CSSA 1-4-03 - JESUS CALLS HIS FOLLOWERS

Swahili

78. YESU ANAWAITA WAFUASI WAKE

“Wakaacha vyote na kumfuata yeye”

 

Shabaha

Kuonyesha namna Yesu alivyoanza kuchagua wafuasi wake. Yesu alikuwa na umri wa miaka thalathini. Alikuwa ana miaka mitatu na nusu zaidi alipoanzakuhuburi kuwafundisha wana wa Israeli injili-habari njema kuhusu ufalme wa Mungu . Mnano muda huo aliwavuta wanaume kumi na mbili kuwa karibu naye, kusikia maneno yake na kuona miujiza ambayo Mungu alikuwa amempatia nguvu ya kuitenda. Baadaye, alipoondolewa kwao, hawa wanaume iliwapasa kuendelea na kazi ya kuhubiri injili.

 

Yohana 1:35 – 51; Luka 5:1 – 11, 27 – 28; 6:13- 16.

 

 

WANAFUNZI WA YOHANA WANAZUNGUMZA NA YESU Yoh. 1:20 – 42

     

Majuma sita yalikuwa yamepita tangu Yesu alipobatizwa. Viongozi wa wayahudi kwa kweli walikuwa wametatizwa waziwazi na yale yaliyokuwa yanatendeka. Waliwatuma baadhi ya makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu kumwuliza Yohana mbatizaji kama yeye ndiye aliyekuwa Kristo. Jibu la Yohana lilikuwa bayana “Mimi siye Kristo” (mstari 20). Aliwambia habari za mtu mmoja ambaye angekuja baada yake na ambaye alikuwa mkuu kuliko yeye. Yohana sasa alimfahamu huyu ni nani, lakini Yesu alikuwa ameshaondoka yapata kama majuma sita, naye Yohana alikuwa akimngoja Yesu kuja kujidhirisha kwa watu.

 

Siku moja baada ya haya Yohana akamwona Yesu akirudi kutoka jangwani, alipokuwa anamsogelea Yohana,Yohana akamtambulisha kwa wanafunzi wake, akisema “Tazama Mwana- kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu” (mstari 29). Wanafunzi wa Yohana walisikiliza kwa makini sana maneno yake hayo.

 

Siku iliyofuata wakati Yohana mbatizaji alipokuwa amesimama pamoja na wanafunzi wake wawili, Andrea (nduguye na Simoni Petro) na Yohana, alimwona Yesu na kwa mara nyingine tena akamtambulisha Yesu kuwa ni “Mwana-kondoo wa Mungu” (mstari36). Na kwa hiyo Andrea na Yohana wakamfuata Yesu, akawaalika waende naye nao wakazungumza naye usiku kucha. Fikiria jinsi walivyo kuwa na bidii ya kusikiliza maneno yake.

 

Andrea alikuwa na shauku ya kumpata ndugu yake na kumwelezea habari hizi za kusisimua “Tumemwona Masihi” (mstari 41). Na wakati Yesu alipomwona Simoni, alisema, “Wewe u Simoni mwana wa Yohana, utaitwa Kefa” (mstari 42) yaani Petro. Yesu alijua kwamba huyu kijana angebadilishwa na yote aliyosikia na kuona. Jina lake pia lingebadilishwa na kuitwa Petro, ikimaanisha jiwe au mwamba, kwani angekuwa imara kama jiwe katika kumtumikia Bwana na kuwa kiongozi kati ya wafuasi wake.

 

YESU ANAKWENDA GALILAYA Yohana 1:43 – 51.

 

Siku iliyofuata Yesu alielekea kaskazini huko Galilaya kule alimkuta Filipo na akamwambia, “Nifuate” (mstari 43). Filipo akajiunga na kundi hilo dogo naye baadaye akaenda na kumkuta rafiki yake Nathaniel. Filipo pia alikuwa na furaha sana, “Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika Torati, na manabii,Yesu mwana wa Yusufu mtu wa Nazareti ” (mstari 45). Nathaniel alikuwa na mashaka sana, alifahamu kutokana na kujifunza mambo ya manabii kwamba masihi angetokea Bethelehemu (Soma Mika 5:2, ambaye tunaelewa yalitimia wakati wa kuzaliwa Bwana Yesu). Lakini Filipo alikuwa amemwona Kristo naye akamhimiza rafiki yake “njoo na uone” (mstari. 46). Na wakati Yesu alipomwona Nathaniel, alimtambua mara moja kuwa ni mtu mcha Mungu na kijana mwaminifu,Bwana akasema “Kabla Filipo hajakuita ulipokuwa chini ya mtini nilikuona” (mstari. 48). Nathanaeli alikuwa mtu mwaminifu, naye alijua kwamba Filipo ni lazima alikuwa mkweli,akasema; “Rabi (yaani mwalimu) wewe ndiye Mwana wa Mungu; wewe ndiwe Mfalme wa Israeli” (mstari 49). Ni jinsi gani Nathanaeli alivyokuwa na ufahamu wa kushangaza tayari , kumtambua Yesu kuwa ni Mwana wa Mungu, yeye ambaye Daudi aliahidiwa kuwa atakuwa mfalme juu ya Israeli (soma 2 Samweli 7:12-13).

 

WAVUVI WA WATU: Luka 5:1 – 11.

 

Simoni, Andrea, Yakobo na Yohana walikuwa wavuvi wa samaki. Walikuwa wamekesha kuvua katika ziwa la Galilaya, lakini hawakuvua samaki. Na ilipokuwa asubuhi wakarejesha mashua zao na kuzisafisha na kuzishona nyavu zo ufukweni. Yesu alikuwa akihubiri kando ya ziwa na kundi la watu lilikuwa kubwa kiasi cha kumfanya akae ndani ya mashua ya Petro. Akamwomba asogeze ndani ya maji mbali kidogo na ukingo wa ziwa ili kwamba awafundishe watu akiwa ndani ya mashua. Alipokuwa amemaliza kusema, akamwambia Petro “pelekeni mashua, mtweke mpaka kilindini, na mshushe nyavu zenu” (mstari 4). Petro aliona kuwa haikuwa na maana yoyote, lakini hata hivyo, kwa kuwa Bwana alikuwa amemwambia, angefanya hivyo. Na mara walipozishusha nyavu zao zikajaa samaki hata ikiwa kwamba nyavu zilianza kukatika, wakamwita Yakobo na Yohana kuja kuwasaidia, upesi kukawa na samaki wengi mno hivi kwamba mashua, zote mbili zikaanza kuzama.

 

Simoni kwa kuona hivyo mara moja akatambua kwamba huo ulikuwa ni muujiza. Namna alivyoaibika sasa kwani alikuwa akiendelea kushughulika kusafisha mashua na kushona nyavu zake wakati Yesu alipokuwa akifundisha watu. Ilimpasa kuwa makini kumsilize Iwapo angehitaji kumfuata Yesu, ilimpasa kuvihesabu vitu vingine vyote kuwa havikuwa vya maana, Bwana, akamwambia “Usiogope”, kwa maana “tangu sasa utakuwa ukivua watu” (mstari 10). Mungu angewapatia chakula chao cha kila siku, kama mwujiza huu ulivyoonyesha waziwazi, iliwapasa kutumia muda wao wakiwa na watu, wakiwafundisha kuhusu ufalme wa Mungu. Na hivyo wakazileta mashua zao hadi nchi kavu na “kuacha vyote, na wakamfuata Yesu”.

 

KUCHAGUA MITUME KUMI NA MBILI: Luka 6:12 – 16

 

Na watu wengi wakamfuata Yesu, wakasikiliza kwa makini mafundisho yake. Hawa waliitwa “wanafunzi” ikimaanisha “wanaojifunza au wale wanaofundishwa”. Kati yao wote, Yesu alichagua thenashara kuwa “mitume”. Mtume ni yule aliyetumwa akiwa na ujumbe, usiku uliotangulia kabla ya kuwachagua hawa kumi na mbili, Yesu alipanda mlimani akaenda kumwomba Mungu. Ulikuwa uamuzi ulio muhimu sana naye alimhitaji Mungu amwongoze, alikesha usiku kucha mlimani, akisali. Na ilipokuwa asubuhi alifika na akawaita wanafunzi wake na kuwateua kumi na mbili, na orodha ya Mitume hawa inapatikana katika Mathayo 10:2 – 4; Marko 3:16; Matendo 1:13,26; na Luka 6:13 – 16.

 

Hao mitume Thenashara ni: -

 

  1. Simon Petro
  2. Andrea, ndugu yake
  3. Yakobo mwana wa Zebedayo
  4. Yohana nduguye Yakobo
  5. Filipo
  6. Tomaso
  7. Mathayo
  8. Yakobo mwana wa Alfayo
  9. Thadayo (aliyeitwa Lebao au Yuda wa Yakobo)
  10. Simoni (aliyeitwa Mzelote au Mkananayo)
  11. Yuda Iskarioti (ndiye aliyemsaliti Yesu)
  12. Bartolomayo.

 

Hawakuwa ni watu mbao dunia ingewachagua kuwa viongozi wa dunia. Watu hawa hawakuwa na elimu au utajiri, lakini Mungu aliijua mioyo yao najinsi ambavyo wangekuwa waalimu wazuri sana. Ni mmoja kati yao aliyedhihirika kuwa hakuna na imani-Yuda Iskariote, ambaye ndiye aliyemsaliti Bwana. Ambaye hatimaye nafasi yake ilikuja kuchukuliwa na Mathias (Soma Mstendo ya Mitume1:26).

 

KUTUMWA KWA WALE KUMI NA MBILI: Mathayo 10:5 – 8

 

Bwana akawatuma wale mitume kumi na mbili kuhubiri wakisema; “Ufalme wa mbinguni umekaribia” (mstari 7). Huu ndiyo uliokuwa ujumbe ambao ilibidi utangazwe kwa wana wa Israeli wote. Bado haukuwa wakati wa watu wa mataifa kusikia ujmbe huu, lakini Yesu akawaambia, “Kuwaendea kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli” (mstari 6). Yeye alikuwa ndiye mchungaji nao Kondoo ilipasa wavutwe kwake. Aliwapa pia nguvu za kufanya miujiza, ili kwamba watu waliohubiriwa wapate kuamini kwamba ujumbe ule uliotoka kwa Mungu. “Ponyeni wagonjwa, takaseniwenye ukoma, fufueni wafu, toeni pepo, mmepata bure toeni bure” (mstari. 8).

 

THAWABU YAO: Mathayo 19:28 – 29.

 

Ni jukumu kubwa lililoje mitume walikuwa nalo, lakini ni heshima ya jinsi gani waliyokuwa nayo pia. Katika uhai wao wote waliteseka kwa ajili ya mambo mengi kutokana na imani yao, walakini Yesu wakati mmoja aliwaambia kuhusu kazi nzuri ajabu watakayoifanya katika ufalme kwa sababu “waliacha vyote na kumfuata yeye”. “ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli” (mstari 28). Lo, ni tumaini la ajabu kiasi gani itakuwa! Wote wanaoacha vitu vyote vya maisha haya na kumfuata yeye watapata baraka nyingi, baraka iliyo kuu kuliko zote itakuwa ni “Kuurithi uzima wa milele” ( mstari.29).

 

FUNDISHO KWETU

Ni lazima tujaribu kuwa wanafunzi wa Yesu, tukijifunza njia zake na kusikiliza neno la Mungu kwa uangalifu, ili tumtii Mungu. Ili tuweze kutenda hili inatupasa kuyaacha mambo yale ambayo yanatuchukulia muda wetu mwingi.

 

Yesu alizungumzia thawabu kuu watakayo pewa wale wote ambao “wanaacha vyote na kumfuata yeye” akasema ya kwamba watapokea mara mia, nao watarithi uzima wa milele (Mathayo 19:29). Kama tutaacha vitu vya dunia na kumweka Mungu kuwa wa kwanza maishani mwetu na kumtii, atatunza na kutubariki sasa. Na kisha Yesu atakaporudi tutapokea uzima wa milele katika Ufalme.

 

MASWALI

Majibu Mafupi

 

  1. Wakati Yohana mbatizaji alipomtambulisha Yesu kwa wanafunzi wake, alisema nini?
  2. Ni akina nani walikuwa wanafunzi wa kwanza kumfuata Yesu?
  3. Yesu alisema jina la Simoni lingebadilishwa na kuwa lipi? Lina maana gani?
  4. Nathanieli alimwambia nini Yesu?
  5. Wanafunzi wanne walikuwa wavuvi wa samaki, Yesu aliwaambia kuwa tangu wakati

huu watavua nini?

  1. Je, neno “Mwanafunzi” lina maana gani?
  2. Je, neno “Mtume” lina maana gani?
  3. Je, Mitume hao kumi na mbili walipewa nini ili kuwasaidia kuwaaminisha watu juu ya

ujumbe wao?

  1. Ni thawabu gani Yesu aliwaahidi mitume wale kumi na wawili?
  2. Je, tutapata nini iwapo tutaacha vitu vyote na kumfuata Yesu?

 

Majibu ya Kina

 

11. (a) Eleza habari ya mwuujiza wa wavu kujaa samaki.

      (b) Ni fundisho gani Yesu alikuwa akiwapatia wanafunzi wake?

 

12.  Yesu aliwachagua wanaume kumi na wawili kuwa rafiki wa karibu na wasaidizi wake.

  1. Je,Yesu alifanya nini kabla hajawachagua watu hawa?
  2. Je, majina yao ni yapi?

 

 

Swahili Title
078 YESU ANAWAITA WAFUASI WAKE
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type