MISINGI YA BIBLIA 03 - AHADI ZA MUNGU

Swahili

3.1 Ahadi za Mungu : Dibaji

 

Kwenye hatua hii ya masomo yetu tumefikia kufahamu upana wa Mungu ulivyo na jinsi anavyofanya kazi kwa kufanya hivyo tumepanga idadi ya makosa yahusuyo mambo haya. Sasa tunataka kuangalia kwa uhakika zaidi mambo ambayo Mungu “amewaahidi wampendao” (Yakobo 1:12; 2:5) kwa kushika amri zake (Yah. 14:15)

Ahadi za Mungu katika Agano la kale zinatumaini la Kikristo ndani yake. Akijitetea hukumuni, Paulo alizungumzia thawabu ijayo iliyomfanya awe tayari kupoteza vitu vyote: “Na sasa nasimama hapa nihukumiwe kwa ajili ya tumaini la ahadi ya baba zetu …….. nami ninashitakiwa na Wayahudi kwa ajili ya tumaini hilo” (mdo. 26:6,7). alitumia muda mwingi wa maisha yake kuhubiri “Habari njema (Injili), jinsi Mungu alivyofanya ahadi kwa mababa, Mungu amewatimizia …… kwa kumfufua Yesu” (mdo. 13:32,33). Paulo alieleza kuwa kuamini hizo ahadi kulitoa tumaini la ufufuo toka wafu (mdo. 26:6 -8 na 23:8). Kufahamu kuja kwa pili yesu kwa hukumu na ufalme wa Mungu ujao (Mdo. 24:25; 28:20, 31).

Ahadi zote hizi zinadhamisha hadithi ya kuwa Agano la kale ni historia tu iliyotembea ya Israel isiyousema uzima wa milele. Mungu hakuamua ghafla miaka 2000 iliyopita kuwa atatupatia uzima wa milele kwa njia ya Yesu. Ni kwamaba kusudi lilikuwa naye tangu mwanzo.

“Katika tumaini la uzima wa milele, ambako Mungu asiyeweza kusema uongo, aliuahidi kabla ya ulimwengu kuanza;akalifunua neno lake kwa majira yake katika ule ujumbe kwa kuhubiri” (Tito 1:2,3). “Ule uzima wa milele, uliokuwa na Baba, ukadhihirika kwetu”(1 Yoh. 1:2)

Kwa kuwa kusudi la Mungu la kuwapa watu wake uzima wa milele lilikuwa naye tangu mwanzo , haikuwa na maana kuwa angebakia kimya kuhusu huo wakati wa miaka 4000 ya kujishughulisha na watu taarifa iliyo katika Agano la Kale. Kwa kweli, Agano la kale limejaa ahadi na unabii ambazo kila moja inatoa maelekezo ya tumaini hili ambalo Mungu amewatayarishia watu wake.

Ni kwa sababu hii ya kuwa kutambua ahadi za Mungu kwa mababa wa Wayahudi ni za muhimu kwa wokovu wetu: zaidi hapa Paulo aliwakumbusha waaminio katika Efeso ya kwamba kabla ya kujua mambo haya, “hawa kuwa na Kristo wakiwa wamefarakana na jamii ya Israeli, wageni wasio wa ahadi ile, mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani” (Efe. 2:12) - ingawa pasipo shaka walidhani ya kuwa imani yao ya awali ya kipagani iliwapa tumaini lingine na maarifa ya kumjua Mungu. lakini hili ni jambo la kufikiria sana kutokujua ahadi za Mungu katika Agano la kale -kwa ukweli “ni kutokuwa na tumaini,na pasipo na Mungu duniani’. Kumbuka jinsi Paulo alivyofafanua tumainai la Kikristo kuwa ni “tumaini la ahadi zilizofanywa na Mungu kwa baba wa Wayahudi” (Mdo. 26:6).

Ni ukweli wa kusikitisha kuwa makanisa machache yanaweka mkazo juu ya sehemu hizi Agano la kale ambazo wanatakiwa. “Ukristo” Ukristo umeharibika tabia na kuwa dini ambayo msingi wake ni Agano Jipya - ingawa hata wakati huo wanaelekea kutumia mistari michache ya kutoka hilo.Yesu ameweka kwa uwazi mkazo unaozunguka njia sahihi:

“Wasipowasikia Musa (yaani, Vitabu vya kwanza vitano vya Biblia alivyoandika) na mnabii, hawatashawishiwa hata mtu akifufuka katika wafu” (Luka. 16:31).

Nia ya mwili inaweza kufikiri kuwa kuamini kwamba Yesu alifufuliwa yatosha (Luka. 16:30), Lakini Yesu alisema ya kuwa pasipo kuelewa vema Agano la Kale, hii haitawezekana kabisa.

Kukata tamaa kwa Wanafunzi baada ya kusulubishwa kulifuatishwa na Yesu kwa kutoangalia kwao kwa makini kwenye Agano la Kale.

“Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote (kwa usahihi) waliyoyasema manabii: Je? Haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake ? Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe” (Luka. 24:25 -27).

Ona mkazo wake juu ya namna Agano lote la kale lilivyomsema yeye. sio kwamba Wanafunzi hawakuwahi kulisoma au kusikia maneno ya Agano la Kale, bali hayo maneno hawakuyaelewa Vizuri, na kwa sababu hii hawakuweza kuyaamini kwa kweli. hivyo kuelewa kwa usahihi neno la Mungu, kuliko kusoma tu, ni muhimu kukuza imani ya kweli. Wayahudi walikuwa washupavu kwa kusoma agano lao la kale (mdo. 15:21), Lakini hawakuelewa mistari yake iliyataja mambo ya Yesu na Injili yake, kwa kweli hawakuamini, na hivyo Yesu akawaambia:-

“Kama mungalimwamini Musa, mungeniamini mimi; kwa sababu yeye aliandika habari zangu. lakini msipoyaamini maandiko yake, mtayaamini wapi maneno yangu? (Yoh. 5:46,47).

Mbali ya kusoma Biblia yao, hawakuwa wanaona ujumbe wa kweli kumhusu Yesu, ingawa walipenda kudhani walikuwa wamehakikishiwa wokovu. Yesu ilimbidi kuwaambia.

“Mwayachunguza maandiko.(Yaani, kwa uzuri -mdo. 17:11); kwa sababu mnadhani kwa ujasiri kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake: na hayo ndiyo yaliyonishuhudia” (Yoh. 5:39)

Na ndivyo inaweza kuwa na watu wengi walio na elimu ya habari ndogo ya maneno ya maana ya matukio baadhi na mafundisho ya Agano la Kale: ni marifa tu ambayo yamechukua kwa kubahatisha. ujumbe wa ajabu wa Kikristo na Injili ya ufalme wa Mungu bado unawaepuka. ni lengo la somo hili kukutwaa toka nafasi hiyo kwa kukueleza maana ya kweli ya ahadi kubwa za Agano la Kale:-

  • Katika bustani ya Edeni

  • Kwa Nuhu

  • Kwa Abrahamu

  • Kwa Daudi

Habari zake zinapatikana katika vitabu vya kwanza vitano vya Biblia (Mwanzo - Kumbukumbu la Torati) vilivyoandika na Musa na katika manabii walio kwenye Agano la Kale. Yote yalishikamana na Injili ya Kikristo inapatikana humu. Paulo alieleza kuwa mahubiri yake ya Injili hii - akasema “Sisemi neno ila yale ambayo manabii na Musa waliyasema, kwamba yatakuwa; ya kwamba Kristo hana budi kuteswa na ya kwamba yeye kwanza kwa kufufuliwa katika wafu atatanganza habari za nuru kwa watu wake na kwa watu wa mataifa” (Mdo. 26:22,23), na katika siku zake za mwisho wimbo ulibakia ule ule: “Yeye (Paulo) akawaeleza kwa taratibu na kumshuhudia ufalme wa Mungu ….. kwa maneno ya sheria ya Musa na ya manabii, tangu Asubuhi hata Jioni” (mdo. 28:23)

Tumaini la Paulo, hilo kuu la Kikristo, liwe tumaini linalotuchochea nasi pia; kama ilivyokuwa nuru yenye utukufu mwishoni mwa tundu la maisha yake, vivyo liwe ni tumaini kubwa kwa kila Mkristo. likiwasha kwa kichocheo hiki, sasa tunaweza “Kuyachunguza Maandiko”.

3.2 Ahadi Katika Edeni

Kisa cha kutia huruma cha kuanguka mtu kimetajwa mwanzo sura ya 3. Nyoka alilaaniwa kwa kunukuu vibaya neno la Mungu na kumjaribu Eva kirahisi. kwa kutokutii kwao mwanaume na mwanamke waliadhibiwa. lakini mwanga wa tumaini unaingia ndani ya picha hii yenye giza Mungu alipowaambia Nyoka: -

“Nami nitaweka Uadui (kuchukua upinzani) kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake: huo (Uzao wa mwanamke) utakuponda kichwa na wewe utamponda kisigino” (Mwanzo. 3:15).

Huu mstari kwa kirefu umeongeza nguvu; tunahitajika kupambanua kwa makini mambo mbali mbali yaliyohusishwa. “Uzao maana yake mwana au mtoto, lakini vile vile unaweza kutaja watu waliojumuika na “Uzao” mmoja. Tutaona baadae ya kuwa “Uzao” wa Abrahamu alikuwa ni Yesu (Gal.3:16), lakini ni kwamba kama tukiwa “Ndani” ya Yesu kwa njia ya Ubatizo, Basi vile vile tumekuwa na uzao (Gal. 3:27 -29). Hili neno “Uzao” pia linatajwa jambo la mbegu (1 Pet. 1:23); hivyo uzao wa kweli utakuwa na tabia ya sifa ya Baba yake.

Uzao wa Nyoka inabidi basi utajwe ule ulio na jamii ya kufanana na Nyoka:-

  • Unaharibu maana ya neno la Mungu

  • Unadanganya

  • Unawaongoza wengine katika kutenda dhambi.

Tutaona katika somo la 6 kuwa hayupo mtu halisi anayefanya hivi, bali ndani yetu

sisi upo.

  • “utu wetu wa kale “ wa mwili (Rum.6:6)

  • “Mwanadamu wa tabia ya asili” (1 Kor.2:14)

  • “Utu wa zamani, unaoharibika (Unaooza) kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya” (Efe. 4:22).

  • “Utu wa kale pamoja na matendo yake” (Kol.3:9).

Huu utu wa dhambi ulio ndani yetu ni “Ibilisi” wa kwenye Biblia, uzao wa nyoka.

Uzao wa mwanamke ulikuwa uwe ni mmoja dhahiri - “utamponda (uzao wa nyoka) kisigino” (Mwa.3:15) huyu mtu alikuwa daima akiuponda uzao wa nyoka, yaani dhambi -“Utakuponda kichwa”. Kumpiga nyoka kwenye kichwa ni pigo la mauti kwa kuwa ubongo wake umo kichwani mwakeMtu pekee anayefaa heshima ya kuwa uzao wa mwanamke inampasa awe ni Bwana Yesu:

“Yesu Kristo, ambaye (kwa msalaba) ameondoa mauti (na hivyo ni nguvu ya dhambi - Rum.6:23) na kuufunua uzima na kutoharibika kwa ile Injili” (2 Tim. 1:10).

“Mungu kwa kumtuma mwanae mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili” yaani Ibilisi wa Biblia, Uzao wa nyoka (Rum. 8:3)

Yesu “alidhihirishwa ili aziondoe dhambi zetu” (1Yoh. 3:5).

“Nawe utamwita jina lake Yesu (maana yake 'Mwokozi’): maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao” (Math.1:21).

Yesu mwenyewe “alizaliwa na mwanamke” (Gal. 4:4) akiwa ni mwana wa Mariamu, Ingawa Mungu alikuwa ni Baba yake. Hivi kwa maana hii, pia, alikuwa ni uzao wa mwanamke, ingawa alitolewa na Mungu kwa namna ambayo hakuna mtu amewahi kutokea wa jinsi hiyo. huu uzao wa mwanamke uliumizwa kidogo na dhambi, uzao wa nyoka - “Utakuponda kisigino” (Mwa. 3:25). Nyoka akiuma kisigino kwa kawaida ni kuumia kwa muda, kukilinganishwa na siku zote kumponda nyoka kichwani. Mifano mingi ya misemo ina asili ya Biblia: “Mponde Kichwani” (Yaani kukikomesha kitu kabisa) labda msingi wake ni kwenye unabii huu wa Yesu akimponda Yesu kwenye Kichwa.

Kuihukumu dhambi, uzao wa nyoka, kwanza ilikuwa kwa dhabihu ya Kristo msalabani - fahamu jinsi mistari ilivyonukuliwa inavyousema ushahidi wa Kristo juu ya dhambi kwa wakati uliopita. maumivu ya muda kwenye kisigino aliyoyapata yesu, basi, kinatajwa kifo chake kwa siku tatu. Ufufuo wake ulithibitisha kuwa maumivu yalikuwa ni ya muda tu, ukilinganisha na pigo la mauti aliloipa dhambi. inavutia ya kwamba hakuna taarifa ya historia ya Biblia inayoonyesha ya kwamba watu wa kusulubiwa walipigiliwa misumari visigino vyao kwenye gogo la mti. Hivyo Yesu “alichubuliwa kisigino” kwa kifo chake. Isaya 53: 4 -5 yaeleza kristo “alichubuliwa” na Mungu kwa kifo chake msalabani. Hii ni wazi inataja unabii wa Mwa.3:15 kuwa Kristo alipondwa na uzao wa nyoka. Walakini mwishowe Mungu alitenda haki kwa mabaya aliyokabiliwa nayo Kristo, amesema hapa kuwa anamchubua (Isaya 53:10) kwa ajili ya kutawala nguvu ya mabaya yaliyomchubua mwanae. Hivyo pia Mungu anatenda kazi kwa mabaya kila anayoyapata mtoto wake.

PIGANO LA LEO

Lakini swali linaweza kuwa limezuka akilini mwako: “Ikiwa Yesu amebatilisha dhambi na mauti (uzao wa nyoka) ni kwa nini mambo hayo bado yapo leo ?” Jibu ni kwamba msalabani Yesu aliangamiza nguvu ya dhambi ndani ya nafsi yake mwenyewe: Unabii wa Mwa. 3:15 ni wa kwanza kumhusu Yesu kupingana na dhambi. Sasa hii inamaanisha ya kwamba kwa kuwa ametualika kuushiriki ushindi wake, hatimaye, nasi pia, tunaweza kushinda dhambi na mauti.

Wale ambao hawajaalikwa kuushiriki ushindi wake , au wanaokataa anapowapa, bila shaka, bado watapata dhambi na mauti. Ingawa dhambi na mauti vinawapata waamini wa kweli, kwa kuunganika kwao na uzao wa mwanamke kwa njia ya ubatizo katika Kristo (Gal. 3:27 -29) wanaweza kusamehewa dhambi zao na kwa hiyo hatimaye wataokolewa toka kwenye mauti, ambayo ni matokeo ya dhambi. Hivyo kwa kuangalia mbele”alibatilisha mauti” msalabani (2Tim.1:10), ingawa sivyo mpaka kusudi la Mungu kwa dunia liwe limekamilika mwishoni mwa baada ya miaka ya elfu hapo watu watakapo koma kufa - mauti hayatashuhudiwa tena juu ya dunia: “maana sharti amiliki yeye (kwa sehemu ya kwanza ya ufalme wa Mungu) hata awawekee maadui wake wote chini ya miguu yake. Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti” (1 Kor 15:25,26).

Kaama “ukibatizwa katika Kristo” basi ahadi kumhusu Yesu, kama zile za mwanzo 3:15, zinakuwa zetu wenyewe; haziwi tena sehemu za kuvutia tu za Biblia, ni unabii na ahadi zilizofanywa kwetu moja kwa moja ! kama uzao wa mwanamke nasi pia, tutapata ushindi wa dhambi juu yetu kwa muhula mfupi. Bwana asiporudi wakati wetu tukiwa hai, nasi pia tutapondwa kisigino kama Yesu, ni kwamba nasi pia tutakufa. Lakini kama kweli tu uzao wa mwanamke , wakati huo hilo “Jeraha” litakuwa ni la kitambo tu. waliobatizwa vema katika kristo kwa kuzamishwa ndani ya maji, wanaunganika wenyewe na mauti yake na ufufuo - kunakoashiria kwa kutoka katika maji

(Ona Rum. 6:3 -5).

Kama tukiwa ni uzao wa mwanamke , basi maisha yetu yatarudisha mfano wa maneno ya Mwa 3:15 - daima kutakuwepo na akili ya kupigana (“Uadui”) ndani yetu, kati ya haki na uovu. Paulo mtume kubwa ameeleza karibu ugonvi wa akilini katika kupingana kati ya dhambi na moyo wake halisi ambao ulichafuka ndani yake (Rum. 7:14 -25).

Baada ya kubatizwa katika Kristo, pigano hili na dhambi ambalo ni tabia ya kawaida ndani yetu litaongezeka na kuendelea kufanya hivyo siku zetu zote. Kwa akili ni vigumu kwa sababu nguvu ya dhambi ni kubwa. lakini kwa maana nyingine sivyo, kwa kuwa tumo ndani ya Kristo, ambaye tayari amepigana na kulishinda pigano. Fahamu jinsi waaminio walivyosemwa wao ni mwanamke katika Waefeso 5:23 -32, kana kwamba kwa kuwa uzao wa mwanamke vile vile tu mwanamke.

Kwa jinsi hiyo hiyo kama uzao wa mwanamke unamaanisha wawili Yesu na hao wanaojaribiwa kuwa na tabia ya kuwa na sifa yake, basi uzao wa nyoka unasemwa sehemu mbili dhambi (“Ibilisi”wa kwenye Biblia) na hao ambao kwa hiari wanaonyesha tabia ya dhambi na nyoka.Watu hawa hawatojari au hawatatoa maana nzuri ya neno la Mungu , ambalo mwishowe litawapeleka katika aibu ya dhambi na kutengwa na Mungu, Jambo lililotokea kwa Adamu na Hawa. Kwa kuwa Wayahudi walikuwa watu hasa walomuua Yesu -Yaani waliuponda uzao wa mwanamke kwenye kisigino - itegemewe ya kuwa walikuwa ni mifano mkubwa wa uzao wa nyoka. Hii imethibitishwa na Yohana mbatizaji na Yesu: -

“Hata alipowaona wengi (Yohana) miongoni mwa mafarisayo na masadukayo (kundi la Wayahudi waliomhukumu Yesu) wakiujia ubatizo wake, aliwaambia enyi uzao wa nyoka ,(Yaani wanaume na wanawake wameumbwa na) Nyoka nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja ?” (Math. 3:7)

“Basi Yesu akijua mawazo yao (Mafarisayo), akawaambia ….. Enyi wazao wa nyoka , mwawezaje kunena mema , mkiwa wabaya ?” (Math.12:25,34).

Ulimwengu - hata ulimwengu wa dini - una tabia hizi hizi za nyoka. waliobatizwa tu katika Kristo hao tu wameunganika na uzao wa mwanamke; wengine wote, wana viwango vinavyopishana, vya mbegu za nyoka. Jinsi Yesu alivyowatendea watu ambao walikuwa mbegu ya nyoka inabidi uwe ni mfano wetu: -

Aliwahubiri kwa roho na upendo na ipasavyo kweli, lakini

Njia zao na fikira havikumvuta, na

Aliwaonyesha tabia ya upendo ulio na Mungu kwa njia aliyoishi.

Lakini kwa yote hayo walimchukia. Bidii yake mwenyewe kuwa mtiifu kwa Mungu kuliwafanya kuwa na wivu. Hata jumla zake (Yoh. 7:5; Marko. 3:21) na marafiki wa karibu (Yoh. 6:66) waliweka vikwazo na wengine wakamwacha na kwenda zao. Paulo alipata jambo hilo hilo alipowalilia waliowahi kusimama pamoja naye katika makubwa na madogo:-

“Je ! nimekuwa adui wenu kwa sababu nawambia yaliyo ya kweli ?” (Gal. 4:14 -16).

Kamwe ukweli sio wa wote; kuujua na kuishi kwa huo kama inavyopaswa siku zote huleta aina nyingine ya matatizo kwetu, hata kusababisha maudhi:-

“kama vile yule aliyezaliwa kwa mwili alivyomuudhi yule aliyezaliwa kwa roho (Kwa elimu ya kweli ya neno la Mungu -1 Petro.1:23), ndivyo ilivyo na sas” (Gal. 4:29).

Ikiwa kwa kweli tumeunganika na kristo yatupasa kuonja mateso yake mengine, hivyo basi tutaweza pia kushiriki katika thawabu yake yenye utukufu. tena Paulo anatuwekea mfano usio na kifani kwa hili:-

“Ni neno la kuaminiwa: kwa maana , kama tukifa pamoja naye, tutaishi pamoja naye pia (kristo); kama tukistahimili, tutamiliki pamoja naye; …..

(2 Tim. 10 -12).

“Ikiwa waliniudhi mimi (Yesu), watawaudhi nanyi pia ……Mambo yote haya watawatendea kwa ajili ya jina langu” (Yoh. 15:20,21)

Yaani, kwa sababu tumebatizwa kwa jina la Yesu (Mdo 2:38;8:16).

Kukubaliwa na mistari kama hii, inajaribu kuleta sababu, “kama huko ndiko kuungana na Yesu, Uzao wa mwanamke, yahusika mambo yote, nisingependa hata kidogo” Lakini bila shaka hatutategemea kuingia jambo lolote ambalo hatuwezi kwa maana ya kushindana nalo. Wakati wa kujitoa nafsi ni dhahiri unatakiwa ili kutuunga wenyewe kabisa na Kristo, Sisi kuungana naye tutasababisha thawabu hii yenye utukufu “Kwani mateso ya sasa hayawezi kulingana na utukufu utakaodhihirika kwetu” Na hata sasa dhabihu yake inawezesha maombi yetu tusaidiwe katika masumbufu ya maisha kuwa hasa yenye nguvu kwa Mungu. Na nyongeza kwa hili yafuatayo ni matumaini yenye utukufu, kwa uzito yameelekezwa katika Biblia nyingi za Kristadelfiani:-

“Mungu ni mwaminifu, ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na hilo jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili” (1Kor. 10:13)

“hata (mambo) nimewaambieni mpatekuwa na amani ndani yengu. Ulimwernguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinnda ulimwengu” (Yoh. 16:33)

“basi, tuseme nini juu ya (mambo) hayo ? Mungu akiwepo upande wetu, ni nani aliye juu yetu ?” (Rum. 8:31).

3.3 Ahadi Kwa Nuhu

Maendeleo ya historia ya mwanadamu yalipokwenda mbele baada ya kipindi cha Adamu na Eva, mwanadamu akaongezeka na kuwa mwovu sana, mambo yalifikia hatua ambayo ustarabu wa uadilifu ukaharibika mno ambapo Mungu akaamua kuuharibu utaratibu wa mambo, Isipokuwa nuhu na familia yake (Mwa. 6:5-8).Akaambiwa atengeneze safina ambayo ndani yake yeye na wanyama wote miongoni mwa waliochaguliwa wataishi kipindi cha wakati hapo ulimwengu utakapokuwa unaangamia kwa gharika. kwa kupita, ipo sababu kubwa ya kisayansi ya kuamini kwamba mafuriko haya makubwa yalitokea kweli, mbali ya taarifa za wazi za maandiko ! Fahamu kuwa dunia (Yaani, hii sayari halisi) haikuharibiwa, wanadamu waovu waliosimamishwa juu yake tu.”Wakafa wote wenye mwili waendao juu ya nchi” (Mwa. 7:21).Yesu (Math. 24:34) na Petro (2Petr.3:6 -12) Wote wawili waliielewa hukumu ya ulimwengu wa Nuhu una mfano mmoja na itakayotokea Kristo atakapokuja mara ya pili. Maovu mengi mno ya mwanadamu katika kipindi cha Nuhu yanalingana na ya ulimwengu wa leo, ambao hu karibu kuadhibiwa Kristo atakaporudi.

Kwa sababu ya udhalimu wa dhambi ya mwanadamu na orodha ya mambo ya kuiharibu sayari hii yenyewe ambayo imeanza, imetokea imani, hata miongoni mwa wakristo, ya kuwa dunia hii itaangamizwa. Wazo hili ni wazi linaonyesha kutokufahamu kabisa ujumbe wa Msingi wa Biblia - wa kwamba Mungu ni mwenye uweza anayejihusisha na mambo ya sayari hii, Na ya kuwa mapema Yesu Kristo atarejea kuusimamisha ufalme wa Mungu hapa duniani.Ikiwa mwanadamu ameruhusiwa kuiharibu sayari hii basi ahadi hizi haziwezi kutungwa barabara. Ushahidi wa maana kuwa ufalme wa Mungu utakuwa duniani unapatikana katika somo la 4 -7 na somo la 5. Wakati ule ule ufuatao utakuwa ni uthibitisho wa kutosha kuwa dunia na utaratibu wa sayari hautaharibiwa: -

  • “Kama dunia aliyoiweka imara milele” (Zab. 78:69);

  • “Nayo dunia hudumu daima”

  • “…….jua na mwezi……nyota…..mbingu amevithibitisha hata milele na milele, ametoa amri wala haitapita” (Zab.148:3 -6).

  • “Dunia itajawa na kumjua BWANA, kama vile maji yanavyoifunika bahari” (Isaya.11:9)

  • (Hesabu 14:21) - Vigumu, ikiwa Mungu ataiacha dunia yenyewe iharibiwe. Ahadi hii bado kutimizwa.

  • “BWANA aliyeziumba mbingu asema hivi; Yeye ni Mungu; ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya; ndiye aliyeifanya imara, hakuiumba ukiwa; aliiumba ili ikaliwe na watu “ (Isaya 45:18). Ikiwa Mungu aliiumba dunia tu aione yaharibiwa, basi kazi yake ilikuwa haifai.

Bali nyuma kabisa katika Mwanzo Mungu aliyahahidi yote haya kwa Nuhu. kama alivyoanza kuishi tena katika ulimwengu ulioumbwa na gharika, labda Nuhu alihofu ya kuwa kutaweza kuwepo maangamizi mengine ya jumla. Popote ilipoanza kunyesha mvua baada ya gharika, Wazo hili lilibidi limjie akilini mwake. Na hivyo Mungu akafanya Agano (mfululizo wa Ahadi) kuwa jambo hili halitatokea kamwe

mara ya pili:-

“Mimi, tazama, nalithibitisha Agano langu nanyi; …… na agano langu nitalithibitisha nanyi, wala kila chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya gharika; …….(Ona mkazo wa “MIMI” - ajabu ya Mungu akichagua kufanya ahadi na mtu mfu !); Mwa.9: 9-12).

Agano hili lilithibitishwa na upinde wa mvua: -

“Hata itakuwa nikitanda mawingu (ya mvua) juu ya nchi, upinde utaonekana winguni: nami nitalikumbuka agano langu …… kati yangu nanyi ….. Agano la milele lililoko kati ya Mungu na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili kilicho katika nchi ……Hii ndiyo ishara (Upinde wa mvua) ya agano” (Mwa 9:13 -17).

Kwa sababu ni Agano la milele kati ya Mungu na watu na wanyama wa dunia, kinachofuata ni kwamba dunia ilipasa watu na wanyama waishi milele humu. Huu wenyewe ni uthibitisho kuwa ufalme wa Mungu utakuwa kwenye dunia hii kuliko kusema mbinguni. Ahadi hii kwa Nuhu ni msingi wa Injili ya ufalme ; inaonyesha jinsi macho ya Mungu yanalenga kwenye dunia hii , na jinsi alivyo na kusudi nayo. hata katika hasira anakumbuka rehema (Heb. 3:2), na huu ndio upendo wake ambao hata viumbe wanyama wake anawajali (1 Kor. 9:9; Yona 4:11).

3.4 Ahadi Kwa Abrahamu

Injili aliyoifundisha Yesu na Mitume kwa msingi haikuwa tofauti na alivyoielewa Abrahamu. Mungu, katika maandiko,”Alimhubiri Abrahamu Injili nzima” (Gal. 3:8) Ahadi hizi ni za maana sana hata Petro alizianza na kumaliza kutangaza hadharani habari njema akiwatajia hizo (mdo. 3:13,25). Kama tunaweza kuelewa alichofunza Abrahamu, ndipo tutakuwa na picha ya msingi kabisa ya Injili ya Kikristo. kuna ishara zingine ambazo zinaonyesha kuwa “Injili” sio jambo fulani ambalo lilianza barabara kwenye kipindi cha Yesu:-

“Tunawahubiri habari njema (Injili) ya ahadi ile waliyopewa mababa, ya kwamba Mungu amewatimizia watoto wetu ahadi hiyo” (Mdo. 13:32,33).

“Injili ya Mungu, ambayo Mungu amekwisha kuiahidi kwa kinywa cha manabii wake (Yaani,Abrahamu,Mwa.20:7) katika Maandiko matakatifu” (Rum. 1:1 -2).

“Maana kwa ajili hiyo hata hao waliokufa walihubiriwa Injili” (1Pet. 4:6) - yaani waamini ambao waliishi na kufa kabla ya karne ya kwanza.

“Maana ni kweli , sisi nasi tumehubiriwa Injili vile vile kama hao” (Ebra 4:2) - Yaani, Israel walipokuwa jangwani

Ahadi zilizofanywa kwa abrahamu zina mambo mawili ya msingi :

  1. Mambo yanayohusu uzao wa Abrahamu (mtoto maalamu) na

  2. Mambo yanayohusu nchi aliyoahidiwa Abrahamu.

Ahadi hizi zimefafanuliwa katika Agano Jipya, na, kuendelea na utaratibu wetu kuifanya Biblia ijieleze yenyewe , tutaunganisha mafunzo ya sehemu mbili za maagano ili tupate picha kamili aya Agano lililofanywa kwa Abrahamu.

Abrahamu awali aliishi Uri, mji wenye ustawi ambao sasa ni Iraki. Watafiti wa mabo ya kale wa siku hizi wanadhihirisha ustaarabu wa hali ya juu ambao ulifikiwa na wakati wa Abrahamu. ulikuwepo utaratibu wa mabenki, utumishi wa Serikali na utaratibu wa kutawala. Akijua hakuna tofauti, Abrahamu aliishia katika mji huu, kama tunavyomjua mtu wa ulimwengu. Lakini ndipo mwaliko wa Mungu ulio wa ajabu ukinijia -ayaache hayo maisha ya walimwengu na kuanza safari kuelekea nchi ya ahadi. Wapi kabisa na kwa ukamilifu haikufanywa dhahiri barabara. Akaambiwa yote, mwishowe ikawa ni safari ya maili 1,500.Nchi ilikuwa ni Kanani -Israeli ya sasa.

Mara kwa mara wakati wa uhai wake, Mungu alimtokea Abrahamu na akarudia na akapanua ahadi zake kwake. Hizi ahadi ndizo msingi wa Injili ya Kristo, basi kama tu wakristo wa kweli mwaliko huo huo unatujia kama ulivyofanywa kwa Abrahamu, ili kuyaacha mambo ya muda mfupi ya maisha haya, na kwenda mbele kwenye maisha ya Imani, Ahadi za Mungu zikichukuliwa kwa kuzithamini, kuishi kwa kufuata neno lake. tunaweza kuwaza vema ni jinsi gani Abrahamu alitafakari juu ya Ahadi alipokuwa anasafiri.”Kwa imani Abrahamu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali atakapopapata kuwa urithi; alitii, akatoka asijue aendako” (Ebra. 11:8).

Tunapoona kwa mara ya kwanza ahadi za Mungu , Nasi vile vile tunaweza kujiona kwamba hatujui hasa ni nchi gani ya ahadi ya ufalme wa Mungu itakavyokuwa. Bali imani yetu katika neno la Mungu iwe hivi ila nasi pia tuwe ni wenye bidii kutii.

Abrahamu hakuwa mtu wa kuzunguka asiyetaka kukosa mahali bila jambo jema moyoni kama kutengemea kubahatisha hizi ahadi. Alitoka kwenye maisha ya ulimwengu ambayo, kwa maneno makubwa yana mambo mengi yaliyo na hali iliyo sawa na yetu wenyewe. Maamuzi yenye sehemu nyingi yanayoumiza aliyakabili yalikuwa na sura moja kwa hayo yaliyotupasa kuyakabiri tunapofikiri ikiwa tukubali na kutenda kazi ahadi za Mungu toka mojawapo ya watu wafanyao mambo mageni, kuangaliwa kwa mzaha katika jicho toka kwa majirani (“amepata dini”) …. Mambo haya yalikwisha julikana kwa Abrahamu. azimio ambalo abrahamu alilihitaji hata kufika katikati nalo lote lilibidi kuwa kubwa mno. Jambo pekee lililotoa azimio hilo pote pote katika miaka ya safari yake ndefu lilikuwa ni neno la ahadi. Ilimbidi kujikumbusha maneno hayo na kila siku akayatafakari hasa yalikuwa na maana gani kwake.

Kwa kuonyesha imani kama hii na kuitenda kazi, tunaweza kuwa na heshima ijayo hiyo kama Abrahamu - kuitwa marafiki wa Mungu (Isaya 41:8), kupata maarifa ya Mungu (Mwa. 18:17) na kuwa na tumaini imara la uzima wa milele katika Ufalme. tena tunasisitiza ya kuwa Injili ya Kikristo msingi wake ni ahadi hizi kwa Abrahamu. Kuuamini kwa kweli ujumbe wa Kikiristo, nasi pia, yatupasa kwa uthabiti kujua ahadi zilizofanywa kwa Abrahamu. Bila hizo imani yetu sio imani. Kwa macho yenye bidii basi tusome na kusoma tena mazungumzo yaliyoandikwa baina ya Mungu na Abrahamu.

NCHI

  1. “Toka wewe katika nchi yako …… uende mpaka nchi ambayo nitakuonyesha” (Mwa. 12:1)

  2. Abrahamu “akaendelea kusafiri ….. mpaka Betheli (ndani katikati ya Israeli).BWANA akamwambia Abrahamu ….. Inua sasa macho yako, ukatazame toka hapo ulipo, upande wa kaskazini na wa kusini na wa mashariki na wa magharibi, maana hii nchi yote uionayo, nitakupa wewe na uzao wako hata milele ….. katembee katika nchi hii katika mapana yake, na marefu yake, maana nitakupa wewe nchi hiyo” (Mwa. 13: 3, 15: 18).

  3. “Siku ile BWANA akafanya agano na Abrahamu, akasema , uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huu mto mkubwa, mto Frati” (Mwa 15:18).

  4. “Nami nitakupa wewe na uzao wako baada yako nchi hii unayoikaa ugeni, nchi yote ya Kaanani, kuwa miliki ya milele” (Mwa 17:8).

  5. “Ahadi ile ya kwamba (Abrahamu) atakuwa mrithi wa ulimwengu” (Rum. 4:13).

Hapa tunaona ufunuo wa kuendelea mbele kwa Abrahamu: -

  1. “Ipo nchi ambayo ningependa hata uende huko”

  2. “Sasa umefika katika eneo. Wewe na watoto wako mtaishi hapa milele” Elewa jinsi ya ahadi hii ya uzima wa milele ilivyoandikwa Pasi na uzuri wa kudanganya au mkazo; mwanadamu angeianzisha hapana shaka ingefanywa kuwa nyepesi.

  3. Eneo la nchi ya ahadi lilifafanuliwa na kuwekwa wazi zaidi:

  4. Abrahamu hakutarajia kupata ahadi katika maisha haya - alikuwa awe ni “mgeni” katika nchi, ingawa baadae ataishi milele humo. kidokezo cha hii ni kuwa atakufa na kisha baadae kufufuliwa na kumwezesha kupata ahadi hii.

  5. Paulo, akiongozwa na Roho kuandika, ni dhahiri aliona Ahadi kwa Abrahamu kuwa na maana ulimwengu wote ni urithi wake.

Maandiko yanaacha nia yake ili kutukumbusha ya kuwa Abrahamu hakupata kuona utimilifu wa ahadi katika zama za uhai wake:-

“Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama nchi isiyo yake (Panadokeza namna ya maisha ya muda) akikaa katika hema” (Ebra. 11:9).

Aliishi kama mgeni katika nchi, labda pamoja na akili hiyo hiyo kutoonwa kwa kukosa usalama wa kutokutembea ambako mkimbizi anaona. alikuwa anaishi kwa shida na uzao wake katika nchi yake mwenyewe. Pamoja na watoto wake Isaka na Yakobo, (ambao ahadi zilirudiwa kwao), “alikufa katika imani” asijapata ahadi , lakini akiisha kuziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni na wasafiri juu ya nchi” (Ebra. 11:13). ona hatua nne: -

  • Akizijua ahadi - kama tunavyofanya katika somo hili

  • Akiisha “Sadikishwa nazo” - kama zilichukua maendeleo ya ushawishi kwa Abrahamu, ni kiasi gani zaidi na sisi ?.

  • Kuzikubali kwa moyo - kwa kubatizwa katika Kristo (Gal. 3:27 -29).

  • Kukiri mbele ya ulimwengu kwa mwendo wetu wa maisha kuwa ulimwengu huu sio nyumbani kwetu hasa, bali tunaishi kwa kutumainia enzi ijayo duniani.

Abrahamu amekuwa shujaa wetu mkuu wa mfano kama tunafahamu mambo haya. mwisho wa kutambuliwa utimilifu wa ahadi ulikuja wakati wa baadae kwa mzee aliyechoka kwa mke aliyekufa; kwa kweli ilimbidi anunue kiwanja cha nchi ya ahadi kwa ajili ya kuzika (Mdo. 7:16). Hakika Mungu “hakumpa urithi ndani yake hata kiasi cha kuweka mguu: Lakini akaahidi kwamba atampa, iwe miliki yake, na ya uzao wake baadae alipokuwa hana mtoto” (mdo. 7:5). uzao wa Abrahamu uliopo sasa unaweza kuona kutopatana wanaponunua au kukodi miliki - duniani ambayo iliahidiwa kwao kuwa yao, urithi wa milele !.

Lakini Mungu anatunza ahadi zake. Itabidi ije siku hapo Abrahamu na wote ambao ahadi zilifanywa kwao watazawadiwa. Waebrania 11: 13, 39,40 neno limekazwa sana: -

“Hawa wote wakafa katika imani, wasijazipokea zile ahadi; Mungu alikuwa ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, ili wao wasikamilishwe pasipo sisi”.

Kwa hiyo Waaminifu wote watapewa thawabu kwenye kilele hicho hicho cha muda, yaani kwenye kiti cha hukumu siku ya mwisho (2 Tim. 4:1,8; math. 25:31 -34; 1 Petro 5:4). Kinachofuata ni yeye kuwako ili kuamuliwa, Abrahamu alikuwa na wengine waliozijua ahadi hizo itabidi wafufuliwe kabla ya hukumu. ikiwa sasa hawajazipokea ahadi ya kwamba watafanyiwa hivyo tu baada ya ufufuo wao na hukumu (yaani kuamuliwa na mwamuzi) Kristo atakaporudi, halipo shauri la pili bali kufahamu kuwa walio sawa na abrahamu kwa imani hivi sasa wamelala wakiwa hawana fahamu, wakisubiri Kristo arudi; Lakini vioo vilivyotiwa picha katika makanisa ya Ulaya yote imejulikana ya kuwa Abrahamu sasa yuko mbinguni, akipata thawabu kwa ajili ya maisha ya imani Maelfu ya watu kwa miaka mamia wameweka picha hizo za zamani, kwa dini wakikubali mawazo kama haya. Je ? utakuwa na ujasiri wenye misingi katika Biblia kuondika haraka nje ya hiyo jamii ?

Uzao (Mbegu)

Kama tulivyoelezwa katika somo la 3:2, ahadi ya uzao kwanza wamhusu Yesu na, Pili, kwa wale walio katika “Kristo” na kwa sababu hiyo nao vile vile wanahesabiwa kuwa ni uzao wa Abrahamu:-

  1. “Nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki ….. na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa” (Mwa. 12:23)

  2. “Na uzao wako nitaufanya uwe kama mavumbi ya nchi: hata mtu akiweza kuyahesabu mavumbi ya nchi, Uzao wako nao utahesabika ….. Maana nchi hii yote uionayo, nitakupa wewe na uzao wako hata milele” (Mwa. 13:15,16).

  3. “Tazama sasa mbinguni , hesabu nyota, kama ukiweza kuzihesabu …… Ndivyo utakavyokuwa uzao wako ….. Uzao wako nimewapa nchi hii (Mwa. 15:5,8)

  4. “Nami nitakupa ……. na uzao wako baada yako …… nchi ya Kanaani, kuwa miliki ya milele; nami nitakuwa Mungu wao” (Mwa. 17:8)

  5. “Na katika kuzidisha nitazidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchnga uliopo pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao; na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia” (Mwa. 22:17,18).

Tena, Abrahamu kufahamu “uzao” kwa kuendelea mbele kulipanuka: -

  1. Kwanza aliambiwa barabara ya kwamba kwa njia nyingine atakuwa na hesabu ya ajabu ya watoto, na kwa njia ya “uzao” wake dunia yote itabarikiwa.

  2. Baadaye aliambiwa ya kwamba atakuwa na uzao ambao utakuja kujumuisha watu wengi. Watu hawa watapata uzima wa milele, pamoja naye, katika nchi ambayo aliwahi kuifika, yaani Kaanani.

  3. Aliambiwa kuwa uzao wake utakuwa mwingi kama nyota za angani. Hii ahadi inaweza kuwa imedokezwa kwamba atakuwa na watoto wengi wa Kiroho (Nyota za mbinguni wengi sawa na wa mwili (kama “mavumbi ya nchi”).

  4. Ahadi zilizotangulia zilitia mkazo wa nyongeza ya uhakika kuwa watu wengi watakao kuja kuwa sehemu ya uzao watakuwa na uhusiano wao na Mungu.

  5. Uzao utakuwa na ushindi juu ya adui yake.

Fahamu kuwa uzao utaleta “Baraka” zipatikane kwa watu walio juu ya uso wa dunia yote.Katika Biblia jambo la baraka mara nyingi limeungwa na kusamehewa dhambi. Isitoshe, huu ni mbaraka mkubwa zaidi wa kupenda Mungu unaoweza kuhitajika. Kwa hiyo tunasoma mabo kama “Heri (amebarikiwa) aliyesamehewa dhambi” (Zab. 32:1); “Kikombe kile cha baraka” (1Kor. 10:16), kinasema kikombe cha divai ambacho kinawakilisha damu ya Kristo kwa hicho msamaha unawezekana.

Mtoto pekee wa Abrahamu aliyeleta msamaha wa dhambi za ulimwengu, kwa kweli ni yesu, na ufafanuzi wa Agano Jipya juu ya Ahadi zilizofanywa kwa Abrahamu unatoa msaada madhubuti : -

“(Mungu) hasemi, kwa wazao, kana kwamba ni wengi, (yaani kwa wingi), bali kana kwamba ni mmoja, (katika mmoja), kwa mzao wako” yaani, Kristo (Gal. 3:16)

“….ambayo Mungu aliagana na baba zetu, akimwambia Abrahamu katika uzao kabila zote za ulimwengu zitabarikiwa. Mungu akiisha kumfufua mtumishi wake Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, ili kuwabariki kwa kuwaepusha kila mmoja wenu na maovu yake” (Mdo. 3:25.26).

Ona hapa jinsi Petro anavyonukuu na kuifasiri Mwa. 22:18: -

Uzao = Yesu

Baraka = Msamaha wa dhambi.

Ahadi ya kuwa Yesu, uzao, atakuwa mshindi juu ya ahadi zake sasa inafaa zaidi kwa uzuri kuwa mahali ikiwa hii inasomwa kwa kutaja ushindi wake juu ya dhambi - Adui mkubwa zaidi wa watu wa Mungu, na kwa sababu hiyo naye Yesu, Pia.

KUJIUNGA NA UZAO

Kwa sasa itakuwa dhahiri kuwa mambo ya awali yaliyo ya msingi wa Injili ya Kristo ilieleweka kwa Abrahamu. lakini ahadi hizi muhimu zilikuwa kwa ajili ya Abrahamu na uzao wake, Yesu. Ni vipi ? kuhusu mtu yeyote mwingine ?. Hata walio wa ukoo wa mwili wa Abrahamu wao wenyewe kuwa hivyo hakuta mfanya mtu yeyote kuushiriki huo uzao mmoja maalum (Yoh. 8:39;Rum. 9:7). kwa njia nyingine yatupasa tuwe moyoni wa shirika wa Yesu, hivyo basi ahadi za mzao zitashirikishwa nasi vile vile. Hii ni kwa njia ya ubatizo katika Kristo (Rum. 6:3 -5); mara nyingi tunasoma ubatizo katika jina lake (Mdo. 2:38; 8:16; 10:48; 19:5). Wagalatia 3:27 -29 isingeweza kuweka maana yoyote iliyowazi:-

“Maana ninyi nyote (yaani mlio wengi tu) mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo. hapana Myahudi wala Myunani (wa mataifa), hapana mtumwa wala huru, hapana mume wala mke; maana ninyi nyote mmekuwa mmoja (kwa kuwa) katika Kristo Yesu kwa ubatizo. na kama ninyi ni wa Kristo (kwa nia ya ubatizo katika jina lake), basi, mmekuwa uzao wa Abrahamu, na warithi sawa sawa na Ahadi”.

Ahadi ya uzima wa milele duniani, kwa kupokea 'baraka’ ya msamaha kwa njia ya Yesu. Ni kwa kubatizwa katika Kristo, uzao, ambaye tunashirikishwa ahadi zilizofanywa kwake ; na hivyo Rum 8:17 inatuita sisi “Warithio pamoja na Kristo”.

Kumbuka kuwa baraka ilikuwa inakuja juu ya watu wote toka pande zote za dunia , kupitia kwenye uzao; na uzao utakuja kuwa ni kundi la watu walioenea duniani pote, kama mchanga ulio kwenye ukingo wa bahari na nyota za mbinguni. kinachofuata ni kwamba hiki kinatokana na kupokea kwao kwanza baraka hivyo wanaweza kuwa uzao. Kwa hiyo uzao mbegu (moja) “Zitasimulia habari za Bwana kwa kizazi kitakachokuja” (yaani watu wengi ; Zaburi 22:30). Tunaweza kueleza kwa ufupi kuachwa ahadi mbili zilizotolewa kwa Abrahamu : -

  1. NCHI

Abrahamu na uzao wake, Yesu, na wale walio ndani yake watairithi nchi ya Kaanani na kupanuka dunia yote, na kuishi humo milele. katika maisha haya hii ahadi hawakuipata, bali watapokea siku ya mwisho, Yesu atakaporudi.

2) UZAO

Kwanza kabisa huyu alikuwa ni Yesu. kwa njia yake dhambi (“Maadui”) za watu ushindi utapatikana, hivyo basi mibaraka ya msamaha itafanywa ipatikane ulimwenguni pote.

Kwa kubatizwa katika jina la Yesu tunakuwa sehemu ya uzao .

Izi hizi njia mbili zinatokea katika mahubiri ya Agano Jipya, na sio ya kushangaza ni mara nyingi yameandikwa ya kwamba watu waliposikia wakiishafundishwa, wakati huo wakabatizwa. huu ulikuwa, na ndivyo ulivyo, mwendo ambao hizi ahadi zinaweza kufanywa kwetu. Tunaweza kuelewa ni kwa sababu gani, Mzee alipokabili kifo, Paulo aliweza kuainisha tumaini lake kuwa ni “tumaini la Israeli’ (mdo. 28:20): tumaini la kweli la mkristo ni tumaini la kwanza la Myahudi. Ufafanuzi wa Kristo ni kuwa “Wokovu watoka kwa wayahudi” (Yoh. 4:22) pia inabidi kutaja haja ya kuwa Myahudi wa Kiroho, hivyo basi tunaweza kufaidika kutoka kwenye ahadi za wokovu kwa njia ya Kristo ambazo ziliahidiwa kwa mababa wa Wayahudi.

Tunasoma ya kwamba Wakristo wa kwanza Walihubiri :-

  1. “Mambo yanayohusu ufalme wa Mungu na

  2. Jina la Yesu Kristo” (Mdo.8:12).

Haya yalikuwa ndiyo mambo mawili hasa aliyoelezwa Abrahamu mwanzoni mwa vichwa vidogo tofauti vya habari:-

  1. Ahadi zinazohusu nchi na

  2. Ahadi kuhusu uzao.

Angalia unapopita neno “Mambo” (yapo katika uwingi) yanayohusu Ufalme wa Yesu. yameelezewa kwa kifupi kuwa “akawahubiri Kristo” (Mdo. 8:5,12). yote hii mara nyingi imechukuliwa kuwa na maana “Yesu anakupenda ! sema bara bara unaamini alikufa kwa ajili yako nawe ni mtu uliyeokolewa !” Lakini fungu la maneno machache “Kristo” ni dhahiri linaelezea kwa ufupi mafunzo ya hesabu ya mambo kumhusu yeye na ufalme ujao. Habari njema kuhusu ufalme huu ambazo zilihubiriwa kwa Abrahamu zilihusika sehemu kubwa katika mahubiri ya kwanza ya Injili .

Katika mji wa Korintho, Paulo, “Kwa muda wa miezi mitatu, akihojiana na watu na kuwavuta katika mambo ya ufalme wa Mungu” (Mdo. 19:8); Katika efeso alikwenda huko na huko “Akihubiri ufalme wa Mungu” (Mdo. 20:25), na kazi yake kabla ya kufa kule Rumi ilikuwa ni ile ile “Akawaeleza kwa taratibu na kuushuhudia ufalme wa Mungu, akiwaonya mambo yake Yesu, kwa maneno ya sheria ya Musa na ya manabii” (mdo. 28: 23, 31). kama kuwepo mazungumuzo mengi mno ya karibu yanayoonyeshwa ya kwamba ujumbe wa msingi wa Injili kuhusu ufalme wa Yesu hayakuwa tu ni mambo ya kusema “Mwamini Yesu” ufunuo wa Mungu kwa Abrahamu ulieleza jambo moja moja zaidi kuliko hivyo, na mambo yaliyoahidiwa ndio msingi wa Injili ya mkristo wa kweli.

Tumeonyesha ya kuwa kubatizwa katika Jina la Yesu kunatufanya kuwa sehemu ya uzao na kwa sababu hii tunaweza kurithi ahadi (Gala. 3:27 -29), lakini ubatizo pekee hautoshi kutuwezesha kupata wokovu ulioahidiwa. yatupasa kubakia ndani ya uzao , katika Kristo, ikiwa tunataka kupokea ahadi zilizofanywa kwa uzao. Kwa hiyo ubatizo ni mwanzo unaostahili; tumeingia kwenye mbio ambazo zinahitajika wakati huo kukimbia. usisahau kwamba kuhusiana na uzao wa Abrahamu hauna maana kwamba tunakubalika mbele za Mungu. Waisraeli ni uzao wa Abrahamu kwa namna nyingine, Lakini hii haina maana kwamba wanaweza kuokolewa bila kubatizwa na kufuatisha maisha yao kwa Kristo na mfano wa Abrahamu; (Rum. 9: 7, 8; 4: 13,14). Yesu aliwaambia Wayahudi, “najua ya kuwa ninyi ni uzao wa Abrahamu ; Lakini mnatafuta kuniua ….. kama mngekuwa watoto wa Abrahamu, mngezitenda kazi zake Abrahamu” (Yohana. 8:37,39), ambaye aliishi maisha ya kumwamini Mungu na Kristo, Uzao ulioahidiwa (Yoh. 6:29).

“Uzao” inabidi uwe na sifa za babu yake ikiwa tunataka kuwa uzao wa Abrahamu wa kweli basi yatupasa sio tubatizwe tu bali tuwe na imani hasa katika ahadi za Mungu, kama aliyokuwa nayo barabara kwa hiyo ameitwa “baba yao wote wanaoamini ….. ambao wanafuata vile vile nyanyo za imani hiyo ya baba yetu Abrahamu, aliyokuwa nayo” (Rum. 4:11,12) “ Fahamuni basi, wale walio wa imani, hao ndio wana wa Abrahamu” (Gal 3:7).

Imani ya kweli inabidi ijionyeshe yenyewe kwa aina nyingine ya matendo kama sivyo, mbele za Mungu, sio Imani (Yakobo.2:17). Tumeonyesha wazi imani yetu katika ahadi hizi ya kuwa tumejifunza na kubatizwa kwanza, hivyo zinatuhusu sisi wenyewe (Gal 3:27 -29).Basi, unaziamini kweli ahadi za Mungu ?. Hili ni swali yatupasa hasa tujiulize katika maisha yetu yote.

AGANO LA KALE NA JIPYA

Itakuwa ni dhahiri kwa sasa kuwa ahadi kwa Abrahamu zinaeleza kwa ufupi Injili ya Kristo. Mkondo mwingine wa mkuu wa ahadi alizoahidi Mungu ulikuwa kwa Wayahudi katika maneno ya sheria ya Musa hizi alisema kuwa kama walikuwa watii kwenye sheria hii, basi wangebarikiwa katika maisha haya (Kum. 28). Haikuwepo moja kwa moja ahadi ya uzima wa milele katika huu mfululizo wa ahadi, au “agano”. Hivyo tunaona kuwa kumekuwepo “Maagano” mawili yaliyofanywa:-

  1. Kwa Abrahamu na uzao wake , umeahidiwa msamaha na uzima wa milele katika ufalme wa Mungu Kristo ajapo. Ahadi hii pia iliahidiwa katika Edeni na kwa Daudi.

  2. Kwa Wayahudi kwenye kipindi cha Musa, wao waliahidiwa amani na furaha katika maisha haya ya sasa kama wangetii sheria ambazo Mungu alimpa Musa.

Mungu alimwahidi Abrahamu msamaha na uzima wa milele katika ufalme, lakini huu utawezekana tu kwa dhabihu ya Yesu. Kwa sababu hii tunsoma kuwa kifo cha Kristo msalabani kilithibitisha alichoahidiwa Abrahamu (Gal. 3:17; Rum 15:8; Dan. 9:27; 2Kor.1:20), hivyo damu yake imeitwa “Damu ya Agano Jipya” (Math. 26:28) Tulikumbuke hili kama Yesu alivyotuambia mara kwa mara tutwae kikombe cha divai, akiashiria mambo yake kutukumbusha mambo haya (Ona 1Kor. 11:25): “Kikombe hiki ni patano (Agano) Jipya katika damu yangu” (Luka. 22:20). Hakuna maana katika “kuumega mkate” kumkumbuka Yesu na kazi yake ila tukifahamu mambo haya.

Dhabihu ya Yesu imefanya msamaha wa dhambi na uzima wa milele katika Ufalme wa Mungu uwezekane. basi akafanya ahadi imara kwa Abrahamu; Yesu amekuwa mdhamini wa Agano lililo bora zaidi (Ebra. 7:22). Waebrania 10:9 yamsema Yesu “Aondoa la kwanza (Agano), ili kusudi alisimamishe la pili” hii inaonyesha ya kwamba Yesu alipothibitisha ahadi zilizofanywa kwa Abrahamu, aliliondoa Agano lingine, hilo lilikuwa ni agano lililotolewa kwa mkono wa Musa. mistari ambayo imenukuliwa kumhusu Yesu inaimarisha Agano Jipya kwa kufa kwake, inadokeza ya kuwa lilikuwepo agano la kale aliloondoa (Webra. 8:13).

Hii ina maana ya kwamba ingawa agano la kuhusu Kristo lilifanywa kwanza, halikuanza kutumika kamili mpaka alipokufa, kwa sababu hii limeitwa Agano “Jipya”. Lengo la Agano la “Kale” lililofanyika na Musa lilikuwa likionyesha mbele kwenye kazi ya Yesu , na kuupa mkazo umuhimu wa kuamini ahadi kuhusu Kristo

(Gal. 3:19,21). Kwa kinyume, kumwamini Kristo kunathibitisha ukweli wa sheria aliyopewa Musa (Rum.3:31). Ya kupendeza kwa kuwa ya zamani, Paulo anaielezea kwa maneno machache: “Torati imekuwa (Mwalimu) kiongozi kutuleta kwa Kristo, ili tuhesabiwe haki kwa imani” (Gal. 3:24). Ni kusudi hili hata torati iliyokuja kwa mkono wa Musa imehifadhiwa, na bado inatusaidia kujifundisha.

Kwanza unaposema mambo haya sio mepesi kuyaelewa; tunaweza kueleza kwa maneno machache kama ifuatavyo: -

Ahadi za kumhusu kristo zilifanywa kwa Abrahamu - Agano Jipya.

Ahadi kwa Israeli zilijumuisha torati aliyopewa Musa - Agano la Kale.

Kifo cha Kristo. Agano la Kale likaisha (Kol. 2:14 -17) Agano Jipya likaanza kutumika.

Ni kwa sababu hii mambo kama kutoa fungu la kumi,kutonza sabato n.k, ambayo yalikuwa ya Agano la Kale , siyo ya lazima siku hizi - ona somo la 9.5. Agano Jipya litakujafanywa kwa Waisraeli wa kuzaliwa watakapotubu na kumkubali Kristo. (Yer. 31:31,32 ; Rum. 9:26,27; Ezek. 16:62; 37:26), Ingawa, kwa kweli Myahudi yeyote afanyaye hivyo na kubatizwa katika jina la Yesu, anaweza kwa mara moja kuingia kwa Agano Jipya (ambalo halimtofautishi Myahudi /mtu wa mataifa -Gal 3: 27 -29).

Hakika kufahamu mambo haya kunatufanya tutambue ukweli wa ahadi za Mungu. Wenye mashaka juu ya mafundisho ya dini walilaumu isivyo haki wahubiri wa Kristo wa kwanza kwa kutotoa ujumbe wa kweli. Paulo alijibu kwa kusema kwamba kufa kwake Kristo ni uthibitisho wa ahadi za Mungu, tumaini walilosema halikuwa jambo la kugusa na kisha kwenda, bali lilikuwa ni toleo la uhakika kabisa: - “Lakini kama Mungu alivyomwaminifu, neno letu (la kuhubiri) kwenu halikuwa ndiyo na siyo. Maana mwana wa Mungu, Kristo Yesu, aliyehubiriwa katikati yenu na sisi, ….. hakuwa ndiyo na siyo, bali katika yeye ni ndiyo. Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni ndiyo, tena katika yeye ni, Amini” (2 Kor.1:17 -20). Kwa kweli huu mwenendo haufanyi kazi wa,'Vyema’, nadhani kunaweza kuwa na ukweli fulani katika hayo yote …….” ?.

3.5 Ahadi Kwa Daudi

Daudi, kama Abrahamu na wengine wengi wapokeaji wa ahadi za Mungu, hawakuwa na maisha rahisi. Alikuwa ni kijana mdogo wa mwisho katika jamaa kubwa ambaye, katika Israeli 1000 K.K., ilimaanisha kuchunga kondoo na kukimbia safari fupi za kupeleka ujumbe au kitu kwa ndugu zake wakubwa wapendao kidogo kuwa na mamlaka (1 Samweli sura ya 15 hadi 17). Katika kipindi hiki alijifunza kufika kumwamini Mungu ambaye watu wachache tangu wakati ule walimkaribia.

Siku ikafika hapo Israeli walipokabiliwa na shindano la mwisho toka kwa majirani zao wenye kuanzisha ugonvi , Wafilisti; walitakiwa wapeleke mmoja k ati yao apigane na jitu kubwa - Goliati ; Mfilisti aliyekuwa wa kwanza kujitokeza akifahamu kuwa yeyote atakayeshinda atamiliki juu ya upande unopoteza pigano. Kwa msaada wa Mungu Daudi akamshinda Goliati kwa kutumia kombeo, lililompatia umaarufu mkubwa kuliko mfalme wao (Sauli). “Wivu ni mkali kama ahera (Kaburi)” (Wimbo ulio bora 8:6). maneno yaliyothibitisha kuwa kweli kwa mateso aliyopata Daudi toka kwa Sauli kwa miaka 20 iliyofuata akimwinda kama panya huko na huko jangwani kusini mwa Israeli.

Hatimae Daudi akawa mfalme, na kuonyesha shukrani zake kwa upendo wa Mungu wake katika maisha yake nyikani, akaazimia kujenga hekalu la Mungu. Jibu toka kwa Mungu likawa mwanae Daudi, Suleimani akawa ndiye atakayejenga hekalu na ya kuwa Mungu alitaka kumjengea nyumba Daudi (2 Sam. 7:4 -13). Ndipo yakafuata maelezo ya ahadi yanayorudia na mambo mengi aliyoambiwa Abrahamu, ambapo pia yalijaa katika maelezo mengine:-

“Nawe siku zako zitakapotimia, ukalala na baba zako, nitainua mzao nyuma yako, atakayetoka viunoni mwako, naye atakuwa mwanangu. Akitenda

maovu, nitamwadhibu kwa fimbo ya binadamu na kwa mapigo ya mwanadamu, lakini fadhili zangu hazitamwondoka, kama vile nilivyomwaondolea Sauli, niliyemwandoa mbele yako. Na nyumba yako, na ufalme wako,vitadhibitishwa milele mbele yako: nacho kiti chako kitafanywa imara milele” (mstari wa 12 -16).

Toka masomo yetu yaliyotangulia tulitazama “Mzao” kuwa ni Yesu. Maelezo yake kuwa ni mwana wa Mungu (2 Samweli 7:4) yanathibitisha hivi, kama yafanyavyo mengine yanayomtaja katika sehemu zingine za Biblia :-

“Mimi ….. shina la mzao wa Daudi”, Yesu alisema (Uf. 22:16).

“(Yesu), aliyezaliwa katika ukoo wa Daudi kwa jinsi ya mwili” (Rum. 1:3)

“Katika uzao wake mtu huyo (Daudi) Mungu amewaletea Israeli Mwokozi, yaana Yesu, kama alivyoahidi” (Mdo. 13:23).

“Malaika alimwambia Bikra Mariamu kuhusu mwanae Yesu: “Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi Baba yake (babu) yake …… ufalme wake hautakuwa na mwisho”(Luka. 1:32,33) Hii ni ahadi inayotumika kwa mzao wa Daudi, katika 2 Sam.7:13, kwa Yesu.

Pamoja na uthabiti wa mzao amejulikana kuwa ni Yesu, idadi ya maelezo sasa yamekuwa ni yenye

maana : -

1) MZAO.

“Mzao wako …… atakayetoka viunoni mwako …… nitakuwa Baba yake, naye atakuwa mwanangu” “ ……Wazao wa mwili wako nitawaweka katika kiti chako cha enzi” (2 Sam 7:12,14 ; Zab. 132: 10,11). Yesu, mzao, hasa alitoka kwa jinsi ya mwili kwa watoto wa Daudi, bali Mungu akiwa ni Baba yake. Jambo hili linawezekana tu kwa kuzaliwa na Bikira kama alivyoelezwa katika Agano Jipya; Mama yake Yesu alikuwa Mariamu, aliyetoka katika ukoo wa Daudi (Luka.1:32), lakini hakuwa na Baba mwanadamu. Mungu alifanya muujiza katika tumbo la Mariamu kwa njia ya Roho Mtakatifu ili kumzaa Yesu, basi Malaika alitoa ufafanuzi “Kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu’ (Luk. 1:35). “Kuzaliwa na Bikira” ilikuwa ndiyo njia pekee ya Ahadi hii aliyoahidiwa Daudi kuweza kutimia vema.

2) NYUMBA.

“Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa jina langu” (2 Sam. 7:13) inaonyesha kuwa Yesu atajenga Hekalu la Mungu - mwili halisi na la Kiroho. Ezekieli 40 -48 ni sura zinazoeleza jinsi Milenia (Miaka 1000 ya kwanza ya ufalme wa Mungu baada ya Yesu kurudi Duniani) hekalu litajengwa Yerusalemu. 'Nyumba’ ya Mungu ni mahali anapopenda kuishi, na Isaya 66: 1,2 tunaambiwa kuwa alikuja kuishi katika mioyo ya watu walio wanyenyekevu wa neno lake. Basi Yesu anajenga Hekalu la kiroho ili Mungu akae ndani, linaloundwa na waamini wa kweli. Maelezo yanamsema Yesu kuwa jiwe la msingi wa hekalu la Mungu ( 1 Pet. 2:4 -8) na wakristo ni mawe ya hekalu (1 Pet. 2:5) yanayopangwa sasa katika nafasi.

3) KITI CHA ENZI

“Nacho kiti cha enzi cha ufalme wake (Kristo) nitakifanya imara milele ….. nyumba yako (Daudi) na ufalme wako ….. kiti chako kitafanywa imara milele (2 Sam.7: 13,16; Isaya 9: 6,7)”. Basi ufalme wa Kristo utakuwa juu ya ufalme wa Daudi wa Israeli; ina maana kwamba ufalme wa Mungu unaokuja utaanzisha tena ufalme wa Israeli - ona somo la 5.3 zaidi kuhusu huu. kwa kutimiza ahadi hii, Kristo itambidi atawale “kiti cha enzi” cha Paulo, au mahali pa utawala. huu utawala wenyewe ulikuwa Yerusalemu. Huu ni ushahidi mwingine wa kuwa ufalme itabidi uanzishwe hapa duniani ili kutimiza ahadi hizi.

4) UFALME

“Nyumba yako na ufalme wako vitathibitishwa imara milele mbele yako” (2 Sam.7:16 mstari unadokeza ya kuwa Daudi atashuhudia kuanzishwa kwa ufalme wa milele wa Kristo. kwa hiyo ahadi hii haikuwa ya moja kwa moja, hata atakapofufuliwa Kristo atakaporudi ndipo ataweza kuona kwa macho yake mwenyewe ufalme ukisimamishwa ulimwenguni pote, na Yesu akiwa anatawala tokea Yerusalemu.

Mambo haya aliyoahidiwa Daudi ni ya muhimu kabisa kufahamu. kwa furaha Daudi aliyasema mambo haya kuwa ni “Agano la milele …..maana ni wokovu wangu wote, na shauku yangu yote” (2 Sam. 23:5). mambo haya yanataja wokovu wetu pia; Kuyafurahia kuwa shauku yetu yote. Hivyo tena maana imeyafanya haya mafunzo kuwa muhimu. Ni jambo liletalo huzuni kama Wakristo kufunza mafundisho yanayopingana kabisa na ukweli huu wa ajabu :-

  • Ikiwa Yesu mwenyewe “aliwahi kuwepo kabla” yaani alikuwepo kabla ya kuzaliwa, basi hizi ahadi hazina maana hata Yesu awe “Mzao” wa Daudi, au kuwa mtoto.

  • Ikiwa Ufalme utakuwa mbinguni , basi Yesu hawezi tena kuanzisha ufalme wa Daudi wa Israeli, wala kuweza kutawala toka kwenye 'Kiti cha enzi’ cha daudi au mahali pa utawala. Mambo haya hasa yenyewe yalikuwa Duniani, na hivyo tena kuyaanzisha tena inabidi iwe ni mahali pale pale.

YALITIMIA KWA SULEMANI ?

Mwana halisi wa Daudi, Suleimani, alitimiza sehemu ya ahadi alizoahidiwa Daudi. Akajenga hekalu halisi la Mungu (1 Fal. 5 -8), akawa na ufalme uliostawi sana. Mataifa toka pande zote yalituma wawakilishi wa kutoa heshima kwa Sulemani (1 Fal. 10), na kukawa na baraka kubwa za kiroho kutokana na kutumia hekalu. kwa hiyo utawala wa Sulemani ulilenga kwa kuonyesha mbele kwenye utimilifu mkubwa zaidi wa ahadi alizoahidiwa Daudi utakaoonekana katika ufalme wa Kristo.

Wengine wamedai kwamba ahadi kwa Daudi zilitimia kabisa kwa Sulemani, lakini hii inakanushwa na yafuatayo: -

  • Ushahidi mwingi wa Agano Jipya unaonyesha kuwa 'Mzao’ ni Kristo, siyo Sulemani.

  • Daudi anaonekana akiunga ahadi alizo ahidiwa na zile zilizofanywa kwa Abrahamu. (1 Nyakati.17:27 Mwa. 22:17,18:).

  • Ufalme wa'Mzao’ hautakuwa na mwisho - wa Sulemani ulikuwa na mwisho.

  • Daudi alitambua kuwa ahadi zilikuwa zinahusu uzima wa milele, ambapo zinapinga kabisa kutaja yeyote wa jamaa yake ya karibu: “sivyo ilivyo nyumba yangu mbele za BWANA; lakini amefanya nami Agano la milele” (2 Sam. 23:5).

  • Mzao wa Daudi ni masihi, Mwokozi wa watu toka dhambi (Isaya 9:6,7; 22:22; Yer. 33:5,6,15; Yoh. 7:42). bali Sulemani alimwacha Mungu baadaye (1 Fal. 11: 1 -3' Neh. 13:26) kwa sababu ya kuoana na walio nje ya tumaini la Israeli.

Tumeacha kitambo sehemu ya 9: Kuharibiwa kwa Mbingu na Nchi (Ufu. 21:1; 2Pet. 3: 6 -12).

Lengo la Mungu likiwa ni kusimamisha ufalme wake hapa duniani (Ona somo la 5), haidhaniwi kuwa ataiharibu hii sayari yenyewe, na somo la 3.3 limeonyesha ya kuwa kwa uthabiti amehahidi kutofanya jambo hili. Mstari uliopo hapo juu kuangamiza mbingu na nchi inabidi uchukuliwe kwa mfano.

Fungu la maneno kutoka Petro laonyesha mfano mmoja kati ya hukumu iliyopita duniani wakati wa Nuhu na itakavyotokea kwenye “Siku ya Bwana” wakati ujao. “Dunia ile ilivyokuwepo wakati ule, iligharikishwa na maji, ikaangamia, Bali mbingu na nchi, zilizopo sasa …… zimewekwa akiba kwa moto zikilindwa hata siku ya hukumu” (2 Pet. 3:6,7).

Petro anaonyesha tofauti kati ya maji yakiwa ni wakala wa kuangamiza kwenye kipindi cha Nuhu, na moto utakaotumika atakapokuja mara ya pili.'Mbingu na nchi’ za kipindi cha Nuhu zenyewe hazikuharibiwa - wenye miili wote’ wenye dhambi waliharibiwa (Mwa. 7:21; 6: 5, 12).'Mbingu na nchi’ kwa sababu hii unatajwa utaratibu wa mambo au muungano wa watu. Wale wasiofahamu hili fungu la maneno wanaelekea kusahau kuharibiwa kwa 'Mbingu’ zinazosemwa karibu. hii haiwezi kuchukuliwa ilivyo - ni mahali ambapo ni makao ya Mungu (Zab. 123: 1), mahali ambapo hakuna wenye dhambi (Hab. 1: 13; Zab. 65: 4, 5), ni ambazo hutangaza utukufu wa Mungu (Zab. 19:1).Kama zinataja jambo lingine katika mfano, basi inabidi nayo 'nchi’.

Mafungu yafuatayo ya maneno yanaonyesha jinsi'Mbingu na nchi’ katika sehemu zingine za Biblia hazitafsiriwi jinsi zilivyo, bali zinataja kidogo mfumo wa mambo ya dunia.

  • “Naliangalia nchi, na tazama ilikuwa ukiwa, haina watu; naliziangalia mbingu, nazo hazina nuru ….. maana BWANA asema hivi, Nchi yote (ya Israeli) itakuwa ukiwa …… Kwa ajili ya hayo nchi itaomboleza na mbingu zitakuwa nyeusi” (Yer. 4:23 -28). Hizi ni hukumu kuja juu ya 'Mbingu na nchi’ za watu wa Israeli ambazo (si mbingu na dunia halisi) zitaomboleza.

  • Hapo kwanza Musa aliwatangazia Waisraeli wote “Sikilizeni, enyi mbingu, nami nitanena; na nchi isikie maneno ya kinywa changu” (Kum. 32:1). mkazo umetiwa wa kuwa palikuwepo aina mbili za watu ambao alizungumza nao:

  1. “Wazee wote wa kabila zenu”na

  2. “Kusanyiko lote la wana wa Israelli” (Kum. 31: 28,30).Wakati ule wazee walilinganishwa na 'Mbingu’ na watu wa kawaida na 'Nchi’.

  • Isaya alianza unabii wake kwa jinsi hii: “Sikieni, enyi mbingu, tega sikio Ee nchi ……. Lisikieni neno la BWANA, enyi waamuzi ……tegeni masikio msikie sheria ya Mungu wetu” (Isa. 1: 2,10). Tena ipo mistari sambamba kati ya mbingu na viongozi; na kati ya nchi na watu.

  • Ataziita mbingu zilizo juu, na nchi pia awahukumu watu wake” Israeli (Zab. 50:4) huu wajisema wenyewe.

  • “Nami nitatikisa mataifa yote … nitazitikisa mbingu na dunia” (Hagai 2:7,21) vile vile.

  • “Maana upanga wangu umekunywa na kushiba mbinguni: tazama utashukia Edomu, … upanga wa BWANA umeshiba damu … maana BWANA …. machinjo makubwa katika nchi ya Edomu” (Isa. 34:5,6) hapa'Mbingu' zimelinganishwa na Edomu; Unabii uliotangulia kama jeshi lote la mbingu litafumliwa’ (Isa. 34:4) kwa hiyo inatajwa Edomu kufumuliwa.

  • Mbingu na nchi zilizotajwa zikifumuliwa au kunyauka katika Isaya 13 wanatajwa watu wa Babeli. katika mfululizo wa taarifa kuhusu Babeli tunasoma ya kuwa Mungu'atazitetemesha mbingu, na dunia itatikiswa itoke katika mahali pake ….. itakuwa kama vile paa aliyetikiswa ….. kila mtu atageukia watu wake, nao watakimbia, kila mtu aende nchi yake mwenyewe” (Isa. 13:13,14). Kuondoka kwa mbingu na nchi kumewekwa sawa na huko kwa watu, Ebra. 9:26 yasema “Mwisho wa dunia” ukiwa unatokea katika karne ya kwanza B.K - katika maana ya kuwa ulimwengu wa Wayahudi ulikuwa unaisha wakati ule.Katika fikira yote haya yakishikwa kwa uthabiti, itegemewe kuwa mistari ya agano Jipya inayotaja mbingu mpya na nchi atakaporudi Kristo itataja utaratibu mpya wa mambo utakaoonekana hapo ufalme wa Mungu ukisimamishwa.

Uchunguzi wa karibu kwa 2 Pet. 3 unathibitisha hivi. tukiisha eleza namna'mbingu na nchi’ za sasa zitakavyoisha, mstari wa 13 unaendelea: “Lakini kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake” Huku ni kunukuu ahadi ya Mungu iliyo katika Isaya 65:17: “Maana tazama, mimi naumba mbingu mpya na nchi mpya”. Mistari inayoendelea katika Isaya 65 yaeleza utaratibu huu mpya kuwa ni hali timilifu hapa duniani:

“Tazama, naumba Yerusalemu iwe shangwe.. Hawatajenga, akakaa mtu mwingine …..mtoto atakufa mwenye umri wa miaka mia (yaani, maisha ya kuishi yatarefushwa) …. Mbwa mwitu na mwanakondoo watalisha pamoja” (Isaya 65: 18 -25).

Baraka zote hizi ni dhahiri zinahusu jambo la ufalme ujao wa Mungu duniani -'Mbingu na nchi mpya zitakazo ingia mahali pa hizi zilizopo zilizosimama kwa huzuni.

Tumeacha kitambo sehemu ya 10: Madai ya'Uisraeli wa Visiwa vya Uingereza’

Wazo limetangulizwa mbele na mtu kama H.W. Armstrong katika 'Ukweli dhahiri’ wa muungano wa ahadi alizoahidiwa Abrahamu zimetimilika kwa Waingereza na watu wa Amerika, ambao, imedaiwa ni wa kabila la Efraimu na Manase. Washirika wa Uisraeli wa Uingereza wanaamini kwamba Wafalme na malkia wa Uingereza wametokea kwa Wayahudi walianza na mfalme Daudi ili kuhakikisha nadharia zao wameweza kusema kwamba Wayahudi wamekataliwa kuwa watu wa Mugnu na watu wa Uingereza wamechaguliwa badala yao.

Ikiwa tafakari ya somo la 3 limefuatwa, itakuwa dhahiri uwa kwa Biblia madai haya hayana ukweli wowote, yafuatayo ni machache kati ya alama nyingi zanyongeza zinazoweza kufanywa: -

  • Watu wote sawa sawa wapo chini ya laana ya dhambi (Rum.3: 23), na kwa hiyo kristo alikufa ili kuwezesha watu watokao mataifa yote wawe na nafsi ya wokovu. malezi ya taifa lolote tutokako siyo ya muhimu kama tumebatizwa katika Kristo na kuwa sehemu ya Israeli kiroho (Gal. 3:27 -29). tumeamriwa kuhubiri Injili kwa mataifa yote. na kubatiza aaminiye (Marko. 16:15,16); hivyo Israeli mpya inakuwa na watu watokao mataifa yote, siyo Uingereza tu.

  • Ni shida kuthibitisha asili ya watu wa Uingereza na Amerika; wao ni watu mchanganyiko toka sehemu nyingi za ulimwengu. kwa sababu tu mtu kazaliwa kwenye nchi hizo hakuna maana ya kuwa wao ni watu walio teuliwa na Mungu.

  • Uisraeli wa Uingereza unadaiwa kwamba baraka alizoahidiwa uzao wa Abrahamu zimetimizwa kwa watu wa Uingereza, bila kujali utii wao kwa Mungu. Hili ni jambo linalopingana na baraka za Mungu ni katika hali ya utii. sura zote za Law. 26 na Kum. 28 zaeleza baraka zitakazokuja juu ya Israeli kama wangetii neno lake, na laana itakayokuja kama hawatii. kudai kuwa Mungu ameipa Uingereza baraka hizi bila kujali utii wao kwa neno lake , na mara nyingi mbele yao huwa wepesi kuliasi, kwa kweli ni kufanya jeuri kwenye maneno ambayo Mungu anatoa baraka hizi.

  • Kidokezo cha kuwa Mungu amewatupilia mbali watu wake wa Israeli na badala yao amewaweka Waingereza kinaruka kwenye uso wa fungu la maneno kama Rum. 11: 1, 2: “Je ! Mungu amewasukumia mbali watu wake ? hasha !. Kwa kuwa mimi (Paulo) ni Mwisraeli, mmoja wa wazo wa Abrahamu, ….. Mungu hakuwa sukumia mbali watu wake aliowajua”.

  • Ufalme wa Mungu ulikuwa ni ufalme wa Israeli zamani (2 Nyak.9:8). ulipinduliwa kwa kutotii, Lakini ufalme utarudishwa tena (Ezek. 21: 25 -27).Ufalme utarudi Yerusalemu (Mika. 4:8) Yesu atakapo tawala juu ya kiti cha Enzi cha Daudi (Luka. 1:32). Watu wa Israeli wa sasa ambao wametawanyika watakusanywa tena toka sehemu mbali mbali za dunia walikotawanyika: “Nitawatwaa wana wa Israeli toka kati ya mataifa walikokwenda na kuwaleta kwenye nchi yao wenyewe. nitawafanya kuwa taifa moja katika nchi yao, juu ya milima ya Israeli” (Ezek. 37: 21,22). Unabii huu umetimia kwa namna Wayahudi asili walivyorudi nchini kwao; utimilifu kamili utakuwa katika ufalme, kurudi kwa Israeli waliopo kwenye nchi yao kunaonyesha itabidi kuja mapema huu ufalme.

Maelezo chini ya ktabu: Wale ambao hasa wamependezwa katika habari hii wanaweza kupata kitabu cha bure, 'Uisraeli wa Uingereza Umepimwa’, kinapatikana kwa wachapishaji.

Somo La 3 : Maswali

 

  1. Ni ipi kati ya ahadi za Mungu inayotabiri kujitahidi daima kushindana kati ya dhambi na haki ?.

  1. Ahadi kwa Nuhu

  2. Ahadi katika Edeni

  3. Ahadi kwa Daudi

  4. Ahadi kwa Abrahamu

 

  1. Zipi kati ya taarifa zifuatazo ni za kweli kuhusu Ahadi katika Edeni ?

  1. Mzao wa nyoka ni lusifa

  2. Kristo na wenye haki ni uzao wa mwanamke

  3. Uzao wa nyoka kwa muda ulipondwa na Kristo

  4. Uzao wa Mwanamke ulichubuliwa kwa kifo cha Kristo

 

  1. Uzao wa Abrahamu utaishi wapi milele ?

  1. Mbinguni

  2. Katika mji wa Yerusalemu

  3. Duniani

  4. Wengine mbinguni wengine duniani

 

  1. Kati ya yafuatayo yapi aliahidiwa Daudi ?

  1. Kwamba mtoto wako mkubwa atatawala milele

  2. Kwamba 'Mzao’ wake utakuwa na ufalme mbinguni

  3. Mzao huyo atakuwa Mwana wa Mungu

  4. Mzao huyo, Yesu, aliishi mbinguni kabla ya kuzaliwa

 

  1. Tunawezaje kuwa uzao wa Abrahamu ?

  2. Je ! dunia itaharibiwa ?

  3. Ahadi za Mungu zinathibitishaje jibu lako kwa swali la 6 ?

8. Eleza Ahadi ya Edeni katika Mwanzo 3:15.

 

Swahili Title
MISINGI YA BIBLIA 03 - AHADI ZA MUNGU
English files
Swahili file
Literature type
Sub type