CSSA 2-3-01 - YAHWEH ESTABLISHES THE KINGDOM OF ISRAEL UNDER DAVID

Swahili

176.BWANA ANAANZISHA UFALME WA ISRAELI  CHINI YA DAUDI 

“Na BWANA akamlinda Daudi kokote alikokwenda”

2 Samweli 5,6,8, 10 na 12:26-31

Baada ya kutawala kwa miaka saba juu ya Yuda huko Hebroni Daudi mwishowe alikubaliwa na makabila yote nao “wakamtia mafuta  Daudi kuwa mfalme juu ya Israeli” (mstari 3) huko Hebroni .Baada ya hili Daudi alikwenda na watu wake hadi Yerusalemu ambayoilikuwaikitawaliwa na Wayebusi na “akaiteka ngome  ya Sayuni”(mstari 7 ), na huko “Yerusalemu ,Daudi  akatawala miaka 33 juu ya Israeli na Yuda” (mstari 5 ). Tunaambiwa kwamba “ Daudi aliendelea kusitawi na kuongezeka utukufu , na BWANA,Mungu wa Majeshi alikuwa  pamoja naye” (mstari 10). Tutaona kwa kadiri tunavyomfuata Daudi akipanua mipaka ya Ufalme wa Israeli,yaani “majeshi  ya BWANA”yalikuwa pamoja naye katika vita zake  naye Daudi alifahamu ya kuwa BWANA, asipokuwa  pamoja naye basi angepigana bure.

DAUDI ANALETA SANDUKU  LA AGANO SAYUNI: 2 Samweli 6, 1 Mambo ya Nyakati  13: 13 .

Tamaa ya kwanza ya Daudi,sasa baada ya kuitekaYerusalemu ,ilikuwa  ni kulileta Sanduku   la Agano la BWANA hadi Sayuni na kuianzisha tena upya ibada ya BWANA. Sanduku lilikuwa limekaa nyumbani mwa Abinadabu huko kiriath – yearimu, lilikiwa limerejeshwa na wafilisti waliokuwa wameliteka wakati wana wa Eli kwa upumbavu walipokwenda nalo vitani.

Daudi akawaarifu watu juu ya nia yake ya kulirejesha Sanduku nao watu wote wakafurahi mno.Liliwekwa katika gari  jipya lilolokuwa likokotwa na maksai wakati ambao Uzza na Ahio ,wana wa Abinadamu waliliongoza gari  hilo ulikuwa ni wakati wa shangwe kuu naye  Daudi pamoja  na nyumba yote   ya Israeli  wakacheza mbele  ya BWANA  kwa aina zote za vyombo vya muziki(mstari 8); lakini kwa bahati  mbaya , katikati ya shangwe  hizo, kifo kikatokea-wale ng’ombe  wakajikwaa nayeUzza  akanyosha mkono  wake ili alitegemeze vizuri Sanduku ndipo alipouawa. Kwa nini kitu  kama hicho kitokee? Kwa nini  Mungu alikasilika?  Sanduku  likawekwa   pembeni   na kuwekwa kwenye nyumba ya   Obed-edomu , naye  Daudi kwa huzuni  kubwa    akufikiri sana ni sababu gani iliyosababisha hata jambo hilo la kutisha litokee.  Haikuchukua muda   mrefu   kabla hajapata jibu –kwani  majibu  kwa matatizo yetu yote yanapatikana  katika  Biblia . Akakumbuka jinsi BWANA alikuwa amemwambia   Musa ya kwamba “mtu yeyote asilibebe sanduku la  Mungu isipokuwa Walawi tu” (1 Mambo ya nyakati15: 2, 13;Kumbukumbu  la Torati  16:8) Nisomo muhimu  jinsi gani  Daudi na Israeli  wote walijifunza. Haijarishi kwamba tuna nia  roho ya jinsi gani  katika  kumtumikia Mungu  iwapo hatumikii  katika njia  yake aliyotuelekeza, yaani kwa kufuatana na Kweli  iliyofunuliwa .Nia ya roho ya dhati  thamani yake ni ndogo sana. Yesu alisema  wote wanaomwabudu Mungu  inawapasa kufanya hivyo katika“roho na kweli ” (Yohana 4: 23; Yoshua 24: 14)

Baada ya miezi mitatu  Daudi  tena alijindaa kulileta Sanduku  hadi Yerusalemu. Kipindi  hiki , walakini  alifanya  hivyo  kwa kufuata  njia sahihi ya Mungu  aliyowaagiza, na hivyo “wana  wa  Israeli  wa kabila la  Walawi walilibeba  sanduku la  Mungu juu ya mabega  yao” (1 Mambo ya nyakati  15: 15) Kulikuwa na shangwe kuu na furaha  wakati  Sanduku lilipokuifikishwa katika jijini la Yerusalemu na  Daudi  mwenyewe alikuwa  amevaa kama kuhani na “kucheza mbele ya BWANA”. Dhabihu  zilianza kutolewa  mwanzo  wa safari  ya Sanduku(baada ya hatua  6, 2 Samweli 6:13) na wakati wa  kufika kwenye  Hema aliyokuwa ameisimika  Daudi (2 Samweli 6:17).Je, tunaweza kufikilia  shangwe  ya moyo  na sifa ya Daudi na watu wake  hasa baada  ya  kutolifikisha Sanduku miezi michache  iliyopita?

Maneno ya Zaburi 69,110,132, na 1 Mambo ya Nyakati 6,8,36, yaliyoandikwa wakati huo ,yanadhihirisha shangwe na sifa hizi.

WAFILISTI WANAIVAMIA ISRAELI: 2 Samweli 5: 17-25, linganisha pia  na 1 Mambo ya Nyakati 14:8-17.

Wakati wafilisti wa walioishi upande wa kusini na magharibi ,waliposikia kwamba Daudi wamemtia mafuta ili kuwa mfalme wa Israeli,walimvamia.Walijitawanya katika bonde la Warefai  lililo upande wa  kusini magharibi ya Yerusalemu kuelekea Bethelehemu . Daudi akashuka akajiimarisha ndani ya ngome huko Sayuni .Akamwuliza BWANA iwapo awashambulie, na ikiwa ndivyo ,je BWANA,atawaweka mikononi mwake? Jibu kutoka kwa Mungu lilikuja mara moja na mfalme jasiri wa Israeli alihakikishiwa ushindi Hivyo Daudi akawapiga na kumpa ushindi huo BWANA “Mungu amewafurikia adui zangu machoni pangu, kama mafuriko ya maji (1 Mambo ya Nyakati 14: 11) .Wafilisiti wakaziacha sanamu zao ,Daudi na wenzake wakazikusanya  na kuzichoma moto. Lakini ushindi huo haukuwa ndiyo mwisho ,Wafilisti wakapanda tena wakajikusanya  katika bonde la Warefai.Daudi akamwuliza  tena BWANA,Mungu na mara hii akaelekezwa kwamba atumie mbinu tofauti .Asiende mbele kama  mwanzo, jinsi Wafilisti walivyotazamia bali atokezee upande wa nyuma yao karibu na miti ya miforsadi , naye akangojea ishara kutoka kwa Mungu kabla ya kushambulia “utakapoisikia sauti ya kwenda katika vilele vya miti ya miforsadi” Mungu alifanya hivi ili kumkumbusha Daudi kwamba ushindi ni BWANA, kwamba malaika wake wako kazini kila wakati kwa ajili ya hatima ya mema kwa Israeli. Lakini kule kungojea malaika watangulie kwanza, Daudi na watu wake walifundishwa kuwa imani ina nguvu zaidi kuliko jeshi lolote lenye nguvu sana,Mungu anaweza kuangamiza adui bila juhudi zetu, nasi inatupasa kila wakati kukumbuka kwamba bila yeye hatuwezi kutenda lolote .Huu hapa ulikuwa ni mfano wa imani iletayo ushindi .Daudi alifuata kabisa mpango wa Mungu wake naye adui akapigwa kutokea Geba mpaka Gaza .Umaarufu wa Daudi ukaenea pote na “ BWANA akatia hofu yake juu ya mataifa yote” (1 Mambo Nyakati 14: 17 ) .Hapa,kuna  fundisho .Je,huwa tunafuata kila wakati mpango ambao Neno la Mungu unaelekeza wakati matatizo yanapotukabili , au  tunayafanya yale tunayoyaona ni mema machoni petu ? Tusiziitegemee akili zetu wenyewe lakini hasa tumtambue Mungu katika njia zetu zote Naye ataelekeza hatua zetu (tazama mithali 3:5,6).

DAUDI ANAPANUA MIPAKA YA ISRAELI: 2 Samweli 8.

Akiwa sasa na Sanduku la Agano lililokuwa Yerusalemu naye Daudi alikuwa ameimarika kama mfalme juu ya Isaeli Mungu akampatia ahadi ile nzuri sana ajabu iliyoandikwa katika 2 Samweli 7: 12- 16 ahadi ya mzao atakayetawala katika kiti chake cha enzi milele .Na mzao yule tumemuona katika  masomo yetu yaliyotangulia kwamba ndiye Bwana Yesu Kristo .Daudi sasa akayaelekeza mawazo yake katika kupanua mipaka ya Israeli na akawashangaza kwa kuwashinda adui zake  pande zote.Na hili lilifanyika katika mapigano maalumu saba .

(1). Akawapiga Wafilisti (2 Samweli 8:1). Tishio la wafilisti lilikuwa halijaondolewa kabisa, nao wakajikusanya kumkabili tena Daudi ,Wakati huu walishughulikiwa kikamilifu walipigwa kabisa na “Gathi na miji yake yote” ilitekwa na watu hawakuutishia tena utawala wa Daudi.
                                                              

(2) Akawapiga Wamoabu (2 Samweli 8:2).Wamoabu yaeleka walimpa sababu Daudi kuwashambulia, nao walitendewa kwa ukali sana , theluthi yao wakauawa na waliobakia wakaachwa (2 Samweli.8: 2 R.S.V ).Na ikawa vitisho kutoka upande wa kusini mashariki vikakoma kabisa.

(3) Akampiga Mfalme wa  Soba  (2 Samweli.8:3-4). Soba ilikuwa kaskazini  mwa Dameski kwenye  miinuko ya kaskazini  mashariki ya safu za  milima lebanoni. Wakati Daudi  aliendelea kaskazini kulejesha mamlaka  yake kwenye mto Frati (2sam.8:3,R.S.V.) alikabiliwa na Hadadezeri, mfalme wa Zoba, aliyekuwa na jeshi kubwa la magari ya farasi na wapanda farasi. Mungu alijibu sala za Daudi nao walipigwa.

(4)  Akawapiga Syria (2 Samweli.8:5,6). Kuna ngazi ya pili katika juhudi hii ya kaskazini. Ushindi wa Daudi ulianzisha vitu viwili kutokea. Kwanza kabisa Wasyria wagomvi kutoka Dameski, upande wa kusini wakaja mbele kumsaidia hadadeza.Lakini (askari) 22,000 walipigwa na Dameski ukazingirwa na kuwekewa ulinzi (ngome).”yahwe alimlinda Daudi kila alipokwenda?(mstari.6).

Kwa upande mwingine Toi, Mfalme wa Hamathi, kaskazini mwa Soba akapeleka ujumbe kumpongeza Daudi.Vyombo vya dhahabu, fedha na shaba nyeupe vililetwa  naye  Daudi akavitoa kwa yahwe, aliye chimbuko la ushindi wake (2Samweli.8:9-12). Hivyo mpaka  wa kaskazini  ulidhibitiwa (ulirejeshwa).

(5) Akawapiga Edomi (2 Samweli.8:13,14). Katika Mstari wa 13, “Wasyria”inapaswa kuwa  “Waedomu” Umaarufu wa Daudi ulisambaa mbali. Abishai  na Yoabu waliamlishwa kuingia  mji wenye  nguvu wa edomu  na kumwangusha adui huyu wa asili wa Israeli (Mambo ya Nyakati18:12, 1 Wafalme 11:15).

Yoabu alibakia kule miezi sita na kuwauwa 12,000 wakiwemo” kila mwanaume katika edomu”.hivyo ndivyo Daudi alivyookolewa kutokana na hawa maadui  wakali kwa upande wa kusini.

(6) Dhidi ya Waamoni (2 Samweli.10:1-14). Daudi akaendelea kuupanga vyema utawala wake,akiupanua uwezo wake “kwa hukumu na haki” (2 Samweli.8:15). Nahashi, mfalme wa waamori, akafa na mwanawe haruni, akatawala badala yake. Daudi akampelekea ishara ya kumpa pole, walakini, ajabu huyu mkuu  wa waamori  alitia shaka juu ya ukweli wake.Walidhani  wajumbe  wa Daudi walikuja  kuupeleleza  mji wao hivyo wakawatanda kwa kuwaaibisha. Hivyo haikuwa njia ya kujibu huruma,hasa kutokana na jirani  mwenye nguvu. Waamori walisikia juu ya hasira (kali) ya Daudi na huku wakiogopa malipo (au kisasi)

Waliomba msaada kutoka kwa waasiria wa Beth-Rehobu na Zoba na kutoka kwa mfalme wa maaka, na wanaume wa Tobu. Hivyo (jeshi la kaskazini) 33,000 kw jumla wakaja kuwasaidia. Yoabu akavigawa  vikosi vyake na kuwashambulia Shamu waliokuwa nyuma ya Israeli. Wakakimbia na hili liliwaogofya Waamori, nao wakakimbia mbele ya Abishai hadi (kuingia) Ralba,uliokuwa mji wao mkuu.

(7) Akawapiga Washami (2 Samweli 10:15-19;11:1,12:26-31). Washami walijikusanya pamoja na wengine ng’ambo ya Eufrate na kuwapinga Israeli. Habari hizi zilipomfikia Daudi, alivuka Yordani na kuelekea kaskazini na kuushinda muungano huko Helamu. Jemadari wao aliangamia na wafalme wote wakatafuta amani na kuwatumikia Israeli.

(8) Dhidi ya Amoni (2 Sam. 11:1; 12:26-31). Ingawaje Daudi alikuwa amepigana dhidi ya Waamoni  tahadhari yake aliielekeza kaskazini alipokuwaakipigana vita  na Wasyria .Na alipokwisha kuwashinda akamtuma Yoabu na jeshi kuelekea mashariki na akawangamiza Waamoni na akauteka  mji mkuu, Rabba .Mji huu baadaye  ulichukuliwa na Daudi .

USHINDI WA DAUDI  NI MFANO WAUSHINDI WA KRISTO

Kama vile Daudi alivyowaangusha adui zake na kupanua mipaka ya Israeli ,vivyo hivyo Kristo  naye ndivyo atakavyowatenda adui zake  wakati atakaporudi .Ataikomboa Israeli kutoka katika mikono na ya adui ake ,na kisha atapanua mipaka ya nchi .Katika kuanzisha ufalme wa Mungu,itakuwa ni lazima kwa mataifa yote kusalimu amri kabisa .Vile vile kama mataifa yalivyoinuka kupigana na Daudi ,hivyo hivyo mataifa yatainuka ili kupigana na Kristo (Zaburi 2: 1- 3) , lakini  hata hivyo yatashindwa na kutiishwa kabisa (Zaburi 2:8-9 ).

Wale walio waaminifu  na watiifu kwa Kristo watapata nafasi ya kusaidia katika kuanzisha ufalme wa Mungu duniani (Ufunuo 2: 26-27) . 

FUNDISHO KWETU:

Daudi alikuwa mtu aliyeupendeza Moyo wa Mungu ,Yeye kila wakati alitamani  Mungu ndiye awe chaguo la kwanza na kufanya kila kilchompendeza Mungu. Hata katika kulileta Sanduku  la BWANA,huko Yerusalemu nia yake ilikuwa sahihi ,lakini tunapata fundisho kutokana na kifo cha Uza kwamba yote yale tutendayo katika utumishi wa Mungu inatupasa tuyatende kwa kadri ya maelekezo ya Mungu. Baada ya tukio hili  la kutisha Daudi aligeukia kwenye Neno la Mungu ili kupata maagizo katika njia ambayo angetenda na hivyo sisi pia inatupasa kutenda kila wakati kwa kufuata maelekezo ya Neno la Mungu. Daudi aliendelea kumwomba kwa Mungu kwa ajili ya  mwongozo katika maamuzi ambayo ilibidi ayafanye naye akamsifu Mungu kwa baraka  na ushindi alioupata. Kwa kweli  Daudi ,BWANA, alikuwa yupo kila wakati  akisikiliza maombi yake na kumlinda kila alikokwenda.Na sisi pia tumweke Mungu kuwa chaguo letu la kwanza katika maisha yetu ili kwamba  tuweze kuzijua  njia zake na kumtii Mungu.                                                                                

REJEA KATIKA  MAKTABA            

“Historia ya Biblia”(H.P.  Mansfield)-Kitabu cha 4,Namba.1,2,3.

“ Mtu yule Daudi”(H.Tennat)-Ukurasa 6.

MASWALI YA MAFUNGU YA MISTARI:

1, Kwa nini  Daudi alifanikiwa katika vita yake dhidi ya adui za Israeli? 
2. Daudi alipopigana na Wafilisti mara ya pili ni maagizo gani maalumu Mungu aliyompatia? Je,ni fundisho gani lililopo katika hili?
3. Onyesha jinsi vita vya ushindi vya Daudi unavyotujulisha ushindi wa kristo.                                  

 MASWALI YA INSHA:

1. Daudi alitaka kuleta Sanduku la BWANA hadi Sayuni. Fafanua yale yaliyotokea na ni fundisho  gani tunalojifunza kutokana na kifo cha Uzza?

2.Nakili ramani ya “mipago ya vita vya Daudi” Katika ukurasa ufaao kuwekwa  ajili ya kuweka kwenye Biblia yao.               

 

Swahili Title
176 BWANA ANAANZISHA UFALME WA ISRAELI CHINI YA DAUDI
English files
Swahili file
Translator 1
Jonathan Nkombe
Literature type
Sub type
Sub sub type