101. KUITWA KWA MTUME MWINGINE
“Mmoja, kutoka kwetu ni lazima achaguliwe ili awe shahidi wa kufufuka kwake pamoja nasi”
MANENO YA MWISHO YA YESU KWA MITUME WAKE (Mistari 1- 8)
Shabaha
Kuonyesha kuwa alipaa kwenda mbinguni baada ya kufufuka kwake na atarudi mapema; nao mitume walimchagua mwanafunzi mwingine kuchukua nafasi ya Yuda Iskariote. 'Mitume ya Mitume' ndicho hicho kitabu cha Biblia, kilichoandikwa na Luka, kinachotuambia mambo yote waliyoyatenda baada ya Yesu kupaa kwenda mbinguni. Baada ya kufufuka kwake Yesu alitumia siku arobaini duniani akiwa na mitume na wanafunzi wengine kabla ya kupaa mbinguni. Wakati huu aliwaambia baadhi ya mambo muhimu kuhusu Ufalme ambao atauweka kwa ajili ya Mungu duniani. Baada ya siku arobaini wanafunzi walimwuliza Bwana iwapo ataweka Ufalme na kutawala akiwa Mfalme wakati huo. Yesu akajibu siyo jukumu lao kuyajua majira na wakati haya yatakapotokea. Hata hivyo Mitume walikuwa na mambo muhimu ya kufanya baada ya Yesu kuondoka. Walitakiwa waihubiri injili katika utawala wote wa dola ya Rumi. Bwana aliwaambia watapokea nguvu za Roho Mtakatifu ili kuwasaidia
Neno “Mtume” maana yake ni “yeye aliyetumwa”. Wangetumwa kwa watu wote Wayahudi na watu wa Mataifa katika dola yote ya Rumi ili waseme mambo yote waliyoyaona na kuyasikia na kujifunza kutoka kwa Bwana Yesu Kristo. Ujumbe ambao Mitume walifundisha uliitwa Injili ambayo maana yake ni “Habari njema” au “Habari za furaha”. Injili ni habari njema ya Ufalme wa Mungu na mambo yote yanayohusu jina la Yesu Kristo. Hakika kweli ni habari njema kwa watu wote wanaoisikia kwa sababu ikiwa wataamini wataokoka (angalia Mkufunzi swali la 72).
YESU ANAPAA MBINGUNI (mstari 9-11)
Yesu alipomaliza kuwaambia Mitume kuhusu kazi ambazo walitakiwa kufanya mara tu akapochukuliwa kutoka kwao na kwenda mbinguni, wakati walipokuwa wakitazama juu kwa mshangao mbinguni Yesu alitoweka katika upeo wa macho yao, alichukuliwa katika mawingu. malaika wawili waliovaa mavazi meupe walitokea na kusema. “Enyi watu wa Galilaya kwa nini mmesimama na kuangalia mbinguni? Yesu huyo huyo aliyechukuliwa juu atarudi kwenu jinsi hiyo hiyo mlivyomwona akienda mbinguni” (mstari 11).
Maneno haya ni muhimu sana na itakuwa vyema kwako kama ujifunza na kuyaweka moyoni mwako. Malaika walikuwa wakiwaambia Mitume jinsi Yesu mwenyewe alivyokuwa akifundisha-ya kuwa atakwenda kukaa mkono wa kulia wa Mungu huko mbinguni. Walimwona wao wenyewe kwa macho yao na kwa hakika atarudi duniani kuuweka Ufalme wa Mungu. Wakati huu umekaribia, na wale wanaomtafuta watamwona upesi.
WANAFUNZI WALIKUSANYIKA GHOROFANI (mistari 12-14)
Yesu alipaa mbinguni kutoka katika mlima wa Mizeituni ambao ulikuwa nje ya kuta za Yerusalemu, Mitume kumi na mmoja walirudi mjini na kisha walikwenda kwenye chumba cha juu walikokuwa wakiishi. Bwana aliwaambia wasiondoke Yerusalemu bali wangojee nguvu za Roho Mtakatifu kama Mungu alivyoahidi(1:4,5) Pale waliendelea kumwabudu pamoja kumwomba Mungu na walikuwa na wanafunzi wengine wapatao kama mia moja na ishirini kwa pamoja.
MTUME MWINGINE NI LAZIMA ACHAGULIWE (mistari 15 - 22)
Wakiwa wamekusanyika pamoja Petro alisema kuwa ni lazima mtume mwingine achaguliwe ili achukue nafasi ya Yuda Iskariote. Utakumbuka kuwa kwa ajili ya uovu alimsaliti Yesu kwa viongozi wa Kiyahudi na wakamsulibisha Yesu, baada ya Yuda kujua alichofanya alikwenda kujinyonga mwenyewe (Mathayo 27:1). Yesu alikuwa amesema kwamba wakati atakaporudi, Mitume kumi na mbili watakaa katika viti kumi na mbili wakija kuhukumu makabila kumi na mbili ya Israeli, (Mathayo 19:20). Kwa hiyo mtumei mwingine alihitajika kutimiza idadi ya kumi na mbili.
MATIA ANACHAGULIWA
Kutokana na wale waliostahili, wanafunzi wawili walichaguliwa Yusufu aliyeitwa Barsaba na Matias.ulikuwa ni uamuzi muhimu kufanya. Kwa hiyo Mitume kumi na moja walimgeukia Mungu kwa njia ya maombi, walimwomba awasaidie kupata chaguo sahihi, maana Mungu alijua mioyo ya watu ilivyo (mistari 24-25), baada ya kuomba walipiga kura na kura ikamwangukia Matia. Mungu alikuwa amejibu maombi yao, kuanzia wakati huo na kuendelea Matia akahesabiwa pamoja na hao wengine.
FUNDISHO KWETU
Na tuwe kama baadhi ya wanafunzi na tumtazame Bwana Yesu Kristo kurudi akitoka mbinguni. Thawabu ya Mumbu itakuwa kwa ajili watu wote wanaomwamini Mungu. Mungu alikuwa ameahidi ya kwamba wale waomwamini Neno lake na amri zake watapewa uzima milele (Warumi 2:7). Wao wataishi hapa dunia wakiwa wafalme na wanyama milele wakiwa pamoja na Bwana Yesu Kristo.
Na tusiwe kama Yuda mwovu aliyetupilia mbali heshima kubwa sana ya kuwa mmoja wa Mtume.Alichagua kupata sifa za wanadamu badala ya uzima wa milele kayika Ufalme wa Mungu.
MAELEZO YA NYONGEZA SIFA ZA KUWA MTUME (Mstari 20-22)
Petro aliona kutoka katika maandiko ya Agano la Kale kwamba mtu mwingine atachaguliwe badala ya Yuda (Mstari 20 linganisha na Zaburi 69:25, Zaburi 109:8). Katika kuchagua Mtume mwingine ilikuwa ni lazima na muhimu kuwa mtu huyo awe:-
1. Awe ambaye alikuwepo wakati wote wa huduma ya Yesu (mstari 21)
2. Awe alikuwepo tangu Yesu alipobatizwa na Yohana Mbatizaji mpaka wakati wa kufufuka kwa
Kristo (mstari 22)
3. Awe alikuwa shahidi (aliona) wakati Yesu akipokuwepo hai baada ya kufufuka kwake (mstari
22)
Tunaeza kuona ni kwanini huyu atakayechaguliwa ni lazima awe sifa maalum. Alitakiwa kwenda kuwahubiri watu ya kwamba Yesu yule ambaye wayahudi walimsulibisha alifufuka katika wafu. Habari njema kuhusu Ufalme inategemea kufufuka kwa Yesu na tumaini la kurudi kwake.
MASWALI
Majibu Mafupi
1. Ni muda gani Yesu alikuwa na Mitume na wafuasi wengine baada ya kufufuka kwake?
2. Mitume walitumaini kuwa Yesu atafanya nini baada ya kufufuka?
3. Yesu aliwaachia kazi gani Mitume wafanye?
4. Neno 'mtume' lina maana gani?
5. Injili ni nini?
6. Mitume walikwenda wapi baada ya Yesu kupaa mbinguni?
7. Bwana aliwaambia Mitume kungoja nini?
8. Ni nani alichaguliwa kuchukua nafasi ya Yuda Iskariote?
9. Ni thawabu gani ambayo mitume waitapata katika Ufalme?
10. Ni nani mwingine ambaye Mungu atampa thawabu wakati Yesu atakaporudi kutoka
mbinguni?
Majibu ya Kina
11. a) Malaika waliwaambia nini mitume kumi na moja pale katika mlima Mizeituni?
b) Maneno haya yana maana gani kwetu?
12. Eleza jinsi mtume mwingine alivyochaguliwa kushika nafasi ya Yuda Iskariote.
Majibu ya Nyongeza
13. Yesu alizungumza nini na wafuasi wake siku arobaini baada ya ufufuka kwake?
14. Kwanini ilikuwa ni lazima kuchagua mtume mwingine kuchukua nafasi ya Yuda Iskariote?
15. Ni sifa zipi za Mtume?