CSSA 1-4-18 - JESUS ENTERS JERUSALEM

Swahili

93. YESU ANAINGIA YERUSALEMU

“Amebarikiwa yeye ajaye kwa jina la Bwana”

 

Shabaha

Kuonyesha jinsi Yesu alivyoipenda Yerusalemu lakini akaongea nyakati za hatari kwa watu wake kwa sababu ya kutokuamini kwao. Wakati wa Pasaka ulikuwa ulikuwa umekaribia tena na barabara za kwenda Yerusalemu zilikuwa zimejaa wasafiri. Watu wengi walikuwa wakitokea Bethania, ambayo ilikuwa barabara ya kwenda Yeriko, ili kuweza kumwona Lazaro, ambaye alikuwa amefufuliwa kutoka katika wafu. Pale katika kijiji kidogo cha Bethania, watu wengi waliamini wakati walipomwona Lazaro akiwa hai tena na wakasikiliza mafundisho ya Yesu. Hii ilifanya wakuu wa makuhani kukasirika na kupanga mbinu za kumwua Lazaro pia (Yohana 12:9-11). Walikuwa wameandaliwa kwenda mbali mno kuwazuia watu wasimwamini Yesu kuwa ni Mwana wa Mungu. Yesu, hata hivyo, alikuwa anajua kuwa muda ulikuwa umekaribia kazi yake kumalizika. Alijua uchungu wa mateso uliokuwa unamsubiri baada ya muda mfupi tu huko Yerusalemu, lakini alikuwaamezimia kuyafanya mapenzi ya Mungu.Siku tano kabla ya Pasaka alikwenda nyumbani kwa Maria, Martha na Lazaro.

 

Marko 11:1-21.Tazama pia Mathayo 21:1-22:1; Luka 9:28-40, 45-48; Yohana12:12-15

 

AKAPANDA YESU JUU YA MWANA PUNDA

Akiwaanatoka Bethania (Yohana 12:12), Yesu alianza kuiandaa safari yake kuelekea Yerusalemu. Kulikuwa na sauti ya kelele za furaha za watu walioungana na Yesu njiani. Akawatuma mitume wake wawili kwenda mbele yake katika kijiji cha karibu, kilichoitwa Bethfage. “Nendeni mpaka kile kijiji kinchowakabili; na katika kuingia ndani yake, mara mtamwona mwanapunda amefungwa, asiyepandwa na mtu bado; mfungueni, kamleteni” (mstari2). Na kama mtu yeyote angewauliza walikuwa wakifanya nini, kumfungua punda na mwanapunda, walipaswa kusema, “Bwana ana haja naye” (3).

 

Na kwa hiyo mitume wakaondoka na kufanya kama walivyoambiwa na akarejea wakiwa na punda na mwana punda wake. Hakuna mtu yeyote aliyekuwa ameshabebwa na huyu mwanapunda, kwa hiyo Yesu akakusudia kumpanda wakati alipokuwa akienda. Ilikuwa ni ishara kwa watu wote kwamba alikuwa ni mfalme wao, kwa kuwa, tangu siku za kale wafalme walifanya hivyo (soma 1:33, 38-39, ambapo Daudi alimtangaza Sulemani kuwa mfalme).

 

YESU ANAINGIA YERUSALEMU

Kwa hiyo wanafunzi wake wakaweka nguo zao juu ya mwanapunda huyo na Yesu akampanda kuelekea Yerusalemu. Watu wengi waliokuwa waliomfuata wakawa na mshangao wa furaha walipoyaona yaliyotendeka. Waliweza kwa haraka kufuata yale yaliyokuwa wamefanywa na mitume wakatandaza nguo zao chini ya njia aliyokuwa akipita, kama ishara ya heshima kwake yule aliyempanda mwanapunda. Bila shaka wanafunzi wenyewe walihisi kuwa hatimeye Yesu ataurudisha ufalme kwa Israeli na kuundoa utawala wa Rumi uliokuwa umechukiwa katika nchi. Wakati watu walipotaka kumweka Yesu kuwa Mfalme kabla ya wakati, hakukubali ufalme. Hata hivyo, sasa, akawahimiza wao wamtambue yeye kuwa ni mfalme wa Israeli.

 

Habari kuwa Yesu amekaribia kuingia Yerusalemu zikaenea katika vijiji na katika nyumba zilizokuwa kandokando ya njia hiyo ya kuelekea Yerusalemu. Watu wengi wakakata matawi ya mizeituni na wakaenda kukutana na Yesu (Yohana 12:12-13). Na kwa kadri watu walivyoongezeka, wakaimba nyimbo za kumsifu na kushangilia, ambapo nyimbo hizo zilikuwa ni kati ya zile zilizo katika Zaburi na hasa zie zilizoimbwa wakati wa Pasaka. “Hosana, Mana wa Daudi: Amebarikiwa yeye ajaye kwa jina la Bwana;Hosana juu mbinguni” (Mathayo 21:9).

 

Na kusanyiko hilo walipofika katika Mlima wa Mizeituni, wakaanza kushuka mlima huo kuelekea Yerusalemu, mji uliochaguliwa, “kundi nzima la wanafunzi wake walianza kufurahia na kumsifu Mungu kwa sauti kuu, kwa ajili ya matendo yote ya uwezo waliyoyaona” (Luka 19:37).

 

Walikuwemo baadhi ya Mafarisayo katika umati huo wa watu ambao waliposikia nyimbo za zaburi zikiimbwa kwa heshima ya Yesu wakashikwa na hasira. Wakamwambia Yesu, “Mwalimu uwakanye wanafunzi wako”; Yesu akawajibu, “Nawaambia ninyi, wakinyamaza hawa, mawe yatapiga kilele” (Luka 19:39-40).

 

Hatimaye Yesu kwa shangwe akaingia Yerusalemu, kama nabii Zekaria alivyokuwa ametabiri miaka mia tano iliyokuwa imepita kabla (Mthayo 21:4-5). Akaingia hekaluni na akatazama sehemu alizoweza kuona. Hapakuwa na badiliko yeyote tangu mara yake ya kwanza, miaka miatatu na nusu kabla, wakati alipozipindua meza na kufukuza wafanyabiashara (Soma Somo 5). Watu wale walikuwa wamekasirika sana alipowingilia wakati huo, hapakuwa na badiiko lolote. Kwa huzuni Yesu aliondoka na kurudi Bethania usiku huo

 

FUNDISHO KUHUSU MTINI

Siku iliyofuata, asubuhi Yesu alirudi Yerusalemu. Alikuwa na njaa, na akaona mti wa mtini, akauendea ili achume matunda ya mtini. Na wakati alipokwenda penye mti, aliona kuwa ingawa mti ule ulikuwa umestawi vizuri sana na ulikuwa umefunikwa na majani mengi ya kijani kibichi, lakini haukuwa na matunda.

 

Jinsi gani taifa la Israeli lilivyokuwa kama mti huu wa mtini. Na kila sehemu Yesu alikokwenda watu walionekana kulipenda Neno la Mungu, na watu wengi wakashangazwa na miujiza yake aliyoitenda. Taifa likaonekana kumcha Mungu. Ilikuwa ni ishara ya nje kutenda haki, kama vile mti wa mtini uliokuwa na majani mengi mazuri ya kijani kibichi. Bado Yesu alilijua pia taifa vizuri kuwa walikuwa hawawezi kuwa matendo mazuri yanayotokana na kazi nzuri ya Mungu. Katika maisha yao walikuwa hawamheshimu. Kwa muda wa miaka mitatu na nusu Yesu alikuwa amezunguka kwa watu wa taifa la Israeli, akiangalia kama kulikuwa na badiliko lolote la mioyo yao, lakini hapakuwa na badiliko.

 

Yesu akasema, “Yasipatikane matunda kwako kamwe tangu leo hata milele”, akaulaani mtini (Mathayo 21:19). Kwa mshangao, wanafunzi wakouna mti wa mtini ukinyauka na kukauka mbele ya macho yao.

 

Yeke yake ndiye aliyejua kwa wakati huo kuwa taifa la Israeli baada miaka michache litanyauka na kufa. Alifahamu kuwa watu waliokuwa wakiimba nyimbo za kumsifu siku kabla ya kifo chake wataungauna pamoja na viongozi wa watu ili wamhukumu kifo. Taifa kama hilo, linalomwua Mwana wa Mungu, lilikuwa linastahili kungamizwa kabisa.

 

KUTAKASWA KWA HEKALU

Akaondoka pale penye mti wa mtini, Yesu akaelekea mjini, akifuatana na wanafunzi wake. Mara hii tena akaingia hekaluni. Tukio aliloliona kwa macho yake lilikuwa ni lilelile aliloliona kabla, lile aliloona miaka mitatu na nusu kabla. Na hii ilikuwa ni nyumba ya Mungu. Makuhani walikuwa wakifanya nini hata wakaruhusu mambo kama hayo kufanyika katika nyumba ya Mungu? Walikuwa ni sawasawa na mti wa mtini usiokuwa na matunda, pamoja na jinsi walivyoonekana mbele za watu lakini hawakuwa na matunda.

 

Walionekana watu watendao haki walipokuwa wakisimama hali wamevaa mavazi yao ya ukuhani lakini katika mawazo ya mioyo yao walikuwa mbali na Mungu. Maana waliweza kuwa majiri kwa ajili ya kuruhusu matendo kama hayo ya uovu kufanyika ndani ya hekalu. Hali Yesu akiwa amekasirika akazipindua meza za wabadilisha fedha na akawafukuza wale waliokuwa wakiuza na kununua, akasema, “Imeandikwa nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala” (Luka19:46).

 

Watu wakastaajabu kwa yale aliyoyatenda nao wakashika maneno yake. Hakika huyu hapa alikuwa kiongozi, ambaye alinena na kutenda kwa mamlaka. Na kwa hiyo walimsikiliza kwa makini wakati alipokuwa akiwafundisha. “Lakini wakuu wa makuhani, na waandishi, na wakuu wa watu walikuwa wakitafuta njia ya kumwangamiza” (mstari 47). Walikuwa wamekwisha amua kumwua Yesu, lakini walikuwa wanamwogopa Yesu na waliwogopa watu wengine pia wala hawakujua jinsi ambavyo wangefanikiwa kumwua. Baada ya muda mfupi, Yesu akaondoka mjini akiwa na wanafunzi wake.

 

FUNDISHO KWETU

Waisraeli walishindwa kuelewa fundisho ambalo Yesu alikuwa anawafundisha. Ulikuewa ni ujumbe wa ule ule ambao Yohana Mbatizaji alifundisha, kabla ya Yesu kuja: “Zaeni matunda”

Tunaweza kujifunza habari historia ktika Biblia na tunaweza kujifunza majibu ya maswali, lakini kama hatuwezi kubadilika kutokana na haya tunayoyasoma na kujifunza, basi juhudi zetu zote kwa Mungu hazimfurahishi. Ni ishara ya nje ili watu watuone.

 

Yesu aliulaani mti wa mtini kwa sababu haukuzaa matunda. Yohana Mbatizaji alisema: “Kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni” (Luka 3:9).

 

Tunaweza kufanya nini? Kama tumekuwa ni wachoyo, ni lazima tubadili mwenendo na tabia zetu na kujifunza tusiwe wachoyo, kufikiria jinsi ya kuwafurahisha wengine. Na kama tumekiwa wenye kiburi na majivuno, ni lazima tujifunza kuwa wapole na tuwasifu wengine tu. Katika maisha yake yote Yesu ameuachia kielelezo kamili. Na mapemaatarudi ili kuona kama tumefanya kwa vitendo yale ambayo tumejifunza. Mpaka atakaporudi ni lazima twendelee kuamini Neno la Mungu na kulitii.

 

MAELEZO YA NYONGEZA

Wakati Yesu alipopanda mwanapunda na kwenda Yerusalemu kama mfalme, watu wengi walistaajabu na kufurahia wakitegemea jambo kushangaza kutokea. Hata hivyo, Yesu alihuzunika. Alihuzunika, siyo kwa sababu ya mateso ambayo alijua kuwa yatampata baadaye, bali alihuzunika kwa ajili ya Yerusalemu. Watu wakiwa katika hali hiyo ya furaha wakiwa wameukaribia mji akautazama mji ambao aliupenda sana na akaulilia Yeruslemu (Luka 19:41). Ulikuwa ni mji ambao Mungu aliuchagua ili kuliweka Jina lake pale (Zaburi 87:2-3; Zaburi 132:13-14; 1 Wafalme 9:3).

 

Naye aliuita mji wa mfalme mkuu (Mathayo 5:35), kwa maana katika mji huo siku moja Yesu atatawaa akiwa ni mfame akiwa ameketi kwenye kiti cha enzi cha Daudi, akiutawala ulimwengu wote (Luka 1:32-33). Hata hivyo Yesu alipoutazama huo mji aupendao, alilia, kwa sababu alijua maangamizi ambayo yangeupata mji huo yaliyokuwa mbele yake. Wale walokuwa wamesimama mbele yake walimsikiaaliposema. “Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote; watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako” (mstari 43-44).

 

Mambo haya yakajakutimia sawasawa kama Yesu alivyokuwa amesema na tena baada ya miaka michache tu tangu alipokuwa amesema. Ilikuwa ni baada ya kuwaonyesha mwujiza katika mfano wa mti wa mtini. Viongozi wa taifa waliwageuza watu wamchukie Yesu na hatimaye wakamsulibisha, kama tutavyoona katika masomo yanayofuata. Mungu asingeweza kuwaachilia watu hao waovu wasiadhibiwe. Na hakuna mmoja ambaye angefikiria kuwa angeweza kuruhusu hekalu hilo lililokuwa zuri sana, lakini jengo tu peke yake lilikuwa halina thamani yeyote, ikiwa ibada zilizofanyika ndani yake zilikuwa ni za kumchukiza Mungu.

 

Kwa hiyo, katika mwaka 70BK, Jeshi la Rumi wakauteka Mji wa Yerusalemu na hekalu wakalitetekeza kabisa. Hakuna jiwe lililosalia juu ya jiwe lingine mpaka leo hii. Watu waliokuwa wamesanyikia ndani ya mji wakati huo walidhania kuwa watasalimika, walifia ndani ya kuta.

 

Na wale waliokuwa wamekimbilia mbali na mji ndiyo waliobakia wakiwa wametawanywa katika mataifa duniani kote. Ni wakati huu tu, katika miaka ya maisha ya wazazi wako au babu zako ndipo Wayahudi wameza kurudi tena katika nchi yao na Israeli limerudi tena kuwa taifa. Na Yerusalemu ambao umekuwa ukikanyagwa na mataifa kwa takribani miaka elfu mbili umerudi tena kuwa mji mkuu wa Israeli kipenzi cha Wayahudi wote kote duniani. Mambo haya yanatfanya tushangae kwa furaha, kwa sababu ni dalili za uhakika kwetu kwamba kuruja ka Kristo kumkaribia.

 

Lakini bado mambo ya kutisha yanaisubiri Israeli kuwapata na watu wake, ambayo hawategemei, ingawaje Mungu aliyaongea hayo kupiti manabii wa Agano la Kale. (Soma Z:14:2-3; Yoeli 3:1-3). Hata hivyo jambo la kushangaza ni kwamba wataokolewa watoke katika wakati huo wa dhiki na mwokozi wao atakuwa Yesu Kristo, mtu yule ambaye wazazi wao walimkataa na kumwua. Jinsi Mungu wetu alivyo wa ajabu, kwa kuonyesha rehema kwa Israeli na kutupatia sisi tumaini la utukufu. Hakika tunatamani sana kuona amani ya Yerusalemu, maana wakati amani itakapokuwepo Yerusalemu, basi itakuwepo amani dunia yote.

 

MASWALI

Majibu Mafupi

1. Yesu aliwatuma wanafunzi wake walete nini kutoka Bethifage?

2. Ni kwa nini Yesu alikwenda kumpanda mwanapunda?

3. Watu walifanya nini kama ishara yaheshimakwa Yesu alipompanda Mwanapunda?

4. Watu waliimba wimbo gani wakati alipokuwa akielekea Yerusalemu?

5. Yesu aliwaambia nini mafarisayo walipomwambia awazui watu wasiimbe?

6. Yesu aliona nini ndani ya Hekalu wakati huu?

7. Ni kwa nini Yesu liulaani mtibwa mtini, wakati elipokuwa njiani kuelekea Mjini?

8. Ni kwa jinsi gani Israeli walivyofarana na mti wa mtini?

9. Yesu aliwambia nini wakati alipowafukuza wafanya biashara kuondoka ndani ya hekalu?

10. Nifundisho gani la mti wa  mzeituni kwetu?

11. Yesu aliingia Yerusalemu siku chache kabla ya Pasaka?

       a. Ni jinsi gani alivyompata  mwana punda wa kumpanda?

       b. Ni kwa nini alipanda mwana punda?

       c. Eleza jinsi ilivyotokea njiani?

12.  a. Nielezekilichotekea, wakati Yesu alipoona mtini, wakati alipokuwanjiani kwenda

           Yerusalemu?

       b. Makuhani walifananaje na mti wa mizeituni?

       c. Yesu lifanya nini alipoingia hekaluni ?

       d. Yesu alisema nini juu ya hekalu?

 

Majibu ya Nyongeza

13. Wakati Yesu alipoendesha  kuelea Yerusalemu, watu walifurahi, lakini Yesu Alihuzunika?

      a. Ni kwa nini Yesu alihuzunika?

      b. Ilitokea nini Yerusalemu mwaka 70BK?

      c. Ni kwa nini inashangaza kuona Yerusalemu ukiwa ni mji wa mfalme mkuu siku hizi?

      d. Ni nani atakayeleta amani Yerusalemu na duniani kote?

 

 

Swahili Title
093 YESU ANAINGIA YERUSALEMU
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type