CSSA 1-3-22 - ESTHER

Swahili

72. ESTA

“Naye huyo Esta alikuwa amepata kibali machoni pa wote waliomwona”

 

Shabaha

Kuonyesha jinsi Esta, msichana Myahudi, aliyepata kuwa malkia wa Uajemi,na kupitia imani yake aliwakomboa watu wake wasiangamie.

 

Mungu alikuwa amesema kwamba atawaadhibu watu wake kwa kuwafukuza watoke katika nchi yao aliyowapatia watu wake kwa ajili ya kutokutii kwao. Waliowateka waliwachukia sana na wakawatesa sana, hata ikawa maisha yao yakawa ya uchungu. Kama tulivyoona katika masomo yetu yaliyopita, kati ya mateka hao walikuwapo wanaume waaminifu, ambao kwa sababu ya tabia ya uelekevu na uaminifu wao walithaminiwa sana na watawala wa nchi hiyo. Imani yao ilisababisha Wayahudi wapate kibali kwa watawala hawa mara nyingi. Mmojawa wa watu hao aliitwa jina lake Mordekai, alikaa mbele ya mlango wa nyumba ya mfalme kule Shusheni, mji mkuu wa Uajemi. Alikuwa na binti mrembo ambaye ni mpwa wake. Ambaye alimtunza katika nchi hii ya kigeni. Ilikuwa ni imani ya Esta iliyowaokoa watu wake wasiangamizwe kabisa katika mikono ya wale waliowachukia.

 

Esta 1.2.3.4.5.6 na 7

 

MALKIA WA UAJEMI ANAVULIWA UMALKIA: Esta 1;2:1-4

Mfalme wa Uajemi wa wakati huo aliitwa Ahasuero, “mtu hodari wa vita”. Ufalme wake ulifika mpaka India kwa upande wa mashariki na kwa upande wa magharibi ulifika Ethiopia. Alifanya sherehe akawaalika watu mashuhuri na wakuu wote katika ufalme wake wahudhurie ili aweze kuwaonyesha utukufu, na fahari na utajiri wa makao ya ufalme wake katika Shushani, na utukufu na heshima ambayo alikuwa nayo. Sherehe hii ilidumu kwa mwezi mmoja, na baada ya mwezi huo akawafanyia sherehe watumishi wake waliomzunguka katika Shushani kwa muda siku saba. Tena Vashti, malkia, naye wakati huo huo akawafanyia karamu wanawake ndani ya nyumba ya mfalme.Na siku ya saba, Ahasuero akamwita Vashti ili afike kwa mfalme ili awaonyeshe wakuu wake uzuri wake, lakini Vashti alikataa kuja. Basi mfalme alikasilika sana kwa nini Vashti alimdharilishe kwa kumfanyia kiburi kama kile kwa kutokumheshimu na akamwaibisha mbele ya wakuu, na watumishi wake. Mfalme alipotaka shauri kwa washauri wake, walifiki kuwa kwa heshima ya mfalme, na kwa kulinda heshima ya wanaume wote kwa wake zao, Vashti asiwe mfalme tena. Ushauri wao ulikuwa,

 

“Basi mfalme akiona vema, na itoke kwake amri ya kifalme, nayo iandikwe katika sheria ya Waajemi na Wamedi isitanguke, ya kwamba Vashti asifike tena mbele ya mfalme Ahasuero; na umalkia wake mfalme ampe mwingine aliye mwema kuliko yeye”

 

Kwa hiyo amri ya kifalme ikapelekwa katika majimbo yote ya ufalme wake wa Uajemi kwamba, “kila mwanamume atawale nyumbani mwake” (mstari22)

 

Kisha washauri wa mfalme wakaweka ushauri mwingine ambalo mfalme alilikubali kwafuraha. Watumishi waliteuliwa kwenda katika majimbo yote ya ufalme wake kuwachagua mabikira warembo na wawapele Shushani. Pale katika nyumba ya wanawake, walikaa mwaka mzima wakijiandae kwenda kukutana na Mfalme wa Ahasuero. “Naye yule msichana atakayempendeza mfalme na awe malkia badala ya Vashti” (mstari 2:4)

 

ESTA ANAKUWA MALKIA: Esta 2:5-20.

Kati ya mabikira waliochaguliwa kwa heshima alikuwa ni msichana Myahudi, Esta, ambaye alipata fadhili haraka kwa Hegai, “mwenye kuwalinda wanawake”. Tena ilikuwa dhahiri kuwa Esta hakuwa tu mrembo, lakini pia alikuwa myenyekevu na mwenye huruma. Alijitayarisha kama wanawake wengine kwa kujipaka mafuta ya utakaso na manukato, na alipokea kila alichoagizwa na Hegai kwa ajili ya utakaso na mavazi yake. Na ilipowadia zamu ya Esta kuingia mbele ya mfalme, “Naye huyu Esta, alikuwa amepata kibali machoni pa wote waliomwona”. Mfalme akampenda Esta sana kuliko wanawake wote, na akamtia taji ya kifalme kichwani pake akamfanya malkia badala ya Vashti. Arusi ilipofanyika, karamu ikafanyika kwa ajili ya heshima ya Esta na watu wote wa Uajemi wakafurahi sana.

 

Kwa wakati wote huu Esta hakudhihirisha kuwa yeye ni Myahudi, maana Mordekai mjomba wake, alikuwa amemwonya asijidhihirishe.

 

HAMANI, ADUI WA WAYAHUDI: Esta 3

Basi katika baraza la mfalme alikuwepo Mwagagi (maana yake, Mwamaleki) jina lake aliitwa Hamani, ambaye mfalme alimpatia cheo cha heshima ya juu. Watumishi wote wa mfalme waliinama, na kumsujudia-isipokuwa Mordekai. Alifahamu kuwa Mungu alikuwa ameshawalaani Waamaleki (Kumbu kumbu la torati 25:17-19) na ibada, ya aina hii alipewa Mungu, na siyo mwanadamu. Watumishi wa mfalme walijaribu kmsihi Mordekai kubali msimamo wake, lakini kwa ajili ya dhamiri Mordekai alikataa. Wakati walipomjulisha Hamani, alikasirika sana. Ni kwa nini huyu Myahudi asionyeshe heshima kama watu wengine pia Shushani? Hasira yake ikageuka na kuwachukia, siyo kwa Mordekai peke yake tu, bali kwa Wayahudi wote. “Kwa hiyo Hamani alitaka kuwaangamiza Wayahudi wote waliokuwa wakikaa katika ufalme wote mzima wa Ahasuero, yaani watu wake Mordekai” (mstari 6)

 

Njia peke ambayo Hamani angeweza kutimiza mpango huo wa mauaji hayo ya kutisha sana, ili kuwa ni kumshawishi mfalme kukubali. Kwa hiyo alimfahamisha mfalme kuhusu mpango huo “kuna taifa lililotawanyika na kukaa mahali mahali katikati ya mataifa” walioko katika majimbo ya Uajemi. Na sheria zao zimefarakana na sheria za kila taifa; “wala hawazishiki amri za mfalme” (mstari 8). Haikuwa busara kwa mfalme kuwavumilia watu kama hao ni heri waangamizwe. Ushauri huu ulionekana ni wa busara kwa Ahasuero. Kwa hiyo akaivua pete yake ya kifalme akavalisha Hamani ili aitumie kwa kutia muhuri waraka ulipoandikwa. “Barua zikapelekwa kwa mikono ya matarishi mpaka majimbo yote ya mfalme kuwaangamiza Wayahudi wote, na kuwaua, na kuwafisha, vijana kwa wazee, watoto wachanga na wanawake pia, siku moja” (mstari 13).

 

Lakini mfalme hakujua kwamba Hamani alikuwa anamanisha kuwaua Wayahudi, wala hakujua kuwa malkia wake mpenzi Esta mwenyewe ni Myahudi

 

 

IMANI YA ESTA YAJARIBIWA: Esta 4

Wakati mfalme na Hamani wanakunywa, Mordekai akachana nguo zake akavaa magunia na majivu, akalia kwa sauti kuu ya uchungu akiwa katikati ya mji. Na katika majimbo yote ya ufalme, kulikuwa na kulia, na kufunga na maombolezo makubwa ya Wayahudi.

 

Esta alihuzunika sana aliposikia habari za uchungu wa Mordekai, akamtuma mtumishi wake ili ayajue mambo hayo. Mordekai akampatia yule mtumishi nakili ya andiko la mbiu ya kuwaangamiza, na kumsisistiza Esta mwenyewe kwa mfalme ili awaombee watu wake. Kisha Esta aliogopa sana, maana alijua kuwa kama mtu atakwenda kwa mfalme pasipo kuitwa, ina maana mtu huyo anauawa. Esta akasema, “wala mimi sikuitwaniingie kwa mfalme yapata siku thelathini” (mstari 11). Ikawa Mordekai alipoambiwa maneno haya, akamtuma mtumishi amwambie Esta jibu, maneno yaliyomfanya atetemeke sana. Wewe usijidhanie ya kuwa wewe utaokoka nyumbani mwa mfalme, zaidi ya Wayahudi wote (mstari 13). Kwa ajili ya amri atakufa, lakini kama hatawaombea kwa mfalme basi Mungu atafanya njia yingine ili kuwaokoa watu wake. Mordekai alisema, “ni nani ajuaye kama wewe hukuujia ufalme kwa ajili ya wakati kama huo?”

 

Maneno haya yalimfanya Esta atambue kuwa Mungu ndiye aliyempatia nafasi ile ya heshima, na kama atamtegemea Mungu, atakuwa ni mwenye rehema atawakomboa Wayahudi mikononi mwa adui zao, kama ambavyo alikuwa akiwaokoa siku za nyuma. Esta akamwambia Mordekai awakusanye Wayahudi wote walioko Shushani wamwombee na wakafunge kwa muda wa siku tatu, naye Esta na wajakazi wake watafunga vilevile kabla Esta hajaingia kwa mfalme. Hivyo Esta akayatoa maisha yake kuwa dhabihu kwa ajli ya kuwkomboa watu wake. “Kisha nitaingia kwa mfalme, kinyume cha sheria; nami nikiangamia, na niangamie (mstari 16)

 

KARAMU YA ESTA: Esta 5

Baada ya siku tatu, Esta akavaa mavazi ya kifalme akaingia katika baraza la nyumba ya kifalme. Na Ahasuero alipomwona Esta pale,alifurahi sana kumwona naakamnyoshea fimbo yake ya dhahabu aliyokuwa nayo mkononi. Kwa maana hiyo Mungu alikuwa amembariki Esta. Mfalme akamwambia Esta, “Malkia Esta wataka nini, nayo ni haja gani uliyonyo, utapewa hata nusu ya ufalme” (mstari 3). Esta alifarijika sana kumwona mfalme akiwa amefurahi alipomwona, lakini kwa busara hakufanya haraka kumwambia mfalme ombi lake. Badala yake alimkaribisha mfalme na Hamani kwenye karamu. Esta hakupata nafasi nzuri ya kumwambia mfalme ukatili wa ile amri ya Mhiti.

 

Esta akaadaa karamu nyingine siku ya pili. Njinsi Hamani alivyopumbazika kwa kiburi na furaha aliyokuwa kupata mwaliko maalum tena. Alipojivuna kwa mke wake na rafiki zake hakuweza kutafakari jambo linaloweza kumwondolea furaha yake yote. Hamani akasema, “Bali haya yote yanifaa nini, pindi nimwonapo yule Mordekai, Myahudi, ameketi mlangoni pa mfalme” (mstari 13). Mke wake na rafiki zake wakampatia wazo ambalo lingemaliza shida yake. “Na ufanyizwe mti wenye mikono hamsini urefu wake,na kesho asubuhi useme na mfalme ili Mordekai atundikwe juu yake:ndipo utakapoingia kwa kicheko pamoja na mfalme karamuni” (mstari 14). Lilionekana kana kwamba ni wazo zuri sana kwa Hamani na akafanya haraka akaufanyiza mti huo.

 

ESTA ANAWAOKOA WATU WAKE: Esta 7

Siku iliyofuata, ndipo Esta alisema ombi lake. Yeye na watu wake walikuwa ni wahanga wa mpango wa uovu wa kuwaangamiza. Mfalme alikasirika sana. Ni nani huyu tena yuko wapi, ambaye moyoni mwake aliyekusudia kufanya hili?

 

Esta akasema, “Ni huyu mtesi tena ni adui, ndiye huyu Hamani mtu mbaya kabisa” (mstari 6). Mfalme alikuwa na hasira sana. Akimfiria mtu ambaye alimwamini, kuwa alikuwa ameitumia cheo chake cha heshima kwa kusudi la kutenda ubaya. Na mmoja wa watumishi wake akamwambia mfalme kuhusu mti wa mikono hamsini urefu ulioandaliwa na Hamani aliouandaa kwa ajili ya Mordekai. Mfalme akaagiza, “Mtundikeni juu yake”. Kwa hiyo, Hamani, adui wa Wayahudi, akatundikwa. Mfalme hakuibatilisha amri ile ya kwanza ambayo ilitiwa muhuri na pete yake mwenyewe. Bali aliandika amri nyingine ya kuwaruhusu Wayahudi wayapiganie maisha yao na mali zao siku hiyo ambayo amri ya pili ilipotangazwa.

 

Kwa imani na uhodari wa Mordekai na Esta, watu wa Mungu wakaokolewa tena kutoka kwa maadui wao.

 

FUNDIHO KWETU

Esta alikuwa ni mrembo, lakini haukuwa uzuri wake tu uliomfanya ajulikane sana. Alikuwa ni mnyenyekevu na mwenye huruma, maana alikuwa amejifunza kuwa tabia hizi zinampendeza Mungu na wanadamu. Aliendelea kuwa mtiifu kwa Mordekai, ambaye alikuwa ni kama baba kwake, na hata baada ya kuwa malkia wa Uajemi. Aliweza kumtegemea sana Mordekai kwa kuwa alikuwa ni mtu mwenye imani kubwa. Na wakati wote Mordekai, alikuwa akimfundisha Esta amtumaini Mungu. Hakika waliamini kuwa Mungu atayasikia maombi yao na ilikuwa ndiyo sababu ya Esta awe na ujasiri wa hata kukubali kuhatarisha hata uhai wake kwa ajili ya watu.

 

Mungu huyalinda maisha yetu na huipimani imani yetu wakati wote,ili aone kama kweli tunamwamini. Kamwe hatujui ni lini mambo tunayoyatenda yatabadilisha maisha ya wengine, na kwa hiyo siku zote inatupasa kuwa tayari kuyatetea na kuyalinda yale tunayoyaamini na tunawajulishe watu wajue kuwa tunamwabudu Mungu.

 

MAELEZO YA NYONGEZA

Katika Somo la 19 tulitaja kwamba Wayahudi walikuwa na maadui wao katika vizai vyote wliowachukia na kuwalaani. Hamani, “adui wa Wayahudi” kuna uwezakano kuwa ndiye mfano wa adui mbaya sana katika Biblia. Chuki yake, ilimfanya akusudie siyo kumwua Mordekai tu pake yake, bali kuwangamiza Wayahudi wote mahali popote walipokuwa. Na yeye alipokwisha kutundikwa juu ya mti, mali zake zote mfalme akampatia Esta (8:1). Mordekai alipewa ukuu sana ambao hata Hamani hakuwahi kupewa, maana “Mordekai Myahudi akawa wa pili wake mfalme Ahasuero” (10:3)

 

Wayahudi wakaishi kwa amani na Mordekai akawaangalia wayahudi katika mambo yote mema kuhusu mahitaji yao.Kwa hiyo laana ya Hamani iligeuka na kuwa baraka kwa watu wa Mungu na Hamani mwenyewe alilaaniwa (Mungu alikuwa ameshamwambia Musa, “Nitawalaani wakulaanio” (Mwanzo 12:3)

 

Tabia ya watu kuwachuki Wayahudi itaendelea kuongezakea na kuwa ya mbaya zaidi wakati huu mpaka kurudi kwa Kristo, lakini Kristo ajapo, Mungu ataigeuza laana yao kuwa baraka. Atawaokoa watu wake na maadui wao wataangamizwa (Sefania 3:8, Yoeli 3:1). Wayahudi (wampendao Mungu kama Mordekai) watapewa vyeo vya ukuu wa heshima na wataishi katika nchi yao kwa amani (Sefania 3:20; Eekieli 39:27-28; Isaya 62:1-2). Na utajiri wa mataifa yalinayochukia Wayahudi utawekwa mikononi mwa watu watakaohusika kusimamisha ufalme wa Mungu (Isaya 60:9-11).

 

Na sisi ni lazima tuwe na imani ya Mordekai na Esta, kama tunataka kushiriki furaha wakati wa ufalme.

 

MASWALI

Majibu Mafupi

1. Ilitokea nini wakati Ahasuero alipomwita Vashti afike kwenye karamu?

2. Ni mpango gani wa uovu alioufikiria Hamani?

3. Ni wazo gani ambalo washauri wa mfalme waliamua ili kumpata malkia mpya?

4. Esta alikuwaje?

5. Mordekai ni nani?

6. Ni kwa nini Mordekai alikataa kuinama mbele ya Hamani?

7. Ni mpango gani mbaya sana ambao Hamani aliupanga?

8. Ni jinsi gani Esta alivyopata mpango mbaya sana ambao Hamani aliupanga?

9. Je, Mordekai alimwambia Esta ni lazima afanye nini?

10. Je,Esta alimwambia Mordekai afanye nini kwa muda wa siku tatu?

11. Wakati Ahasuero alipomwona Esta akiwa amesimama ndani ya baraza,alifanyaje?

12. Mke wa Hamani alimwambia afanye nini?

13. Hamani ilimtokea nini mwishowe?

 

Majibu ya Kina

 

14. Elezea jinsi Vasti aivyoacha kumtii mfalme na namna Esta alivyopata kuwa malkia

15. (a) Eleze jinsi Mordekai alivyomkasirisha Hamani?

      (b) Ni mpango gani mbaya sana ambao Hamani aliupanga?

      (c) Ni jinsi gani Hamani alivyofanya hata mfalme akakubali?

 

Majibu ya Nyongeza

 

16. Eleza jinsi Mungu alivyomshusha Hamani na kumwinua Mordekai mpaka kwenye heshima?

17. Ni jinsi gani Mungu atakavyogeuza laana ya maadui wa wana wa Israeli kuwa baraka wakati

      Kristo atakaporudi?

 

Swahili Title
072 ESTA
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type