CSSA 1-4-17 - THE RAISING OF LAZARUS

Swahili

92. KUFUFUKA KWA LAZARO

“Mimi ndimi ufufuo na uzima”

 

Shabaha

Ni kuonyesha kwamba Mungu alimpatia Yesu nguvu za kufufua waliokufa. Haikuwa mbali kutoka Yerusalemu, Mji mdogo wa Bethania ulipokuwa ambapo Martha na Mariamu walipokuwa wanaishi pmoja na ndugu yao Lazaro. Walikuwa rafiki wa karibu na Yesu, ambaye alikuwa akiitwa nyumbani kwao mara nyingi ili kupumzika. Wakati Yesu alipokuwa akihubiri upende wa pili wa Yordani, kifo kikatokea katika familia hii kipenzi. Bwana Yesu akatumia nafasi hii kuonyesha nguvu kuu za Mungu alizompatia na kuwathibitishia wengi kuwa yeye ni Mwana wa Mungu.

 

Yohana 11:1-46

 

UJUMBE WA YESU

Nyumba iliyokuwa na furaha katika Bethania ghafula ilikuwa kimya. Lazaro alikuwa anaumwa sana Kadri siku zilivyokuwa zinapita hali yake ilikuwa inakuwa mbaya zaidi. Ni mwujiza pekee yakee yake ndiyo ungeweza kumponya. Maria na Martha wao walijua kuwa Yesu angeweza kumponya. Kwa hiyo, wakamtumamjumbe ili amtafute na kumweleza, “Bwana, tazama, yeye umpendaye hawezi?" Na Yesu aliposikia hivi, alisema, “Ugonjwa huu siyo wa mauti, bali kwa ajili ya utukufu wa Mungu; ili Mwana wa Mungu atukuzwe kwa huo” (mstari 4).

 

Hata hivyo, Yesu haukuongozana na mjumbe huyo mara moja bali alikawia siku mbili zaidi mahali pale alipokuwa. Na baada ya muda mfupi Lazaro akafariki. Alifahamu kuwa Lazaro atakufa, na ingawa aliiona hali halisi ya huzuni ya kutisha ya rafiki zake wapendwa kule Bethania, lakini alijua kuwa kifo hicho kingempatia nafasi ya kuonyesha utukufu wa Mungu kwa namna ya ajabu zaidi kuliko kama angekwenda haraka kumponya.

 

Isitoshe, Yesu hakuhitaji kurudi kule Bethania ili kumponya Lazaro, maana kwa nguvu za Mungu angeweza “kusema neno” na kumponya,kama alivyokuwa amemfanyia yule mwana wa diwani (Somo la 6), lakini safari hii aliamua asifanye hivyo.

 

LAZARO ANAKUFA

Yesu akaendelea kuhubiri upande wa pili wa Yordani naye Lazaro akafariki. Kwa uwezo wa roho ya Mungu, Yesu alikuwa anajua jambo litakalotokea. Alifahamu mshituko ambao wangeupata Maria na Martha kutoka na yeye kutokwenda kumponya Lazaro. Bado wangehuzunika kwa muda ili kwamba mwisho Mungu aweze kutukuzwa. Baada ya siku mbili Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Na twendeni Yudea tena” Wanafunzi wake walikuwa na hofu sana walipomsikia akisema hivi maana walijua kuwa maisha yake yatakuwa hatarini kutokana na hasira za viongozi wa Wayahudi.

 

Walipojua kuwa amekusudia kwenda, Tamaso alisema, “Twendeni na sisi huko ili tufe pamoja naye”(mstari 16). Na jinsi wao walivyokuwa wanampenda. Yesu akawaambia wanafunzi wake, “rafiki yetu Lazaro, amelala; lakini ninsakwenda nipate kumwamsha” (mstari 11). Wanafunzi wake wakashangaa. Kama Lazaro alikuwa amelala, hakika hiyo ilikuwa ni dalili nzuri; kweli ingemsaidia kupata nafuu tena. Na kisha Yesu akawaambia waziwazi alikuwa akimaanisha nini. “Lazaro amekufa”(mstari 14)

 

IMANI KUBWA YA MARTHA

Kwa muda huo Yesu na wanafunzi wake walikwenda Bethania, Lazaro alikuwa amekufa ilikuwa ni siku ya nne na walikuwa wameshamzika. Na Yesu alipokuwa amekaribia pale kijijini, Maria alimkimbilia ili kukutana naye. Alikuwa amesikia kuwa Yesu yuko njiani anakuja. Na mara alipomwona, Martha alimwambia, “Bwana, kama ungalikuwepo hapa, ndugu yangu hangalikufa” (mstari 21,22).

 

Yesu akamfariji akamwambia, “Ndugu yako atafufuka” (mstari23). Martha; aliamini kwamba, “Najua ya kuwa atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho” (mstari 24). Kisha Yesu akawambia, “Mimi ndimi huo ufufuo. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi na uzima” (mstari 25). Watu wote wanakufa, bali wale wamwanio Bwana Yesu Kristo na kuishi kwa kufuatana na mafundisho yake, atafufuka wakati Yesu atakaporudi. Na watu hao hawatakufa tena. Wao wataishi milele. Na hili lilikuwa ni tumaini la Martha pia. Na pasipo kusisita, akiwa na uhakika kabisa alimjibu, “Mimi nimesadiki, kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yule ajaye ulimwenguni” (mstari 27).

 

Na sasa akiwa ameshampata Bwana Yesu na akiwa ametiwa nguvu na mazungumzo waliyokuwa nayo, Martha alikwenda kumtafuta Maria na akamwambia kwa faragha, “Mwalimu yupo na anakuita” (mstari 28).

 

Maria akaondoka ndani ya nyumba haraka kwenda kumlaki Bwana.

 

LAZARO ANAFUFUKA

Wakati Maria alipomwona Yesu, maneno yake ya kwanza yalikuwa: “Bwana, kamawewe ungelikuwapo hapa ndugu yangu asingekufa” (mstari32). Alikuwa amehuzunika sana na wakati Yesu alipomwona akilia na pia Wayahudi wengine waliokuwa wamefuatana na Maria nao walikuwa wanalia, Yesu na yeye akalia. Akawauliza kaburi la Lazaro mahali lilipo. Na baadhi ya Wayahudi, waliomwona Yesu akilia, wakasema, “Angalieni jinsi alivyompenda”. Na wengine wakasema, “Je! huyu aliyemfumbua macho yule kipofu, hakuweza kumfanya na huyu asife?” (mstari 36-37).

 

Watu wote wakakusanyikia pale penye kaburi alimozikwa Lazaro, alikuwa amezikwa katika nguo za kitani, yamkini kaburi lake lilikuwa lilichongwa katika mwamba upande wa mlima. Lilikuwa limefunikwa kwa njiwe ambalo liliwekewa muhuri. Ndipo Yesu akasema, “Liondoeni jiwe” (mstari 38). Ilikuwa ni siku ya nne tangu afariki. Ni dhahiri kuwa mwili wake uikuwa umeanza kuoza na kunuka pia na Martha alikuwa akihofia jambo hilo kuwa Yesu atakuwa anajua hivyo.

Taratibu Yesu alimwambia, “Mimi, sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu” (mstari 40). Kwa hiyo jiwe lilivingirishwa, likaondolewa na Yesu akamwomba Baba yake, akamshukuru Mungu kwa kuwa anamsikia na kwa kumpatia nafasi hiyo muhimu ili kuonyesha nguvu za Mungu kwa watu.

 

Kisha, kwa sauti kuu, akaita, “Lazaro, njoo” (mstari43). Kwa mshangao na kwa furaha ya wale waliokuwa wamesimama pale, Lazaro akatoka ndani ya kaburi akatembea hali akiwa bado amefungwa sanda.Yesu akasema, “mfungueni, na mmwache aende zake”(mstari 44)

 

WENGI WAKAAMINI

Wayahudi wengi sana baada ya kuuona mwujiza huu wa kushangaza, ambapo mtu aliyekuwa amekufa alirudi kuwa hai. Mara hii tena Yesu alidhihirisha nguvu za Mungu alizopewa, ili watu wapate kumwamini kuwa yeye ni Mwana wa Mungu.

 

Baadhi ya walikuwepo siku ile, hata hivyo, walikuwa wale wenye mioyo migumu, ambao walikataa kuamini kile walichokiona kwa macho yao kuwa ni kweli. Badala yake, walikwenda kwa Mafarisayo na kuwaambia yote yaliyotenda. Mara moja mkutano wa kamati (Sanhedrin) uliitishwa na Wakuu wa makuhani na Mafarisayo na wakaamua kwamba Yesu ni lazima auawe. Waliweza kuona kuwa watu wengi sana sana walikuwa wakiendelea kumwamini. Ni lazima hali hiyo isitishwe kabisa vinginevyo utawala wa Rumi utaingilia kati.

 

Na kama hali hiyo ingetokea basi viongozi wote walikuwa wakiogopa wasipoteze nafasi zao za uongozi mbele ya watu. Ni jinsi gani walivyokuwa waovu.Kuanzia wakati huo na kuendelea wakaamua kupanga njama za kumwua (mstari 53)

 

FUNDISHO KWETU

Maria na Martha walikuwa wakata tamaa kwa kuwa Yesu hakufika kwa muda mwafaka kuweza kumsaidia ndugu yao kabla hajafariki. Na hatimaye waliweza kufahamu kuwa kuchelewa kwa Yesuilikuwa ni mhimu sana ili waweze kuona fundisho kuu la mwujiza wa ufufuo wa ndugu yao, uliosababisha Mungu kutukuzwa.

 

Wakati mwingine inaonekana kwetu, kuwa Mungu hajibu mombi yetu. Huwa anajibu, lakini huwa wakati mwingine jibu la Mungu ni tofauti na tunavyotegemea. Hata baba zetu hawa wa duniani huwa hawatupatii kila kitu tunachowaomba kila wakati, kwa sababu wanajua kuwa siyo vyote vinavyokuwa vizuri kwetu wakati huo. Na hivyo ndivyo anavyofanya Baba yetu wa mbinguni. Jambo moja tunalolijua kama Mungu alivyotuambia kupitia mtume Paulo, “Katika mambo yote, Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao, yaani wale walioitwa kwa kusudi lake” (Rumi 8:28).

 

Hebu na tuwe kama Maria na Martha, walioendelea kumwamini Yesu hata baada ya ndugu yao kufariki. Na kama Maria alivyosema, tunajua kuwa Yesu atarudi tena duniani kuwafufua rafiki zake wote waliolala mauti na atawapatia thawabu kwa ajili ya imani yao uzima wa milele, maana alisema, “Mi mi ndimi ufufuo na uzima”.

 

MAELEZO YA NYONGEZA

Tunafahamu kuwa Lazaro aliendelea kuishi na Maria na Martha hadi wakati wote watatu walipofariki. Lazaro kwa wakati huo hakufufuliwa tena, lakini wote watatu walishiriki tumaini la utukufu, na wakati Kristo atakaporudi, atawafufua waliokufa na kuwapatia wafuasi wake waaminifu uzima wa milele.

 

Na baadhi ya viongozi wa Wayahudi, wa, walioitwa Masadukayo, hwakuamini katika ufufuo. Hata hivyo tunafahamu kuwa Ibrahimu aliamini kwamba Mungu atawafufua waliomufa (soma Hesabu 11:17-19) na ndivyo hata Daudi livyoamini (soma Matendo ya Mitume 2:29-31). Ibrahimu ni lazima afufuliwe ili aweze kupokea ahadi ya kuirithi nchi ya Israeli, kwa kuwa Mungu alimwahidi nchi hiyo yeye na uzao wake milele (Mwazo 13:14-15). Daudi ni lazima afufuliwe kutoka katika wafu kwa sababu Mungu aliahidi kwamba uzo wake, Bwana Yesu Kristo, ambaye ataketi katika kiti cha enzi Yerusalemu milele na Daudi atamwona kwa macho yake (2 Samweli 7:16). Hili lilikuwa ni moja ya fundisho muhimu sana la Mitume, baada ya Yesu mwenyewe kufufuka. Ni zaidi ya mara moja, Mtume Paulo aliweza kujitetea mwenyewe mbele ya viongozi, alithibitisha: “Kwa ajili ya ufufuo wa wafu, ninahukumiwa mbele yenu hivi leo” (Matendo ya Mitume 24:21. Soma pia 24:14-15; 26:6-7; 23:6). Alipokuwa akiwaandikia Wakorintho alisema kwamba kama hakuna kiyama ya wafu, sisi tutakuwa na hasara ya mambo yote, maana ahadi zote za Mungu alizoahidi zinategemea ufufuo.

 

Yesu Kristo mwenyewe alikuwa ni wa kwanza kufufuka kutoka kwa wafu na kuishi milele (1 Wakorintho 15:20). Na wote wamwaminio Kristo na wakiwa wamebatizwa watapata thawabu wakati atakaporudi (1 Wakorintho 15:23).

 

MASWALI

Majibu ya Mafupi

1. Ni nani walikuwa rafiki wa Yesu walioishi Bethania?

2. Ni ujumbe gani ambao Maria na Martha walioutuma?

3. Ni kwanini Yesu hakwenda mara moja Bethania?

4. Ni kwanini mitume alihofia wakati alipowaambia kuwa waende Yudea?

5. Lazaro alikuwa mekufa, lakini Yesu aliwaambia nini wenafunzi wake kuhusu Lazaro?

6. Je, Yesu alimwambia Martha kuwa yeye ni nani?

7. Maria na Martha kila mmoja alimwambianiniwalipokutana naye?

8. Walipofika penye kaburi la Lazaro, Yesu aliwambia wafanye nini?

9. Ilikuwa ni siku ngapi tangu afariki?

10. Baada ya Yesu kumwomba Mungu, alili, akapaza sauti. Alipaza sauti Akasemaje?

11. Palitokea nini baada ya Yesu kuita kwa sauti?

12. Baada ya Wakuu wa Makuhani na Mafarisayo kusikia mwujiza huu wa kushangaza

waliamu nini?

Majibu ya Kina

13. Yesu alipokea ujumbe wa huzuni kutoka kwa Martha na Maria kuwa Lazaro

anaumwa. Elezea yaliyotokea na jinsi dada hao walivyopata furaha tena.

 

Majibu ya Nyongeza

14. Yesu akasema, “Mimi ndimi ufufuo na uzima”

(a) Martha aliamini ninikuhusu ufufuo?

(b) Ni kwa nini Ibrahimu na Daudi ni lazima wafufuke?

(c) Ni akina nani tena watakaofufuliwa?

(d) Ni lini ufufuo utakapofanyika?

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Swahili Title
092 KUFUFUKA KWA LAZARO
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type