79. ARUSI YA KANA
“Mwanzo huu wa miujiza, Yesu alioufanya huko Kana ya Galilaya; na akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini”.
Shabaha
Ni kuonyesha namna Yesu kwa mara ya kwanza alivyoonyesha uwezo wake katika mwuujiza wa kugeuza maji kuwa divai.
Uwezo aliokuwa nao Yesu, nguvu za Roho Mtakatifu, alikuwa amepewa na Mungu wakati alipobatizwa. Wanafunzi wake walikuwa hawajamwona akitumia nguvu hii. Wao waliamini yale Yohana mbatizaji aliyowaambia, ya kuwa alikuwa “ndiye mwana Kondoo wa Mungu” (Yohana 1:36) nao walimfuata.Walisikiliza neno lake na kufanyika wanafunzi wake, lakini walipoiona miujiza yake, walithibitisha kwamba Yesu ndiye Kristo .
Yohana 2:1 – 11.
DIVAI INAKWISHA:Yohana 2:1– 4
Muda mfupi sana baada ya Yesu kukusanya wafuasi wake wachache na wakiwa wamemzunguka, alialikwa kwenye arusi huko Kana ya Galilaya. Mama yake Yesu naye alikuwepo na wanafunzi wake walialikwa pia. Arusi kila wakati lilikuwa tukio la furaha. Nyakati zile sherehe na fuaha pamoja na wana ukoo (familia) na marafiki mara nyingi lililokuwa linadumu kwa siku nyingi.
Kitu fulani kilitokea kwenye arusi hii ambacho kingeweza kuharibu furaha ya tukio na kuleta aibu kwa mwenyeji-ni divai kuisha kabla sherehe haijaisha. Mariamu alipogundua hali hii ya kuaibisha, alimwambia Yesu, “Hawana divai” (mstari 3). Yesu alitambua kwamba Mariamu alitumaini kuwa yeye angeweza kusaidia naye akamwambia Mariamu; “mwanamke nina nini mimi nawe?” (mstari 4). Alitaka mama yake atambue kwamba kila jambo atakalolitenda kuanzia wakati huo na kuendelea, tangu ubatizo wake, alitenda ili kumpendeza Mungu. Ingawaje kwa vyovyote alikuwa ana mpenda mamaye sana;na alipenda kumpendeza ilimpasa kufanya kazi ya Babaye tu. Hata hivyo haukuwa wakati wake wa kujulikana hadharani kwa watu wote. Ingawaje alitenda mwujiza wakati huu ikiwa dalili ya kwanza kwa wanafunzi wake na wale waliokusanyika arusini, kwamba yeye alikuwa ndiye Kristo.
MAJI YANAGEUKA KUWA DIVAI. Yohana 2:5 –10
Inaonekana Mariamu alielekea kufikiri kwamba Yesu angesaidia,Mariamu akawambia watumishi; “Lolote atakalo waambia, fanyeni” (mstari 5). Kwenye maingilio ya nyumba kulikuwa na mabalasi makubwa sita ya maji, yalikuwepo pale ili kwamba wageni wanapofika waweze kuosha mikono yao kabla ya kula siyo kwa sababu walikuwa wachafu, lakini ilikuwa desturi ya wayahudi (Soma Marko 7:3). Yesu, akawambia watumishi “Yajalizeni hayo mabalasi maji”. Walipokuwa wameyajaza kabisa hadi juu kabisa akawaambia wayachote na kumpelekea mkuu wa meza. Ilionekana kama ni kinyume cha utaratibu wao ajabu lakini hata hivyo Mariamu alikuwa ameshawaambia kutenda lolote ambalo Yesu angewaambia . Kwa mshangao wao, walipochota-hayakuwa maji, bali divai kutoka kwenye mabalasi yale makubwa ambayo wao wenyewe walikuwa wameyajaza maji. Mkuu wa meza alipoionja divai hiyo, alimpongeza bwana arusi kwa kuwapatia divai iliyo njema sana. Watu wengi huleta divai iliyo bora mwanzoni, “lakini”, mkuu wa meza akasema “wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa” (mstari 10).
KWA NINI YESU ALIFANYA MIUJIZA: Yoh. 2:22
Nguvu za Mungu ni kuu zaidi ya nguvu yoyote ambayo mtu anaweza kuwa nayo. Unaweza kukumbuka wakati Mungu alipopeleka mapigo juu ya Farao na kwa Wamisri wote na kwamba wana mazingaombwe walijaribu kumnakiri Musa. Kwa ujanja wao, ilionekanana mwanzoni kana kwamba wao pia waliweza, lakini hatimaye hata wao ilibidi wakubali kwamba zilikuwa ni nguvu za Mungu zikitenda kazi ndani ya Musa. Hivyo katika miujiza Yesu aliyoitenda alikuwa akiwaonyesha watu ni kiasi gani cha nguvu Mungu alikuwa amempatia. Alikuwa ni Mwana wa Mungu naye Mungu alikuwa pamoja naye. Katika Matendo ya Mitume 2:22 Petro anamwelezea yeye kuwa ni “Yesu wa Nazareti; mtu aliyedhihirishwa kwenu kwa miujiza na maajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu”. Katika Yohana 2:11 tunaambiwa: “Mwanzo huu ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini”. Hivi ndivyo hasa Mungu alivyokusudia watu waliiona miujiza na kuamini maneno yake. Ni kwa njia hii Bwana Yesu Kristo aliwafundisha watu kumpa utukufu Mungu, kwani Mungu ndiye aliyempa nguvu za Roho mtakatifu.
FUNDISHO KWETU.
Katika miujiza yote aliyoifanya Yesu, alisimama kuwafundisha watu masomo maalumu. Huu ndiyo uliokuwa mwujiza wa kwanza alioutenda Yesu nao ulikuwa na fundisho kubwa na muhimu sana. Mabalasi ya maji yalikuwapo pale “kwa desturi ya utakaso wa Wayahudi (mstari6), maji yalikuwa kwa ajili ya kuosha mwili, yaliwafanya wajione wasafi, lakini hayo yasingeweza kumfanya mtu kuwa safi ndani, yaani, ndani ya moyoni mwake”, Yesu alifundisha kwamba ni lazima tuwe “wasafi moyoni” (Math 5:8). Maneno ambayo Yesu aliyasema yangeweza kumbadilisha mtu na kumfanya kuwa safi ndani. Tunaposoma Neno la Mungu na kulitafakari na kulitunza mioyoni mwetu, linatubadilisha. Basi nasisi tulisome Neno hilo kila siku, naye Mungu atafurahi kuona mabadiliko hayo ndani yetu.
MASWALI
Majibu Mafupi.
- Ni wapi Yesu alialikwa kuhudhuria sherehe ya arusi?
- Ni nani waliokwenda naye?
- Divai lipokwisha, ni nani aliyemwomba Yesu asaidie?
- Yesu aliwaambia watumishi wafanye nini?
- Ni jambo gani la ajabu lilitokea kwenye maji ndani ya mabalasi?
- Mkuu wa meza alisema nini?
- Ni kwa jinsi gani Yesu aliweza kuyageuza maji yawe divai katika sherehe ya arusi ?
- Ni kwa nini Yesu alifanya miujiza?
Majibu ya Kina
- Eleza habari ya muujiza wa kwanza alioutenda Yesu huko Kana ya Galilaya
- (a) Eleza unavyofahamu kuhusu mabalasi yale sita katika sehemu ya kuingilia
nyumba
(b)Yesu alibadilisha maji kuwa divai.Ni kwa jinsi gani Neno la Mungu linaweza
kutubadilisha?