97. MASHITAKA JUU YA YESU
“Hatuna mfalme, ila Kaisari”.
Shabaha
Ni kuonyesha jinsi Yesu alivyoshitakiwa kwa uongo na Wayahudi na watu wa Mataifa na akahukumiwa kifo. Wakati Yesu alipojisalimisha kwa maaskari ambao walikuja kumkamata, wanafunzi wake hawakujua la kufanya. Walihofia maisha yao, kwa kuwa ikiwa watu hawa watamwua Yesu, hawatawaua pia wanafunzi wake? Hawakuelewa pia kwamba imempasa Yesu kufa kwanza, ili maandiko yatimizwe, na kisha baada ya hapo atukuzwe. Petro na Yohana hata hivyo hawakuweza kukata tamaa. Walifuatilia ni lipi litakalompata bwana yao mpenzi, ambaye alikuwa amejiandaa kuyatoa maisha yake kwa ajili yao. Walkuwepo pale nyumbani kwa Kuhani Mkuu wakati Yesu alipokuwa akiulizwa maswali.
Yohana18:19-40; 19:1-16. Soma Mathayo 26:57-27:26; Marko 14:53-15:15; Luka 22:54- 23:25.
NYUMBANI KWA KUHANI MKUU
Kuanzia wakati huo na kuendelea Yesu alichukuliwa kutoka kwa mtu mmoja mwenye mamlaka hadi kwamwingine. Na sasa viongozi wa Wayahudi walikuwa wamemkamata yeye, walipumzika usiku ule tu na siku iliyofuata walimtafutia mashitaka ambayo hukumu yake ilikuwa ni kifo, kama walihitaji kumwua Yesu kabla ya sikukuu ya Pasaka kuanza. Kwa hiyo walimpeleka Yesu kwanza kwa Anasi, ambaye aliishi makao makuu ya Kuhani Mkuu, lakini ingawa mtu huyu alimwuliza Yesu Maswali mengi, hakupata kosa lolote la kumsaidia ili kumshitaka Yesu. Na kutoka hapo, maaskari walimpeleka kwa Kayafa, aliyekuwa kuhanib Mkuu. Wakuu wa makuhani, wazee na wandishi walifika kwa kuwa asubuhi ilikuwa imeanza. Kufuatana na sheria, mashahidi wawili walitaiwa kuthibitisha hatia ya mtu (Kumbukumbu la Torati 17:6). Wakawaleta mashahidi wengi wa uongo, lakini hata hivyo hawakusema neno lolote juu yake limpasalo kufa. Na mwisho mtu mmoja akawaleta mashahidi wawili wa uongo waliokuwa tayari kumshitaki Yesu, hata hivyo ushahidi wao ulitofautiana. (Kumbuka, kuwa katika baraza hili walikuwepo watu wawili ambao walikuwa waaminifu na wapenda haki. Nikodemu na Yusufu wa Alimataya, ambao hatimaye waliuchukua mwili wa Yesuna kumzika, wasingekubaliana na mambo yaliyokuwa yanaendelea pale.Hawakuwa na uwezo wa kuwazuia, lakini walifahamu kuwa Yesu hakuwa na hatia. Kwa hiyo wale wazee waovu wa baraza, waliotaka Yesu asurubiwe, walijifaya kufanya mambo yote yaonekane kufanyika kwa uhalali). Katika maswali yote aliyoulizwa, Yesu alikuwa kimya na akanyamaza. Kayafa akawa amechanganyikiwa sana. Kama kweli wangemkuta na kosa lolote, wangeweza kumshitaki Yesu kwa kosa hilo. Na hatimaye Kayafa akamwuliza moja kwa moja: “Utuambie kama wewe ni Kristo, Mwana wa Mungu”. Hili lilikuwa swali ambalo Yesu angelijibu kwa furaha. “Wewe umesema”, alijibu (maana yake, “Ndiyo, mimi ndiye”), na akaongeza, “Tangu sasa mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu ya mbinguni. Kuhani Mkuu akararua mavazi yake, akisema, Amekufuru; tunahajaganitenaya mashahidi? Tazameni, sasa mmesikia hiyo kufuru yake; mwaonaje ninyi? Wakajibu, wakasema, Imempasa kifo” (Mathayo 26:63-66). Kuanzia hapo na kuendelea ndipo Yesu wakamtemea mate ya uso, wakampiga makonde na wakampiga makofi na maaskari jeuri wa kuhani mkuu, hawakumwogopa tena, kama walivyokuwa kule bustani, kwa jeuri wakamdhihaki. Yesu akavumilia yote na wala hakupinga, maana kweli alikuwa ni Mwana wa Mungu.
YESU MBELE YA PILATO
Siku iliyofuata asubuhi walimpeleka haraka Yesu kwa Pontio Pilato, ambaye alikuwa ni mtawala (Gavana) wa Rumi pale. Na sasa walikuwa wameshaamua kuwa Yesu ni lazima afe, walitaka Warumibwamsurubishe, wampigilii misumari juu ya mti. Kwa mjibu wa Sheria, kila mtu aangikwaye juu ya mti “alikuwa amelaaniwa na Mungu” (Kumbukumbu la Torati 21:23). Walitaka kila mmoja amwone na wamfikirie kuwa amelaniwa na Mungu. Wakamwambia Pilato kuwa Yesu amesema kuwa ni Kristo, mfalme, akijifanya mkuu kinyume na Kaisari, mtawala wa Rumi. Pilato akamwuliza Yesu, lakini hakumwona na kosa lolote mtu huyu aliyekuwa amesimama kwa upole mbele yake. Hii ilisababisha Wayahudi wawe na hasira. Kwa hiyo wakamshitaki kuwa “anasababisha fujo, amepotosha watu kuanzia Galilaya mpaka Yerusalemu”. Na Pilato alipowasikia wakitaja “Galilaya”, aliamua kumpeleka Yesu kwa Helode, ambaye kwa wakati huo alikuwa Yerusalemu, maana Galilaya ilikuwa iko chini ya mamlaka ya Herode( Luka 23:2-7).
YESU MBELE YA HERODE
Helode alikuwa amesikia habari nyingi kuhusu Yesu. Alifurahi sana kupata nafasi hii ya kumwona Yesu. Yamkini alitegemea kuwa atatenda mwujiza. Ingawa alimwuliza maswali mengi, lakini Yesu alikataa kumjibu mtu huyu mwovu. Wakuu wa Makuhani na waandishi walisimama kando wakitazama walipiga kelele wakimshitaki. Herode, hata hivyo hakuna kosa lake yeye na maaskari wake walipokwisha kumdhihaki, alimrudisha tena Yesu kwa Pilato (Luka 23:8-11).
YESU MBELE YA PILATO TENA
Pilato alitegemewa kumwachilia Yesu, maana yeye na Herode hakuna aliweza kuona kosa la Yesu, na Pilato alifahamu “kuwa wanamshitaki kwa sababu ya wivu” (Mathayo 27:18). Alihangaika sana yeye pia alipopokea ujumbe wa kuitwa kwa dharura kutoka kwa mke wake, akisema: “Usiwe na neno na yule mwenye haki; kwa sababu nimeteswa mengi leo katika ndoto kwa ajili yake” (mstari 19). Pilato sasa alikuwa na nia ya kumruhusu Yesu aondoke kwa uhuru. Ilikuwa ni desturi ya gavana kumsamehe mfungwa mmmoja Myahudi mara moja kwa mwaka, wakati kama huu, kwa sababu ilikuwa ni sikukuu maalum. Kwa hiyo Pilato aliitumia desturi hii ili kujaribu kumwachilia Yesu. Alikuwepo mfungwa kwa wakati huo, jina lake Banaba, mtu mbaya, jambazi na mwuaji. Ndipo Pilato akamleta Baranaba na akawauliza, “Mnataka niwafungulie yupi? Yule Baraba au Yesu aitwaye Kristo” (mstari 17). Alitegemea kuwa watu wataona tofauti iliyopo kati ya watu hawa wawili. Lakini wakuu wa makuhani na wazee alikuwa wameshawashauri watu wote wa mkutano kuwa waombe Baranaba na Yesu afe. Akawauliza watu amfanye nini Yesu, nao wakasema kwa sauti, “msulubishe”. Pilato akashangaa: “Kwani, ni ubaya gani alioutenda?” Hii iliwafanyawapigekelele kwahasira, “msulibishe” (Marko 15:12-14). Pilato akasema, “Je, nimsulubishemfalme wenu?”(Yohana 19:15). Pilato alitaka kuwatuliza watu, ingawaje alifahamu kwamba Yesu hakustahili kufa. Kwa hiyo akaomba aletewe bakuli la maji na akanawa mikono yake hadharani mbele ya watu akasema, “Mimi, sinahatiakatika damu ya mtu huyu mwenye haki, yaangalieni haya ninyi wenyewe”. Watuhawakujali. Wakajibu, “Damu yake na iwe juu yetu, na ya watoto wetu” (Mathayo 27: 24-25). Matokea ya uovu huu ya machukizo ya maneno haya ilikuwa kwamba Mungu akaleta hukumu ya kutisha kwao katika mwaka 70KK, kwa ajili ya kumkataa Mwana wake na watoto wao wmeendelea kuwa katika mateso tangu wakati huu. Kwa hiyo Pilato, “akipenda kuwarithisha makutano akawafungulia Baraba, na akamtoa Yesu baada ya kumpiga mijredi, ili asulubiwe” (Marko 15:15).
FUNDISHO KWETU
Bwana Yesu Kristo, katika mashitaka yote ya kutisha, ametuachia kielelezo kizuri ajabu ili sisi tuwezekufuata. Na aliposhitakiwa kwa uongo kuwa ametenda maovu, hakuweza kujitetea mwenyewe. Alipopigwa na kudhihakiwa hakurudisha. Mtume Petro aliyakumbuka mambo haya vizuri na mwisho aliandika juu ya habari yao katika waraka: “Maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yetu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake. Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekanakinywani mwake. Yeye alipotukanwa hakurudisha matukano; alipoteswa, hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki” (1 Petro 2:2-23). “Aliyastahimili yote haya (na lilikuwepo baya zaidi ambalo lilikuwa mbele yake), kwa sababu ya furaha iliyowekwa mbele yake” (Waebrania 12 :2). Alifahamu kwamba itampendeza Baba yake. Hatuwezi kamwe kuyakabiri mambo yale aliyoyastahimili, lakini Mungu anatutaka tuonyeshe imani kama hiyo na ujasiri kila mara tunapokutana na majaribu. Pia kuna mafundisho tunayoweza kujifunza kutokana vitendo vya Pilato na watu. Pilato alikuwa na wasiwasi na nafasi yake ya gavana, kuliko kufanya lililo la haki. Ni jinsi gani alivyokuwa mtu dhaifu sana. Hata watu pia walikuwa wepesi sana kugeuka kuachana na yle yaliyokuwa y haki na kufuata ushauri wa mbaya wa viongozi waovu. Wakati tunapojua jambo lililo kweli na la haki, hebu tulifanye hilo. Hatutakiwi kuruhusu matendo mabaya yatupofushe sisi kwenye kweli, maana mabaya huongoza kwenye chuki na chukihuongoza kwenye mauaji, kma ilivyokuwa katika siku hizo.
MAELEZO YA NYONGEZO
Tukio lingine moja la kuhuzunisha lilitokea usiku huo.Wakati Yesu alipokuwa amekamatwa, wanafunzi wote walikimbia. Petro na Yohana wakafuata “kwa mbali” mpaka wakafika nyumbani kwa Kuhani Mkuu.Yohana yeye akaingia kwa kuwaalikuwa anafahamika kwa Kuhani Mkuu (Yohana 18:15) na akarudi kuongea na mtumishi anayelinda mlango, ambaye alimruhusu Petro kuingia ndani. Pasipo kujua afanye nini, Petro akawa ameketi kati ya watumishi na maafisa ambao walikuwa wanaota moto. Ndipo mjakazi ambaye ndiye aliyemruhusu aingie akamwona pale na akamtazama sana kwa makini akamwuliza, “Wewe nawe, je, humwanafunzi mmojawapo wa mtu huyu?” Lakini Petro akasema, “Si mimi” (Yohana 18:16-17). Hata ikawa baada ya muda mfupi tu akaenda mahali penye behewa, na mtu mmoja akamtazama akamwambia: “Wewe nawe, u mmoja wao”. Lakini, Petro akaseme, “Si mimi” (Luka 22:58). Na baaa ya saa moja, watu waliokuwa wamesimama karibu na Petro wakamwambia tena, “Hakika u mmoja wao, kwa sababu u Mgalilaya wewe”. Petro akakana tena, na kwa hasira akawajibu, “Simjui mtu huyu mnayemnena” (Marko 14:70-71). Ikawa baada ya hapo tu jogoo akawika. Na wakati huo huo, Yesu ambaye alikuwa ndani, akageuka na kumtazama Petro. “Petro akalikumbuka lile neno la Bwanajinsi aivyomwambia, Leo kabla hajawika jogoo utanikana mara tatu” (Luka 22:61-62). Jinsi Petro alivyokuwa na aibu nyingi, na hasa baada majivuno kwamba alikuwa yuko tayari kwenda gerezani na kushughulikia Bwana. Hata ikawa furaha ya habari hii haiishii pale, maana Petro akawa miongoni mwa viongozi wakubwa wa eklesia. Hakika kwa kweli alitubu na hatimaye alivumilia mambo mengine, ikiwa ni pamoja vifungo na kifo, kwa ajili ya Bwana wake. Lipo onyo kubwa sana katika hili kwa ajili ya sisi wote. Wakati Yesu alipowatuma kwanza wanafunzi wake kuhubiri uflme wa Mungu, aliwaambia mateso watakayovumilia. Yesu akasema “Nanyi mtakuwa wenye kuchukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu” (Mathayo 10:22). Lakini hawakutakiwa wawe waoga, kwa kuwa watu watakaosema na kumkili mbele ya watu kwamba wanamwamini Kristo, watapewa thawabu atakapokuja. “Bali mtu yeyote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni” (mstari 33). Na hili ni onyo. Tunapaswa kuonyesha upendo kwake katika mambo yote kama Petro alivyofanya baadaye.
MAASWALI
Majibu Mafupi
1. Wakati Yesu alipokamatwa alipelekwa wapi kwanza?
2. Wazee wawili wa baraza hawakupendezwa jinsi mashitaka yalivyoendeshwa. Hawa
walikuwa ni nani?
3. Ni swali gani ambalo Kuhani Mkuu alimwuliza Yesu mwisho
4. Kuhani Mkuu alimshitaki Yesu kuhusu nini?
5. Ni nani aliyekuwa gavana wa Rumi wakati huo?
6. Ni kwa nini Wayahudi walitaka Yesu afe kwa kuangikwa msalabani?
7. Je, Pilato alimwona Yesu kuwa na hatia?
8. Ni kwa nini Herode alifurahi aliopomwona Yesu?
9. Ni ujumbe gani Herode aliupata kutoka kwa mke wake?
10. Alikuwepo mtu mmoja ndani ya gereza ambaye watu walitaka Pilato amwachilie. Alikuwa
ni nani na kwanini alikuwa gerezani?
11. Watu walitaka Pilato amtendeeje Yesu?
12. Wakuu wa Makuhani walisemaje wakati Pilato aliposema, “Nimsulubishe mfalme
wenu?”
13. Pilato alifanya nini kuonyesha kuwa alimwona Yesu hana hatia?
14. Ni kwanini Yesu alivumilia haya yote?
15. Baraza la Wayahudi lilisema kuwa Yesu alistahili kifo?
a. Kuhani Mkuu alisema nini kuonyesha kuwa Yesu alifanya makosa?
b. Yesu walimshitaki shitaka gani walipompeleka kwa Pilato?
c. Ni kwa nini Pilato alitaka amwachilie Yesu?
d. Watu walitaka Pilato amfungulie nani?
16 a. Pilato alifanya nini wakati watu walipotaka Yesu asulibiwe?
b. Onyesha ni jinsi gani watu hawakujali
c. Ni hukumu gani ya kutisha ambayo Mungu aliileta kwa watu wake kutokana na hili?
17 a. Elezea jinsi Petro alivyomkana Yesu katika nyumba ya Kuhani Mkuu
b. Tunapata fundisho lipi kutokana na tabia ya Petro?
c. Jinsi gani Petro alivyobadilika?