117. PAULO AKIWA KORINTHO
“Usiogope, bali nena, wala usinyamaze: Kwa kuwa mimi ni pamoja nawe...kwa maana mimi nina watu wengi katika mji huu”
Shabaha
Kuonyesha kwamba Mungu anaweza kuwaita watu kutoka mahali popote kwa ajili ya Injili na ni lazima sisi tuwe tayari ili kuisema Kweli mahali popote tunapokuwa. Baada ya Paulo kuondoka Athene, alisafiri kwenda mji wa Korintho upande wa kusini. Mji wa Korintho ndiyo uliokuwa mji mkuu wa Uyunani eneo la kusini na ilikuwa nchi nyembamba yenye bandari mbili, moja kila upande. Kwa ajili ya bandari hizi, ulikuwa ni mji wenye shughuli nyingi na watu pamoja na wafanyabishara kutokana sehemu mbalimbali za dunia walifika katika masoko ya Korintho. Kama ilivyokuwa miji yenye utajiri, ulikuwa mji wenye ouvu mwingi sana, lakini tunaona jinsi Mungu alivyomwongoza Paulo aende kule ili nuru ya Injili ili iwageuze wengi waache uovu wao na kumtumikia BWANA.
Matendo ya Mitume 18. 1 – 18
PAULO ANAKAA NA AKILA NA PRISILA (mstari 1 - 3)
Wakati Paulo alipofika katika mji huu mkubwa, aliwakuta Wayahudi wenzake wawili Akila na mkewe Prisida. Nao pia kwa muda huo walikuwa wamefika Korintho, kwa maana wao pia walikuwa wamelazimishwa kuondoka Rumi. Mtawala Klaudia alikuwa ametoa amri kwamba Wayahudi wote waondoke katika mji. Akila alikuwa mtengenezaji wa mahema kama Paulo alivyokuwa. Kwa hivyo Paulo aliishi pamoja nao na wakafanya kazi pamoja wawakitengeneza maisha yao kwa biashara hii kule Korintho. Tunafahamu kuwa Paulo aliwahubiri Injili na ndiye hasa kwa ajili ya ujumbe wake kwao Akila na Prisila waliongoka na kuiamini Kweli wakati huo. Paulo mara nyingi huwatamka hawa kuwa ni rafiki waaminifu na kazi ya kubwa waliyoitenda kwa ajili ya Kristo katika nyaraka au barua zake. Anawaita “wasaidizi wangu katika Yesu Kristo” na inaonekana kwamba Akila na Prisila walihatarisha maisha yao kwa ajili ya Paulo. (Warumi 16:3 -4).
PAULO ANAHUBIRI INJILI KATIKA SINAGOGI (mstari 4 – 8)
Kama ilivyokuwa desturi ya Paulo alikwenda kwenye sinagogi katika siku ya sabato ambako alihubiri Injili kwa Wayahudi na watu wa Mataifa walioamini. Baadaye Sila na Timotheo waliwasili wakitokea Makedonia ambako Paulo alikuwa amewaacha nao wakamletea habari njema ya eklesia ya kule. Hili lilimtia moyo Paulo na aliweza kwenda kuhubiri akiwa na nguvu mpya akiwaonyesha Wayahudi Maandiko ya kwamba Yesu alikuwa ndiye Kristo (mstari 5). Kama ilivyotokea mara kwa mara, Wayahudi wengi ambao hawakuweza kupata majibu kutokana na maneno ya Paulo walianza kukaidi na kumtukrna. Hayo yalimfanya Paulo kukasirika naye akawakung’atia nguo zake na kusema “damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu, mimi ni msafi! Nami kuanzia sasa nitawaendea mataifa” (mstari 6). Hapo karibu na sinagogi mtu aliyeitwa Yusto aliishi hapo. Yeye alimwabudu Mungu, naye akamwalika Paulo kwenda nyumbani mwake na kuendelea na kazi ya kuhuburi. Kati ya wale waliomsikiliza alikuwamo Krispo, kiongozi mkuu wa sinagogi yeye pamoja na nyumba yake yote waliamini. Wakorintho wengi ambao hawakuruhusiwa kuhudhuria katika sinagogi waliweza kumsikiliza Paulo katika nyumba ya Yusto. Katika mji huu wa uovu, watu hawa walifurahia kusikia njia ya wokovu. Wakaamini na kubatizwa
BWANA ANANENA NA PAULO KATIKA MAONO (mstari 9 - 11)
Akielewa jinsi Wayahudi walivyokuwa na hasira, Paulo aliogopa sana kwa mara nyingine tena kuwa ndugu watateswa kwa ajili ya kweli, na kwamba kuihubiri Injili kungezuiliwa. Hata hivyo, usiku mmoja Bwana alimtokea katika maono akamwambia: “Usiogope, bali nena, wala usinyamaze, kwa kuwa mimi ni pamoja nawe, wala hakuna mtu atakayekushambulia ili kukudhuru; kwa maana mimi nina watu wengi katika mji huu” (mstari 9 -10). Kwa maneno haya ya kutia moyo, Paulo aliendelea kulihubiri Neno la Mungu bila hofu. Sasa alifahamu kwamba Mungu alikuwa na kazi kubwa ya kufanywa na yeye katika mji huu na kwamba Mungu atamlinda na kuibariki kazi yake. Kwa hiyo aliendelea na kazi yake huko Korintho kwa muda wa mwaka mmoja na miezi sita.
MATATIZO KATIKA KORINTHO (mstari 12 – 18)
Paulo alifundisha Injili kwa bidii sana, nayo chuki ya Wayahudi ikaongezaka mno. Hatimaye hawakuweza tena kuizuia hasira yao na wivu wao. Wakamkamata Paulo na kumpeleka mbele ya kiti cha hukumu cha Galio, aliyekuwa mtawala wa Rumi katika Korintho. Wakamshitaki kwa kusema kuwa mtu huyu huwavuta watu ili wamwabudu Mungu kinyume cha sheria ya Musa, lakini Galio hakuliona kuwa ni jambo la mhimu kwa kuwa lilihusu mabishano ya dini, naye akawafukuza kutoka mbele ya kiti chake cha hukumu. Ndipo Wayunani waliokuwa ni wakazi wa Korintho wakaamua kuwasaidia kwa kuwapatia Wayahudi mbinu. Wakamchukua Sosthene aliyekuwa mkuu wa sinagogi, wakampiga mbele ya kiti cha hukumu cha Galio. Na Galio hakujali kwa kuwa yeye alifahamu kuwa kesi iliyokuwa mbele yake ilikuwa imekwisha Tunaona kuwa ingawaje Paulo alikuwa amekamatwa, lakini Mungu alimlinda kama Mungu alivyokuwa amemwahidi ya kuwa atamwokoa kwa kumtoa katika mikono ya Wayahudi wanaomchukia. Baada ya tukio hili Paulo aliendelea kuhubiria kwa muda kiasi huko Korintho kabla ya kuaondoka pamoja na Akila na Prisila kwenda Efeso. Hatimaye, Paulo aliwaandikia nyaraka waumini wa Korintho akiwatia moyo waendele katika mafundisho ambayo alifuwafundisha (1 Wakorintho na 2 Wakorintho).
FUNDISHO KWETU
Mara hii tena tunatiwa nguvu kwa namna Paulo alivyoweza kufanya kazi bila kuchoka, ya kuhubiri habari ya wokovu katika Korintho. Hata sisi pia tunatakiwa kufanya kazi kwa bidii katika kumtumikia Mungu naye atatulinda kama Mungu alivyomlinda Paulo. Angalia jinsi Paulo anavyoonekana kupata nguvu za kufanya kazi wakati Sila na Timotheo walipofika kumsaidia. Sisi nasi inatupasa kuelewa kwamba tunaweza kuwatia moyo wengine na wao pia wakatutia moyo kutenda mapenzi ya Mungu. Tujaribu kila wakati kuwa na urafiki wa karibu na watu wale wanaolipenda Neno la Mungu.
MASWALI
Majibu Mafupi
- Paulo alipofika kwa mara ya kwanza huko Korintho alikaa na rafiki zake Wayahudi wawili. Walikuwa akina nani hao?
- Ni kwa nini watu hawa wawili walikuja Korintho?
- Paulo alifuata biashara gani?
- Apulo alikwenda kuhubiri wapi baada ya kutoka ndani ya sinagogi la Korintho?
- Ni Myahudi yupi maarufu aliyekubali kuongoka kwa kuipokea Kweli katika Korintho?
- Ni kwa jinsi gani Mungu alimtia moyo Paulo kuendela kuhubiri katika mji wa Korintho?
- Wayahudi wenye wivu walijaribu kufanya nini ili kumzuia Paulo kuhubiri walipomkamata huko Korintho?
- Walimtuhumu Paulo kwa shitaka lipi?
Majibu ya Kina
- Mungu alikuwa na kazi kubwa sana kwa ajili ya Paulo huko Korintho
- Eleza yote unayoyajua kuhusu mahubiri yake kule.
- Ni kwa namna gani Mungu alimtia moyo Paulo ili kuendelea katika kazi
- a) Eleza jinsi Wayahudi walivyochochea vurugu na kumsumbua Paulo huko Korintho.
b) Ni kwa jinsi gani Wayahudi walivyoshauri ili kuweza kufanya ghasia ile?