CSSA 1-4-06 - THE NOBLEMAN'S SON

Swahili

81. MWANA WA DIWANI

“Na mtu yule akaaamini neno ambalo  Yesu alimwambia , naye akaenda zake”

 

Shabaha

Nikuonyesha jinsi Diwani alivyomwamini Yesu na mwanaye akapona. Baada ya kutumia siku mbili akizungumza na watu wa wasamaria, Yesu alikwenda kasakazini huko Galilaya na kundi dogo la wanafunzi wake. Akarudi tena Kana, ambako alikuwa amefanya mwujiza wake wa kwanza wa kugeuza maji kuwa divai. Kwenye tukio lile wengi waliamini walipoona ule mwujiza. Wakati huu Yesu alitazamia watu kuamini maneno waliyoyasikia akisema. Tutaona nguvu ya ajabu aliyokuwa nayo hasa.

 

Yohana 4:46 – 54

 

KILIO CHA KUOMBA MSAADA: Yohana 4:43 – 47

 

Wakati Yesu alipokuwa Kana, Diwani mmoja alikuja kwa haraka akitokea Kapernaumu, yapata umbali wa kilomita ishirini na tano. Hatuambiwi jina lake, lakini neno “diwani” linaonyesha kwamba alikuwa afisa wa utawala, pengine akimtumikia Herode Antipasi, aliyekuwa mtawala wa ile ya nchi. Mtawala huyu alikuja kumwona Yesu, kwa kuwa alikuwa na huzuni kubwa. Kwa kuwa mwanaye alikuwa mgonjwa sana. Na mara aliposikia kuwa Yesu alikuwa amerudi kutoka Yerusalemu kwenda Galilaya, kwa shauku alikwenda kumtafuta ilikumwomba msaada amsaidie. Mwanaye alikuwa mahututi sana ,akikaribia kufa naye akamwomba Yesu ili aende kumponya mwanaye. Umaarufu wa Yesu ulikuwa umeenea haraka kila mahali nchini. Mambo aliyoyasema na mambo aliyoyatenda Yerusalemu mara moja yalisababisha watawala wa kiyahudi kuwa na hasira na wivu. Wale waliokuja kutoka Galilaya kwa ajili ya sikukuu walipeleka habari za matukio haya kwenye miji yao ya nyumbani. Hivyo sasa aliporudi Galilaya, “Wagalilayawalimpokea, kwa kuwa wameyaona mambo yote aliyooyatenda huko Yerusalemu wakati wa sikukuu” (mstari 45). Na hapa Galilaya kulikuwa na msimamo tofauti kati ya watu. Walimkaribisha huku wakiwa na shaukukuonamiujizazaidi ambayoilisababisha awe umaarufu

 

MUUJIZA WA PILI HUKO KANA: Yohana 4:48 – 50.

 

Kwa hiyo yule mtawala akaja kwa Yesu, kwa kusudi hasa la kuomba msaada. Yesu akamwambia, “msipoona ishara na maajabu, hamtaamini kabisa” (mstari 48). Kumbuka jinsi Yesu alivyomkumbusha mama yake kwenye arusi ya Kana kwamba ilimpasa kutenda kazi ya Baba yake. Kazi yake ilikuwa kuhubiri Ufalme wa Mungu, ili kwamba watu waamini na kutubu. Kusudi la Yesu ilikuwa hasa kubadili mioyo na akili za watu Yule mtawala alipoyasikia maneno ya Yesu hakuweza kufikiri kiti kingine zaidi, bali mtoto wake aliyekuwa amekaribia kufa. Kakika mtu huyu, ambaye alikuwa amesikia mengi sana kumhusu yeye,angemsaidia “akamwambia, Bwana naomba ushuke kwangu mapema asijafa mtoto wangu” (mstari 49).

 

Yesu akamwambia “Enenda; mwanao yu hai. Mtu yule akalisadiki lile neno aliloliambiwa na Yesu, naye akashika njia” (mstari 50)

 

Bila shaka yule mtawala alibaki kusikiliza zaidi kuhusu Ufalme wa Mungu. Hili ndilo lilikuwa jambo muhimu ili kwamba aweze kuamini kuwa Yesu ndiye aliyekuwa Kristo na kubadilisha njia zake na kumpa Mungu utukufu. Jinsi mzigo mkuu ulivyoondolewa kutoka mabegani mwa maskini yule wakati aliposikia Yesu akimwambia, “Mwanao yu hai” alikwenda zake nyumbani moyo wake ukiwa umejaa shukrani na furaha.

 

DIWANI NA NYUMBA YAKE WANAMWAMINI YESU: Yohana 4:51 – 54.

 

Siku iliyofuata, wakati akisafiri kurudi nyumbani, watumishi wake wakakutana naye njiani na kumweleza habari njema “Mwanao, yu hai” (mstari51). Hili halikuwa la kumshitua yule mtawala, kwani alikuwa ameamini maneno hayo hayo ya Yesu. Aliwauliza watumishi wake ni muda gani mwanaye alipokuwa amepona. Wakamwambia, “Jana wakati wa saa saba homa ilimwacha” (mstari 52). Ulikuwa ndiyo wakati ambapo Yesu aliyasema maneno haya mazuri ajabu, “Mwanao yu hai”. Diwani yule alipoeleza habari yote kwa familia yake na watumishi wake, walishangaa na wao wote wakamwamini Yesu kwamba hakika alikuwa ndiye mwana wa Mungu.

 

FUNDISHO KWETU:

 

Yule Diwani alifahamu kwamba hakukuwawa na tumaini lolote kwa mwanaye isipokuwa tu Yesu awe tayari kumsaidia. Hiyo ndiyo iliyokuwa sababu ya kumwomba Yesu kufika Kapernaumu. Ilibidi afahamu fundisho ya kwamba BWANA ni Mungu kwa walio karibu na pia kwa waliombali (soma Yeremia23:23–24). Mungu anaposema, Neno lake hutendeka, hivyo Mungu alimpatia Yesu nguvu za kufanya miujiza na matendo ya uponyaji, na katika yote lililokuwa la yali muhimu ilikuwa ni yeye “kusema neno”

 

Inatubidi kamwe tusisahau ya kwamba yote aliyoyasema Mungu yatatendeka. Amesema kuwa Kristo atarudi na kufufua wafu (ambao ni mwujiza mkuu sana) na kuonyesha nguvu zake kuu duniani tena. Kama tutaliamini Neno lake kama yule Mtawala alivyofanya, tunaweza kufurahi wakati atakapokuja.

 

MAELEZO YA NYONGEZA

Yesu akamwambia yule mtawala, “Enenda; mwanao yu hai. Na yule mtu akaliamini neno lile alilolisema Yesu (mstari 50). Ni imani kubwa iliyoje aliyoionyesha yule Mtawala. Kuwa na “imani” inamaanisha “kuamini” ni kuthibitika katika akili zetu kwamba kitu fulani ni kweli. Habari za ajabu tunazozisoma katika Biblia zimejaa wanaume na wanawake wa imani. Ni watu walioamini kwamba Mungu alilolisema hakika yake litatimia. Tunasom katika Warumi10:17 kuwa “imani chanzo chake ni kusikia... Neno la Mungu” Tunaweza kujifunza kuwa na imani kwa njia ile ile kama Mtawala yule. Yeye alisikia maneno ya Yesu naye akaamini. Hakubisha; hakuwa na mashaka. Yeye “akaenda zake” (mstari 50). kwa kusoma Biblia na kusikiliza kwa makini maneno ya Mungu, yaliyosemwa na manabii na Yesu na Mitume, tunajifunza kuwa na imani. Wakati yule Mtawala alipoyasikia maneno ya Yesu, aliamini na kutii. Haitoshi kusoma na kuamini tu, yatupasa kutii pia, ni hapo tu tutakapoamini na kutii ndipo tutampendeza Mungu.

 

MASWALI

Majibu Mafupi

 

  1. Wakati Yesu alipokuwa Kana, Mtawala mmoja alimjia. Je, Mtawala huyu alitoka

wapi?

  1. Kwa nini Mtawala huyo alikuja kumtafuta Yesu?
  2. Alitaka Yesu afanye nini?
  3. Yesu alimwambia nini Mtawala yule lililomfanya afurahi?
  4. Kwa nini yule Mtawala aliwauliza muda mwanaye alipoanza nafuu?
  5. Wakati yule Mtawala alipoeleza yaliyotokea, familia yake na watumishi wake walifikiri

 nini?”

 

Majibu ya Kina

 

  1. Wakati Yesu alipokuwa Kana, Mtawala mmoja kutoka Kapernaumu alikuja kwake.

Eleza habari hiyo.

  1. Yule Mtawala alikuwa amesikia nguvu za Yesu za kufanya miujiza
    1. Je,nini Mtawala alitaka Yesu afanye?
    2. Ni somo gani Yesu alitaka yule Mtawala ajifunze

 

Majibu ya Nyongeza

 

9.    (a) Ni kwa jinsi gani Mtawala alionyesha imani yake?

      (b) Ni jinsi gani sisi tunaweza kujifunza kuwa na imani?

 

Swahili Title
081 MWANA WA DIWANI
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type