206. KUWAFUNDISHA WANFUNZI WAKE
(i) Sifa na heri “akafunua mdomo wake akawafundisha”
Katika somo lililopita tuliona jinsi kwa sla aliwachagua wanafunzi wake 12 ambao baadaye waliendeleza kazi ya kueneza injili. Sasa wanafundiwswa katika karama za uadilifu amabzo ilikuwa waonyeshe katika maisha yao iwapo walikuwa wampendeze Bwana wao. Na kuonekana wenye kustahili kushiriki katika ufalme wa Mungu, mafunzo hayo ni kama ujumbe uliopewa kutoka kwa mfalme kwenda kwa watumishi wake wengiwa vizazi vyote ingawaje mafundisho hayo yanawahusu kimsingi wanafunzi wa Yesu, watoto wanaweza kujifunza inamaanisha nini kuwa wanafunzi wake. Hapo wataweza kuelewa na kuheshimu vipawa. Vipaji au karama na matendo ya wale waliompokea Kristo na wanaojaribu kuishi kwa mihimili iliyoorodheshwa katika heri au sifa hizi.
Heri au sifa
Hizi zinamaanisha baraka zinaelezea hali ya furaha ya aina ya juu kabisa, raha ambayo hakluna chochote au yeyote anayeweza kuiondoa kw asababu inatoka kwa Mungu. Ni uhakikisho wa upendo wa Mungu unaoendelea sasa na daima.
Heri na sifa kwa pamoja zinafanyika ufafanuzi wa muumini anayekubaliwa na Mungu. Dalili hazimaanishi kuonyeshwa moja moja ndani ya watu wengi, bali zinamueleza mtu mmoja kikamilifu.
Yesu mwenyewe ndiye alikuwa mfano wa watu aliymuelezea, wengine inawapasa kujaribu kukuza karama hizi hizi ambazo Yesu anasema zitawazawadia na mahali katika ufalme wa Mungu. Walakini, mafundisho yakle hayawahusu wale walio nje ya kweli, yanaeleza tabia au karama za uadilifu za watu mmoja mmoja (binafsi) wanaoelewa agano la Mungu.
Kkuwa heri ana sifa nane, mistari 11 na 17 kwa kweli haimo ndani ya kundi lka zile nan kwa sabbu ni utekelezaji wa heri ya mwisho (mst10) kwa wanafunzi wenyewe, kuwahimiza katika juhudi zao kuendeleza tabia ya haki inayofanana nay a Kristo. Mafunzo hay ohayo ynapatikana katika Luka 6.
- Masikini katika Roho (Mathayo 5:3)
Neno “Masikini” hapa linamaanisha “masikini kabisa bila ya njia ya kugeukia kupata ahueni” hivyo “masikini katika roho” inamueleza mtu anayetambua uhohehahe wake, dhambi na umasikini war oho na hana popte pa kugeukia ila kwa Mungu. Mtu huyu masikini namuomba Mungu kwa uongozi na msamaha, na anatambua ya kwamba kwake yey binafsi hawezi kufanya chochote zaidi ya hayo hategemei tena juu ya lolote ambalo mwili unaliona linapendeza (linavutia) ila anatambua ya kwamba chanzo cha kwlei cha hekima ni neno la Mungu. (tazama msimamo wake kw aneno lile katiak Isaya 66:2), inapendeza sana kuona ya kwmaba matokea ya mwisho ya umasikini huu ni utajiri mkuu kwa wote wanaoedndeza taboa inayoonyesha katika heri na sifa hzi kwao ufalme wa Mungu unapewa angalao hawajapata bado ile zawadi yao ya hakika kabisa.
Angalao ufalme wa Mungu unaitwa “ufalme wa mbinguni” kwa sababu ndiyo ufalme wa yule mmoja anayekaa huko mbinguni sivyo ulivyo s”siyo ufalme ulio mbinguni”
- Wale waliao (Mathoyo 4:4)
Ni jambo lisilo la kawaida ya kwamba waliao (waom,bolezao) wana furaha. Kwa njia gani hili ni hivyo? Yesu hapa anarejelea kwa aina Fulani tu ya waombolezao, ni waumini walio ndani ya sikitiko kuu kwa sababu ya vitu kama dhambi au jaribu au majaribu yaw engine, au kutokuwepo kwa Kristo au kwa sabbu ya hali ya uovu wa jamii. Lakini kulia huku kunawalketa karibu zaidi na mUngu sasa nao wanastarehe na hamasa katika kufahamu juu ya “nyakati za kuburudisha” zitakazokuja (Matendo ya Mitume 3:19-21; Ufunuo wa Yohana 21:4 ona pia Isaya 61:1-3)
- Wapole (Mathayo 5:5)
Wapole ndiyo watiifu (wanyenyekevu) awanaokubali mapenzi ya Mungu kwa furaha. Upole siyo udhaifu, lakini tabia inayopatikana ndani ya watu wenye nguvu sana, kama Yesu na Musa (Hesabu 12:3), unakuja kutokana na kutupa chini kiburi na ubinafsi kwa kuomba akila ya kiroho, wapole kila wakati wako tayri kumsikiliza Mungu (Zaburi 25:9 ona pia mst 10-14). Kwa sababu wanafundishika sasa, Mungu atawapatia ulimwengu kwa urithi (Zaburi 37:11)
- Kuwa na njaa na kiu ya haki (Mathayo 5:6)
Nguvu yote na maana ya heri hii inatolewa katika “amebarikiwa na ni heri yule anayatamani mno haki yote” mtu anayebainishwa ni yule mmoja asiyeridhika hadi haki ipatikane ulimwenguni, anatamani kwa dhati haki yake mwenywe kwa imani au kuonekana na Mungu kwa mwenye haki. Na kwa watu wote kuwa waadilifu. Anatamani haki kamili siyo haki inayochanganyikana na dhambi kidogo wakati nafasi ipatikanapo.
Kiini (au chanzo) cha haki ambacho mtu mwenye njaa na kiu ya kiroho angakigeukia na neno la Mungu. Petro alisema “kama watoto wachanga waliozaliwa upya yatamanini yale maziwa ya neno ili kwa hayo mpate kukua” (1Petro 2:2). Ni katika neno hili ambamo anapokea (au anpata) kuridhika. Yesu alisema “mimi ndimi chakula cha uzima; yeyote ajaye kwangu hataona njaa kamwe, nay eye aniaminiye hataona kiu kamwe” (Yohana 6:35; ona pia Isaya 55:1-3)
- Wenye rehema (Mathayo 5:7)
Ile tamaa kui kwa ajili ya haki inapasa ilingane na rehema na msamaha wakati wengine wanaposhindwa. Yahwe mwenywe anatuonyesha hili katika tabia yake (Kutoka 34:6-7). Kuendelea kupata rehema kutoka kwa Mungu kupitia kwa Kristo, inatupasa tuonyeshe rehema na msamaha kwa wengine (Zaburi 18:25). Tusiwe wepesi kuhukumu watu ila tujaribu kuelewa, ili tuwe na shauku kutatua tatizo.
Kuna sababu nzuri sana kwa nini tuwe wenye rehema (au fadhili). Mungu ametupenda sisi anye ni Mungu w rehema. Iwapo tumegushwa kweli na fadhili za Mungu tutaionyesha katika msimamo wetu kw awatu wanaotuzunguka. Tutakuwa na tama ya kutenda kitu kwake (au kwa ajili yake) ambaye amefanya mengi mno kwa ajili yetu. Karama ya rehema inapatikana ndani ya wale walio watiifu kw aamri kuu ya pili (Mathayo 22:39)
- Wenye moyo safi(Mathayo 5:8)
Safi inamaanisha “isiyochanganyka” au “huru kutokana na uchafu” usafi wa moyo (akili) utaoongeza kwenye matendo ya hakli na kweli. Moyo siyo safi iwapo vitu vya mtu binafsi visivyoheshimu Mungu vinachanganyika na vitu vya maslahi matakatifu ya Mungu. Kwa asili, mioyo ya watu siyo safi na ikiachwa peke yake watu wote watazawadiwa kifo (linganisha Yohana 17:9-10). Utakaso (usafisaji) unaweza tu kupatikana kwa kuwa makini ndani ya yule aliye safi na mtakatifu, na kupokea (kukubali) toleo lake kwa kusafishwa katika ubatizo. Kusogea kwa MUNgu, sasa kutaongoza kwenye “kumuona Mungu” katika wakati ujao (ona 1Yohana 3:2-3)
- Wapatanishi (Mathayo 5:9)
Wazo lililomo ndani ya neno kwa amani ni “chochote ambacho kinatengeneza mema kwa ajili ya watu” siyo tu kutokuwepo vita. “kuleta amani kunadhihirisha ya kwamba bidii inahitajika kwa amani kuopnekana”. Kupatanisha ni kazi ya kujenga, kunaanz ana kunyamazisha roho isiyotulia ya mtu mwenyewe na kuja kwa mUngu. Ndipo mtu inampasa kujifunza yykuishi kwa usawa na wengine, akikubali mapungufu yao bil kutazama zaidi kutoka kwao kuliko yeye alivyo tyari kutoa, usawaziko huu utaongoza kwenye maisha yaliyojaa amani mabayo hakuna mtu au mazingira yanaweza kuangamiza.
Amani ni “tunda la roho” na “kazi ya haki”(Wagalatia 5:22’ Isaya 32:17). Wale wasiokuwa na mioyo safi hawatapata amani ya hakika (au amani halisi), kwani “hakuna amani kwa waovu”(Isaya 48:22)
- Kuudhiwa kwa ajili ya haki(Mathayo 5:10).
Tabia ya mtakatifu siyo ya kuvutia kwa dunia. Vile vile kama Yesu alivyoudhiwa kwa sababu ya haki, hivyo ndivyo muumini wa kwlei atakavyoudhiwa kwa sasa, uzuri wa mtakatifu unaonyesha wengine kuw awakosaji (wenye dhambi), wanaochukia nuru na hawataki kubadili njia yao (Linganisha Yohana 3:20)
Ni katika hekima yake mUngu kwa mtu kuteseka kwa sababu ya kutenda yaliyo sahihi, akiyachukulia kwa subira na hata kwa shangwe (1Petro 2:20). Matokeo haya huijaribu imani ya mtu na kuikuza tabia yake ikimfanya amtegemee yeye zaidi na zaidi kwa nguvu ya Mungu. Mungu anaahidi ya kwamba Yesu Kristo atakuja kuleta raha kwa wenye haki wanaoteswa laikin atawaaibisha watesao –waovu (2Wathesalonike 1:7-10)
Mistari (aya) 11 -12
Mistari hii inahusu moja kwa moja wanafunzi wa Yesu ambao alikuwa akiwahubiria kutoka ukingoni mw amlima. Yesu alijua ya kwamba maudhi machungu yangekuwa juu yao iwapo wangeaamini na kuyafanyia kazi mafundisho yake. Lakini, wangalipata raha kwa ufahamu wa kwamba Bwana wao mpendwa alivumilia, akapata “ukamilifu kwa mateso”na kuzawadiwa taji ya uzima(linganisha Waebrania 12:1-3; 2:10; 5: 8-9). Wakati Petro na mitume walipopigwa na watawala huko Yerusalemu muda Fulani baadaye, walishangilia kwa sabbu walikuwa na heshima ya kuteswa kwa kuunga mkono (au kutumikia) kazi ya Kristo (Matendo ya Mitume 5:41) badala ya kusikitika walikuwa na kisa kuruka kwa shangwe.
Somo kwetu
Tabia iliyobainishw ana Yesu katika heri hizi ni zile za mtu kamili na mUngu. Kwa kufuata tabii hii mwanafunzii wa Kristo inampasa.
-
- Kutambua umasikini wake na kutafuata utajiri wa kudumu katika Kristo
- Kusikitikia halki yetu duniani na kutamani nyakati za raha ya milele
- Kukuza nguvu za tabia kwa upole, wakifundishwa na Mungu
- Kutafuata haki ya Mungu binafsi na kwa dunia yote
- Kuwa tayari daima kusamehe na siyo kulaumu kwa ukali
- Kutenda kw ania safi, mkiwa na uaminifu usiogeuka kwa Mungu
- Kuweka amani baada ya kuwekwa huru kutokana na nguvu ya dhambi ndani yake mwenyewe, warudishe na wengine
- Kuwa tayri kupata upinznai na lawama kwa kutopunguza mihimili (au hadhi) mbele ya watu wengine, mkitambua heshima ya kuteswa kwa ajili ya Mungu.
Zoezi :Tazama kama unaweza kushika kichwa aya 1-11, ni zoezi la faida sana kufanya hivyo
Maktaba ya rejea
“The tenolimo of the master” (L.G.Sargent) part II
“A life of Jesus” (m.Purkis) pages 129-137
Maswali ya fungu
- Onyesha jinsi tabia iliyobainishwa na Yesu katika heri ndiyo ya mtu kamili wa Mungu
- Onyesha kutokana na heri namna masikini walivyobarikiwa na waliao watapata furaha
- Jadili namna vijana wa Kristadefia wanaweza kuwa wapole na wenye mioyo safi wakati wakiwa shuleni
Maswali ya insha
- Kwa kifupi eleza tabia ya mtakatifu kama ilivyoanishwa katika heri
- Eleza (fafanua) maneno yafuatayo ambayo Yesu aliyatumia wakti wa hotuba yake mlimani ni kwa nani yanahusika “wamebarikiwa” “ufalme ni wao”, “watamwona Mungu”, “wana wa Mungu” na “haki”
PICHA YA TUFANI