193. WAYAHUDI WALIOKUWA UHAMISHONI
"Kado y mito ya Babeli , ndiko tulikoketi.Tukalia tulipoikumbuka tulipoikumbuka Sayuni" (Zaburi 37:1)
Alipokuwa akipigana na jeshi la Misri alishtushwa na habari aliyoipata kuhusu kifo cha baba yake, Nebukadreza haraka haraka alimweka mtoto wake Yehoyakimu chini ya amri awe anamlipa kodi, akateka vyombo vya nyumba ya BWANA, akachukua baadhi ya vyombo vya nyumba ya BWANA akavipeleka mpaka Babeli, akachukua mateka wachache kwenda nao hadi Babeli. Kijana Danieli, wa nyumba ya kifalme wa Yuda, alikuwa ni mmojawapo kati ya mateka waliopelekwa katika uhamisho wa kwanza. Alikuwa aungane na watu wengine wengi katika uhamisho ambao ulifuata kila baada ya miaka kadhaa, hadi kiti cha enzi cha Daudi kilipopinduliwa, na utumwa wa miaka 70 ukaanzisha mabadiliko na ulikuwa ni chanzo cha maadili kwa watu hao ambao walikuwa wamemwasi BWANA.
Danieli 1 na 3
UHAMISHO WA WAYAHUDI
Kupinduliwa kwa ufalme wa Yuda hakukamilika katika usiku wa manane. Orodha ifuatayo ni ya uhamisho wa miaka kadha wa kadha ili itusaidie kuwa kielelezo cha kurudiarudia mara nyingi kwa hatua za kupinduliwa kwa kiti cha enzi cha enzi cha Daudi (Ezekieli 21:27).
1. Katika mwaka wa nne wa Yehoyakimu (Danieli 1:1).
2. Miaka 6 baadaye -watu 3,023walitekwa nyara (Yeremia 52:28)
3. Mwaka uliofuata - watu 10,000 pamoja na Yehoyakimu (2 Wafalme 24: 12-16)
4. Miaka 10 baadaye- watu 832 (Yeremia 52:29)
5. Mwaka uliofuata baadaye - watu wengine wa ngazi za juu (wa ukoo wa kifalme) (2 Wafalme 25:11-12).
6. Miaka minne baadaye inapatana na mwaka wa 23 wa Nebukadreza-watu 745 walipelekwa katika uhamisho wa mwisho (Yeremia 52:30)
BABELI
Babeli ulikuwa "utukufu wa falme, uzuri wa kiburi cha Wakaldayo" (Isaya 13:19). Herodatasi anasema kwamba Babeli ulizungushiwa ukuta wa matofali ya kuchoma wenye upana mita 26:7 na kimo cha mita 107:7. Na juu ya kuta hizo kulikuwa na mistar miwili ya nyumba na barabara katikati yake. Mlango wa kuoingia ndani ya mji kulikuwa na milango 100 ya shaba. Mto Frati uliugawa mji katika sehmu mbili ambazo ziliunganishwa katikati na daraja lililokuwa na upana wa upana wa mita 9:2. Sehemu zilipatikana kila sehemu kwa maana ilikuwa ni sehemu ya maisha ya watu wa Babeli. Mahekalu yalikuwa ni mamia kwa jinsi yalivyokuwa mengi na madhabahu zilihudumia wageni waliokwenda kuhiji na kufanya biashara pia. Wakuu wa hekalu waliendesha sahughuli za hazina, maduka ya jumla, sehemu ya ununuzi, mabada ya kuhifadhi (bidhaa), mabenki na mashirika ya kutoa mikopo. Hayo ndiyo yaliyokuwa mazingira ya ibada sanamu yaliyowateka mateka wa Kiyahudi. Wengi wao waliomboleza kwa uchungu mkubwa kwa ajili ya nchi yao na nyumba ya Mungu (Hekalu). Walilia sana walipoikumbuka Sayuni (tazama Zaburi 137). Walipokuwa wakiangalia mateka Wayahudi zaidi walipofika na kudhalilishwa kwa viongozi wao, kwa mfano Sedekia, polepole walianza kuwa na toba kwa ajili ya maovu ya taifa lao na kukataa ibada ya sanamu za hao waliowateka. Walitiwa moyo na unabii maarufu wa Isaya (Isaya 13) na Yeremia (Sura 51) uliotabiri kuhusu kuangamizwa kwa Babeli, Ishara za Ezekieli, na imani na ujasiri wa Danieli na wenzake, iliwaimarisha watu waliokuwa wameadhibiwa kwa ajili ya huu utumwa walirejea kwa nguvu kwa ajili ya kumwabudu Mungu mmoja wa kweli. Wayahudi waliochukuliwa mateka waliishi katika jamii ndogo ndogo kila mahali katika nchi yote ya Babeli. Walitiwa moyo na Mungu aliyewaambia kujenga nyumba na kupanda bustani, kuoa na kuanzisha familia (Yeremia 29:4-7). Kwa sababu iliwapasa wakubali ukweli kuwa wangebaki utumwani kwa muda wa miaka 70. Ezekieli nabii aliishi nao na kujaribu kuwaonyesha kwa Neno na kwa ishara kwamba utumwa wao ungekuwa wa muda mrefu.
DANIELI: MKUU WA MANABII
Nabii mwingine aliyefanya mambo makubwa ya kuelimisha upya watu wa Mungu waliokuwa uhamishoni, alikuwa Danieli. Alikuwa ni wa ukoo wa kifalme na katika Danieli 10:11 anaelezwa kuwa "mtu apendwaye sana" na BWANA. Danieli alichukuliwa mateka pamoja na wengine wa ukoo wa kifalme.Aliishi zaidi ya ile miaka 70 ya utumwa (Danieli 1:21), na kwa hiyo kulitokea mabadiliko makubwa kutoka maisha ya uasi hadi kuwa taifa lenye kumcha Mungu waliporudi kutoka utumwani yalikuwa ni makubwa hii ni kutokana na ushahidi wa uaminifu wake Danieli na wengine ambao walionyesha kumcha Mungu katika nchi iliyojaa sanamu. Inafikiriwa kuwa Danieli alikuwa na umri kati ya miaka 17-18. Na katika Danieli 1:3 neno "watoto" ni "Yeledi", ikimaanisha "kijana". Hivyo katika miaka yake ya kubalehe, Danieli alionyesha imani kubwa katika ufahamu mambo ya Mungu. Jinsi ilivyo muhimu kwetu kumkumbuka muumba wetu katika siku zetu za ujana (Muhubiri 12:1)!
HEKIMA YA KIPAGANI YAHUKUMIWA - Danieli 1:1-4
Wakati Nebukadreza alipoivamia Yerusalemu alichukua vyombo katika Hekalu la BWANA na kuvipeleka katika Babeli na akaviweka katika hekalu la mungu wake. Kitendo hiki kilikuwa ni jaribio la kuonyesha ukuu wa mungu Beli kumzidi BWANA, Mungu wa Israeli. Danieli na rafiki zake watatu, Hanania, Mishaeli na Azaria waliewekwa chini ya uongozi wa Wakaldayo, ili wajifunze hekima yote na lugha ya Wakaldayo (mstari 40). Nebukadreza alikuwa akijaribu kulazimisha ili wayaamini mafundisho ya kipagani, ili aweze kuwaondoa kwenye Kweli. Hawa watumwa vijana walikuwa na majina yao yaliyompa heshima Mungu wa Israeli lakini Nebukadreza akayabadilisha majina yao ili kuheshimu miungu ya Babeli.
DANIELI ambaye jina lake linamaanisha "hukumu ya Mungu" alipewa jina la Belteshaza ambalo linamaanisha "mtunzaji wa hazina iliyofichika ya Beli"
HANANIA "BWANA amekuwa wa neema" lilibadilishwa kuwa Shedraki linamaanisha "uvuvio wa jua" jua likiwa ni mojawapo ya miungu ya Babeli.
MISHAELI "Nani kama Mungu" lilibadilishwa kuwa "Meshaki" aliye mali ya mungu mke shaka" na
AZARIA lenye maana ya "aliyesaidiwa na BWANA", likaabadilishwa na kuwa Abednego, likiwa na maana ya mtumishi wa moto uwakao au "mtumishi wa Nebo".
Kwa kubadili majina yao Nebukadreza alitaka wajiinamishe na kujihusisha na ibada ya Babeli, nao kama wangekubaliana na mafunzo haya, ndipo bangewapatia heshima. Hili ni onyo kwa watu wote vijana-ulimwengu daima unawavutia kuelekea kwenye njia zao za uovu-mwe imara na kupingana na majaribu, naye Mungu atawabariki (kama vile) alivyombariki Danieli na rafiki zake watatu.
DANIELI NA WENZAKE WATATU WANAKATAA CHAKULA NA DIVAI - Danieli 1:5-21
Danieli na rafiki zake waliagiziwa posho ya mfalme ya kila siku ya chakula na divai (mstari 5). Lakini Danieli alikusudia "moyoni mwake ya kwamba hatajitia unajisi" (mstari 8). Chakula na divai waliyopewa vilikuwa kwanza vinatolewa kwa sadaka kwa sanamu, naye Danieli aliazimia kuwa hatajihusisha kabisa na aina ile ya chakula na divai. Kula chakula cha aina ile ingeonyesha ya kuwa alikuwa ni mtu ambaye anaabudu sanamu na kwa hiyo "alikuwa ajiepushe na chochote kilichoonekana kuwa na dalili ya uovu" (linganisha na Matendo ya Mitume 15:29; na 1 Wakorintho 8:10; 10:28). Kwa hiyo Danieli akamwomba mkuu wa matowashi kuwa awapatie mtama wale na maji wanywe. Lakini yule msimamizi alisita kufanya hivyo kwa sababu alimwogopa mfalme. Hakupenda nyuso zao zionekane vibaya, ukilinganisha na nyuso za wenzao ambao walikula chakula mfalme. Lakini ikakubaliwa kuwa kwa siku wangekula mtama (mboga za majani, unga na matunda) na kunywa maji, na mwisho wa muda huo wangelinganishwa sura zao na wale wengine. Ndipo "hata mwisho wa zile siku kumi nyuso zao zilikuwa nzurio zaidi na miili yao ilikuwa imenenepa zaidi kuliko wale vijana wote waliokula chakula cha mfalme” (mstari 15). Kwa hiyo, vijana tunahakikishiwa kwamba "tukimtegemea BWANA katika njia zetu zote, atatuongoza na kutufanikisha njia zetu" (linganisha na Mithali 3:1-6). Mungu akambariki Danieli na rafiki zake watatu "na aliwapa maarifa na ujuzi katika elimu na hekima” (mstari 17).
IBADA YA KIPAGANI YAHUKUMIWA - Danieli 3
Baada ya ndoto ya Nebukadreza (ambayo tutajifunza habari zake kwa kina katika somo linalofuata) alijenga sanamu ya dhahabu na kuamrisha kwamba kila mmoja aibudu au la atahukumiwa adhabu ya kifo. Hili liliwafanya Shedraki, Meshaki na Abednego wawe katika hali ngumu. Rafiki hawa watatu wakafungwa, wakikubali amri ya mfalme kuhudhuria (linganisha 1 Petro 2:13-15) lakini walipoamrishwa kuiabudu ile sanamu, waliamua kumtii Mungu kuliko kumtii mwanadamu (Matendo ya Mitume 5:6-10). Walisimama waziwazi walipokataa kusujudu prostratembele ya sanamu iliyomtukuza mwanadamu. Walikuwa wakizitii dhamiri zao. Kuna nyakati pia ambapo na sisi inatupasa kusimama imara katika mambo yale tunayoyaamini, bila ya kujali matokeo ya chuki. Na tuimarishwe katika imani yetu kwa mfano huu mkubwa wa ujasiri wa kukabiliana na mateso. Dharau yao ilimjaza mfalme hasira kali. Hakuwa tayari kuvumilia utovu wa nidhamu wa kutokutii wa aina yoyote. Aliwaita mbele yake na kuwapatia nafasi moja ya mwisho na kama wasingekubali basi wangetupwa ndani ya tanuru iliyokuwa inawaka moto mkali, Mfalme akasema; "Naye ni nani Mungu yule atakaye waokoa ninyi na mikono yangu?" (mstari 15). Kwa utulivu wa ujasiri walimjibu mfalme " kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia anaweza kutuokoa kutoka kwenye tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme. Basi, kama si hivyo, ujue, Ee Mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako,wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu ambayo umeisimamisha" (mstari 17:18). Nebukadreza akajaa dhahabu mno na kuamarisha kuwa watie moto ile tanuru mara saba kuliko kawaida yake ya kutiwa moto. Kisha wakafungwa na kutupwa motoni, lakini wale waliowatupia ndani ndio waliokufa kwa moto. Lakini Nebukadreza alipochungulia ndani ya tanuru, alistaajabu. Akasema, "Je, hatukutupa watu watatu, hali wamefungwa, katikati ya moto? Tazama, naona watu wanne, nao wamefunguliwa" (mstari 24-25). Mungu alikuwa amempeleka malaika wake, ili kuwaokoa watumishi, na kwa kufanya hivyo akadhihirisha imani ya watumishi wake. Ndipo Shedraki, Meshaki, na Abednego wakaondoka kutoka ndani ya moto . Na watu wote wa Babeli wakashangaa kuona watu hao kwamba moto haukuwa na nguvu juu yao, wala nywele zao hazikuteketea, wala harufu ya moto haikuwapata hata kidogo 9 (mstari 27).
Katika njia ya ajabu yule malaika wa Mungu "alifanya kituo, akiwazunguka wamchao na kuwaokoa" (Zaburi 34:7).
Ndipo mfalme akakubali kwamba Mungu wa Israeli alikuwa ndiye alikuwa Mungu mwenye nguvu zote. Kwa hiyo, mfalme akaweka amri ya kwamba huyo Mungu wa Israeli ndiye anayestahili kuabudiwa "kwa kuwa hakuna Mungu mwingine anayeweza kuokoa namna hii" (mstari 29).
FUNDISHO KWETU
Ile miaka 70 ya utumwa iliwaadibisha na kuwanyenyekeza Wayahudi waliokuwa katika uhamisho. Walikuwa wamekwenda utumwani kwa kuwa walikuwa wakiabudu sana sanamu na walitegemea siraha za mwili na katika muda wao wa kuishi katika uhamisho walipitia mabadiliko makubwa muhimu. Walikuwa wamechukuliwa utumwani kwa faida yao wenyewe ili kwamba watakaporudi katika yao wawe thabiti katika imani. Walitiwa moyo na Yeremia, Ezekieli, na Danieli. Na sisi pia inatupasa tuishi kama wageni na wasafiri tukiwa na tumaini letu linalolenga huko Sayuni. Tunatiwa moyo na hawa watu wenye imani ili tuendelee kujitenga na mambo yanayotuzunguka, yasiyompendeza Mungu na kutazamia kurudi kwa Bwana Yesu Kristo ambaye anakuja kuhukumu dunia kwa haki na kuwapatia watakatifu waaminifu waliobakia thawabu.
MAKTABA YA REJEA
"Historia ya Biblia" - Kitabu cha 6 Namba 9-11
MASWALI YA FUNGU
1. Ni jinsi gani Nebukadreza alivyowalizamisha Danieli na rafiki zake watatu imani zake za kipagani?
2. Ni kwa nini Danieli na rafiki zake watatu hawakukubali kula na kunywa divai ya mfalme?
3. Onyesha namana rafiki zake watatu wa Danieli walivyomtii Mungu kuliko kuliko mwanadamu.
MASWALI YA INSHA
1. Fafanua jinsi Danieli na rafiki zake watatu kwa nini walikataa kula chakula cha mfalme na mafundisho tunayojifunza kutokana na habari hii?
2. Eleza ni kwa nini rafiki wa Danieli walitupwa katika tanuru la moto mkali na ueleze namna na ni kwa nini waliokoka