CSSA 2-3-06 - THE GLORY OF SOLOMON'S REIGN — IT'S WEALTH AND FAME

Swahili

181. UTUKUFU WA ENZI YA SULEMANI – UTAJIRI WAKE NA UMAARUFU:

Kwa sababu Mungu aliipenda Israeli milele, kwa hiyo akakufanya wewe kuwa Mfalme”

 

1 Wafalme 7;9 19; 2 Mambo ya Nyakati 8 na 9.

 

SULEMANI MJENZI. 1Waf. 7:1-12; 1 Waf. 9:10-24

 

39. Ukiongezea ujenzi wa Hekalu tukufu la BWANA, (kama somo la 5 linavyoeleza), Sulemani alijijengea ikulu yake mwenyewe yenye kupendeza sana na akajenga nyumba nyumba kwa msitu wa Lebanoni. Akajenga miji “kwa ajiri ya magari yake ya vita na miji kwa ajili ya wapanda farasi wake” (mstari 19) na miji ya akiba. Alijenga pia jumba la kifalme kwa ajili ya binti Farao wa misri aliyekuwa mmoja wa wake zake (Sura 7:8; 9:24). Akatengeneza bustani za kifalme na bustani zilizokuwa na maziwa ya maji (au birika zamaji) ya muda, viunga vya mauwa na mashamba ya mizabibu (Mhubiri 2:4-6). Ukumbi wa Hukumu wa Sulemani ulikuwa mkubwa wenye kimo kirefu, kuta zake zikapabwa na mierezi, ambamo mlikuwemo kiti cha enzi kikubwa (kilichojengwa) kwa pembe za ndovu zilizofunikwa kwa dhahabu na kuzungukwa na simba. Humo Sulemani alitoa Hukumu (maamuzi) yake ya kifalme (1 Wafalme 7:11) ikielekezea utukufu wa Kriso jinsi utakavyokuwa mkubwa baadaye ambaye inasemekana kwamba atakuwa na “kiti cha enzi, kikubwa cheupe” cha hukumu (Ufunuo 20:11).

 

Ukumbi wa Hukumu unaelekeana na kuunganishwa na “Nyumba kubwa ya Mwitu wa Lebanoni” palikuwa na ukumbi wa nguzo ambamo (usaili au mazungumzo) ya biashara au sherehe za kitaifa zilifanyika. Safu ya nguzo kubwa sana za mraba za mwerezi zilisimamisha paa la “Nyumba kubwa ya Mwitu wa Lebanoni” (1 Wafalme 7:1-5). kwenye kuta zilizopambwa zilitungikwa nao 500 za dhahabu (1 Wafalme 10: 16, 17) zilitumika kwa ajili ya maandamano ya kifahali ya mfalme, tukio ambalo lilimpendeza sana Malkia wa Sheba alipofika. Hata vyombo vya kunywea na sahani, zilizowekwa ndani ya nyumba ziliongeza uzuri wa kupendaza wa nyumba hii, vilikuwa vya dhahabu au “dhahabu iliyosafika”. Lakini kwa upande wa madini ya fedha “fedha haikuhesabiwa kuwa kitu katika siku ya Sulemani (mstari 21). Utukufu mkuu zaidi utaonekana katika uzuri wa majengo ya kifalme wakati (tazama Isaya 60: 11, 13, 17).

 

SULEMANI ANAFANYA BIASHARA – 1 Wafalme 10: 21-29.

Sulemani alitawala misafara ya kaskazini – kusini, na kwa msaada wa (Shamu) Wafoinike akajenga jeshi la meli zilizokuwa Ezioni - geberi kubeba shaba yake iliyoku imesafishwa na biashara nyinginezo. Meli hizo zilifanya safari kuelekea kusini hadi Ethiopia, Yemeni, Uarabuni na India mara moja kila baada ya miaka mitatu, zikareta dhahabu, fedha, pembe za tembo, sokwe na Tausi (1 Wafalme 9:26.10: 22). Umakini wake katika biashara unaonekana pale ambapo ndiye aliyekuwa wakala (muwakilishi) ambaye kwa kupitia kwake Wahiti na Waaramu walipaswa kufanya mapatano ili kununua farasi kutoka Kilikia au magari ya vita kutoka Misri (1 Wafalme 10: 28, 29). Hizi na shughuli nyingine zilifanya fedha kuwa kama mawe na mierezi kuwa kama mikuyu katika mji wa Yeruslemu. Kila mwaka talanta za dhahabu 666 (ikiwa sawa na zaidi ya tani 3) zilitiririka kuingia katika hazina ya Sulemani (1 Wafalme 10: 14).

 

MALKIA WA SHEBA ANAMTEMBELEA SULEMANI – 1 Wafalme 10: 1-13; 2 Mamboya Nyakati 9:1-12

Sifa ya umaarufu wa Sulemani zilienea katika dola zote za dunia, na kwa upande wa Sheba ilipelekwa habari kwa Malkia juu ya mfalme mwenye hekima atawalaye katika Israeli. Kwa kadiri habari za kina kuhusu utukufu wa ufalme wake zilivyomfikia Malkia ndiyo alivyotamani kuutembelea ufalme ili kujionea yeye mwenyewe ufalme wa Israeli na kuzungumnza na Mfalme Sulemani. Sheba ni eneo la nchi ambalo lipo upande wa kusini, mashariki wa ghuba ya Uarabu, sehemu ambayo ilisifika kwa ajili ya manukato. Wanahistoria, wataalamu wa mambo ya kale wanatueleza kwamba ulikuwa ufalme tajiri sana uliokuwa na majengo makubwa na yenye kutukuka.

Malkia wa shaba aliamua kumwuliza Sulemani maswali mengi ya fumbo ili kumjaribu na kuona iwapo alichokuwa amekisikia ni cha kweli. Naye kwa mshangao akaona kuwa Sulemani alijibu maswali yake yote (1 Wafalme10: 1 -3). Malkia siyo kuwa alizungumza na Sulemani tu, bali aliliona Hekalu, akaiona nyumba ya Sulemani, akawaona watu waliomtumikia, naye pi akaiona hekima ya serikali ya Sulemani mfalme wa Israeli na kila kitu kilitendeka kwa ubora wa hali ya juu. Roho yake ikazimia kwa hayo yote aliyoyaona (mstari 5). Baada ya vyote hivi alimwambia Sulemani kwamba hakuwa amesikia hata nusu ya utukufu wa Ufalme wote. Akaendelea kusema, “Heri watu wako, na heri watumishi hawa wako, wasimamao mbele yako siku zote, wakisikia hekima yako. Na ahimidiwe BWANA, Mungu wako, alipendezwa nawe, ili akuweke juu ya kiti cha enzi cha Israeli: kwa kuwa BWANA aliwapenda Israeli milele, kwa hiyo amekufanya kuwa mfalme, uhukumu kwa haki” (mstari. 8-9).

Malkia wa Sheba akampatia Sulemani zawadi nyingi za thamani sana za dhahabu, vito vya thamani na manukato, na Malkia akarudi katika nchi yake.

 

ALIYE MKUU KULIKO SULEMANI - Luka 11: 31

Wakati Yesu alipozunguka na watu katika siku yake aliwakumbusha jinsi Malkia wa Sheba alivyokuja kusikia hekima ya Sulemani na akampatia BWANA utukufu kwa sababu ya yale aliyoyaona. Hivyo ndivyo Yesu, aliye mkuu kuliko Sulemani, alisema hekima ya Mungu, na watakuwepo watu wa Mataifa (Wapagani) watakaosikia na kumsikiliza Yesu. Pia kama Malkia wa Sheba alivyokuja na zawadi (nyingi kwa Sulemani, hivyo hivyo ndivyo Mataifa yatakavyofanya tena siku zinazokuja, wakati Yesu atakapouanzisha Ufalme wenye Mataifa watamletea zawadi zao (linganisha Zaburi 72: 10, Isaya 60: 9). Hivyo Sulemani na utawala wake inatujulisha ufalme wa mbele (au inatupatia picha kwa sehemu kidogo) juu ya Yesu Kristo na ufalme wake. Hili linaonyeshwa kwenye mlinganisho ufuatao:-

 

Sulemani

Bwana Yesu kristo

1.

Mwana wa Daudi

Ndiye aliyekuwa Yesu (Mathayo 1: 1)

2.

Alipokea hekima kwa Mungu

Ndivyo alivyofanya Yesu (Isa. 11: 1-3)

3.

Utawala wake ulikuwa wa amani

Ndivyo utakavyokuwa utawala wa Yesu (Zaburi 72: 7)

4.

Ufalme wake ulikuwa mtukufu

Hivyo ndivyo Ufalme ule wa Kristo utakavyo kuwa (Zekaria 6: 13)

5.

Mataifa mengi walimtumikia

Mataifa yote watamtumikia Kristo (Zab.72:11; Wafilipi 2: 9-11)

6.

Alijenga Hekalu

Yesu atajenga Hekalu huko Yerusalemu.


FUNDISHO KWETU:

Enzi za mafanikio na utukufu wa Israeli ilikuwa kwa sehemu kutokana na kukamilika kwa maandalizi makini ya Daudi na zaidi kutokana na baraka za BWANA katika kulikubali ombi lisilo la ubinafsi la Sulemani la kupewa hekima na ufahamu. Chini ya mtawala mwnye nguvu lakini mwenye hekima ufalme ule mkubwa uliimarika. Ilikuwepo amani nyumbani na nje iliyozoeleka na watu wakawa wenye furaha na salama. Watu wa Mataifa walivutiwa sana kumwabudu BWAANA, yote haya ilikuwa ni kuthihilisha Ufalme mkuu zaidi, utakaoanzishwa na Mwana wa Mungu. Lakini utukufu huu ulidumu kwa muda mfupi. Sulemani alihaidiwa baraka za ajabu, lakini iwapo mfalme na watu walitamwacha BWANA na amri zake, Mungu angewaadhibu kwa ukali. Utajiri wa Sulemani, silaha na wanawake vilimletea hatari ya kuanguka. Sisi pia tumeahidiwa baraka za Baba iwapo tutautafuta kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake (Mathayo 6:24-34). Kama tukikwepa kunaswa na shughuli za maisha haya kwa unyenyekevu wa kumcha Mungu katika kila hali ya maisha ya kila siku, tunaweza kutegemea kushiriki kwa furaha kwenye Ufalme wake wa utukufu wa aliye mkuu kuliko Sulemani. Na kwa hiyo “sasa tu mkumbuke Muumba wetu siku za ujana wetu” na “tumche Mungu na kuzishika amri zake” (Mhubiri 12: 1, 13).

 

REJEA KWENYE MAKTABA:

Historia ya Biblia” (H.P. Mansfield ) – Kitabu cha. 4, No. 7-9.

Mkono wa Mungu unaoonekana” (R. Roberts) – sura 24.

Njia za kutosheleza” (R. Roberts) – sura 18.

Watafiti wa Biblia” – (G. Ernest Wright) – sura 8.

Rafiki wa Biblia” – Appendix 68.

 

MASWALI YA FUNGU:

  1. Linganisha utukufu wa enzi ya utawala wa Sulemani na ule utukufu utakaokuwa wa Enzi ya utawala wa Kristo.

  2. Ni nani aliyemtembelea Sulemani - na alisema nini kuhusu Sulemani na ufalme wake?

  3. Ni kwa jinsi gani ufalme wa Sulemani ulivyokuwa ufalme bora na tajiri?

 

MASWALI YA INSHA:

1. Eleza safari ya Malkia wa Sheba kwa Sulemani.

2. Eleza utajiri na umaarufu wa enzi ya utawala Sulemani.

 

Swahili Title
181 UTUKUFU WA ENZI YA SULEMANI – UTAJIRI WAKE NA UMAARUFU
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type