Ushirika - Somo 02

Swahili

Ushirika– Kanisa ni nini?

Somo la 2: Ushirika

Ushirika ni nini?

Kulingana na ufafanuzi wa kamusi Ushirika ni kwenye kilimo,au shirika lolote ambalo linamilikiwa na kuendeshwa na wana kikundi au wanachama wa shirika ambao wanagawana faida au masilahi. Na mwishowe ,Ushirika huwa unahusu maridhiano ya kusaidiana kwa kufanya kazi pamoja; ili kutimiza lengo lao.

Makundi mengi ya watu huwa wanaanzisha ushirika na kuna uwezekano hata wewe umewahi kujiunga na kikundi kimojawapo au viundi viwili vya namna hii. Na kama haujawahi kuwa mwanachama wa kikundi chochote basi nitashangaa.

Kanuni

Ninapokuwa mtu moja, uwezo wangu wa kununua unakuwa ni mdogo. Ninapo kwenda dukani, nikiuliza bei ya kununua mahindi ni dhahiri nitapewa bei. Uwezo wangu wa kumshawishi muuzaji ili anipunguziwe bei utakuwa mdogo. Kama muuzaji akisema kuwa bei ya gunia moja ni shilingi 20,000/=, ni hakika kuwa itabidi ni nunue gunia moja kwa shilingi 20,000/= . Na sitaweza kununua nusu ya gunia hata kama lengo langu ni kununua nusu ya gunia, maana muuzaji hatakubali kuligawa gunia. Nia yangu ya kununua nusu ya gunia au kununua robo ya gunia itanigharimu kulipa shilingi 20,000/

Hatua ya kwanza katika Ushirika, ni kutambua kuwa unapokuwa mtu mmoja itakupasa kwenda kwa huyu muuzaji mmoja kufuata bidhaa ya aina moja mara kwa mara; kwa miaka mingine. Kwa hiyo utakuwa na uwezo mdogo wa kumshawishi muuzaji. Hapo utaweza kufanya mkataba na muuzaji wa duka. “ Nitakuja dukani kwako mwaka huu mara nne , na muda huu nitahitaji ¼ ya gunia ya mahindi kila nitakapokuja dukani”. Tayari itakupasa kuweka akiba kiasi cha fedha shilingi 60,000/=kwa mwaka katika mfano wetu huu. Hiki siyo kuwa ni kiasi cha fedha kisicho kuwa cha muhimu!

Hatua ya pili katika Ushirika, ni kutambua kuwa unapokuwa mtu mmoja; unapaswa kuwa na familia wanaoishi nyumba moja pamoja na wewe. Unaweza kuwa unaishi pamoja na mke wako, unaweza kuwa unaishi pamoja na wazazi, na pia unaweza kuwa na watoto wako. Tufikirie kuwa, ni jumla ya watu 10 ambao unaishi nao nyumbani. Sasa, una nafasi ya kununua mzigo mkubwa wa kutosha kutoka kwa muuzaji. Badala ya kununua gunia moja la mahindi kwa mwaka, sasa unahitaji magunia 10 ya mahindi. Muuzaji wa duka ataona , manufaa ambayo wataipata kutoka kwenu ninyi kwenda kununua mahindi kwake kwa kuwa ninyi nyote mnaagiza mara moja ( ni tofauti kama watu wote 10 kila mmoja angeagiza peke yake. Muuzaji ataweza kukubali kupunguza bei ya kila gunia moja la mahindi. Tufikirie kuwa bei ya gunia moja ni shilingi 15,000/=. Kama familia sasa unaokoa kiasi cha shilingi 450,000/= kwa mwaka katika mfano wetu huu..Ni kiasi ambacho kinakuwezesha hata kununua nguo nzuri sana ya Kitenge cha gharama.

Kwa hiyo, fikiriakuwa fedha ambayo ingeokolewa unapoongeza kiasi cha hisa cha ushirika hadi kufikia idadi ya watu 100 au hata watu 1,000!

Wewe, na wanachama wengine wa ushirika pamoja na muuzaji wa duka mtanufaika wote. Wanachama watanufaika kwa kiasi cha bei kupungua , mazingira pia yatanufaika kwa kuwa uchafu utakuwa kidogo; na muuzaji wa duka atanufaika maana kwa ataweza kuwa na bidhaa ya kutosha . Na pande zote mbili watanufaika kwa njia ya masaidiano haya kwa kufanya kazi pamoja ili kutimiza malengo yao .


 

Ekklesia kama Ushirika

Utakuwa umeshatambua kuwa ekklesia (Ikklesia) ni kundi la watu ambao ni rahisi kuweza kuunda ushirika kama tulivyoeleza hapo juu. Wanaweza kununua bidhaa kwa wingi, na hatimaye wakagawana bidhaa hiyo kuulingana na idadi yao. Na baadhi ya makundi ya Kristadelphia huwa wanafanya jambo hili. Hili siyo jambo geni, Ikklesia (Ekklesia) ya karne ya kwanza walifanya hivyo mara nyingi; na hata Masinagogi ya Wayahudi ndivyo walivyofanya (kama tutakavyoona baadaye)

Hata hivyo, tunapotafakari suala la Ikklesia (Ekklesia) kama Ushirika, mafundisho hayaishii kwenye mambo ya faida ya fedha. Waumini wa Ekklesia wanafanya kazi pamoja wakiwa ni kundi wanaofanya kazi pamoja. Wakati tunapo batizwa tunafanya mkataba kwanza na Mungu: ndipo tunapo ahidi Mungu kuwa tutamfuata na kumtii. Na pili, tuna fanya mkataba na Ekklesia (Ikklesia) duniani kote :kwa kupeana mkono –wa kuume wa shirika. Lengo kubwa ni kwamba kila muamini aingie katika ufalme wa Mungu, kwa njia ya kumsaidia kila mmoja ili apitie katika mlango ule ambao ni mwembamba, na njia ambayo imesonga iendayo uzimani. (Mathayo 7:14).

Ushirika wetu na Mungu

Kuna mambo mengi sana ambayo Mungu anayahitaji kwetu, lakini hapa yapo baadhi katika mambo haya:-

  • Mungu anataka tuwemo katika Ufalme wake (Luka 12:32; Waefeso. 1:5; Wafilipi. 2:13; 2 Wathesalonike. 1:11).

  • Mungu anataka tudhihirishe tabia zake na za Mwanaye (Yohana17:3) - Na hii ndiyo sababu Mungu alijitayarisha kumwandaa Mwanaye wa pekee (Yohana 3:16).

  • Mungu anataka dunia yote ijae maarifa yake kuanzia mwisho wa dunia mpaka mwisho mwisho wa dunia (Hesabu 14:21). Na ndiyo sababu tunahubiri.

  • Mungu anataka tumtii (1 Samweli 15:22).

  • Mungu anataka tumwabudu yeye (Zaburi 96:9).

  • Mungu anataka tumwamini yeye (Waebrania 11:6).

Nia yetu ya kuwa ndugu wanaume na wanawake katika Kristo inatakiwa tuwe tunataka tuwe watu wenye tabia nzuri, tuweze kuwa hata zaidi ili tuwe kama Mungu,; na kudhihirisha tabia zile anazozipenda – watu wengi hawalielewi jambo hili, badala yake wanabatizwa kwa sababu kabisa ya tabia za kimwili:

  • kupata huduma za kijamii

  • kupata fedha

  • ili aweze kuwa mwimbaji wa kwaya

  • au kwa sababu wanapenda kuishi milele

Kama ni kwa ajili ya hizi motisha tunakosea, na kama tunajitambua kuwa tupo kwenye kundi hili basi tunatakiwa haraka sana tubadili nia zetu

Pande zote (Mungu na waamini) wanapata manufaa kutoka na makubaliano. Wakati tunapo batizwa ndipo tunapoingia kwenye agano (Warumi 6). Na sasa, pande zote mbili zinanufaika. Huu ndiyo ushirika wetu na Mungu; yaani mapatano yetu

Wakati wowote tunapotenda dhambi mojawapo, tunajiweka sisi wenyewe nje ya ushirika na Mungu. Na tunapojiweka sisi nje ya ushirika na Mungu., basi tunahitaji kuomba msamaha ; kwa sababu tumevunja mapatano yetu na Mungu wetu. Kwanza kabisa tunatakiwa tutubu (Mathayo 9:13; Marko 6:12; Matendo ya Mitume 2:38), na kisha tunaomba msamaha. Na ndiyo sababu tunatakiwa tuhudhurie ibada ya kushiriki Mkate na Divai kila juma. Toba yetu siyo tendo la mara moja tu, tukio la siku ya ubatizo, toba yetu ni jambo ambalo tunapaswa kufanywa kila wakati. Ubatizo haumanishi kuwa sasa tumeokoka . Biblia hutuelezea kuwa, sisi ni mawe yaliyo hai, tukiwa tumejengwa; tuwe hekalu la Mungu (1 Petro 2:4-5).

Ushirikiano katika Ikklesia

Ni hali inayofanana tunapofanya agano na Mungu tunapobatizwa, kwa hiyo tunafanya agano na ndugu zetu wanaume na wanawake wakati tunapo batizwa; tendo hili tunaliita: “Mkono –wa kuume wa shirika”. Ni jambo sahihi tunapolifanya katika Kristo maana ni kitendo kilichotenda katika Biblia siku zilizopita miaka mamia ya miaka iliyopita (Waebrania 6:2; Hesabu 6:24-26).

Katika kufanya tendo hili tuna waahidi ndugu zetu wanaume na wanawake kuwa tutawasaidia kwenye safari yao ya Ufalme, pia na wao wanaobatizwa wanatu ahidi kutusaidia sisi.

Kama vile tunavyo shindwa kutimiza kabisa ushirika wetu na Mungu, na ndivyo pia tunashindwa mara kwa mara kutimiza ushirika wetu na ndugu zetu wanaume na wanawake. Na ndio utaratibu unaotumika katika kutubu na kusamehewa kwetu na Mungu, ndio pia tunapaswa kutubu na kuwaomba msamaha ndugu zetu wanaume na wanawake (Mathayo 18:21-22).

Tunaposhiriki Mkate na Divai tunaambiwa kwanza tujihoji sisi wenyewe(1 Wakorintho 11:28). Kabla ya kushiriki ni wazo njema kuangalia ndani ya kusanyiko hilo, ili kujua kama kuna ndugu mwanamume au mwanamke ambaye “hauna ushirika” naye, basi usishiriki pamoja naye – maana mnapaswa kupatana kwanza (Mathayo 5:24).

Ushirika kama ilivyo kushirikiana kwa matendo

Ushirika ni jambo ambalo tunafanya kujihushisha nalo kwa ukamilifu. Ifuatayo ni orodha ya baadhi ya mifano ya mambo ambayo tunapaswa kuyatenda katika ushirika. Hii siyo orodha ya matendo yote , lakini inaelezea baadhi ya mifano ambayo tunakiwa tufahamu na tuwe tunayatenda

  • Kuhudhria mara kwa mara kwenye kusanyiko kama ilivyo desturi

  • Kushirikiana mawazo tuliyojifunzo wakati wa masomo ya kila siku ya Biblia

  • Kutunza na kuweka usafi mali za Ikklesia

  • Kuheshimiana

  • Kuhifadhi mali za Ikklesia ( siyo jengo pekee yake, bali kuhakikisha pia vitabu vyote mfano : Biblia , vitabu vya Nyimbo nk vinatunzwa vizuri)

  • kwenda kuwaona wagonjwa,walemavu na wazee

  • kuandaa masomo ya Biblia

  • Kufundisha vijana

  • Kazi za vijana

  • Kuhubiri Injili

  • Kuandaa vikao(mikutano) vya wazee pamoja na Ekklesia ambayo ni mwenyeji

  • kutayarisha chakula kwa ajili ya mikutano/vikao

  • kusafisha vyoo

  • Kuwashirikisha wengine masomo ya Gazeti la Kristadelphia

  • kuandika barua kwa ndungu waishio mbali na Ekklesia

  • kutumiana SMS / ujumbe /barua pepe / ujumbe wa WhatsApp

  • kuzungumza na ndugu walio katika upweke

  • kuombeana

  • kutembelea Ekklesia ambayo inayohitaji msaada wa mafundisho au Mahubiri

Ni dhahiri kuwa inaonesha kuwa kutokana na orodha ya mambo haya yaliyotajwa kila muamini wa Ekklesia(Ikklesia) ni wa thamani sana, na kazi zetu zote ni lazima zionekane kuwa ni mojawapo ya ushirika wetu wa kushirikiana sisi kwa sisi.

Na kuwa Ikklesia(Ekklesia) yetu huwa hawachangamani na watu wasio amini. Maana kuna Ikklesia moja ambayo duniani kote- ni moja. Hatuna Maikklesia/Maekklesia( kana kwamba ni nyingi) kwa kuwa duniani yapo makanisa mengi. Sisi ni Ikklesia moja .Tunapozungumzia Ikklesia za mahali au sehemu yanaweza kuwa makosa ya sarufi; lakini yanaambatana na imani yetu kuwa kuna Ikklesia(Ekklesia) moja.

Maisha katika Sinagogi

Neno la Kiebrania kuhusu sinagogi ni beit k'neset. “Maana yake nyumba ya mkutano” na kwa sababu hiyo maana yake inakaribiana sawa na neno la Kiyunani 'sinagogi' lenye maana ya “kusanyiko” .

Kwa karne nyingi, sinagogi hasa ilitumika zamani kuwa sehemu(kituo) cha kukusanyikia Wayahudi.

Wakati wa Utawala wa Rumi, sinagogi ilitumika kwa ajili ya dini,utamaduni na kituo cha jamii ya Wayahudi. Kwa hiyo miji mingi maarufu na zaidi ya mji mmoja: utafiti mmoja unakadiria kuwa katika Mji wa Yerusalemu ulikuwa na jumla ya sinagogi 365 wakati wa Paulo. Pamoa na ibada ya Sabato, sinagogi ilitumika kwa shughuli nyingi. Sinagogi yakumbukumbu ya mamboya kale inaweza kutupatia mshangao wa thamani au fahari ya “dunia”

  1. Shule ya Biblia. Masinagogi yalitumika kama shule za watoto, kwa ajili ya kusoma na kufafanua Maandiko Matakatifu wakati ibada ya maombi, na wakati masomo ya kila wakati kwa watu wazima

  2. Mahakama. Ndani ya sinagogi, zilitolewa adhabu kwa wakosaji wa sheria za Wayahudi.Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwa watawakamata na kuwaudhi; watawapeleka mbele ya masinagogi. Paulo alipigwa “ na Wayahudi” —ndani ya masinagogi— mara tano na kupigwa fimbo( mapigo) mara thelathini na tisa

  3. Ukumbi. Josephus, Myahudi mwana historia katika karne ya kwanza, anaeleza mkutano wa kisiasa uliofanyika ndani ya sinagogi huko Tiberia

 

  1. Hoteli. Sinagogi ilitumika kama hosteli pia, kulikuwa na vyumba kwa ajili ya Wayahudi waliokuwa wasafiri, wafanya biashara na masikini.

  2. Hazina. Fedha zilikusanywa ndani ya sinagogi kwa ajili ya kusaidia wenye shida na masikini zilitunzwa ndani ya sinagogi. Ndani ya sinagogi nje ya Palestina, fedha zilikusanywa kila mwaka kwa ajili ya kuchangia Hekalu la Yerusalemu.

Na kwa maana nyingine, kila kazi iliyo husu maisha ya Wayahudi yalifanyika katika sinagogi. Kwa hiyo hatutasitaajabishwa na Paulo kuchangua utaratibu huu alipoanza kazi ya umishenari. Kwanza, watu wasinge weza hasa kwenda kwenye sinagogi kwa ajili ya kusali au kujifunza Neno la Mungu.Walikuwa na vikao vya waumini ndani ya sinagogi, walianzisha misaada ya kusaidia jamii ya Wayahudi

Kubomolewa kwa Hekalu mwaka 70 BK, kulichochea zaidi matumizi ya sinagogi, kwa kuwa masinagogi yalihusika sana katika mambo yaliyohusu utamaduni na mambo ya kutunza na ufundishaji wa ibada zilizofanywa na Rabi yaani Walimu wa Wayahudi. Na muda wa ziada ikawa “nyumba ya sala” na mara nyingi yaani ilikuwa “ nyumba ya kujifunzia”, pia.

Katika kulinganisha hili, tulia ufikirie ni kwa kiasi gani majengo yetu ya Ikklesia yanatumika. Je, ni majengo yasiiyotumika? Wafrika hawatumii ovyo majengo, wala Wayahudi wa karne ya kwanza. Wala Wakristadelphia hawatumii majengo ovyo. Majengo yetu ( au masinagogi kama wengine wanavyopenda kusema) yasitumike ovyo, ni sehemu zetu muhimu ndani yake ushirika wetu hutendeka humo. Basi, tutumie mali zetu hizi vizuri katika kumtumikia Bwana. Na milango yake kila wakati iwe imefunguliwa, na tuweze kuwaonesha watu wengine kupitia ushirika wetu na kwa njia ya imani tumeungana pamoja, pia sisi ni familia moja, yaani wana na mabinti wa Mungu.

 

Swahili Title
Ushirika - Somo 02
African text
carl Hinton
Literature type
Sub type