CSSA 1-5-11 - PAUL AND BARNABAS PREACH THE GOSPEL IN CYPRUS

Swahili

111. PAULO NA BARNABA WANAHUBIRI INJILI KATIKA KIPRO (CYPRUS)

“Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa ajili ya kazi ile niliyowaitia”

 

Shabaha

Kuonyesha jinsi Mungu  alivyowachagua Barnaba na Sauli kwa mara ya kwanza kuihubiri Injili za mbali, wakianzia na Kipro. Ingawa Wayahudi wengi waliiamini Injili na kubatizwa, lakini wengi wao walikuwa ndiyo maadui wa Kweli.Kwa hiyo wanafunzi walisafiri nchi za mbali na wakatanyika kwenda sehemu mbalimbali ulimwenguni na Injili ya Neno la Mungu ikihubiriwa kwa Wayahudi na kwa  watu wa Mataifa.

 

Matendo ya  Mitume 11:19-26; 13:1-13

 

ANTIOKIA (Matendo ya  Mitume 11:19-26)

Upande wa  Kaskazini wa Yudea, katika nchi ya Shamu (Syria) palikuwa na Antiokia, mji ambao ulikuwa mkubwa sana na maarufu. Wanafunzi waliotoka nchi za mbali walikuja katika mji huu na wakahubiri watu wengi katika mji huu na watu wengi sana wakaongoka kwa kuiamini Kweli. Eklesia kubwa ikaanzishwa na ''watu wengi wakaongezeka kwa upande wa Bwana''. Eklesia ya Yerusalemu ikamtuma Barnaba ili awaimarishe na kuwatia moyo waamini wapya ambao wengi wao walikuwa ni watu wa Mataifa. Sauli wakati huo alikuwa amerudi Tarso, mji wa nyumbani kwao, naye Barnaba akasafiri umbali upatao kama km 200 kutoka Antiokia kumtafuta Sauli na kumleta hadi eklesia ya Antiokia. Wakafanya kazi ya kufundisha watu muda wa mwaka mzima (Matendo ya  Mitume 11:24-26). Antiokia (katika Syria au Shamu) ulikuwa ni mji ambao mkuu katika kuhubiri Injili. Licha ya Barnaba na Sauli kuhubiri, lakini walikuwepo wengine pale ambao ni walimu na manabii na wakati sasa ulifika Injili ihubiriwe zaidi kwa watu wa Mataifa (Matendo ya  Mitume 11:24-25). Na ikuwa ni hapa Antiokia ambapo ''wanafunzi waliitwa Wakristo kwa mara ya kwanza'' (Matendo ya  Mitume 11:26) ikiwa na maana ya “wafuasi wa Kristo''. (Lakini soma swali la mkufunzi Namba 5).

 

WITO KWA AJILI YA KUTUMIKA (Matendo ya  Mitume13:1-3)

Siku moja, ndugu hawa walipokuwa pamoja wakimwabudu Mungu, Roho  Mtakatifu akasema, “Nitengeeni  Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia” (mstari 2). Kwa hiyo pamoja na maombi ya ndugu wa Antiokia ye kuwatia moyo, Barnaba na Sauli wakatengwa kwa mara ya kwanza kwa ajili ya safari nyingi na ndefu katika kumtumikia Kristo.

 

WANAKWENDA KISIWA CHA KIPRO (mstari 4-8 )

Walipoondoka Antiokia, wakaenda Seleukia, ambayo ndiyo bandari iliyokuwa karibu sana, wakasafiri na Meli kwenda Kipro ambacho ni kisiwa kikubwa upande wa Mashariki wa bahari ya Mediteraniani. Barnaba alikuwa mzaliwa ni Kipro (Matendo Mitume 4:36) na sasa alitakiwa kupeleka ujumbe wa Injili aliousikia na kuuamini katika nchi yake. Na pia katika safari alimchukua Yohana Marko, mpwa wake ili awasaidie katika kazi hii maalumu. Ikawa meli ilipofika bandari ya Salami, hawa ndugu wakawa wa kwanza kuingia katika sinagogi na wakahubiri pale. Kisha wakatembea kwa miguu mpaka Pafo mji mkuu wa Kipro. Liwali wa Kirumi Sergio Paulo, akataka kusikia Neno la Mungu kutoka kwao. Alikuwa ni mtu mwenye akili sana na alikuwa amevutiwa sna na ujumbe ambao aliusikia ndugu hawa watatu walipokuwa wanahubiri. Lakini alikuwa na Myahudi aliyeitwa Bar Yesu (na alijulikana kwa jina  la Elima, mchawi au mtu afanyaye ushirikina), ambaye alikuwa ni nabii wa uongo. Elima alibishana na Barnaba na Sauli, maana aliweza kuona kuwa Liwali alipenda sana Injili na yeye akataka kumgeuza nia ili asiikubali ile imani na hivyo asiendelee kuisikiliza Injili.

 

ELIMA ANAADHIBIWA (mstari 9-12)

Ikawa Elima alipozidi kulipinga Neno la Kweli, ndipo Sauli, hali akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho,  “Tazama mkono wa Bwana uko juu yako; nawe utakuwa kipofu, usilione jua kwa muda” (mstari 11). Maana alikuwa adui wa haki yote, mpotoshaji, ambaye hakutaka Liwali aipokee Kweli. Na sasa yeye mwenyewe anakuwa kipofu ghafla na anaomba watu wamwongoze kwa kumshika mkono. Mungu alikuwa anamfundisha somo. Naye Liwali akastaajabu sana. Mwujiza huu wa kumpofusha Elima ulisababisha Liwali aamini mambo yale aliyokuwa ameanza kuamini.

 

SASA SAULI ANAITWA PAULO (mstari  9)

Utaona kuwa kuanzia wakati huu, katika maandiko ya Luka aliyoyaandika katika Kitabu cha Matendo ya Mitume, Sauli anaitwa Paulo, ikiwa na maana ya “mdogo”. Anajulikana kuwa ni “Mtume kwa watu wa Mataifa”, kwa sababu kazi yake kubwa ilifanyikia kwa watu wa Mataifa.

 

FUNDISHO KWETU

Tunaona jinsi Barnaba na Paulo walivyofanyakazi, ya kuhubiri ujumbe mzuri sana wa wokovu katika Yesu Kristo. Walijiandaa kusafiri umbali mrefu sana na kwa kupata dhiki nyingi, kwa sababu walitaka kumtumikia Mungu na wakawasaidia wengine kwa kuwafundisha ili wafahamu Kweli ya  Neno la Mungu. Na sisi tufuate mfano wa watu hawa wawili waaminifu, kwanza kwa kusoma Neno la Mungu na njia zake na kisha kwa kuwaambia watu kuhusu njia hii nzuri ya wokovu. Unaweza kukutana na watu kama Elima, ambao siyo kwamba ni vipofu kwa mambo ya Mungu tu bali pia hutaka kuwapofusha watu wengine ili wasiiamini Kweli. Mungu atashughulika nao. Na sisi ni lazima, kama vile  Paulo na Barnaba walivyoendelea kuihubiri Injili.

 

MASWALI

Majibu Mafupi

1.    Ni kwa nini Barnaba alitumwa kwenda Antiokia?

2.    Ni jinsi gani  Sauli na Barnaba walivyochaguliwa ili waibebe Injili kwenda nchi za mbali?

3.    Sauli na Barnaba walimchukua nani?

4.    Ni nani alikuwa Liwali wa Kisiwa cha Kipro?

5.    Ni nani aliyekuwa nabii wa uongo ambaye alijaribu kumpotosha Liwali?

6.    Je, ni jambo gani lililompata nabii wa uongo wa Kipro?

7.    Je, jina la Sauli lilibadilishwa na kuitwa jina gani?

 

Majibu ya  Kina

8.    Eleza habari ya Sauli na Barnaba wakati walipohubiri katika  Kisiwa cha Kipro?

9.    Ni kwa nini Elima aliadhibiwa?

 

Swahili Title
111 PAULO NA BARNABA WANAHUBIRI INJILI KATIKA KIPRO (CYPRUS)
English files
Swahili file
PDF file
Literature type
Sub type
Sub sub type