76. YESU ANABATIZWA NA YOHANA
“Kubali hivi sasa,kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote".
Shabaha
Kuonyesha jinsi Yohana mbatizaji alivyoitayarisha mioyo ya watu kwa ajili ya ujio wa masihi; na jinsi Yesu mwenyewe alivyobatizwa.Yohana alijiandaa mwenyewe kule jangwani kwa ajili ya kazi kuu ambayo Mungu alikusudia Yohana aifanye “Kwa maana utatangulia mbele za uso wa Bwana umtengenezee njia zake” (Luka 1:76). Masihi, yaani Kristo, alikuwa karibu kutokea kwa Israeli naye Yohana alikuwa atangaze hilo na ambaye aliendelea kutangaza kwa watu kwamba mfalme wao alikuwa anaku kuja.
Mathayo 3; Marko1:1–11; Luka3:1–22
YOHANA ANAANDAA KUJA KWA MASIHI.
Kama tulivyosoma sehemu ya mwisho ya masomo, Yohana alikuwa mtoto wa pekee sana, malaika Gabrieli alikuwa amemwambia Zakaria kwamba mtoto huyu angekua na kuwa kama Eliya nabii,aliyeigeuza mioyo ya wengi katika Israeli kuwarejeza kwa Mungu wao (Luka 1:17)
Wakati Yohana alipokua, alimwacha baba yake na mama yake na kwenda jangwani, mbali na faraja zote za familia ya nyumbani kwao,alijifunza kumtegemea Mungu kwa ajili ya mahitaji yake yote. Chakula chake cha kila siku kilikuwa ni nzige na asali ya mwitu, Naye Yohana mwenyewe mavazi aliyoyavaa ilikuwa ni singa za ngamia, na mshipi wa ngozi iunkni mwake (Mathayo 3:4; linganisha na Eliya katika 2 Wafalme 1:8). Huko, akiwa katika upweke wa jangwa, Yohana alikuwa anajiandaa kutangaza tangazo lake kwa wana wa Israeli. Na watu wote iliwapasa kusikia habari na kujitayarisha wenyewe.
Wakati ulipofika, Mungu alimpeleka kwenye nchi ya milima ya Yudea na katika nchi zote zinazozunguka Yordani kutangaza ujumbe wake. Masihi mfalme wao, anakuja. Iliwapasa wajiandae kukutana naye, manabii muda mrefu uliopita walikuwa wametabiri habari ya masihi (Yaani, Mfalme aliyepakwa mafuta na Mungu), na ambaye angetokea kwa watu wake ili kuwaokoa.
Kila mmoja alizungumzia juu ya Yohana, baadhi walisema kwamba alikuwa ndiye masihi, lakini Yohana akasema “Mimi siye”. Yohana mwenywe aliwaambia yeye alikuwa ni nani: “Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani. Inyosheni njia ya Bwana, kama vile alivyonena nabii Isaya” (Yohana1:23 angalia Isaya 40:3).
UJUMBE WA YOHANA
Yohana alikuwa mwalimu mwenye nguvu, makini na hodari katika kuhutubu.Mungu alikuwa amemjaza roho mtakatifu tangu tumboni mwa mamaye (Luka 1:15) na kwa hiyo aliweza kuwaambia watu hasa jinsi Mungu alivyowaona,ulikuwa ni wakati wao wa kutubu – yaani, kubadili njia zao, “Tubuni kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia”; aliwambia watu wote waliokwenda kumsikia (Math 3:2). Na watu wote waliguswa na maneno yake wakamwuliza; “Tufanye nini basi” (Luka 3:10). Hivyo Yohana aliwaambia watubu na kubatizwa, akawaambia jinsi walivyokuwa wabinafsi na wasio na mawazo kabisa. Mwenendo wa aina hiyo haukumpendeza Mungu. Iiwapasa wabadili njia zao na kuwa wakarimu kwa wangine, wamshukuru Mungu na kuridhika na walivyokuwanavyo. Nilazima wamwonyesha Mungu ya kwamba wanazipenda njia zake na kuwa walikuwa tayari kumsikiliza Masihi atakayempeleka, na watamfuata.
Habari ya kazi za Yohana zilipofika masikioni mwa Waandishi na Mafarisaya huko Yerusalemu walifikiri ni bora zaidi kujionea wenyewe ni nini watu walikuwa wakifurahia. Wao iliwapasa kuwa viongozi katika Israeli, wakiwafundisha watu sheria za Mungu na njia zake, lakini badala yake walikuwa wamewapotosha watu. Yohana alipowaona wakija aliwaambia kwa ukali mbele ya watu wote akawaita “uzao wa nyoka” kwa sababu walikuwa wamewadanganya watu, kama vile nyoka katika bustani ya Edeni alivyo mwambia uongo Eva na kumdanganya. Yohana aliwaambia; basi, “Zaeni matunda yapasayo toba”. Pia wao ni lazima wabadili njia zao, la sivyo Mungu angeleta hukumu za kutisha juu yao katika miaka ambayo ingefuata.
Na watu wowote kati yao walipokwenda kwa Yohana na kutubu dhambi zao alishuka nao majini na huko akawabatiza. Miili yao ilizama kabisa majini, ilikuwa ni ishara ya kwamba maisha yao ya zamani ilibidi yafe. Walipoibuka kutoka majini walikuwa sasa tayari kuanza maisha mpya, na njia nzuri ya maisha siyo kwa kujipendeza wao wenyewe, bali kwa kumpendeza Mungu.
YESU ANABATIZWA KATIKA MTO YORDANI.
Katika miaka mitatu na nusu ya kuhubiri kubatiza, Yohana hakujua ni nani hasa alikuwa masihi.Siku moja mtu alijitokeza kutoka katika umati mkubwa wa watu na kwenda kwa Yohana. Aikuwa ni binamu yake Yesu. Yohana alimjua ni mtu wa namna gani. Hakujua yeyote aliye mnyoofu na mcha Mungu kuliko Yesu. Huyu hakuwa ndiye aina ya mtu aliyekuwa akimhubiri, alikuwa akiwaambia waovu na wenye dhambi kutubu na kubatizwa, mtu huyu hakuwa mwenye dhambi, hivyo wakati Yesu alipomwambia Yohana ambatize; Yohana alisema “mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu?” (Mathayo 3:14).
Hata hivyo, Yesu, alijua kuwa watu wote wanahitaji ubatizo. Yesu akamwambia Yohana “ndivyo itupasavyo kuitumiza haki yote” (Math 3:15). Hivyo Yesu pia akazama ndani ya maji ya mto Yordani, naye Yohana akambatiza. Naye,Yesu alipopanda kutoka majini jambo la ajabu likatokea. Yesu alipokuwa akisali, na mara mbingu zikafunguka na Roho wa Mungu akiwa katika umbo la njiwa akatua kichwaki pake. Na sakuti ikasikika kutoka mbinguni ikasema, “Huyu ndiye mwanangu mpendwa, ninayependezwa naye” (mstari 17). Na hapa alikuwepo “mpakwa mafuta wa Mungu” masihi wa Mungu, kwa maana Mungu alikuwa amempaka mafuta kwa Roho mtakatifu. Na sasa Yohana alimtambua kwamba huyu ndiye wote walikuwa wakimgojea. Kazi ya Yohana ilikwisha, Nasa, Yesu mwenyewe angeendeleza kazi ya kuhubiri, akisema “Tubuni kwa kuwa ufalme wa mbinguni umekaribia” (Mathayo 4:17).
FUNDISHO KWETU
Njia za Mungu ni sahihi nasi inatupasa kujifunza kuzitafuta njia zake na kutembea katika njia hizo. “Mawazo yangu siyo mawazo yenu, wala njia zenu siyo njia zangu. Na kama vile mbingu zilivyo juu zaidi kuliko nchi, kadhalika njia zangu njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu. Asema BWANA” (Isaya 55:8 – 9). Ni Bwana Yesu kristo peke yake ambaye hakuwa na dhambi, mawazo yake yote yalikuwa mawazo ya Mungu naye katika njia zake zote alimtii Mungu. Inatupasa kujaribu kumfuata Bwana Yesu Kristo. Inatulazimu kujifunza njia za Mungu kwa kusoma Biblia kila siku. Na Kisha tutakapokuwa ni wakubwa tutaona kwamba inatupasa kubatizwa ili kumpendeza Mungu, kama Yesu alivyofanya.
MAELEZO YA NYONGEZA
Je, nabii Isaya alisema mambo gani yaliyomfanya Yohana naye ayaseme kama alivyofanya? “Wote wenye mwili ni majani, Na wema wake wote ni kama ua la kondeni; majani yakauka, ua lanyauka; Bali Neno la Mungu wetu litasimama milele” (Isaya 40:6 – 8). Sisi sote ni wenye “mwili”; wote kwa pamoja; tu wana na binti za Adamu. Tunakua na kusitawi kama maua mazuri ya shambani. Na kisha baada ya muda si mrefu, tunazeeka na hatimaye tunakufa, ni kama vile maua ya nyikani, ambayo pamoja nauzuri wake hufifia, husinyaa na kufa. Hili linawapata watu wote tangu Adamu. Na kama hilo ndilo lingekuwa tumaini letu, maisha ya ngekuwa kitu kibaya mno. Ni kitu gani sasa kilichopo kinachoweza kuyafanya maisha yawe ya thamani na kutupatia matumaini ya uzima wa milele? Ni neno la Mungu, Biblia inayodumu milele (soma 1 Petro 1:24 –25).
Hatuwezi kuanza tukiwa watoto wachanga mno kujaribu kubadili njia zetu. Mawazo ya mwili na matendo ya mwili yanakuja kiurahisini rahisi sana kuwa wachoyo, wasio na mawazo, wasio wema, wavivu, wasio tii, na kadhalika. Mungu anatutaka tubadili tabia zetu kutoka katika njia hizo za kimwili na kuwa watoto wacha Mungu-watiifu, wema, wakarimu, wenye mawazo, wenye bidii na wasio jipenda wenyewe, kusoma na kuyafikiria maneno ya Mungu kila siku kunaweza kutubadilisha, kwani lilikuwa neno lake Mungu katika akili ya Yesu Kristo lililomwezesha kuwa mtiifu kamili kwa Baba yake.
MASWALI:
Majibu mafupi
- Je, Yohana alipokua aliishi wapi?
- Je,ni nini kilikuwa chakula cha Yohana na mavazi yake?
- Je, Yohana alikuwa akiandaa njia kwa ajili ya nani?
- Je, Yohana aliwaambia watu kuwa inawapasa wafanye nini?
- Je, Yohana alisema nini wakati Yesu alipomwambia ombatize?
- Je, Yesu alimwambia nini Yohana kuonyesha kuwa ni kwanini alitaka abatizwe?
- Yesu alibatizwa wapi?
- Sauti kutoka mbunguni ilisema nini?
- Ni kwa jinsi gani mawazo ya Mungu ni tofauti na mawazo ya wanadamu
- Ni wapi tunaweza kujifunza mawazo ya Mungu na njia za Mungu?
Majibu ya Kina
- Eleza jinsi Yohana alivyowaandaa watu kwa ajili ya kuja kwa masihi.
- Eleza nini kilitokea waketi Yesu alipobatizwa?
Majibu ya nyongeza
- (a) Ni nini kinachowatokea “wote wenye mwili” (yaani, wanaume na wanawake
wote)?
(b) Ni nini kinachodumu milele na kinaweza kutupatia maisha ya milele?
(c) Tutakuwa watu wa aina gani iwapo tutasoma Neno la Mungu na kufikiria kila
siku?