90. MCHUNGAJI MWEMA
“Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo”.
Shabaha
Ni kuonyesha kuwa Mungu huwalinda wale wapendao njia zake;na ya kwamba Yesu ndiye mchungaji mwema. Katika somo letu lililopita jinsi Yesu alivyowaonyesha Mafarisayo kuwa wao ni viongozi “vipofu” wa watu.Maana wao wenyewe hawakuweza kuijua Kweli wazi wazi, na kwa sababu wakiwa ni viongozi wa watu walikuwa hawafai. Yesu aliendelea kuwaambia kiongozi wa kweli wa watu wa Mungu jinsi anavyopaswa kuwa. Maana Israeli kwa kweli walikuwa ni sawa na mchunaji waliohitaji mchungaji mwema wa kulisha.
Yohana10:1-16,26-28
MAISHA YAMCHUNGAJI: Yohana 10:1-6
Nyakati za Biblia, maisha ya mchungaji yalikuwa tofauti na siku zetu hizi. Mchungaji wa Israeli alikuwa anakuwa na kundi dogo la kondoo na aliwajua kondoo wote kila mmoja kwa jina lake. Kwa maana aliwalisha tangu walipokuwa ni wanakondoo hadi wanapokuwa wakubwa; kwa kweli walikuwa ni marafiki wa kudumu. Na wakati wa mchana aliwaongoza kondoo mara nyingi aliwatafutia kondoo wake malisho mabichi, aliwaongoza alipokuwa anawapeleka penye maji mazuri na hata wakati mwingine kama njia ilikuwa ni mbaya kwa wanakondoo basi angewabeba mikkononi wale ambao ni wadogo sana.Na kila mara aliwalinda dhidi ya wanyama wa mwitu, ambao wangeweza kushambulia kundi la kondoo, kwa maana yeye ndiyebaliyekuwa ni mlinzi wa kondoo hao. Kwa kweli kondoo ni wanyama wapole sana wasikuwa na tumaini a kuweza kujilinda wenyewe. Kwa hiyo mchungaji ni lazima awakinge kondoo, hata kama ingemaanisha kupoteza uhai wake yeye mwenyewe.
Na wakati wa usiku angewapeleka zizini, zizi lilijengwa kwa mawe, na mlango ulilindwa na baabu. Bawabu ndiye aliyefungua mlango nao kondoo wakaingia ndani ya zizi. Hapo kondoo wangekuwa salama wasingeza kushmbuliwa na wanyaa wa mwitu. Zizi lilichangiwa na idadi kadhaa ya wachungaji waaminifu mbao mlinzi aliwafahamu vizuri wote. Lakini hakuna mgeni aliyeruhusiwa kuingia mlangoni. Mwizi angejaribu kupanda ukuta wa zizi ili aibe kondoo; hata hivyo mchungaji mwaminifunzi alikuwa macho wakati wote.
Na asubuhi, kila mchungaji aliwaita kondoo wake kwa majina, kila kondoo aliijua sauti ya bwana wake, kwa furaha kondoo walikimbilia kule alipokuwa bwana wao wakiwa na uhakika wa kupata ulinzi kutoka kwake. Na wakati mwingine, ilikuwa ni muhimu mchungaji ampate mchngaji wa mshahara, ili awatunze kondoo wake. Huyu mchungaji wa mshahara hakuwa na upendo kama wa yule mchungaji ambaye kondoo ni mali yake. Wakati matatizo yalipofika mchungaji wa mshahara alikimbia ili kuyaokoa maisha yake, akiwaacha kondoo wakitawanyika na kuliwa na wanyama wa mwituni.
WATU WANGU WAMEKUWA KONDOO WALIOPOTEA.
Wakati wote Mungu aliwafananisha watu wa Israeli na kondoo zake (Zaburi 11:3). Musa na Daudi, ambao ni watu wawili waliokuwa viongozi wakubwa sana wa watu wa Mungu, hawa walifundishwa kama vile wachungaji (Kumbuka jinsi Daudi alivyowaokoa kondoo wake wasiliwe na simba na dubu (soma1Samweli 17:34-35).
Kwa hiyo hawa wawili walijua jinsi ya muwaongoza watu wa Mungu. Kuna wakati, katika hisoria za Israeli ambapo walikuwepo wachungaji wasiokuwa waaminifu amba hawakujali kundi la kondoo kabisa, na watu wakawa wamepotoshwa au wakafundishwa kinyume na Kweli ya njia za Mungu (Yeremia 50:6). Na hivyo ndivyo walivyokuwa Waandishi na Mafrisayo siku za Yesu. Yesu alizungumzia habari hii ya mchungaji na kondoo alikiwafundisha wao “lakini wao hawakuelewa na mambo hayo aliyowaambia” (mstari 6).
MIMI NDIMI MLANGO: YOHANA10:7-10
Yesu akasema mimi ndimi mlango wa kondoo (mstari 7) Wao, walidai kuwa walikuwa ni wachungaji; lakini wachungaji ni lazima waingie ndani ya “zizi” kwa kupitia “mlangoni” (mstari 2). Mchungaji wa kweli wa watu wa Mungu ni lazima awalete kwa Yesu. Lakini Mafarisayo walimchukia Yesu. Hawakumwamini Yesu, na walifanya kila waliloliweza kuwazuia watu wasimwamini Yesu. Walikuwa ni wevi na wanyang'anyi (mstari8), waliokuja kuiba, kuharibu na kuchinja (mstari10). (Kumbuka jinsi walivyoshindwa hata kuwajali wale waliokuwa wagonjwa zamani walioponywa. Tutayaona mambo ya namna hii katika masomo yanayofuata). Na ikiwa Yesu ni “mlango”, ni nani basi ambaye ni bawabu au yule anayefungua mlango? Ni Mungu mwenyewe, atakaye wafungulia wote wanaobisha mlango (Mathayo 7:7-8).
MIMI NDIMI MCHUNGAJI MWEMA: Yohana:11-15
Nitofauti ipi iliyo hapo kati ya mchungaji na mtu wa mshahara. Mtu wa mshahara hukubali kuwaongoza kondoo lakini, kondoo zikiwa si mali yake. Kondoo hao hawaijui sauti yake na wala haonyeshi kuwajali au kuwathamini. Kondoo huwa hawawi salama mikononi mwake. Mafarisayo walikuwa sawa sawa na watu hawa. Walijifikiria wao wenyewe (soma Mathayo 23:5-7) na walikuwa wakitafuta utukufu na heshima kutoka kwa watu.
Lakini Yesu kwa upande mwingine, si mchungaji mwema, mwaminifu na mwenye huruma. Watu wote wamwaminio yeye ni kondoo zake. Yeye anawajua wote kwa majina yao na wao wanaifhamu sauti yake. Wale wamwaminio daima husoma Neno la Mungu hutafuta sauti yake ili iwaongoze na kuwafariji. Katika Neno la Mungu wanapata chakula na maji kwa maana Yesu alisema: “Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa; naye aniaminiye hataona kiu kamwe” (6:35 soma pia somo la 12). Aliwajali sana kondoo zake hata akautoa uhai wake kwa ajili ya kondoo zake. Ni upendo gan mkubwa angekuwa nao kuliko huu.
NA KONDOO WENGINE NINAO
Yesu alikuja kwa kondoo walio kuwa wamepote, Wayahudi (Mathayo 15:24). Alikuwa ni “mwenye huruma kwa watu wote, kwa sababu walikuwa kama kondoo wasiokuwa na mchungaji" (Marko6:34), na yeye anataka awarudishe wakiwa salama katika zizi. Yesu pia alisema kwamba, “Na kodoo wengine ninao, ambao si wazizi hili; na hao nao imenipasa kuwalete, na sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja" (Yohana 10:16). Hawa, kondoo wengine ni watu wa mataifa (watu ambao si waisraeli) kama vile sisi wenyewe, ambao tunabidii na kujiunza Neno la Mungu na kuitii “sauti" yake.
Zizi ni Eklesia ambamo tunaingia kwa kupitia “mlango", yaani, Kristo. Na njia ya kuingia katika Eklesia ni ubatizo kwa njia ya Kristo. Pulo na mitume wengine walihubiri injili kwa mataifa baada ya Yesu kukufuka kutoka kwa wafu. Hawa walikuwa wachungaji waaminifu waliokuwa wakiwaita watu waje kwa Mungu na wajifunze habari za Kristo. Kwa ajili ya mahubiri yao Mungu “akawafungulia mataifa mlango wa imani" (Matendo ya Mitume 14:27), ili kwamba wale waliosikia injili waweze kuingia. “Kuna zizi moja tu la kondoo", maana yake, Eklesia (kusanyiko la watu walioitwa na Mungu) moja ambalo ni mkusanyiko wa wayahudi na watu wa mataifa wamwaminio Kristo.
Tunayo baraka kubwa namna gani kusikiliza Neno la Mungu likiw linafundishwa na ndugu zetu waaminifu siku hizi waki waalika watu watu waingie ndani ya eklesia kwa njia ya ubatizo.
|
Yesu |
Mchungaji Mwema |
|
Mafarisayo |
Wezi na wanyang'anyi (mstari 1,8) au wachungaji wa mshahara (mstari 12,13). |
|
Eklesia |
Zizi la kondoo (mstari 16) |
|
Yesu |
Mlango (mstari 7) |
|
Mungu |
Bawabu mlinda mlango (mstri 3) |
|
Wale wamwanio Kristo
|
Kondoo, wanaoiskia sauti ya mchungaji (mstari 27,28), Wayahudi kwanza |
|
Watu wa mataifa wanaomwamini Kristo |
kondoo wengine wanaosikia sauti ya mchungaji (mstari 16) |
FUNDISHO KWETU
Ni faida kubwa iliyoje, kuhesabiwa miongoni mwa kondoo wa Mungu, na kwa kuwa na Yesu Kristo ambaye ni mchungaji na kiongozi wetu. Kama tutaendelea kusikiliza sauti yake, anapozungumza nasi kwa njia ya Neno la Mungu, yeye ataendelea kuwa mwaminifu. Dunia hii tunamoishi kuna mbwa mwitu wengi, watu ambao wanataka kutuharibu, kwa kutuongoza katika njia zao za uovu. Ni lazima tubakie ndani ya eklezia na kutafuta raha ya kweli hapo, kama tunataka kuwa salama.
MASWALI
Majibu Mafupi
1. Ni jinsi gani mchungaji anavyowalinda kondoo wakati wa mchana?
2. Wakati wa usiku mchungaji huwaongoza kondoo kuwapeleka wapi?
3. Ni jinsi gani kondoo wanavyoingia ndani ya zizi?
4. Ni nani anayemfungulia chungaji mlango?
5. Ni jinsi gani kondoo humfahamu ni mchungaji yupi wa kumfuata?
6. Je Yesu alisema ninani ambaye ni “mlango?”
7. Na ninani anayeufungua mlango huo?
8. Ni nani ambaye ni mchungaji mwema?
9. Ni kwa jinsi gani mchungaji wa mshahara hutofautina na mchungaji mwema?
10. Ni nani ambao ni kondoo wa Yesu?
11. Na “kondoo wengine” aliowasema Yesu ni?
12. Ni jinsi gani tunavyoweza kuingia katika zizi la Yesu?
Majibu ya Kina
13. Yesu alisema mfano ambao katika alijisema kuwa ni yeye “ni Mchungaji Mwema"
(a) Ni kwa vipi Yesu amefanana na mchungaji mwema?
(b) Ni jinsi gani alivyoonyesha upendo wake mkuu?
(c) Kondoo wa Yesu ni?
(d) Ni jinsi gani tunavyoweza kuwa kondoo wa Yesu?
14. (a) Andika majina yaviongozi wakubwa katika Israeli ambao walikuwa wachungaji?
(b) Ni kwa jinsi gani Mafarisayo walikuwa sawa sawa na wachungaji wa Mshahara?
(c) Ni kwanini Mafarisayo walikuwa wakijaribu watu wasimsikilize Yesu
“Mchungajimwema?"
(d) Ni jinsi gani tunavyoweza kuzikwepa njia mbaya za ulimwengu?