142. MAPIGO NA PASAKA
Musa alikuwa karibu kuingia Ikulu ya Farao tena, siyo kama mwana, bali akiwa balozi wa BWANA. Ujumbe alioupeleka ulikuwa “wape watu wangu ruhusa waende kunitumikia”.
Kusudi la BWANA halikuwa la kuwapatia uhuru Israeli kutoka utumwani tu bali pia kuwaonyesha Wamisri Ukuu wake na nguvu zake. Alikuwa anakwenda kujidhihirisha mwenyewe kuwa ndiye Mungu mmoja na wa kweli, na kulifanya taifa kubwa la Misri na mfalme wake mwenye kiburi na kujiona kutetemeka mbele yake.
Hili tendo lilifanyika karne zilizopita, mataifa ya wasioamini wanakumbuka njia ambayo BWANA, Mungu wa Israeli alipata ushindi juu ya Wamisri, linganisha Yoshua 2:9-11; 1Samweli. 6:6
KUTOKA 11 na 12
MUSA ANARUDI MISRI
Mungu alijidhihirisha pale penye kichaka kwamba alikuwa amedhamiria kuwakomboa watu wake Israeli. Sasa alianza mfululizo wa matukio ambayo angeyatumia ili kutimiza nia yake hiyo.
Kwanza, alimwita Haruni kwenda mlima Sinai kukutana na mdogo wake, Musa. Hao wanaume wawili ndipo wakaingia katika nchi ya Gosheni na kupeleka ujumbe wa ukombozi wa BWANA, kwa wazee wa Israeli (Kutoka 4:27-31)
MUSA NA HARUNI MBELE YA FARAO (Kutoka 5)
Mashindano makuu sasa yalianza kati ya BWANA na Farao. Musa, akimwakilisha Mungu, alikwenda tena kwenye baraza la Farao, sehemu ile ile ambayo alikuwa ametumia miaka arobaini ya maisha yake (Kutoka 7:7; Matendo ya Mitume 7: 23,30). Ombi lake la kwanza lilipuuzwa na pamoja na Haruni walifukuzwa mbele ya Farao (Kutoka 5;1-9). Ili kuonyesha dharau yake kubwa kwa BWANA, aliongeza mzigo juu ya wana Israeli. Hawakupatiwa majani, na walitakiwa kutimiza idadi ileile ya matofari! (Kutoka 5:10-19). Hii ilikuwa hali isiyowezekana nao watu katika huzuni zao wakawainukia Musa na Haruni na kuwalaumu kwa kuwa mateso yaliongezeka (Kutoka 5:20-23).
Hatua kwa hatua, huyu mtawala mwenye nguvu wa taifa lililokuwa kubwa sana wakati ule alikuwa anyenyekeshwe na wakati huo Musa aweze kuwa mkuu zaidi na zaidi mbele yake. Kusudi la pambano hili na Farao Mungu alilielezea kuwa: “ili kukuonyesha uweza wangu, tena kwamba Jina langu litangazwe katika dunia yote” (Kutoka 9:16). Misri ingeziona nguvu kuu ya BWANA zikidhihirishwa katika matukio yatakayo lifika taifa hilo. Misri ingeguswa na matukio, na sehemu kubwa ya matukio hayo yangewasaidia wana wa Israeli kuamini (soma Kumbukumbu la Torati. 4: 34-37; 7:8-9).
Wakati Musa alipokwenda mbele ya Farao kwa mara ya pili, alitupa chini fimbo yake mbele yake nayo ikageuka kuwa nyoka. Lakini, kwa ujanja wao, nao wachawi wa misri wakafanya kilichoonekana kuwa sawa na alivyofanya Musa. Farao akakataa kupokea ishara hii ya nguvu ya Mungu hata baada ya fimbo ya Musa kuwaacha wachawi bila kuwa na nyoka zao! (Kutoka 7:10-13). Baadaye Farao angelazimishwa kukubali ukuu wa kwa BWANA kwa mapigo ambayo yangefuata.
MAPIGO (Kutoka 7:14-25)
-
Maji kuwa Damu – Kutoka 7:14-25
Wamisri walijivunia mto mkubwa wa Nile na waliuabudu kama ni mungu. Hawakuwa na chanzo kingine cha maji. Pigo hili liliwafanya kuuchukia mto wao na kuchukia harufu ya uvundo wa samaki wake waliokufa. Lakini wachawi waliiga hili na kwa hiyo Farao akafanya moyo wake kuwa mgumu.
-
Vyura – Kutoka 8:1-5
Mungu akafanya Vyura kutoka majini na wakaifunika nchi nzima. Wakaingia katika nyumba zote za Wamisri. Chura naye pia alikuwa akiabudiwa na Wamisri, lakini sasa Farao alikuwa amemwomba Musa ili amsihi BWANA kuwaondoa maana lilifanyika kuwa pigo. Mungu akasikia maombi ya Musa na pigo likasimamisha wakati ule ule alioomba Farao. Kule kusimamishwa tu kwa pigo kuliimarisha ubishi wake Farao na kwa hiyo hakumsikiliza Musa (linganisha Isaya 26:10)
-
Makundi ya Chawa – Kutoka 8:16-19
Pigo hili lilikuwa chungu zaidi kwa sababu kulikuwa na chawa “juu ya wanadamu na juu ya wanyama”,ambao walisababisha kila mtu na mnyama wakose raha na wapate maumivu Wachawi hawakuweza kuiga hili na walikubali kuwa “hiki ni kidole (chanda) cha Mungu”, lakini Farao hakuwasiliza.
-
Mainzi: Kutoka 20-32.
Jambo la maana katika pigo hili ni kuwa ulikuwepo mpaka kati ya Wamisri na wana wa Israeli (mstari 21-23). Tangu siku hiyo na kuendela mapigo yalianguka juu ya Wamisri tu.
-
Tauni juu ya wanyama: Kut. 9:8-12
Ugonjwa wa kutisha ulizuka, uliosababisha kuua mifugo yote ya Misri, ambao walifikiriwa na watu kuwa “wakfu” .
-
Majipu ya kuwasha juu ya mwanadamu na juu ya mnyama – Kutoka 9:8-12
Hili liliwadhuru hata wachawi wenyewe pia. Hata hivyo pamoja na mateso haya yote mabaya, Farao alibaki mkaidi kwa kukataaa maombi yaliyorudiwa rudiwa na Musa kwa ajili ya kuwapa ruhusa watu wa Mungu.
-
Dhoruba ya Mvua ya mawe -Kutoka 9:13-35
Jinsi ilivyokuwa yenye kutisha dhoruba hii kwa watu wa Misri, kwa kuwa mvua yenyewe ilikuwa haijulikani kabisa kwao (Zekaria 14:18). Angalia ya kwamba baadhi ya Wamisri sasa walianza kuwa na hofu kwa BWANA (mstari 20), kwa ajili ya kutimiza kusudi lake.
-
Nzige – Kutoka 10:1-20
Kutokana na ukaidi wa kijinga wa Farao pigo hili lilianguka juu ya Misri na wakala mimea yote ya nchi, hata ikawa Farao alimsihi Musa amsamehe dhambi yake. Tena BWANA alikuwa mwenye rehema na akawaondoa nzige, lakini Farao akaufanya moyo wake kuwa mgumu tena.
-
Giza nene – Kutoka 10: 24-29
Pigo hili la kutisha lilifutilia mbali jua, ambalo lililokuwa linaabudiwa na Wamisri akiwa mungu wao mkuu. Tena Farao akakataa ombi la Musa, hivyo alimwacha na maneno “mimi sitakuangalia uso wako tena!”
-
Pasaka:
Pigo la mwisho la kutisha lilikuwa linakaribia kuja juu ya Misri ili kumlazimisha Farao awape ruhusa Israeli kuondoka. Kifo kiliwekwa kuua kila mzaliwa wa kwanza wa kila familia katika Misri, ikiwa ni pamoja wazaliwa wote wa kwanza wa wanyama.
-
Maandalizi kwa ajili ya Pasaka- Kutoka 12:1-4
Waisraeli waliambiwa kila mtu atake(aombe) chombocha fedha kwa jirani zao Wamisri, ambao kwa hiari yao waliwapatia. Muda ulikuwa wa mwezi wa Abibu, mwezi wao mpaya wa kwanza, kwa kuwa tendo la kutoka Misri ndio ungekuwa o mwanzo wao mpaya.
Katika siku ya kumi walichukua kondoo dume wa mwaka mmoja, asiye na lasoro. Kisha siku ya kumi na nne walimchinja “katikati ya jioni mbili” (yaani kati ya saa 9 mchana na saa 12 jioni) mstari 6 (pembezoni). Damu ya mwana kondoo iliwekwa ndani ya bakuli na kunyunyiziwa kwenye miimo ya milango na kizingiti cha juu ya fremu zake katika nyumba zao kwa kutumia tawi la mti wa hisopo. Kisha yule mwana kondoo aliokwa mzima mzima (mstari 9). Wana wa Israeli walikuwa katika hali ya matazamio jioni ile. Iliwabidi wakae majumbani mwao (mstari 22) na kula nyama ya mwana kondoo pamoja na mboga za majani zenye uchungu na mkate usiotiwa chachu (mstari 8). Hawakutakiwa kuvunja mfupa wowote wa mwanakondoo (mstari 46). Walitakiwa wayachome motoni mabaki yoyote yaliyokuwa yamebakia (mstari 10). Walitakiwa wale chakula hicho kwa haraka-haraka, wakiwa wamefunga viatu vyao miguuni, mavazi yao yakiwa yamefungwa na fimbo zikiwa mikononi mwao (mstari 11). Wakati wakisherehekea, malaika wa mauti alipita katika nchi yote ya Misri akiwapiga wazaliwa wa kwanza wa kila familia. Ni pale tu alipoona damu kwenye kizingiti ndipo “alipopita juu” bila kuleta mauti (mistari 12-13,23). Usiku huu wa kutisha ukafanyika siku ya kumbukumbu kwa wana wa Israeli na mpaka leo hii Wayahudi huishika sherehe ya Pasaka (linganisha mstari 14). Usiku ule ule ambapo Misri ilipoteza kila mzawa wa kwanza, wana wa Israeli waliokolewa kutoka kwenye utumwa katika nchi ya Misri (mstari 27).
-
Yesu ndiye Pasaka wa kweli – 1 Wakorintho 5:7
Inashangaza namna Yesu alivyotimiza kuwa mfano wa mwana kondoo wa pasaka (Yohana 1:19). Yesu aliingia Yerusalemu siku ya kumi ya mwezi wa kwanza na “kubaki” humo mpaka muda wa kusulibiwa kwake siku nne baadaye. Damu yake ilimwagika kwa ajili ya ukombozi wa wale wanaomwamini na wako tayari kuiacha Misri (utumwa wa dhambi).
Alikuwa dhabihu kamilifu kwa kuwa hakukuwa na kasoro yoyote iliyoonekana kwake. Kutokutenda kwake dhambi na haki yake ilifanya iwezekane kwa Mungu kumfufua kutoka kwa wafu na kumwinua mpaka mkono wake wa kuume sasa ni mpatanishi kwa ajili ya wale wanaotafuta msamaha wa dhambi na njia mpya ya maisha. Yesu alishirika pasaka pamoja na wanafunzi wake kabla ya kifo chake. Wakati wa chakula hiki alisema “agano jipya” katika kumwaga damu yake. Hili agano jipya lingempatia mtu njia ya wokovu kutokana na utumwa wa dhambi na kifo.Kama watu watapokea dhabihu yake na kumtii Mungu, ndipo watakaposhiriki pamoja naye katika “sherehe ya wokovu” katika ufalme wa Mungu(Mathayo 26:26-29). Tangu dhabihu ya Yesu waumini wote waliobatizwa katika eklesia zake wanashiriki mkate na divai kwa kumbukumbu ya ukombozi. Katika kufanya hivyo wanatiwa moyo kuutazama ulimwengu huu, kama Misri -katili, na anayetia watu utumwani, na yenye giza (dhambi), akaishia ikiishia katika kifo: na kumtazama Mungu ambaye ni mwenye nguvu na awezaye kutuokoa sisi kutoka katika kifo.
-
Pigo la mwisho mfano wa Hukumu Ijayo – Luka 21:24-28
Watu wa dunia leo wanakataa kumsikiliza Mungu ingawaje analeta adhabu juu yao. Wanaifanya mioyo yao kuwa migumu na kukataa kumheshimu Mungu. Kwa sababu hii majanga makubwa yanatokea duniani. Majanga haya ni ya asili, na yanatokana na shughuli zote za binadamu - kwa njia ya siasa, hudumu za jamii, uchumi, dini na mazingira. Yanatokea mara kwa mara na kwa madhara makuu zaidi. Ni watu waliojiandaa kwa ajili ya tukio kuu kuliko yote katika historia yao- kutokea kwa Mwana wa Mungu duniani. Kwa atawaokoa watu wake Israeli kutokana na kongwa la mataifa (Yeremia 16:14; 15; Ezekieli 36: 21-24; Warumi 11:25-27). Kisha ndipo atawaokoa mataifa kutoka kongwa la dhambi na kuwaongoza wote, Myahudi na mtu wa Mataifa, katika maisha mapya ya kumtumikia Mungu. Yesu alituonya “tukeshe” ili kwamba tusikutwe “tumelala” katika siku ile (Luka 21:34-36)
VITABU REJEA:
"The Story Of The Bible" (H. P. Mansfield)—Pp. 258-277
"Elpis Israel" (J. Thomas)—Pp. 290-292; 295-297
"Visible Hand Of God" (R. Roberts)—Chapts. 11-14
"Law Of Moses" (R. Roberts)—Chapter 21
"Christadelphian Instructor"—Questions and Answers Nos. 91, 92
MASWALI YA FUNGU
-
Orodhesha mapigo yale kumi
-
Ni kwa nini Mungu alileta mapigo juu ya Misri?
-
Elezea sikukuu ya Pasaka iliyoshikwa na wana wa Israeli huko Misri.
MASWALI YA INSHA
-
Elezea jinsi wana wa Israeli walivyoishika Pasaka ya kwanza. Onyesha matokeo ya usiku ule kwa upande wa wana wa Israeli na kwa upande wa Misri.
-
Fafanua jinsi Yesu alivyokamilisha mfano wa kuwa mwana kondoo wa pasaka
-
picha ya mlango na upako wa damu ya Pasaka.