126 - MUNGU NDIYE MWANDISHI WA BIBLIA
Kama tukiiangalia dunia katika maajabu yake kwa kina au tukitazama anga, tunaona kazi ya Mungu ambaye ndiye Muumbaji. Lakini huo ni ushahidi uliodhahili ulionyamaza kimya. Hata hivyo Mungu aliwawezesha Manabii wake na Mitume kuweka kumbukumbu ya kusudi la Mungu. Ndani ya Biblia zetu tunasoma kuhusu kusudi lake hili na ujumbe wa tumaini la ajabu.Mungu alikuwa ameshasema kwamba atamtuma Bwana Yesu Kristo kuirejesha tena dunia kwenye hali ya amani na ushirika wa pamoja ambao hapo mwanzo liwahi kuwepo wakati wa Uumbaji. Ujumbe huu, ambao umeandikwa sehemu nyingi katika Biblia, imeandikwa kwa faida yetu sisi binafsi, ili tuweze kuiamini na kutii maagizo yake. Tunayo kila sababu njema ya kuamini kweli ya Biblia, kwa kuwa Mungu ndiye mwandishi wake.
2Timotheo 3:14-17; 2Petro 1:19-21
BIBLIA NI NENO LA MUNGU
Neno “Biblia” linatokana na neno linalomaanisha “kitabu” na “Biblia Takatifu” inamaanisha “kitabu cha pekee” (au kitabu kilichotengwa). Kweli Biblia ndicho kitabu ambacho ni muhimu kuliko vyote, na ni cha pekee na ni tofauti kuliko vitabu vingine vyote, kwa sababu ni Neno lake Mungu. Kwa kweli ni makitaba ya vitabu 66 (vitabu 39 ni vya Agano la Kale na vitabu 27 ni vya Agano Jipya) vilivyoandikwa na waandishi zaidi ya 40 kutoka katika nchi mbalimbali, katika kipindi kipatacho miaka 1600. Waandishi hawa hawakupata nafasi ili kulinganisha maandiko yao yaweze kufanana, lakini pamoja na waandishi hawa kutoishi sehemu mmoja na kwa wakati mmoja, maandiko haya, yana ujumbe mmoja mkuu wa tumaini, kwa sababu Mungu ndiye Mwandishi.
Ni jinsi gani tunavyoweza kuelezea tendo hili? Ingawaje watu ambao ni tofauti ndio waliadika, hawakuandika kwa kufuyafuata mawazo yao wenyewe; lakini waliandika 'wakiongozwa na Roho Mtakatifu' (2 Petro1:21,Waebrania 1:1). Hii ndiyo maana yake hasa ya kunuu: ''Kila andiko lina pumuzi ya Mungu'' (2 Timotheo 3:16). Kwa hiyo Biblia ni Neno la Mungu,na yote imeandikwa kwa pumzi ya Mungu. Ndiyo sehemu peke yake tu ambapo tunaweza kujifunza ukweli kuhusu Mungu na kusudi la Mungu kwa wanadamu.
Tunaamini kwamba Biblia ni Neno la Mungu. Na Biblia yenyewe inajishuhudia katika sehemu mamia ya vifungu vingi ambamo tunasoma matamshi kama: “Mungu alisema” “BWANA alisema”, na “Neno la BWANA lilimjia…” Hili pia linathibitishwa na umoja wa mafundisho yake kutoka kitabu cha Mwanzo mpaka Ufunuo. Ingawaje ni watu wengi walioandika Biblia, na mazingira yao ya kuishi yalikuwa tofauti, lakini kazi yao kwa jumla imeunganisha kwa ukamilifu ujumbe wote Biblia inao ujumbe mmoja ambao kamwe haujipingi wenyewe. Usahihi wake pia umethibitishwa katika historia yote na unabii mwingi ambao umetimizwa.
HISTORIA
Historia ya zamani za kale zilizoandikwa katika Biblia hata mara moja hazijaonekana kuwa na makosa. Kwa hakika, hivi karibuni wataalamu wa mambo ya kale wamegundua ushahidi unaoonyesha kwamba watu na sehemu ambazo hapo mwanzo nje ya Biblia hazikujulikana, lakini hakika zilikuwepo zamani. Wataalamu wa mambo ya kale waliwadhihirishia baadhi ya wapinzani wakubwa wa Biblia wa karne ya 19 kuwa ni waongo.
Biblia siyo tu ina kumbukumbu ya jinsi Mungu alivyoshughulika katika mambo ya wanadamu zamani za kale, ila pia huelekeza mambo yatakayotokea siku za mbele, kuthibitisha kuwa Biblia ni kazi ambayo mwandishi ni Mungu mwenyewe. Watu wanaweza kuandika kuhusu matukio ya zamani, lakini Mungu peke yake ndiye ajuaye mambo ya siku zijazo. Ndani ya Biblia ameyasema mapema baadhi ya mambo ambayo yangekuja kutokea, mengi ya mambo hayo tayari yamekwishatimia. Mungu alitamka katika Isaya 46:9-10 “Maana Mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; mimi ni Mungu wala hapana aliye kama mimi; nitangazaye mwisho tangu mwanzo na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado”. Pia katika Amosi 3:7-8 “Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lolote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake…Bwana MUNGU amenena,ni nani awezaye neno ila kutabiri?”
UNABII
Mungu amefunua kusudi lake kwa manabii wake na watumishi wake kwa umakini wa ajabu kwa kina, ambapo kumbukumbu yake ni hakika kuwa ni ya Mungu. Bila msaada wa Mungu hakuna mtu ambaye angaliweza kuleta ujumbe wa aina hiyo, ambao uliandikwa zamani za kal , na bado tunashudia mambo hayo yakitimizwa katika siku hizi. Kwa uthibitisho huu wa kinabii uliotimia tunaweza kungojea kwa uhakika mkuu, unabii ambao bado haujtimia huko mbeleni. Uhakika wetu unategemea katika unabii wa zamani uliopita ambao umetimia kwa kadiri ulivyoandikwa, mfano:-
-
Babeli bado ungali ni magofu (Isaya 13:19-21; Yeremia 51:37) Ninawi bado iko katika utupu,ukiwa na uharibifu (Nahumu 2:10)
-
Misri ni kati ya mataifa duni kabisa (Ezekieli 29:15)
-
Tiro imemezwa na bahari nayo imefanyika mahali halisi kabisa pa kutandazia nyavu (Ezekieli 26:5)
-
Israeli walikuwa wametawanywa katika mataifa yote (Kumbukumbu la Torati 28:64) na sasa wameanza kukusanyika na kurudi tena (Yeremia 30:11; 27:21-22)
-
Taifa la kaskazini linaloichukia Israeli (ambalo ni Urusi) limejitokeza (Ezekeli 28:2-7; 15-16).
MUNGU ALIVYOJIDHIHIRISHA KATIKA BIBLIA
Tukifahamu kwamba Biblia ni Neno lenye pumuzi ya Mungu lililovuviwa, ni muhimu kufahamu kwamba Maandiko Matakatifu yanadhihirisha kuhusu Mungu. Kama tunahitaji uzima wa milele inatupasa kumjua Mungu mmoja wa kweli na wa pekee (Yohana 17:3) na kumwabudu Mungu katika roho na kweli (Yohana 4:23).
Mungu ni Mmoja: Hapo mwanzo, watu walifahamu kuwa yupo Mungu mmoja tu. Na kwa kadri muda ulivyokuwa ukiendelea walianza kuabudu vitu vingine, kama jua, mwezi, na nyota, ambavyo viliumbwa na Mungu mwenyewe. Na kisha wakaunda sanamu za dhahabu, fedha, miti na mawe, na wakaviabudu; lakini amri yake kwa watu wa Mungu ilikuwa, “Sikia,Ee Israeli, BWANA, Mungu wetu,BWANA ndiye mmoja” (Kumbukumbu la Torati 6:4). Mungu asema hivi, “Mimi ni BWANA; … wala hapana Mungu zaidi ya mimi” (Isaya 45:18,21)
Kuna watu leo wanaodai kuwa wanamwamini Mungu mmoja, lakini wanahubiri kwamba ana Nafsi Tatu- ''Watatu katika mmoja na mmoja katika watatu”, inayofanya mpangilio awepo Baba, Mwana na Roho Mtakatifu; na kuwa wote wakiwa sawa wakati wote na kuwa wana nguvu sawa . Lakini hili ni kosa kwani tumeona namna Mungu alivyojitangaza mwenyewe kuwa ni Mmoja alipojifunua kwa Israeli. Hili vilevile limeonekana katika Agano la Jipya. Tazama lilitokea katika Marko 12:28-34 ambapo Yesu alinukuu Kumbukumbu la Torati 6:4 na kumwambia yule mwandishi aliyefahamu hili, “Wewe hu mbali na Ufalme wa Mungu”.Ufafanuzi kuhusu umoja wa Mungu unaweza kuonekana katika Galatia 3:20; Efeso 4:5-6; 1 Timotheo 1:17 6:15-16
Yesu Kristo, Mwana wa Mungu:Yesu ni Mwana wa Mungu, alizaliwa kwa njia ya nguvu za Roho Mtakatifu, aliyemjilia Mariamu mama yake. Aliyeambiwa, “kwa sababu hiyo hicho kitachozaliwa,kitaitwa Mwana wa Mungu” (Luka 1:35).Wakati Yesu alipobatizwa, Mungu alisema,“Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye”. (Mathayo 3:17)
Yesu mwenyewe alikataa kwamba hakuwa sawa na Baba yake. Alisema, “Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; ….kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi, bali mapenzi ya Baba aliyenituma” (Yohana 5:30; 14:28). Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu,na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu (Waefeso 1:3; 1Wakoritho 8:6; 1 Timotheo 2:5)
Roho Mtakatifu: Roho Mtakatifu siyo nafsi ya tatu ya utatu. Roho yake Mungu ni nguvu isiyoonekana ambayo kwa hiyo Mungu aliumba vitu vyote na ambayo kwa hiyo nguvu viumbe wakawa hai (Zaburi 104:30). Wakati nguvu ya Mungu inapotumika kutenga au kwa ajili ya makusudi maalumu, kama vile matendo ya miujiza,inaitwa ''Roho Mtakatifu''. “Takatifu” ina maanisha “kilichotengwa” au “kilichowekwa kando”. Yesu Kristo alipokea nguvu hii ya Roho Mtakatifu alipobatizwa (Matendo ya Mitume 10:38). Tafadhali rejea kwenye “Kitabu cha Mwongozo”, masomo Namba. 16-19.
TABIA YA MUNGU : (Kutoka 34:6-7)
Kuna pande mbili za tabia za Mungu: haki na rehema. Alimjulisha tabia hii Musa katika Kitabu cha Kutoka 34:6-7 na Kumbukumbu la Torati 5:9-10. Mungu ni mwema, mwenye upendo na mwenye kusamehe, lakini Mungu anasisitiza kwamba wanadamu wamwangalie yeye na kutii amri zake (Zaburi 103:8-18).
Mungu ni mwenye rehema na neema kwa wale wanao mwendea Mungu kwa njia aliyojiwekea katika Neno lake. Leo hii mtu anapokelewa na Mungu kwa njia ya imani na ubatizo kupitia Mwanaye, Yesu Kristo. Lakini iwapo watu wanaendelea kufanya dhambi wala hawatubu Mungu atawaadhibu, kwa sababu yeye ni Mungu mwenye haki naye hawezi kuacha kuijali dhambi.
Yesu alionyesha pande zote mbili za tabia ya Mungu katika maisha yake. Alikuwa mwenye upendo na mwenye kusamehe kwa wale waliotubu, lakini aliwaonya kwa nguvu watu wenye kiburi, watenda maovu kama vile waandishi na Mafarisayo wa siku zake.
KUSUDI LA MUNGU (Hesabu 14:21)
Kusudi la Mungu kama lilivyofunuliwa ndani ya Biblia limetamkwa katika Hesabu 14:21: “Hakika yangu, kama niishivyo, tena kama dunia yote hii nzima itakavyojawa na utukufu wa BWANA”. Fungu hili jinsi lilivyo muhimu! Hapa Mungu anasema, kwa kiapo cha Mungu anatupatia hakika ya kwamba dunia siku moja itampatia Mungu sifa na utukufu.
Hili ni hakika kama ilivyo uhakika wa uwepo wake Mungu. Kwa uhakikisho huo twaweza kutazamia kwa kuamini kabisa kuwekwa kwa Ufalme wa Mungu hapa duniani.
Tumeona kuwa kuna ushahidi mwingi kwamba Mungu yupo, na kwamba Mungu kama aishivyo kwa hakika ndiye mwenye nguvu za kuongoza uumbaji milele na milele. Tunayo kila sababu nzuri sana, kwa ajili hiyo, kuamini tamko la Mungu kwamba dunia hii itajawa na utukufu wa BWANA kama vile maji yanavyoijaza bahari.
Wakati Ufalme wa Mungu utakapokuwepo ndipo wanaume na wanawake watampatia Mungu sifa na utukufu kwa unyenyekevu na kuhudumu katika utii. Katika hali hiyo dunia aliyoumba Mungu itaona ikirudi kwenye amani na mapatano kati ya Mungu na mwanadamu. Katika masomo yatakayofuata tutatafakari jinsi Mungu alivyotenda kazi hapo zamani, na hata sasa anafanya kazi , ili kuweza kutimizwa kwa kusudi hili la utukufu.
VITABU REJEA:
"Christadelphian Instructor" (R. Roberts)—Nos. 1-19, 41-46
"Elpis Israel" (J. Thomas)—Chapter 1
"Story of the Bible" (H. P. Mansfield)—Foreword, Chapters 1 and 2
"The Ways of Providence" (R. Roberts)—Chapters 1 and 2
MASWALI YA AYA
-
Biblia iliandikwa na watu wengi katika nyakati tofauti na walioishi sehemu tofauti. Tunawezaje kuthibitisha kuwa Biblia ni Neno la Mungu?
-
Ni kwa namna gani kweli ya Biblia imeonekana katika historia na unabii? Toa mifano.
-
Eleza unavyofahamu maana ya “roho ya Mungu” na “Roho Mtakatifu”.
-
Biblia inafunua nini kuhusu Mungu na tabia yake?
-
Kusudi la Mungu ni nini?
MASWALI YA INSHA
-
Tunaushahidi gani kwamba Biblia ni Neno la Mungu lenye pumuzi ya Mungu?
-
Onyesha kwa kutumia maandiko matakatifu kuwa Mungu ni Mmoja na wala siyo sehemu ya “Utatu”.