CSSA 2-3-20 - BELSHAZZAR'S FEAST — DANIEL IN THE LION'S DEN

Swahili

195. SHEREHE YA BELSHAZA - DANIELI KATIKA SHIMO LA SIMBA

"Mungu wangu amewatuma malaika, naye ameyafunga makanwa ya simba"

 

Baada ya kifo cha Nebukadreza ambaye enzi yake ilidumu kwa muda wa miaka 43, orodha ya wafalme waliotawala, lakini walitawala kwa muda mfupi tu. Ndipo Belshaza mjukuu wa Nebukadreza akawa mfalme ambaye alitawala badala ya baba yake, Nabonida. Wakati huo Danieli alikuwa bado ana cheo chake kikubwa. Kulikuwa na shauku kubwa kati ya Wayahudi waliokuwa utumwani pale Babeli; wale waliokuwa wakifuatilia ishara za nyakati, walikuwa wamesikia kuwa mfalme mpya alikuwa amechukua madaraka huko Uajemi-jina lake alikuwa ni Koreshi. Kama miaka ipatayo 200 hivi kabla, Isaya nabii ametabiri ya kuwa hilo ndilo lingekuwa jina la mfalme ambaye angeipindua Babeli. Nabonida alikuwa nje ya Babeli akikusanya jeshi ili kumshambulia Koreshi, naye Belshaza alibaki Babeli akingojea kurudi kwa baba yake.

 

Danieli 5 na 6

 

SHEREHE YA BELSHAZA - Danieli 5:1-4

Belshaza alikuwa ni mtu mwenye hila; mwenye kiburi na mwenye kujitukuza; hakuliogopa jeshi la Koreshi ambaye alikuwa ameukaribia mji wa Babeli. Alikuwa na imani thabiti kuwa hakuna lenye nguvu la kuweza kuchukua mji huu mkubwa. Wakati baba yake alipokuwa akiliandaa jeshi ili kumshambulia Koreshi, Belshaza aliwafanyia karamu kubwa wakuu wake 1000. Wakati wa sherehe watu walikunywa divai nyingi mno bila kipimo na haikuchukua muda Belshaza akawa uchi. Belshaza hakulijali jeshi lililokuwa linakuja na katika hali yake ya kulewa akaagiza kwamba "wavilete vile vyombo vya dhahabu, na vya fedha ambavyo baba yake, Nebukadreza (babu yake-angalia pembezoni) alivitoa katika hekalu lililokuwako Yerusalemu; ili kwamba mfalme, na wakuu wake, na masuria wake wapate kuvinywea, wakanywa divai wakaisifu miungu ya dhahabu, ya fedha, na shaba, na ya chuma, na mbao, na ya mawe " (mstari 3-4). Hilo lilikuwa kosa la kifo. Kwa kuvitumia vyombo hivi ambavyo vilitoka Hekaluni, Belshaza alikuwa akimdhihaki Mungu, lakini Mungu huwa hadhihakiwi. Vile vyombo ndivyo ambavyo vilionyesha "mtakatifu kwa BWANA" vilifanyika kana kwamba ni vitu vya kawaida vya kuchezewa na mfalme mpagani mwenye kujivuna na mpumbavu. Mpumbavu, pia kwa kuwa alikuwa amesahau hofu ya Mungu na utisho wa BWANA alioonyeshwa Nebukadreza katika tukio lililotangulia kabla (Danieli 2:47; 3:28,29; 4:34-37).

 

MAANDISHI UKUTANI - Danieli 5: 5-9

Wakati sherehe ikiendelea na vinywaji, ilipofikia kilele ghfla mfalme akahangaika sana kwa hofu kuu, sura yake ikabadilika, na "magoti yake yakagongana" (mstari 6). Huyu ambaye ni mtu wa mwilini kwa tukio hilo "akachanganyikiwa " kwa hofu kuu kabisa. Akaona maandishi ya vidole vya mkono wa binadamu yakiwa ukutani na hapakuwa na mkono au mwili ulioshikana na kiganja; kilikuwa ni kiganja tu peke yake. Kiganja hicho kilikuwa kimejaa maandiko yaliyokuwa ukutani. Ukimya mkubwa ulikijaza chumba cha sherehe. Baridi ya hofu ya kifo ikawa, "imeingia nyumba ya.

Ndipo Belshaza akawaita wanajimu wake, na Wakaldayo na wachawi na akasema, "Mtu awaye yote, atakayesoma maandiko haya, na kuniambia tafsiri yake, atavikwa mavazi ya zambarau na mkufu wa dhahabu shingoni mwake, naye atakuwa mtu watatu katika ufalme (mstari 7). Walijaribu kwa kadri walivyoweza, lakini wale watu wenye hekima hawakuweza kuyasoma maandiko yale kwa kuwa kile kiganja kilikuwa kimejaa yale maandiko. Hekima yao iligeuka upumbavu na "waaibishwe wote wanaoabudu sanamu; wajivunao kwa vitu visivyofaa" (Zaburi 97: 7).

 

DANIELI ANATAFSIRI MAANDIKO - Danieli 5: 10-29

Ndipo malkia akakumbuka msaada ambao Danieli alimpataia mfalme Nebukadreza kabla "Yupo mtu" akasema," mwenye maarifa na ufahamu, anaweza kutafsiri ndoto". Hivyo Danieli, mwenye umri wa miaka 80, akapelekwa mbele ya mfalme na akapewa ahadi ya utajiri ambao wenye hekima wa Babeli walikuwa wameahidiwa kama wangeweza kuyasoma yale maandiko na kuyatafsiri (mstari 16). Lakini Danieli kwa utulivu akamjibu mfalme huyu aliyefadhaika, "Zawadi zako zishike wewe mwenyewe, na thawabu zako mpe mtu mwingine; walakini nitamsomea mfalme maandiko haya, na kumjulisha tafsiri yake" (mstari 17). Kwanza Danieli, bila hofu, na kwa maneno ya kuchukia, akamkumbusha Belshaza kwamba alikuwa ni Mungu aliyempatia babu yake, Nebukadreza ufalme na ndiye Mungu mwenyewe aliyeuondoa ufalme kutoka kwake. Belshaza alikuwa amekataa kukubali hilo naye sasa alikuwa ameisifia miungu ya dhahabu na ya fedha akamdharau kabisa yule Mungu wa mbinguni. "Ndipo kile kiganja (kitanga) cha mkono kikaletwa kutoka mbele zake (mstari 24); kiganja kilitolewa ili maandishi yaweze kuonekana. Maandishi yaliyoandikwa yalikuwa ni haya: MENE, MENE, TEKELI UPHARSIN (PERESI). Danieli nabii akasema, na tafsiri ya maneno ndiyo hii: MENE- Mungu ameuhesabu ufalme wako na kuukomesha. TEKELI-Umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka. UPHARSIN au PERESI-Ufalme wako umegawanyika, nao wamepewa Wamedi na Waajemi.

 

"Ndipo Belshaza akatoa amri, nao wakamvika Danieli mavazi ya zambarau, wakatia na mkufu wa dhahabu shingoni mwake na kumfanya mtu wa tatu katika ufalme" (mstari 29). Usiku ule ule jeshi la Wamedi na Waajemi wakauteka na kuutwaa mji huo. Walikuwa wamegeuza kingo za mto uliokuwa unapita katikati ya mji na wakauingia mji kupitia katika kingo za mto huo zikiwa kavu. "Usiku huo huo Belshaza mfalme wa Wakaldayo akauawa" (mstari 30). Hata ikawa ukweli wa maneno ya Babu yake yakatimia katika tukio la kweli la kutisha: "Mfalme wa mbinguni, maana matendo yake yote ni kweli, na njia zake ni za adili; na wale waendao kwa kutakabari, yeye aweza kuwadhili" (Danieli 4:37).

 

KUPINDULIWA KWA BABELI NI MFANO WA MATUKIO YANAYOTENDEKA WAKATI HUU

Kupinduliwa kwa ufalme wa Babeli siku zilizopita inatumika kama mfano ambapo mataifa yatapinduliwa siku zijazo wakati Kristo atakaporudi kuanzisha ufalme wa Mungu hapa duniani (Soma Ufunuo 16:12-21). Kama vile ambavyo Belshaza alivyokataa kumtambua Mungu kuwa ndiye mkuu atawalaye vyote, ndivyo dunia ya leo isivyomtambua Mungu kuwa ndiye mwenye nguvu zote, dunia inayotuzunguka huabudu miungu yao ya dhahabu, na ya fedha, na matendo yao ni yenye kuzidharau njia za Mungu. Lakini kamwe Mungu hatayavumilia hayo kamwe, na kama vile Wamedi na Waajemi walivyoiangusha Babeli, ndivyo Mungu ataileta siku ya Amargedoni juu ya dunia ya sasa ambayop imeendelea kudumu katika maisha ya uasi na kuelemewa na ulevi. Watashtishwa na kurudi ghafla kama mwivi anavyokuja, dunia itatetemeka kwa ajili ya kurudi kwa Bwana Yesu Kristo ambaye ataleta hukumu za kutisha mbele yao, hasa wale waliojaribu kumdhihaki BWANA na kuleta aibu na kuliangamiza taifa la Israeli, watu wa Mungu.

 

DANIELI ANAPATA SIFA NA HESHIMA KWA DARIO - Danieli 6:1-5

Baada ya Babeli kutekwa, Koreshi alimweka Dario Mmedi kukatawa juu cha kiti cha enzi. Dario aliwateua wakuu 127 kutawala ufalme na juu ya wakuu hao kulikuwa na wakuu 3 - na miongoni mwa hawa wakuu 3, Danieli akapata heshima kuliko hao wote. Dario alimpenda sana Danieli "akapata sifa kubwa kuliko wakubwa na maliwali kwa kuwa roho bora ilikuwa ndanio yake; naye mfalme akaazimu kumweka juu ya ufalme wote" (mstari 3). Danieli akaheshimiwa sana na mfalme na kupendwa ajili ya uaminifu wake na utumishi wa moyo kwa watu na kwa Mungu wake. Hili lilifunua wivu wa wale wakumbwa wengine nao wakaazimia wamwondoe Danieli, kwa hiyo wakafikiria mpango wa hila wa kumwangamiza. Walijua kuwa Danieli alikuwa mwaminifu nao wakasema "hatutapata sababu ya kumshitaki Danieli huyo, tusipoipata katika mambo ya Mungu wake” (mstari 5).

 

AMRI YA KIPUMBAVU YA MFALME - Danieli 6:6-9

Wakaamua kuwa wataweza kumwondoa Danieli, kwa kuonekana kuwa analeta sabau kwa sababu ya yeye alimwabudu Mungu wa Israeli akisali kila siku kwa ajili ya kuomba "amani ya Yerusalemu". Wakamshauri mfalme kuweka amri ya kifalme kuwa mtu awaye yote asisali au kuomba kwa mungu yeyote kwa muda wa siku therathini, ila kwako, mfalme. Kama sheria hii ingevunjwa basi mtu aliyekosa kwa kutotii amrii angetupwa katika shimo la simba. Walimwambia mfalme kuwa wakubwa wote walikuwa wamekubaliana katika shauri hili, lakini walikuwa waongo kwa sababu Danieli hakukubaliana na amri hiyo. Basi, mfalme akakubaliana na wazo hilo naye akayatia sahihi maandiko ili iwe amri. Na sasa kwa vile sheria ilikuwa imetiwa sahihi, ilikuwa ni lazima itumike na isingeweza kubadilika.

 

MTU MWAMINIFU WA MAOMBI - Danieli 6:10-11

Wale wakubwa wenye hila walifahamu kwamba Danieli alisali mara tatu kila siku akimwomba Mungu wake. Asubuhi, mchana, na jioni alipiga magoti chumbani kwake akasali huku madirisha yaliyokuwa yakielekea upande wa Yerusalemu yakiwa yamefunguliwa. Danieli alifahamu kuwa amri ilikuwa tayari imetiwa saini kumkataza mtu yeyote kusali, lakini alidhamiria kwamba hakuna kitu chochote kitakacho mkataza kumwomba Mungu. Maisha yake yote alikuwa ni mtu mwenye tabia ya kusali, kwake lilikuwa zoezi lisiloweza kubadilika. Basi akapiga magoti mbele ya dirisha na kusali. Jinsi alivyokuwa mwenye imani na ujasiri. Alionyesha kwamba alikuwa tayari "kumtii Mungu kuliko wanadamu" (Matendo Mitume 5:29). Kama mtume Paulo, Danieli kwa dhamiri safi kabisa alikuwa ameishi mbele za Mungu hadi kufikia siku hiyo (Matendo ya Mitume 23:1). Hofu ya matokeo haikumbadilisha nia hata aweze kugeuka upande kwa kuacha kusali mbele za Mungu, ambaye alikuwa akimwambudu tangu alipokuwa kijana mdogo.

 

DANIELI ANATUPWA KATIKA TUNDU LA SIMBA - Danieli 6: 12-17

Wakubwa wale hawakupoteza muda kumfahamisha mfalme ili ajue kuwa Danieli alikuwa amevunja amri ile. Mfalme aliposika hilo "alihuzunika sana, na akakaza moyo wake ili kumponya Danieli", akajitaabisha hadi jua likachwa akijaribu kutafuta jinsi ya kumwokoa Danieli, lakini amri ilikuwa imekwisha kuwekwa saini isingeweza kubadilika. Alifahamu kuwa washaui wake walikuwa wamemdanganya ili kumwangamiza mtu mwenye haki. Kwa oyo mzito mfalme alifahamu kwamba Danieli ilimpasa kutupwa katika tundu la simba. Ndipo mfalme akamwambia Danieli, "Mungu wako unayemtumikia daima, yeye atakuponya". Ni maneno ya ajabu yaliyoje! Kwa maana alitambua kuwa BWANA angewerza kumwokoa pale ambapo yeye asipoweza kuokoa. Baada ya Danieli kutupwa katika tundu la simba, lile tundu lilifunikwa na kuwekewa kwenye jiwe.

 

IMANI ILIZUIA MAKANWA YA SIMBA - Danieli 6:18-23

Mfalme alihuzunishwa mno na mashitaka yaliyomhusu Danieli, hata hakupata usingizi, akakesha usiku kucha, akafunga. Alisukumwa kuhisi na kuamini yasiyowezekana! Hakuna mtu yeyote aliyewahi kutoka akiwa hai ndani ya tundu la simba, ni kwa nini Danieli aweze kupona? Lakini lakushangaza ni kwamba aliamini na akatumaini kumwona Danieli akiwa hai mara tu usiku utakapokwisha na jua litakapopambazuka juu ya mji. Simba walao watu hawakuwa na madhara kama vile vitoto vichanga vya paka chini ya ulinzi wa malaika wa BWANA (Zaburi 34: 6, 7). "Mfalme akaondoka asubuhi mapema, akaenda kwa haraka pale penye lile tundu la simba" (mstari 19). Alipofika pale tundu la simba akamlilia Danieli. “Je, Mungu wako unayemtumikia daima, amerweza kukuponya na simba hawa?" (mstari 20).

 

Ndipo Danieli akamjibu mfalme, "Mungu wangu amemtuma malaika wake, na ameyafumba makanwa ya simba, nao hawakunidhuru" (mstari 23). Fikiria ni furaha kubwa iliyoje na furaja aliyoipata mfalme. Mfalme "alifurahi sana" ndipo Danieli akatolewa katika lile tundu. Imani ambayo inatokana na kuamini ilimwokoa (Waebrania 11:33). Kisha mfalme akaamuru kuwa wale wakuu waliomshitaki Danieli, waletwe pamoja na watoto wao, na wake zao, wakawatupa katika tundu la simba na wale simba wakawashinda wakaivunja mifupa yao vipande vipande kabla hawajafika chini ya shimo.

 

DARIO ANAMTUKUZA MUNGU ALIYE HAI - Danieli 6:25-28

Dario alifurahi sana hata akaweka amri ya kwamba watu wote "watetemeke na kuogopa mbele za Mungu wa Danieli; maana yeye ndiye Mungu aliye hai, adumuye milele, na ufalme wake ni ufalme usioharibika, na mamlaka yake itadumu hata mwisho. Yeye huponya na kuokoa, hutenda ishara na maajabu mbinguni na duniani, ndiye aliyemponya Danieli na nguvu za simba" (mstari 26, 27). Je, mfalme alipata wapi haya maarifa ya bkumjua Mungu wa Israeli? Bila shaka ni kutoka kwa Danieli. Alikuwa ameshuhudia muujiza naye alikuwa amesadikishwa kuwa Mungu wa Danieli alikuwa Mungu aliye hai. Kristo atarudi upesi duniani na ataweka amri ili kwambna kila mtu duniani ni lazima amwabudu na kumtumikia Mungu aliye hai.

 

FUNDISHO KWETU

Belshaza alikuwa "amejikinai na mwenye kiburi (majivuno) na kwa makusudi alimdhihaki Mungu, lakini Danieli kwa imani na ujasiri alimwambia mfalme waziwazi. Danieli hakuwa na shida na zawadi zilizotolewa na mfalme ambaye alimkufuru Mungu wa Israeli waziwazi. Alikuwa kuwa kuangushwa kwa dola ya Babeli kulikuwa kumekaribia na kuwa zawadi zile hazikuwa na maana yoyote. Dunia kwa sasa inajaribu kutuvutia ili tufanye kinyume na ile Kweli, inatupasa tuziepuke kila aina ya raha na anasa ambazo ni za muda mfupi - lakini mambo haya ya dunia ni ya kitambo tu. Kristo anakuja, naye anakuja akiwa na thawabu za utajiri udumuo kwa ajili ya kuwapatia wale wote ambao waliendelea kuwa waaminifu. Je, ni kwa jinsi gani Dario alivyotofautiana na Belshaza! Dario alikuwa tayari kumsikiliza Danieli na alikuwa ni mwepesi wa kutambua kwamba Mungu wa Danieli alikuwa ndiye Mungu wa kweli.

 

Danieli kwa imani yake aliweza kuokoka katika kinywa cha simba, na ilikuwa ni kutokana na mfano wake mzuri ambao aliweeza kumhakikishia Dario kuhusu kuiamini Kweli. Mwenendo wetu mzuri, kama wa Danieli unaweza kufungua nafasi kwetu kuwaonyesha Injili watu wale wanaotuzunguka. Danieli alikuwa mtu wa maombi na bila kukosa alisali mara tatu kila siku. Mungu anapendezwa ikiwakwa mioyo yetu tunamgeukia, na kumwelekea kila siku, tukijua ukwelinkuhusu nguvu zake za kuokoa na kuitambua kuwa yeye ndiye Mungu mwenye hekima na uweza wote mbinguni na duniani.

 

MAKTABA REJEA

 

Historia ya Biblia” ( H.P. Mansfield) - Kitabu cha 6,Namba 11, 12.

 

MASWALI YA VIFUNGU

1. Ni kwa jinsi gani Belshaza alimdhihaki Mungu?

2. Belshaza aliona kitu gani kilichomfanya aogope na kutetemeka?

3. Ni kwa nini wakuu walimwonea wivu Danieli, na ni mpango gani walioufanya ili kumwondoa Danieli katika cheo chake?

4. Danieli alifanya nini aliposikia mpango wa wale wakuu, onyesha jinsi imani ilivyozuia makanwa ya simba wakati Danieli alipovunja amri ya mfalme?

 

MASWALI YA INSHA

 

1. Ni kitu gani kilichotoke wakati wa sherehe aliyoiandaa Belshaza? Je, habari hii inafundisho gani kwetu sisi leo?

2. Eleza kwa kina mpango wa hila kuhusu Danieli, na jinsi alivyoipokea ile amri ya mfalme na fundisho kwetu leo?

Swahili Title
195 SHEREHE YA BELSHAZA - DANIELI KATIKA SHIMO LA SIMBA
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type