118. KWELI INAFIKA EFESO
“Siyo miungu, waliotengenezwa kwa mikono”
Shabaha
Kuonyesha uweza wa nguvu ya mafundisho ya Paulo kule Efeso na jinsi fujo zilivyoanzishwa na watu wa Mataifa ambao walihofia kupoteza chanzo chao cha utajiri. Paulo aliwasili Efeso akiwa pamoja na Akila na Prisila na ingawaje Wayahudi kule walikuwa tayari kusikiliza, naye Paulo alikuwa na shauku ya kurudi tena Yerusalemu, kabla ya kuanza safari nyingine ndefu. Kwa hiyo Paulo aliwaacha Prisila na Akila pamoja na Waefeso ili waendelee na kazi ya kuhubiri Injili.
Matendo ya Mitume 19
PAULO ANARUDI EFESO (Mstari 1 - 10)
Ilikuwa ni katika safari ya Paulo ya tatu na ambayo ilikuwa ndefu kuliko zote ya kuhubiri, ambapo mwishowe alikwenda kuishi Efeso, ambayo ilikuwa ni bandari inayoendelea iliyokuwa ufukwe wa bahari ya mwa bahari ya Aegeani. Efeso ulikuwa ni mji wenye utajiri na watu wake walipenda anasa sana, na kiburi chao kilijikita kwenye Hekalu zuri sana la Diana, ambalo kwa wakati huo lililoelezwa kuwa “Ajabu ya Kwanza” ya ulimwengu wa kale. Katika miji huu, ulijulikana sana kwa kutenda dhambi na kwa ibada ya sanamu, ilionekana kuwa Kweli haitaweza kuendelea pale. Lakini kwa msaada wa Mungu na juhudi zisizochoka za Paulo, pamoja na Akila na Prisila kazi ya kueneza Injili ilibarikiwa. Paulo alizungumza na Wayahudi katika Sinagogi lao kwa miezi mitatu, lakini wale waliofanya mioyo yao kuwa migumu waliitukana Injili na waliwaambia watu wote katika mkutano. Kwa hiyo Paulo alifikiri kuwa ni busara kuwatenganisha wale walioamini na kuwafundishia sehemu nyingine. Akakodisha chumba cha kufundishia cha mtu mmoja aliyeitwa Tirano na akendelea pale kwa muda wa miaka miwili. “Hata wote waliokaa Asia wakalisikia neno la Bwana Yesu, Wayahudi kwa Wayunani” (mstari 10).
NGUVU YA INJILI (mstari 11 - 12)
Paulo alikuwa na nguvu za Roho Mtakatifu kwa ajli ya kufanya miujiza ya kupita kawaida, kuthibitisha kwamba yale aliyokuwa akifundisha ilikuwa ndiyo neno la Mungu la kweli. Hata ikawa “leso na nguo” zilizougusa mwili wa Paulo vilitumika kuwaponya watu mgonjwa (mstari 12). Baadhi ya Wayahudi walidhani wangeweza kuiga miujiza hii kwa sababu kutumia jina la Yesu Kristo tu.Wana saba wa Kuhani Mkuu walidhani wangeponya watu kwa njia hii. Siku moja walipojaribu uponyaji huu kwa mtu aliyekuwa mgonjwa wa akili aliwarukia, akawashambulia na kuwajeruhi hata wakakimbia hali wakiwa uchi. Kila mtu huko Efeso alisikia habari hii ya kushangaza na hao watu waliofanya hivyo wakawa wameaibika. Wakaona kwamba Jina la Yesu lilikuwa ni la kutii na kuheshimiwa. Hivyo Mungu aliwafundisha somo na hata watu wengi wa Waefeso pia walianza kuona namna wale watu walivyokosea na jinsi ilivyowapasa kubadili njia zao. Walielewa kwamba ibada ya kipangani kwa mungu mke Diana ilikuwa ni ya makosa na kwamba matendo ya makuhani na makuhani wanawake yalikuwa ni uovu. Watu hawa wakaamua kukusanya vitabu vyao vyote vya uchawi na kuvichoma haradharani. Uliwaka moto mkubwa sana na wakafanya hesabu ya thamani ya vitabu vilivyochomwa, wakaona ya kwamba yapata thamani ya vipande vya fedha 50,000 huo ulikuwa ni utajiri mkubwa sana katika miaka hiyo! “Hivyo ndivyo Neno la Bwana lilivyozidi na kushinda kwa nguvu” (mstari 20).
MJI UKAJAA GHASIA (mstari 23 - 34)
Masonara wa vyombo vya fedha katika Efeso walikasirika sana walipowaona watu wengi wakiacha kuabudu Diana, mungu mke. Hawa watu wasingevinunua tena sanamu zao! Hivyo wangepoteza wateja wao wote. Mmoja wao Demetrio aliwaita watu ambao walikuwa masonara waliokuwafua fedha na kusema “Enyi wanaume, mnajua kwamba utajiri wetu hutoka katika kazi hii” akalalamika kwamba Paulo alikuwa amewashawishi watu kwamba sanamu zilizotengenezwa kwa mikono siyo miungu hata kidogo. Mpaka hapo Paulo atakapokuwa amezuiliwa kabisa vinginevyo biashara yao ingepotea kabisa na hata hekalu la mungu wao mke, Diana lingedharauliwa na kuhesebika si kitu. Ndipo hao watu wafua vyombo vya fedha wakajazwa na ghadhabu na kupiga kelele, wakisema “Diana wa Waefeso ni mkuu” (mstari 28). Kelele za hasira za masonara wafua vyombo vya fedha zikaenea mjini haraka sana na kukawa na ghasia mji mzima. Wakaenda mbio hadi wakaingia mahali pa michezo huku wakiwakamata Gayo na Aristarko waliosafiri pamoja na Paulo. Pakawa na ghasia na machafuko makubwa kabisa, kwani baadhi yao walipiga kilele wakisema hivi, na kundi lingine walipiga kelele wakisema hivi. Kwa kweli, watu wengi sana katika kusanyiko lile hawakuijua sababu yakukusanyika kwao pamoja. Paulo alipofahamu kwamba Gayo na Aristarko kuwa maisha yao yalikuwa hatarini, alitaka kuingi bila hofu yoyote katikati ya kundi lile, lakini wanafunzi wa Efeso wakamwomba kwa kumsihi asijihusishe na kundi lile. Myahudi mmoja alitaka kusema na kusanyiko lile labda kuwaeleza kwamba hawakuwa na uhusiano wowote na wanafunzi. Hata hivyo, lile kusanyiko walipojua kuwa yule alikuwa ni Myahaudi, walianza kupiga kelele na kutamka tena “Diana wa Waefeso ndiye mkuu” Hili liliendelea kwa muda wa kama saa mbili.
KARANI WA MJI ANAWATULIZA WATU (mstari 35 – 41)
Hatimaye, Karani wa mji aliwatuliza watu na kuwaambia kuwa walikuwa wapumbavu sana. Aliwaeleza kwamba ilikuwa ikijulikana duniani kote kwamba watu wa Efeso walikuwa wakimwabudu Diana. Haikupo sababu yoyote ya wao kuanzisha ghasia katika mji. Akawaambia kuwa, Paulo na wafuasi wake hawakufanya uvunjaji wa sheria yoyote ile-kwa maana hawa “hawakuiba vitu vya hekalu na wala kumtukana mungu mke wetu” (mstari 37). Alielewa kuwa kwa ghasia zao wangepata matatizo makubwa kutoka kwa watawala wa Kirumi na kwahiyo akawatawanya. Baada ya machafuko hayo, Paulo aliwakusanya wanafunzi, akawakumbatia na kuendelea na safari yake.
FUNDISHO KWETU
Jinsi ilivyokuwa tofauti kati ya ndugu za Bwana Yesu Kristo na wale waabudu wa ibada ya kipagani ya mungu mke, Diana. Ndugu walikuwa tayari kuchoma hadharani vitabu vya uchawi na kugeuka kutoka katika ibada ya sanamu na kumcha Mungu mmoja wa kweli. Watengenezaji wa sanamu walipendelea utajiri wao kuliko kumwabudu mungu mke. Fedha - ndiyo ilikuwa mungu wao. Na hivi, ndivyo ilivyo kwa watu wengi sana siku hizi. Tusipende vitu vya dunia hii ambayo inapita, bali tuopende Kweli, maana Kweli inadumu milele. Paulo alimwandikia Timotheo, “Shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha” (1 Timotheo. 6: 6 -10), walakini “utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa”. Kama vile Paulo, na sisi inatubidi bila ya hofu yoyote tuweze kusimama kwa ajili ya Kristo na kuwasaidia wengine kujifunza utajiri wa kweli wa injili ya wokovu.
Maswali
Majibu Mafupi
- Waefeso walikuwa watu wa aina gani?
- Watu katika Efeso waliobudu nini?
- Paulo alihubiri wapi katika Efeso alipondoka kwenye Sinagogi?
- Paulo alihubiri pale kwa muda gani?
- Ni miujiza gani ya kipekee ambayo Mungu aliifanya kupitia Paulo?
- Baadhi ya Wayahudi walifanya nini walipoiona miujiza aliyoifanya Paulo katika Efeso?
- Watu walifanya nini na vitabu vyao vya uchawi walipomwamini Paulo?
- Kwa nini Demetrio alikasirika?
- Watu wote walipiga kelele wakisemaje?
Majibu ya Kina
- Baadhi ya watu walijaribu kuiga miujiza aliyoifanya Paulo.
- Eleza mambo yaliyowatokea
- Watu wengi walifanyaje waliposikia kuhusu jambo hili?
- Demetrio aliitisha mkuatano wa watu waliokuwa masonara wa vyombo vya fedha
- Alisema nini?
- Eleza nini kilitokea baada ya mkutano huo