CSSA 2-4-03 - BELIEF IN THE MESSIAH AT SAMARIA

English

203. Imani kwa Masihi huko Samaria

“Tumemsikia sisi wenyewe, na kujua kuw ahuyu ndiye Kristo mwokozi wa dunia”

Kwa muda (kipindi) kifupi baada ya kuonana na Nikodemu Yesu alikuw akihubiri na kubatiza katika Yudea. Yesu alifahamu kwamba Wafarisayo (wachukizao) walikuwa wamesikia juu ya mafanikio yake. Kwa sababu ya upinzani wap kwake aliondoka Yudea na kuelekea kaskazini huko Galilaya. Aidha alikuwa apitie nchi yenye uadui na Samaria, njia (barabra ya moja kw amoja au avuke Yordani na kwend aukingoni mwa mto upande wa mashariki kwa kawaida ikiwa njia salama zaidi lakini isiyoend amoja kwa moja. Akachagua kusafiri kupitia Samria.

Somo letu linahusu matukio yalliyotokea kwa sababu ya uamuzi wa kupitia Samaria tunagusia  mazungumzo kati ya Yesu na mwanamke wa Samasria, yaliyoelekea hadi Wasamaria wengi kumwamini Mesia (Masihi) somo linatufundisha sisi kwamba Mungu humpokea yeyote anayemsogelea yeye kw aroho na kweli.

 

Yohana 4:1-42

Wasamaria, walikuwa wazawa wa watu waliorudishwa katika Israeli kutokea kwa Wanasyria baada ya kuwachukuwa kabila kumi za Israeli kwend autumwani karibu mwaka wa 750 kabla ya Kristo. (Rejea hatua 3 somo la 14). Wayahudi waliobaki walioleana na wageni na ibada sahihi ya Yahwe ilichanganyikana na ibada za miungu ya kipagani na ikafanyika uchafuzi wa kweli. Hekalu lilijengwa mlimani Gerizimu katika mkoa wa Samaria na hivyo ukaanz amdahalo iwapo ibada ya Kiyahudi au ya Kisamaria ndiyo ilikuwa sahihi. Chuki kubwa ilikuwepo kati ya makundi haya mwili, angalao Wasamaria walidai kuwa naukoo pamoja na Wayahudi. Walidai kuwa walikuwa wazawa wa Yusufu mwana wa Yakobo, kupitia kwa Efraimu na Manas. Alikuwa nimmwanamke Msamaria amabye kwa mila za Kiyahudi ilibidi amchukie na kumdharau, aliyezungumza na Yesu.

 

Kisima cha Yakobo

Kisima cha Yakobo kilikuwepo penye bonde lililo kati ya milima Ebali na Gerizimu kule Sikari karibu na Shekemu. Kisima hicho kilikuwa kimechimbwa na Yakobo katika kipande cha nchi kilichonunuliwa kwa mkaazi wa mkoa huo lakini ambacho kwa yakini kilikuwa sehemu ya kambi ya Abrahamu (tazama Mwanzo 33: 18-20; Matendo ya Mitume 7:16). Kilikuwa na kina cha mita 40 na maji yalikuwa yakibubujika yaani yalikuwa ni maji “hai”. Tunapoangalia historia ya shughuli za Mungu kwa watu wake kule Shekemu tunapata mkazo katika ibada ya Mungu, agano za ahadi, na utakaso wa kazi za uovu. Ukombozi kupitia kwa Kristo ilibidi kufundihwa hapa kwa kuzingatia msingi huu.

 

Mazungumzo yasiyo kawaida(Yohana 4:7-20)

Yesu na wanafunzi walikuwa wakisafiri kuelekea klaskazini kupitia Samria. Akiwa mwenye kiu na mchovu, Yesu alipumzika pale kivulini wakati wanafunzi wake wakienda kununua chakula eneo la karibu, ni kwlei alihisi madhaifu yanayowapata watu wote. Wakti akiwa ameketi hivyo pale kisimani, kwa makusudi Yesu akaomba maji anywe. Kutokana na mila na desturi ya Wayahudi angaliuwa na budi kutambua uwepo wake kabisa, lakini akaona fursa kubwa kueneza utando wa njili hapo.

Yule mwanamke alikuwa amemtambua Yesu kuwa Myahudi na kwa hiyo alijibu kwa mshangao kiasi, “inakuwaje kwamba uliye Myahudi unaniomba maji ya kunywa mimi niliye mwanamke Msamaria” kwani Wayahudi hawana ushirikiano na Wasamaria”(mst 9). Hakumlaumu ila alihamsisha kwa kumwambia kwamba angalimfahamu angalimuomba yeye ampatie “maji ya uzima” sasa maji ya “uzima” ilikuwa ndiyo maelezo kwa ajili ya maji yayaendayo au ‘Yabubujikayo” na kisima kilikuwa wakati mwingine kikiitwa “zawadi ya Mungu” kwa hali asili huyo mwanamke alimwelewa Yesu kikawaida. Jibu hili lisilotazamiwa lililmtatiza kani hakuelewa kuwa Yesu alikuwa naongelea uzima wa milele.

Akajibu jibu la Yesu, mwanamke kwa heshima alisema “Bwana huna chombo chochote cha kuchotea, na kisima kina kina kirefu, utapata wapi maji hayo ya uzima? Je wewe ni mkuu kuliko Baba yetu Yakobo…..?” akaendelea kwa kulinganisha maji asili na maji ya kweli ya uzima ambayo angaliweza kutoa “yoyote anywaye maji ambayo nitampatia atakuwa ndani yake kisima cha maji yayoelekeza kwenye uzima wa milee”. Lakini kwa sababu akili yake ilikuwa bado inawazia juu ya maji asili na siyo kisima cha uzima wa milele, aliona faida ya wazi wazi ambayo yule mgeni alisema angaliweza kutoa. Sasa akawa ndiye mwenye kuomba maji anywe kwa shauku akaomba.

Katika hatua hii Yesu akabadilisha maongezi, alikuwa mnyenyekevu na mwenye shauku, walakini yule mwanamke alikuw abado hajui alikuwa na nani na ni aina gani ya nguvu ilikuwa nazo. Yesu ndipo alipotoa ombi la kawaida kabisa “nenda kamwite mume wako na aje hapa”. Kama kwamba alitaka naye kushiriki katika zawadi pia. Akajibu kwamba hakuwa na mume na Yesu kwa kubaini siri za maisha yake binafsi alimleta katika kutambua ya kuwa alikuwa nabii, wali siyo mgeni tu aliyezumgumza kwa tanzia. Bado hakuwa katika ngazi ya kufahamu ya kwamba Yesu alikuwa nabii mkubwa kuliko Musa (Kumbukumbu la Torati 18:15-18). Kwa haraka aliacha suala la maisha yake ya uovu na kuchukua nafasi hiyo kupata utatuzi kwa swali kuu la kama mlima Gerizimu au Yerusalemu ndipo palikuwa mahali sahihi pa kuabudia.

 

Ibada ya kweli ya Mungu (Yohana 4:21-25)

Katika jibu lake, Yesu aliweka vitu vingi mbalimbali vitu hivi ni vyenywe maana kwetu pia. Alisema

  1. Maangamizo yatakuja juu ya Gerizimu na Yerusalemu na hivyo kuzuia kuabudu pote pawili(hili lilitokea yapata miaka 40 baadaye)
  2. Ukombozi unaotokea kwa Wayahudi, kupitia tumaini lla Israeli lakini
    1. “Waabuduo wa kweli watamwabudu Baba katika Roho na kweli” yaani kw aakili na kwa umakini pamoja na imani sahihi na wala siyo kwa muonekano wa nje (linganisha Yoshua 24:14 maneno haya yalisemwa katika eneno karibu lilelile ambapo Yesu alikuwa akisimama muda ule) siyo kwa kuchanganyikiwa kama Wasamaria walivyofanya
    2. Baba anawatafuata waabudu wa kweli kumwabudu yeye (linganisha Isaya 66:1-2). Mungu anataka Wahayudi kumtumikia kwa heshima unyenyekevu katika akil na vitendo
    3. Mungu ni roho, yani yeye ni mwenye akili na siyo kinyago kisichohai. Kw ahatua Fulani, jibu la Yesu lilimfanya yule mwanamke atamnbe wajibu wake kwa Mungu. Bila shaka alihisi katika nguvu za jibu lake ya kwamba Wasamaria walikosea kwa hakika mwanamke alikubaliana na hilo wakati alipoharakisha kuongeza ya kwamba Masihi angaliwafundisha Wasamaria yaliyo kwlei angalipokuja.

 

Imani juu ya Masihi kule Samaria (Yohana 4:26-35)

Kasha (ndipo) ukaja ufunuo kutoka kwa Yesu “Mimi nisemaye nawe ndiye Masihi” kwa mwanamke Msamaria alikuwa ameshasema hadharani u-Masihi wake.

Akiacha mtungi wake wa maji yule mwanamle akarudi haraka mjini kuwaita jirani zake. Wakati huo huo Yesu akaeleza kwa wanafunzi wake waliokuwa wamerejea punde ya kwamba alikuwa na akzi kuu na shangwe ya kupindia mioyo ya watu mjini Sikari. Kwa macho yake ya imani aliweza kuona Wasamaria wengi wakitubu< kwani yule mwanamke alikuwa akisambaza ujumbe ya kuwa Masihi alikuwapo nje ya mji, nao walikuwa wakija kmwona. Jinsi ilivyopendeza mapokezi ya watu yalivyoonyesha. Jinsi ilivyokuwa tofauti na Wayahudi ambao walikuwa wamempinga Yesu kabla ya kuondoka Yudea. Wasamaria wengi waliamini kwa sababu ya maneno Yesu aliyoyasema kwao. Wakitafuta maji ya uzima walimuomba abaki kwao. Kwa siku nyingine mbili Yesu akawaonyesha “kipawa cha Mungu” hakika mavuno mhali hapa yalikuwa makuu

 

Somo kwa ajili yetu

Yesu aliongelea “maji ya uzima” kwa wale wanaoona kiu ya kiroho Yesu anawez akuwapa maji haya. Ndilo neno la Mungu na hili linaweza kuwaongoza watu kwenye uzima wa milele (Yohana 5:39,; 17:3). Nabii Isaya alitumia lugha kama hiyo aliposema Lo, kila mmoja aonaye kiu, njooni kwenye maji….. egemea sikio lako uje kwangu, sikia na roho yako itaishi” (Isaya 55:1-3)

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Lakini kunatakiwa mahitaji Fulani kwa wale wanaokuja kwake Mungu, inapasa wamuabudu kwa hali sahihi. Hili linatuhusu sisi pia., Mungu natafuata toba yetu na halafu ibada kwake yeye katika uaminifu, utakatifu, kweli na roho. Hili lina maana ya kwamba inatubidi kujifunz amapema kutoa maisha yetu kwa Mungu, kuamini ile kwlei na bila kujaribu kujifanya au kujionyesha kuwa tunamtumikia Mungu, kama tunaamini kwa kweli ya kwamba Yesu ndiye hakika “mwokozi wa dunia”basi Mungu amatuahidi sisi uzima wa milele iliyo heshima ya juu kabisa kwa ajili ya mwanaume au mwanamke yoyote.

 

Maktaba ya rejea

“The Gospel of John”(J. CARTER) chapter 4

“Story of the Bible”(H.P.Mansfield) vol 8 pp.118-127

“A life of Jesus” (M.Purkis) pages 76-80

“Nazareti Revisited”(R.Roberts) chapter 14

 

Maswali ya paragrafu

  1. Wasamaria walikuwa ni nani na waliamini nini?
  2. Yesu alimwambia nini mwanamke Msamaria kuhusu ibada ya kweli?
  3. Ni kwa jinsi gani Yesu alimwonyesha mwanamke Msamaria ya kuwa alikuw anabii?

 

Maswali ya insha

  1. Eleza maongezi ambayo Yesu alikuwa nayo pamoja na mwanamke wa Samria kwenye kisima cha Yakobo
  2. Yesu alisema nini kuhusu ubishi uliokuwepo kati ya Wayahudi na Wasamaria juu ya ibada ya kweli?

 

PICHA YA WATU

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Swahili Title
203. Imani kwa Masihi huko Samaria
English files
Literature type
Sub type
Sub sub type