CSSA 2-1-02 - THE CREATION OF THE HEAVEN AND THE EARTH

Swahili

127. KUUMBWA KWA MBINGU NA NCHI

Katika somo letu lililopita, tulijifunza kwamba Biblia ni Neno la Mungu na kwamba katika Neno hilo tunasoma kuhusu mpango wake na kusudi lake na dunia. Somo hili litashughulika na mwanzo wa kusudi hilo- juma la Uumbaji.

Maajabu ya asili yanaonyesha kazi ya Mungu katika Uumbaji (Zaburi 19:1), lakini watu wengi leo hawaamini kwamba Mungu ndiye aliyeumba vitu vyote hapo mwanzo. Shuleni vijana wanafundishwa kuwa viumbe hai vilitokea kwa bahati tu wa muunganiko wa kemikali miaka mamilioni iliyopita. Wanafundishwa kwamba aina tofauti za viumbe hai vilitokea kutokana na matokeo yanayoitwa “mabadiliko”. Inafundishwa kwamba mwanadamu mwenyewe “alibadilika” kutokana na wanyama wenye umbo dogo.

Huu siyo ukweli, na wala haliwezi kuthibitishwa. Wanasayansi wenyewe wanakubali kwamba hiyo ni “nadharia” (yaani, jaribio la kuelezea namna kila kitu kilivyoweza kuwepo; badala ya kukubali kuwa Mungu ndiye Muumbaji). Maajabu ya asili hayawezi kuelezeka ikiwa tutamwacha Mungu ambaye ndiye mwenye kubuni na Muumbaji. Katika Biblia, Mungu anaeleza vitu vyote viliumbwa kwa namna gani na anafunua kusudi lake katika kuviumba (Rejea kwenye mawazo kuhusu “mabadiliko” nyuma ya sehemu hii).

Mwanzo 1; 2:1-3.

KUSUDI LA UUMBAJI (Hesabu 14:21; Hes. 2:14)

Kusudi la Mungu katika uumbaji lilikuwa ni kuijaza dunia utukufu wa Mungu, lakini hili halijatimizwa bado. Uzuri na maajabu ya uumbaji wa vitu vyote vyenye mwili kuanzia kwa vitu vikubwa mno mpaka kwa ua dogo sana au mdudu mdogo mno, inaonyesha kazi ya uumbaji wake wa kushangaza.Hata hivyo, utukufu utakaoonekana katika Ufalme utakuwa ukionekana ndani ya wanaume na wanawake wanaoonyesha tabia ya Mungu katika maisha yao.

Katika nyakati zote Mungu amekuwa akiita kutoka katika mataifa “watu kwa ajili ya Jina lake” (Matendo ya Mitume15:14). Watu hawa watakuwa ndiyo waliokombolewa kutoka katika vizazi vyote ambao wataonyesha utukufu wake wakati ujao, katika dunia ambayo itarudishiwa uzuri wake wa asili na amani. Jinsi utakavyokuwa mzuri ufalme ule, wakati watakatifu waliopewa uzima wa milele wataonyesha tabia kamilifu ya Mungu katika maisha yao; wakifundisha kwa mwongozo wao na kwa mifano yao namna watu wenye mwili na damu wanavyowapaswa kumtumikia Mungu.

Historia ya mwanadamu imejaa kumbukumbu ya uovu na matatizo. Hata utukufu maridhawa wa asili unaharibiwa na uchoyo wa mwanadamu na ujinga, lakini Mungu ataondoa hali hii wakati Ufalme wake utakapowekwa duniani. Ndipo kila kitu kwa kweli kitaangaza utukufu wake, kama ilivyotabiliwa ndani katika Maandiko Matakatifu kama vile Zaburi 72 na Mika 4:14.

“HAPO MWANZO” (Mwanzo 1:1-2; Mithali 3:19)

“Mwanzo” ni jina la kitabu cha kwanza katika Biblia, lina maana mwanzoni. Kitabu hiki kinatufahamisha kuwa Mungu ndiye Muumbaji. Mungu mwenyewe ametamka kwamba aliumba dunia na wanadamu (Isa. 45:18). Huu ni mstari wa ajabu kwani ni nukuu nyingine inayoonyesha kuwa Mungu ni mmoja (Tazama somo la 1) na kwamba aliumba mbingu na nchi kwa ubunifu na kwa kusudi. Hakuiumba ukiwa. Dunia itakaliwa na watu ambao siku moja watampa Mungu sifa na utukufu Mungu watakapokuwa wanaendelea kufurahia maajabu ya wakati wa Enzi ya Ufalme huo wa Mungu.

Katika Mwanzo 1:1,2 tunaambiwa kwamba “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi”. Nayo Nchi “ilikuwa ukiwa, tena utupu”- bila ya kuwa na utaratibu, pasipokukamilika? ilikwa giza na bila uhai. Kwa hiyo Mungu akaanza kuweka kila kitu katika utaratibu, tayari kwa uzima alioukusudia kuuweka humo ili alitimize kusudi lake.

Mstari wa pili unatueleza ya kwamba “roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji”. Roho ni nguvu za Mungu-ambayo kwa hiyo vitu vyote viliumbwa (Zaburi 104:30;Ayubu 33:4). Kazi hii ya matengenezo ilitokea yapata miaka 6,000 iliyopita. Mungu alisema neno, na malaika wakatekeleza amri hiyo, na kwa hiyo kazi ikawa imefanyika (Zab. 33:6-9; 103:20-21)

SIKU SITA ZA UUMBAJI (Mwanzo 1:3-31)

Kila moja ya siku za Uumbaji ilikuwa ya muda wa masaa 24. Kwa maana tunasoma ikawa“jioni na ikawa asubuhi siku ya kwanza” na kadhalika. Lakini angalia utaratibu wa uumbaji.

Siku ya Kwanza-mistari 3-5: Mungu akafanya nuru ili kuangaza katika giza. Nuru akaiita Mchana,na giza akaliita Usiku.

Siku ya Pili- mistari 6-8: Mungu akafanya anga na akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale maji yaliyo chini ya anga. Akafanya mawingu yatokee na mbingu nayo ikatokea.

Siku ya Tatu- mistari 9-13: Maji yaliyokuwa juu ya nchi yakusanyike katika bahari, ili pakavu paonekane, Mungu akapaita pale pakavu nchi.Mungu akaamuru nchi itoe majani, miti mingine na kila aina ya miti ikaota katika nchi.

Siku ya Nne- mstari 14-19: Mungu akafanya (au “akateua” –linganisha Zaburi 104:19) mianga miwili,Jua litawale mchana, na mwezi (pamoja na Nyota) utawale usiku. Hivyo viliwekwa ili kuleta hali inayotakiwa kwa ajili ya uhai duniani.

Siku ya tano- mstari 20-23: Samaki wakatokea baharini. Na wanyama wengine pia wanaoishi majini wakatokea, na ndege wa aina zote warukao angani waliumbwa

Siku ya sita- mstari 24-31: Mungu aliumba wanyama ambao wanaishi katika nchi kavu kama vile wanyama wa kufungwa, wanyama wa porini na watambaao. Akatazama kazi yake yote ya mkono wake na kuona ni njema. Lakini vyote hivi havingeweza kamwe kuonyesha na kumpa utukufu Mungu kwa jinsi inavyompendeza. Hivyo mtu aliumbwa kwa mfano wa Mungu; ili kwamba awe na uwezo wa kuonyesha tabia ya Mungu, naye akawekwa kuwa mtawala juu ya wanyama wote walioumbwa. Matunda na mazao ya nchi yalikuwa yatumiwe kama chakula kwa ajili ya mtu na mnyama. “Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana”. Pamoja na kwamba mtu aliishi kwa amani na ushirika na viumbe vyote alivyoviumba Mungu, kazi yote ya mikono ya Mungu hakika kwa vyovyote vile ilikuwa njema sana. Ni mojawapo ya furaha ya Ufalme ujao duniani kwa ajili yetu, tunapotazamia dunia kuumbwa kama bustani ya Edeni na kushangaza kwa uzuri wa kazi ya uumbaji wa Mungu.

Wakati Mungu aliposema kuwa kila alichokiumba kilikuwa“chema sana”, hili neno lilimjumuisha na mtu. Katika hali hii mtu hakuwa mwenye kufa au kutokufa. Alikuwa “mwema sana” kimaumbile naye alizungukwa na hali njema tu. Alikuwa bado hajapimwa ili kuona kama angemtii Muumba wake.

Siku ya Saba- Mwanzo 2:2-3: Katika siku hii Mungu akastarehe au “akaacha” kufanya kazi zake (Mwanzo 2:2-3). Baadaye katika historia, siku ya saba au “sabato” ilitengwa kuwa “siku ya kustarehe” kwa wana Israeli, ili kwamba wastarehe wasifanye kazi zao na badala yake watumie muda huo kufanya mambo ya Mungu (Kutoka 31:16-17).

Nabii Isaya aliwaonyesha wana wa Israeli namna walivyopaswa kuitunza sabato. Walikuwa wameigeuza “siku ya kustarehe” kuwa siku ya mtu kufanya anasa zake na kusababisha watu wao kupata taabu. Badala yake, walitakiwa kuwaonyesha watu rehema na wema na kufurahia kufanya mapenzi ya Mungu (soma Isaya 58)

Mungu alisema, ya kwamba sabato ilikuwa “ishara kati ya mimi na wana wa Israeli milele; na maana siku 6 BWANA alizifanya mbingu na nchi, na akastarehe siku ya saba na kupumzika”. Hili linathibitisha ya kuwa siku za uumbaji zilikuwa siku halisi za masaa 24 kwa siku kama tunavyozielewa. Hakuna amri kwa wafuasi wa Kristo kuishika siku ya saba “sabato” tu. Ni lazima waione kila siku kuwa ndiyo siku ya kufanya kazi ya Mungu.

RAHA YA SIKU YA SABA NI KIVULI CHA UFALME (Waebrania 4:4-11)

Raha ya sabato ilielekeza mbele kwenye milenia ya saba (miaka elfu moja) tangu uumbaji, wakati Ufalme wa Mungu utakapowekwa duniani. Katika Waebrania. 4:9-11 tunasoma - Basi, imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu. Kwa maana yeye aliyeingia katika raha yake amestarehe mwenyewe katika kazi zake, kama vile Mungu alivyostarehe katika kazi zake. Basi,na tufanye bidii kuingia katika raha ile.

''Starehe” ile ya miaka elfu moja itakuwa wakati ambapo wanadamu wanatakiwa kuacha kazi zao na nia zao zitaigeukia njia ya Mungu. Kwa furaha watasema, “Njooni , twende juu mlimani kwa BWANA, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake;maana katika Sayuni itatoka Sheria,na Neno la BWANA katika Yerusalemu“(Isaya 2:2-4). Kwa hiyo utakuwa wakati wa amani na mapenzi mema kwa watu wote, kwa kuwa nabii anasema ''taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe” (mstari 4)

Watakatifu (watu wenye miili ya utukufu ambao ni wafuasi wa Yesu Kristo) wataishi na kutawala na Kristo miaka elfu moja, na hii ndiyo “starehe au raha” ya wakati ujao iliyoahidiwa kwa watu wa Mungu (Ufunuo. 20:4,6)

VITABU REJEA:

See "Five Facts That Show the Theory of Evolution to be False"—Appendix Pages

"Elpis Israel" (J. Thomas)—Chapter 2

"The Story of the Bible" (H. P. Mansfield)-Chapter 3

"The Visible Hand of God" (R. Roberts)-Chapter 2

"Wrested Scriptures" (R. Abel)—Section C

"First Principles of Bible Marking Course"—(C.S.S.S.)—pages 12-15

 

MASWALI YA AYA

  1. Mungu alikusudia nini katika uumbaji?

  2. Malaika walishiriki namna gani katika kazi ya Uumbaji?

  3. “Sabato” ilikuwa ni nini?

  4. Eleza namna raha ya ''sabato” inavyoelekeza mbele wakati wa Ufalme unaokuja.

 

MASWALI YA INSHA

  1. Utaratibu wa Uumbaji ulikuwaje kama iliyoandikwa katika Mwanzo 1? Uumbaji ulichukuwa muda gani?

  2. Fafanua jinsi utakavyomweleza rafiki yako wa shuleni ni kwa nini unakataa nadharia ya mabadiliko na kwa nini unaamini kwamba vitu vyote viliumbwa na Mungu kwa muda wa siku 6.

Swahili Title
127 KUUMBWA KWA MBINGU NA NCHI
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type