139. YUSUFU ANASHABIHIANA NA KRISTO
Somo letu lililopita (somo la 13), lilituonyesha jinsi Mungu alivyoiongoza familia ya Yakobo na kumfanya Yusufu kuwa mtawala nchini Misri. Na hatimaye akawalinda Israeli.
Somo hili linaonyesha namna Mungu alivyosimamia matukio ya maisha ya Yusufu ili yawe taswira au dalili ya maisha na majukumu ya Bwana Yesu Kristo
Mwanzo 45
MAANA YA KUSHABIHIANA NI NINI?
Shabihi ni ulinganifu wa vitendo vinavyoambatana na matukio mbalimbali ya kiBiblia kama inavyo ainishwa na watangulizi wa mambo yatakayotokea baadaye ambayo ni makubwa kuliko ya mwanzo. Maana nyingine ya shabihi ni mtu ambaye amekusudiwa kuwa kielelezo cha matukio makubwa kuliko ya mwanzo.
Ni “taswira” ya matukio yajayo, na kama taswira ni kivuli cha matukio yanayoonekana ambayo ni kivuli cha mambo yasiyoonekana kwa kukosekana undani halisi wa jambo lenyewe. Siyo kwamba ushabihiaji na taswira vinaenda sambamba.Ni muhimu kukumbuka tofauti zilizopo kama ilivyo kujifunza kufanana kwa vitu.
MASHABIHIANO NI NAMNA YA MAFUNDISHO
Mungu mara nyingi anafafanua matukio kwa njia ya Neno lake kwa kutumia mashabihiano au mifano. Tumekwisha kuona jinsi baadhi ya matukio katika maisha ya Ibrahimu na Isaka yanavyo elekeza kwenye matukio ambayo Kristo angeyatenda katika maisha yake. Kwa mfano katika kumtoa Isaka (Mwanzo 22) tunaweza kuona taswira au kushabihiana kwa dhabihu na ufufuo wa Kristo.
Kutangatanga kwa wana wa Israeli jangwani Mtume Paulo analiita jambo hilo kuwa "vielelezo" kwetu (1 Wakorintho. 10:6, 11). Kwa maelezo ya ziada, tunasoma "mifano au "vielelezo siyo kuwa tuwaige mabaya yao". Paulo anatufundisha tujifunze kutokana na na uzoefu wao na "siyo kufuata" mambo yale yaliyosababisha wao washindwe. Mfano ni kama fumbo au masimulizi yenye maana iliyofichika. Maisha aliyoishi Yusufu yanalinganishwa na sanaa inayoibua hisia za ndani za fumbo ya maisha ya Yesu Kristo, ingawaje Yusufu aliishi miaka elfu mbili kabla ya Yesu Kristo Kuzaliwa.
YUSUFU ANAVYOSHABIHIANA NA KRISTO
Yusufu anafananishwa na Yesu katika mambo haya:-
-
Wote wawili Yusufu na Yesu walipendwa na baba zao, lakini walichukiwa na ndugu zao (Mwanzo 37:4-8; linganisha Mathayo. 3:17; Yohana 15:25)
-
Ndugu zake Yusufu walimwonea wivu kwa sababu ya njozi zake zilizoelekeza mbele kuhusu mamlaka yake juu yao. Watawala wa kiyahudi walimwonea wivu Yesu kwa sababu ya mamlaka na kukubalikawa kwake na watu (Mwanzo 37:5-7; linganisha Yohana 19:15; Mathayo 27:18).
-
Ndugu zake Yusufu walipanga njama za kifo chake na vivyo hivyo nao Wayahudi walipanga kifo cha Yesu (Mwanzo 37:18-20 linganisha Mathayo 21:38, 26:4)
-
Nduguze Yusufu walinuia kumwua na kumtupa ndani ya shimo, kama vile kifo. Huko Misri alitupwa gerezani ingawa hakutenda dhambi yoyote. Wayahudi, Wamataifa (Warumi chini ya Pilato) walikubaliana kumwua Mwana wa Mungu asiye na dhambi yoyote (Soma Mwanzo 37:26-28; 39:20-21; linganisha Mathayo 27:26; Matendo ya Mitume 4:25-27, ambapo Wayahudi na watu wa Wamataifa fa waliungana pamoja).
-
Kama vile Mungu alivyomtoa Yusufu kutoka gerezani na kumteuliwa kuwa wa mtawala wa pili kwa Farao, ndivyo alivyomfufua Yesu kutoka kaburini na kumpatia hali uzima wa milele na heshima ya kuwa upande wa mkono wake wa kulia (Mwanzo 41:14; 39-42 linganisha Matendo ya Matendo 3:24, 33; 3:13-21).
-
Nduguze Yusufu walitafuta msaada wake wakati walipokuwa na shida. Hawakumfahamu na kumsujudia hata nchi akiwa mtawala. Hivyo hivyo wakati ujao wana wa Israeli wakati wa dhiki kuu wataokolewa kwa Kristo. Mwanzo hawatamtambua, lakini watakapotambua kwamba ndiye Masihi kwa kuona alama za kusulubiwa miguuni na mikononi mwake watalia kwa kuomboleza na kuogopa sana (Mwanzo 45:1-8 linganisha Zekaria 12:10-14, 13:6; Isaya 49:6)
-
Yusufu hakujali dhambi zao na akawapatia eneo zuri sana huko Misri. Ndivyo hata Bwana Yesu Kristo atawarejesha Israeli na kuwawezesha kurithi nchi ya ahadi na katika amani na mafanikio. Chini ya utawala wake watakuwa “kichwa” wala hawatakuwa “mkia” kati ya mataifa (Mwa. 45:5, 9-11 linganisha na Zakaria 2:12; Mika 4:7-8)
MAFUNDISHO KUTOKANA NA MAISHA YA YUSUFU
Maisha ya Yesu yanafanana sana na maisha ya Yusufu yalivyokuwa. Tunaweza kutazamia kazi ambazo Kristo atazifanya baadaye kuwa sawa sawa na matukio aliyoyafanya Yusufu wakati wa utawala wake. Kwa kweli manabii wanatuambia hayo na ndivyo itakavyokuwa. Kutokana na maisha ya Yusufu tunaweza kutazamia wakati ujao kurudi kwa Kristo ambaye atajidhihilisha kwa watu wake. Atawakusanya, kuwarejesha na kuwabariki katika Ufalme ambao hivi karibuni atauanzisha. Kwa hiyo tunafahamu kwa sehemu mambo yale ambayo Kristo atatenda wakati wa kurudi kwake na hili linatusaidia kuweka picha ya Ufalme akilini mwetu.
Ili kujitayarisha kwa ajili ya utukufu wa wakati ule inatupasa kujifunza somo la maisha ya Yusufu. Ni lazima tujiulize wenyewe ni sifa gani zilizo sababisha Yusufu astahili kupendwa na kutawala. Tunaona jinsi maisha ya Yusufu yalivyoongozwa na kutawaliwa na Mungu ili kwamba kusudi lake kwa famili ya Yakobo litimie. Inabidi pia tuzingatie jinsi Mungu anavyoongoza matukio maishani mwetu. Kama tutafuata maagizo yake katika Neno Lake tutakuwa kati yao wale watakao furahia kumheshimu katika kipindi cha enzi cha Ufalme wa ajabu.
MUHTASARI
-
Kufanana kwa karibu sana kati ya maisha ya Yusufu na maisha ya Kristo ni ukweli kabisa na wenye kushangaza.
-
Mateso ya Yusufu yalikuwa yanaonyesha mbele kuhusu mateso makubwa ya Kristo. Kupewa kwake madaraka makubwa kunaonyesha ufufuo na utukufu wa wakati ujao wa Bwana Yesu Kristo.
-
Familia ya Yakobo ilinyenyekezwa na halafu kupokelewa kutokana na kutukuzwa kwa Yusufu aliyepewa madaraka makubwa sana- hivyo hivyo pia Israeli watanyenyekezwa kabla ya kurejeshwa na Masihi wao aliyetukuzwa.
-
Wale wanaofuata maagizo ya Mungu, kama Yusufu, nao pia watabarikiwa na aliye mkubwa kuliko Yusufu, yaani Bwana Yesu Kristo katika nchi ya ahadi.
VITABU REJEA:
"Elpis Israel" (J. Thomas)—Part 2, Ch. 3 "The Parable of Joseph"
MASWALI YA VIFUNGU
-
(a) “Kushabihiana” ni nini?
(b) Toa mifano jinsi hili lilivyo aina ya mafundisho katika Maandiko Matakatifu.
-
Onyesha jinsi alivyotendewa Yusufu na nduguze kwa ajili ya chuki yao na kupanga kumuua kuwa ni mfano wa jinsi alivyotendewa Kristo na Wayahudi.
-
Tunaweza kutegemea jambo gani litakalo watokea wana wa Israeli wa asili wakati wa kuja kwa Kristo mara ya pili? (tumia habari ya mfano wa Yusufu akijitambulisha mwenyewe kama mtawala wa nduguze.
MASWALI YA INSHA
-
Eleza jinsi maisha ya Yusufu yalikuwa mfano wa kuja kwa mara ya kwanza kwa na kurudi mara ya pili kwa Kristo.
-
Andika maelezo ya tabia ya maisha ya Yusufu yanayotupatia mafundisho katika ujana wetu.