumu lake maalum ilikuwa nikuwaweka mahakimu na waamuzi katika nchi na kufundisha torati ya Mungu kwa watu wote waliokuwa wamerudi tena.
Mungu akawaleta watu waaminifu kwa ajili ya kujenga madhabahu na Hekalu, na sasa makuhani waaminifu wakageuza mioyo yao kufuata sheria ya Mungu ili waweze kufanikiwa “Kwa maana huyo Ezra alikuwa ameuelekeza moyo wake kuitafuta sheria ya BWANA, na kutenda na kufundisha maagizo na hukumu katika Israeli.” (Ezra 7:10)
MASWALI
Majibu Mafupi
1. Mungu alisema kuwa watu wake watakaa Babeli kwa miaka mingapi?
2. Ninani aliyemtaja Koreshi kwa jina kabla ya miaka mia mbili?
3. Koreshi aliwaambia Wayahudi wafanye nini?
4. Koreshi aliwapatia Wayahudi nini wapeleke Yerusalemu?
5. Waliporudi Yerusalemu walijenga nini kwanza?
6. Wakati walipoishika Sikukuu ya vibanda walikuwa wakifurahia nini?
7. Mwaka wa pili walijenga sehemu gani ya Hekalu?
8. Watu walishangilia wakati msingi ulipowekwa. Walikuwa wakifurahia nini?
9. Wasamaria ni nani?
10. Ni kwa nini Zerubabeli hakuwaruhusu Wasamaria wawasaidie kujenga Hekalu?
11. Ni jambo gani lililosababisha watu wasiendelee kujenga Hekalu?
12. Ni manabii gani wawili waliowatia moyo kuanza tena kujenga Hekalu?
13. (a) Miaka sabini baaba ya Nebukadreza kuangamiza Yerusalemu, wanaume waaminifu
waliokuwa Babeli walipatwa na mshangao. Kwa nini?
(b) Koreshi aliaandika sheria ipi?
14. Eleza kilichotokea msingi wa Hekalu ulipowekwa?
15. (a) Mfalme mmoja wa Uajemi alizuia kazi ya kulijenga tena Hekalu. Kwa nini?
(b) Mfalme wa Uajemi mwingine aliyefuata alipoisoma amri ya Koreshi alisema nini?
Maelezo ya Nyongeza
16. (a) Ezra alikuwa ni nani?
(b) Kazi yake ilikuwa ni ipi?