CSSA 2-4-05 - THE CALLING OF THE DISCIPLES

English

205. KUITWA KWA WANAFUNZI

“Kama mtu atanifuata na ajikane mwenyewe…”

Wanfunzi wa Yesu hawakuchaguliwa wote kwa mara moja ila mmopja mmoja na wawili wawili. Wawili wao wa kwanza walikuwa wanafunzi wa Yohana Mbatizaji, aliyeagiza waende kwa Yesu. Wakati wanafunzi walivyoendelea na Yesu elimu yao juu ya neno la Mungu iliongezeka sana, nao walijifunza kutoka kwake ya kwamba uanafunzi wa kweli unamaanisha kuwa mtu amweke Mungu mbele awe wa kwanza katika maisha yake. Muda ulivyozidi kuendelea ilikuwa muhimu kuchagua kutoka kati ya wanafunzi wanaume (watu) kumi na mawili ambao wangekuwa na mamalaka maalumu ya kuhubiri na kudumisha kweli. Hawa watu wakaitwa mitume (ma-apsoteli). Iwapo tunatamani hatimaye kufanyika kuwa wanfunzi wa kufanya yote yawezekanayo kuyatendea kazi siku kwa siku. (Yohana 1:29-51; Luka 5:11, 27-23; 6:12-16)

 

Wanafunzi wa kwanza (yohana 1:28-51)

Ubatizo wa Yesu ulipokelewa ulichukuliwa kw adhati na Yohana Mbatizaji, Yesu alipomjia katika jangwani majuma sita baada ya ubatizo ule siyo ajabu ya kwamba Yohana apige kelel “Tazama mwanakondoo wa Mungu achukuaye dhambi za ulimwengu”. Siyo hivyo tu lakini Yohana aliwafunza wanafunzi wake kuhusu ubatizo ule “niliona na kushuhudia ya kwamba huyu ni mwana wa Mungu” kwa ujulisho huo, wanfunzi wa Yohana walikuwa tayri wakati yahana alipomuonyesha Yesu siku iliyofuata na Kusema”tazama mwanakondoo wa Mungu”.

Wanfunzi wawili walioitika mara moja walikwa ni Yhana (ambaye baadaye aliandika hadithi za injiili na Andrea wotewawili walikuwa wavuvi wa Galilaya. Walikuwa na shauku kufahamu zaidi juu ya “mwanakondoo wa Mungu”na kwa ukaribisho huu wakatumia usiku ule kukaa naye. Atahri ya saa zile za kutia moyo wakiwa pamoja na Yesu inaonekana katika harakisho (mbio) za Andrea kumtafuata nduguye Simoni  alipomuona akainuka “tumempata Masihi”

Pamoja walirudi kwa Yesu ambaye alipomtazama Simioni aksema kiasi cha maneno makubwa “wewe ni Simoni mwana wa Yona utaitwa Kefa au Petro.” Yesu alimkadiria mwanafunzi huyu, Simoni alikuwa mchanganyiko wa unyenyekevu, mwelekeo mbele na kupendeka. Akaendelea kuitwa Petro, ambayo ikitafsiriwa ina maanisha jiwe au mwamba, imani yake iliyokuwa kama jiwe, ikijaribiwa kwa mitihani ingalikuja kuanzisha inakusanyiko (eklesia) nyakati za matendo ya mitume.

Siku iliyofuata aliamua kusafiri kuelekea kaskazini kupitia Galilaya kwenye miji ya wanafunzi wale watatu, kabla hajaondoka akamwita Filipo, naye pia alikuwa akitokea Bethsaida mji wa nyumbani kwao Petro na Andrea, huenda pengine naye pia alikuwa mwanafunzi wa Yohana naye akiwa na shauklu ya kukutana na “mwana wa Mungu” Yesu aliona ndani ya Filipo karama za uanafunzi na akamwita, alisema “nifuate” akiwa na hisia za uokeaji kama Andrea Filipo akakimbia kumwita Nathanieli. Yawezekana hawa rafiki wawili walikuwa wameshaogelea juu ya Masihi. Hivyo tunaweza kuwazia dukuduku la Filipo alipombainisha Yesu “tumempata yule ambaye Musa katika torati na manabii, walimuandika Yesu wa Nazarethi, mwana wa Yusufu”. Nathanieli akamsikia akisema “tazama mu-israeli hakika, asiye na hila ndani yake” Nathanieli akastuka na kuuliza jinsi Yesu alivyomfahamu, Yesu alijua yaliyomo moyoni mwake na akimtambua mtu wa sala na uaminifu akasema “kabla Filipo hajakuita, ulipokuwa chini ya mtini nilikuona” Nathanieli alishangaa(alishikwa na fadhaa). Hapa mbele yake apalikuw ana mmoja ambaye Musa katika torati na manabii walimuandika, mmoja ambaye aliweza kusom,a mioyo ya watu mbali na mipaka (viwango) vya utafityi (tafakari) ya kibinadamu. Kwa mshangao akamaka “Bwana wewe ndiye mwana wa Mungu, wewe ndiye mfalme wa Israeli” Yesu aliitikia kw afuraha imani hiyo na kumwahidi Nathanieli ya kuwa angeona vitu vikuuu, miujiza ambayo ingeonyesha kwa jicho la imani ya kwamba mbingu zilifunguka juu ya mwana wa Mungu na malaika walihudumia na kuongoza kila tendo lake.

Atarudi tenda akiwa hakimu(Yohana 5:27) pamoja na malaika wa Yahwe (Mathayo 25:31) kumsaidia kuanzishaufalme wa Mungu. Nathanieli atakuwepo kushiriki siku ya utukufu wake Kristo. Na, sisi kw aimani ifananayo na ile ya Nathanieli tutazamie kuwepo katika siku ile tukufu.

 

Wavuvi wa watu(Luka 5:1-11)

Yesu akawaacha baadhi ya kundi lake dogo la wanafunzi kurudi nyumbani kwao na kwa zamii zao na kumbukumbu zao. Akili zao zingalirejea kwenye miezi ya matukio yale ya bonde la Yordani, huko Yerusalemu na kule Samaria, mioyoni mwao walielewa ya kwamba alikuwa ndiye Masihi, na sasa mengine yoyote yalionekana yasiyo na maana kulingana na kuwa wanafunzi wake. Bila shaka walitamani kurudi kwao, walikuwa tayari kwa wito wake.

Kukamatwa na kifo cha Yohana Mbatizaji kilifanyika kama dalili kw aYesu ya kuanza kazi yake kamili hadharani. Kutoka wakati ule Yesu alianza kuhubiri na kusema “tubuni kwnai ufalme wa mbinguni umewadia” (Mathayop 4:17)

Huduma hiyo ilihusu kuhubiri na kuita wanafunzi, tunasoma ya kwamba Yesu alikuja ukingoni (pwani) ya bahari ya Galilaya. Simony na Andrea walikuwa wakiosha nyavu zao baada ya usiku kucha wa kuvua bila kupata chochote. Waliposimama waliona kundi linakaribia kumzunguka mtu ambaye mara moja walimtambua, alikuwa ndiye Bwana wao mpendwa lile kundi anaandika “lilimzonga ili kusikia neno la Mungu” (Luka 5:1) akiwa na ari kufundisha watu wake njia ya Mungu, Yesu akapanda ndani ya mojawapo ya mashua zake na kufundisha lile kusanyiko lililosimaa ukingoni. Mafunzo yakiwa yamemalizika, Yesu sasa akageukia kwenye mahitaji ya wanafunzi wake, hitaji la hakikisho, akadhihirisha nguvu yake kwa mfano ambao ungalgusa moyo wa wavuvi hawa.

Yesu akamwambia Simoni kuendesha mashua hadi kulindini na kuteremsha nyavu zao kwa kuvua samaki. Twaweza kufikirei (kuona) namna SImoni allivyoinua kamba za macho yake ambaye alifikiri alijua yote wapi na jinsi gani kuvua, ambao ulikuwa mwingi (mkuu) ungalionyesha utovu wa kutii maelekezo ya Yesu. Lakini kwa heshima ya Yesu hakulalamika na kubisha kwa ujuzi wake aliokuw abora zaidi “lakini kwa neno lako nitashusha nyavu)

Mara hiyo bahari ilichemka kwa samaki warukao, kwa wingi hivi kwamba nyavu zikawa zinakatika kwa uzito wa mavuno makuu vile haraka kuita msaaada wa wavuvi wengine, Simoni alifanya bidii muda wote akijisema sema jinzi alivyokwa mpumbavu kuweka shaka kwamba Yesu alikuw amkuu katika vitu vya kiroho na kwenye kila eneo la maisha ya kila siki likiwemo eneo lake maalumu, uvuvi. Alikuwa ameona miujiza kabala lakini huu ulikuwa muijuza uliomshutua yeye mno na kumsukuma kuangukia magotini na kusema “ondoka kwangu, kwani mimi ni mtu mwenye dhambi ee Bwana” akijihisi asiye stahili kabisa, Petro alijifunza somo muhimu la uanafuzi imani kamili kwa Umasihi wa Yesu. Hisia ya mshangao na uduni ulishirikisha na hao wavuvi wote wanne. Akiwatuliza na kuwatia moyo imani yao, Yesu alisema “msiogope, kutokea sasa mtakuwa wavuvi wa watu” wanafunzi hao hawakuhitaji ishara nyingine. Wakajiziacha mashua yao pamoja na mavuno (mzigo) ule mkubwa na mara hiyo “wakaacha vyote, na kunifuata” (mst 11)

Somo la jinsi gani limo ajili yetu katika miujiza wa kusanyo lile ku la samaki. Yesu ni Bwana katiika kila suala la maisha, pamoja nay ale ambamo tunafikiri tunayajua yote kabisa. Uzoefu wetu na kujiamini katika mwendo wetu mdogo wa maisha unaonekana dhahili mno wakati tukimkabili mwana wa Mungu, na nguvu yake yote na upendo wake. Tunaaibika tunapoangalia nyumba juu ya maisha yetu na kuona nyakati Fulani ya kwamba katika kujitegemea kwetu tummejibidisham, bila kwenda popote, mpaka tukubali maagizo ya Yesu na kupata ya kwamba matatizo yetu yametatuliwa na maisha hao yetu kutajirihshwa na baraka zake. Ndipo kw akuamini katika ukubwa wa mapenzi yaek, tunajiba kw akuanza mwendo kumfuata yeye na kufanyika wavuvi wa watu.

 

Kuitwa kwa Mathayo(Luka 5:27-32)

Mathayo alikuwa Myahudi asiyekubalika, kazi yake ilikuw ani kutoza kodi kwa ajili ya Warumi watawala waliochukiwa na Waisraeli. Lakini kwa kule kuwekwa katika nyumba ya kodi iliyotawala barabara kuu pale Kaperinaumu angekutana na watu kila siku waliokuwa wakisafiri mara nyingi umbali mrefu sana wakwia na ndugu zao wagonjwa ili tumfikia huyu nabii mkuu. Angekuwa na ufahamu wa habari za ajabu na uponyaji, pengine alifahamiana na wanafunzi na kwa hakika akishangaa moyoni mwake kuhusu maana ya matukio haya ya kusisimu. Kazi yake pia ilileta chuki na kijicho juu yake mwenyewe, bila shaka angetumaini ya kwamba kwa kuwa Yesu. Aliwahurumia masikini na wanaoteswa ya kwmaba huruma hiyo hiyo na kutia moyo siku moja ingemfikia naye.

Yesu alikuja kwake siku moa, alisema “nifuate” Mathayo hakuhitaji kusukumwa akaacha vyote akasimama na kumfuata. (mst28). Kamatendo ka kuagana njia ya zamani ya maisha yake, Mathayo aliwaalika watoza kodi wengine kwenye sherehe kubwa, kulikuwa kuagwa kwake lakini aliona kuwa ilikuwa fursa kwa ajili rafiki zake kukutana na Yesu, lakini waandishi na Mafarishayo walijaribu kuamsha chuki ya wanafunzi dhidi ya watoza kodi. Kabla hawajaharibu uaminifu wa wanafunzi, Yesu akatoka mbele na kuwatetea wanafunzi wake, Mathayo akiwemo kwa kusema “wale walio wazima hawahitaji daktari, bali wale walio wagonjwa, sikuja kuwwaita wanye haki, ila wenye dhambi wapate toba”(mst31-32). Shughuli yake ilikuwa ile ya mganga, akiponya magonjwa kimwili na kiroho, ambapo wao, kinyume kwake walijaribu kuwa na mkabala na watu wa daraja la chini. Katika kujifanya wenywe kuwa wenye haki waliogopa “kuchafuliwa”

 

Wale kumi na wawili (Luka 6:12-16)

Jumla ya wanaume na wanawake waliojiunga kwa Yesu wakaongezeka haraka haraka alipokuwa akihutubia injili ya ufalme na kufanya miujiza, muda ulivyoendelea kuwalazima, ili kudumisha kazi yake kuelekea usikivu.

Haikuwa kazi rahisi kuchagua na kwa sababu ya umaana wake Yesu alienda mlimani, na “kukesha uski kucha katika sala kwa Mungu” asubuhi akafanya chaguo lake.

Jua ya wengi tunafhamau machache walakini tunafahamu ya kwamba ukimwacha Yuda, walikuwa waaminifu kwa wadhifa yaliyowekwa juu yao, walionyeshaudaifu wa kiutu, na kushindwa nyakati Fulani, kutekeleza maelekezo ya Bwana wao, lakini walijifunza kutokana na makos ayao. Hawakuwa wenye elimu ya juu sana, wala hawakuchaguliwa kwa ajili ya uwezo wa kusema ila kwa sababu ya tabia yao.

 

Maktaba ya rejea

“A life of Jesus” (M.Purkis) pages 61-65,95-95; 114-119

“Nazarethi Revisited”(R.Roberts) chapter 12,16,22

“The Gospel of John” (J.Carter) pages 28-39

“Story of the Bible”(H.P Mansfield) Vol 8, pages 90-94, 117 -120, 143-145

 

Maswali ya fungu

  1. Eleza mkutano wa kwanza wa Angrea na Petro na Yesu
  2. Eleza hisia ya Petro juu ya mavuni ya miujiza ya samaki
  3. Namna gani Mathayo aliitwa kuwa mwanafunzi?

 

Maswali ya Insha

  1. Eleza hisia za wanfunzi wa Yohana kwa Yesu
  2. Onyesha jinsi uvuvi wa miujiza samaki ilivyowafunza wanafunzi haja ya imani kamili kwamba Yesu ni Bwana Kweli

 

 

Somo kwetu

Ari ya mwanzo katika Yesu yaweza kuwa njia ya kuwajulisha wengine kwa Yesu. Sisi wote twaweza kuonyesha ari yetu katika ufahamu ya kwamba Yesu kwlei ndiye Masihi na mwana wa Mungu.

            Ari hiyo itajaribiwa kwa mazingira ya kila siku ya maisha kuona kama sisi tunaamini kwlei ya kwmaba Yesu ni Bwana  katika kila hali ya maisha yetu.

            Wakati Fulani tutatambua ya kuwa imani, yetu siyo kamili kama iinavyotakiwa na kwa unyenyekevu tutainamisha vichwa kwa ukuuu wa upendo wa Kristo.

            Yesu kwa sala aliwateua wanafunzi wake kumi na mbili. Umoja wa karibu kati ya mwana na baba ni mfano bora sana klwa ithbati yetu katika nguvu ya sala kwa mahitaji madogo na makubwa.

 

Wanafunzi kumi na mbili

Simony Pertro, pia akiitw aKefa , jiwe (kutoka Kiaramu kwa ajili ya Petro Yohana 1:42), mwana wa Yohana (Bar Yona , Mathayo 16:17) mvuvi wa Bethsaida (Mathayo 4:18; Yohana 1:44).mwanzoni mwanafunzi wa Yohana mbatizaji, aliyeoa (Marko 1:30, 1Wakorintho 9:5) aliandika barua mbili na kumshauri Marko kuandika injili yake

Andrea – nduguye Petro aliyekuw amwanafunzi wa Yohana mbatizaji (Yohana 1:34,40) aliwajulisha Wayunani kwa Yesu (Yohana 12:20-23).

Yohana – Mvuvi na mwana wa Zebedayo, mtu wa Bethsaida naye (mathayo 4:21. Luka 5:10) pamoja na Yakobo waliitwa Boanerge “wana wa ngurumo”(Marko 3:17) pengine binamu ya Yesu ambaye alipendwa na Yesu (au ambaye alimpenda). Aliandika injili barua tatu na ufunuo.

Yakobo- ndugu yake Yohana (Marko 1:19) mama yao huenda alikuwa ni Salome dada yake Maria (Linganisha Mathoyo 27:26; Marko 15:40; 16:1 Yohana 19:25).

Filipo – wa Bethsaida pia katika Galilaya (Yohana)

Bartolomayo inamaanisha mwana wa Tolmaiakifikiriwa na wengi kuwa ni Nathanaeli aliyetajwa mara mbili tu (Yohana 1:45; 2:2) kutokea Kana ya Galilaya.

Mathayo aliitwa pia Lawi (Mathayo 9:9; Luka 5:27) mwana wa Alfayo. Mtum,ishi au mtoza kodi au mkusanyaji wa Galilaya, aliandika injili ya kwanza

Thomaso aliitwa pia Didymo, ikimaanisha “pacha” (Yohana 11:16) pia alionana na Bwana mfufuka (Yohana 20:24-29)

Yakobo mwana wa Alfayo (Mathayo 10:3) pengine Yakobo mdogo au kidogo (Mathayo 27:56; Marko15:40; 16:1; Luka 24:10)

Labben Thaddayo pia aliiwa Yuda, siye Iskarioti (Luka 6:16, Yohana 14:22) alifikiriwa na wengine kuwa ndugu yake Yakobo “ndugu yake Bwana” (Yuda 1; Luka 6:16, Wagalatia 1:19)

Simoni Zelote wakti Fulani mwanchama wa chama cha siasa kilichoitwa Zelote (Luka 6:15). Neno Mkananayo ilitumika kwak ni budi iwe la Kikananayo kutokea Kana, Kiaramu kwa Wayunani (Wagiriki) WAzelote (Mathayo 10:4)

Yuda Isjariote mwana wa Simoni Iskariote (Yohana 6:7; Rumi) Iskariote ni “ish-Kerioth” mtu wa Keriothi kusini mwa Yuda (Yoshua 15:25) alimsaliti Yesu na baadaye alibadiliwa na Mathia (Matendo ya Mitume 1:23-26)

 

 

Swahili Title
205. KUITWA KWA WANAFUNZI
English files
Literature type
Sub type
Sub sub type