CSSA 1-4-16 - THE PRODIGAL SON

Swahili

91. MWANA MPOTEVU

“Huyu mwanangu alikuwa amekufa,naye amefufuka; alikuwa amepotea; naye ameonekana”.

 

Shabaha

Kuonyesha jinsi Yesu alivyofundisha kuwa kwa mfano kuwa Mungu ni Baba mwenye upendo, mwenye kusamehe dhambi watoto wake. Ingawaje viongozi wa Wayahudi walimchukia Yesu, lakini watu wa kawaida walifurahia kumsikiliza.Maneno yake yalikuwa ni ya faraja na yakiwaonyesha watu Mungu alitaka nini wao wafanye.Mafundisho yake yalikuwa ni waziwazi na rahisi kueleweka, kwa wale waliokuwa wanataka kumpendeza Mungu. Mara nyingi walikuwa “watoza ushuru na wenye dhambi” waliodharauliwa na Waandishi na Mafarisayo, waliokuwa wakimzunguka Yesu na kusikiliza mifano yake. Siku moja alisema mifano mitatu kuhusu jambo la “kupotea” - kondoo aliyepotea, shilingi iliyopotea na mwana aliyepotea. Watu wengi katika Israeli walikuwa “wamepotea” - walikuwa wamekwenda kinyume na ibada ya kweli. Na kwa hiyo Yesu alitumwa na Mungu ili kuwatafuta na kuwarudisha tena kwenye ibada ya kweli ya Mungu.

 

Luka 15:11-32

 

MFANO WA MWANA ALIYEPOTEA

Mtu analikuwa na wana wawili. Mkubwa alikuwa ametulia na mchapa kazi, lakini mdogo alikuwa hakutulia na asiyetosheka. Siku moja yule mwans mdogo alimwuliza baba yake ampatie urithi ambao siku moja ungekuwa mali yake. Alitaka kusafiri na kutumia fedha, kutafuta marafiki wapya na kuishi maisha yake ya anasa. Bila shaka baba yake yule kijana mdogo alihuzunika kwa kumwona mwana wake akiondoka nyumbani na kwenda duniani kuchanganyikana na wageni.

 

Yule mwana “akakusanya vyote, na akasafiri kwenda nchi ya mbali”(mstari 13). Aliishi maisha ya uovu na akazitumia pesa zake vibaya akiwa na marafiki wapya aliowapata ambao walimsaidia kuutumia urithi wake. Kwa muda, pesa zikawa zimekwisha-na “marafiki” waliomsaidia kutumia pesa yake wakawa nao pia wameondoka. Hakuna walichojali kwa ajili yake. Uhusiano wao na yeye ulikuwa wa uchoyo. Na sasa bila ya kuwa na fedha na bila marafiki, sasa angeishi vipi “kiulizo”. Kufanya mambo yawa mabaya zaidi, Nchi ile ikawa na njaa. Na hatimaye akapata kazi ya kuwalisha nguruwe. Jinsi kazi hii ilivyokuwa ya machukizo kwa Wayahudi (soma Kumbukumbu la Torati 14:8). Alikuwa mezama chini kiasi gani. Wakati alipokuwa tajiri aliweza kufurahia mema yote na sasa alikuwa ameshushwa kabisa kulisha nguruwe. Alikuwa na njaa sana akawa akitamani kujishibisha makombo ya yaliyokuwa yamebakizwa na nguruwe, “nawala hakuna mtu aliyempa kitu” (mstari 16)

 

NITAONDOKA NA KWENDA KWA BABA YANGU

Licha ya njaa na aibu, yule kijana alifikiria na kukumbuka maisha ya nyumbani na baba yake mpendwa. Alifahamu kuwa watumishi wa baba yake hawana njaa. Watumishi wa baba yake wakati wote walikuwa na “chakula tele na hata kusaza”, lakini sasa hapa alikuwa anakufa kwa njaa. Na kwa hiyo akaamua moyoni mwake afanye nini. Atarudi kwa baba yake na kusema, “Baba; nimekosa juu ya mbingu na mbele yako, sisitahili kuitwa mwana wao tena; nifanye kama mmoja wa watumishi wako” (mstari 18-19). Na sasa alikuwa ameaibika kwa ajili ya tabia ya upumbuvu wake mwenyewe kwamba agefurahia kuwa mtumishim katika nyumba ya baba yake. Alifahamu kuwa baba yake alikuwa mwema na mwenye fadhiri na alitegemea kuwa angemsamehe na kumpokea tena. Akisha azimia moyoni mwake, akaenda nyumbani kwa baba yake.

 

BABA YAKE ANAMPOKEA

Na baba yake aliishi kwa matumaini ya mwana wake kurudi kwa hiari yake mwenyewe. Alitamani sana na kutegemea kumwona kila siku. Na kwa hiyo ilikuwa hivi, huyu kijana alipokuwa amechoka sana, akiwa na dhaifu kwa njaa na akitembea polepole akielekea nyumbani, “alipokuwa angali mbali, baba yake alimwona; akamwonea huruma, akaenda mbio akamwangukia shingoni, akambusu sana” (mstari 20).

 

Lililomsumbua baba yake ilikuwa kumwona mwana wake akiwa katika hali hiyo ya kutisha. Mwana wake hata hivyo, alikuwa na wazo kuu moja tu moyoni mwake-kukiri na kutubu kwa baba yake jinsi gani alivyokuwa mpumbavu na kuomba msamaha.

 

Yule mwana akamwambia, “Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele yako, sisitahili kuitwa mwana wao tena; nifanye kama mmoja wa watumishi wako” (mstari21). Hata ikawa kabla hajamaliza kusema baba yake akaingilia. Badala ya kuwa na hasira kama yule mwana alivyotegemea; baba yake akawa nimwenye furaha sana kwa kumwona mwana wake akitubu, na baba yake akawaambia watumishi haraka; watayarishe chakula ili wafurahie sikukuu.

 

“Lileteni upesi vazi lililo bora, mkamvike; mtieni na pete kidoleni, na viatu miguuni; na mleteni ndama yule aliyenona mkamchinje, nasi tule na tukafurahi; kwa kuwa huyu mwanangu alikuwa amekufa naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana” (mstari 22-24).

 

Ni badiliko kubwa la ajabu ndani ya yule mwana sasa. Katika nchi hiyo ya mbali alikuwa “amepotea”, sawa na mtu aliyekuwa amekufa. Ni mpaka pale alipokuwa fukara na akitaabika kwa njaa ndipo alipotambua upumbavu wake ulivyokuwa. Maisha yake ya huzuni yalimfundisha somo. Baba hakuwa na mawazo hayo ya kumweka mwana wake miongoni mwa watumishi wake, na badala yake alimpatia vazi jipya, mkufu na viatu. Wote kwa pamoja walikaa pamoja kwenye sherehe hiyo maalumu.

 

NDUGU YAKE MKUBWA ANAKASIRIKA

Sherehe hii yote, hata hivyo ndugu mkubwa hakushiriki. Yeye alikuwa shambani akifanya kazi, na alipokaribia nyumbani, alisikia sauti ya muziki na kucheza. Alimwita mmoja kati ya watumishi na kumwuliza sauti ya sherehe anayoisikia nyumbani ni ya nini.

 

Yule mtumishi alikuwa na furaha kubwa sana kumwelezea habari njema. “Ndugu yako amekuja na baba yako amemchinja ndama aliyenona, kwa sababu amempata tena yu mzima” (mstari 27).

 

Ndugu yake mkubwa hakufurahishwa na kitendo. Alikasirika sana na akakataa kuingia kuungana na familia yake katika chakula. Kwa hiyo baba yake alimfuata nje na akamwomba aungane familia katika furaha hiyo. Baba alijibiwa kwa hasira na majibu ya uchungu kutoka kwa mwanaye mkubwa.

 

“Tazama, mimi nimekutumikia miaka mingapi hii; wala sijakukosa amri yako wakati wowote, lakini hukunipa mimi mwana-mbuzi, nikafanya furaha na rafiki zangu”(mstari 29).

 

Hakuona sababu ya jinsi walivyofurahia kurudi nyumbani kwa mdogo wake huyo ambaye alikuwa hafai kabisa kwa lolote. Alionyesha moyo wa namna gani. Ilimwondolea kabisa mapenzi ya kufanya kazi ya baba yake. Hata hivyo baba yake alikuwa ni mwenye furaha sana na wala siyo kwamba hakujali kazi aliyokuwa akifanya yule mwana wake mkubwa.

 

“Baba kamwambia, Mwanangu, wewe u pamoja nami siku zote,na vyote nilivyonavyo ni vyako”(mstari 31).

 

Hakuweza kutambua jinsi mdogo wake alivyoamua kurudi nyumbani kwa sababu hatimaye alitambua jinsi alivyokuwa mpumbavu? "Huyu ndugu yako alikuwa amekufa naye amefufuka, na alikuwa amepotea naye ameonekana" (mstari 32).

 

FUNDISHO KWETU

Kuna wakati tunakuwa sawasawa na ndugu kama hawa, siyo kweli? Kwa kweli ni rahisi sana kuwa wachoyo na wapumbavu na kuwa waharibifu kama yule kijana,ambaye ni mwana mdogo alivyokuwa mwanzo. Kama angetulia tu kwa baba yake, ambapo alikuwa salama, mambo yote yangeendelea kuwa mazuri, lakini alitaka kufurahia anasa na starehe za dunia. “Anasa” hizi mwisho wake zilimfikisha kwenye matatizo.Alikuwa ni sawa na mtu aliyekufa. Hebu na tuwe busara zaidi kuliko hiyo,kwa maana tunafahamu kwamba hapa duniani hakuna furaha ya kweli. Hata kama tukitenda dhambi, tunapaswa kunyenyekea na kukubali kubadilisha njia zetu. Hii ndiyo aina ya moyo ambao Mungu anataka kuuona ndani yetu.

 

Mara nyingi, labda, tunaweza kuwaonyesha tabia kama ile iliyoonyeshwa na moyo wa yule ndugu mkubwa aliposikia mdogo ake kuwa amerudi nyumbani. Hakufurahi kabisa na wala hkumsamehe mdogo wake. Ndani ya moyo wake haikuwepo nafasi kabisa ya kuamini kuwa ndugu yake mkosaji ataweza kutubu. Tunapaswa kila wakati kuwaonyesha moyo wa huruma wale waliotukosea, kwa sababu sisi sote tunamkosea Mungu, na wote tunahitaji Mungu atusamehe dhambi zetu.

 

MAELEZO YA NYONGEZA

 

Ni nini basi maana iliyojificha ya mfano huu? Bila shaka Mungu ndiye anayewakilishwa na huyu baba mwenye kuwapenda wana wote wawili. Mungu wakati wote anajali jinsi tunavyojitahidi kumpendeza na ataendelea kufurahishwa na hilo, tunafahamu, kuwa thawabu za kazi zetu atakapoweka ufalme wake. Mungu yupo tayari kuwasamehe wale wanaotenda dhambi mara tu wanapotubu.

 

Farisayo na yule wenye dhambi aliokuwa wamedharauliwa,walikuwa sawa na yule mwana mdogo. Walikuwa wamepotea na walimhitaji mtu wa kuweza kuwarejesha tena kwa Mungu. Na hii ilikuwa ni kazi ya Bwana Yesu Kristo ambaye kwa furaha aliwaonyesha njia ya wokovu.

 

Mafarisayo, wao waliji-hesabia haki wenyewe,walikuwa sawasawa na yule mwana mkubwa. Wao pia walipaswa kusikiliza maneno ya Yesu lakini walikuwa na kiburi.

 

MASWALI

Majibu Mafupi

 1. Mtu alikuwa na wana wawili. Je, mwana mdogo aliomba nini?

 2. Mwana mdogo alifanya nini baada ya baba yake kumpatia kile alichokuwa ameomba?

 3. Ilitokea nini baada ya feha zake zote kuisha?

 4. Yule mwana alipotambua jinsi alivyokuwa mpumbavu alikwenda Wapi?

 5. Baba yake alipomwona alifanya nini?

 6. Baba yake aliwambia watumishi wake walete nini?

 7. Ndipo, baba akasema: “Huyu Mwanangu...”Malizia sentensi.

 8. Ndugu mkubwa alijisikiaje aliposikia yale ambayo baba alimtendea nduguye mdogo?

 9. Je, ndugu mkubwa alijumuika kwenye sherehe?

10. Tufanye nini kama alivyofanya yule mdogo ambalo Mungu hufurahishwanalo?

 

Majibu ya Kina

11. Baba alikuwa na wana wawili. Eleza habari kuhusu mwana  mdogo

(a) Aliomba apewe nini?

(b) Alipoondoka nyumbani ilitokea nini?

(c) Ilitokea nini aliporudi nyumbani?

(d) Ni kwanini baba yake alimsamehe?

12.  (a) Ndugu mkubwa alifanana na ?

      (b) Ni jinsi gani alivyoonyesha hisia zake wakati mdogo aliporudi Nyumbani?

      (c) Hatutakiwi tufanye kama Ndugu mkubwa. Je, tunapaswa tufanye  nini?

13. (a) Ni jambo gani lililosababisha yule mwana mdogo aamue kurudi nyumbani?

      (b) Alipanga amwambie baba yake nini?

      (c) Je, baba alimwonyesha  upendo namna gain?

 

Majibu ya Nyongeza

14. Katika mfano wa mwana mpotevu,sema maana ya mfano kwa kuoonyesha:

(a) Baba anamwakilisha nani?

      (b) Mwana mdogo anawakisha nani?

      (c) Mwanamkubwa anawakisha nani?

 

Swahili Title
091 MWANA MPOTEVU
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type