CSSA 1-4-05 - NICODEMUS, THE PHARISEE, COMES TO JESUS

Swahili

80. NIKODEMO, AMBAYE NI FARISAYO ANAKUJA KWA YESU

“Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona Ufalme wa Mungu”

 

Shabaha

Ni kuonyesha jinsi Yesu alivyolitakasa hekalu na kumfundisha Nikodemu njia ya wokovu.

Baada ya arusi ya Kana, Yesu alikwenda Kapernaumu kwa muda mfupi pamoja na Mariamu, mama yake, na ndugu zake na wanafunzi wake. Na kutoka huko alikwenda Yerusalemu kuitunza Pasaka. Ilikuwa ni hapa ambapo alianza kuwaonyesha watu jinsi walivyokwenda kinyume na ibada ya kweli ya Mungu. Hapa vile vile, alikutana na farisayo aliyekubali kusikiliza kwa makini maneno yake.

 

Yohana 2:12-16; 3:1-21

 

YESU ANATAKASA HEKALU: Yohana 2:13 –16

 

Hekalu hili lililokuwa Yerusalemu lilikuwa ndilo hekalu la tatu kujengwa pale. Kwanza, lilikuwepo Hekalu la Sulemani (1 Wafalme 5:5) na baadaye, wakati wana wa Israeli waliporejea kutoka utumwani, hekalu la pili lilikuwa limejengwa wakati Zerababeli alipokuwa mtawala (Soma Ezra 5:2). Sasa, miaka mingi baadaye, hekalu la Herode lilijengwa mahali pale pale lilikingamana na bonde la kidroni, lilikuwa jengo la kupendeza sana, ambalo lilijengwa kwa miaka arobaini na sita, na wayahudi walijivunia sana hekalu hili. Ni mahali hapa wayahudi kutoka pande zote za nchi walikuja kumwabudu Mungu na kutunza sikukuu ambazo Mungu alizowamuru kutunza.Ni wakati huu Yesu alipokuja kuishika pasaka, alichokiona kilimfanya akasirike sana.

 

Badala ya kuwa wakimya, waadilifu na wenye mawazo ya nia kwa Mungu wakati wa kuabudu, aliona ndani ya hekalu “wauzaji wa ng’ombe na kondoo na njiwa, na wabadilisha fedha wakikaa” (mstari 14). Pale palikuwepo mvumo wa kutisha wa kelele na mabishano yakizidi kelele za wanyama, wengine wakiuza, wengine wakibishana kuhusu bei huku wakitoa fedha za kigeni za wasafiri ili kubadilisha katika fedha za nchini waweze kununulia sadaka na matoleo. Wote kwa pamoja walikuwa wapenda fedha waroho, mioyo yao hawa watu ilikuwa mbali na Mungu wao. Ilimfanya Yesu aghadhabike kweli kweli.

 

Akasokota kikoto cha kamba, na kuwafukuza wale wafanya biashara nje ya hekalu, na kondoo na dume la ng'ombe lililohasiwa. Kisha akazimwaga fedha za wenye kuvunja (kubadilisha) fedha na kuzipindua meza zao. Akawaamrisha watu wenye njiwa na waondoke. Nao, walikimbia mbele yake, huku wakifahamu kwamba walikuwa wamevunja sheria za hekalu. Sauti yake yenye hasira iliwafuata “Msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara” (mstari 16). Yalikuwa maneno ya nguvu, lakini ya kweli. Wanafunzi wake walipoona yaliyotokea walikumbuka maneno ya Zaburi 69:9 “Wivu wa nyumba yako umenila”. Maneno haya yaliyokuwa yanasema kuhusu upendo mkuu wa Kristo kwa Baba yake uliomjaza chuki ambayo watu wa Mungu wanapaswa kuwa nayo kwa ajili ya nyumba ya Mungu ambayo adabu imekosekana.Na kwa hiyo akaanza kuitakasa nyumba ya Baba yake. Miaka mitatu baadaye alipokuwa amekaribia siku za kumaliza kazi yake, Yesu Kristo alikwenda tena Hekaluni na kuona aina ile ile ya vitendo (Luka 19:45 – 46). Wana wa Israeli hawakuwa wamejifunza somo 1 (Soma somo la 19).

 

NIKODEMO ANAMTEMBELEA YESU USIKU: Yohana 3:1 – 5.

 

Yesu akakaa Yerusalemu kwa muda kadhaa, akitenda miujiza kati ya watu ambao walikusanyikia katika mji. Wengi wao waliamini walipoiona miujiza aliyoifanya. Yesu akatambua kwamba alikuwa akipendwa sana na watu wengi, lakini hakuwaamini, kwani alijua jinsi watu wanavyo weza kubadilika haraka.

 

Watawala wa Israeli walikuwa hawachangamani na watu wa kawaida. Walisimama kando na kuangalia kwa mbali. Hata hivyo alikuwapo mtu mmoja kati yao, farisayo aliyeitwa Nikodemo, aliyeangalia aliyoyatenda Yesu na kuyafikiria kwa makini yale Yesu aliyoyasema. Nikodemo alikwenda kwa Yesu usiku kujifunza zaidi juu ya huyu mtu aliyesema kwa mamlaka namna ile ya kutenda miujiza ambayo hakuna mtu wa kawaida yeyote awezaye kuifanya. Nikodemo bila shaka alifikiri haingekuwa busara kwake, akiwa mtawala wa wayahudi kuonekana akimtembelea Yesu baada ya msukosuko aliouanzisha hekaluni. Hivyo alikwenda usiku, “Rabi” (Yaani “Mwalimu”) akasema, “Twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye” (mstari 2). Nikodemu alikuwa mkweli, ilikuwa ni dhahiri kuwa Mungu alikuwa na Yesu.

 

KUZALIWA KWA MAJI

 Hata hivyo,Yesu,aliendelea kuzungumza kuhusu jambo fulani ambalo Nikodemu hakulielewa kabisa “Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu”, Yesu akasema (mstari 3.). Sasa Nikodemo alielewa ya kwamba mtu anaweza kuzaliwa mara ya pili. Basi Yesu alimanisha nini? Akaendelea kufafanua kuwa kuna njia nyingine ambayo tu naweza kuzaliwa. “Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona Ufalme wa Mungu” Watu wote wanazaliwa kwa mara ya kwanza wakiwa watoto wachanga, lakini, mbele za macho ya Mungu lililo la muhimu sana ni kuzaliwa mara ya pili. Watu wakifikia kulielewa Neno la Mungu na kuamua kutubu (yaani, kubadili njia) na kumtii Mungu, na kubatizwa. Kwa njia hili wanamuonyesha Mungu nia yao ya kuacha matendo yao ya kale ya kujipendeza wenyewe, na badala yake, hutaka kuanza njia mpya ya uzima ya kumpendeza Mungu. Ni maisha mpya yanayoanzia siku ya ubatizo. Na hivyo ubatizo unaitwa “kuzaliwa kwa maji” ni Neno la Mungu tu liwezalo kumbadilisha yeyote na kumfanya kuwa tayari kwa ubatizo. Mtu yeyote yule anaweza kuzama majini na kuibuka tena lakini atakuwa hajabatizwa isipokuwa Neno la Mungu limemwezesha kubadili njia zake. Mabadiliko kwanza huanzia akilini mwetu. Hivyo inatupasa kujaza akili zetu na Neno la Mungu.

 

KUZALIWA KWA ROHO

Yesu akamwambia Nikodemo kwamba isipokuwa “mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho hawezi kuingia ufalme wa Mungu” (mstari 5). Alikuwa anaongelea juu ya mwanzo mwingine mpya. Mara hii alikuwa akiongelea lile badiliko la utukufu ambalo litatokea juu ya miili yetu wakati tutakapopewa uzima wa milele. Hili litatokea Yesu atakaporudi, baada ya ufufuo, hili ndilo tumaini kuu tulilonalo iwapo tunapenda Neno la Mungu.

 

Aina hizi za kuzaliwa zitatokea tu ikiwa Neno la Mungu linatubadilisha sisi. Jinsi Biblia, Neno la Mungu lilivyo zuri ajabu,hakika linapoweza kumbadilisha mtu mmoja kati yetu na akawa kiumbe kipya, anayestahili kuingia katika Ufalme wa Mungu.

 

HATIMAYE NIKODEMO ANAAMINI

 

Nikodemo hakufikiria njia hii kabla. Aliona ilikuwa ni vigumu kuelewa. “Yawezaje kuwakanaje mambo haya? alimwuliza Yesu (mstari 9). Jibu la Yesu ni dhahiri kuwa lilimfedhehesha Nikodemu kidogo. “Wewe u mwalimu wa Israeli, na mambo haya huyafahamu?” (mstari 10). Mafarisayo wengi sana walikuwa na kiburi nao walichukia namna Yesu alivyowakosoa. Kiburi kinaweza kutupofusha na kutufanya tusiwe waaminifu, lakini Nikodemu hatimaye aliamini kwa moyo wake wote kuwa Yesu alikwa ndiye masihi aliyeahidiwa. Alikuwa msemaji kwa ajili ya Yesu wakati viongozi wa wayahudi walipowadhihaki wale waliomwamini (Soma Yohana 7:50 – 52). Ni Nikodemu, pia ambaye baadaye alimsaidia Yusufu wa Arimathaya kuuchukua mwili wa Yesu kutoka msalabani na kuuweka kaburini (Yohana 19:39 – 42).

 

FUNDISHO KWETU.

Yesu alizunguka katika nchi ya Israeli akitenda mema mengi lakini watu mara nyingine walichukizwa na maneno aliyoyasema kwa sababu aliwaonyesha makosa yao. Vitu kama uchoyo, kiburi na kupenda fedha vilimchukiza sana. Aliwafukuz. wafanyabiashara warchoyo katika nyumba ya Baba yake kwa sababu alichukia matendo yao aibu,maana walipenda fedha kuliko kumpenda Mungu.

 

Ni rahisi sasa siku hizi kuwa wachoyo na wenye kutamani,kila wakati kwa kutaka vitu. Siku hizi maduka yamejaa vitu vipya vizuri na vya kupendeza kuvinunua. Watoto shuleni kila wakati wana vitu vipya vya kuonyesha au kuongelea, vitu ambavyo vinanunuliwa kwa fedha. Hata hivyo, tuna kitu cha thamani sana, na kizuri ajabu ambacho kinadumu milele, na wala fedha haiwezi kukinunua (Soma Isa. 55:1 –2). Mwandishi wa busara wa Mithali anayo mengi ya kusema kuhusu mambo haya; “Si afadhari kupata hekima kuliko dhahabu? Naam, yafaa kuchagua ufahamu kuliko fedha” (Mithali 16:16). Kwa masikitiko, tunajifunza katika somo linalofuata, ya kuwa ilikuwa ni kwa ajili ya “kupenda fedha” kulikosababisha Yuda amsaliti Bwana Yesu (Marko 14:10 – 11), soma somo la 22).

 

Yohana mbatizaji alikuwa amewakosoa mafarisayo na masadukayo kwa kiburi chao. Walifikiri kuwa hawakuwa na haja ya kutubu (Mathayo 3:7 – 9), lakini Mungu anawachukia “moyo wenye kiburi” (Mithali 16:5). Ni kwa sababu ya kiburi chao, mafarisayo na masadukayo walikataa kuamini kwamba Yesu alikuwa ndiye Kristo. jinsi alivyokuwa na hekima Nikodemo kumsikiliza Yesu na kumwamini. “Heri aliyemfanya BWANA kuwa tumaini lake, Wala hakuwaelekea wenye kiburi, Wala hao wanaogeukia uongo”. (Zaburi 40:4. Hii ni zaburi ambayo inazungumzia kuhusu mateso ya Kristo mikononi mwa Wayahudi waovu). Inatupasa kufuata mfano huo iwapo sisi, pia tunataka kuingia katika ufalme wa Mungu.

 

MAELEZO YA NYONGEZA: Yohana 3:14 – 15.

 

Kuna kitu kingine ambacho Yesu Yesu alimwambia Nikodemu kuonyesha mbele jinsi Yesu atakavyosulubiwa msalabani “Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hanabudi kuinuliwa” (mstari 14). Je, unakumbuka habari ya tauni ya nyoka waliowauma Waisraeli kule jangwani na wakufa? Mungu alimwambia Musa kutengeneza nyoka wa shaba na kumwinua juu ya mti, na yeyote aliyemtazama yule nyoka wa shaba kwa imani, yaani, kuamini kwamba Mungu angewaponya, alipona (Soma Hesabu 21:6–9). Yesu angeinuliwa juu, akigongomewa mtini na watu waovu, lakini mtu yeyote aliyeona hayo na akamwamini yeye, ataokoka. “Ili kila aaminiye asiangamie, bali awe na uzima wa milele” (mstari15). Ni tumaini la ajabu lilioje tunapewa, siyo kwa Nikodemo peke yake, bali nii kwa dunia nzima.

 

 

MASWALI

Majibu Mafupi

 

  1. Ni kwa nini watu walikwenda katika hekalu Yerusalemu?
  2. Yesu alipoingia Hekaluni aliona nini kilichomfanya akasirike?
  3. Yesu alisema nini alipowafukuza ndani wafanya biashara?
  4. Ni nani aliyekwernda kumwona Yesu usiku?
  5. Je, Nikodemu aimfikiria Yesu kuwa ni nani?
  6. Ina maana gani kuzaliwa kwa maji?
  7. Je, mtu inampasa afanye nini kabla hajabatizwa?
  8. Ni lini tutakapo zaliwa kwa Roho?
  9. Ni kitu gani kinatubadilisha hivi hata tunaweze kuzaliwa kwa maji na kwa Roho?
  10. Je, Nikodemo alimwamini Yesu?

 

Majibu kwa Kina

  1. Fafanua: -

      (a) Ni jambo gani Yesu aliloliona hekaluni lililosababisha akasirike?

      (b) Alitenda nini kuhusiana na hilo?

 

12. Kutokana na somo hili tunajifunza mambo mawili ambayo Mungu anayachukia -

      kupenda fedha na kiburi

      (a) Tunajifunza nini juu ya kupenda fedha?

      (b) Ni kwa vipi Nikodemo ni mfano kwetu kuhusu kiburi chetu?

 

Majibu ya Nyongeza

 

1. Je.Yesu alikuwa akijaribu kumfundisha nini Nikodemu aliposema “Mtu asipozaliwa

    kwa maji na kwa Roho hawezi kuingia ufalme wa Mungu?”

  1. Ni kwa nini Yesu alimkumbusha Nikodemu kuhusu habari .. ya nyoka juu ya mti?

 

 

Swahili Title
080 NIKODEMO, AMBAYE NI FARISAYO ANAKUJA KWA YESU
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type