Juni 10
Katika Waamuzi 7, Gideoni anaonyesha ni kwa kiasi gani anamtumainia Mungu baada ya kupata uzoefu wa ishara za Mungu katika sura ya 6. Mungu alisema kwamba, idadi ya watu wa Gideoni waliokuwa wamekusanyika katika jeshi ilikuwa kubwa sana, Mungu anatoa sababu zake kuhusu jambo hili, mstari wa 2. Ni muhimu kutopokea sifa kwa kitu chochote ambacho tunafikiri kwamba tunakipata, ni Mungu ambaye anafanikisha mambo kwa ajili yetu. Wanaume 22,000 wanaliacha jeshi lake, na Gideoni angali anatumaini! Mungu bado anasema ni wengi sana na jeshi linapungua hadi watu 300. Mungu hahitaji “nguvu” za kibinadamu ili kufikia jambo lolote, anahitaji tuwe na imani kwake. Sisi sote tuna mashaka, Gideoni bado alifanya na Mungu akamsaidia kujinasua katika jambo hili kwa kumwambia aende kwenye kambi ya adui na kuona kile kinachotokea, mstari wa 13-16. Huyu alikuwa ni mtu mwaminifu aliyesadiki nguvu za Mungu na aliwatia moyo wengine waliokuwa karibu naye kwamba, Mungu alikuwa pamoja nao. Ijapokuwa walikuwa wachache tu, Mungu alileta ushindi mkuu wakati ambapo Israeli walikuwa katika mojawapo ya maeneo yao ya chini kabisa. Gideoni hakuwa na kiburi alipopiga kelele katika mstari wa 18, alikuwa akiwakumbusha Wamidiani ndoto zao za usiku, alikuwa akitumia hofu zao walizoziweka hapo na Mungu! Watu wake walitumia kilio kilekile, mistari 19-21. Mungu ndiye aliyewaangamiza adui, mstari wa 22. Gideoni hakupokea sifa kwa mafanikio hayo, Waamuzi 8 mstari wa 22-23, alitoa hoja kwamba mwamuzi wa sasa alikuwa ni Mungu kwani ndiye aliyewatawala. Cha kusikitisha Gideoni anaonekana kuweka mfano mbaya hapa katika kuweka naivera ya dhahabu, mstari wa 27, tunapaswa kuwa waangalifu sana kuhusu hisia tunazotoa kwa wengine, je, itatufanya sisi na wao kujikwaa? Labda nia ilikuwa kwamba efodi hii iwe ukumbusho, lakini cha kusikitisha ilitumiwa vibaya na kuwa mtego - hayo ndiyo mambo ambayo Mungu anatuonya kuyahusu! Inaonekana Gideoni aliwaweka watu wacha Mungu wakati wa maisha yake, lakini cha kusikitisha kwamba hii haikudumu, mstari wa 33.
Kwa hiyo, ni muhimu sana tuwafundishe wengine njia za Mungu ili waweze kuongoza katika njia ya kimungu baada ya sisi kushindwa. Ni muhimu sana kwa sababu tunajua kwamba Mungu hatapendezwa na uasi. Isaya 34 inaweka hili wazi kabisa. Kutakuwa na hukumu juu ya mataifa wasiomcha Mungu, kama ilivyokuwa wakati wa Gideoni, mstari wa 2. Baba wa Edomu alikuwa Esau, alikataa njia za Mungu (Mwanzo 25: 29-34); baadae Edomu taifa hilo halikumheshimu Mungu na watu wake na halikuwaruhusu kupita katika nchi yao wakati Musa alipokuwa akiwaongoza (Hesabu 20:14-21). Siku zote kuna matokeo ya kutomkubali na kumheshimu Mungu, na Mungu ana siku ya kisasi, mstari wa 8. Hili si jambo la kupendeza sana, lakini Mungu atakomesha uasi, na kwa sababu anafanya hivyo, ni jambo la haki kuona kuwa - Mungu daima hakosei, mstari wa 11. Wakati mwingine tunaweza kuwa na papara na tunataka Mungu atende sasa, lakini tuwe na subira ya Yakobo 7, mstari wa 5. Yakobo anatutia moyo tujifunze mifano ya watu wengine wacha Mungu, kama Ayubu na manabii, mstari wa 10-11. Tunaweza kuongezea mfano wa Gideoni pia kwa sababu alionyesha imani kamili katika Mungu ingawa, kama Ayubu, alikuwa akiteseka pia. Tunapaswa kuamini kwamba kila kitu kiko kwa wakati wa Mungu. Kwa sasa, tunapongojea Mungu atende, tunapaswa kujaribu kutenda kama Yesu. Mistari ya 1-6 inapozungumzia kutegemea mali kwa matajiri, inazungumzia kanuni inayofanana na Gideoni na ukubwa wa jeshi lake la awali; sio idadi au mali ambayo itaokoa, ni Mungu. Kwa kweli idadi na mali vinaweza kutuondoa kutoka kwa Mungu, kwa hiyo, inapotokea kuwa jaribu kwetu, Mungu huiondoa. Yakobo ana masomo kwa ajili yetu katika hali mbalimbali, tukijua kwamba tunashindwa, lakini kwamba daima tunapaswa kutiana moyo na kutubu, mistari 19-20. Hivyo, mtumainini Mungu pekee, mbaki wanyenyekevu, vumilieni, mkitiana moyo na daima muwe tayari kuheshimiana na kushiriki, mstari wa 13-16. Maombi ni sehemu muhimu sana ya maisha ya mtu mcha Mungu, Gideoni aliomba, na hapa tuna mfano wa Eliya ambaye "alikuwa mtu kama sisi", mstari wa 17-18, aliomba mvua isinyeshe ili kuonyesha kwamba Mungu alikuwa akitawala. Kwa hiyo, tunapaswa kusali pia ili jina la Mungu litukuzwe.