CSSA 2-3-09 - ELIJAH THE PROPHET WARNS THE HOUSE OF AHAB

Swahili

184. NABII ELIYA ANAIONYA NYUMBA YA AHABU

"Hakutakuwa na umande wala mvua miaka hii, ila kwa neno langu"

 

Kutokana na kugawanyika kwa taifa katika makabila kumi na makabila mawili, makabila kumi ya kaskazini yalijukana kuwa ni ISRAELI na makabila mawili ya kusini yakajulikana kuwa ni YUDA. Muda wa miaka iliyofuata mgawanyiko huu wa taifa, Ufalme wa Israeli (makabila kumi ya kaskazini) ukafifia kiroho, na wafalme wake wakaenenda kutenda maovu na kuabudu sanamu. Ahabu ndiye aliyekuwa Mfalme aliyekuwa akiketi katika kiti cha enzi, wakati nabii Eliya alipotumwa kwao. Na kuhusu Ahabu imeandikwa kuwa "Akazidi kumghadhibisha BWANA, Mungu wa Israeli, kuliko wafalme wote wa Israeli waliomtangulia" (1 Wafalme 16:33). Alimwoa Yezebeli, bintiye Ethibaali, Mfalme wa Sidoni. Alikuwa mwanamke mwovu sana aliyeabudu sanamu ya Baali, tena akamshawishi mumewe kujenga madhabahu kwa ajili ya Israeli ili kuabudu mungu huyu wa Kipagani. Na kuhusu Ahabu na Yezebeli imeandikwa, "Lakini hapakuwa na mtu kama Ahabu aliyejiuza atende maovu machoni pa BWANA, ambaye Yezebeli mkewe alimchochea" (1 Wafalme 21:25). Hivyo kuwepo kwa viongozi wa aina hiyo wenye kuhamasisha ibada ya sanamu na kutenda uovu, watu wa Israeli walikuwa katika ukengeufu na hali ya kutotii wakati BWANA alipomtuma kwao mtumishi wake Eliya.

 

1 Wafalme 17 na 18.

 

KUTOKEA GHAFLA KWA ELIYA 1 Wafalme 17:1

Ghafla na kwa nguvu mtu mgeni na mwenye kuvalia nguo za rangi alitokea katika baraza la Ahabu. Alikuwa mtu aliyefunikwa na nywele nyingi, aliyevaa mshipi wa ngozi kiunoni mwake na shuka lililozungushwa mabegani mwake (linganisha 2 Wafalme 1: 8) - Eliya, Mtishbi, akasimama mbele ya Mfalme Ahabu na kutamka ujumbe wake wa kushangaza, "Kama BWANA, Mungu wa Israeli aishivyo ambaye ninasimama mbele zake hakutakuwa na umande wala mvua miaka hii, ila kwa neno langu (1 Wafalme 17:1). Na ikawa baada ya kutamka ujumbe huu akatoka mbele ya mfalme. Miaka mingi kabla, Mungu alikuwa ametabiri kuwa "angepeleka ukame kama aghabu juu ya Israeli kama wangemwacha na kugeukia miungu mingine" (Kumbukumbu la Tolati 11:16-17). Na kwa hiyo walikuwa wamejiletea aghabu hii ya kutisha kutokana na uovu wao wenyewe.

 

ELIYA KATIKA KIJITO CHA KERITHI1 Wafalme 17:2-7

Mungu akamwagiza Eliya kuvuka mto Yorodani na ajifiche katika kijito cha Kerithi. Ukame ulipokauka nchini, Ahabu alimtafuta kila mahali yule nabii aliyekuwa ametabiri kuwa ukame huu ungetokea. Wakati huu Eliya alitunzwa na maji ya kijito na kunguru walimletea mkate na nyama asubuhi na jioni. BWANA alikuwa amesema "Nami nimewaamuru kunguru kukulisha huko" (mstari 4). Kati ya njia nyingi za kukumbukwa ambazo Mungu angeweza kumpatia chakula, ikatokea kuwa kwa zoezi la adhabu ya kutegemea kunguru, ndege najisi kwa Eliya (Mambo ya Walawi 11:15). Kama vile kuonyesha nguvu juu ya vitu vyote alivyonavyo Mungu, hawa ndege wanaochukua uchafu ambao nyakati za njaa kwa kawaida hula chochote anachokipata, "wakabadilishwa" badala ya kuwa "wale wanaouchukua uchafu, na kuwa walishaji". Lakini kulikuwa na somo lingine la kujifunza.

 

ELIYA HUKO SAREPTA

Kama vile kunguru, ndege ambaye ni najisi (mchafu) ilikuwa ni mfano wa watu ambao ni Wapagani wasiooshwa kwa Neno la Mungu (Mambo ya Walawi 20:22-26). Lakini katika shauri kilicho "kichafu" kilikuwa "kimetakaswa" na kutumiwa kumlisha chakula nabii wa Mungu. Ndege ambaye ni safi au mnyama aliye safi angeweza kutumiwa, lakini halikuwa kusudi la Mungu kumtumia katika tukio hili. Eliya alikuwa akifundishwa kuwa wale waliokuwa kuwa wakifikiriwa kuwa "wasio safi" au najisi kwa Isaraeli wangeweza kutakaswa mioyo yao kwa njia ya imani. Eliya alikuwea anakaribia kuambiwa kwenda kwa mwanamke Mpagani mwenye imani, akiwa na ujumbe wa uzima. Mungu hakuwa mwenye kuwapendelea watu. Baada ya muda kijito cha Kerithi kilikauka kwa sababu ya ukame, na Mungu akamwambia Eliya "Ondoka, uende Sarepta ulio mji wa Sidoni, ukae huko. Tazama, nimwemwagiza mwanamke mjane wa huko akutunze" (mstari 9). Angalia jinsi mwanamke mjane anavyolinganishwa na kunguru (mstari 4).

 

Agizo hili la Mungu la kumtafuta mwanamke mjane katika mataifa aliyeishi katika wilaya moja ile ile aliyoishi Yezebeli bila shaka lilionekana ni jambo geni katika masikio ya Eliya (linganisha 1 Wafalme 16:31 na 1 Wafalme 17:9). Lakini huyu mwanamke Mpagani alidhihirisha imani ya kushangaza kwa Mungu wa Israeli. Alikuwa tayari amesha jiandaa kujiakana yeye mwenyewe na mwanaye na pia hata wasiutumie ule unga kidogo uliokuwa umebakia na kwa sababu ya imani hii yule nabii wa Mungu wa Israeli akaahidi kuwepo kwa chakula kisichoisha na mafuta yasiyoisha (mstari 11-15). Yeye Mpagani, alipona njaa wakati watu wengi katika Israeli walikufa kwa njaa kwani yeye alikuwa na imani ambayo Israeli waliikosa. Bila imani haiwezekani kumpendeza Mungu (linganisha Waebrania 11: 6, 35; 1 Wafalme 17:23).

 

ELIYA ANAONANA NA AHABU 1 Wafalme 18:1-20

 

Mungu akamwambia Eliya kwamba anaelekea kuumaliza ukame na kuleta mvua akamwambia Eliya aende kujidhihirisha kwa Ahabu. Ikawa Ahabu alipomwona Eliya alimshutumu yeye kwa kumwambia kuwa "Je, ni wewe! Ewe mtaabishaji wa Israeli?" (mstari 17). Lakini Eliya bila woga wowote alimjibu; "si mimi niliye wataabisha Israeli; bali ni wewe, na nyumba ya baba yako, kwa kuwa umeziacha amri za BWANA; nawe umewafuata mabaali" (mstari 18). Kisha Eliya akaamrisha kwamba Israeli wakusanyike pamoja waende hadi mlima wa Karmeli na manabii 450 wa baali na wale manabii 400 wa Ashera.

 

MASHINDANO KATIKA MLIMA KARMELI:HAPANA TENA KUSITASITA KATIKA NIA MBILI

- 1 Wafalme 18:21-40.

 

Pamoja na Israeli wote na kundi kubwa la manabii wa uongo mbele yake, yule nabii shujaa akatoa changamoto akasema "Mtasitasita katika mawazo mawili hata lini? BWANA akiwa ndiye, Mungu, mfuateni; bali ikiwa Baali ni Mungu, haya! mfuateni yeye" (mstari 21). Watu wote wakawa kimya. Eliya akatamka kwamba yeye, akiwa mwakilishi pekee wa BWANA, alikuwa akishindana na manabii mia nne na hamsini wa Baali. Akaweka mtihani mdogo tu kama kipimo ili ufumbuzi wa tatizo upatikane. Watu wote wakakubali. Manabii wa Baali iliwapasa kutayarisha dume la ng'ombe na kumlaza juu ya kuni kwenye madhabahu yao na wasiweke moto chini yake. Na kisha ilikuwa waite miungu yao ili ishushe moto na kuoiteketeza dhabihu ile. Na Eliya naye angefanya vile vile, naye Mungu yule ambaye angejibu ndiye angekuwa Mungu wa kweli. Lakini, manabii wa Baari waliita tangu asubuhi hadi adhuhuri na hakuna jibu lililopatikana: "Ikawa, wakati wa adhuhuri Eliya akawafanyia dhihaka, akasema mwiteni kwa sauti kuu; maana ni mungu huyo; labda anazungumza, au anashughuli, au anasafiri au labda amelala, sharti aamshwe" (mstari 27). Wakazidi kupiga kelele - "Ee Baari, utusikie", nao wakajikatakata na visu, lakini ilipofika jioni hakukuwa na jibu. Kisha zamu ya Eliya ilifika, akaitengeneza madhabahu ya zamani ya BWANA, ambayo ilikuwa imevunjika. Akachukua mawe kumi na mbili yakiwakilisha makabila kumi na mbili na kuitengeneza madhabahu, kisha akaweka ng`ombe dume juu ya kuni zilizokuwa juu ya madhabahu. Akachimba mfereji kuzunguka madhabahu na kumwaga mapipia kumi na mbili ya dhabihu na kuni, nao mfereji ukajaa maji. Ilikuwa ni wakati wa kutoa dhabihu jioni, saa ya kusali, Eliya akaliitia Jina la BWANA, na kusema, "Ee BWANA, Mungu wa Ibrahimu, na Isaka, na wa Israeli, na ijulikane leo ya kuwa wewe ndiwe Mungu katika Israeli" (mstari 36). Ilikuwa ni ghafla, tena pasipo hata kupewa neno la kuwatahadharisha, moto kutoka mbinguni ukashuka juu ya dhabihu na haukuteketeza kuni tu bali pia hata kuni na dhabihu na hata mawe, mavumbi na maji vilevile. Kwa hofu na mshangao mkuu; watu walianguka chini kifudifudi kwa ajili ya kudhihirika kwa ukuu wa nguvu za Mungu. "Na watu wote walipoona, wakaanguka kifudifudi; wakasema, BWANA ndiye Mungu; BWANA ndiye Mungu" (mstari 39). Wasingeweza tena kusitasita tena katika njia mbili; kwa kuwa tatizo lilikuwa limekwisha kutatuliwa. Eliya hakupoteza muda na kuamuru manabii 450 wa Baali wauawe penye kijito cha Kidroni. Na pia inatupasa kukubali kuwa hakika kuna MUNGU MMOJA TU NA IMANI MOJA: hatuwezi kuwatumikia mabwana wawili (Mathayo 6).

 

UKAME UNAKWISHA - 1 Wafalme 41-46.

Na kwa njia ya uthibitisho wa nabii kuwa BWANA peke ndiye Mungu wa kweli. Eliya akatangaza mwisho wa ukame. Akamwambia Ahabu kula na kunywa "kwani pana sauti ya mvua nyingi" (mstali 41). Eliya akapanda juu ya kilele cha mlima Kalmeli na kuomba kwa bidii kwa ajili ya mvua (linganisha Yakobo 5:17-18). Akamwambia mtushi wake aende na kumtazama kuelekea baharini kuangalia iwapo kulikuwa na dalili ya mvua. Anarudi na kumwambia, "hakuna kitu" (mst. 43). Mara sita Eliya aliomba na mara sita mtumishi hauwa ameona chochote cha kueleza. Lakini alipoakwenda mara ya saba, mtumishi akamwa mbia kuwa kuna wingu dogo, kama mkono wa mtu. Mungu alikuwa akijibu maombi ya Eliya. Punde si punde mawingu ya ngrumo yakakusanyika hadi "mbingu nyeusi kwa mawingu na upepo, ikanya mvua nyinngi" (mst. 45). Ahabu akakimbia mbio na gari la vita mpaka Yezerieli. Wakati uohuo Eliya kwa nguvu alizopewa na Mungu akalishinda gari, na kuwasili Yezeberi kabla ya mfalme.

Mapinduzi ayo Eliya aliyaleta hayakudumu kwa mda mrefu. Bado kazi ya Eliya haijakamilika. Ataendaelea tena na kazi yake baada ya kufufuliwa kutoka kaburini wakati wa kuj kwake yesu kristo. Kazi yake itakuwa kutayarisha mioyo ya watu wa Israel kwa ajili ya mfalme wao (Mathayo 4:5-6). Twaweza kuitazamia siku ambayo Mungu atawafanya watu wake "kuwa taifa moja katika hiyo juu ya milima ya Israeli; na mfalme wao atakuwa wao wote; wala hawatakuwa tena mataifa mawili, wala hawatagawanyika kuwa falme mbili tena, hata milele" (Ezekieli 37 :22).

 

FUNDISHO KWETU:

Na tuzingatie jinsi neno la BWANA lilivyo na nguvu katika midomo ya manabii - hata kuweza kufunga au kufungua mbingu; kuleta moto au mvua kutoka huko. Kama watu - wa Mataifa na siyo wana wa Israeli wa ukoo wa Ibrahimu, na sisi, ni sawa na yule mwanamke wa Sarepta, tunaokolewa kwa njia ya imani na utii. Hatutakiwi kusitasita katika njia mbili. Hatuwezi kutumikia mabwana wawili, na Mungu na kuipenda dunia. Kwa hakika Mungu anapenda tumpenda kwa moyo WETU wote kwa roho yake yote na kwa akili yako yote. Hii ndiyo amri iliyo kuu kuliko zote.

 

MAKTABA REJEA:

Historia ya Biblia (H.P Mansfield) - Kitabu cha 5, Namba 1.

"Mkono wa Mungu unaoonekana" (R.Roberts) - Sura 19.

"Eliya Mtishbi" (J. Martin) - Sura 1-6

 

MASWALI YA VIFUNGU

1. Ni sehemu gani Mungu alimwambia Eliya ajificha kwanza na ni jinsi gani Mungu alivyomtunza?

2. Ni kwa jinsi gani mwanamke wa Sarepta aliokoka?

3. Elezea dhabihu ya Eliya na na namna Mungu alivyoonyesha kuwa ameikubali?

4. Eliya alikwenda juu ya mlima Karmeli na kuomba mvua inyeshe-eleza nini kilitokea.

5. Kazi ya Eliya bado haijamalizika, ni lini atakapoianza tena na kazi yake itakuwa ipi?

 

MASWALI YA INSHA:

1. Eleza habari jinsi Mungu alivyomtunza Eliya; ni mafundisho gani tunayoweza kujifunza kutokana na hili?

2. Fafanua mashindano kati ya Eliya na manabii wa Baali, na ni mafundisho gani tunaweza kujifunza kutokana na hili?

 

Swahili Title
184 NABII ELIYA ANAIONYA NYUMBA YA AHABU
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type