1.1 Uwepo wa Mungu
“Mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kuwa yeye yupo na kwamba huwapa dhawabu wale wamtafutao” ( Ebr 11:6). Lengo la masomo haya ni kuwasaidia wale wanomwendea Mungu, wakiisha mwamini “Kwamba yupo”; kwa sababu hii hatutajitia kwenye ushahidi usiothibitisha imani ya kuwa Mungu hayuko.katika kupima muundo wa miili yetu (Zab 139:14) Ushahidi wa kielelezo katika ua, Kukazia macho juu kwenye anga pana wakati wa usiku kukiwa wazi bila mawingu, haya na mengine yasiyohesabika, Mawazo ya kangaliifu juu ya maisha, hakika yanafanya imani ya kutosadiki kuwa Mungu hayupo iwe ni ya kushangaza. Kusadiki kuwa Mungu hayuko hakika inahitajika imani zaidi kuliko kuamini yupo,pasipokuwepo Mungu mpangilio haupo, Kusudi au kutoa maelezo ya asili ya Ulimwenguni basi hii itafikiriwa katika maisha ya mtu asiyeamini kuwa Mungu yupo. Tukikumbuka hili, siyo ajabu kuwa watu wengi wanakiri kwa kiwango fulani cha kumwamini kuwa Mungu yupo hata katika jamii ambayo vitu vya mwili ni Mungu anayeshinda maisha ya watu.
Lakini ipo tofauti pana kati ya kuwa na fikra isiyodhahiri ya kwamba ipo nguvu ya juu, na hasa kweli kuwa na uhakika kwa kile ambacho Mungu anampa mtu anayemtumikia kwa Uaminifu. Waebrania 11:6 jambo hili tunasoma;
“Yatupasa tuamini kuwa (Mungu )yupo na Kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao kwa bidii”
Maelezo mengi ya biblia ni historia ya watu wa Mungu Israeli; mara kwa mara neno limetolewa kwamba kukubali kwao kuwa Mungu yupo hakukulingana na imani zao kwa ahadi zake.Waliambiwa na mkubwa kiongozi wao Musa'Kwa hiyo ujue…….Ukaweke moyoni mwako, ya kuwa BWANA ndiye Mungu katika mbingu juu, na katika nchi
chini, hapana mwingine. Basi, zishike sheria zake, na amri zake (Kum. 4:39:40).
Neno hili hili limetolewa - ufahamu wetu katikati yetu ya kuwa Mungu yupo hakumaanishi kwamba tunakubalika mbele za Mungu bila kufikiri.Ikiwa bila mchezo tunakubali kwamba kwa kweli tunaye Muumba,'Kwa sababu hiyo tuzishike sheria na amri zake’ Ni shabaha ya mfululizo huu wa masomo kuelezea amri hizi jinsi zilivyo na namna ya kuzishika. Tunapochungunza maandiko kwa kufanya hivi, tutakuta kwamba imani yetu kuwa Mungu yupo inatiwa nguvu.
‘Imani chanzo chake ni kusikia, na kusikia huja kwa neno la Mungu’ (Rum 10:17). Vile vile,(Isaya 43:9-12) yaonyesha namna ya kufahamu unabii wa Mungu kuhusu wakati ujao - Unabii unatufanya tujue'kuwa mimi ndiye’ (Isa. 43:13)- yaani hilo jina la Mungu, 'Mimi niko ambaye NIKO’ kwa ukamilifu ni kweli (Kut. 3:14.) Mtume Paulo alifika kwenye mji unaoitwa Beroya, eneo hili kwa sasa liko kaskazini mwa Uyunani ( Ugiriki) kama kawaida, akahubiri injili (Habari njema) ya Mungu; lakini badala ya watu kusikia neno la Paulo alilokuwa anasema, tunasoma kwamba, “ Walilipokea kwa kusikia neno (la Mungu, sio la Paulo) kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo. Basi watu wengi miongoni mwao wakaamini ( mdo 17:11,12)
Imani yao ilikuja kwa kuwa mioyo yao ilikuwa wazi, sawa sawa (‘ Kila siku’) na kwa utaratibu wa (‘mambo hayo’) waliyachunguza katika Biblia, Basi kupata imani ya kweli haikuwa Mungu aliwafanya wawe nayo ghafla kwa aina fulani ya upasuaji wa moyo wa kiroho, pasipo kujihusisha na neno la Mungu. Ni jinsi gani basi watu wa Ulimwengu wanaweza kufuata kwa moyo pigano juu ya maovu la Bill Graham au uamsho wa mikutano ya wapentekoste kisha wanahama tena kama'Waamini’ ? Ni muda gani wameendelea katika masuala haya wakiwa wanachunguza maandiko kila siku ? Kwa kweli kukosekana huku kwa imani ambayo msingi wake upo kwenye Biblia bila shaka kunaonyesha utupu wa'Waongofu’ hawa na kujikuta baadae kwa wanayopata Wakristo, na ni kwa sababu gani wengi wanaondoka kutoka kwenye Ushirika wa Madhehebu ya wa-Injilisti.
Masomo haya lengo lake ni kukupa mjengo wa utaratibu wako mwenyewe kuchunguza maandiko, ili kwamba nawe pia uweze basi kuamini muunganiko kati ya kusikia Injili ya kweli na kuwa na imani ya kweli mara nyingi kumejitokeza wazi katika taarifa ya kuhubiri injili.
-
“Wakorintho wengi waliposikia waliamini wakabatizwa” (mdo 18:8)
-
Watu wasikie neno la Injili, waamini ( mdo 15:7)
-
Ndivyo tuhubirivyo, na ndivyo mlivyoamini'(1 Kor. 15:11)
-
‘Mbegu’ Kwenye mfano wa mpanzi ni neno la Mungu (Luka 8:11) wakati katika huo wa mti wa haradali ni imani ( Luka 17:6) kwa kuona kwamba imani huja kutokana na kupokea'Neno kwa imani’ ( Rum 10:8) “Maneno ya imani, na mafundisho mazuri” ( 1Tim 4:6), katika moyo ambao upo wazi kumwamini Mungu na neno lake (Gal 2:2, Ebr 4:2)
-
Mtume Yohana anaisema taarifa iliyoandikwa ya maisha ya Bwana kuwa anasema' kweli (Yaani ukweli) ili nanyi mpate kusadiki’ ( Yohana 19:35).Basi neno la Mungu limeitwa ‘Kweli’(Yoh:17:17) ili mpate kuamini.
1.2 Nafsi yake Mungu
Ni mwenye enzi, Mungu aliyeandikwa katika Biblia na kwamba ni kweli, mtu wa kugusika, naye yupo katika umbo. Vilevile ni mafunzo ya kwanza ya Ukristo kuwa Yesu ni mwana wa Mungu. Ikiwa Mungu hana umbo , basi haiwezekani yeye kuwa na mwana ambaye alikuwa ni 'Chapa ya nafsi yake' (Ebr 1:3) Tena inakuwa vigumu kuendeleza maisha ya uhusiano wake na mungu ikiwa Mungu ni wazo lililo kwenye akili zetu, Mkusanyiko wa roho mahali popote juu katika anga lisilo na kitu. Ni huzuni kusikia kwamba dini za watu wengi zina wazo lisilo la kweli lisilotambulika kuhusu Mungu. Yeye akiwa mkubwa mno kuliko sisi, inaeleweka ya kwamba imani ya watu wengi imeweka kikwazo kwenye ahadi dhahiri kuwa mwishowe tutamwona Mungu. Israeli walikosa imani ya kumwona Mungu alivyo (Yoh. 5:37) ni dhahiri ana umbo halisi, Imani hii huja kutokana na kumjua Mungu kwa kuamini neno lake
Heri walio safi wa moyo, Maana watamwona Mungu (Math 5:8)
Na watumwa wake (Mungu) watamtumikia, nao watamwona uso wake, na jina lake(Jina la Mungu ) litakuwa katika vipaji vya nyuso zao (Uf 22:3-4)
Tumaini hili la ajabu kama kweli tunaliamini litaonyesha matokeo ya matendo kwenye maisha yetu:
-
Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote na huo utakatifu, ambao hakuna mtu atakaye mwona Bwana asipokuwa nao (Ebr 12:14)
-
Tusiape, kwa kuwa aapaye kwa mbingu, Huapa kwa kiti cha Mungu na kwa yeye na kwa yeye aketiye juu yake ( Math 23:22) hii itakuwa haina maana ikiwa Mungu sio mtu mwenye mwili.
-
Tutamwona kama alivyo (akidhihirika katika kristo ) na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu (1 Yoh 3:2,3)
Katika maisha yetu haya kumfahamu Mungu wetu wa mbinguni, hakujakamilika sana. Tunaweza kutazama mbele, kupitia giza linalotatanisha la maisha haya hadi mwisho wa kukutana naye. Kumwona kwa macho yetu hapana shaka kutakuwa sawa na kumfahamu kwa akili zaidi. Kutoka vina vya masumbufu ya mwanadamu. Ayubu aliweza kufurahia uhusiano wake wote na Mungu ambao utimilifu wake atauona mwisho wa siku.
Na baada ya ngozi yangu kuharibiwa hivi (Yaani katika mauti),Lakini pasipokuwana mwili wangu (Yaani pasipo mwili unaoharibika ) nitamwona Mungu;Nami nitamwona mimi nafsi yangu,na macho yangu yatamtazama, wala si mwingine (Ayubu 19:26,27)
Mtume Paulo aliyatazamia maisha mengine yasiyo machungu yasiyo na msukosuko: “Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; Wakati ule tutaona uso kwa uso” ( 1Kor 13:12)
USHAHIDI WA AGANO LA KALE
Ahadi hizi zilizo katika Agano Jipya zimejengwa juu kwenye ushahidi wa mambo yake makubwa ya Agano la kale, Kuwa ni Mungu aliye na mwili. Ushahidi hauwezi kukaza zaidi lakini ni mwanzo wa kukubali hali ya Mungu kama tunataka kuwa na ufahamu wa kweli yoyote kuhusu dini ambayo msingi wake upo kwenye Biblia. Agano la Kale lina mazungumuzo ya Mungu kuwa ni mtu na mtu uhusiano wa mtu na mtu pamoja Mungu, ambao Agano la Kale na Jipya linausema ni wa pekee kwa tumaini la Ukristo wa kweli. Yafuatayo ni majadiliano ya nguvu kwa ajili yake, Mungu aliye na mwili.
“Mungu akasema, Na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu” (Mwa. 1:26) Hivyo mtu amefanywa kwa mfano na sura ya Mungu, Kama ilivyodhihirika kupitia Malaika. Yakobo 3:9 anasema … Wanadamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu. Maneno haya hayatumiki kutaja mfano wa akili ya mwanadamu, kwa kuwa hali ya fikra zetu zipo mbali kabisa toka zake Mungu na katika njia nyingi kwa kikubwa zimepingana na haki yake.”Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu, asema Bwana. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu” ( Isa 55:8 - 9 ). Kwa hiyo mfano na sura, tunavyoshirikiana naye Mungu, inabidi uwe ni mfano wa mwili- Lakini yeye hana wa dhambi.
Popote Malaika walipoonekana duniani wamesemwa kuwa wana umbo la watu, kwa mfano, Abrahamu aliwakaribisha malaika bila kujua, akizania kuwa walikuwa watu wa kawaida. Sisi jinsi tulivyoumbwa kwa mfano wa Mungu kwa kweli maana yake ni kwamba tunaweza kufahamu jambo lingine kuhusu mtu halisi, ndivyo tulivyo, lakini tunafanana. Basi, Mungu tunaye mshabihi siyo mtu mwingine asiyedhahiri ambaye hatuwezi kumfikiria.
“Wao wenyewe Malaika wanafanana na Mungu. Hivyo Mungu aliweza kumsema Musa, “Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, maana wazi wazi wala si kwa mafumbo. Na umbo la Bwana yeye ataliona” (Hesabu 12:8) Haya yalikuwa yanamtaja Musa, akifunzwa na Malaika aliye kuwa na jina la Bwana (Kut. 23:20:21) Ikiwa Malaika alikuwa na umbo la Bwana, Inaonyesha kuwa Mungu amefanana na Malaika Yaani - Kimwili ana umbo la Mwanadamu. “BWANA alisema na Musa uso kwa uso kama vile mtu asemavyo na rafiki yake. (Kut. 33:11: Kum. 34:10 ). Bwana alijidhihirisha katika Malaika wake, ambaye uso na kinywa alifanana na Bwana mwenyewe.
“Kwa maana yeye anatujua umbo letu, (Zab. 103:14).Ana tutaka yeye, tumfikirie kuwa ni mtu, Baba ambaye tunaweza kuunganishwa naye.Huyu ataelezwa kwa ushahidi mwingi wa mikono ya Mungu, Viganja,Macho n.k. Ikiwa Mungu alikuwa ni furushi la Nafsi mahali fulani katika mbingu, ambazo inabidi ziwe Mungu, ni wazo letu kama tukitaka utu wake; basi ushahidi huu unatupotosha kukuza kusudi lolote.
“Maelezo ya sehemu ya makao ya Mungu, Wazi wazi yanaonyesha kwamba “Mungu” ana mahali pake; “Mungu yuko Mbinguni”( Mhubiri 5:2);Maana ametazama toka patakatifu pake pa juu, toka mbinguni BWANA ameiangalia nchi (Zab 102:19,20); “Usikie huko mbinguni, Makao yako” (1Fal. 8:39). Lakini kwa kupambanua zaidi kuliko hivi tunasoma kwamba Mungu ana “Kiti cha Enzi” (2 Nya. 9:8, Zab 11:4; Isa. 6:1,66:1).Lugha kama hii ni ngumu kuitumia nafsi isiyo wazi kabisa, inayokaa katika milki ya Kimbingu. Mungu amesemwa kuwa “Ameshuka kuja chini” wakati mwenyewe anapojidhihirisha. Hapa panadokeza makao ya Mungu yaliyo mbinguni. Inakuwa vigumu kueleza wazo la udhihirisho wa Mungu bila kukubali hali ya umbo la Mungu. Isaya 45 ina ushahidi tele wa Mungu kujihusisha kwake katika mambo ya watu wake: “Mimi ni BWANA, wala hapana mwingine ….., mimi ni BWANA anayetenda haya yote …., Mimi, BWANA nimeiumba Ole wake ashindanaye na Muumba wake … Mimi, naam, mikono yangu mimi, imezitanda mbingu …, niangalieni mimi mkaokolewe, enyi ncha zote za dunia. mstari hasa kweli huu wa mwisho unaonyesha uwepo wake Mungu - Anawataka watu wamwangalie yeye, Kuwaza uwepo wake halisi pamoja na jicho la imani.
Mungu amejifunua kwetu akiwa ni mwenye kusamehe anayesema, maneno kwa watu. Hata hivyo msamaha na usemi unaweza tu kutoka kwa mtu: ni matendo ya akili, Hivyo Daudi alikuwa ni mtu aliyeupendeza moyo wa Mungu (1 Sam 13: 14), inaonyesha kwamba Mungu ana moyo, unaoweza kunakiliwa kwa kiwango kidogo na mtu, ingawa mwanadamu wa mwili haupendezi moyo wa Mungu. Mafungu ya maneno kama BWANA akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani akahuzunika moyo (Mwa. 6:6), hufunua hisia ya Mungu, mwenye ufahamu kuliko kuwa kishindo cha roho ya kuwazika katika hewa. Hapa tunasaidiwa tukubali jinsi kwa kweli tunaweza pande zote mbili kumpendeza na kutokumpendeza, Kama mtoto anavyoweza kwa baba wa mwili.
IKIWA MUNGU SI MTU MMOJA
Kama Mungu si wa kweli, mmoja mwenye kuwepo, Basi wazo la kupenda mambo ya roho ni vigumu kushikana nayo. ikiwa Mungu ni mwenye haki kabisa lakini si mtu mwenye umbo, basi kwa kweli hatuwezi kuiwazia haki yake ilivyodhihirika kwa watu. Pande zote mbili, Ukristo uliokenguka na wayahudi wana wazo la kwamba haki ya Mungu inaingia katika maisha ya watu kwa njia ya
‘Roho Mtakatifu’ Asiyedhahiri ambaye kwa namna isiyoeleweka tunafanywa mfano kwenye akili ya Mungu, na kukubalika kwake. Kwa maneno mengine, mara tukitambua ya kwa mba yupo mtu mwenyewe aitwaye Mungu, basi tunaweza kurekebisha tabia yetu kufuata atakavyo, Kwa msaada wake utokao kwenye ushawishi wa neno lake na kwa kuleta sifa inayoonyesha tabia ya Mungu katika utu wetu.
Lengo la Mungu ni kujidhihirisha mwenyewe katika mkutano wa watu waliotukuzwa. Jina la kumbukumbu yake, YEHOVA ELOI, linamaanisha hivi ( Atakaye kuwa kwa wenye nguvu ni tafsiri iliyo karibu sahihi.) ikiwa Mungu si mtu mwenye umbo, basi thawabu ya waaminifu katika ufalme wa Mungu ujao duniani inaonyesha ya kwamba watakuwa nayo wazi tena dhahiri wakiwepo katika mwili, Ingawa hawatakuwa katika udhaifu wa mwili wa Mwanadamu tena. Ayubu alitamani' Siku ya mwisho’ atakapofunguliwa na mwili wake ( Ayubu 19:25:27); Abrahamu itabidi awe mmojawapo wa wale wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi ambao wataamka…… Kwa uzima wa Milele wa nchi ya Kanani (Dan. 12:2) hivyo basi ataweza kupata ahadi ya urithi wa milele wa nchi ya kanaani, Sehemu inayoonekana katika dunia hii
(Mwa. 17:8.) “ Na wataua wake watashangilia….. waimbe kwa sauti kuu vitandani mwao….. ili kufanya kisasi juu ya mataifa (Zab 132: 16; 149: 5,7) Kushindwa kwa watu wote wa pande mbili, Wayahudi na watu wa mataifa,
Kutambua mafungu ya maneno kama haya vyema, kwa ukubwa wa maneno yenyewe Kuletwa ahadi za kuonekana kwa Abrahamu, kumeongoza watu kwenye imani potovu la' Nafsi haifi’ ya kwamba Mwanadamu halisi anakuwepo hai akifa. Wazo hili halina msaada wa Biblia kabisa. Mungu hapatikani na mauti, Mtu mwenye utukufu, analifanya lengo lake, ili kwamba wanaume na wanawake waweze kuitwa na kuishi katika ufalme wake ujao kwenye dunia hii, Kushiriki sifa, zilizoelezwa katika umbo la mwili.
Waaminifu wameahidi wa kwamba watarithi mwili wa Mungu (2 Pet. 1:4) Ikiwa Mungu si mtu mmoja, basi hii ina maana tutaishi milele kwa roho zisizo na mwili. Lakini hili si fundisho la Biblia. Tutapewa mwili kama ule wa Yesu. (Flp. 3:21), Nasi tunajua kwamba tutakuwa na mwili halisi kwenye ufalme mwili utakaokuwa na mikono macho na masikio (Zek. 13:6, Isa. 11:3 ), mafunzo ya Mungu kuwa ni Mmoja, kwa sababu hii yanasimulia Injili ya Ufalme.
Itakuwa wazi kwamba hakutaweza kuwa na wazo la kujua Ibada, dini au uhusiano mmoja na Mungu mpaka itambulike kuwa Mungu ni mtu mmoja, na kwamba kwa mwili sisi ni mfano wake. Ingawa ni mfano usio kamili sana unahitajika kuukuza kufuata mfano wa akili yake, Hivyo basi, tutaweza kupata utimilifu wa mfano wake unaoonekana katika ufalme wa Mungu. Maana nyingi zaidi na faraja tunaweza kupata kutoka mafunzo ya maneno ambayo yanamtaja Mungu kuwa ni Baba aliye na upendo, akiturudi kama Baba afanyavyo kwa mwanae (mfano. Kum. 8:5). Katika maneno yenyewe ya mateso ya Kristo tunasoma kwamba,'Lakini BWANA aliriidhika kumchubua’ (Isa. 53:10 ),Ingawa “Alimlilia Mungu” aliisikia sauti yangu…….. Kilio changu kikaingia masikioni mwake (Zab.18:6). Ahadi ya Mungu kwa Daudi kuhusu mzao atakaye kuwa ni mwana wa Mungu ilitakiwa azaliwe kwa Muujiza kwa Mwanadamu; Ikiwa Mungu hakuwa ni mtu mmoja, asingekuwa na mwana huyo.
Kumfahamu Mungu kwa usahihi ni ufunguo unaofungua maneno mengi mengine ya muhimu katika mafundisho ya Biblia. Lakini kama uongo mmoja huongoza kwenye uongo mwingine, Hivyo dhana potovu juu ya mungu inaficha utaratibu wa kweli ambao maandiko yanatoa. Kama umepata kuona kuwa hii sehemu inadhibitisha, au hata ikiwa ni ndogo, basi, swali linakuja. Je? Unamjua Mungu kweli?. Sasa tutachunguza maandiko ya Biblia zaidi kuhusu yeye.
1.3 Jina La Mungu Na Tabia Ya Sifa Yake
Ikiwa Mungu yupo, inafaa kufikiri kuwa atakuwa amevumbua njia nyingine ya kutuambia habari zinazo mhusu yeye mwenyewe. Tunaamini ya kwamba Biblia ni ufunuo wa Mungu kumjulisha Mwanadamu, na humo ndani ya kitabu tunaona kudhihirika tabia ya sifa ya Mungu. Hii ndio sababu Neno la Mungu linasemwa kuwa ni'Mbegu’ yake (1 Petro 1:23) Kwa kuwa kama likigeuza hali ya mioyo yetu, kiumbe mpya anaumbwa ndani yetu ambaye ana sifa za Mungu (Yakobo. 1:18, 2Kor. 5:17). Kwa hiyo sisi wenyewe tunapotumia zaidi neno la Mungu na kuchukua masomo sisi wenyewe, ndivyo zaidi tutafanana mfano wa mwana wake ( Rum, 8:29) ambaye kwa tabia ya sifa alikuwa mfano kamili wa Mungu (Kol. 1:15).Kwa hii imelala thamani ya kusoma sehemu za historia ya Biblia, Zimejaa kadhia ya masomo jinsi Mungu alivyojishughulisha na watu pamoja na matifa, Daima akionyesha msingi ule ule wa sifa.
Katika Kiebrania jina la mtu mara nyingi lilileta tabia ya sifa zao au taarifa zinazowahusu. Mifano mingine iliyowazi:
-
‘Yesu’'Mwokozi’ Kwa kuwa atawaokoa watu wake kutoka dhambi zao’ (Math. 1:21)
-
‘Abrahamu’'Baba wa mkutano mkubwa’ Maana nimekufanya kuwa baba wa mataifa mengi’(Mwa. 17:5)
-
‘Hawa (Eva)'Uhai’ Kwa kuwa alikuwa mama wa wenye uhai wote (Mwa. 3:20)
-
‘Simeoni’'Kusikia’ Kwa kuwa bwana amesikia kwamba nalichukiwa, kwa sababu amenipa mwana huyu (Mwa. 29: 33).
Katika Yeremia 48:17, kuwajua watu wa Moabu ni sawa sawa na kufahamu jina la moabu.Mara nyingi zaburi zinamlinganisha Mungu mwenyewe na jina lake, neno lake na matendo (Zab. 103:1, 105:1, 106:1,2,12,13.) Kwa sababu hii itegemewe kwamba majina ya Mungu na heshima vitatupatia habari nyingi kuhusu yeye mwenyewe, kwa kuwa yapo maelekeo mengi ya tabia ya sifa na kusudi kwa kweli ana jina zaidi ya moja.Somo lenye kueleza jambo moja moja la jina Mungu linafaa baada ya Ubatizo; kufahamu zaidi sifa na tabia ya Mungu kumeelezwa katika jina lake, ni jambo lingine ambalo liendelee wakati wa maisha yetu yote katika Bwana. Linalofuata sana kwa hilo, mengi ni Utangulizi.
Musa alipotaka aelimishwe kwa undani kuhusu Mungu ili imani yake iimalike wakati wa kipindi kisicho sahaulika sana cha maisha yake. Malaika,'Alitangaza jina la BWANA: BWANA,BWANA Mungu, Mwingi wa huruma, Mwenye fadhili, Si mwepesi wa hasira, Mwingi wa rehema na kweli, Mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, Mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; Wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia,’ (Kut. 34:5-7)
Huu ni ushahidi ulio wazi wa kwamba majina ya Mungu yanaweka sifa zake.Tendo la kuwa nazo ni uhakika kuwa ni mtu mmoja, si busara kufikiri ya kwamba fungu la roho laweza kuwa na dalili na sifa ya tabia hizi ambazo vile vile zaweza kuendelezwa ndani yetu wanadamu.
Mungu amechagua hasa jina moja ambalo amependa ajulikane na kukumbukwa na watu wake, ni kwa ufupi, maelezo mafupi, ya kusudi lake kwa watu.
Israeli walikuwa watumwa Misri, Walihitajika kukumbushwa lengo la Mungu kwao. Musa aliambiwa awaambie Jina la Mungu, ili kwamba hili liwasaidie kuwaletea kusudi la kuondoka Misri na kuanza safari kuelekea nchi ya Ahadi (1Kor. 10:1) Nasi pia tunahitajika kuelewa mambo ya msingi yahusuyo jina la Mungu kabla ya kubatizwa na kuanza safari yetu ya kuelekea Ufalme wa Mungu. Mungu aliwaambia Israeli kuwa Jina lake alikuwa YAHWEH-YAHU (Zab 89:8 uv); Maana yake“Mimi niko ambaye NIKO” au limetafsiriwa kwa usahihi zaidi,'Nitakuwa ambaye Nitakuwa’(Kut 3:13-15) Jina hili, kidogo likapanuka wakati ule:” Tena Mungu akamwambia ( Ikiwa ni nyongeza) Musa, Hivi ndivyo utawaambia wana wa Israel, BWANA (Yahweh) Mungu wa Babu zenu, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, ….Hili ni Jina langu Milele, la kumbukumbu yangu kwa vizazi vyote. (Kut. 3:15). Kwa sababu hiyo jina kamili la Mungu ni “BWANA Mungu”
Zaidi Agano la kale liliandikwa kwa Kiebrania na tafsiri ya Kiswahili ni lazima kutukia visivyo sawa sawa wakati ujapo wa kutafsiri maneno ya Kiebrania hasa neno “Mungu” mengi ya maelezo moja moja yakosekana - Tafsiri yetu ya Kiswahili imetoka kwenye Kiingereza. Moja ya maneno yanayotumiwa na Kiebrania limetafsiriwa'Mungu’ ni Elohim (ELOI) maana yake'Wenye Nguvu’ Kumbukumbu ya jina la Mungu, jina ambalo anatutaka tumkumbuke, kwa sababu hiyo.
YAHWEH ELOHIM - YAHU ELOI
Maana yake
ATAKAYEDHIHIRIKA KATIKA KUNDI LA WENYE NGUVU.
Kwa hiyo ni kusudi la Mungu kuidhihirisha tabia ya sifa yake, Umuhimu wake katika kundi kubwa la watu. Kwa kulitii neno lake tunaweza kukuza sifa zingine za Mungu ndani yetu wenyewe sasa, hivyo basi kadri ya busara sana. Mungu alijifunua mwenyewe kwa waamini wa kweli katika maisha haya.lakini jina lake Mungu ni la Unabii wa wakati ujao hapo dunia itakapo jaa watu watakao kuwa sawa naye, pande mbili kwa tabia na mwili (2Petr 1:4). Ikiwa tunataka kuungana na lengo la shabaha ya Mungu na kuwa kama Mungu bila hata kufa tena, kuishi milele katika uadilifu wote uliokamilika, basi yatupasa sisi wenyewe tujiunge na jina lake.
Namna ya kufanya hivi ni kubatizwa katika jina, yaani la Yahweh Elohim (Math. 28:19). Hili linatufanya tuwe watoto (‘Uzao’) wa Abrahamu (Gal,. 3:27-29) uliohaidiwa kurithi milele nchi (Mwa. 17:8; Rum. 4:13) Kundi la wenye nguvu (Elohim -Eloi) ambao unabii wa jina la Mungu utatimilika. Limeelezwa zaidi kwa habari katika
somo la 3.4.
1.4 Malaika
Yote ambayo tumeyapima sana katika somo hili yanaletwa pamoja kwenye tafakari ya Malaika:
-
Viumbe walio na mwili
-
Huchukua jina la Mungu
-
Wao ni njia ambayo roho wa Mungu anatenda kazi ya kutimiza mapenzi yake
-
Wanapatana tabia na kusudi lake
-
Na kwa hiyo wanamdhihirisha yeye.
Tumetaja kwenye somo la 1.3 ya kwamba moja kati ya maneno yanayotumika zaidi katika Kiebrania lililotafsiriwa “Mungu” ni' Eloi’ ambalo hasa maana yake ' Wenye nguvu’ hawa,'Wenye nguvu’ ambao huchukua jina la Mungu wanapotokea wana weza kuitwa 'Mungu’ kwakushirikiana kwao pamoja na naye karibu. Hawa viumbe wanaitwa Malaika.
Taarifa ya uumbaji wa ulimwengu katika mwanzo 1 inatuambia ya kwamba Mungu alitamka amri halisi kuhusu Uumbaji'Ikiwa hivyo’ walikuwa ni Malaika waliotimiza amri hizo:
“Enyi Malaika zake, mliohodari mtendao neno lake, mkiisikiliza sauti ya neno lake (Zab. 103:20).
Kwa sababu hii busara husadiki kuwa tunaposoma 'Mungu’ akiumba ulimwengu, kazi hii kweli ilifanywa na Malaika. (Ayubu 38:4-7) anadokeza vile vile namna hii. Sasa ni wakati mzuri kuelezea kwa kifupi matukio ya uumbaji kama yalivyoandikwa
Mwanzo 1:
Siku ya Kwanza‘ Mungu akasema, Na iwe nuru, Ikawa’ (Mstari 3)
Siku ya Pili 'Mungu akasema, Na iwe anga katikati ya maji, likayatenga maji na maji.Mungu akalifanya anga ,akayatenga yale maji yaliyo juu ya anga na yale yaliyo chini ya anga: Ikawa hivyo’ (Mstari 6,7)
Siku ya Tatu ‘Mungu akasema, Maji yaliyo chini ya mbingu na yakusanyike mahali pamoja, (akifanya Bahari na Bahari kuu) ili pakavu paonekane; Ikawa hivyo’ (Mstari wa 9)
Siku ya Nne ‘Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu… Ikawa hivyo’ (Mstari 14:15)
Siku ya Tano ‘Mungu akasema, Maji na yajae kwawingi na kitu kiendacho chenye uhai …. ndege waruke juu ya nchi ….. Mungu akaumba kila kiumbe chenye uhai (Mstari wa 20:21), Ikawa hivyo.
Siku ya Sita ‘Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe haikwa jinsi zake…. Mnyama wa kufugwa,nacho kitaambaacho …. Ikawa hivyo (Mstari 24)
Siku hiyo hiyo ya sita mtu aliumbwa. Mungu akasema, na tufanye mtu kwa mfano wetu, na kwa sura yetu (Mwa 1:26). Tuliwahi kutoa maelezo juu ya mstari huu katika somo la 1.2. Kwa muda uliopo, tunataka kujua hapa ya kwamba.'Mungu’ sio tu anatajwa Mungumwenyewe katika utu'Na tufanye mtu’ inaonyesha kuwa Mungu anatajwa mtu zaidi ya mmojaNeno la Kiebrania linalotafsiriwa hapa'Mungu’ ni Elohim (Eloi), Maana yake'Wenye nguvu’ Ukiwa ni ushahidi unaotaja Malaika. Ukweli ni kwamba Malaika walituumba sisi kwa mfano wao maana yake ni kuwa wana sura ya mwili ule ule kama tulio nao. Kwa sababu hiyo ni wa kweli, wa kugusika, viumbe wenye mwili, wakishiriki mwili ule ule kama wa Mungu.
‘Mwili’ Kwa maana hii unatajwa kwa msingi jinsi mtu mwingine alivyo kwa sababu ya muundo wa mwili wao. Katika Biblia ipo “Miili” ya aina mbili katika maana halisi ya neno haiwezekani kwa wakati huo huo kuwa miili hii ya aina mbili.
Mwili wa Mungu (‘Mwili wa Uungu’)
Hauwezi kutenda dhambi (Mkamilifu) Rum 9:14,6:23; Zab. 90:2, Math 5:48,Yak 1:13)
Haupatikani na Mauti ( 1Timotheo 6:16)
Una nguvu tele na uweza ( Isaya 40:28)
Huu ndio mwili wa Mungu na Malaika na ambao alipewa Yesu baada ya kufufuliwa (Matendo 13:34; Ufunuo 1:18; Ebr. 1:3) Huu ndio mwili ambao tumeahaidiwa kupewa (Luka 20:35,36; Isa. 40:28,31)
Mwili wa mwanadamu
Hujaribiwa na kutenda dhambi ( Yak 1:13-15 )kwa nia mbaya ya asili
(Yer 17:9; Marko 7:21-23) Huangamia mautini, Yaani unapatwa na kifo ( Rum. 5:12,17; 1Kor 15:22) Una kikomo cha nguvu, sehemu mbili, kwa mwili (Isa. 40:30) na kwa akili ( Yer 10:23)
Huu ni mwili ambao watu wote, wema na wabaya, kwa sasa wanao mwisho wa mwili huo ni kifo (Rum 6:23). Ulikuwa ni mwili ambao Yesu alikuwa nao wakati wa maisha yake ya mwili unaokufa hapa duniani (Ebr. 2:14-18,Rum. 8:3 Yoh 2:25, Marko 10:18)
MATENDO YA KUONEKANA NA MALAIKA
Malaika wakiwa na mwili wa Uungu, inabidi wawe hawana dhambi na kwa sababu hiyo hawawezi kufa kwa kuona kwamba dhambi huleta mauti (Rum. 6:23). Inapasa wawe na umbo halisi na mwili wa kuwepo mauti “Na yaletwe basi maji kidogo ukanawe miguu, mkapumzike chini ya mti huu”(Mwanzo 18:4)
Wawili kati ya hao Malaika wakati ule walikwenda kwa lutu katika mji wa Sodoma. Tena, walitambuliwa kuwa ni watu na lutu pamoja na watu wa Sodoma.'Basi, wale malaika Wawili wakaja Sodomaa jioni aliowakaribisha wakae kwake usiku. Lakini watu wa Sodoma wakaja kwenye nyumba yake, wakiuliza kwa namna ya kutisha,'Wawapi wale watu waliokuja kwako usiku huu ?’ Lutu akawasihi,' Watu hawa msiwatende neno’ Taarifa ya maandiko ya Mungu pia inawaita ni'Watu’, Wale watu ( Malaika ) wakanyoosha mikono yao, wakamwokoa Lutu, Basi wale watu wakamwambia Lutu ….., BWANA ametutuma tuuharibu Sodoma (Mwanzo 19: 1,5,8,10,12,13).
Ufafanuzi wa Agano jipya juu ya matukio haya yanadhibitisha kwamba Malaika wanafanana na umbile la watu. “Msisahau kuwafadhili wageni; Maana kwa njia hii wengine (Kwa mfano Lutu na Abrahamu ) waliwakaribisha Malaika pasipo kujua (Ebr 13:2)
Yakobo alishindana usiku kucha na mtu mmoja ( Mwa 32:24) ambaye baadae tumeambiwa kuwa alikuwa Malaika (Hosea 12:4)
Watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe walikuwepo kwenye ufufuo (Luka 24:4) na wakati wa kupaa (Mat. 1:10) Yesu, kwa uhakika hawa walikuwa ni Malaika.
Ona vidokezo vya'Kipimo cha Kibinadamu, maana yake cha Malaika’ (Uf 21:17).
MALAIKA HAWATENDI DHAMBI
Malaika wakiwa na mwili wa Uungu, hawawezi kufa, kwa sababu dhambi huleta mauti, Basi wao hawawezi kutenda dhambi. Maneno ya asili katika lugha ya Kiyunani na Kiebrania yaliyotafsiriwa'Malaika’ maana yake ni mjumbe; Malaika ni wajumbe au watumishi wa Mungu, Watiifu kwake, Kwa hiyo hawafikiriwi wao kuwa ni wenye dhambi. Kwa hivyo neno la Kiyunani’Agelos’ lililotafsiriwa'Malaika’ vile vile limetafsiriwa'Wajumbe’ Wanaposemwa wanadamu kwa mfano Yohana mbatizaji, (Math 11:10) na wajumbe wake (Luk. 7:25) wajumbe wa Yesu (Luk. 9:52) na watu walioupeleleza mji wa Yeriko (Yak. 2:25). Kwa kweli inawezekana kwamba'Malaika’ katika maana ya wajumbe wanadamu wanaweza kutenda dhambi.
Mafungu ya maneno yafuatayo ni wazi kwamba Malaika wote ( Sio tu baadhi yao) kwa umbile ni watiifu kwa Mungu, na hivyo hawawezi kutenda dhambi.
‘BWANA ameweka kiti chake cha Enzi mbinguni Na Ufalme wake unavitawala vitu vyote (Yaani haiwezekani kuwepo uasi juu ya Mungu mbinguni)Mhimidini BWANA, Enyi Malaika zake, Ninyi mlio hodari, mtendao neno lake, Mkisikiliza sauti ya neno lake Mhimidini BWANA, enyi majeshi yake Yote; Ninyi watumishi wake mfanyao mapenzi yake (Zab. 103:19-21)
“Msifuni, enyi Malaika wake wote …. Majeshi yake yote ( Zab 148: 2 )
Je ! hao wote si roho (Malaika ) watumikao, wakitumwa kuwahudumia wale watakaourithi wokovu ? ( Ebra. 1: 13,14 )
Kurudiwa kwa neno'Wote’ linaonyesha ya kwamba Malaika hawajagawanyika katika makundi mawili, kundi moja zuri na jingine lenye dhambi. umuhimu wa kufahamu vema umbile la malaika ni kwamba thawabu ya waaminifu ni kushiriki mwili wao. “Wale wahesabiwao kuwa wamestahili…. Hawaoi wala hawaolewi … wala hawawezi kufa tena. kwa sababu huwa sawa sawa na Malaika (Luk 20:35, 36).
Hili ni neno la muhimu kulishika. Malaika hawawezi kufa'Maana hatwai asili ya Malaika (Kwa kuwa tangu asili hawajatenda dhambi). Ila atwaa asili ya mzao wa Abrahamu -,sababu ya dhambi’ (Ebr 2:16) Ikiwa Malaika waweza kufanya dhambi, Basi wale ambao watakuwa wamestahili thawabu ya Kristo atakapo kuja bado wataweza kutenda dhambi pia, Na kwa kuwa dhambi huleta mauti (Rum 6:23) kwa sababu hiyo hawataweza kuwa na uzima wa milele, kama tukiwa na uwezekano wa kutenda dhambi ni kufanya ahadi ya Mungu ya uzima wa milele haina maana, kwa kufahamu kuwa thawabu yetu ni kushiriki mwili ule wa Malaika. Ushuhuda wa'Malaika (Luk. 20:35,36) unaonyesha kwamba hakuna aina ya Malaika wema na wenye dhambi; ipo aina moja ya Malaika tu.
Ikiwa Malaika waweza kutenda dhambi, Basi Mungu ameachwa hana nguvu za kutenda tendo la haki katika maisha yetu na mambo ya ulimwengu, kwa kufahamu kuwa ameeleza kwamba anafanya matendo yake kwa njia ya Malaika zake( Zab 103:19-21) Wamefanywa kwa'Roho wa Mungu katika maana ya kwamba anatimiza yote kwa nguvu zake. Akitenda kazi katika Malaika (Zab 104:4). Kwamba wanamwasi Mungu haiwezekani. Mkristo amwombe kila siku, Mungu ili ufalme uje duniani, ili mapenzi yake yafanyike kama sasa yanavyofanyika mbinguni (Math 6:10) Ikiwa Malaika wa Mungu iliwapasa washindane na Malaika wenye dhambi huko mbinguni, basi, kwa utimilifu mapenzi yake hayakuweza kufanyika huko, na kwa sababu hiyo hali hiyo hiyo itapatikana kwenye ufalme wa Mungu ujao. Kutumia maisha ya milele kwenye ulimwengu ambao utakuwa ni uwanja wa vita kati ya dhambi na utii, kwa shida hayo sio matazamio ya kutia moyo, lakini hilo, kwa kweli, sio ndiyo suala lenyewe.
MALAIKA NA WATU WANAOAMINI
Ipo sababu nzuri ya kuamini kuwa kila mwamini wa kweli ana Malaika pengine mmoja maalumu-wa kuwasaidia katika maisha yao:-
‘Malaika wa BWANA hufanya kituo, akiwazungukia na kuwaokoa wamchao’ (Zab 34:7)
Mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio (Yaani wafuasi dhaifu- Zek, 13:7 Mat 26:31)…Malaika wao mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu’ (Mat. 18:6,10)
Wakristo wa kwanza ni wazi waliamini kwamba Petro alikuwa na Malaika mlinzi (Matendo 12:14,15).
Watu wa Israeli walipita katika bahari ya Shamu, waliongozwa na malaika kwenye jangwa kuelekea nchi ya Ahadi. Kutembea kupitia katika bahari ya shamu maana yake ni Ubatizo wetu katika maji (1Kor 10:1), Hivyo nasi vile vile ina maana tusadiki kuwa baadae tunaongozwa na kusaidiwa na Malaika tunaposafiri katika jangwa la maisha kuel;ekea nchi ya ufalme wa Mungu.
Ikiwa Malaika wana weza kuwa waovu katika maana ya kuwa wenye dhambi, basi Ahadi hizi za Malaika kuongoza na kushawishi katika maisha yetu zinakuwa laana badala ya Baraka.
-
Basi tufahamu ya kuwa Malaika ni Viumbe………
-
Wenye mwili ulio sawa na Mungu na huonekana kwa mwili
-
Ambao hawawezi kutenda dhambi
-
Daima hufuata amri za Mungu
-
Wao ni njia ambayo Mungu katika Roho nguvu hunena na
-
kutenda kazi (Zab. 104:4)
LAKINI..?
Makanisa mengi ya'Kikiristo’ yana wazo la kwamba Malaika wanaweza kutenda dhambi, na kwamba Malaika wenye dhambi sasa hivi wapo na wao wanahusika na dhambi pamoja na matatizo yaliyopo hapa Duniani. Tutajadili zaidi vya kutosha juu ya kutofahamu vema jambo hili kwenye somo la 6. Kwa sasa tutatengeneza vipengele vifuatavyo:-
Inawezekana kwamba uumbaji ulikuwepo uliotutangulia sisi wa kweli, yaani huo ulioandikwa katika Mwanzo 1. Pia inaweza kusadikika ya kwamba Malaika waliopo walikuja kuwa na fahamu za'Wema na Ubaya’ (Mwa. 3:5) walipo kuwa katika hali kama hii tuliyonayo katika maisha haya.
Ya kwamba viumbe wengine walioishi kwa kipindi kile walitenda dhambi hatujakatazwa kufikiri; lakini yote haya ni mawazo ambayo mioyo ya watu hupenda kujishughulisha. Biblia yatuambia kile ambacho tunakihitaji kujua kuhusiana na hali iliyopo, ambayo ni kwamba hawapo Malaika watenda dhambi, Malaika wote ni watiifu kwa Mungu kabisa.
Hawawezi kuwepo viumbe wenye dhambi mbinguni, kwa kufahamu kuwa Mungu'ana macho safi na hawezi kuangalia uovu’ (Ab. 1:3) katika maelezo haya, Zaburi 5:4,5 yatuambia:-
‘Mtu mwovu hatakaa kwako. wajivunao hawatasimama mbele za macho yako’ yaani makao ya mbinguni. Jambo la kwamba ulikuwepo Uasi juu ya Mungu mbinguni na Malaika watenda dhambi ni wazo linalopingana kabisa na maneno yaliyotolewa.
Neno la kiyunani lililotafsiriwa'Malaika’ maana yake'Mjumbe’ linataja wanadamu, kama tulivyoonyeshwa'Wajumbe’ wanadamu hawa wanaweza kwa kweli kufanya dhambi.
Ya kwamba upo uovu, viumbe wenye dhambi ambao juu yao mwelekeo wa maisha yote yasiyofaa wanaweza kutupiwa lawama kwa kawaida ni moja ya Imani zaidi iliyoshikiliwa katika Upagani.Kwa njia hiyo hiyo mambo yanayohusu Krismas yameingia kwenye kile kinachodhaniwa ni'Ukristo’ Basi, vile vile Ukristo una fikra hizo za Kipagani
Yapo mafungu ya maneno ya Bibilia yaliyojaa tele ambayo yanaweza kutoeleweka kusaidia wazo hili la Malaika wenye dhambi kwa sasa wapo. Haya yamepimwa katika 'Kumsaka Shetani’ yanapatikana kwa wachapishaji - Mafungu haya ya maneno hayawezi kuruhusiwa kupingana na mafunzo tele ya Biblia kwa kutofautiana na haya yaliyokwisha tolewa.
Tumeacha Kitambo sehemu ya 1:'Mungu ni roho’ (Yohana 4:24)
Katika somo la pili tunafafanua kwa utaratibu zaidi jinsi Roho wa Mungu alivyo. Tunaweza kutoa maelezo kwa ufupi sababu zilizoonyeshwa hapo kwa kusema kwamba roho wa /ya Mungu ni nguvu au pumzi yake ambayo kwa hiyo nafsi yake mwenyewe, Utu wake na tabia, vimedhihirika kwa mwanadamu kwa njia ya matendo yake ambavyo Roho huyo anatimiza.Hivyo'Mungu ni Roho’ kama katika Yohana 4:24 atafsiriwe vema kwa kuwa Roho yake ndiyo inafanya utu wake.
Mungu amesemwa kuwa yumo katika vitu vingi, kwa mfano:-
‘Mungu wetu ni moto ulao’ (Ebr. 12:29)
‘Mungu ni Nuru’ (1 Yoh. 1:5)
‘Mungu ni Pendo (1 Yoh.4:8)
‘Neno (Kiyunani'Lagos’ - Mpango, Lengo,Kusudi, wazo) alikuwa Mungu’ (Yoh 1:1)
Hivyo,'Mungu’ ni sifa yake. Ni kosa lililo wazi kuleta sababu za kupinga kwamba sifa za upendo wa Mungu ni za kuwazika, kwa kuwa tunasoma kwamba 'Mungu ni pendo’ tunaweza kumwita mtu mwingine Mwema wenyewe; lakini hii haina maana kwamba haupo bila mwili ni namna ya kuwepo yeye ndiko kunatudhihirishia wema kwetu.
Roho ikiwa ni nguvu ya Mungu, mara nyingi tunasoma Mungu akiituma au akiiongoza roho yake kutimiliza mabo yake kwa kupatana na mapenzi yake na tabia ya sifa yake. Hata ameelezewa kuwa anaumba roho (Yaani Upepo UV). Kusema kwamba Mungu na roho yake katika maana safi iliyo halisi ni msemo ule ule kwa namna nyingine - katika maana inakuwa Uwepo wa Mungu.
Mifano ya Mungu akiiongoza Roho yake ni mingi, inaonyesha mtengano wa Mungu na Roho yake:-
‘Yeye (Mungu) aliyetia kati yao Roho yake mtakatifu’ (Isa. 63:11)
‘Nitatia Roho yangu (Mungu) juu yake (Yesu )’ ( Math.12:18)
‘Baba huwapa Roho mtakatifu’ (Luk. 11:13)
‘Roho akishuka kama hua toka Mbinguni’ (Yoh. 1:32)
‘Nitawamwagia watu wote Roho yangu’ (Matendo. 2:17).
Kwa kweli ushahidi juu ya 'Roho wa Mungu’ ni uhakika wa kutosha kuwa Roho sio Mungu mwenyewe. Tofauti hizi kati ya Mungu na Roho ni shida nyingine ilio kwa wale wanao amini kuwa Mungu ana Nafsi'Tatu’ ambazo Mungu amelingana na Yesu na Roho Mtakatifu. Jambo hili kama lingekuwa la kweli, na kama Mungu amedhaniwa kuwa sio mtu, basi halikadharika hata Yesu naye sio mtu halisi.
Kwa umuhimu sana, Mungu asiye mtu hata sala kuelekea kwake inakuwa haina maana, kwenye alama ambayo sala ni mazungumuzo kati ya fahamu zetu na wazo la Mungu ambalo lipo katika akili zetu. Daima tunakumbushwa kwamba tunamwomba Mungu ambaye ana Umbo makao yake yapo Mbinguni (Mhu. 5:2; Math. 6:9,5:16, 1Fal. 8:30) na kwamba Yesu sasa yuko mkono wa kuume huko ili kutoa maombi yetu mbele zake (1Pet. 3:21, Ebr. 9:24).
Ikiwa Mungu si mtu binafsi, maneno haya yametolewa bila kuwa na maana. Bali, Mungu akieleweka kuwa ni wa kweli, Baba mwenye upendo, Sala ya kumwomba inakuwa ya kweli, Jambo lililowazi na dhahiri - hasa tukizungumza na mtu mwingine ambaye tunamwamini ana mapenzi sana na anaweza kujibu.
Tumeacha Kitambo sehemu ya 2:'Matumizi ya jina la Mungu’
Tumefahamu kwamba Jina la Mungu na hilo la mwanae Yesu yana maana ya kina sana. Tunaposema 'Mungu’ tunagusa juu ya kila mwelekeo wa kusudi lake la Ajabu la upendo na kweli. Ya kwamba Jina la Mungu litumike bure kama upole usio na maana au kwa maelezo ya kukasirisha, ni moja ya mambo ambayo mtu hufanya na kumnena vibaya zaidi Muumba wake. Kwa sababu hii kila mtu anayetaka kumpendeza Mungu na kumheshimu atafanya kila jitihada kutotumia vibaya Jina la Mungu kirahisi- rahisi. Katika jamii ulimwenguni pote kufuru hii imekuwa sehemu ya kawaida kwa Lugha za siku hizi; Kukatisha ile iliyokuwa ni tabia ya mazoea haita kuwa kazi rahisi. Sala ya kweli ya kuomba msaada wa Mungu hakika itasikika. Wale ambao wapo ndani ya shughuli yetu ya kuwaongoza na kuwavuta, Mf. Watoto, pia watakumbushwa hatari ya kukufuru:”Maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia alitajaye jina lake bure (Kum. 5:11)
Kwa upande mwingine wapo wale wanaosisitiza kwamba tusipotumia maneno ya Kiebrania Yahweh au Yehova (Njia tofauti ya kutamka neno lile lile) Tunapozungumuza kuhusu Mungu, wakati huo tunakuwa tumepotea sana. Miongoni mwao zaidi ya hawa ni Chama cha mlinzi, wanasisitiza kuwa Mkristo asipojiita mwenyewe ni'Shahidi wa Yehova’ Basi hana uhusiano na Mungu.
Kwa kufanya hivi, watu hawa wanatumia jina takatifu la Mungu na la ajabu kuchochea aina fulani ya mfumo wa Imani wa kuelimisha kiroho, ambapo wanawadharau watu wengine tu kwa matamshi au matumizi ya neno moja. Hii sio kusema kuwa ni vibaya kutumia Jina la Mungu; Hasa kweli linafaa kutumika kwenye Sala zetu wenyewe mara tukibatizwa kwa usahihi katika Jina lake. Ingawa hivyo, Agano Jipya halitupatii ishara yoyote kuwa hili ni lazima au inatakiwa na Mungu. Aliongoza kuandika Agano Jipya hivyo basi liliandikwa kwa Kiyunani (Kigriki) likitumika neno moja la'Mungu’ -‘theos’ likiwa na maana “Mtu mkubwa”.
Hakuna tofauti iliyofanywa ndani yake kati ya'Mungu’ na 'Yahweh’ wala haipo amri yoyote dhahiri inayohusiana kwa waamini wakiwa ni jumuiya wajiiteje.Petro anamsema mwamini kuwa ni “ Mkristo” kuliko kumwita ni'Mtu wa Yehova’ au jambo lingine kama hili (1 Petro 4:16) kutilia mkazo zaidi katika matumizi ya Jina la 'Yehova’ kunapelekea kupunguza thamani ya kazi na Nafsi ya BWANA'Yesu’ kwa njia hii ambayo wakristo wengi wa kiinjili wanatia msukumo zaidi kwenye jina na kazi ya Yesu huku wakiacha kuangalia nafsi ya nguvu zaidi iliyo ya Mungu.
Majina mengine ambayo jumuia ya waaminiao ya wakristo wa kwanza waliyojiita wenyewe, hayatii ndani jina la Yehova:-
‘Jamii ya Israeli’ (Ef. 2:12)
‘Mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza’ (Ebr. 12:23)
‘Kanisa lake Mungu’ (Matendo 20:28)
‘Kanisa la Mungu aliye hai, Nguzo na Msingi wa kweli’ (1 Timotheo 3:15)
‘Nyumba ya Mungu’ ( 1 Timotheo 3:15)
Tunapopita, ujue kuwa waamini hawakujiita wenyewe'Wakristo’. Neno hili maana yake lilikuwa la kuvunja heshima, hawa watu wa Kristo walibezwa na maadui zao.
Tumeacha Kitambo sehemu ya 3: 'Ufunuo wa Mungu’
Kinachufuata sio rahisi kukishika chote wakati tunaposoma kwanza,lakini umuhimu wa jambo tunalolizungumzia litakuwa dhahiri kadri masomo yake yanavyosonga mbele. Tunajumuisha kwenye maana hii ili uliache somo hili lote Msingi wa Biblia ukisha pimwa wenye ufunuo kuhusu Mungu mwenyewe.
Jina la Mungu laweza kuchukuliwa na yeyote ambaye amemchagua kujifunua au kujidhihirisha yeye mwenyewe. Hivyo watu na Malaika sawa sawa na Yesu huweza kuchukua jina la Mungu. Hili ni jambo la muhimu ambalo linatufunulia mengi ya Biblia. Hata mwana anaweza kuchukua jina la Baba; ana mambo mamoja na Baba yake, anaweza kuwa na jina lile lile la kwanza- lakini si mmoja na kuwa mtu yeye yule kama Baba. Kwa njia hiyo hiyo mwakilishi wa kundi anaweza kusema kwa niaba ya kundi, anaweza kumpigia mtu wa kwenye shughuli na kusema, Haloo ! hapa ni wakulima, Si Bw. Wakulima, bali anachukua jina lao kwa kuwa anafanya kazi kwa niaba yao. Basi hiyo hata kwa Yesu ilikuwa hivyo.
MALAIKA HUCHUKUA JINA LA MUNGU
Tumeambiwa katika Kutoka 23:20,21 ya kwamba Mungu aliwaambia watu wa Israeli kuwa Malaika atawatangulia mbele yao;'Jina langu limo ndani yake’, waliambiwa. Jina lake Mungu ni'Yahweh’. Basi, Malaika huchukua jina la Yahweh, na hivi anaweza kuitwa Yahweh, au BWANA kwa herufi kubwa neno BWANA linatokana na Yahweh, katika Biblia UV ya Kiswahili ni sehemu moja tu Zaburi 89:8 utakuta neno
YAHU = YAHWEH. Tumeambiwa kuwa katika kutoka 33:20 Mtu hataniona uso akaishi; lakini katika Kutoka 33:11 tunasoma kwamba “BWANA”(Yahweh) alinena na Musa uso kwa uso, kama mtu anaposema na rafiki yake - Yaani kirafiki. Hakuwa ni BWANA, Yahweh mwenyewe alikuwepo, aliyenena na Musa uso kwa uso, Kwa kuwa hakuna mtu anayeweza kumwona Mungu yeye mwenyewe. Alikuwa ni Malaika aliyechukua jina la Mungu ndiye aliye fanya hivyo, na tunasoma habari za BWANA akisema uso kwa uso na Musa wakati hasa ni Malaika aliyefanya hivyo (Mdo. 7:30-33).
Ipo mifano mingine mingi ya maneno' Mungu' na BWANA ikitaja Malaika wakiwa Mungu mwenyewe. Mfano mmoja ulio wazi ni Mwa. 1: 26 “Mungu (Malaika) akisema, na tufanye mtu kwa mfano wetu”
WATU NA JINA LA MUNGU
Moja ya maneno ambayo yanayosaidia sana katika kuelezea yote haya ni katika Yohana 10:34-36. Hapa Wayahudi walifanya kosa ambalo wengi wanaoitwa'Wakristo’ wanafanya leo. Walidhani kuwa Yesu alikuwa anasema kuwa yeye ni Mungu mwenyewe. Yesu alisahihisha kwa kusema “Haija andikwa katika sheria yenu, nimesema Ninyi ni Mungu ? Ikiwa aliwaita Miungu ….. inakuwaje mimi ….” Mnaniambia ninakufuru, kwa sababu nalisema, Mimi ni mwana wa Mungu ? Yesu kwa kweli alikuwa anasema 'Katika Agano la Kale watu waliitwa Miungu; mimi nasema ni mwana wa Mungu, basi imekuwaje mnaudhika sana? Yesu kwa kweli alikuwa ananukuu toka Zab 82 mahali ambapo waamuzi wa Israeli waliitwa'Miungu’.
Kama ilivyoonekana, Jina kamili la Mungu katika Kiebrania ni 'Yahweh Elohim’ likiwa na maana, Nitadhihirika katika kundi la wenye nguvu. Waamini wa kweli ni wale wengi wenye nguvu katika maana ndogo ya maisha haya nao watakuwa na nguvu tele kwenye Ufalme. Kwa mlinganisho huu wote umeonyeshwa kwa Isa. 64:4 na 1 Kor.2:9.
“Watu hawakusikia, wala kufahamu kwa masikio, wala jicho halikumwona Mungu, ila wewe, atendaye mambo kwa ajili yake amngojaye” Paulo ananukuu mstari huu katika 1 Kor.2:9-10: Imeandikwa, Jicho halikuyaona, wala sikio halikuyasikia wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu, mambo ambayo Mungu amewaandalia wampendao. Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Fungu la maneno katika Isa. 64:4 linasema hakuna hata mmoja isipokuwa Mungu anaweza kufahamu mambo aliyowaandalia waamini; Lakini 1Kor. 2:10 mstari unasema kwamba mambo hayo yamefunuliwa kwetu, hivyo katika maana sisi ni “Mungu”: sio Mungu mwenyewe katika utu, bali ufunuo wa Mungu kwa matokeo kuwa tumebatizwa katika jina lake na kujua Ukweli.
YESU NA JINA LA MUNGU
Sio jambo la kushangaza kwamba Yesu, Ikiwa ni mwana wa Mungu na ufunuo wake mkuu kwa watu, Pia naye atachukua jina la Mungu. Aliweza kusema “Nimekuja katika jina la Baba yangu” (Yoh.5:43). Kwa utii wake, Yesu alipaa kwenda mbinguni, naye Mungu akampa jina lipitalo majina - Jina la Yahweh, la Mungu mwenyewe
(Fil. 2:9).basi hii ndiyo sababu tunasoma Yesu anasema katika Uf 3:12 “Nami nitaandika juu yake (Mwamini) Jina la Mungu wangu……na jina langu mwenyewe, lile jpya”Kumbuka Yesu alitoa kitabu cha Ufunuo miaka mingi baada ya kupaa kwenda mbinguni na akiisha kupewa jina la Mungu, kama ilivyoelezwa katika Wafilipi 2:9.
Hivyo anaweza kuliita jina la Mungu “Jina langu Jipya”; Jina ambalo hivi karibuni alipewa. Sasa tunaweza kuelewa vema Isaya 9:6, mahali ambapo kuhusu yeye tumeambiwa “Jina lake (Ujue kuwa) utaitwa, Mshauri wa Ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, ….” Huu ni Unabii wa kwamba Yesu atachukua majina yote ya Mungu ya kwamba atakuwa ni ufunuo wote wa Mungu kwetu.Na ndivyo kwa maana hii aliitwa “Emmanueli” maana yake 'Mungu ni pamoja nasi’ ingawa yeye hakuwa Mungu.
Somo La Kwanza : Maswali
1.Ni nini kitakachotusaidia zaidi kuamini Mungu ?
-
Kwenda Kanisani
-
Maombi na Kusoma Biblia
-
Kuzungumuza na Wakristo
-
Kutazama maumbile.
-
Yapi ya haya yafuatayo ni ufafanuzi sahihi zaidi wa Mungu ?
-
Ni wazo tu katika mioyo yetu
-
Kipande cha Roho katika Hewa
-
Mungu Hayupo
-
Mtu halisi wa Umbo
-
Je ? Mungu ni
-
Ummoja
-
Utatu
-
Miungu wengi katika mmoja
-
Haiwezekani kufafanua kwa njia ya yoyote
-
Jina la Mungu' Yahweh Elohim’ lina maana gani ?
-
Yeye atakaye kuwa
-
Atakayedhihirika katika kundi la wenye nguvu
-
Mkuu
-
Nguvu
-
neno'Malaika lina maana gani ?
-
Kama mtu
-
Aliyefunikwa na Mabawa
-
Mjumbe
-
Msaidizi
-
Je ? Malaika anaweza kutenda Dhambi ?
-
Ni kitu gani kinacho kudhihirishia kuwa Mungu yupo ?