CSSA 2-3-21 - RESTORATION UNDER CYRUS

Swahili

196. UJENZI MPYA CHINI YA KORESHI

"Weka uso wako kuangaza juu ya patakatifu pako"

 

Yuda walikuwa utumwani huko Babeli. Muda wote wa uhamisho, waaminifu waliamini kuhusu kurudi kwao kwa sababu ya unabii wa Ezekieli na Yeremia. Nabii Yeremia kwa uvuvio wa Mungu, alitabiri juu ya kuanguka kwa Babeli, na kurudi kwa wana wa Israeli katika nchi yao, baada ya kutimia kwa miaka sabini ya utumwa. Danieli mtu wa maombi, akiwa ameshuhudia kuanguka kwa Babeli, na akifahamu nini Neno la Mungu lilisema kuhusu kurudi kwa watu wa Mungu na kujenga upya baada ya kipindi hicho kuisha, alimwomba BWANA "weka uso wako kuangaza patakatifu pako palipo ukiwa" (Danieli 9: 2, 17). Wakati ulipofika mji wa Babeli ulitekwa na Wamedi na Waajemi. Amri nyingi zilitolewa baadaye za kuwaruhusu Israeli kurudi katika nchi yao nakulijenga upya Hekalu la Yerusalemu.

 

Ezra 1, 3, 5 na 6

 

AMRI YA KORESHI - Ezra 1:1-4; 2 Mambo ya Nyakati 36: 22-23

Miaka mia mbili kabla ya tukio nabii Isaya alikuwa amemtaja mtu mmoja, Koreshi kuwa mchungaji wa BWANA, mpakwa mafuta wake, atakaye washinda mataifa na kutenda mapenzi ya Mungu, "hata kuusema Yerusalemu, utajengwa, na kwa Hekalu msingi wako utajengwa" (Isaya 44: 28 - 45:4). Kama ilivyokuwa imetabiriwa katika unabii huu maaarufu, Koreshi (mfalme wa Uajemi) alikuwa katika mji wenye nguvu, Babeli na kuuteka. Korteshi alitawala kwa ushirikiano na Dario kwa muda wa miaka miwili. Wakati Dario alipokufa, Koreshi ndipo aliipotawala Babeli peke yake na mara moja akaanzisha sera kuhusu uvumilivu wa dini. Na akawapa ruhusa watu waliokuwa wametekwa na Babeli kurudi katika nchi zao, ikiwa walipenda kurudi. Alionyesha upendeleo maalumu kwa Wayahudi.

 

UJENZI MPYA UNAANZA - Ezra

Taharuki ikajaa katika mioyo ya watu wengi nao wakatiana moyo "kwenda kujenga nyumba ya BWANA, iliyo Yerusalemu" (Ezra 1:5). Kiasi cha watu 50,000 walirejea katika kurudi kwa kwanza kwa wahamiaji. Kuanza ujezi mpya wa Hekalu (Ezra 2: 64-65). Zerubabeli aliteuliwa kuwa mtawala na Yoshua kuwa kuhani Mkuu (Ezra 3:2) na ndipo ifuatayo ilipotimizwa "madhabahu ya Mungu wa Israeli ilijengwa na dhabihu husika zilitolewa” (1 Ezra 3:1-6) katika mwezi wa saba wa mwaka wa kwanza. Huu ulikuwa ndio mwezi wa sikukuu ya mahema, ambayo ilisherehekewa kwa ajili ya ukombozi wa kutoka Misri. Ni umaarufu mkubwa kiasi gani uliomo katika ukombozi wa ulio karibu kutokea ugenini huko Babeli wakati wakisherehekea sikukuu hii?

 

- Fedha zilitumika kupata vyombo na utumishi kwa ajili ya kuweka msingi wa Hekalu (Hesabu 3 :6-7).

- Kazi ya msingi ilianza katika mwezi wa pili wa mwaka wa pili (mstari 8-9)

 

Wakati misingi ya Hekalu ilipokuwa ikiwekwa, ibada maalumu ya shukurani ilifanyika, Yoshua kuhani mkuu akiwa amevaa mavazi matukufu ya cheo na makuhani na Walawi wakiwa pia wamevaa nguo zao, kwa pamoja na wanamziki na waimbaji waliimba nyimbo za kumsifu BWANA kupitia Zaburi tukufu za Danieli (Ezra 3:10). Vilima vinavyouzunguka Yerusalemu vilitoa mwangwi wa kelele za furaha zilizotoka kwa watu. Lakini wengi wa makuhani na walawi wa viongozi, ambao waliukumbuka utukufu wa Hekalu la Selemani kabla ya kuangamizwa miaka 70 iliyotangulia, walilia kwa nguvu kwa sababu Hekalu jipya halingeweza kulinganishwa na utukufu na uzuri wa lile la Selemani (mstari 12 -13). Na baadaye nabii Zekaria aliwakemea watu wale waliofanya ulinganisho wa namna ile "kudharau siku ya mambo madogo" (Zekaria 4:10). Watu ambao ni mabaki waaminifu watabarikiwa na Mungu, lakini mara nyingi huvunjwa moyo na kukata tamaa kwa ajili ya ufinyu wa maono ya watu wengine wengi.

 

KUSUMBULIWA NA WAPINZANI- KAZI INASITISHWA - Ezra 4

Watu wa mataifa katika nchi walitaka kusaidia kujenga Hekalu (Ezra 4: 2). "Hebu tujenge pamoja na ninyi, kwani tunamhitaji Mungu wenu, kama ninyi mnavyofanta...." Walakini ibada yao ilikuwa mchanganyiko wa kweli kidogo na upotofu mwingi, nao Yoshua na Zerubabeli walifahamu kuwa ikiwa watu hao watajumuishwa katika kazi ya ujenzi ni wazi kuwa ukweli ungedhalilishwa. Jibu lao lilikuwa, "Hamna shirika nasi, kujenga nyumba ya Mungu wetu, lakini sisi wenyewe kwa pamoja tutamjengea BWANA, Mungu wa Israeli, kama mfalme Koreshi wa Uajemi alivyotuagiza” (Ezra 4:3). Jibu hili lilisababisha tatizo na upinzani kwa ajili ya mpango wa ujenzi, na hatimaye kazi ikasimama. Hawa "wachochezi" waliwavunja watu moyona kujaribu kuwagawa; wakaandika hata barua za mashitaka kwa Ahusuero (mstari 6), mwana wa Koreshi, lakini hili lilishindwa kusimamisha kazi. Lakini, baadaye, barua nyingine wakati huo ilipelekwa kwa Artashashita (mstari 7) kuhani wa kipagani ambaye alikuwa amechukuliwa kiti cha enzi cha Uajemi. Kwa hiyo liliwekwa tamko kusitisha kazi ya ujenzi (Ezra 4:17-22). Maadui, baada ya kupata majibu, kwa furaha wakaharakisha kwenda sehemu ujenzi ulikokuwa ukifanyika na kuwalazimisha kusitisha kazi.

 

ONYO LA MANABII- KAZI INAANZA TENA - Ezra 5

Watu wakavunjika moyo, na muda si muda wakaregea kuhusu kazi ya hiyo ujenzi, wakajihusisha kazi za maslahi yao binafsi. Ilikuwa katika hali hii kufa moyo kwamba manabii, Hagai na Zekaria wakawasihi watu, waliokuwa wamejihusisha na mambo ya kuendeleza maslahi yao binafsi. Hivyo hivyo, sisi pia tunaweza kushindwa iwapo tunazama katika mali ambazo dunia inatupatia na kusema mioyoni mwetu "Bwana wangu anachelewa kuja" (Mathayo 24:48). Hagai aliwasihi kwa kuwaonya watu wazitafakari njia zao na kutangaza hasara ya kilimo chao kuwa yalikuwa ni matokeo yaliyosababishwa moja kwa moja na ulegevu wao kiroho. Lakini kama wangebadili njia, aliwahakikishia kwamba baraka zingekuja badala ya laana (Hagai 1:7-11; 2:15-19). Hivyo kwa njia maonyo ya nguvu ya manabii watu walisukumwa kuanza kufanya kazi. Licha ya uadui kwa upande wa Tatinai, mtawala wa Shetha-boznai kazi ya ujeni iliendlea, "Jicho la Mungu lao lilikuwa juu ya wazee wa Wayahudi, hivi kwamba hawakuweza kuwafanye waache kazi" (Ezra 5:5). Maadui waliuliza swali, "Ni nani amewaamrisha kujenga nyumba hii?" (mstari 9). Wayahudi wakajibu kuwa walifanya hivyo kwa amri ya Koreshi, nao wakaipuuza amri ya Artashasta ambayo iliwakataza kujenga. Tatinai, Shetha-boznai na washiriki wao, wakachukua hatua juu ya jambo na kumwandikia Dario wa pili, walijulisha kuwa kulikuwa na uasi katika jimbo la Wayahudi, na walitilia shaka kwamba Koreshi aliwahi kutoa amri kuhusu ujenzi, wakashauri kwamba Dario wa pili ahathibitishe jambo hili kama ni kweli (Ezra 5: 6-17).

 

KUMALIZA KUJENGA HEKALU - Ezra 6

Kwa neema yake Mungu kumbukumbu ya amri ile ilikuwa imehifadhiwa na Dario akaipata (Ezra 1:6). Akawajibu Tatiani na Shetha-boznai barua yao, akisema "iache kazi hii ya nyumba ya Mungu iendelee, mwacheni mtawala wa Wayahudi na wazee wa Wayahudi wajenge nyumba hii ya Mungu mahali pake... ya kwamba wasizuiwe. "Akatoa amri kwamba gharama zote kwa ajili ya Hekalu zitolewe kutoka kwa Wasamaria, kwamba watatoa dhabihu zao kila siku, na akatishia kuwaangamiza watu wt wote ambao watabadiri amri yake au kuliteketeza Hekalu!” (mstari 6-12). Tunaweza kufikiria jinsi walivyoshituka na wale Wasamaria waoga na namna sala zao zilivyo kuwa aibu tu walipofanya haraka kuanza kuwasaidia Wayahudi. Kazi ya kujenga upya Hekalu iliendelea na hatimaye ilimalizika baada ya miaka minne ya kazi ya kujenga (Ezra 4: 24) (linganisha 6:15). Kuna fundisho katika habari hii, Wayahudi walipodharau nyumba ya Mungu walipata matatizo, lakini walipoanza tena kazi na kushinda vikwazo waalibarikiwa kupita matarajio yao. Na ndivyo ilivyo kweli hata sasa, kwa maana BWANA hajabadilika. Tukimkaribia Mungu, atatukaribia sisi. "Anaweza kutenda makuu kupita yote tumwombayo" (Yakobo 4:8; Waefeso 3: 20).

 

HEKALU LA KIZAZI KIJACHO

Bwana Yesu Kristo hivi tarudi ulimwenguni kuanzisha ufalme wa Mungu. Makao makuu ya ufalme huu yatakuwa, lile Hekalu la ajabu lililo Yerusalemu. Uzuri wa utukufu wa Hekalu hili umeelezwa kwa kina katika kitabu cha Ezekieli sura ya 40-48. Hagai anauelezea utukufu wa Hekalu la Masihi akisema, "fedha ni yangu, nayo dhahabu ni yangu", asema, BWANA wa Majeshi, utukufu wa baadaye wa nyumba hii, utakuwa ni mkuu zaidi kuliko ule wa zamani" (Hagai 2:8-9 Biblia Toleo la Kiswahili Union Version). Katika Biblia vifungu kiasi kuhusu Hekalu hili kuonyesha kuwa itakuwa "nyumba ya sala kwa ajili ya mataifa yote" (Tazama Zekaria 14:16; Marko 11:17; Isaya 56:7; Isaya 2:1-5; Zaburi 122).

 

FUNDISHO KWA AJILI YETU

BWANA alimwambia Isaya miaka mia mbili kabla ya tukio kutokea ya kuwa Koreshi angefanya jambo lingesababisha Wayahudi kurudi Yerusalemu baada ya utumwa wa miaka sabini katika Babeli. Wakati ulipotimia Babeli ulitekwa na amri zilitolewa kuwaruhusu watumwa kurudi kwao. Kwa kweli "Akaaye juu sana anatawala falme za wanadamu, naye humpatia yeyote amtakaye... " (Danieli 4:17). Sisi, kama vijana kwa shauku sana tunamngoja Bwana Yesu Kristo, inatupasa kufikiria matukio ya kisiasa yanayo tokea duniani siku hizi ili kwamba tuweze kutambua "ishara za nyakati". Tunatakiwa tukumbuke kuwa Mungu ndiye anayeongeza hatima ya mataifa akilindaa tendo la mwisho ambalo lina ashiria wakati ule ambao ufalme wa Mungu utaanzishwa hapa duniani, wakati lile Hekalu tukufu litajengwa huko Yerusalemu. Siku ile msingi ulipowekwa wazee waliokumbuka lile Hekalu – adhimu - la Sulemani walilia walipolinganisha Hekalu hili jipya na lile la zamani. Nabii Zekaria aliwakemea wale waliofanya ulinganisho huu kwa maneno "yeye aliyedharau siku ya vitu vidogo" (Zekaria 4:10). Tunaweza kuangukia katika kosa la aina hiyohiyo ikiwa tunaipima kazi ya kweli kwa kutumia vipimo vya wanadamu. Lakini ikiwa tunatumia wakati wetu kwa kufanya kazi ya kujitolea huduma zetu kwa ajili ya Kristo, baraka za Baba wa mbinguni zitafurika; nasi hatutakuwa kama wale wazee, ambao "walidharu siku ya vitu vidogo".

 

Hekalu lililojengwa na chini ya uongozi wa Zerubabeli lilikuwa ni kiuli cha Hekalu lililo kuu na lenye utukufu zaidi, ambalo litajengwa na Kristo, muda mfupi ujao. Hata hivyo leo tunaweza kufanyika Hekalu (mahali Mungu anapokaa) tukitakasa miyo yetu kwa kuzishinda tamaa za mwili na katika maisha yetu kujenga zile tabia za maadili ya Mungu anayoyataka kwetu. "Ninyi ni hekalu la Mungu aliye hai" (1 Wakorintho 6:16).

 

MAKTABA YA REJEA

"Nabii wa makabila kumi yaliyopelekwa utumwani" (J.Carter)

"Historia ya Biblia" (H.P. Mansfield) - Kitabu cha 7, Namba 1,2

"Zitafakarini njia zenu" (H.P.Mansfield)

 

MASWALI YA VIFUNGU

1. (a) Mungu alimwambia nini nabii Isaya kuhusu Koreshi?

(b) Nikwa jinsi gani unabii huu ulitimia?

2. Eleza ni kwa nini kazi ya kujenga upya Hekalu ilisimamishwa?

3. Ni mambo gani makuu yaliyokuwemo katika barua ambayo Tatinai na wenzake walimwandikia Dario wa pili?

4. Kwa nini Yoshua na Zerubabeli walikataa kuwaruhusu Wasamari kuwasaidia kulijenga upya Hekalu?

 

MASWALI YA INSHA

1. Eleza kazi za Hagai na Zekaria katika kulijenga upya Hekalu, ni mfano gani tunaweza kupata kutokana na kazi yao?

2. Fafanua ni matukio yaliyotokea wakati wa ujenzi mpya wa Hekalu na ni kwa nini kazi ilisimamishwa?

 

Swahili Title
196 UJENZI MPYA CHINI YA KORESHI
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type