CSSA 1-5-12 - PAUL AND BARNABAS PREACH AT ANTIOCH

Swahili

112. PAULO NA BARNABA WANAHUBIRI ANTIOKIA

''Tazama, tunawageukia Mataifa''

 

Shabaha

 Kuonyesha jinsi Injili ilivyohubiriwa Antiokia na Pisidia; Wayahudi walipoikataa lakini watu wa Mataifa wakaipokea kwa furaha. Paulo, Barnaba na Yohana Marko waliondoka Cyprasi na wakaenda mji wa Perge. Hapa Yohana Marko aliondoka na kurejea Yerusalemu. Lakini Paulo aliugua sana alipokuwa eneo hili. Na bila shaka baadhi yetu wangeamua kurudi nyumbani, kwa kufikiria kuwa Mungu asingeruhusu tuendelee kuhubiri ikiwa tunaumwa kama vile alivyoungua Paulo, lakini Paulo hakuweza kufikiria hivyo na hivyo hakurudi nyumbani. Paulo aliitwa na Roho Mtakatifu kuhubiri (Matendo ya Mitume 13:2) na kwa hiyo alithibisha kwa kuendelea kuwa mwaminifu kufanya kazi ambayo Mungu alimwitia. Ni kwa jinsi gani fundisho hili lilivyo la maana sana kwetu kufuata! Kwa kutoka Perge walisafiri km 160 kuelekea mji wa Antiokia. Safari yao ilikuwa ni ya kupita barabara iliyokuwa inapitia sehemu za milima ambazo zilikuwa ni za hatari sana kwa kuwa yalikuwa ni maeneo mazuri sana kwa majambazi au wanyang'anyi kuweza kujificha.

 

Matendo ya Mitume 13:14-52

 

PAULO ANAHUBIRI ANTIOKIA KATIKA MJI WA PISIDIA (mstari 14-15)

Katika Biblia Antiokia zinazotajwa ni mbili:- Antiokia iliyo katika Syria, ni mji ambao ndipo Paulo na Barnaba walimalizia safari yao hapo, na Antiokia ambayo tunaisoma sasa, Antiokia katika Pisidia; ziangalie katika Atlasi ya Biblia yako ili usije kuzichanganya katika akili yako. Wakati Paulo na Barnaba walipofika Antiokia waliingia katika sinagogi siku ya Sabato, kama ilivyokuwa desturi yao, wakaketi. Na baada ya kusomwa Torati na Chuo cha Manabii, wakuu wa sinagogi walitambua kuwa kuna wageni ndani na hivyo wakawaambia, “Ndugu, kama mkiwa na neno la kuwafaa watu hawa, lisemeni”.

 

PAULO ANALIHUTUBIA SINAGOGI (mstari 16-41)

Na hivi ndivyo Paulo alivyokuwa anataka, nafasi ya kuwaambia watu kweli kuhusu Yesu Kristo. Paulo aliposimama mbele ya watu waliokuwa wamekusanyika, alisema, “Enyi waume wa Israeli, nanyi mnaomcha Mungu sikilizeni”. Paulo aliwaambia wayasikilize kwa makini maneno yale atakayoyasema, kwa maana alikuwa anakwenda kuwaonyesha katika Maandiko yao kwamba Yesu wa Nazareti alikuwa kweli ndiye Kristo, Masihi wa Israeli. Paulo akaendelea taratibu kuonyesha sehemu za Maandiko Matakatifu katika Agano Jipya na akathibitisha kwamba Mungu aliahidi kuja kwa mtu mmoja ambaye huyo kwa ajili ya angeondoa dhambi za watu wa Israeli na kuwapatia matumaini ya uzima wa milele. “Basi, na ijulikane kwenu, ndugu zangu, ya kuwa kwa huyo mnahubiriwa msamaha wa dhambi” (mstari 38). Na njia hii iliwezekana tu kwa sababu Mungu alimfufua kutoka kwa wafu. Hii ilikuwa ni habari hakika kwa mtu yeyote aliyependa kusikiliza. Paulo akamalizia hotuba yake, kwa kuwaonya watu wanaodharau na kukataa maneno yake kuhusu Yesu-au vinginevyo watajiletea ghadhabu hukumu ya Mungu juu yao (mstari 38).

 

WENGINE WAKAPENDA KUSIKIA INJILI (mstari 42 – 43)

 Ndani ya Sinagogi walikuwemo Wayahudi na Waproseliti (Waproseliti walikuwa watu wa Mataifa waliomini katika imani ya kumwabudu Mungu wa Israeli) watu walipokuwa wakitoka ndani ya Sinagogi, wengi kati yao waliomsikiliza Paulo walimwomba kuzungumza nao katika juma ambalo lingefuata.Walipendezwa mno, hata wakaona kwamba hawangengojea hadi sabato nyingine ambayo ingefuata kumsikiliza zaidi. Wengine walimfuata Paulo na Barnaba mpaka walikukokuwa wakiishi, nao wale ndugu wawili walivyoendelea kuwafundisha wale watu wakaamini kwamba waliyosikia yalikuwa ni ya kweli.

 

WAYAHUDI WAKAJAA WIVU (mstari 44 - 45)

 Katika juma lile, habari ya ujumbe aliokuwa akifundisha Paulo ikasambaa upesi, sabato iliyofuata karibu mji mzima wakakusanyika kulisikia Neno la Mungu. Wayahudi walipowaona makutano waliokuja kusikia, wakajaa wivu sana na kuyakanusha maneno yale aliyoyasema Paulo. Walimpinga na kumtukana maana yake, walisema mambo ya uwongo na wakasema matusi mengi katika mambo yanayohusu Yesu, kama vile Wayahudi walivyompinga Yesu wakati walipokuwa wakimsulibisha. Wivu mara nyingi unasababisha watu kutenda mambo bila kufikiri. Hapa Wayahudi waliyaziba masikio yao waisikie kweli na hata kuipinga, kwa sababu tu walimwonea Paulo wivu.

 

“ANGALIENI, TWAWAGEUKIA MATAIFA” (mstari 46 – 52)

Paulo na Barnaba kwa ujasiri waliwageukia Wayahudi wakasema, “Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza; lakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, na kujiona nafsi zenu kuwa hamkustahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia Mataifa” (mstari 46). Jinsi gani walivyokuwa wapumbavu, kwa kuwa siyo tu kwamba walikataa kusikiliza neno la Mungu bali pia walipoteza matumani yote ya uzima wa milele. Lakini watu wa Mataifa walifurahi na kumtukuza Mungu. Wakafurahia sana ajabu la Injili, hata ikawa neno la Bwana likaezwa kila mahali katika eneo la Antiokia. Na kwa kadri watu wa Mataifa walivyozidi kuamini zaidi na zaidi, uadui wa Wayahudi nao ukaongezeka. Wakawachochea wanaume na wanawake ambao walikuwa ni viongozi katika mji na kusababisha ghasia hata Paulo na Barnaba wakafanyiwa fujo, na hatimaye waliwafukuza na wakawatoa katika mipaka ya wilaya yao. Mitume wakakung’uta mavumbi ya Antiokia yaliyokuwa miguuni mwao na kwenda zao (linganisha na Mathayo 10:14). Waliwaacha wanafunzi nyuma yao waliojaa furaha kwa sababu walikuwa wamepata ile Kweli na walikuwa wamepewa Roho Mtakatifu (mstari 52).

 

FUNDISHO KWETU

 Tunaona jinsi Paulo haraka alivyochukua jukumu la kuwaeleza watu Injili. Hata wakati wayahudi walipompinga, aliendelea kutangaza ile Kweli, kwani aliielewa nguvu ya Neno la Mungu. Alifahamu kwamba kama watu wangekuja kwa uaminifu wa moyo mzuri wa kusikia na kufikiria Neno la Mungu, wangeliamini. Hatahivyo, kila mara, wapo wale ambao, kutokana na wivu na ugumu wa moyo, siyo tu kwamba wanakataa kulisikiliza Neno la Mungu, bali pia wanajalibu kuwazuia watu wengine wasilisikilize pia. Na tuwe tayari kuisema Kweli kama Paulo alivyofanya, bila kujali watu wanasema nini, Mungu atatubariki. Ni shukurani iliyoje tunayokuwa nayo Mungu kwa ajili ya kuhubiri watu wa Mataifa, kwa maana hivi ndivyo ile Kweli ilivyokuja kwetu, ambao siyo Wayahudi kwa kuzaliwa.

 

MAELEZO ZAIDI

Soma Matendo ya Mitume 13:46 kwa uangalifu. Paulo anasema kuwa ilikuwa ni lazima Neno la Mungu lihubiriwe kwa Wayahudi kwanza. Mungu alikuwa anawapatia wayahudi, waliomsulibisha Yesu nafasi ya mwisho ili watubu na kumwamini. Huu ndiyo uliokuwa ujumbe wa Petro katika siku ya Pentekoste (soma Matendo ya Mitume 2:36-38). Pia, wakati Petro alipomponya yule kiwete, aliwaambia Wayahudi. “Basi sasa ndugu, ninajua kuwa mliyatenda haya kwa kutokujua kwenu, kama na wakuu wenu walivyotenda ... Tubuni basi, mrejee” (Matendo ya Mitume 3:17-19). Jinsi gani rehema ya Mungu ilivyokuwa nzuri sana kwao! Machoni pa Mungu walikuwa “wapendwa kwa ajili ya baba zao” (Warumi 11:28); hii ni kwa sababu Mungu alimpenda Ibrahimu, Isaka na Yakobo, aliwapenda Wayahudi waliokuwa uzao wao, na aliwataka Waisraeli wawe waaminifu kama baba zao. Wayahudi wengi waliamini, lakini wengi zaidi walikuwa na chuki sana na wakaongeza dhambi zao juu yao kwa kumwua Stefano (Matendo ya Mitume7). Katika somo lililopita tuliona jinsi Barnaba na Paulo walivyotumwa kwenda nchi za mbali kuhubiri Injili, ambapo Paulo anatuambia kuwa ni “Uweza wa Mungu uletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani (Watu wa Mataifa) pia” (Warumi 11:16). Kila wakati walikwenda kwenye sinagogi kwanza ili kuwahubiri Wayahudi (mfano Matendo ya Mitume 13:5,14). Na sasa tunamwona Paulo akiyasoma maandiko ya Agano la Kale (Matendo ya Mitume 13:47) imenukuliwa kutoka Isaya 49:6 kuthibitisha kuwa Mungu kila wakati alikusudia kwamba Mataifa watapewa tumaini moja la wokovu (angalia pia Maelezo ya Nyongeza, Somo la 9). Hukumu, ambayo inahusu onyo la Bwana Yesu kuhusu Wayahudi wasioamini (Luka 21: 6,20-24), hatimaye ilikuja kuwapata mwaka 70 KK, wakati mjii wa Yerusalemu ulipoangamizwa na Wayahudi wakatawanyika ulimwenguni kote.

 

MASWALI

Majibu Mafupi

  1. Paulo na Barnaba walifanya nini katika sabato ya kwanza walipokuwa kabisa kule Antiokia katika Pisidia kwa mara ya kwanza?
  2. Katika Hotuba ya Paulo, alikuwa anataka kuwafundisha nini kutokana na Maandiko yao wenyewe?
  3. Je, Paulo alisema kuwa ilikuwa ni nini “kwa mtu huyo walihubiriwa?”
  4. Ni nani aliyekuwa ndani ya Sinagogi akimsikiliza Paulo?
  5. Ni jinsi gani Wayahudi walivyohisi walipowaona makutano siku ya sabato iliyofuata?
  6. Wayahudi walifanya nini wakati Paulo alipokuwa akisema?
  7. Paulo alisema ni nani ambaye alikuwa alimewahukumu Wayahudi huko Antiokia kwamba hawakustahili

      uzima wa milele?

  1. Ni nani waliipokea Injili kwa furaha huko Antiokia?

 

Majibu ya Kina

  1. Katika hotuba ya Paulo ndani ya Sinagogi huko Antiokia, katika Pisidia Paulo alisoma maandiko ya Agano

      la Kale.

  1. Alikuwa akiwaambia habari ya nani?
  2. Habari njema ilikuwa nini?
  3. Nini kingelitokea ikiwa wangedharau maneno haya?
  1. Eleza yaliyotokea huko Antiokia katika Pisidia siku ya sabato iliyofuata.

 

Majibu ya Nyongeza

  1. a) Ni lipi lilikuwa jibu la ujasiri la Paulo kwa Wayahudi wa Antiokia huko Pisidia?

b) Kwa ufupi sema maneno haya yana maana gani?

 

 

 

 

Swahili Title
112 PAULO NA BARNABA WANAHUBIRI ANTIOKIA
English files
Swahili file
PDF file
Literature type
Sub type
Sub sub type