2.1 Roho ya Mungu: Ufafanuzi
Mungu akiwa ni mtu halisi (ieleweke kuwa tunaposoma mtu hatuna maana kuwa ni Mwanadamu) kwa sababu hiyo anayo mawazo na hisia, basi itegemewe kuwa atakuwa na namna nyingine ya kushirikiana mawazo na nia yake pamoja nasi, watoto wake na kwa kutenda kazi katika maisha yetu kwa mfano ambao una tabia ya sifa yake.Mungu anafanya mambo yote haya kwa 'Roho’ yake kama tunataka kumjua Mungu na kuwa na uhusiano wenye matendo pamoja naye, tunahitaji kufahamu jinsi hii “ Roho ya Mungu” na namna inavyotenda kazi.
Sio vyepesi kafafanua neno 'Roho’ hasa lina maana gani, ikiwa uliwahi kwenda kwenye sherehe fulani, tuseme harusi, unaweza kutoa maelezo ya jinsi mambo yalivyokwenda 'Watu waliohudhuria walikuwa na Roho nzuri’ Kwa msemo huu tunaelewa Kuwa una maana kwamba watu walikuwa wakarimu, wenye tabia nzuri n.k. mambo yote hayo yanafanywa na neno 'Roho’ iliyokuwepo pale. Hali kadharika Roho ya Mungu kwa njia nyingine inafanya muhutasari wa kila jambo linalo muhusu yeye. Neno la Kiebrania lililotafsiriwa “Roho” kwa lugha yetu katika Agano la Kale kwa uwazi kabisa limefafanuliwa Kuwa ni “Pumzi” au “nguvu”; kwa hivi roho ya Mungu ni 'Pumzi’ yake, Nafsi ya Mungu kabisa, ikieleza mawazo yake. Tutatoa mifano ya neno 'Roho’ lilivyotumika kuhusu mawazo ya mtu mwingine au mapenzi katika somo la 4.3. Ni dhahiri kwamba Roho sio tu inataja tupu nguvu ya Mungu ni kutoka Warumi 15:19 “Nguvu ya Roho ya Mungu”
Ni mafundisho ya Biblia yaliyo ya kawaida ya kwamba jinsi mtu afikirivyo anajieleza katika matendo yake (Mithali. 23:7, Mathayo. 12:34); mawazo kidogo ya matendo yetu wenyewe, yanadhibitisha jambo hili. Tunafikiria kitu fulani na kisha tunakitenda. “Roho” yetu au nia inaweza kuonyesha juu ya ukweli kwamba tunaumwa njaa na tunahaja na chakula. Tunaona ndizi zimo jikoni, hivyo nia ya'Roho’ wakati huo inabadilika na kuwa tendo. Tunanyoosha mkono na kuchukua ndizi, tunamenya na kula. mfano huu rahisi unaonyesha kwa sababu gani neno'Roho’ lina maana mbili zote Pumzi au Nia, na vile vile Nguvu.Roho yetu ya nafsi yetu, yanatajwa mawazo yetu na hivyo pia matendo tunayofanya ya kuonyesha mawazo hayo au mapenzi yaliyo ndani yetu. Kwa kadri ya utukufu zaidi, Roho ya Mungu ipo hivyo hivyo, ni nguvu inayoonyesha nafsi ya utu wake, mapenzi na kusudi. Mungu anafikiri na hivyo anatenda mambo. “………Kama vile nilivyoazimia (Yaani nilivyofikiria), ndivyo itakavyokuwa, na kama nilivyokusudia, ndivyo itakavyotokea”.
NGUVU ZA MUNGU
Mafungu mengi ya maneno yanaonyesha Roho ya Mungu na nguvu zake. Kwa kuumba Ulimwengu,’ Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. Mungu akasema, iwe Nuru:'ikawa nuru’ (Mwa.1:2,3)
Roho ya Mungu ilikuwa ni nguvu / uweza ambao vitu vyote, kama Nuru viliumbwa.'Hizo mbingu hupambwa kwa Roho yake, mkono wake umemchoma nyoka aendaye mbio’ (Ayubu. 26:13).'Kwa neno la bwana mbingu zilifanyika: na jeshi lake kwa pumzi ya kinywa chake’ (Zab. 33:6). Basi, Roho ya Mungu ni maelezo ya:-
Pumzi yake
Neno lake
Mkono wake
Kwa hiyo ni kwa nguvu zake anafanya vitu vyote. Waumini huzaliwa mara ya pili kwa mapenzi yake (Yoh. 1:13). Ambayo ni Roho yake (Yoh. 3:3-5). Mapenzi yake yanafanya kazi kwa Roho. Akiunena uumbaji wote wa asili, tunasoma “Waipeleka Roho yako, wanaumbwa: nawe (kwa Roho yako) waufanya upya uso wa nchi” (Zab.104:30). Hii Roho / Nguvu vile vile inavihifadhi hai vitu vyote, sawa sawa na kuumbwa kwao. Ni rahisi kudhani kwamba maisha haya yamepatikana kwa bahati bila kuingizwa Roho ya Mungu. Ayubu, mtu aliyechoshwa na maisha haya, alikumbushwa na Nabii mwingine: “(Mungu) akajikusanyia Roho yake na pumzi zake; wenye mwili wote wataangamia pamoja, nao wanadamu watarejea Kuwa mavumbi”(Ayubu. 34:14,15).Alipoondoka katika bonde la mfano mmoja wa huzuni, Daudi alimwomba Mungu aendelee kumtegemeza na Roho hii, yaani, kuhifadhi uhai wake (Zab. 51:12).
Tutaona katika somo la 4.3 Roho ambayo tumepewa sisi sote na viumbe inayohifadhi uhai wetu. Ndani yetu tuna “Pumzi ya Roho ya uhai” (Mwa. 7:22) tuliyopewa na Mungu wakati wa kuzaliwa (Zab. 104:30; Mwanzo. 2:7). Hivi inamfanya awe ni Mungu wa Roho za wenye mwili wote. (Hes. 27:16; linganisha Ebra. 12:9). Kwa Kuwa Mungu ni mwenye nguvu ya uhai unaohifadhi viumbe vyote, Roho yake ipo kila mahali. Daudi alitambua kwamba kwa Roho yake Mungu daima alikuwa naye popote pale alipokwenda, na kwa Roho/ Nguvu aliweza kujua kila kona ya moyo wa Daudi unavyofikiri. Hivyo, Roho ya Mungu ndio inamfanya awe kila mahali, ingawa yeye mwenyewe makao yake ni mbinguni.
“Wewe wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu; umefahamu wazo langu tokea mbali..…Niende wapi nijiepushe na Roho yako? Niende wapi niukimbie uso wako ? Nikikaa pande za mwisho wa bahari; huko nako mkono wako wa kiume utanishika (Yaani, kwa Roho)” (Zab.139:2,7,9,10).
Jambo hili likifahamika vema linatudhihirishia Mungu kuwa Mungu ni mwenye nguvu sana, Nafsi itendayo kazi, watu wengi wamepevuka wakiwa hawajui vema'Kusadiki kwa Mungu’, katika mioyo yao Mungu amekuwa na wazo tu akilini akiwa ni sanduku jeusi kumjua Mungu wa kweli na uwepo wake kabisa akituzunguka pande zote kwa roho yake, kunaweza kubadili sana wazo letu la uhai.
Tumezungukwa na Roho yake,kila siku tunashuhudia matendo yake, yanayotufunulia Mungu alivyo. Kwa yote haya, Daudi alipata faraja kikamilifu nia yake ilipobadilika:”Maarifa hayo ni ya Ajabu; yanishinda mimi” (Zab. 139:6) Lakini majukumu huja na maarifa haya; inatubidi tufahamu kwamba matendo na mawazo yetu yapo wazi kwenye mtazamo wa Mungu. kama tunapima hali yetu mbele zake, hasa tukifikiria juu ya Ubatizo, tunahitaji kukumbuka hii moyoni. Maneno makuu ya Mungu kwa Yeremia yanatumika kwetu pia. Je! mtu yeyote aweza kujificha mahala pa siri, nisimwone? asema Bwana. Je! mbingu na nchi hazikujawa (Kwa Roho) nami (Yer.23:24)
ROHO MTAKATIFU
Tumeona ya kwamba Roho mtakatifu ni wazo pana kufahamu; ni nia na mwelekeo wake, pia ni nguvu inayoweka mawazo yake yafanye kazi. “Maana (Mtu) aonavyo nafsini mwake ndivyo alivyo - yaani, jinsi mtu anavyowaza moyoni ndivyo alivyo, (Mithali 23:7); hivyo basi, ndivyo Mungu mawazo yake yalivyo, kwa maana hiyo ndivyo ilivyo Roho yake (Yohana 4:24). Ingawa hii haina maana ya kwamba Mungu si yake mwenyewe (Tazama tumeacha kitambo tulichoandika sehemu ya 1). Kutusaidia kuelewa upana huu wa roho ya Mungu, mara nyingine tunasoma'Roho wake Mtakatifu’.
Neno “Roho Mtakatifu” linapatikana karibu kila sehemu katika Agano Jipya peke yake. Biblia ya kiswahili maneno Roho ya Bwana na'Roho Mtakatifu’ yametumika wazi. Hili ni sawa na mafungu ya maneno'Roho ya Mungu’ au Roho ya Bwana. Hili lipo dhahiri katika maneno kama ya Matendo 2, yanatoa taarifa ya kumwagiwa mitume Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste. Petro alisema kwamba Unabii wa Yoel ulikuwa unatimia, ambapo imesemwa nitawamwagia'Roho yangu’ (Mdo. 2:17). Tena, katika
Luk. 4:1 tunasoma habari ya kwamba Yesu “akiwa amejaa Roho Mtakatifu alirudi toka Yordani; baadae kwenye sura hiyo hiyo Yesu akasema Unabii wa Isaya 61 unatimia. “Roho ya Bwana Mungu i juu yangu”katika masuala yote mawili (na katika mengi mengine) Roho Mtakatifu amelinganishwa na neno lililo katika Agano la Kale “Roho ya Mungu”.
Fahamu vile vile ni jinsi gani Roho Mtakatifu alivyo sambamba na nguvu za Mungu kwenye mafungu ya maneno yafuatayo:-
“Roho Mtakatifu atakujilia juu yako (Mariamu), na nguvu zake aliye juu zitakufunika kama kivuli” (Luk. 1:35)
“Nguvu za Roho Mtakatifu ……. Kwa nguvu za ishara na maajabu, katika nguvu za Roho Mtakatifu” (Rum. 15:13-19)
“(Kuhubiri) Injili yetu kumekuja …… katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu” (1 Thes. 1:5)
“ Ahadi ya Roho Mtakatifu kwa wafuasi ilisemwa kuvikwa uwezo toka juu” (Luk. 24:49).
Yesu mwenyewe “alitiwa mafuta ya Roho Mtakatifu, na nguvu” (Mdo. 10:38).
Paulo aliweza kutoa mahubiri yake kwa kuonyesha nguvu za Mungu za bila kukanushwa.
“Neno langu na kuhubiri kwangu …….Kwa dalili za Roho na nguvu” (1 Kor.2:4)
2.2 Maongozi ya Mungu
Roho ya Mungu tumeifafanua ya kwamba ni Uweza wake, Mawazo, Maelekeo au tabia ambayo anaifunua kwa matendo yanayofanywa na Roho yake. Tulitaja katika sehemu iliyotangulia jinsi gani Roho ya Mungu ilionekana kazini katika uumbaji: “ Hizi mbingu hupambwa kwa Roho yake” (Ayubu. 26:13) -Roho ya Mungu ikatua juu ya uso wa maji kuleta viumbe vilivyopo (Mwa. 1:2). Hata hivyo tunasoma kwamba'Kwa neno la Bwana mbingu zilifanyika, na jeshi lake lote . (Zab. 33:6). Kama ilivyoonyeshwa mfano wa taarifa iliyo katika mwanzo ya Kuwa 'Mungu alisema’ vitu viliumbwa, vikatokea. Kwa hiyo, Roho ya Mungu imeonyeshwa sana kabisa neno lake - kadri maneno yetu yanavyoonyesha mawazo yetu ya ndani na matakwa - yetu halisi kwa usahihi kabisa. Kwa busara Yesu alisema'Kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake’ (Mathayo. 12:34) Basi, kama tunataka kutawala maneno yetu, kabla ya yote yatupasa tugeuze mawazo yetu. Hivyo neno la Mungu, ni wazo la Roho yake au mawazo. Hii ni baraka ya kwamba katika Biblia tuna maneno ya Mungu yameandikwa ili tuweze kuifahamu Roho ya Mungu au nia yake. Mungu alifanya muujiza huu kwa kueleza Roho yake katika maneno yaliyoandikwa kwa njia ya KUVUVIWA. Neno hili msingi wake umezunguka neno'Roho’
KUVUVIWA -KUONGOZWA NA ROHO
“Roho” inamaanisha “Pumzi” au kupumua, “Kuvuviwa” maana yake ni “ Kupuliziwa Pumzi”. Hapa pana maana ya kwamba maneno ambayo watu waliandika “Wakivuviwa” toka Mungu yalikuwa ni maneno ya Roho ya Mungu. Paulo alimtia moyo Timotheo kwamba asijione kuwa mzoefu wa Biblia hata asahau ukweli kwamba ni maneno ya Roho wa Mungu, na kwa sababu hiyo tumepewa yote ambayo twahitaji ili kwamba tuwe na elimu ya kweli katika kumjua Mungu:-
“tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yanaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika KristoYesu.Kila andiko lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza na kwa kuwaadibisha katika haki, ili mtu wa Mungu awe kamili; amekamilishwa apate kutenda kila jambo jema (2 Tim. 3:15 -17)
Ikiwa kuvuviwa na maandiko kunaweza kutoa elimu ya jumla, basi haipo haja ya kuwa na 'Nuru ya ndani’ nyingine ya kutuonyesha ukweli juu ya Mungu. Lakini ni mara ngapi watu husema mawazo yao wenyewe na ujuzi kuwa ndio chanzo cha wao kumjua Mungu ! ikiwa linakubalika neno lenye kuvuviwa na Mungu kikamilifu linatosha kumwandaa mtu katika maisha ya Ukristo, hakuna haja ya nguvu nyingine ya haki katika maisha yetu. Kama ipo hii haja, basi neno la Mungu halijatuandaa kikamilifu, kama Paulo alivyotuahidi Kuwa litafanya hivyo. Kushika Bibilia mikononi mwetu na kuamini kwamba Biblia ni neno la Roho ya Mungu huchukua imani nyingine kabisa. Israeli walivutwa kusikiliza kile ambacho Mungu katika neno lake, kama ilivyo kwa “Wakristo” wengi siku hizi. Sisi sote tunahitaji kwa uangalifu kuwaza katika Waebrania 4:2:-
“Sisi nasi tumehubiriwa habari njema vile vile kama hao (Israeli walipokuwa jangwani):Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu halikuchanganyika na imanindani yao walisikia.
Badala ya kusimama katika imani timilifu iliyo kwenye nguvu za Roho / neno la Mungu lililosikiwa, Kiroho ni rahisi kuvutwa na kuchukua njia ya mkato. Kwa kudhani kwamba nguvu ya haki hutujia ghafla juu yetu itakayo tufanya tubadilike mbele za Mungu, kuliko kujua inabidi kupata uchungu wa kuyaleta maisha yetu kutii neno laMungu, kwa hiyo kuruhusu roho ya Mungu ivute mioyo yetu kwa kweli.
Kutopenda kufahamu mno nguvu kubwa za kiroho zilizo ndani ya neno la Mungu matokeo yake'Wakristo’wamediliki kuhoji ikiwa maandiko yote tele yameandikwa kwa uongozi wa roho ya Mungu. Wamedokeza kwamba mengi sana tuyasomayo ndani ya Biblia yameandikwa na watu wenye busara zamani kwa mawazo yao tu. Lakini kwa matokeo, Petro anakomesha mawazo ya maneno ya jinsi hii:-
“Nasi tuna lile neno la Unabii lililo imara zaidi, ambalo mkiliangalia kama taa….Mkijua neno hili kwanza, (Kuwa muhimu) ya kwamba hakuna Unabii katika maandiko upatao kutafsiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu; Bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu (2Petro. 1:19 -21 UV)
“Zaidi ya yote” yatupasa tuamini kwamba Biblia imeandikwa kwa uongozi wa Mungu.kwa sababu hii tumeifanya kuwa mlango wa msingi mmoja katika mapatano ya maneno yanayoelezea mashauri ya Imani ya Kristadelfiani (Christadelphlan statement of faith)
WAANDISHI WA BIBLIA
Kwa hiyo, ni muhimu kabisa kuwa na imani thabiti ya kuwa maandiko yamekuja kwa kuvuviwa na Mungu;bila kuzuiwa na mtu, Waandishi wa Biblia walivuviwa na Roho, kwa sababu hii waliyoandika hayakuwa yao wenyewe. Kwa kuwa neno ndio kweli (Yoh.17:17) linakaripia na kuadibisha (2 Tim.3:16 -17), kwa watu wengi, sio ajabu kuona kwamba neno haliwaelimishi - maana ukweli unauma.Nabii Yeremia alisumbuka sana kutokana na upinzani alioupata kwa sababu ya kusema maneno yaliyovuviwa na Mungu, basi aliamua asiyaandike wala kutangaza maneno aliyopewa. Lakini basi kuandika neno la Mungu ni zao la mapenzi ya Mungu kuliko matakwa ya mwanadamu,'Akaongozwa na Roho ya Mungu’ kwa hiyo akawa hana uchaguzi wa jambo hili.'Umenihadaa, Nami nimehadaika……Nami nikasema sitamtaja wala sitasema tena kwa jina lake, basi ndipo moyoni mwangu kumekuwamo kama moto uwakao, uliofungwa ndani ya mifupa yangu, Nami nimechoka kwa kustahimili, wala siwezi kujizuia’. (Yer. 20:7,9).
Vivyo hivyo, Balaamu alipotaka kuwalaani Israeli, Roho ya Mungu ikamfanya awabariki badala yake
(Hes. 24:1 -13; Kum.23:5)
idadi ya kushangaza ya watu ambao Mungu aliwaongoza kutamka neno lake, walipita kwenye vipindi vya kutopenda kufanya hivyo. Orodha ni ya kuvutia:-
Musa (Kut. 4:10)
Ezekieli (Ezek. 3:14)
Yona (Yon. 1:2,3)
Paulo (Mdo. 18:9)
Timotheo (1 Tim. 4:6 -14)
Balaamu (Hes. 22:24)
Yote hayo yanatudhibitishia tulichojifunza katika 2 Pet. 1:19 -21 ya kwamba neno la Mungu si wazo la watu binafsi, bali ni sababu ya watu kuvuviwa kuandika yaliyofunuliwa kwao. Nabii Amosi alinena “Bwana Mungu amesema, ni nani awezaye neno ila kutabiri ?” (Amosi 3:8) kwa kitambo, Musa alipoteza akili yake mwenyewe, Kule kuvuviwa kwake na Mungu kulikuwa na nguvu sana: “Maagizo hayo yote Bwana alimwambia Musa…….” (Hes. 15:22, 23); maneno haya yalisemwa na Musa hasa (mstari wa 17)
Ushahidi mwingine wa maendeleo haya ni kwamba waandishi wa Biblia hawakutambua kikamilifu mambo waliyokuwa wanaandika. walitafuta maana ya tafsiri sahihi -'Wakafunuliwa kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yenu walihudumu katika mambo hayo’ waliyoandika (1Petro. 1: 9-12) maneno waliyoandika hasa, hayakuwa ni tafsiri yao wenyewe, bali hayo waliyochunguza. Yafuatayo yanatoa mifano iliyodhahiri:-
Daniel (Dan. 12:8 -10)
Zakaria (Zak. 4:4 -13)
Petro (Matendo 10:17)
Kama watu hawa walivuviwa kwa sehemu tu, basi hatuna njia ya kulifikia neno la kweli au Roho ya Mungu.Ikiwa hakika lile waliloandika lilikuwa neno la Mungu, basi, kwa hiyo iliwabidi waingiliwe kikamilifu na Roho ya Mungu wakati wa kipindi cha kuvuviwa pengine neno la Mungu lisingekuwa limehakikishwa. Kufahamu kwamba neno la Mungu ni la kale kabisa, linatupatia zaidi kusudi la kusoma na kutii.'neno lako limesafika sana, kwa hiyo mtumishi wako amelipenda’ (Zab. 119:140)
Kwa hiyo, vitabu vya Biblia ni kazi yake Mungu kwa njia ya Roho yake, kuliko Kuwa na vitabu vya watu.Ukweli wa jambo hili umeonyeshwa kwa kupima jinsi Agano jipya linavyoshuhudia maandishi ya Agano la Kale:-
-Math. 2:5 panasemwa ni jinsi gani 'yaliandikwa na manabii’ Mungu alikuwa anaandika kwa kupitia kwao.
‘Roho Mtakatifu alivyonena kwa kinywa cha Daudi….’ (Mdo. 1:16)
-Hivi ndivyo petro alivyonukuu toka Zaburi: linganisha na (Ebra. 3:7)
-‘Roho Mtakatifu alinena vema kwa kinywa cha Nabii Isaya’ (mdo. 28:25
- ndivyo alinukuu Paulo katika Isaya (Luk 3:4) anasema kama ilivyoandikwa katika chuo cha maneno ya nabii Isaya kuliko kusema, Kitabu cha Isaya tu.
Kwa hiyo wanadamu waliobuni vitabu vya Biblia hawakuwa muhimu kulingana na Wakristo wa kwanza, Ukweli ni kwamba maneno yao yalivuviwa na Roho ya Mungu na ndiyo iliyokuwa ya maana.
Tutamalizia sehemu hii kwa orodha ya mistari inayoonyesha Kuwa Roho ya Mungu imefunuliwa kwetu ndani ya neno lake lililoandikwa:-
-Yesu alisema wazi wazi,'Maneno hayo niliyowaambia……. Ni Roho’ (Yoh. 6:63);Alisema ni ya kuvuviwa toka kwa Mungu.
(Yoh. 17:8, 14:10).
-Tumesemwa ya Kuwa tumezaliwa mara ya Pili pande mbili kwa Roho (Yoh. 3:3-5) na kwa neno la Mungu (1Pet. 1:23)
-‘Tazama nitawamwagia Roho yangu, na kuwajulisheni maneno yangu’ (Mith. 1:23)yanatia pamoja kufahamu neno la Mungu kweli na tendo la Roho yake juu yetu kusoma kitabu bila kuelewa yaliyoandikwa hakuna faida, kwa kuwa Roho / nia ya Mungu huwa hatujafunuliwa.
Kuna usawa kati ya Roho ya Mungu na neno lake katika mafungu ya maneno: “ Roho yangu iliyo juu yako, na maneno yangu niliyoyatia kinywani mwako ….” (Isaya 59:21)‘Kwa ajili ya neno lako, na kwa moyo wako mwenyewe (Roho)’ (2 Sam. 7:21); 'Nami nitatia Roho yangu ndani yenu (katika mioyo yenu, tazama maneno yenyewe)…;
Nitatia sheria yangu ndani yao …… na katika mioyo yao nitaiandika’
(Ezek. 36:27, Yer.31:33).
UWEZA WA NENO LA MUNGU
Roho ya mungu haishuhudii nia yake / madaraka peke, bali pia ni nguvu ambayo yaelezea mawazo hayo, ya kuwa neno /Roho yake sio tu ni taarifa yake; vile vile kuna nguvu inayofanya kazi katika neno hilo
Kuufahamu ukweli uweza huo kutatufanya tuwe na shauku kuutumia; mawazo yoyote ya kutuzuia kusonga mbele yaliyo pamoja na kufanya hivyo yatashindwa kwa elimu yetu na kutii neno la Mungu kutatupatia nguvu tunazohitaji kusonga mbele kutoka mambo madogo ya maisha haya, kuelekea kwenye wokovu. Kutokana na mengi yaliyompata, Paulo aliandika:-
“ Siionei haya Injili (Neno) ya kristo: maana ni uweza wa Mungu uletao wokovu” (Rum.1:16)
Luka 1:37 ameandika jambo lile lile “ Hakuna neno (Roho) lisilowezekana kwa Mungu”.
Kwa hiyo, kujifunza Biblia na kuyaelewa kuyatumia katika maisha yetu ni mwendo unaoendelea. Hauhusiani kabisa na bila kuwa mwema , kujaribu kufundisha elimu ya kibinadamu na vile vile Ukristo wa makanisa mengi wa kujisikia vema, ambako maneno machache yananukuliwa kifupi, lakini hakuna juhudi imefanywa ili kufahamu au kuyatumia. “Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu” 'Kwa amri (Neno) la Uweza (wa Mungu)’ (Ebr. 4:12; 1:3).'Neno la ujumbe wa Mungu ….. litendalo kazi pia ndani yenu ninyi mnaoamini’ (1Thes. 2:13). Kwa neno, Mungu anafanya kazi katika mioyo ya waumini wa kweli, kila saa ya siku.
Ujumbe -Msingi wa Injili unaojifunza basi ni uweza kweli wa Mungu; kama ukiuruhusu kweli kufanya hivyo, Injili inaweza kufanya kazi katika maisha yako na kukubadili; uwe mtoto wa Mungu, ukionyesha Roho / nia ya Mungu kwa kiwango fulani katika maisha haya, ukiandaliwa katika badiliko la kupata mwili wa kiroho wa Mungu Kristo atakaporudi (2Pet. 1:4). Mahubiri ya Paulo yalikuwa katika “Kuonyesha dalili ya Roho na nguvu” (1Kor. 2:4).
Tumezungukwa na hao wenye imani nusu katika Biblia kuwa ni Neno la Mungu, mbali na madai ya kumtumikia Kristo. Kwa mfano mmoja wanadai wanamwamini Mungu, Lakini wanashindwa kufahamu kwamba yeye anaishi kweli. Kwa kukana kabisa kuwa maandiko yamevuviwa, na ukuu wake juu ya mwazo na nia zetu, wanakana nguvu za Mungu. Maneno ya 2 Tim 3:5 yanatujia akilini:'Wenye mfano wa utauwa, lakini wanakana nguvu zake’ yaani, nguvu za neno la Injili
Msimamo wa imani yetu unadhihakiwa na ulimwengu ('Je ! unaamini kama hivyo, Unaamini ?’), ndivyo Paulo na kundi lake la wahubiri: “Kuhubiri neno la msalaba kwao wanapotea ni upuuzi, bali sisi kwetu tunaookolewa ni nguvu ya Mungu” (1Kor.1:18) Tukikumbuka haya yote, hatuwezi kila mmoja kushika Biblia mikononi mwetu na kipimo kikumbwa cha kuiheshimu, kuisoma na shauku zaidi ya kufahamu na kutii. ?.
MWENENDO WA WATU WA MUNGU KATIKA NENO LAKE
Kusoma haraka taarifa za Biblia zaonyesha kwamba waandishi wa Biblia sio tu walitambua kwamba walivuviwa, bali waliwaona waandishi wengine wa Biblia kuwa wanaongozwa na Mungu. Bwana Yesu alikuwa ni bora zaidi katika jambo hili. Yesu aliponukuu toka Zaburi na Daudi, alianza maneno “Daudi katika Roho ……” (Math. 22:43), akionyesha kutambua kwake ukweli wa kwamba maneno ya Daudi yalivuviwa. Vile vile aliyasema,” Maandishi” ya Musa (Yoh. 5:45-47), kwa kuonyesha kwamba alimwamini Musa kuwa aliandika vitabu vitano. (Pentateuch). Wakristo waitwao watafuta makosawakuu katika Biblia wamekuwa na shaka ikiwa Musa aliweza kuandika, lakini ni dhahiri mwenendo wa Kristo unapingana na njia zao. Aliyaita maandishi ya Musa kuwa ni 'amri ya Mungu’ (Marko. 7:8,9)Kundi hilo hilo la wenye mashaka wasioamini wanadai kwamba mengi yaliyo kwenye Agano la Kale ni hadithi, Yesu alisema Malikia wa sheba ukiwa ni ukweli unaofahamika kihistoria (Math. 12:42); hakusema, 'kuwa ni hadithi inayoendelea juu ya Malikia wa sheba ….’
Mwenendo wa Mitume ulikuwa wa hali moja na wa Bwana wao. Umeandikwa kifupi na Petro aliyesema ya kwamba uzoefu wake mwenyewe kusikia maneno ya Kristo kwa masikio yake mwenyewe alipatwa na'Lile neno la Unabii lililo imara zaidi’
(2Pet. 1:19 -21). Petro aliamini kwamba nyaraka za Paulo yalikuwa ni'Maandiko’ zaidi kama'Maandiko mengine’ msemo ambao kwa kawaida umetumika juu ya Agano la kale maandishi yake. Hivyo, Petro aliona nyaraka za Paulo kuwa ni zenye mamlaka kama Agano la Kale.
Yapo mengi ambayo yametajwa katika matendo, Nyaraka na ufunuo katika Injili (kwa mfano, linganisha (Mdo 13:51, Math. 10:14) yakionyesha sio tu kwamba yote yalivuviwa na Roho yeye yule, bali kwamba taarifa za Injili ziliandikwa kwa uongozi wa Mungu na waandishi wa Agano Jipya. Paulo katika (1 Tim. 5:18 ) ananukuu sehemu mbili Kum.25:4 (katika Agano la Kale) na Luka 10:7 kuwa ni'Andiko’. Paulo alifanya kazi nzito ya maana kwamba ujumbe wake ulitoka kwa Kristo, sio kwake mwenyewe (Gal. 1:11 -12; 1 Kor. 2:13; 11:23; 15:3) kazi yake ilitambuliwa na mitume wengine, hivyo Yakobo 4:5 ananukuu maneno ya Paulo kwa Gal. 5:17 kuwa ni “Andiko”
Mungu 'amesema’ nasi kwa Kristo; kwa hiyo hatuna haja na Ufunuo mwingine zaidi (Ebr. 1:2). Yaweza kuonekana kuwa Biblia inataja maandishi mengine yaliyovuviwa yasiyopatikana sasa. (k.m. kitabu cha Yasheri, maandishi ya Nathani, Paulo kwa Wakorintho na waraka wa tatu wa Yohana unadokeza kwamba Yohana aliandika barua ambayo haikutunzwa katika kanisa ambalo Diotrefe alikataa kutii). Ni kwa sababu gani maandishi haya hayakutunzwa kwa ajili yetu ? Ni dhahiri, kwa kuwa mambo yenyewe hayakuwa yanatuhusu sisi.
Mara nyingine imedaiwa kwamba pole pole vitabu vya Agano Jipya vikakubalika kuwa vilivuviwa, Lakini ni hakika kwamba Mitume waliona maandishi ya kila mwingine kuwa yalivuviwa haikosi huku ni kudhibitisha uongo. Ilikuwepo miujiza ya kipawa cha Roho ili kupima ikiwa nyaraka na maneno yaliyodaiwa kuvuviwa kuwa kweli yalikuwa hivyo (1Kor. 14:37, 1Yoh. 4:1, Uf. 2:2). Hii ina maana kwamba nyaraka zilizovuviwa mara moja zilifahamika kuwa zimeandikwa kwa uongozi wa Mungu. Kama ulikuwepo uchaguzi wowote wa Mwanadamu asiyeongozwa kwa yale yaliyoingia katika Biblia yetu, ndipo kitabu kisingekuwa na Mamlaka.
2.3 Vipawa Vya Roho Mtakatifu
Kwa nyakati mbalimbali Mungu alipo shughulika na watu, alituma watumie nguvu zake ('Roho Mtakatifu’) hao watu. Lakini, nguvu hii haikuwa katika namna ya “ Hundi isiyo ya maandishi” kama ilivyokuwa, kuwawezesha kutenda walivyotaka siku zote kutumia Roho huyu Mtakatifu ilikuwa ni kwa kusudi maalumu. Kazi ilipotimizwa vizuri, kipawa cha Roho Mtakatifu kiliondolewa. Yatupasa tukumbuke kwamba Roho ya Mungu hutenda kazi kwa njia ambayo inapelekea mbele kusudi lake lililo moyoni mwake. Mara nyingi lengo lake linaacha muhula mfupi wa mateso katika maisha ya watu ili kuleta karibu kusudi lake la muda mrefu (tazama somo la 6.1) hivyo hatumainiwi huyo Roho Mtakatifu kutumika kutuliza uchungu wa maisha haya katika mwanadamu. Chochote kitulizo hiki kinamalizwa, kitakuwa kwa ajili ya kusudi la hali ya juu kinachoelezea hali ya Mungu kwetu.
Msimamo wa Ukristo wa walio wengi umeonekana kwa namna tofauti kabisa katika Roho Mtakatifu siku hizi; fikira zimetolewa kama kumwamini Kristo kuna thamani fulani kwa sababu ya faida ya mwili, k.m. kuponywa wagonjwa, ambayo Roho Mtakatifu amedhaniwa atatoa uponyaji. Huu utaeleza ni kwa sababu gani nchi zenye vurugu ya vita kama Uganda wamejitokeza watu wanaodai wana vipawa vya Roho ya kuponya na kihistoria mara nyingi kadhia ya jinsi hii ni matukio yanayojitokeza wakati ule ule wanadamu wanapokuwa na shida kubwa. Hii ndani yake yenyewe yanaonyesha madai ya kuwa na Roho katika hali ya mashaka mengine; Ikiwa mtu anatafuta jambo la kumpatia maarifa hayo yaliyo bora kuliko mambo ya mwanadamu yalivyo, ni rahisi kudai limepatikana jambo lingine linalojaza hesabu.
‘Wakristo’ wengi siku hizi wanadai wana vipawa vya Roho ya kutenda miujiza, lakini wanapo ulizwa kuhusu nini hasa madhumni yao, wanadokeza maana isiyotumainiwa. Mungu ametoa Roho yake bila kutengwa kwa kutimiza jambo moja hasa, malengo yaliyo ainishwa. Kwa sababu hii wale ambao walikuwa na vipwa vya Roho walijua hasa watavitumia kwa jambo gani. Basi hawakufaulu tu kwa sehemu katika kufanikiwa kwao walipovitumia. Hii hutofautiana na kushindwa kwingi na matibabu nusu yaliyo na wale wanaodai kuwa na vipawa vya kuponya leo.
Mifano yote ifuatayo inaonyesha sababu dhahiri na mambo yaliyokuwa nyuma ya kupewa vipawa vya Roho. Hapakuwepo hata kidogo masuala haya yoyote yanayozungumziwa kuwa pamoja na vipawa, wala hawakuwepo wenye vipawa walioweza kuvitumia kiasi kama walivyoona inafaa. Kwa sababu tunazungumzia Roho ya Mungu, haidhaniwi kwamba watu waliongoza matumizi yake, kwa kuwa walipewa ili kufahamu matakwa fulani ya Mungu kwa namna yake maalumu, kuliko hivyo vya watu walivyotumia hivyo kwa kitambo (Linganisha Isaya 40:13)
-Mwanzoni katika historia ya Israeli, waliagizwa watengeneze hema lenye madoido, (‘Maskani’) ambalo ndani yake kutakuwa na madhabahu na vitu vitakatifu vingine vitaweza kutunzwa; maelezo yalitolewa jinsi ya kufanya vitu vyote vilivyokuwa vya lazima kwa ajili ya kumwabudu Mungu. Kutimiza hii kazi,Mungu aliwapa watu fulani Roho yake 'Walijazwa Roho ya Hekima ili waweze kushona mavazi ya Haruni …..’ (Kut. 28:3)
-Mmoja wa watu hawa, Bezaleli, “Alijazwa Roho ya Mungu, katika hekima na Maarifa, na ujuzi wa kazi ya kila aina ….. kuwa fundi wa dhahabu, na …. Kukata vito kwa kutiwa mahali …. Na kufanya kazi ya ustadi iwayo yote” (Kut. 31: 3 -5).
Kitabu cha Hesabu 11:14 -17 kinatupatia habari ya jinsi baadhi ya Roho /nguvu aliyopewa Musa ilichukuliwa toka kwake wakapewa wazee wa Israeli, kwa kusudi la kuwawezesha kuamua kwa usahihi manung’uniko ya watu na kumpunguzia mzigo Musa. Kabla ya kifo chake, kipawa cha Roho kiliamishwa kutoka kwake akapewa Yoshua ili kwamba, naye vile vile, aweze kuwaongoza watu wa Mungu kwa Uzuri (Kut. 34:9)
Tangu wakati ule watu wa Israeli walipoingia nchi yao hadi kupata mfalme wao wa kwanza (Sauli) waliongozwa na watu walioitwa waamuzi. Wakati wa kipindi hiki watu walionewa na adui zao, lakini kitabu cha waamuzi kimetupatia taarifa jinsi Roho ya Mungu ilivyowajilia baadhi ya waamuzi, kwa muujiza wawaokoe Israeli toka kwa wavamizi wao Othiniel (Amu. 3:10), Gideoni (Amu. 6:34) na Yefta (Amu. 11:29) hawa wanaonyesha mifano hii:-
Mwamuzi mwingine, Samsoni, alipewa Roho ya kumuua Simba
(Amu. 14:5,6); kuua watu 30 (Amu. 14:19) na kukata kamba alizofungwa (Amu. 15:14). Huyu'Roho Mtakatifu’ Hakuwa na Samsoni siku zote alimjilia kutimiza mambo dhahiri na kisha aliondolewa.
Mungu alipokuwa na ujumbe maalum na watu wake, Roho ilimwongoza mtu mmoja miongoni mwao kunena neno la Mungu. Ujumbe ulipokwisha, kipawa cha Roho ya kutamka kwa niaba ya Mungu kiliondolewa mara moja, matamshi ya mtu yanakuwa ni yake mwenyewe tena sio ya Mungu. Moja ya mifano mingi:-
“Roho ya Mungu ikamjia Zekaria ……naye akawaambia (Watu), Mungu asema hivi, kwa nini ninyi kuzihalifu amri za Bwana….? (2 Nyak. 24:20)
Mifano mingine tazama 2 Nyak. 15: 1,2 na Luk. 4:18,19.
Kutokana na jambo hili, inakuwa bayana kwamba kupokea kipawa cha kutumia Roho ya Mungu kwa kusudi maalumu haikuwa
Ni uhakika wa wokovu
Ni jambo lililodumu katika maisha yote ya mtu
Ni nguvu ya Roho iliyojificha ndani yao
Ni jambo fulani linalopatikana kwa mtu kusikia furaha moyoni mwake
Inabidi kusema kwamba kumekuwa na sababu nyingi zisizodhahiri kuhusu vipawa vya Roho mtakatifu. Watu wanadai hupokea Roho Mtakatifu, na katika kumbi nyingi za Injili mhubiri hupunga mikono ya 'Kupokea vipawa vya Roho’ mbele ya wale wanaoona 'Wanampokea Yesu’ lakini swali inabidi liulizwe, Vipawa gani ? yaonekana kwamba watu hawajui hasa ni kipawa gani wanacho. Samsoni alipewa kipawa cha Roho kuua Simba (Amu. 14:5,6); alipomwona mnyama akiunguruma alijua hasa ni Roho gani aliyopewa na kwa sababu gani. Moyoni mwake hakuwa na shaka yoyote. Hii ni tofauti ngumu kwa wale ambao siku hizi wanadai wamempokea Roho Mtakatifu, huku hawawezi kufanya tendo lolote lililodhahiri, wala kujua ni vipawa gani walivyodhani wanavyo.
Bila shaka hakuna njia nyingine bali kumalizia kwamba watu wa jinsi hii waliwahi kuwa na mkazo wa mawazo mioyoni yaliyounganika na Ukristo, na mzunguko uliofuata katika mwenendo wa maisha yao wakiwa wameachwa na fikira ngeni za upya ndani yao wenyewe. Wakijua hivi, wameshika maneno ya Biblia juu ya vipawa vya Roho Mtakatifu, wakimalizia kwa kusema “Hivi inanibidi kuona mambo yakitendeka ! naye mchungaji wao walio na furaha huwapapasa kichwani na kusema,'Ni sawa hasa !
Bwana asifiwe ! akitumia mambo haya kuwa ni 'Ushahidi’ anapojaribu kuwadhibitishia wengine wampokee Roho Mtakatifu. Chanzo cha dhihaka hii hutokana na kukosa kuielewa Biblia tangu mwanzo wa elimu aliyokuwa nayo mtu kabla ya 'Kuongoka’ kwao wanakodhania.Tunaposhindana na udanganyifu wa mawazo yetu wenyewe (Yer. 17:9), yatupasa tutunze nyayo zetu juu ya mwamba ulio Imara ya mambo ya Biblia. Hakuna humu kinachohitajika wazi zaidi kuliko kujifunza ni jinsi gani Roho ya Mungu hufanya kazi. sote tunapenda kuwaza Kuwa nguvu za Mungu zatenda kazi nasi katika maisha yetu. Lakini ni jinsi gani na kwa sababu gani anafanya hivyo ? Je ! tuna vipawa kweli vya Roho kama watu walio katika taarifa za Biblia ? kama kweli tunataka kumjua Mungu na Kuwa na uhusuiano ulio hai naye, tutatambua umuhimu unaofaa kuelewa mambo haya.
SABABU ZA KUWA NA VIPAWA KATIKA
KARNE YA KWANZA
Tunapokumbuka mambo makuu tuliyojifunza tayari kuhusu vipawa vya Roho ya Mungu, sasa tunageukia taarifa iliyomo katika Agano Jipya juu ya vipawa vya Roho vilivyokuwa na kanisa la Kwanza (Yaani, vikundi vya waumini walioishi kwenye kizazi kilichokuwapo baada ya kipindi cha Yesu.)
Kristo agizo lake la mwisho, kwa mitume lilikuwa kwenda ulimwenguni pote kuhubiri Injili (Marko.16:15,16). Walilitekeleza agizo hili, na neno la kifo chake Kristo na ufufuo katika ujumbe wao ndio ulikuwa wa Kwanza. Lakini kumbuka kwamba wakati ule halikuwapo Agano Jipya kama tunavyolijua. Kama walivyosimama maeneo ya sokoni na katika masinagogi wakinena kuhusu mtu huyu Yesu wa Nazareti, masimulizi yao yangeonekana ya ovyo -Juu ya seremala toka Israeli aliyekuwa mkamilifu, aliyekufa kisha kufufuliwa kwa utimilifu barabara Agano la kale lilivyotabiri, ambaye sasa alikuwa anawataka wabatizwe na kufuata mfano wake. Katika siku hizo, watu wengine tena walikuwa wanajaribu kuwajenga wafuuasi wa dhehebu. Ikabidi iwepo njia nyingine ya kuwathibitishia ulimwengu kwamba ujumbe ulio hubiriwa na Wakristo ulitoka kwa Mungu mwenyewe, wala si kutoka kwenye elimu ya kikundi cha wavuvi waliotoka Kaskazini mwa Israeli.
Katika siku zetu tunavutwa na taarifa za Aganao Jipya juu ya kazi na mafunzo ya Yesu ili tuhakikishe kwamba ujumbe wetu unatoka kwa Mungu; Lakini katika siku hizo, kabla halijaandikwa na kupatikana, wahubiri walikubaliwa kutumia uweza wa Mungu - Roho wake Mtakatifu ili kutokeza ukweli wa kile walichokuwa wanasema. Hii ilikuwa ni sababu bayana ya kutumia vipawa mbele ya macho ya Ulimwengu; kukosekana Agano Jipya lililoandikwa pia kulifanya iwe shida kwa makundi mapya ya waumini kupevuka katika Imani. Matatizo yaliyojitokeza mengi ya utendaji kati yao yasingelikuwa na ufumbuzi ulio wazi, kwa wao mwongozo ungelikuwa mdogo katika kukua ndani ya imani iliyo kwa Kristo. Basi, kwa sababu hizi, Vipawa vya Roho Mtakatifu vikapatikana ili waumini wa kwanza waongozwe katika ujumbe ulioandikwa kwa uongozi wa Mungu, mpaka taarifa ya Agano Jipya juu ya ujumbe huu na mafundisho ya Yesu yalipoweza kuandikwa na kusambazwa.
Kama ilivyokuwa, sababu hizi za kugawiwa Roho Mtakatifu kwa wingi ilikuwa dhahiri:-
-“(Yesu) alipopaa kwenda (Mbinguni) ….. akawapa wanadamu vipawa (vya Roho) ….Kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma (ya kuhubiri) itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe” yaani waumini (Efe. 4:8,12).
-Basi Paulo aliwaandikia waumini waliokuwa Rumi, 'Natamani sana kuwaona, nipate kuwapa karama ya Rohoni’, (Kipawa cha Roho) ili mfanywe imara (Rum. 1:11).
Kuhusu kutumia vipawa kwa kudhibitisha mahubiri ya Injili, tunasoma:-
“Injili yetu haikuwafikia kwa maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu na uthibitifu mwingi” kwa miujiza iliyotendeka (2 Thes. 1:5 linganisha 1:5,6)
-Paulo aliweza kutaja “Neno alilolitenda Kristo kwa kazi yangu, mataifa wapate kutii, kwa neno au kwa tendo (la miujiza) kwa nguvu za ishara na maajabu, katika nguvu za Roho Mtakatifu” (Rum. 15: 18,19)
-Kuhusu wanaohubiri Injili, tunasoma, “Mungu naye akishuhudia pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi na kwa mgawanyo ya Roho Mtakatifu” (Waebrania 2:4)
-Kampeni ya kuhubiri Injili kule Kipro ilionyesha maajabu, hata ikawa “Liwali alipoyaona yaliyotendeka, akaamini, akiyastajabia mafundisho ya Bwana (Mdo. 13:12).
Maajabu yalimwongoza aheshimu kwa kweli mafunzo aliyoelimishwa. Vile vile pande za Ikonio, “Bwana … alilishuhudia neno la neema yake, akawajalia ishara na maajabu yatendeke kwa mikono yao” (Mdo. 14:3)
Yote haya yameelezwa kwa kifupi juu ya utii wa mitume kufuatia yale waliyoambiwa wahubiri: “ Wakatoka na kuhubiri kila mahali, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulidhibitisha neno kwa ishara zilizoambatana nalo” (Marko. 16:20).
MAMBO DHAHIRI KATIKA NYAKATI ZA NAMNA YAKE MAALUM.
Kwa hiyo, hivi vipawa vya Roho vilitolewa ili kufanya mambo dhahiri katika nyakati za namna maalumu .hivi laonyesha kosa la kudai kwamba Kuwa na kipawa cha Roho ni maisha yote ya mtu. Mitume, akiwemo Petro, “Walijazwa na Roho Mtakatifu siku ya Pentekosti, baada ya Yesu kupaa (Mdo. 2:4) kwa hiyo waliweza kunena kwa Lugha ngeni ili kuanzisha kuhubiri Injili ya Kikristo kwa kuitangaza kwa watu. Wenye mamlaka walipojaribu kuwatia nguvuni, “Petro akajaa Roho Mtakatifu” akaweza kuwajibu na kuwadhibitishia …. (Mdo. 4:8). walipoachiwa toka gerezani wakaweza kuendelea kuhubiri kwa usaidizi wa vipawa -“Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakasema neno la Mungu kwa Ujasili” (Mdo. 4:31)
Msomaji mwangalifu ataona kwamba taarifa haisemi kwamba'Tayari walikuwa wamejaa Roho’ Walijazwa na Roho Mtakatifu kufanya mambo halisi, lakini ilibidi wajazwe tena ili kutimiza jambo lingine katika mpango wa Mungu. Paulo vile vile “Alijazwa Roho Mtakatifu” alipobatizwa, lakini miaka mingine baadae “alijazwa tena Roho Mtakatifu” ili kumwadibu mtu mwovu kwa kumpiga upofu (Matendo. 9: 17; 13:9)
Katika kusema vipawa vya miujiza, Paulo aliandika kwamba waumini wa kwanza walipata “ Kadri ya kipimo cha kipawa chake Kristo” (Efe.4:7). Neno la Kiyunani 'Kadri ya kipimo’ maana yake “Sehemu ndogo au Kiasi”. Yesu peke yake ndiye aliyekuwa na vipawa bila kipimo, yaani alikuwa na uhuru wote wa kutumia kama alivyotaka (Yoh. 3:34). Sasa tutafafanua hivyo vipawa vya Roho vinavyoonekana kutajwa zaidi walikuwa navyo katika karne ya kwanza.
VIPAWA VYA ROHO KATIKA KARNE YA KWANZA
UNABII
Neno la Kiyunani'Nabii’ maana yake ni mtu anayetabiri neno la Mungu kwa mambo yaliyombele kabla jambo halijatokea - Basi ni kusema kwamba ni mtu aliyevuviwa kunena maneno ya Mungu, ambayo katika vipindi yalikuwa yanatabiri matukio ya wakati ujao (tazama 2 Pet. 1:19 -21). Hivyo,'Manabii’ - hao walio na kipawa cha kutoa unabii 'Walitoka Yelusalemu kwenda Antioki. Akasimama mmoja wao aliyeitwa Agobo, naye alionyesha ishara kwa Roho ya Kuwa itakuwepo njaa kubwa ulimwenguni pote: ilitokea katika siku za Klaudio Kaisari. Ndipo wanafunzi, kila mtu kwa kadri ya uwezo wake waliamua kutuma msaada kwa ndugu’ (Mdo. 11: 27 -29). Aina hii ya Unabii dhahiri, wa hali ya juu. Ambao ulikuwa wazi na ukamilifu ulikuwa kwa miaka michache, unakosekana kabisa miongoni mwao ambao sasa wanadai wana kipawa cha unabii; kweli, ni hakika mno kuwa katika kanisa la kwanza hiki kipawa kilikuwemo kati yao kwa kweli, hata walitoa muda wao na pesa ili kukabiliana na shida iliyokuwa imetabiriwa. Mifano michache ya jambo la aina hii yaweza kupatikana makanisa yaitwayo leo'Yaliyojazwa Roho’.
UPONYAJI
Kwa Kuwa mitume walikuwa wanahubiri habari njema (Injili) ya ufalme ujao wa Mungu wenye ukamilifu duniani, walifaa wauthibitishe ujumbe wao kwa kuonyesha miujiza ambayo ilionjesha kwa sehemu kipindi hicho kitakachokuwa, hapo “Macho ya vipofu yatakapofumbuliwa na masikio ya viziwi yatapozibuliwa. Ndipo kilema ataruka ….” (Isaya 35: 5- 6). Zaidi kuhusu hali ya mambo kwenye ufalme wa Mungu tazama somo la 5. Ufalme wa Mungu utakaposimikwa duniani, ahadi za jinsi hii kama hizi hazitatimia kwa nusu kipimo, wala ufalme kutokuwa halisi hapa au sivyo. Kwa hivyo uthibitisho wa Mungu kwa huo ujumbe waufalme ulikuwa katika nguvu, wazi wazi usioweza kukanushwa; kwa hoja hii mingi ya miujiza ya uponyaji iliyofanywa na waumini wa kwanza ilikuwa machoni pa watu wote waweze kuona.
Mfano mashuhuri unapatikana pale Petro alipomponya mwombaji kilema aliyewekwa kila asubuhi penye mlango wa hekalu katika Matendo 3:2 tunasoma kuwa walimuweka kila siku - hivyo alizoeleka sana machoni pa watu. Akiisha ponywa kwa karama ya Roho iliyotumiwa na Petro, “Akaondoka upesi akasimama, akaanza kwenda, akaingia ndani ya Hekalu pamoja nao akaenda kuruka ruka … watu wote wakamwona akienda, akimsifu Mungu. Wakatambua ya Kuwa yeye ndiye alikuwa akiketi na kuomba sadaka kwenye mlango mzuri wa Hekalu; Basi, alipokuwa akiwashika Petro ….. watu wakamkusanyikia mbio katika tao … wakishangaa sana” (Matendo ya Mitume 3: 7 -11)
Ndipo Petro akaanza mara moja kusema kwa sauti kuhusu ufufuo wa Kristo. Wakiwa hawana la kuuliza, na wanapouona ushuhuda usiopingika mbele ya macho yao katika namna ya mwombaji aliyeponywa, tunaweza Kuwa na hakika ya kwamba waliyaelewa maneno ya Petro Kuwa yametoka kwa Mungu. Mlangoni mwa Hekalu “Saa ya Kusali” (Mdo. 3:1) Watu walikuwa wamesongamana, kama kwenye duka watu wanavyosongamana. Ilikuwa ni mahala kama hapo, Mungu alichagua kudhibitisha mahubiri ya neno lake kwa Muujiza huu uliodhahiri. Vivyo hivyo katika matendo 5:12 tunasoma ya kwamba “Kwa mikono ya mitume zikafanyika ishara na maajabu mengi katika watu”. Kadhia zifanywazo na wapentekosti wanaoponya na wengineo huzunguka mambo yaliyotokea pembeni mwa makanisa, kuliko njiani palipo wazi ili watu waone, na katika mkusanyiko wa'Waumini’ walio katika hali ya Roho ya kutazamia'Ishara’itokee, kuliko mbele ya watu wote wenye mioyo migumu.
Acha isemwe hii nafasi kwamba mwandishi wa sasa amekuwa na ujuzi mkubwa wa kujadili matukio haya na wanaodai siku hizi wamekuwa na Roho. Vile vile kwa kushuhudia kadhia nyingi za walio na Roho. Lakini 'Ushuhuda wangu mwenyewe’ wa kuona uponyaji mwingi ni ambao hauko dhahiri, na katika tiba nzuri sana kwa sehemu, haitakiwi kuwa katika mwendo wa kuzidi kutia maelezo; Mshirika yeyote wa makanisa haya mwaminifu atakubali kwamba mengi ya haya yanaendelea. Kwa nafasi nyingi nimezungumza na rafiki zangu wapentekoste wazuri, “Sio kwamba sipendi kuamini kuwa unaweza kuwa na uweza huu mkubwa. Lakini Mungu katika nyakati zote ni bayana ameonyesha ni nani aliye na nguvu zake na nani hana; hivyo si vibaya kwangu kukuuliza hali ya mafundisho yako, ambayo kwa sasa siwezi kwa kuwa hayawezi kupatana na maandiko” Kamwe hujawa bayana 'Kufafanua Roho na Nguvu’ kwa kunieleza mimi.
Kwa namna nyingine kabisa na kwa kufikiri kwangu, Wayahudi wenye msimamo mkali wa karne ya kwanza walifunga mioyo yao katika uwezekano wa kwamba wakristo walikuwa na vipawa vya kufanya miujiza ya Roho ya Mungu. Lakini hata hivyo iliwabidi wakubali, “Mtu huyu anafanya Ishara nyingi” (Yoh. 11: 47) na “Ishara mashuhuri imefanywa nao … ni dhahiri kwa watu wote wakaao Yerusalemu; wala hatuwezi kuikana” (Mdo. 4:16). Vivyo hivyo wale waliosikia mitume wakinena kwa lugha' Walishikwa na fadhaa” (Mdo. 2:6). Wapentekoste waongeao bila busara siku hizi hawafanyi hivyo. Ukweli ni kwamba watu wameweka katika hali inayofaa sana kwa 'Wapentekosti’ wa sasa na kuweza kukana kwamba kwa kweli wanatimiza miujiza, hapana shaka ni hatua ya maana kwa mjadala huu. kama ishara moja tu imekuwa ni habari kuu Yerusalemu pote, Je ! si haki kutoa shauri la kwamba ikiwa muujiza wa kweli ulifanywa Uingereza au bustani iliyo Nairobi, wakati huo kungekuwa na kutambua ya kwamba vipawa vyenye miujiza ya Roho ya Mungu vipo leo ? Badala yake, Wapentekosti wanangojea ulimwengu ushikilie aina zifuatazo za 'Ushahidi’ kuwa ndio sababu zao za kuamini :-
-(Hatimaye) kuponywa vidonda vya tumbo; njia ya kupona imedhaniwa ilianza baada ya mkutano wa maombi.
-Sehemu za mwili zilizolemaa kunyooka.
-Macho au Masikio yakipona, ingawa mara nyingi hali hurudi kama awali.
-Kuondolewa misiba mwilini.
Katika mifano hii inabidi kujumlisha kwa kusema kuwa magari ya kubebea wagonjwa yaliwachukua wagonjwa toka Hospitali hadi kituo cha Krusedi ya uponyaji cha T.O Osborn kilicho Nairobi, nchini Kenya; Madereva walikabiliwa na mashaka ikiwa wakae au warudi, walisalia - vile vile wagonjwa hawakupata ahueni yoyote.
Hata hivyo changamoto inataka watu waje kwenye mikutano hii kama matangazo yasemavyo:-“ Njooni mtarajie Muujiza” kwa matakwa ya Roho ya binadamu namna zote hatua imepangwa inayotoa shauri yenyewe kama mfano huu. Hakuna mahala popote katika Agano Jipya panapodokeza kidogo mambo haya mengi ya matakwa ya Roho ya binadamu yenye lugha laini iliyohitajika kabla ya kutokea Muujiza au ishara. Ni dhahiri kwamba baadhi ya wale walioponywa katika karne ya kwanza hawakuwa na imani - k.m. mtu mmoja hakumjua Yesu alikuwa ni nani (Yoh. 5: 13; 9:36) .
Mfano mmoja wa Roho ya kuhoji -hoji unatimizwa na akili iliyopotoka na maombi yanayorudiwa mara ya pili, Sauti za ngoma na mziki wenye sauti. hapawezi kuwa na shaka kama ya busara yoyote kumjua Mungu - na jambo lolote lingine - kwa yote hayo yapo nje ya maana. mwandishi ameweza kukumbuka alivyohudhuria mikutano kadhaa katika sehemu mbali mbali, kila wakati alijisikia kuumwa kichwa kutokana na bidii ya kuendelea kuwa na busara iliyo sawa sawa, Ufahamu wa Biblia kwa kukabili jaribu la kutaka kupotezwa na mlio wa Ngoma na kupiga makofi. Kama yote hayo yanaonekana kuwa ya lazima kutangulia kabla ya kufanywa “Ishara” ya Wapentekosti basi ni ushahidi wa kutosha kwamba 'Uponyaji’ ni matokeo ya hangaiko la moyo na kutengenezwa Roho ya mwanadamu, kuliko shughuli moja kwa moja ya Roho ya Mungu. Kwa namna nyingine kabisa, Petro aliweza kutumia karama ya kweli ya ishara kwa kuponya watu walipolala katika njia kuu (Mdo. 5:15); Kutumia Paulo karama zenye miujiza mwenyewe alishuhudiwa na mtumishi wa Serikali asiyeamini (Mdo. 13: 12,13), vile vile na wapagani walioishi katika mji wa Listra (Mdo. 14: 8 - 13). Kama zilivyotakiwa kwa kusudi kabisa na hali ya karama za Roho, mambo ya uponyaji yalifanywa hadharani, na kwa njia yoyote hakukuwa na dalili ya kusita na maelezo mengine yoyote ila kukubali ya kwamba hapa kuna nguvu za Mungu zinazoonyeshwa dhahirii na watumishi wake.
Tokeo moja ambalo Kristo alionyesha uponyaji wa miujiza lilikuwa jinsi hii “Wakastaajabu wote (Yaani walioona), wakamtukuza Mungu, wakisema, Namna hii hatujapata kuona kamwe” (Marko. 2:12).
LUGHA
Mitume, baadhi yao walikuwa ni wavuvi wasiotengenezwa vizuri (k.m. Kielimu), walipata agizo kubwa la kwenda ulimwenguni pote, wakahubiri Injili (Marko. 16: 15, 16).Labda wazo lao la kwanza hasa lilikuwa,‘Lakini sijui kusema lugha nyingine !’ kwa wao halikuwa suala la 'Sikujifunza vizuri lugha nilipokuwa shuleni’ maana hawakuwa na shule. Juu yao wote imeandikwa ya Kuwa ni'Watu wasio na elimu, na wasio na maarifa’ (Mdo. 4:13) lilipokuja jambo la aina hiyo. hata kwa wahubiri walioelimika zaidi (k.m Paulo), Lugha ilikuwa bado ni kikwazo kikubwa kushindana. walipofanyika waongofu, tegemezi walilohitaji Kuwa nalo ni juu ya kila mmoja kwa kujengana (Agano Jipya lilipokuwa bado halijaandikwa) maana yake ilikuwa kwamba kutokuelewana lugha na kila mmoja lilikuwa ni tatizo kubwa.
Katika kushinda hili, wakapewa karama ya kunena katika lugha ngeni (‘Ndimi’) na kuweza kuzifahamu. Ni bayana kuna upinzani kabisa kati ya mtazamo huu wa 'Ndimi’ na huu wa Wakristo wengi waliozaliwa mara ya pili, wanaoeleza matamshi yao yenye furaha katika sauti zisizotambulika Kuwa ni ndimi. Mtafaruku huu unaweza kuondolewa kwa kuonyesha kwamba Biblia inaposema “Ndimi” ni'lugha ngeni’.
Siku ya Pentekosti, ambayo ni sikukuu ya Wayahudi, mapema baada ya kupaa juu mbinguni Kristo, mitume “ Wote walijazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kunena lugha nyingine ….. Makutano wakakutanika (Mara nyingine karama ikaonyeshwa !). wakiwa wameshikwa na furaha, kwa Kuwa kila mmoja aliwasikia akinena kwa lugha yake. Wakashangaa wote, wakastaajabu na kuambiana, Tazama, hawa watu wasemao si wagalilaya hao ? Waparthi, Wamedi … tunawasikia hawa wakisema kwa lugha zetu … wakashangaa wote”(Matendo ya mitume 2: 4-12) Haielekei ya kwamba huu mkazo maradufu wa mshangao wa watu na kustaajabu kwao ulikuwa wa lazima ikiwa walisikia mambo yasiyo na maana tu yakinenwa na hao wenye kadhia ya Kuwa na karama siku hizi.; yanayozuka katika maneno madogo ya uchokozi au kutopendelea, kuliko mshangao na uthibitisho unaotokana na kufahamu maneno yaliyonenwa, yaliyoshuhudiwa katika matendo 2.
Katika matendo ya mitume 2: 4-11 lugha zilizoandikwa zipo bayana na sehemu nyingine ya maandiko ya Agano Jipya; maneno “Watu wa kila Taifa na Lugha” yametumika mara tano katika Ufunuo kwa kusema watu wote walio kwenye sayari -dunia hii (Uf. 7: 9, 10:11, 11:9, 13:7, 17:15).Neno la Kiyunani‘ Ulimi’linatokea katika toleo la Kiyunani la Agano la Kale (Liitwalo'Septuagint’) na maana ya lugha (tazama mwa. 10:5, Kum. 28:49, Dan. 1:4) - katika Biblia yetu ya Kiswahili Kum. 28:49 ni sawa na Kiyunani.
1 Kor. 14 ni orodha ya maagizo yahusuyo kutumia kipawa cha Ulimi; mstari. 21 unanukuu Isaya 28:11 kuhusu ni jinsi gani kipawa hiki kitatumika kwa kushuhudia juu ya Wayahudi:'Katika sheria imeandikwa, kwa midomo (Ulimi) ya watu wageni na kwa lugha nyingine atasema na watu hawa’ Kwa awali Isaya 28:11 inataja wavamizi wa Israeli wakisema na wayahudi kwa lugha (“Ndimi”) ambazo hawakuzifahamu. Usawa uliopo kati ya 'Ulimi’ na 'Midomo’ unaonyesha ya kwamba 'Ndimi’ zilikuwa ni lugha ngeni. vipo vionyesho vingi vingine katika 1 Kor. 14 vya kwamba “ndimi ni lugha ngeni. Sura hii ni hukumu ya Paulo iliyovuviwa yenyewe kuhusu matumizi mabaya ya karama yaliyokuwa yanafanywa katika kanisa la kwanza, kama hivi, yanatoa namna nyingi juu ya ufahamu wa karama za Ulimi na Unabii. Sasa tutajaribu kutoa jumla ya fafanuzi chache juu yake. Aya ya 37 ni mstari wa kufungua:-
“Mtu akijiona Kuwa ni nabii , au mtu wa Rohoni, ayatambue hayo ninayowaandikia ya kwamba ni maagizo ya Bwana”
Ikiwa mtu awaye yote anadai Kuwa na karama ya Roho, yampasa akubali kwamba maagizo yanayotangulia juu ya kutumia karama ni kwa kuvuviwa na Mungu. Awaye yote ambaye anaasi hizo amri leo basi ni dhahiri wanakubali kwamba wanaona inafaa kudharau maneno yaliyoandikwa kwa Uongozi wa Mungu.
Aya ya 11 -17:-
“Basi nisipoijua maana ya ile sauti nitakuwa kama mjinga kwake yeye anenaye, naye anenaye atakuwa mjinga kwangu.
Vivyo hivyo nanyi, kwa kuwa mnatamani sana kuwa watu wenye karama za Rohoni, takeni kwamba mzidi sana kuwa nazo ili kulijenga kanisa.
Kwa sababu hiyo yeye anenaye kwa lugha na aombe apewe kutafsir
Maana nikiomba kwa lugha, Roho yangu huomba, lakini akili zangu hazina matunda.
Imekuwaje basi, Nitaomba kwa Roho, tena nitaomba kwa akili pia, nitaimba kwa Roho, tena nitaimba kwa akili pia.
Kwa maana wewe ukibariki kwa Roho, yeye aketiye mahali pa mjinga ataitikiaje, Amina, baada ya kushukuru kwako, akiwa hajui usemalo.
Maana ni kweli, wewe washukuruu vema,bali yule mwingine hajengwi.
Basi kunena kwa lugha ambayo wale walio katika ibada hawaelewi haina maana. “Kusema bila maana nzuri” hakufai, maana ni jinsi gani yaweza kusemwa “Amina” ya ukweli mwishoni mwa 'Sala’ iliyoundwa kwa kupayuka -payuka kusikoweza kufahamika ? kumbuka kwamba “Amina” maana yake “Iwe hivyo’ yaani, nakubali kabisa na kilichosemwa katika sala hii. kunena lugha isiyoeleweka mbele za ndugu zako haiwajengi, asema Paulo.
Ninaukumbuka ugawaji vitabu vidogo nje ya ya mkutano wa kufukuza maovu uliofanywa na Billy Graham,wakiombwa watu warudi tena katika Ukristo ambao msingi wake ni katika Biblia. Mwanamke aliyeshikwa na msisimko akajaribu kunivuta kwa maneno yake ya kwamba mafundisho yangu ya Kristadelfiani 'Yaliongozwa na Ibilisi’ kwa kupayuka katika 'lugha’ kwa muda wa dakika 10. Kwa namna yoyote sikuweza 'kujengwa’ na hiyo, kwa kweli jambo hili ndilo hasa lile Paulo aliagiza lisifanywe kabisa.
Aya ya 18:-
“Namshukuru Mungu ya Kuwa nanena kwa lugha zaidi ya ninyi nyote”
Kwa sababu ya kusafiri kwake katika maeneo mbali mbali kumhubiri, Kristo, Paulo alihitaji karama ya lugha ('Ulimi’) zaidi kuliko wote.
Mstari wa 19:-
“Lakini katika Kanisa napenda kunena maneno matano kwa akili zangu nipate kuwafundisha wengine, zaidi ya kunena maneno kumi elfu kumi kwa lugha”.
Hivi ni wazi kabisa. Mimi nitafanya vema kumhubiri Kristo kwa sentensi chache zilizo katika lugha ya Kiswahili kuliko mimi kuhubiri masaa mengi kwa lugha ngeni - au kuongea maneno yasiyofahamika vema.
Mstari wa 22:-
“Basi, hizi lugha ni ishara, si kwao waaminio bali kwao wasioamini, lakini kuhutubu si kwa ajili yao wasioamini bali kwao waaminio”.
Kwa hiyo matumizi ya lugha yalitakiwa yatumike zaidi katika kwenda nje kuhubiri Injili. Lakini wote wenye kadhia ya kunena kwa 'Lugha’ watoka miongoni mwa makundi ya 'Waaminio’ au (Kwa kuonekana) kwa mmoja wao anayepata wakati akiwa peke yake. Upo ukosefu sugu kwa mifano ya watu hawa ya kuweza kunena kimaajabu kwa lugha ngeni ili kueneza Injili. Mwanzoni mwa miaka ya 1990
ulifunguka mlango mpana katika kuhubiri Injili ya Kristo pande za Ulaya Mashariki, Lakini makanisa (yanayojiita) ya 'Kiinjili’ ilibidi yagawe vitabu vyao vilivyo na lugha ya Kiingereza kwa sababu ya vizuizi vya lugha ! kwa kweli karama ya kunena kwa lugha mpya ingetumika ikiwa walikuwa nayo ? naye Mwinjilisti wa mikutano mikubwa Reinhardt Seiber, huku akiwa na kadhia ya kuwa na Roho kwa ajabu bado ilimbidi aseme na makutano kwa kumtumia mkalimani pande za Kampala, Uganda.
Aya ya 23:-
“Haya ! Ikiwa kanisa lote limekusanyika pamoja, na wote wanene kwa lugha, kisha ikawa wameingia watu wajinga au wasioamini, Je ! hawatasema ya kwamba mna wazimu ?”
Hili ndilo jambo hasa limetokea. Waislamu na wapagani pamoja wamedhihaki mwenedo wao wa ovyo (Upuuzi) wa hao wanaodai wanacho kipawa cha ulimi Afrika Magharibi pote. Hata mkristo aliye sawa akilini akitega sikio kuzunguka kona ya mkutano wa Wapentekoste atadhania ya kuwa washirika walikuwa na wazimu.
Aya ya 27:-
“Ikiwa mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, naye mtu mmoja atafsiri”.
Watu wawili watatu ndio waliohitajika kunena wakati wa Ibada. Haielekei kwamba walikuwepo wenye lugha zaidi ya tatu tofauti zilizosemwa na wasikilizaji wowote. Ibada itakosa mshikamano wote muda mfupi ikiwa kila sentensi ya msemaji ikibidi itafsiriwe zaidi ya mara dufu. Ikiwa karama ya lugha imekuwepo kwenye mkutano uliofanyika katikati ya jiji la Dar -es -Salaam, wamehudhuria watu wanaoongea Kiswahili, na wengine ni Waingereza na Wajerumani wakiwa ni watalii waliohudhuria,
Wanenaji wanaweza kuanza :-
Mtumishi: Habari za jioni.
Lugha ya msemaji wa kwanza: Bon Soir (Kifaransa)
Lugha ya msemaji wa pili: Guten abend (Kijerumani)
Lakini kwa kawaida wanapaswa kunena “ Kwa zamu”, anaanza mmoja baadaye afuate mwingine. Utatokea mtafaruku kwao wakinena kwa wakati huo huo; lakini kwa sababu ya msimamo uliopo unaochochewa na mawazo ya 'Kunena kwa Lugha’, tukio linakutwa katika vichwa vya watu wengi wakati huo huo. Tumegundua kwamba mara mtu mmoja akianza, wengine nao upesi wanavutwa kufanya hivyo hivyo.
Karama ya Lugha mara nyingi ingetumika pamoja na hiyo ya kutoa Unabii, ili kwamba ujumbe uliovuviwa kutoka kwa Mungu utabiriwe (kwa kutumia kipawa cha kutoa Unabii) mfano wa kutumia jinsi hii vipawa viwili unaweza kupatikana katika
Mdo. 19:6. Lakini, ikiwa kwenye mkutano mjini Dar -es-Salaam ukihudhuriwa na watu wa Tanzania na wafaransa wengi wageni, msemaji akinena kwa kifaransa, watu wanaoongea kiswahili waliopo'Hawajengwi’. Kwa hiyo kipawa cha kutafsiri ulimi
(au Lugha) kingekuwepo, ili kwamba kila mmoja aweze kufahamu, kama -katika mfano wetu siku hizi, katika kutafsiri toka kifaransa kwenda kiswahili au Kifaransa kwenda kiingereza. Vivyo hivyo ikiwa swali limeulizwa na mtu anayeongea kifaransa, mnenaji hawezi kumwelewa bila msaada, hata kama alikuwa na karama ya kunena kwa kifaransa pasipo mwenyewe kukielewa. Kwa sababu hiyo kipawa cha kutafsiri kitakuwepo kusaidia suala hili.Bila kuwepo mtu mwenye kipawa cha kutafsiri kinapohitajika, kipawa cha ulimi hakitatumika:“ …….. mmoja na afasiri. lakini asipokuwepo mwenye kutafsiri na anyamaze katika Kanisa (1 Kor. 14:27,28). Jambo la hakika ni kwamba watu wengi siku hizi walio na kadhia ya kuwa na Karama ya'Ulimi’ wananena kwa 'lugha’ ambazo haziwezi kueleweka na yeyote, na bila mwenye kutafsiri, ni hakika suala la uasi kwa maagizo haya.
Mstari wa 32, 33 :-
“Na Roho za manabii huwatii manabii. Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani, Vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya Watakatifu.”
Kwa hiyo tendo la kuwa na karama za Roho Mtakatifu lisitiwe pamoja na ujuzi anaomchukua mtu nje ya mambo ya ufahamu wa kawaida; Roho huwa chini ya uongozi wa mtumiaji, kuliko lazimisho linalo wachukua upande mwingine ili kwamba watende bila kujua mara nyingi kwa makosa imedaiwa kwamba mashetani au 'Roho wachafu’ huwamiliki'Wasiookoka’ (tazama somo la 6.3), Bali ni kwamba Roho Mtakatifu wanajazwa waaminio. Lakini nguvu za Roho zilizotajwa katika 1 Kor. 14:32 zilikuwa chini yake mwenye kuiongoza kwenye kusudi la namna yake maalum; haikuwa shurutisho hai la wema ikipambana na nguvu ya uovu iliyo ndani ya mwili wa mwanadamu. Isitoshe awali tumeonyesha ya kwamba nguvu hizi za Roho Mtakatifu ziliwajia mitume wakati fulani ili kufanya mambo ya namna yake maalum, si kuwa nazo daima.
Ombi kwa wenye Kuwa na karama watumie kwa namna inayofaa upendo na amani ya Mungu na kuchukia machafuko (aya ya 33) Laonekana limeangukia kwenye masikio ya viziwi katika makanisa ya wa -Pentekosti wa siku hizi.
Aya ya 34: -
“Wanawake wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii kama vile inenavyo torati nayo.”
Katika fungu hili la kutumia karama za Roho, hakujawekwa kukatazwa ya kwamba wanawake wasitumie karama wakati wa ibada ya kanisa. kutoangalia hili kwa upana linatarajiwa ikiwa jambo lililopo la kunena kwa 'Machafuko ya kupayuka’ laweza kuelezewa kwa maneno ya kuchochewa mawazo likipita toka kwa mtu mmoja hadi mwingine katika mkusanyiko wao. Wanawake, Watoto - na yeyote anayekuwapo kwa hiyari - anaweza kuambukizwa na msimamo wa jinsi hii, kwa hiyo wanafanya matamshi ya kusikia furaha moyoni, yanayoishia kuwa kama ni 'lugha’.
Wanawake wajitokezao kwa kusemwa 'Wananena kwa lugha' na 'kutoa Unabii’ katika makanisa ya sasa hawapatani na agizo lililo wazi la aya hii. Maneno ya Upuuzi, ambayo ni mabaya yatokayo kwa watu ya kwamba Paulo alikuwa mchukia wanawake yamezimwa kwa aya chache baadaye: “Mtu akijiona kuwa ni nabii au mtu wa Rohoni, na ayatambue haya ninayowaandikia ya kwamba ni maagizo yatokayo kwa Bwana” (1Kor. 14:37) siyo ya kutoka kwa Paulo mwenyewe.
Awaye yote aaminiye Biblia kuwa imevuviwa, basi, inambidi akubali kwa maagizo haya yaliyo katika 1 Kor. 14 si ya kufanyia mchezo bayana wa kuyabeza; kufanya hivyo kunaashiria kutokuwa na imani ya kutosha katika maandiko kwamba yameandikwa kwa uongozi wa Mungu pekee - au maneno yenyewe yajieleze kwamba huyu mtu hana karama ya Roho, kwa kuwa mtu mwingine asiye na karama atakana kwamba maagizo yaliyo katika 1 Kor. 14 ni maagizo ya Bwana yaliyo kwa ajili yetu.
Kuwanza kwa akili timamu maneno haya yatuambia, yanaharibu sana. katika mwangaza huu, ni vipi uweze kusalia Kuwa mshirika wa kanisa hili,au kupenda kufanya ibada nao.
Maneno yakiwa chini ya kitabu kwa sehemu hii, ni yenye maana sana ya kwamba hayo madhehebu yenye kadhia ya kunena kwa lugha yamedhibitishwa kisayansi Kuwa na huzuni upesi kulinganishwa na watu walio katika malezi mengine. Keith Meador, Profesa wa magonjwa ya moyo katika chuo kikuu cha Vanderbilt, Marekani, alianza uchunguzi mkubwa kujifunza kuchanganua uhusiano uliopo kati ya huzuni iliyo moyoni na malezi yaliyo katika dini. Aligundua kwamba “ Idadi kubwa ya wenye huzuni ….. miongoni mwa Wakristo wa madhehebu ya Kipentekosti ilikuwa 5.4% kulinganishwa na 1.7 % kwa uchunguzi wa kundi zima” matokeo ya kazi hii yameandikwa katika kitabu cha mambo ya kila siku, 'Hospital and Community Psychiatry, Des, 1992.’
Maandishi ya kuvutia katika ukurasa, yaliyofikiwa kwenye dhana hiyo hiyo baada ya kuchunguza sana, yalitokea katika jarida lingine liitwalo International Herald Tribune, la Feb. 11, 1993; na kichwa cha habari yenyewe: “Wapentekosti wapo orodha ya juu wanapokuja na huzuni” Ni kwa sababu gani wapo kwenye hali hii ? kwa kweli inabidi wawiane na uhakika wa kwamba 'Ujuzi unaojipatia’ wa tendo la Kuwa na Roho, ambao wapentekosti (na wengineo) wenye kadhia hii, si lolote zaidi ya Kuwa wanauchungu sana wa m ioyo yao dhidi ya mazoea.
2.4 Kurudishwa kwa vipawa
Vipawa vyenye miujiza ya Roho ya Mungu vitatumika tena na waumini ili kwamba ulimwengu huu wa sasa ubadilishwe uwe Ufalme wa Mungu, Kristo atakaporudi. Basi vipawa vimetajwa Kuwa ni 'Nguvu za zamani (Zama) zijazo’ (Ebr. 6:4, 5); naye Yoeli 2: 26 -29 umwagaji mkubwa wa karama baada ya toba ya Israeli. Uhakika sana wa kwamba vipawa hivi watapewa waaminio Kristo akirudi ni ushuhuda wa kutosha ya kwamba kwa sasa vipawa watu hawana - Kwa kuwa Mkristo awaye yote mwenye macho yaliyo wazi pande zote mbili Maandiko na matukio ya ulimwengu, ni hakika kurudi kwa Bwana inabidi kuwa amekaribia sana (tazama yaliyo mwisho wa kitabu cha 3).
Upo Unabii dhahiri wa Biblia kama katika maana fulani kwa kipindi cha kati ya karne ya kwanza, vipawa vilipokuwepo, na kuja mara ya pili ilibidi vipawa vya Roho viondolewe:-
“ ……Ukiwepo Unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwepo maarifa, yatabatilika. kwa maana tunafahamu kwa sehemu (yaani, nusu); na tunafanya Unabii kwa sehemu; lakini ijapo ile iliyokamili,iliyo kwa sehemu itabatilika (yaani, kuondolewa)”. 1 Kor. 13:8 -10 - Karama za Roho zilikuwa za muda tu.
Karama za Roho walizokuwa nazo katika karne ya kwanza ilibidi ziondolewe 'Ilipokuja ile iliyokamili’ Hii si kuja mara ya pili Kristo, kwa Kuwa kipindi hicho karama za Roho zitatolewa tena. Neno la Kiyunani lililotafsiriwa'Kamili’ maana yake hasa ni kile ambacho kimetimilika au Kizima; akimaanishi kwa lazima Kuwa ni kitu kingine kisicho na dhambi.
Hiki kitu kizima kitaingia mahali palipo na maarifa yaliyo kwa sehemu ambayo Wakristo wa kwanza walikuwa nayo kama tokeo la Kuwa na kipawa cha kutoa Unabii. Kumbuka kwamba kutoa unabii kilikuwa ni kipawa cha kutabili maneno yenye kuvuviwa na Mungu ; ni taarifa iliyoandikwa ya maneno haya yanayoifanya Kuwa Biblia.
Kwenye karne ya kwanza, Muumini wa kawaida alijua sehemu ndogo tu ya Agano Jipya kama tunavyolijua. Alisikia maneno mengine ya Unabii toka kwa wazee wa kanisa lake juu ya matukio mbali mbali ya matendo ; aliweza kujua vema juu ya maisha ya Yesu, na aliweza kusikia vema barua moja au mbili za Paulo zikisomwa kwa sauti. Lakini mara taarifa ilipoandikwa ya maneno ya Unabii na kuweza kutimilika na kugawanywa, hapakuwepo na haja ya kipawa cha kutoa Unabii kiendelee wawe nacho. kile ambacho kilikuwa kamili, kwa sababu hiyo kilichoingia mahali pa huduma ya karama ya Roho, basi likawa ni Agano Jipya lililotimilika:-
“Kila andiko lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki, ili mtu wa Mungu awe kamili (ametimilika)” 2 Tim. 3:16 -17.
Kile ambacho kinafanywa kuwa kamili, au kutimilika, ni'Maandiko yote’; hivyo mara'Maandiko yote’ yalipovuviwa na kuandika, “ Kile ambacho kilikuwa kamili” kikawa kimekuja, nazo karama zenye miujiza zikaondolewa.
Waefeso 4: 8 -14 yaweka sasa wazi kikamilifu sawia fumbo lisiloeleweka vema:-“(Yesu) alipopaa juu (katika mbingu), ….akawapa wanadamu vipawa (vya Roho) ….. kusudi mwili wa Kristo ujengwe: hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani (yaani, Imani moja), na kumfahamu sana mwana wa Mungu, hata Kuwa mtu mkamilifu …. Ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu”.
Vipawa vya karne ya kwanza vilitolewa hadi mtu alifikia kukamilika au apevuke, (yaani, akomae) nao waraka wa 2 Tm. 3:16- 17 unasema ya Kuwa “ Hadi mtu wa Mungu awe kamili” kwa kufahamu mwongozo wa 'Maandiko yote’ Tena, Kol. 1:28 unatufundisha ya kwamba 'Ukamilifu’ huja kwa kuitikia katika Neno la Mungu. Mara maandiko yote yakishikwa. Hakuna udhuru kweli wowote tena wa kukatizwa na wingi wa mafundisho yatolewayo na makanisa mbali mbali. Ipo biblia moja tu, na Kuwa
“Neno lako ndiyo kweli” (Yoh. 17:17), kwa kujifunza katika kurasa zake tunaweza kufikia “Umoja wa imani”, imani moja ambayo Efe. 4:13 inaizungumzia. kwa hiyo wakristo wa kweli wamefikia kuishika hiyo imani moja; kwa maana hiyo wametimilika (wamekuwa'Kamili’) kwa kutokana na 'kile ambacho ni kamili’ au kimetimilika, Neno la Mungu lote - lililoandikwa.
Kwa kupita, tazama ni jinsi gani Efe. 4:14 unalinganisha kuwa chini ya utumishi wenye karama za miujiza, na utoto kiroho; na kwa maneno yenyewe ya kutoa unabii, namna karama zenye miujiza zilipoondolewa. 1 Kor. 13:11 unasema hayo hayo. Kufanya makelele haya kuhusu kuwa na karama za roho, basi si ishara ya kukomaa kiroho. Kusonga mbele kila msomaji wa maneno haya kufanye sasa kuelekea kufahamu kwa kina neno la Mungu lililoandikwa. Na kufurahia utimilifu wa msingi wa ufunuo wa Mungu mwenyewe ndani yake kwetu, kwa kuitikia neno katika Utii wa kunyenyekea.
KADHIA ZILIZOPO ZENYE KUWA NA ROHO
Hatimae, hesabu ya maana nyingine inabidi ifanywe kuhusu kadhia zilizorudiwa za hao wadhaniao wana vipawa vyenye miujiza sasa:-
-“Wanenao kwa lugha” siku hizi wanaelekea kurudia rudia maneno yale yale mafupi zaidi na zaidi tena, k.m. “lala, lala, lala, shama, shama. Yesu, Yesu ……” huu sio mpangilio uliojumuika na maneno ya lugha yoyote; mtu akimsikia mwingine akinena katika lugha ngeni, mara kwa mara inawezekana ya Kuwa wanaongelea jambo fulani kwa mfano mzuri wa matamshi ambao watu hutumia, ingawa hatuwezi kuyaelewa maneno hayo. Lakini wanenao lugha siku hizi hawaangalii jambo hili, uhakika ni kwamba lugha wanenayo haijengi kanisa, ambapo hiyo ilikuwa shabaha ya kutolewa karama kwenye karne ya kwanza.
-Wapentekosti wengine wanatoa kadhia ya kwamba kunena katika lugha ni ishara ya Kuwa 'Wameokoka’na kwa sababu hii kila mwongofu wa kweli hii ishara itafuatana naye. Kadhia hii inagongana na ugumu wa maelezo kuhusu makanisa ya kwanza ulikuwa mwili, ambapo wale wanaomiliki karama tofauti - tofauti walikuwa kama viuongo mbali mbali. si kila mtu alikuwa mkono au mguu, na vivyo hivyo si kila mmoja alishika kipawa kimoja chochote, k.m Lugha. 1Kor.12:17, 27 -30 mistari hii yote inabainisha wazo hili:-
“Kama mwili wote ukiwa jicho, kuwapi kusikia ? kama mwili mzima ni sikio kuwapi kunusa ? …. Basi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake. Na Mungu amewaweka wengine katika kanisa , wa kwanza Mitume, wa pili Manabii, wa tatu Waalimu, kisha Miujiza, kisha karama ya kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za Lugha. Je! wote ni Mitume ? wote ni Manabii.? Wote wana karama za kuponya wagonjwa ? wote wanena katika lugha ? wote wafasiri.
Awali, maana hiyo hiyo imeonyeshwa katika mlango huo:-
“Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule; mwingine imani katika Roho yule yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule yule mmoja; na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine Unabii; na mwingine kupambanua Roho; mwingine aina za lugha; mwingine tafsiri za lugha; lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye. Maana kama mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo” (1Kor. 12: 8 -12)
Mkazo wa jinsi hii hauwezi kutoangaliwa:-
Shida nyingine kwa ubishi wa Mpentekosti ni kwamba Filipo aliwaongoa watu wengi katika mji wa Samaria - yaani, walibatizwa katika maji baada ya kuelewa Injili, lakini hawakupokea karama za Roho; kwa Kuwa baada ya hivi, Petro na Yohana waliwaendea “ ….. Waliposhuka, wakawaombea wampokee Roho Mtakatifu …. Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao waka mpokea Roho Mtakatifu …..Simoni aliona Kuwa watu wanapewa vipawa vya Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono yao mitume” (mdo. 8: 4 -18). inawezekana kwamba kupewa vipawa vya Roho ilikuwa ni kuwekewa mikono juu yao tu, tendo ambalo Wapentekosti hawalifanyi mara nyingi siku hizi.
Wapentekosti wengine wanasema kwamba kunena kwa lugha si ushahidi wa kuwa umeokoka. Huu ni ukweli unaojitokeza kuwa ipo tofauti kubwa ya mafundisho kati ya wenye kadhia ya kushika vipawa. Baadhi ya watu wa 'Kiroho’ huamini kwamba ufalme wa Mungu utakuwa duniani, ambapo wengine wanasema utakuwa mbinguni. Wakatoliki 'wa Kiroho’ wanasema kwamba Roho Mtakatifu anawaambia wamwabudu Bikira Maria na Papa, wakati wapentekoste wengine 'wa Roho’ wanasema ya kwamba wao huongozwa na Roho Mtakatifu anayewaamuru wamkane Papa, wamwone kuwa yeye ni mnyama na mpinga Kristo, wanapinga mafundisho ya Katoliki. Hata hivyo Yesu alisema pasipo shaka kwamba wale walio na msaidizi, “ ambaye ni Roho Mtakatifu” wataongozwa 'kwenye kweli yote’ ….tena siku ile (hamtahitaji) kuuliza neno lolote …..Msaidizi …..atawafundisha mambo yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia” (Yoh. 16: 13,23; 14: 26).
Usingekuwepo Mgawanyiko wowote katika mafundisho ya msingi miongoni mwao wenye kuwa na msaidizi - uhakika ni kwamba upo, unaonyesha kwamba wale wanodai wanaye hawamchukui kwa kusema kweli. Udhaifu umeonekana kwa baadhi ya hao wasemao ya kuwa wenye msaidizi, Katika Biblia ili kuthibitisha imani zao lakini wanaonekana kwamba hawajaongozwa katika kweli yote na maarifa kabisa ya msaidizi.
-Umuhimu mkubwa uliofuatana na baadhi kwa kunena katika lugha haupo sawa na taarifa za Biblia. Orodha ya vipawa katika Waefeso 4:11 haitaji, orodha kama hii inatokea chini katika 1 Kor.12: 28 -30. kwa kweli, zipo nafasi tatu pekee zilizoandikwa katika Agano Jipya mahali ambapo kipawa kilitumika (mdo. 2:4; 10:46; 19:6).
Madai ya kunena katika lugha na kufanya miujiza kulikotimizwa na Wakristo wa roho siku hizi inabidi yapimwe karibu na taarifa yenye maana ambayo tumeiandika katika somo hili kuhusiana na kazi ya Roho Mtakatifu. Kutengeneza maana yenye msingi ni kwamba lolote ambalo watu hawa wamelitimiza, haliwezi kuwa ni tokeo la wao kuwa na Roho Mtakatifu. Yeyote aletaye sababu za kusaidia mashauri ya kuwa wanamiliki karama za Roho, anayo kazi kubwa ya kufanya ili kujibu maneno ya Biblia tuliyotoa.
Ingawa hiyo ni sababu yenye maana katika kutazamia baadhi ya maelezo ya sababu gani uzushi wa kuponya kwa sehemu na kunena kwa'Lugha’ (Kwa mtindo wa kunena kwa kupayuka - payuka) hutokea.
Imefahamika kwamba wanadamu hutumia sehemu ndogo ya nguvu ya ubongo wao - chini ya 1%, kulingana na makadirio mengine. Tena, akili (Moyo) imetambuliwa kuwa inaweza karibu kutawala viungo vya mwili; hivyo kwa nguvu zao za mwili hivyo huamini kuwa moto hauwezi kuunguza, Wahindu wametembea juu ya moto nyayo zao zikiwa wazi bila kuungua. kwa vipindi vya kuchochewa, upo uwezekano wetu kutumia asilimia kubwa ya uwezo wa ubongo wetu kuliko kawaida, na kwa sababu hiyo kuwa na uwezo ya kutimiza matokeo ya viungo juu ya mwili wetu unapokuwa nje ya matendo ya kawaida. Hivyo, kwa kuchochewa na mapigano, askari anaweza kutojua kabisa kuwa mkono wake umekatika mpaka muda wa baadae.
Imani ya dini kuwa katika hali ya moto na msisimko unaoamshwa na nyimbo fulani, na mvuto wa kiongozi wa kiroho, inawezekana kabisa mambo yaliyo nje ya miliki ya kawaida kwa mwanadamu yatatokea.'Miujiza’ iliyodaiwa kufanywa na'Wakristo’ wa leo ni ya mpango mmoja isiyofuata utaratibu kama ya majaribio ya dini nyingine; Vivyo hivyo hata dini ya waabudu uchawi imejaribu mambo hayo hayo ya kunena kwa kupayuka - payuka, Waislamu vile vile wanaweza kutumik a kama 'Ishara’ za mpango wa namna hii na hizo zilizodaiwa na Ukristo wa sasa. Lakini maana nzima ya karama za Roho zilizomilikiwa katika karne ya kwanza ilikuwa kuonyesha bayana ukuu wa Ukristo wa kweli juu ya dini nyingine zote. Uhakika ni kwamba 'Miujiza’ ya Ukristo wa siku hizi upo kwa mpangilio wa namna moja na dini nyingine, yaonyesha kwamba karama za Roho Mtakatifu zilizokuwa katika karne ya kwanza kwa sasa hazishikwi na watu.
Taarifa nyingine zenye maana katika eneo hili zimetolewa katika Upentekosti wa Williamu Camp bell (Makanisa ya Kristo, mwaka 1967). Anaonyesha ya kwamba dini nyingi za kipagani zina jambo hili hili la kunena 'Lugha’. Hivyo katika sehemu ya Kawaii, makuhani wa Mungu Oro wamewaza kuwa anafunua nia yake kwa sauti isiyosikika ambayo inatafsiriwa na makuhani wengine. Jambo hilo hilo hutokea katika mikutano ya Pentekosti. Ushindi unaoendelezwa na Uislam juu ya Ukristo katika sehemu nyingi za Afrika kwa kweli usingeonekana kama 'Ukristo’ wa watu wengi ulikuwa unafanya miujiza ya kweli kwa utaratibu na kwa nguvu zenye kuthibitisha za wale waliokuwa karne ya kwanza. Kwa kweli wale wenye kuwa na'Msaidizi’ wa kipawa cha Roho Mtakatifu watafanya, naam, “Kazi kubwa” kuliko alizofanya Yesu (Yoh. 14: 12,16). Udhuru wa kwamba Wakristo wanaweza kufanya miujiza ya namna hii kama walikuwa na imani zaidi, hapa wanakumbana na shida kubwa. Aidha wakiwa na karama zenye miujiza ya msaidizi, au wakiwa hawana, na kama wanadai kwamba wanafanya - “ Kazi kubwa kuliko hizi atafanya” (Yoh. 14:12) - si'Utaweza kufanya’ !
2.5 Biblia ni Mamlaka pekee
Toka kile ambacho tumeona mpaka hapa katika somo hili, Roho ya Mungu inataja nia na kusudi lake, na nguvu ambazo anaweka vitu hivyo katika kutenda kazi. Tumetoa mkazo wa kwamba Roho hiyo kwa maelezo ya kwamba imefunuliwa kwetu katika kurasa za neno la Mungu. Matatizo mengi ya Ukristo wakati ule yote yameshuka katika kosa la kuhuzunisha kufahamu hili. Kwa kuwa ni vigumu kusadiki kuwa huu uwezo mkubwa umewekwa katika kitabu kimoja, sehemu zake zinazotuwia vigumu kuzielewa, ni kuvutwa kuona ya kwamba kuna namna ingine ya ufunuo wa Mungu kwa watu, kuliko Biblia. Kwa sababu ya hatia kubwa ya mwili wa mwanadamu (Yer. 17:9) unapata usafi kweli wa neno la Mungu (Yoh. 17:17) hivi huwa vigumu kuvumilia, wengi wameshindwa katika jaribu hili kwa kudai au kutaka namna nyingine ya ufunuo unaovutia zaidi katika nia ya mwili .
Sasa mifano michache imetolewa:-
Dini
Mfano mwingine wa
Ufunuo waliodai
Uvutiaji huu kwa faida ya mwanadamu
Mashahidi wa Yehova
Uchapishaji wa majarida Chama cha mlinzi, ambayo yameonwa kuwa yamevuviwa.
Hakuna bidii ya mtu inayohitajika kutafakari usahihi wa tafsiri ya Biblia jibu kwa kila jambo
Ukatoliki
Matamshi ya Papa na mawazo ya makuhani, wanadai yenyewe ni mawazo ya aina ya Mungu.
Hakuna haja ya kusoma Biblia -zamani Ukatoliki uliwavunja moyo watu na hata Kukatazwa kufanya hivi. Kuweka tumaini kwa wanadamu badala ya kufanya juhudi mtu ahakikishe mwenyewe
Wamormoni
Kitabu cha Mormoni
Kimeondoa hitaji la mafunzo ya Biblia ambayo ni magumu kuelewa. Kitabu cha Mormoni kinatoa nafasi ya wokovu kwa watu wote, wakati Biblia inasema kwamba kuna watu wengi wanaoishi na kufa bila tumaini kwa kutoitwa katika maarifa ya Injili
Ukristo wa
Kiroho.
‘Nuru ya ndani ambayo Imesemwa Kuwa ni Roho Mtakatifu
Wanasadiki chochote wanachohisi ni sawa, kama inavyodhaniwa Roho ya Mungu inaongoza na Kuvuviwa katika njia zisizo unganika na Biblia.
Yote haya yanatokeza haja ya kufahamu ukubwa wa Biblia kuwa ni neno la Mungu, na kuchunguza kurasa zake kwa kupata ujumbe wa kweli. Swali, “Biblia moja, Makanisa mengi - ni kwa nini ?” kwa upana limejibiwa linapofahamika ni jinsi gani kila kanisa lina, kwa kiwango fulani, limedai namna nyingine ya ufunuo wa Roho ya Mungu, yaani, mapenzi yake, mafunzo na fikira, kwa nyongeza katika huo wa Biblia.
Kama unataka kupata kanisa moja la kweli, imani moja ya kweli na ubatizo mmoja wa kweli (Efe. 4:4 -6), wito unapasa kukujia kwa sauti kubwa na dhahiri - “Rudi katika Biblia !”
Tumeacha kitambo tulichoandika sehemu ya 4:
Je ! Roho Mtakatifu ni Mtu?
Somo la 2.1 na 2.2 yametoa ushahidi mkubwa wa kwamba Roho ya Mungu unatajwa uweza wake, unaotoa “Nia” yake katika kila njia pana. Kwa sababu ya namna Roho ya Mungu itendavyo kazi vivi hivi ni kioo sahihi cha nafsi na utu wa Mungu, baadhi ya watu wameleta ubishi na kusema ya kwamba Roho ya Mungu ni mtu ambaye pia ni Mungu. Kusoma tena kwa makini sehemu zilizotangulia zitaonyesha ya kwamba Roho ya Mungu ni akili na uweza wake; kama hivyo ndivyo, basi hakuna mfano wa kwamba nia - akili au nguvu yaweza kuwa mtu. Umeme ni nishati - nguvu isiyoonekana ambayo inatoa matokeo kwa mtu anayeutumia, lakini umeme hauwezi kuitwa ni mtu, Roho ya Mungu ina upendo wake, kama sehemu ya tabia yake, na tena unatajwa uweza wake, lakini hautajwi kuwa ni mtu aliyejitenga toka kwake.
Ni makosa ya kuonekana wazi kama shauri hili lilivyokosewa (la Roho Kuwa ni mtu) na kuonekana, ni dhana iliyoaminiwa na 'Wakristo’ walio wengi, kwa kuwa wanasadiki mafundisho ya 'Utatu’. Kwa maana hii imesemwa kuwa wapo Miungu watatu ambao kwa njia isiyoeleweka vile vile kuwa ni yule yule Mungu Baba, Roho Mtakatifu na Yesu. Watu hao hao wametoa kadhia kuwa Mungu si mtu, lakini wanasema ya kwamba Roho Mtakatifu ni mtu; hapa maneno yanaachana kabisa. Tena, Roho Mtakatifu atafanywa kuwa ni Baba ya Yesu.
Kuna sababu nzuri ya kuamini ya kwamba'Utatu’ kimsingi lilikuwa ni wazo la kipagani lililoingizwa katika Ukristo - basi hili neno halitoki katika Biblia. Wakiisha kubali dhana hii ya kuwa Mungu ana nafsi tatu, ndipo Wakristo wamelazimika kufikia wazo lisilo kweli na gumu kueleweka la kwamba uweza / Roho ya Mungu ni mtu, aliye Mungu tena, ingawa si Mungu. Wanapokabiliwa na maneno yaliyo mbali na akili kwa maono yao, njia ya kukwepa watu wengi zaidi ni kwa watu hawa kudai kwamba Mungu ni siri, nasi tukubali mambo haya kwa imani pasipo kutaka maelezo yenye maana ya akili.
Kwa maana hii ni kushindwa kutazama ushahidi ulio katika Agano Jipya katika Siri ya Mungu kuwa imefunuliwa ndani ya neno na kazi ya Kristo:-
“Kwa maana ndugu zangu sipendi msiijue siri hii” (Rum. 11:25).
“Kwa kuhubiri kwake Yesu ……. Na ufunuo wa ile siri” (Rum. 16:25)
“Akiisha kutujulisha siri ya mapenzi yake” (Efe. 1: 9; 3:3).
“Angalia, nawaambia ninyi siri …..” (1 Kor. 15:51).
Mahubiri ya Paulo yalikuwa “Katika kujulisha ile siri ya Injili” (Efe. 6:19; Kol. 4:3).
“Siri ile ……. Sasa imefunuliwa kwa watakatifu” (Kol. 1: 26, 27).
Kwa mkazo huu wote - ni kwamba - ni kule si sasa kuna siri yoyote iliyofungamana na mafundisho makubwa, atakuwepo tu mtu mwingine aliye gizani ambaye atadai kwamba kuna siri. Na mtu huyu hana wasi wasi wa kwamba Biblia inaita jina badala ya “Babeli” utaratibu wa dini ya upotovu ulioelezewa katika ufunuo, ni 'Siri’ (Uf. 17:5)? kidokezo dhahiri ni kwamba utaratibu huu unatangaza ya kuwa imani zake ni siri; lakini waumini wa kweli wanafahamu siri ya mwanamke huyo (Uf. 17:7).
Fikira hizi zisizo dhahiri, kwa kweli zimetarajiwa toka kwao wawekao fahamu zao kwa Mungu juu ya mawazo ya vitu kama akutanavyo mwanadamu, au shughuli zisizo wazi, zisizoeleweka za nguvu nyingine kiroho juu ya fikira zao. kama kweli tunatarajiwa kweli kuwa wanyenyekevu katika fundisho la Neno la Mungu , kinachofuata tena tunatakiwa kutumia nguvu za kufikiri na akili ya kupata elimu ili kwamba tuvumbue ujumbe wake.
Mhubiri awaye yote wa Injili ambaye taarifa zake zimo katika Biblia, hakukimbilia kamwe kusema,'Hii ni siri sana, hamwezi kuanza kuielewa’ badala yake, tunawasoma wakiwasihi watu kutumia akili nao wavutwe na wazo litokalo katika Maandiko.
Katika kuhubiri kwake aina ya Injili kubwa ambayo tunaiona katika masomo haya, Paulo “ alihojiana nao kwa njia ya Maandiko, akayafunua na kuwaeleza ya kwamba ilimpasa Kristo kuteswa, na kufufuka katika wafu” (Mdo. 17:2,3). Huu ulikuwa ni utaratibu wenye muundo wa kufikiri maneno ya Biblia wastani wake ulio bora; fungu hili la maneno linatangulia taarifa “Paulo, kama ilivyokuwa desturi yake …… alihojiana nao ……. “ Basi, huu ulikuwa ni mtindo wa kawaida yake (tazama tena Mdo. 18:19). Kwa kupatana na huu, kipindi cha kampeni kubwa pale Korintho, Paulo “alitoa hoja zake katika Sinagogi kila sabato, akijaribu kuwavuta Wayahudi ……. (Lakini) walipopingana …..” (Mdo. 18:4-6). Wale walioongoka walienda njia ya ushawishi wa maneno ya Paulo ambayo msingi wake umo ndani ya Biblia; hapa hayakuwa 'Maono ya Yesu ndani ya chumba changu’; 'hisia zilinijia zisizoelezeka’, 'Nilikutana na Bwana jioni moja’.
Elewa vile vile, ya kwamba habari iliyovuviwa inatoa ombi la maneno yenye akili na busara, kwa kuonyesha kwamba “Walipingana wenyewe” vivyo hivyo kule Antiokia, Paulo na Barnaba “walisema nao (neno), wakawatia moyo …..” (Mdo. 13:43). Eneo lao lililofuata la kusita lilikuwa ni Ikonio, mahali ambapo “Walinena kundi kubwa …. Waliamini “ (Mdo. 14:1).
Baadaye kidogo aliposimama kutetea maisha yake, maneno yale yale yenye utukufu na busarra yaliendelea katika kuvuviwa tumaini imara la Paulo kwa sababu ya kipindi kijacho: “Alitoa hoja zake katika habari ya haki, na kuwa na kiasi, na hukumu itakayokuja” na udhahiri huu unaopenya hata mwenye kubeza, hakimu wake “alihofu” (Matendo ya mitume 24:25).
Kwa kuwa kuongoka kwetu kunakuwa juu ya msingi huu wa njia ya kutumia akili, tunaweza kutoa maelezo yenye busara ya Biblia na tumaini letu na mafundisho:-
“ kuwa tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizae habari za tumaini lililo ndani yenu”(1Petro. 3:15).
Kusema katika sauti yenye busara juu ya matukio ya mtu mwenyewe si kutoa hoja ya tumaini la Injili. Utegemezi unaoendelea juu ya ushuhuda wenyewe kama njia ya kuhubiri Wakaristo wengi wa Kiinjili, ukosefu wa 'hoja ya jibu la kutumia’ unajitokeza kwa 'tumaini’ lao. Maelezo yote yamezuka miongoni mwa Wakristo hawa kwa'kuwawezesha katika kushiriki yale Bwana aliyofanya katika maisha yangu’ n.k. Hizi hadithi fupi za maisha ya mtu zatofautiana vikali na maneno ya Paulo, “Hatujihubiri wenyewe, bali Kristo (2Kor. 4:5) - na kama toka mtu aliyekuwa na uhusiano binafsi na Yesu” zaidi kuliko wengi.
Maneno ya kutumia akili, maana ya jinsi ya kuongoka kwetu kibiblia yaweke mfano mzuri wa uhusiano wetu mpana na Mungu katika siku zetu zilizobaki. Mifano yetu, kama siku zote, ni ya Wakristo wa kwanza waliyotumia kwa “Kutoa Hoja” katika kutatua matatizo yao ya mambo ya kutoa mashauri (Mdo. 6:2).Nyaraka za Agano Jipya tena zinawasadikisha wasomaji wao wafahamu kutumia akili ya maneno ya Biblia. Basi, “Kwa akili ya kufahamu” jinsi makuhani wakuu walivyokuwa chini ya torati ya Musa, tunaweza kuelewa habari moja moja kuhusu kazi ya Kristo (Ebra. 5:3) akiisha unena upendo wa Mungu unaozidi katika Kristo, Paulo anatoa sababu ya kwamba ndiyo “Ibada yenu yenye maana (Kutuumia akili) sisi wenyewe kujitoa kabisa kwake katika kuitikia (Rum.12:1). Basi kuitikia kwetu katika maneno ya Biblia ni kumoja na kutumia 'akili’ yetu kunakopatikana toka katika neno la Mungu.
Katika mwangaza wa yote haya, yatakuwa dhahiri kwamba si busara kudai ya kuwa roho ya Mungu ni nafsi peke yake ambayo si Mungu lakini wakati huo huo ni Mungu - na kwa kukabili wazo hili kwa kusema kwamba jambo hili lote ni lenye siri na kwamba kutumia akili si muhimu, kwa maneno ya Biblia halikubaliki. kama hatuwezi kuchukua maneno toka Maandiko, basi kujifundisha kote Biblia ni bure, hakuna haja ya kuwa na Biblia, ambayo inaweza kupimwa kama maneno yanayofikiriwa kuwa kweli matamu tu au neno la kitabu kinachovutia. hiki kitabu pia kinaonekana kuwa juu ya makabati ya Wakristo wengi.
Ingawa hivyo, katika tumaini lao, baadhi ya wanaosadiki kuwa Roho ya Mungu ni mtu wanajaribu kutoa sababu za Biblia. Mafungu ya maneno yaliyonukuliwa ni yale ambayo yanataja roho wa Mungu kwa msemo wa peke yake, kama “Mfariji -Msaidizi” katika Yoh. 14:16, au ushahidi wa kuwa roho “alihuzunishwa”.
Tumeonyesha kwa kuandika bayana katika somo la 4.3 kuwa “Roho ya Mwanadamu yaweza kuchukizwa (Mdo. 17:16), kufadhaika (Mwa.41:8) au kushangilia (Luka. 10:21). “Roho” yake, yaani, nafsi yake hasa, akili na kusudi lake, vinavyozusha matendo yake, kwa hiyo husemwa kuwa ni mtu tofauti, lakini bila shaka, si hivyo hasa, Vile vile, Roho ya/wa Mungu, yaweza kusemwa kwa jinsi hiyo hiyo.
Tena inabidi ieleweke ya kwamba mara nyingi Biblia imetumia msemo kutaja kitu au jambo kama ni mtu inaposema mambo ya kuwazika, kama. Hekima imetajwa kana kwamba ni mtu katika kitabu cha Mithali 9:1. Hivi ni kwa kutuonyesha mtu gani aliye na hekima anavyofanana katika kutenda matendo;'Hekima’ haiwezi kuwepo isipokuwa ndani ya akili ya mtu, ndivyo shauri hili la kuita kitu kana kwamba ni mtu limetumika. Maelezo zaidi juu ya hili, tazama tumeacha kitambo …… sehemu ya 5,
“Jambo la kuita kitu kama mtu”.
Tumeacha kitambo sehemu ya 5: Kawaida ya kuita kitu kana kwamba ni Mtu
Wengine itakuwa vigumu kufahamu maelezo ya kawaida yanayomtaja Ibilisi kuwa ni kiumbe au mtu, kwa sababu Ibilisi ametajwa mara nyingi katika Biblia kana kwamba ni mtu, labda maelezo haya yanawachanganya watu wengine. Haya kwa urahisi yameelezwa kwa kuonya kuwa ni sura za Biblia zilizotambulika za kwamba kitu kisicho na uhai kama Hekima, Mali, Dhambi, na Kanisa vyote hivi vinatajwa kana kwamba ni mtu, lakini katika suala la Ibilisi pekee baadhi ya nadharia za kuwazika tu zimetungwa kuzunguka pande zote. Mifano ifuatayo itaeleza kiini:-
HEKIMA IMEITWA KAMA MTU
“Heri mtu yule aonaye hekima, na mtu yule apataye ufahamu. Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi. Yeye anathamani kuliko marijani, wala vyote uvitamanivyo havilingani naye”
(Mithali 3:13 -15).
“Hekima ameijenga nyumba yake, amezichonga nguzo zake saba”
(Mith. 9:1)
Mafungu haya ya maneno, kwa kweli sura zilizobaki ambamo yanaonekana, yanaonyesha ya kwamba hekima imeitwa kana kwamba ni mtu kama mwanamke katika Biblia ya kiingereza, bali kwa sababu hii, hakuna mtu anayewaza ya kuwa hekima ni mwanamke halisi mzuri anayetembea akizunguka pande zote za dunia; wote wanajua kwamba ni tabia ya kutamanika sana ambayo watu wote walijaribu kujipatia.
MALI IMEITWA KANA KWAMBA NI MTU.
“Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili: kwa maana atamchukia huyu na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na Mali” (Mith. 6:24).
Hapa tunasoma Mali imefananishwa na Bwana. Watu wengi wanajitahidi mno kupa ta mali na kwa njia hii anakuwa ni Bwana wao. Yesu anatuambia hapa ya kwamba hatuwezi kufanya hivyo na halafu kumtumikia Mungu inavyostahili wakati huo huo. Fundisho ni jepesi lenye maana, lakini hakuna mtu awaye yote anayekubali toka hili ya kwamba mali ni mtu aliye na jina.
DHAMBI IMETAJWA KAMA NI MTU
“…… kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi” (Yoh. 8:34). “ Dhambi imetawala katika mauti” (Rum. 5:21). “Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii, mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii, kwamba ni utumishi wa dhambi uletao mauti, au kwamba ni utumishi wa utii uletao haki” (Rum. 6:16)
Kama ilivyo katika suala la Mali, dhambi imelinganishwa hapa na Bwana, nao wale watendao dhambi ni watumwa wake. Si usomaji mzuri kwa fungu la maneno linalothibitisha kwa kukubali ya kwamba Paulo anafundisha ya kuwa dhambi ni mtu.
ROHO IMEITWA KANA KWAMBA NI MTU FULANI
“Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote: kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe …” (Yoh. 16:13).
Hapa, Yesu aliwaambia mwanafunzi wake ya kwamba watapokea nguvu za Roho Mtakatifu, nalo jambo hili lilitimia kwenye siku ya Pentekoste, kama lilivyoandikwa katika matendo 2:3 -4, mahali ambapo pamesemwa ya kuwa “Kukawatokea ndimi zilizogawanyika, kama ndimi za moto, uliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa “Roho Mtakatifu” kwamba mamlaka yao itakuwa kwa Mungu. Roho Mtakatifu hakuwa mtu fulani bali ilikuwa ni nguvu, na Yesu alipokuwa anainena alitumia tamshi lake'Yeye’.
MAUTI IMEITWA KAMA MTU
“Tazama, farasi ya rangi ya kijivu jivu, na yeye aliyempanda jina lake ni Mauti” (Ufunuo. 6:8)
TAIFA LA ISRAELI LIMEITWA KANA KWAMBA MTU
“Mara ya pili nitakujenga, nawe utajengwa, Ee bikira wa Israeli mara ya pili utapambwa kwa matari yako ……” (Yer. 31:4).'Hakika nimesikia Efraimu, akijililia hivi; umeniadhibu nami nikaadhibika, kama ndama asiyeizolea nira; unigeuze, nami nitageuzwa; kwa maana wewe u Bwana,
Mungu wangu’ (Yer. 31:18).
Fungu lenyewe la maneno haya linafunua dhahiri ya kwamba nabii hamtaji bikira halisi au Efraimu akiwa ni mtu, bali ni taifa la Israeli, ambalo katika mfano huu limetajwa kana kwamba ni mtu.
WAAMINIO KATIKA KRISTO WAMEITWA KANA KWAMBA NI MTU MMOJA
“Hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana mwana wa Mungu, hata kuwa'Mtu’ mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo” (Ef. 4:13).”Upo mwili mmoja” (Ef. 4:4) “Ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake” (1Kor. 12:27). “……Kristo ni kichwa cha Kanisa: naye ni mwokozi wa mwili” (Ef. 5:23). “Naye (Kristo ndiye kichwa cha mwili; ….. sasa anayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu, tena nayatimiliza katika mwili wangu yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo, kwa ajili ya mwili wake,yaani, Kanisa lake” (Ko.. 1:18,24). “Nimewaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi” (2 Kor. 11:2) “ …..harusi ya mwana kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari” (Uf. 19:7)
Ni bayana haya hizi zote zataja jamii ya watu waliokuwa waumini wa kweli wa Kristo, mara nyingine wametajwa ya kuwa ni'Kanisa’ Ingawa hili halipaswi kujumuishwa na makanisa yoyote ya kiorthodox yaliyopo siku hizi, ambayo ni muda mrefu yamekoma kuwa ni ya waumini wa kweli kwa Kristo.
Waumini wa kweli, yaani, wanaoshika na kuamini mafundisho ya kweli yaliyofundishwa katika Biblia, mara nyingine wametajwa kuwa ni “Bikira safi” wakionyesha usafi wa maisha wanayoendea'Kama mwili’ mfano unaofaa kwa kuwa kiasi kama mwili wa asili ulivyo na viungo vingi, vivyo kanisa la kweli lina majukumu mengi na kufanya kazi mbali mbali. Kanisa linaposhuhudiwa kuwa ni “Mwili”, hakuna mtu anayekosea maana ya mtu mmoja mmoja, wala watafanya kosa juu ya Ibilisi au shetani maana ya upuuzi kuwa ni mtu asiye na desturi ya kawaida au malaika aliyetupwa, wanawake hawakupata mawazo mabaya toka katika makanisa yaliyopotoka kwa siku zilizopita.
Yametengenezwa katika “Ufalme wa wakristo Umepotoka” (Christeridom Astray) na Robert Roberts.
Tumeacha kitambo sehemu ya 6: Mambo ya kelvini
Miaka mia chache iliyopita, Kelvini alifundisha wazo la kwamba uteuzi ulikuwepo katika maisha yetu hapo kabla, hivyo basi uchaguzi wa kufanya tupendavyo kwa hiyari hauna juhudi juu ya wokovu wetu; aidha tulikwishachaguliwa kabla ili tupate wokovu au kukataliwa. wazo hili tena limeweka sura mpya katika mashauri mengine siku hizi:
kama hakuna maana kufanya bidii kubwa ya kujifunza Biblia au dini, kwa sababu kama tunaokolewa basi tutakuwa namna yoyote.
Ya kama yupo kiumbe aitwaye Ibilisi atulazimishaye kutenda dhambi na kuleta matata katika maisha yetu bila kujali mapenzi yetu. Wazo hili lisilo la kweli limejadiliwa katika somo la 6.
Ya kama hakuna haja kuomba matunzo ya Mungu katika hali ya maisha yetu, kama kulindwa wakati wa safari, kwa kuwa namna yoyote kila jambo lilikwisha pangwa. Walimwengu wana msemo, mara nyingi limesikika kwa bahati katika vyumba vya kuondokea wasafiri uwanja wa ndege,'Kama namba yako itatokea, itatokea tu’.
Makanisa ya kiinjili yanafundisha ya kwamba kwa muumini haiwezekani au kufahamu Biblia bila Roho Mtakatifu kutusaidia tuelewe.
Zipo sababu nyingi kamili za Biblia za kukataa hii aina ya elimu : -
Wazo lote la kumtii Mungu linafanywa kuwa ni upuuzi. tunaendelea kuambiwa siku zote katika Biblia kwamba yatupasa kutunza amri za Mungu, na kwa kufanya hivyo tunaweza kumpendeza au kutompendeza. Jambo hili lenye maagizo halina maana ikiwa Mungu anatulazimisha tumtii. Kristo anatoa wokovu kwa “Watu wote wanaomtii”
(Ebra. 5:9).
Waebrania 11 yaonyesha kwamba Mungu anapoingilia katikati ya maisha yetu na hatimaye kutupatia wokovu kumehusisha na imani yetu. Mifano mingi ya Biblia kuomba wokovu wa Mungu shida haiwi na maana kama kila jambo lilikwisha pangwa kabisa. Vivyo hivyo wazo la wokovu likiwa ni toleo la imani yetu kwa Kristo haliwi na maana tena.
Ubatizo ni sharti la wokovu (Marko. 16:16; Yoh. 3:3 -5). Hili wenye imani ya Kelvini wamekana. lakini, wokovu umewezekana kwa sababu ya kazi ya Kristo (2Tim.1:10), si kupitia wazo la kuwazika la kuchaguliwa kabla ya wakati . yatupasa sisi wenyewe kwa ufahamu tuchague kujiunga naye, mpango tunaofanya kwa kubatizwa. Mafungu ya maneno katika warumi 6:15 -17 yanatunena tunavyobadili mabwana katika Ubatizo, toka maisha ya dhambi hadi kuwa mtu wa kutii. “Kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii, mmekuwa watumwa wake yeye mnayemtii”. Lugha hii ya kujitoa mtu mwenyewe ni dhahiri inadokeza mapenzi ya hiari kama yalipopingana na kwisha chaguliwa kusiko na sharti. Kujitoa ni kwa kutii katika moyo mafunzo ya Injili (Rum. 6:17).
Hakuna maana kwa Mungu kutoa neno lake, kama namna yoyote tulikwisha chaguliwa. tena hakuna maana ya kuhubiri; lakini Biblia, pande zote mbili katika amri na kuandika mifano ya hii, inaonyesha kwamba ni kwa kuhubiri neno hata wanaume na wanawake kufika katika wokovu. “…..Neno la wokovu huu” (Mdo. 13:26) inabidi lipelekwe kwa watu.
Tutahukumiwa sawa sawa na matendo yetu (Uf. 22:12). Kwa nini, kama kutenda kwetu matendo tupendayo si muhimu katika kulingana na wokovu ? Paulo alisema ya kwamba Wayahudi wamejihukumu wao wenyewe kuwa hawastahili uzima wa milele kwa kulikataa neno la Mungu (Mdo. 13:46). Walikuwa wanajihukumu wenyewe - Mungu hakuwazuia. kama tukisema ya kwamba Mungu amewachagua watu wengine tangu mwanzo kupata wokovu na wengine wahukumiwe, basi kwa matokeo Mungu anawashurutisha watu kuwa watenda dhambi, kwa jinsi hiyo hiyo kama alivyotaka kuwalazimisha watu kuwa wenye haki. Kwa sababu ya dhambi ya Adamu “Mauti imewafikia watu wote, maana wote wametenda dhambi” (Rum. 5:12). ndiyo maana watu hufa, ikiwa ni adhabu kwa ajili ya dhambi kwa maana nyingine katika kipindi kabla ya dhambi ya Adamu.
1 Kor. 10 na mafungu mengi mengine ya maneno yameshika mfano wa waliokuwa zamani waliwahi kuwa na uhusiano na Mungu, lakini wakati ule wakaanguka, yakiwa maonyo kwa waumini. Uhakika ni kwamba upo uwezekano wa kuanguka toka hali ya neema (Gal. 5:4) maana yake ni kwamba hapawezi kuwepo 'aliyewahi kuokolewa siku zote akiwa ameokolewa’ utaratibu wa wokovu kama unavyotakiwa na wenye imani ya Kelvini. Tukiendelea tu kushika mafundisho ya kweli tutaweza kuokolewa (1 Tim. 4:16).
Ni dhahiri Yesu alifundisha ya kwamba kuelewa neno la Mungu kunategemea hatua fulani iliyo juu ya bidii yetu kufanya tupendavyo. “Asomaye, na afahamu” (Mathayo. 24:15). Hivi tunajiruhusu wenyewe kufahamu neno - hatulazimishwi. kati ya hivi upo usawa wa maneno yaliyorudiwa mara nyingi na Yesu ya kuwa “Aliye na masikio yenye kusikia ……. Na asikie” au afahamu. Kwa sababu hii kuwa na masikio yanayosikia, kumelinganishwa na kusoma neno la Mungu. Kwa kuwa Roho ya Mungu kwa ukuu sana imedhihirika katika neno lake kwa upana ambao Yesu aliweza kusema kwamba maneno yake yenye kuvuviwa na Mungu ni “Roho” (Yoh. 6:63) haiwezekani kwamba roho ya Mungu itatenda kazi juu ya mwanadamu, bila neno lake, ili kumshurutisha mwanadamu kuwa mtii katika neno.
“Yeyote atakaye” na “ayatwae maji ya uzima bure” (Uf.22:17), kwa kuitikia neno la uzima lipatikanalo katika Injili. Kwa kweli, hapa, ni kupenda kutenda atakavyo mtu kuliko kuchaguliwa tangu mwanzo bila kufikiri haja yetu binafsi kupata wokovu. vivyo hivyo matendo 2:21 “Na itakuwa kila (awaye yote) atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa” kwa kubatizwa katika jina hilo.
Tumeacha kitambo sehemu ya 7 : “Nanyi mtapokea Roho mtakatifu”
Petro alihutubia mkutano mkubwa siku ya Pentekoste, akamalizia kwa ombi lililo katika aya ya 38 kutubu, kubatizwa na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu. Huku kutajwa kipawa cha Roho ya Mungu kupo katika maneno yenyewe ya mitume wakiisha tumia karama hizo za kunena katika lugha katika mkutano, kunaelezea ya kwamba kufanya hivyo walikuwa wanatimiza unabii wa Yoeli unaohusu kupewa karama za kufanya miujiza (Mdo. 2:16 -20).kwa sababu hiyo inafaa kukubali kuwa ni kweli kwamba Petro alikuwa anaahidi karama za Roho kwa ule mkusanyiko wa Wayahudi waliokuwa wanamsikiliza. Mkutano ulikuwa ni wa Wayahudi, si watu wa Mataifa (Mdo. 2:5).Unabii wa Yoeli kupewa karama ulihusika hapo kwanza na Wayahudi pekee. Basi, Petro ana maana hii kwao: “Ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu” (Mdo. 2:39), labda ilikuwa yataja unabii wa Yoeli ya kwamba Wayahudi watapewa Roho na watoto wao (Mdo. 2:17 linganisha Yoeli 2: 28 -32). Panaweza kuwa na kidokezo hapa cha kwamba ahadi ya karama hizi zenye miujiza ilikuwa kwa vizazi vile viwili pekee - waliokuwa wanamsikiliza Petro, na watoto wao.
Tumeonyesha ya kwamba mwishoni mwa karne ya Kwanza (Yaani, karibu miaka 70 baada ya hotuba ya Petro) vipawa vilifikia mwisho. Jambo hili tena limethibitishwa na taarifa za kihistoria. Pia kipindi cha vizazi hivyo vipawa vya Roho vilipatikana kwa watu wa Mataifa: “Na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie” (Mdo. 2:39). Fahamu jinsi watu wa mataifa wanavyoelezewa ya kuwa “walio mbali” katika Waefeso 2: 14 -17.
Walakini, kuna sababu nzuri ya kuamini kwamba lililotokea katika Mdo. 2 ulikuwa ni utimizo mdogo tu wa hayo maneno ya Yoeli 2. Utimilizo mkubwa utakuwa hapo Israeli akiisha vamiwa na Jeshi kisha nalo likiisha haribiwa (Yoeli. 2:27), “Hata itakuwa, baada ya hayo ya kwamba nitamimina Roho yangu juu yao wote wenye mwili …..” (2:28). Si hata hayo masharti yakionekana tutaweza kutafuta utimizo wowote mwingine wa maneno ya Yoeli, mbali toka utimilizo huo mdogo ulionekana siku ya Pentekoste kama ulivyoelezewa katika matendo ya mitume 2.
Ahadi ya kupokea kipawa cha Roho baada ya ubatizo, bado kinaweza kusomwa na ushahidi mwingine kwetu leo. Kuna roho moja, lakini yaweza kuthihirika kwa njia mbali mbali (1 Kor. 12:4-7; Efe. 4:4).Katika karne ya kwanza hii ilikuwa katika vipawa vya miujiza; sasa kama vimeondolewa ni halali kabisa katika kuona utimilizo wa hiki “Kipawa cha Roho” kwa namna nyingine kilivyoahidiwa. “Kipawa cha Roho Mtakatifu”chaweza kutajwa 'Kipawa ambacho ni Roho Mtakatifu’, au katika kipawa ambacho Roho Mtakatifu anakisema yaani - kipawa cha msamaha wa wokovu ambao Roho -Neno lenye kuvuviwa la Mungu liliahidiwa. Ipo mifano mingi mingine ya matumizi haya ya neno “ ya, cha, na wa” (yenye kufahamika kuwili, katika ustadi) “Maarifa ya Mungu” (kol. 1:10) yaweza kuwa na maana maarifa ambayo Mungu anayo. Au maarifa juu ya Mungu. “Upendo wa Mungu” na “Upendo wa Kristo”
(1 Yoh. 4:9; 3:17; 2Kor. 5:14) ina maana upendo ambao Mungu na Yesu wamekuwa nao kwetu, au upendo ambao tunao kwao. “Neno la Mungu” laweza kuwa na maana neno kumhusu Mungu. Au neno ambalo limetokea kwa Mungu. Kipawa “cha” Roho Mtakatifu basi chaweza kutajwa kipawa ambacho Roho Mtakatifu anawezesha mambo na kuzungumzia sawa na kipawa ambacho kina nguvu za Roho Mtakatifu.
KIPAWA CHA ROHO : MSAMAHA
Rum. 5:16 na 6:23 inaeleza wokovu kuwa “Kipawa” - ikivuta mlinganisho na “Kipawa” cha Roho katika mdo. 2:38.Yaonekana kabisa kuwa matendo 2:39 unanukuu toka Yoeli 2:32 kuhusu wokovu kana kwamba hivi ndivyo kipawa cha Roho kilivyonukuliwa. Petro alitaja kipawa kilichokuwa kimeahidiwa kwa wale “Walio mbali” anataja katika kusema kwa Isaya 57:19: “Amani (ya Mungu kwa kusamehewa) kwake yeye aliye mbali”. Waefeso 2:8 aya hii inaeleza kipawa hiki kuwa ni wokovu, na kusema kwamba “katika Roho mmoja (Kipawa hiki) sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Baba” (2:18). hiki kimefanywa thabiti kwa uhakika kwamba Efe. 2:13 -17 tena kinatajwa kwa kusema katika Isaya 57:19: “Ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo. Kwa maana yeye ndiye amani yetu …..akaja akahubiri amani kwenu ninyi mliokuwa mbali” Isaya 30:1 unawalaumu Wayahudi kwa kuutafuta msamaha kwa njia yao wenyewe kuliko toka kipawa cha Roho ya Mungu:'Wajifunikao kwa kifuniko (upatananisho) lakini si cha Roho yangu, wapate kuongeza (Badala ya kutoa) dhambi juu ya dhambi” Isaya 44:3 unaeleza msamaha wa siku hizi kwa Israeli kwa maneno haya: “Kwa maana nitamimina maji …… na vijito vya maji juu ya mahali pakavu (ukavu kiroho - Isa. 53:2): nitamwaga Roho yangu juu ya wazao wako, na baraka yangu juu yao utakaowazaa” Baraka ya uzao wa Ibrahimu ni kwa kusamehewa kwao kwa njia ya Kristo (Mdo. 3: 25, 26) msamaha uliopo hapa ni sawa na kumwagiwa Roho juu ya Wayahudi.Huu msemo wazi wa Yoeli 2, na matendo 2. Gal. 3:4 unaweka yote haya katika maneno mengi sana; ili kwamba baraka ya Ibrahimu (Msamaha) uwafikie mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho” Basi 1 Kor. 6:11 unanena kuoshwa dhambi zetu “Kwa Roho ya Mungu wetu” Upo usawa kwa warumi kati ya sisi kupokea “neema …..upatanisho …. Roho” (1:5; 5:11; 8:15), na kuonyesha muungano kati ya kipawa (“Neema”) ya Roho na msamaha unaotuongoza hata kupata upatanisho. Ni vigumu kuelezea zaidi ni kiasi gani Agano Jipya linategemea msemo na mtungo wa maneno ya Agano la Kale, hasa kwa mtazamo wa kwanza wa Wayahudi na ushawishi uliokuwa na nyaraka. Mara kwa mara katika vitabu vitano vya kwanza katika Biblia (Pentateuch) na Yoshua Mungu anaahidi kuwapa nchi watu wake - “nchi akupayo Bwana Mungu wako uimiliki” ni maneno ya kawaida. Kifani cha nchi iliyochini ya Agano Jipya ni Wokovu; basi ni kipawa cha Mungu ambacho sasa ni mtazamo, na kuwa pamoja na msamaha wa dhambi. Gal. 3: 2,5 linganisha na 3:8 -12, inasawazisha kupokea roho na. Kupokea baraka za Ibrahimu za wokovu na msamaha. “Ahadi ya Roho”(Gal. 3:14) imesemwa katika maneno yenyewe ya ahadi kwa Ibrahimu.
Petro aliwataka wayahudi watubu kabla ya kuweza kupokea kipawa; hiki kilihusisha sala ya mtu binafsi. hapo yaonekana kusadiki ya kwamba kipawa cha Roho ni namna ya kuelezea sala iliyojibiwa. Kupewa “Vitu vyema wale waombao” katika sala ni mamoja kama kupewa (kipawa) cha Roho Mtakatifu (Math. 7:11; linganisha Luk. 11:13).Wafilipi 1:19 unasawazisha “Kuomba kwenu ni kuruzukiwa Roho wa Yesu Kristo”. Vile vile, 1 Yoh. 3:34 tunasoma ya kwamba tunapewa Roho kama toleo la kutii kwetu amri; aya ya 22 inasema kwamba kutii amri hizo kunapelekea kujibiwa maombi yetu. Basi, ujasiri wetu ni kwa sababu maombi yetu yamesikiwa (1Yoh. 5:14) na tena kuwa na Roho (1 Yoh. 3: 21, 24; 4: 13), elewa maelezo haya yanalingana Neno'Kujifunza’ kwa neno la kiyunani ni'Charis’, mara nyingi limetafsiriwa “Neema” litaonyesha kwamba mara nyingi limetumika kwa muunganiko na kipawa cha Roho.
“Kwa (kipawa) cha neema ya Bwana Yesu Kristo tutaokoka” (Mdo.15:11). Lakini wazo la'neema’ mara nyingi limegawanyika na ombi lililojibiwa (kama kutoka 3: 12; 34:9; Hesabu 32: 5; Zab. 84:11; 2Kor. 12:9; Ebr. 4:16; Yakobo. 4:6 na mstari wa 3). Zakaria 12:10 unasema siku ya mwisho kumwagiwa “Roho ya neema na kuomba” wayahudi. Huu unaelezea kwa ufupi tunachodokeza - kuwa sala (“Maombi”) yanaleta kipawa cha Roho katika maana ya msamaha, na huku kupewa Roho kwa kujibu maombi kumeonyeshwa katika namna ya toba ya kiyahudi ya karne ya kwanza na siku za mwisho. kwa maneno hayo hayo yenyewe ayasemayo Paulo, “Karama na mwito wa Mungu” kufikia toba na msamaha (Rum. 11 29).
MSAIDIZI
Kukaribia huko huko kunaweza kutumika katika ahadi ya msaidizi katika milango ya Yohana 14: na 16. Kimsingi huyu alitajwa ni nguvu zenye miujiza walizopewa wafuasi, ambao waliahidiwa hapo kwanza, pia ahadi inaweza kutuhusu nasi katika maana isiyo na miujiza. Karama zilikuwa kwa “Kuwakumbusha mambo yote, niliyowaambia” (Yoh. 14:26), kwa kuthubutu kuwezesha kuandika taarifa za Injili.
Neno “kuwakumbusha” lenyewe lawekea mipaka jambo lenye miujiza ya ahadi ya msaidizi kwa wafuasi, walioishi na Yesu wakati wa utumishi wake. Waliweza kuwa na maneno ya Yesu tu yaliyorudi katika kumbukumbu zao na msaidizi. Lugha ya ahadi ya'Msaidizi’ inatumika pia katika uwezo wa Biblia iliyokamilika. Kwa sababu hiyo tunaweza kumalizia ya kuwa hizi na ahadi nyingine za Roho zilitumika katika mfano wa miujiza kwenye karne ya kwanza, lakini sasa yatuhusu sisi katika ufunuo wa Roho kwa njia ya neno la Mungu lililoandikwa katika Biblia. Bila shaka, ni kweli kwamba Roho ya Mungu ilidhihirika katika neno lililoandikwa zamani, lakini hili ulikuwa ni ufunuo wa sehemu ukilinganishwa na utimilizo (“Ukamilifu”) ambao sasa tunao katika neno la Mungu lililokamilika (1 Kor.13:9 -13). kwa sababu hii ni kwamba haujakuwepo ufunuo wowote mwingine ulioandikwa toka kwa Mungu baada ya kuondolewa karama mara Agano Jipya lilipokamilika. Kadhia za kitabu cha Wamormoni na vingine kama hivi vilivyochapishwa, vinadokeza kwamba Biblia si ufunuo uliotimilika - kutokuwepo karama za roho leo kunathibitisha ni hivyo. Kama tunataka kuutumia utimizo wote wa Mungu katika ufunuo wake ulio katika Biblia, yatupasa tutumie kila sehemu yake, sehemu zote mbili Agano la Kale na Agano Jipya, wakati huo tu mtu wa Mungu anaweza kuanza kuwa kamili kama ukamilifu wa Mungu, uliodhihirika katika neno.
Tumeacha kitambo sehemu ya 8 : “ Na ishara hizi zitafuata“ (Marko. 16:17).
Neno hili limekazwa, ya kwamba kila mtu aaaminiye kweli atapokea karama zenye miujiza. Lakini hili linathibitisha mno -“Watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono juu ya wagonjwa, nao watapona” (Marko 16:18). Hii si ahadi ya mambo ambayo kinadharia yaweza kutokea ikiwa aaminiye alikuwa na imani ya kutosha; hizi zilikuwa ahadi za uhakika kwa udhahiri kitakachofanywa na Waaminio. Ishara hizi zilipofanywa kwa uwazi, ahadi ya mstari huu haiwezi kutuhusu sisi kwa wakati uliopo. Unaweza kukumbuka jinsi Paulo aliweza kumshika nyoka mwenye sumu bila kugongwa (Mdo. 28: 3 -7), uthibitisho wa mahubiri yake ukatokea ya kuwa yametoka kwa Mungu.
Wakristo wa madhehebu yaitwayo yote ya kiroho waliodai kuwa na karama kipindi cha wakati uliopita miaka mia moja iliyopita, haukuwepo ushuhuda wenye ukweli wa nguvu hizi kutendwa. Kila aaminiye asipoweza kuonyesha ishara za ukubwa huu, ahadi hii haitahusu leo. Hii inatuacha na dhana tuliyoileta toka kwenye uchunguzi wetu kwa Biblia ifundishayo kuhusu Roho: hizi karama zenye miujiza zilikuwa na wakristo wa kwanza katika karne ya kwanza, lakini zilikoma kushikwa baada ya Agano Jipya maandiko yake kukamilika.
Aya ya mwisho kwa Marko 16 inadokeza kuwa miujiza “itafuatana” na hao walioamini kwa madhumni maalum ya kuthibitisha neno la Injili lililosemwa “Ishara zitafuatana na hao waaminio …….. wakaenda na kuhubiri kila mahali, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kuthibitisha neno kwa ishara zilizofuatana nalo” (Marko 16:17,20). Mara neno lililotamkwa likaandikwa kwa ukamilifu, kama tulivyonalo sasa katika Agano Jipya, hapakuwa na haja ya Ishara za Miujiza kuwafuata wale walioamini.
Maelezo yaliyoandikwa chini ya Ukurasa :
Siku hizi yameenea mno madai ya kuwa na karama za Roho ya kwamba katika mwaka 1989 mijadala miwili ya halaiki ilifanyika kati ya mchungaji wa dhehebu la kiroho, Yohana Liliekas, na Wakristadelfiani wawili; Bwana John Allfree na mwandishi wa sasa. Mwendo ulikuwa: “Je ! karama zenye miujiza ya Roho Mtakatifu wanayo watu leo?” Mwaliko ulitumwa kwenye makanisa mengi ya U.K; ukatokea mkutano wa watu walioungana zaidi ya watu 1000. Inastahili kusadiki ya kwamba' Ushuhuda’ mzuri sana wenyekuwa na karama ungeonyeshwa. Nakala ya Habri inapatikana toka kwa :
SLP 2950, Mbeya
Somo la 2 : Maswali
1.Kati ya haya yafuatayo ni maneno gani yana maana ya 'Roho’ ?
a) Nguvu b) Takatifu
-
Pumzi d) Mavumbi
-
Roho Mtakatifu ni nini ?
-
Mtu b)Nguvu
c) Uweza wa Mungu d)Sehemu ya Utatu.
-
Biblia iliandikwa kwa jinsi gani ?
-
Watu waliandika mawazo yao wenyewe
-
Watu waliandika Mungu alikuwa na mawazo gani
-
Watu walivuviwa na Roho ya Mungu
-
Baadhi ya sehemu walivuviwa, sehemu nyingine hapana.
4. Ni sababu zipi zifuatazo zilitolewa zenye karama ya miujiza ya Roho ?
-
Kusaidia tendo la kuhubiri Injili
-
Kuendeleza kanisa la kwanza
-
Kuwashurutisha watu wawe wenye haki
-
Kuwaokoa mitume toka katika shida zao wenyewe.
5. Kutoka wapi tunakoweza kujifunza kweli ya Mungu ?
-
Kwa sehemu katika Biblia, kwa sehemu toka fikira zetu wenyewe
-
Toka Roho Mtakatifu akituambia jambo moja moja mbali ya kusoma Biblia
-
Toka katika Biblia pekee
-
Toka kwa watumishi / Makuhani wa dini
-
Taja baadhi ya karama za Roho zilizokuwepo karne ya Kwanza.
7. Ni lini ziliondolewa ? Je ! yawezekana kuwa nazo sasa ?
8. Ni jinsi gani Roho Mtakatifu anaweza kufanya kazi katika maisha yetu leo ?