88. MSAMARIA MWEMA
“Enenda zako, nawe ukafanye vivyo hivyo ”
Shabaha
Kuonyesha jinsi Yesu alivyojibu swali “Jirani yangu ni nani? Tumekwisha kuona kuwa Mafarisayo walipenda sifa za watu. Walikuwa wenye kujiona kuwa na haki, wakijisifia kwa kazi zao nzuri” Mungu hakufurahishwa na aina ya haki ile hata kidogo. Aliwataka watu kunyenyekea mbele yake, Mafarisayo na Waandishi (mara nyingi wakiitwa wana sheria), ambao walikuwa viongozi wa wana wa Israeli , walikuwa mfano mbaya kuigwa. Yesu alisema, msitende mfano wa matendo yao, kwani wanasema, lakini hawatendi (Mathayo 23:3).
Luka 10:25-37
MWANASHERIA AZUNGUMZA NA YESU
Siku moja wakati Bwana Yesu alipokuwa akiwafundisha watu, mtu mmoja alisimama na kumwuliza swali. Mtu huyu alikuwa mwanasheria, mtu aliyesomea sheria ya Musa kwa uangalifu mkubwa na kuelewa vyema sana ni nini ilifundisha kuhusu njia wanayotakiwa watu waishi kumpendeza Mungu.
Akiamini kuwa angemdhalilisha Yesu mbele ya watu wote, mwanasheria yule aliuliza swali akimpima. Hakuwa akitaka jibu, kwa sababu alikuwa na uhakika tayari alilijua jibu “Bwana, nifanye nini ili kuurithi uzima wa milele? Aliuliza, naye Yesu akajibu, “Ni nini kimeandikwa katika sheria? Unasomaje? Hili halikuwa tatizo kwa yule mwanasheria, ambaye mara moja alijibu, Umpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote, na jirani yako kama nafsi yako” Jibu lake lilikuwa jema sana, kwani alikuwa ameweka pamoja mistari miwili muhimu sana kutoka kwenye vitabu vya sheria – kumbukumbu la Torati 6:5 na Mambo ya Walawi 19:18). Na baadaye Yesu, pia aliunganisha mistari hii miwili ya maandiko, na kusema “Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabiii (Mathayo 22:40).
Kwa hiyo,Yesu akajibu, umejibu vyema, fanya hivyo, nawe utaishi (mstari 28). Mwanasheria yule alifahamu jibu sahihi; angeweza kunukuu sheria kwa moyo, lakini maneno ya Yesu yalimwonyesha kwamba kulikuwa na kitu fulani anachopaswa kutenda ikiwa alitaka uzima wa milele. Mwanasheria aliweza kuona bayana kwamba hakufanikiwa kumfedhehesha Yesu kabisa,na kinyume chake yeye mwenyewe sasa alijihisi asiye na raha. Akitumaini kutunza heshima yake mbele za watu alimwuliza Yesu, “na jirani yangu ni nani?” (mstari 29)
Yesu akatambua kwamba hapa palikuwa na kitu fulani ambacho mwanasheria hakukijua. Ili yeyote asifanye kosa lolote kuhusu jibu lake, Yesu alitoa mfano.
YESU ALIMJIBU MWANASHERIA KWA MFANO
Yesu akaanza kusema; “Mtu mmoja alishuka kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko naye akaangukia mikononi mwa wanyang'anyi”. Barabara ya kwenda Yeriko ilikuwa na mteremko mkali na miamba na ilipitia katika nchi ya milima yenye mapango mengi, mahali ambapo palifaa kwa kujificha wanyang’anyi. Watu walitumia kusafiri kilometa zile thalathini kwenda Yeriko wakiwa katika vikundi vidogo ili waweze kujihami kutokana na hatari za njiani. Huyu mtu katika mfano huu alisafiri peke yake na njiani akashambuliwa na wezi, ambao “walimvua nguo zake, wakamwumiza na kuondoka, wakimwacha katika hali ya kaaribu ya kufa” (mstari 30) wakamweka kando ya barabara.
Kabla ya muda mrefu msafiri mwingine alikuja katika barabara ile ile. Alikuwa kuhani alipomwona yule mtu maskini akilala pale mwenye kuhitaji msaada, alichagua kujali mambo yake na kuendelea na safari yake.
Baadaye, akaja mlawi sehemu ile, alipomwona yule msafiri aliyezimia akilala barabarani, naye akapitiliza. Hawa wote wawili kuhani na mlawi, walielewa sheria inasema “umpende jirani yako kama nafsi yako”. Hata hivyo, wakatafakari, kwamba yule msafiri aliyelala kwa kupigwa pembeni mwa barabara hawakuhitaji kumjali. Pengine, ni kwa vile alikuwa “karibu ya kufa” alikuwa amepitiliza hali ya kusaidiwa kwa vyovyote vile. Hivyo wakachagua kutokumshughulikia na kwenda zao.
Muda mfupi baadaye msamaria akaja katika barabara ile yenye ukiwa. Alipomwona yule msafiri mwenye mkosi moyo wake mara moja ukamhurumi, wazo lake la kwanza lilikuwa kumpatia msaada, akaenda alikokuwa na kukagua vidonda vyake. Kisha kwa uangalifu akavifunga “akavimiminia mafuta na divai” kadiri walivyokuwa wakifanya siku zile,kwa ajili ya kutuliza na kuponya.
Baada ya kufanya vema alivyoweza, akamnyanyulia juu ya punda wake na kwendelea polepole na safari hadi walipofika penye nyumba ya wageni. Hapo alimweka katika hali ya kupumzika kadri alivyoweza, siku ya pili akampa mwenye nyumba ya wageni dinarii mbili (ikiwa sawa na nusu ya shekeli katika fedha za kiyahudi) na kusema “Mtunze huyu; na chochote utakachotumia cha ziada, nitakapopita tena, nitakulipa” (mstari 35).
YESUAMWULIZA MWANASHERIA SWALI
Akisha kumaliza kusema mfano wake, Yesu alimwuliza yule mwanasheria, “Ni yupi sasa kati ya hawa watatu, unafikiri yeye alikuwa jirani yake yule aliyeangukia katikati ya wezi?” (mstari 36).
Kulikuwa na jibu moja tu bila kupenda yule mwanasheria alijibu, “Ni yule aliyeonyesha huruma kwake” (mstari 37). Alikuwa ni msamaria aliyeonyesha “huruma” kwa yule msafiri, sasa wayahudi walikuwa wakiwadharau wasamaria kwa karne nyingi na hawangewazia kwamba wangesitahili sifa kwa njia yoyote ile. Jinsi gani hadithi ya Yesu ilivyokuwa yenye kugusa! Kuhani na mlawi walishindwa kutenda vile Mungu alivyotaka, ila msamaria ndiye alionyesha huruma. “Enenda zako, nawe ukafanye vivyo hiyo” Yesu akamwambia yule mwanasheria aliyejiona (mstari 37).
FUNDISHO KWETU:
Kulikuwa na kitu kimoja kumhusu msamaria ambacho kilimfanya awe tofauti na wale waliokuwa na kiburi kwa ajili ya elimu au ufahamu wao wa sheria ya Mungu. Alionyesha huruma. Mara nyingi kwenye Biblia tunasoma jinsi Mungu alivyowakasirikia wana wa Israeli kwa sababu hawakuonyesha huruma. Mungu mwenyewe ni mwingi wa huruma (Kutoka 34:6–7) naye anatutaka tuonyeshe tabia ya aina hii maishani mwetu.
Zipo njia nyingi tunazoweza kuonyesha huruma, kama yule msamaria mwema alivyotenda. Ina maanisha kuona yale tuwezayo kuyafanya kusaidia wengine, kuwafariji, kuwasamehe, kuwa wema na wenye mawazo mema kwa ajili ya werngine. Juu ya yote twaweza kuwasaidia watu kuelewa injili ya ujumbe wa wokovu. Hii ndiyo njia ambayo Mungu ameonyesha huruma kwetu (1 Petro 1:3). Ni wema na huruma kuu ya kiasi gani tunayoweza kuonyesha zaidi ya kuwafundisha wengine kuwa Kristo atarudi tena.
Yule mwanasheria alikuwa sahihi aliposema inatupasa kumpenda Mungu kwa moyo wetu wote na kwa roho yetu yote na kwa nguvu zetu zote na kwa akili yetu yote. Mtume alisema “Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu,kwamba tuzishike amri zake” (1 Yohana 5:3). Mwanasheria alijua kuwa ilikuwa ndiyo iliyo sahihi, naye Yesu akamwambia, “Fanya” hilo. “Iweni watendaji wa neno" Yakobo akasema, “wala siyo wasikilizaji tu, huku mkijidanganya wenyewe” (Yakobo 1:22)
MAELEZO YA NYONGEZA:
MAANA YA MFANO
Kama kawaida kila wakati, mfano huu wa Yesu ulikuwa na maana iliyofichika
- Yesu ndiye Msamaria, alichukiwa na viongozi wa wayahudi, waliofikiri kuwa walielewa sana sheria za Mungu kuliko yeye. Yesu, aliye bora kuliko watu wote, alishika sheria ya Mungu, kwani alitenda mambo yote ambayo Mungu aliyahitaji.
- Sisi ni kama yule msafiri, tulikuwa kama wafu kwa sababu ya dhambi zetu. Mungu amesema “Roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa” (Ezekieli 18:4). Kama Yesu asingetusaidia, tungekufa, aliitwa “Yesu” ikimaanisha “Mungu ataokoa” “maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao” (Mathayo1:21).
- Alitupatia “mafuta na divai” vinavyowakilisha ujumbe wa Injili unaopatikana katika Neno la Mungu. Ni neno la Mungu linalotupatia tumaini la uzima wa milele. Iwapo tutausikiliza ujumbe wake uponyao tutaishi.
- Msamaria alimpatia mtunza nyumba ya wageni dinari mbili au nusu ya shekeli kusaidia kumwokoa yule mtu kwa kumlipia matunzo yake. Chini ya sheria kiasi hiki kilikuwa ndiyo bei ya ukombozi. Ilikuwa ni fedha iliyolipwa kwa Mungu na kila mwana wa Israeli. Yesu ni mkombozi wetu, bei aliyolipa ilikuwa damu ya uzima wake ili tupate kuokoka (kukombolewa) kutokana na dhambi zetu (1 Petro 1:18 – 19).
MASWALI
Majibu Mafupi
- Ni swali gani mwanasheria alimwuliza Yesu mara ya kwanza?
- Ni jibu gani lilikuwa sahihi kwa swali hilo?
- Ni kwa nini Yesu alieleza habari ya msamaria mwema?
- Ni tukio gani la kutisha lililotokea kwa msafiri aliyetoka Yerusalemu kwenda Yeriko?
- Watu wangapi walipita pale na kumwona yule mtu akilala njiani? Walikuwa ni akina nani?
- Ni yupi kati yao alisimama kumsaidia?
- Yesu alipouliza ni nani aliyetenda kama jirani, yule mwanasheria alisemaje?
- Ni kwa namna gani msamaria alikuwa tofauti na Kuhani na Mlawi?
- Tunamwonyeshaje Mungu kwamba tunampenda yeye?
Majibu ya Kina
- Mwanasheria alimwuliza Yesu, “Jirani yangu ni nani”?
Eleza mfano uliotolewa na Yesu akijibu swali hili.
- (a) Yesu alimweleza mwanasheria afanye nini?
(b) Jinsi gani Mungu ameonyesha rehema kwetu sisi?
(c) Ni fundisho gani tunalojifunza kutokana na hadithi hii?
Majibu ya Nyongeza
12. (a) Ni kwa vipi Yesu ni sawa na Msamaria katika hadithi hii?
(b) Ni kwa namna gani sisi ni kama yule msafiri?
(c) Je, “mafuta na divai” vinawakilisha nini?
(d) Zile dinari mbili ambazo ni sawa na nusu shekeli inawakilisha nini?