CSSA 1-1-04 - CAIN AND ABEL

English

4. KAINI NA HABILI

“Habili alitoa sadaka nzuri zaidi kwa Mungu kuliko Kaini”

Shabaha

Kuonyesha kuwa mtu kama apendavyo yeye hawezi kumwabudu Mungu bali “wanaomwabudu Yeye ni lazima wamwabudu Yeye katika Roho na Kweli”.

Tayari tumekwisha jifunza kuwa Mungu anahitaji utii. Ni kutokana na Adamu na Hawa kutomtii Mungu kuliko sababisha Mungu awafukuze kutoka katika bustani ya Edeni. Kama adhabu kwa dhambi zao maisha yao yote yangekuwa ya kufanya kazi ngumu na huzuni mpaka hatimaye kufariki. Hili ndilo lililowatokea wazao wote wa Adamu na Hawa. Wote wamekuwa  ni wa mwilini ndiyo kusema wote wamekufa na watu wote- isipokuwa Bwana Yesu Kristo, wametenda dhambi.

Tutaona katika habari hii watoto wao wa kwanza, Kaini na Habili, jinsi kutokutii tena kulivyo adhibiwa. Mwanzo Sura 4

KAINI NA HABILI WANATOA DHABIHU: Mwanzo.4:1-7

Kaini alikuwa ni mtoto wa kiume wa kwanza kuzaliwa na Adamu na Hawa. Alikua na “akawa ni mkulima wa ardhi’’. Alipanda mbegu za matunda, labda kila aina ya nafaka na mboga za majani (Mstari wa 2). Na mdogo wake, Habili, yeye alikuwa ni “mfugaji wa kondoo”.

Siku moja wana hawa wawili walikwenda kumwabudu Mungu na wakapeleka dhabihu zao katika madhabahu. Kaini alipeleka baadhi ya mazao yake aliyokuwa amelima yawezekana kuwa yalikuwa ni mazao mazuri kabisa katika mavuno yake. Habili alitoa mzaliwa wa kwanza katika mifungo yake, mwanakondoo mzuri au mwana kondoo aliyekuwa bora kabisa aliyekuwepo.

Na kila mmoja alipenda kumpendeza Mungu kwa njia ya sadaka yake aliyokuwa anamtolea. Mungu alipendezwa na sadaka moja tu ambayo alipendezwa nayo.

“BWANA akamtakabali Habili na sadaka yake lakini kwa Kaini na sadaka yake BWANA hakumtakabari” (mistari 3-5)

Ni kweli kuwa Kaini alitoa dhabihu ambayo haikutakiwa na Mungu. Alipoona dhabihu ya Habili ikiwa imekubaliwa alikasirika na kumwonea wivu. Mungu alijaribu kuhojiana Kaini: “Kama ukitenda vema, hutapata kibali?”(msitari wa 7) Mungu yuko tayari kusamehe wakati wote. Jambo pekee ambalo Kaini angefanya ili kuwa ni kunyenyekea mbele za Mungu na kutoa Dhabihu inayo kubalika. Lakini hakufanya hivyo.

Habili alitii na akafanya kama Mungu alivyotaka lakini Kaini alikuwa ni mtu mbinafsi yeye alifanya kama alivyotaka na siyo kama Mungu alivyotaka.

CHUKI HUSABABISHA KIFO.MWANZO 4:8-12

Kadri Kaini alivyofikiria  yaliyotokea ndivyo alivyozidi kukasirika sana. Alikuwa na kiburi sana hata asiweze kubadili mawazo yake na sasa akaanza kumchukia ndugu yake. Hata hivyo Habili hakutenda baya lolote; alikuwa amefanya yale yaliyo kuwa sawa machoni pa Mungu.

 

Kisha ikawa siku moja walipokwenda uwandani, Kaini akamwua ndugu yake, Habili. Chuki ilimwongoza kuua. Kaini alitenda kitendo cha uovu wa dhahili. Mara nyingine tena Mungu alimwuliza Kaini“ yuko wapi Habili ndugu yako?” Kaini alijibu polepole “ sijui, kwani mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?”(mstari 9). Alijaribu kuficha kitendo hiki cha kutisha kwa Mungu akisema kama vile hahusiki kabisa na Habili. Hata hivyo Mungu alifahamu kwa uhakika alichokifanya Kaini na hivyo kumwambia adhabu ya kutisha kwake. Hapo mwanzo alifurahia kuwa mkulima lakini sasa ardhi haitamletea mazao mazuri. Alifukuzwa kutoka nyumbani kwake na atoke penye madhabahu ya Mungu na kuzurura katika nchi maisha yake yote.

REHEMA YA MUNGU INAONYESHWA KWA KAINI.MWANZO 4:13-16

Kaini akamwambia BWANA , “Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki ”(mstari 13).

Kama Kaini aliweza kusikitika ilikuwa ni kwa sababu aliadhibiwa siyo kwa sababu alitenda dhambi. Lakini Mungu alikuwa mwenye rehema . Alitoa ahadi kwa Kaini kuwa hakuna mtu atakayeweza kumdhuru kwani aliweka alama juu yake na kusema mtu yeyote atakayemwua ataadhibiwa saba mara saba. Kaini alifukuzwa mbele za Mungu na kwenda kuishi katika nchi ya Nodi. Ikiwa na maana ya “mafichoni”. Adamu na Hawa walipata mtoto mwingine wa kiume Seti kwani Mungu aliteua uzao mwingine badala ya Habili (mstari.25).Mtu huyu alikuwa akimpenda Mungu na akamtumikia Mungu na akimpendeza kama alivyokuwa Habili.

UZAO WA SETI NA KAINI

Kama vile Habili, Seti alikuwa mtu mwenye haki na uzao wake ulijulikana kuwa ni “Wana wa Mungu”(Mwanzo:2). Kizazi cha Kaini kama alivyokuwa baba yao, walikuwa waovu na waliopenda kulipiza kisasi kwa maadui zao.

Kwa hiyo kabla ya gharika kulikuwa na watu wa aina mbili ulimwenguni, wale waliofuata njia za Mungu na wale ambo hawakufuata njia za Mungu. Na kundi hili la mwisho walijijengea miji mikubwa wakafanya kila kitu kilichowapendeze wao. Muziki, sanaa, mali au silaha za kivita(Mwanzo 4:19-24) ni vitu vilivyowapendeza wao. Hata hivyo, wana wa Mungu  kwa muda walijitenga na dunia na njia zake, kitu pekee kilicho cha tofauti na siku zetu ni tarehe! Tusizifuate njia za Kaini (Yuda mstari 11)

FUNDISHO KWETU

Sababu hasa ya dhambi ya Kaini ni kwamba alitaka afuate njia yake mwenyewe. Na huu ni uchoyo – chanzo cha dhambi zote kwanza ni uchoyo halafu kiburi na majivuno kisha hasira. Alimwua ndugu yake na kisha kusema uwongo “yuko wapi ndugu yako Habili?” Mungu alimwuliza, sijui, aljibu Kaini na kuongeza kwani mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?”(Mwanzo 4:9). Hakukubali kuwa ni mlinzi wa ndugu yake na kwamba siyo jukumu lake kumlinda mwingine isipokuwa yeye anajilinda mwenyewe. Na tuelewe kwamba dhambi ni uchoyo unaokua kutoka ubaya hadi ubaya zaidi. Iwapo hatutaachana na dhambi na kumgeukia Mungu, dhambi itaharibu maisha yetu, na kadri dhambi inavyokua ndiyo kadri tunavyokuwa na huzuni na kuwa na chuki. Wakati unapokosea mwambie Mungu umekosa na umwombe Mungu msaada wake ili uachene dhambi hiyo.

MAELEZO YA NYONGEZA

Tulijifunza katika somo lililotangulia kwamba Mungu alitoa vazi la kufunika dhambi. Hii ilidhihirishwa kwa mara ya kwanza Adamu na Hawa“ mavazi ya ngozi kwa kumwaga damu ya mnyama”. Hii ilikuwa inaelekeza mbele kwa Bwana Yesu Kristo ambaye damu yake ilimwagika pale msabani.

Wakati tunapobatizwa sisi tunamvaa Kristo (Wagalatia. 3:27) na dhambi zetu husamehewa. Hapana shaka Habili alifahamu hili vizuri kuliko Kaini. “Kwa imani Habili alitoa dhabihu iliyo bora zaidi kuliko Kaini”(Waebrania  11:4) alijua kwamba dhabihu ya mwanakondoo ilielekeza mbele kwa “Mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya Ulimwengu”(Yoh 1:29) Mungu hapendi mtu yeyote afe milele bali wote tuokolewe kupitia mwana wake Bwana Yesu Kristo.

MASWALI

Majibu Mafupi

1. Ni majina gani ya wana wawili wa Adamu na Hawa?

2. Kaini alikuwa akifanya kazi gani?

3. Habili alikuwa akifanya kazi gani?

4. Kaini alimtoalea nini Mungu?

5. Habili alimtolea nini Mungu ?

6. Ni sadaka ya nani ilikubaliwa na Mungu ?

7. Mwana aliyezaliwa badala ya Habili jina lake aliitwa nani?

Majibu ya Kina

1. Kwa nini Kaini alimwua Habili?

2. (a) Kwa nini Mungu hakupendezwa na sadaka iliyotolewa na Kaini?

    (b) Kaini ilimpasa afanye nini?

3.   Eleza Kaini alimfanya nini Habili na jinsi Mungu alivyomwadhibu Kaini.

Majibu ya Nyongeza

4. Ni kwa nini dhabihu ya Habili ilikuwa bora kuliko ya Kaini?

 

Swahili Title
004 WALIPOKARIBIA KUMALIZA SAFARI - NYOKA ZA MOTO.
English files
Swahili file
African text
CSSA
Translator 1
Jonathan Nkombe
Literature type
Sub type
Sub sub type