CSSA 1-5-21 - A CAPTIVE IN CAESAREA

Swahili

121. MFUNGWA KATIKA KAISARIA

“Mtu huyu hana tuhuma juu yake, inayostahili kifo au kifungo”

 

Shabaha

Kuonyehsa jinsi Paulo alivyokamatwa huko Yerusalemu na Karisaria na jinsi Mungu alivyomlinda wakati Wayahudi walipotaka kumwua. Kitendo cha askari wa Kirumi kumkata Paulo i kuliokoa uhai wake. Wayahudi walikuwa wamepiga kelele “mwondoe huyu” lakini kile alichotaka Paulo alitaka aseme nao, ili kugeuza mioyo yao imwelekee Mungu kwa kuwafundisha habari njema kwamba Yesu alikuwa ndiye Masihi wao. Walitaka kumwua, lakini yeye alitaka kuwaokoa. Paulo alimwomba Lisia mkuu wa Warumi kama angemruhusu ili kusema na watu akiwa kwenye usalama wa ngome ya Antonia. Lisia alikuwa amewazia kuwa Paulo alikuwa mhuni, lakini alishangaa kwamba aliweza kuzungumza lugha ya Kiyunani na kwamba alikuwa mwenyeji wa Tarso. Hivyo akatoa idhini yake naye Paulo akasimama kwenye ngazi za ngome akawapungia mkono wake kunyamazisha watu, akasema na Wayahudi katika lugha ya Kiebrania.

 

Matendo ya Mitume 22,23,24

 

PAULO ANAZUNGUMZA NA WATU (Matendo ya Mitume 22:1-22)

Walipokuwa wakimsikiliza, Paulo kwanza alianza kusimulia historia yake. Alikuwa Myahudi, aliyelelewa kwa uangalifu sana kwa kufuata sheria ya mababa wa zamani chini ya miguu ya Gamalieli, alikuwa ameelimishwa katika dini ya Kiyahudi. Alikuwa na amewatesa kwa juhudi wafuasi wote wa Yesu wa Nazareti, lakini yeye mwenyewe akaamini alipokuwa safarini kwenda Dameski, na akabatizwa. Yesu mwenyewe, aliyekuwa amefufuka kutoka kwa wafu, akasema naye kuwa: “nitakutuma uende mbali kwa watu wa Mataifa” (mstari 21). Hayo yalitosha kwa wayahudi wote waliokuwa wamesimama katika kundi lile Kule tu kutaja “watu wa Mataifa” kuliwachukiza mno. Wakatupa mavazi yao na kurusha-rusha mavumbi juu na kupiga kelele “mwondoe mtu huyu katika nchi, kwa maana hafai aishi” (mstari 22).

 

PAULO MBELE YA BARAZA LA SANHEDRINI (Matendo ya Mitume 22: 23 -30, 23: 1- 10)

Kuona lile kundi likiwa tayari kufanya vurugu tena yule mkuu wa Warumi akaamua kumpeleka Paulo ndani na kumwuliza maswali. Safari hii ilimpasa kupigwa,au apigwe kwa mijeledi ya Kirumia. Na wakati walipomfunga kwa mikatale, Paulo alisema, “Je ni halali kumpiga mtu aliye Mrumi?” Wakati Jemadari yule alipofahamu kuwa Paulo ni raia wa Kirumi aliacha mara moja, kwani kwa kumpiga Paulo angeyahatarisha maisha yake. Lisia alishangaa. Ni kwa nini Wayahudi walimchukia mtu huyu? Hivyo akaamua kumpleka Paulo mbele ya Sanhedrini, ambalo ndilo Baraza Kuu la Wayahudi, ili kujua alikuwa amefanya nini hata kusababisha hasira zao. Ni lazima ilikuwapo sababu iliyowafanya wamechukia jinsi ile. Paulo aliposimama mbele ya Sanhedrini, akatambua kwamba walikuwepo Mafarisayo ambao wanaamini kuwa ufufuo upo na wengine walikuwa Masadukayo wasioamini kuwa kuna ufufuo. Hivyo Paulo akasema; “mimi ninahukumiwa kwa ajili ya tumaini la ufufuo wa wafu” (mstari 6). Mara moja hili lilisababisha wagawanyike katika makundi mawili na hapa tena yule askari mkuu wa Rumi akaja kumwokoa Paulo, kwani alidhani Paulo angeraruliwa na Wayahudi wenye hasira.

 

UJUMBE WENYE FARAJA (mstari 11)

Bwana Yesu Kristo aliyajua matatizo yote ya Paulo. Maana alikuwa ametendewa hivyo hivyo na ndugu zake, Wayahudi. Kwa hiyo usiku uliofuata Bwana akasimama karibu na Paulo kumwimarisha “Paulo, uwe na moyo mkuu, kwa sababu, kama ulivyonishuhudia habari zangu Yerusalemu, imekupasa kunishuhudia vivyo hivyo Rumi nako”.

 

MPANGO WA KUMWUA (mstari 12-22)

Wayahudi walimchukia Paulo vibaya mno hata ikawa kwamba walikuwa tayari kwenda umbali wowote ili kumwua. Watu arobaini waliapa kutokula wala kunywa mpaka watakapokuwa wamemwua Paulo. Wakapanga njama wakishirikiana na makuhani wakuu na wakuu na kuamua kumwomba mkuu wa ngome ya Warumi kumleta Paulo tena kwenye Sanhedrin wakijifanya kwamba walihitaji kumwuliza maswali zaidi. Walipanga kumvlizia Paulo alipokuwa njiani ilia kumwua. Kwa bahati njema mpwa wa Paulo alisikia njama hiyo, akamwambia Paulo, na kisha kumweleza Mkuu wa Warumi. Lisia aliamua kumhamisha Paulo usiku ule kwenda Kaisaria chini ya ulinzi mkali.

 

ALIKWENDA KAISARIA NA KIFUNGO (mstari 23-35)

Mipango iliandaliwa na kundi kubwa la askari lilimsindikiza Paulo kwenda Kaisari – askari 200. walikuwemo wapanda farasi 70 na washika mikuki 200 wakawa tayari kuondoka Yerusalemu saa tatu usiku ule. Walikuwa wampeleke Paulo kwenye ikulu ya mtawala (Gavana) wa Kaisaria, lakini ilikuwa ni muhimu kula kwanza pale Antipatri usiku. Na siku iliyofuata waliendelea na safari mpaka kaisalia.  Lisia alikuwa ameandika barua ya ufafanuzi kwa Gavana Feliki, kuhusu mfungwa wake mpya. Alifahamu kwamba Paulo alichukiwa na Wayahudi, lakini akamwambia Feliki alichoelewa “na wala hakushitakiwa kwa neno lolote la kustahili kufa wala kufungwa” (mstari 29). Kwahiyo aliwaambia Wayahudi kwenda Kaisaria kutoa tuhuma zao kwa Feliki.

 

PAULO ANAPELEKWA MBELE YA FELIKI NA FESTO (Matendo ya Mitume 24:22-27)

Ingawaje Paulo alikuwa mfungwa lakini Mungu alikuwa pamoja naye. Feliki alitoa amri kwamba rafiki yoyote wa Paulo aliyetaka angeweza kumtembelea. Ni jinsi gani mtume alivyoshukuru katika kipindi hiki cha miaka miwili aliyokuwa mfungwa. katika Kaisaria kulikuwa na mabadiliko ya Magavana mwisho wa kipindi kile, Lakini Feliki, akitaka kuwapendeza Wayahudi alimwacha gerezani. Gavana mpya, Festo, pia alisikia shauri la Paulo na akataka kumrudisha Yeusalemu, lakin Paulo akajibu, “Ninataka rufani kwa Kaisari” (Matendo ya Mitume 25:11). Lakini ukumbuke kuwa Bwana alikuwa ameshasema kwamba Paulo ilimpasa “alichukue Jina langu mbele ya Mataifa na wafalme na wana wa Waisraeli” (Matendo ya Mitume 9:15). Waweza kuona namana yote yalivyowa yanatimia? Kaisari alikuwa ndiye mtawala mkuu, au mfalme, naye alitawala huko Rumi. Ukumbuke kwamba Mungu alikuwa amemwambia Paulo, “imekupasa kunishuhudia vivyo hivyo Rumi nako” (Matendo ya Mitume 23:11).

 

FUNDISHO KWETU

Tusisahau kamwe kwamba Mungu anapenda kujishughulisha na watu wake. “Malaika wa BWANA hufanya kituo, akiwazungukia wamchao na kuwaokoa” (Zaburi 34:7). Mungu almwokoa Paulo kutokana na kifo katika matukio mengi sana na kumtunza wakati alipokuwa mfungwa kwa kuwa kazi yake ya kuhubiri Injili ilikuwa bado haijamalizika. Mungu alitaka aende Rumi pia kuhubiri kule.  Ukumbuke daima kwamba kazi ya watu waovu haiwezi kubadilisha mipango ya Mungu. Kwa hiyo tunatakiwa kumwamini Mungu kila wakati.

 

MASWALI

Majibu Mafupi

1.    Paulo aliposema akiwa kwenye ngazi, ni neno gani moja lililowakasirisha Wayahudi?

2.    Jemadari aliamua kufanya nini Paulo?

3.    Nini kilimfanya abadili mawazo yake?

4.    Malaika alimwambia nini Paulo gerezani katika ngome ya Antonia?

5.    Ni nini baadhi ya Wayahudi walisema hawangefanya hadi wamwue Paulo?

6.    Ni nani aliyesikia mpango wa njama zao?

7.    Jemadari aliamua kufanya nini aliposikia kuhusu mpango wa Wayahudi?

8.    Je, Jemadari alifikiria kwamba Paulo alistahili kuwa mfungwa?

9.    Ni kwa muda gani Paulo alikuwa gerezani Kaisaria?

10. Festo alipotaka kumrejesha Paulo huko Yerusalemu, Paulo alisemaje?

 

Majibu ya Kina

11.  (a) Eleza ni kiapo gani Wayahudi arobaini wa Yerusalemu waliweka?

      (b) Jemadari wa kikosi cha Rumi alifanya nini alipogundua hayo? Eleza habari yote?

 

 

 

 

Swahili Title
121 MFUNGWA KATIKA KAISARIA
English files
Swahili file
PDF file
Literature type
Sub type
Sub sub type