89. KUPONYWA KWA KIPOFU
“Mimi ni nuru ya Ulimwengu.”
Shabaha
Kuonyesha jinsi Yesu alivyomponyesha mtu aliye kuwa kipofu na akamwamini Yesu. Ikawa Yesu na wanafunzi wake walipokuwa wakitembea katika mitaa ya Yerusalemu siku ya Sabato, wakamkuta mtu mmoja kipofu tangu kuzaliwa. Alikuwa ni mtu anayefahamika sana, aliyekuwa akikaa hapo na kuomba kila siku;mana hakuwa na njia nyingine ya kupata riziki yake ya kila siku. Wanafunzi wake walipomwona mtu huyo pale; walimwuliza Yesu ni kwa nini mtu yule alizaliwa kipofu. Je, ni kwa sababu ya dhambi zake mwenyewe au wazazi wake ndiyo waliotenda dhambi? Hata hivyo Yesu alijua kuwa yule kipofu hakutenda dhambi wala wazazi hawakutenda dhambi hata yule mtu azaliwe kipofu!
Udhaif, magonjwa na kifo viliingia duniani kwa sababu ya uasi wa Adamu na Eva tangu mwanzo. Isipokuwa wakati wa Ufalme wa Kristo tu, ambapo watu watakuwa wamemrudia Mungu na kumtii Yeye; “wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena” (Ufunuo 21:4)
Yohana 9
MIMI NI NURU YA ULIMWENGU
Yule kipofu aliishi ulimwengu wa giza tangu kuzaliwa kwake. Ni kwamba hayakuwa makosa yake. Na sasa akawa amewasikiliza kwa makini kundi la watu waliokuwa wamesimama karibu na yeye; akamsikia Yesu akisema, “Muda nilipo ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu”. Kama huyu kipofu angeweza kuona nuru tu basi, angekuwa huru. Na wala asingeomba tena.
Yesu akawa amepata nafasi nyingine tena ya kuwaonyeha wanafunzi wake, nguvu za ajabu ambazo Mungu alikuwa amempatia ili awafundishe watu mafundisho muhimu. Yesu alipokuwa na nafasi ilikuwa ni lazima aifanye kazi ya Baba yake. “Imenipasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka, maadamu ni mchana”(mstari 4).
Mara tu baada ya kuuawa na watu waovu,kama yeyemwenyewe alivyokuwa akijua. Ndipo kazi yake ingekuwa imekwisha.
YESU ANAMPONYA KIPOFU
Wakati alipokwisha kujibu swali la wanafunzi wake (mstari 2) Yesu akafanya jambo la ajabu. “Alitema mate chini akafanya tope kwa yale mate. Akampaka kipofu tope za macho; kamwambia, Nenda kana we katika birika la ya Siloamu” (mstari 6-7). Yule mtu akaenda kunawa kama Yesu alivyomwambia na akanawa zile tope na kuziondoa akaona.
Wakati majirani zake walipomwona, hakuwa kipofu tena bali alikuwa sasa anaona, walishangaa sana. Wakasema; “Siyo huyu aliyekuwa akiketi na kuomba?”. Hawakuwahi kusikia kabla mwujiza wa aina hiyo na kwa hiyo walishindwa kuamini. Lakini wengine walikuwa na uhakika kuwa ndiye huyu aliyekua kipofu na wengine walisema, siyo yeye ila amefanana naye. Na yule mtu mwenyewe akasema, “Mimi, ndiye”. Alikuwa anafahamu vyema kuliko mtu yeyote kuhusu kuponywa upofu wake watu wakamwuliza, "macho yako yalifumbuliwaje?" Naye akajibu, “Mtu yule aitwaye Yesu, alifanya tope akanipaka macho yangu, na kisha akaniambia; Nenda Siloamu ukanawe: Na nikaenda kunawa, ni kapata kuona”(mstari 11). Walipomwuliza huyo Yesu yuko wapi, yule mtu hakujua alikokuwa. Waliona ni vyema kumpeleka yule mtu kwa Mafarisayo.
ALIYEKUWA KIPOFU ZAMANI NA MFARISAYO
Ilikuwa ni siku ya sabato, Yesu alipomponya yule aliyekuwa kipofu. Kumbuka kuwa alikuwa amemponya mtu kule Kapernaumu ndani ya Sinagogi siku ya sabato. Na sheria ya Musa inasema, “Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni sabato ya BWANA, Mungu wako” (Kutoka 20:8-11).
Hakika ilikuwa ni kazi ya Mungu, kumponya kipofu; lakini Mafarisayo hawakuamini kuwa Yesu alitoka kwa Mungu. Kwa hiyo wakamshitaki kwa kuvunja sheria ya sabato (soma maelezo ya nyongeza Somo la 9).
Kila wakati, Mafarisayo walikuwa wakikasirishwa sana kwa kumwona Yesu akifanya miujiza ya jinsi hiyo, kwa sababu walikuwa wakimwonea wivu. Na kama wngemkata akiwa anaafanya miujiza siku sabato, wangesababisha kazi yake nzuri ionekane kuwa ilikuwa ni mbaya kabisa. Kwa hiyo yule aliyekuwa kipofu zamani alipopelekwa kwao na kuwaambia jinsi Yesu alivyomponya; walimwambi, “Mtu huyu hakutoka kwa Mungu,kwa sababu haishiki sabato”(mstari16). Watawala wa Israeli, “wao ndiyo waliokuwavipofu”. Ingawa ushahidi ulikuwa ni wa wazi wazi mbele ya macho yako; hawakuweza kuona nguvu za Mungu. Na baadhi yao walikubali kuwa mtu mwenye dhambi asingeweza kufanya miujiza ile. Kwa hiyo kukawa na matengano kati yao wenyewe. Hakuna yeyote-aliyejua la kuwaza, lakini kuongezeka kwa chuki ya viongozi juu ya Yesu kukawa dhahiri. Na ikaendelea kuwa mbaya sana, hadi walipomsulubisha msalabani.
MAFARISAYO WANAWAITA WAZAZI WAKE
Mafarisayo walikataa kukubali kuwa yule mtu aliyepelekwa kwao na ambaye alikuwa anaona; kwamba alizaliwa kipofu.Kwa hiyo waliwamwita wazazi wao. Wakasema, “Je! huyu ndiye mwana wenu, ambaye mnasema kuwa alizaliwa kipofu?” Hata hawakuamini kama kweli wazazi wake walisema ukweli. “Amepataje sasa kuona?”, (mstari 19).
“Tunajua kuwa huyu ndiye mwana wetu, na alizaliwa kipofu”, walijibu. “Lakini ni kwa njia gani amepata kuona, hatujui;au ni nani aliye mfumbua macho, hatumjui” (mstari20-21). Waliwaogopa Mafarisayo, kwa sababu walijua kwamba mtu yeyoye atakaye mwamini Yesu kuwa ni Masahi (Kristo) angetegwa na sinagogi. Kama wange kubali kuwa Yesu ndiye amemponya mtoto wao, Mafarisayo wasingewaruhusu kuingia ndani ya sinagogi. Na kwa hiyo wakasema hatumjui.
Mafarisayo walipaswa kumwuliza yeye mwenyewe. “Yeye ni mtu mzima”. Wazazi wakasema, “mwulizeni yeye mwenyewe, atajisemea mwenyewe” (mstari 21). Wakamwita mara ya pili yule mtu; “mpe Mungu utukufu”; wakasema. “Tunajua kuwa mtu huyu ni mwenye dhambi” (mstari 24). Na sasa yule mtu alikuwa ameishiwa uvumilivu kwa Mafarisayo. Walitaka wasikie tena maelezo, waone kama wanaweza kupata ukweli wenyewe. Lakini maelezo yalikuwa ni rahisi wao wakakataa kumwamini. Naye akasema; “Ninajua jambo moja tu ya kwamba nilizaliwa kipofu na sasa ninaona” (mstari 25). “Kama huyu mtu hakutoka kwa Mungu, basi asingefanya lolote” (mstari 33).
Imani rahisi kiasi hicho ilisababisha Mafarisayo kukasirika.Wao walitakakupata uthibitisho kuwa Yesu ni mwenye dhambi, na haijajirishi wao wamesemaje, watu walimwamini Yesu kwa sababu ya miujiza ya kushangaaza aliyoifanya. Asingeweza kuitenda miujiza kama hiyo bila nguvu za Mungu. Na hivyo wakamtoa katika sinagogi yule mtu aliyeponywa upofu. Wakati alipokuwa kipofu, watu walimhurumia; na sasa anaona watu hawa hawahitaji kuwa naye. Wala hata hawawezi kumruhusu amwabudu Mungu.
YESU ANAMWONA YULE MTU
Ikawa Yesu aliposikia kuwa yule mtu amefukuzwa katika Sinagogi, likwenda kumtafuta. Yesu akamwambia, “Wewe, wamwamini Mwana wa Mungu”. Yule mtu akamwuliza; “Ninani, Bwana, nipate kumwamini”. Yesu akamwambia, “Wewe, umemwona; yeye unayesema nawe, ndiye”. Yule mtu akasema, “naamini, Bwana”, kwa maana alimtambua Yesu kuwa ndiye aliyemponya (mstari 36-38). Yule mtu sasa akawa ni mwenye furaha tena. Baada ya Mafarisayo kumwondoa asimwabudu Mungu, yule mtu akampata Mwana wa Mungu na akamwamini. Siyo kwamba angeona vitu vilivyokaribu naye tu; bali pia angeweza kuiona Kweli. Angeweza kuona kuwa, Yesu ni “nuru ya ulimwengu”.
FUNDISHO KWETU
Biblia katika sehemu nyingi inasema kuwa Neno la Mungu ni “nuru”, na dhambi naujinga (kutokuijua Kweli) kuwa ni “giza” (kwa mfano Zaburi 119:105; Yohana 8:12; Waefeso 5:8-11; 1 Wathesalonike 5:4-5). Yesu alikuja ili alete nuru Ulimwenguni. Yesu Kristo, kwa sasa yuko mbinguni yuko mkono wa kuume wa Mungu. Na ingawaje hayupo pamoja nasi, kama alivyokuwa kabla; tunalo Neno la Mungu kwa ajili ya kujaa katika mioyo yetu, na akili zetu tuzijaze na “nuru”. Hakuna sababu ya sisi kuwa vipofu kama Mafarisayo.Kama tutaweza kuelewa Neno la Mungu tutaona mambo mazuri ajabu ambayo Mungu alitenda wakati uliopita na atayatenda wakati ujao; wakati atakapomtuma Yesu Kristo kurudi duniani.
YESU ANAWAKEMEA MAFARISAYO
Yesu alielezea fundisho la mwujiza wa uponyaji wa yule mtu kipofu ambaye aliponywa kwa wote ambao walihita kusikia. Baadhi ya Mafarisayo walitambua kuwa alikuwa akiwaambia wao; wakamwuliza: “Je, sisi nasi tu vipofu?" Baadhi ya Mafarisayo waliofikiri kuwa walizielewa vizuri njia za Mungu kuliko mtu yeyote. Walidhani kuwa wanaona. Kwa maana ya hapa; “Kuona” maana yake ni “kujua au kufahamu”. Tayari tumekwisha ona katika masomo yaliyotangulia kuwa hawakutambu njia za Mungu sawasawa (Yesu alimweleza Nikodemu hivyo, na hatimaye Nikodemu alimwani Yesu. Soma Yohana 3:10-12; 7:50-52:9; 39). Mara nyingi Yesu aliwaita hao kuwa ni “viongozi vipofu” (Mathayo 15:14; 23:24). Kiburi chao kiliwaposha wasiweze kuamini kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu. Ni fundisho la ajabu kwetu sisi.
MASWALI
Majibu Mafupi
1. Je, ni kwa muda gani mtu yule kipofu alikuwa kipofu?
2. Yesu aliweka nini kwenye machoni yake?
3. Yesu alimwambia yule mtu aende akanawe wapi?
4. Ni kwanini Mafarisayo waudhika sana wakati yule aliyekuwa kipofu zamani alipokwenda
kwao?
5. Ni kwanini wazazi wa yule mtu waliwaogopa Mafarisayo?
6. Mafarisayo walisema nini kuhusu Yesu?
7. Mafarisayo walimfanya nini yule aliyewahi kuwa kipofu?
8. Ni nani aliyekwenda kumtafuta yule mtu baada ya kufukuzwa katika Sinagogi?
9. Yesu alimwambia yule aliyewahi kuwa kipofu amwamini nani?
Majibu ya Kina
10. Wakati Yesu alipomwona kipofu siku moja katika Yerusalemu alimponya.
(a) Eleza jinsi alivyomponya?
(b) Ni kwanini alimponya yule kipofu?
(c) Yesu alifanya kazi za nani siku ya sabato?
11. (a) Sheria za Musa zinasemaje kuhusu sabato?
(b) Ni kwa nini Mafarisayo walisema kwamba Yesu alikuwa akivunja sheria?
(c) Ni kazi ya nani Yesu aliyofanya siku sabato?
Majibu ya Nyongeza
12. Yesu akasema, "Mimi ni nuru ya Ulimwengu."
(a) Ni jambo lipi la kwanza alilolitenda kwa ajili ya yule aliyekuwa kipofu?
(b) Yule aliyewahi kuponywa alijifunza nini kuhusu Yesu?
(c) Ni kitu gani kilichowapofusha Mafarisayo wasimwani Yesu?
(d) Ni kipi kinachotujaza sisi nuru?