CSSA 2-2-02 - THE CREATION OF THE HEAVEN AND THE EARTH

Swahili

152. MAJASUSI 12 KATIKA NCHI

“Na sisi wenyewe tulikuwa kama panzi”

Hatimaye watu walifika Parani na kisha Kadeshi, kusini mwa Nchi ya Ahadi. Kadeshi ilikuwa chemichemi katika nyikakali, kwa hiyo walipofika mahali hapa waliona tofauti kubwa na mandhari ya ukame waliyopitia (Yeremia 2:6-7).

Sasa walikuwa wamepiga kambi kwenye mpaka wa Nchi. Musa aliwahimiza sana “Tazama, BWANA, Mungu wako, ameiweka nchi mbele yako; haya panda, itamalaki, kama BWANA, Mungu wa baba zako, alivyokuambia; usiogope wala usifadhaike.” (Kumb. 1:21).

Watu walionyesha ukosefu wa imani kwa kumwomba Musa awatume wapelelezi (m. 22). Hiihaikuwa nia ya Mungu lakinialiruhusu na kumwagiza Musa ipasavyo(Hesabu 13:1-2). Matokeo yaombi hilo ni vifovya Waisraeli wengi, muda mfupi tu baada ya wapelelezi kurudi na kuchelewesha urithi wao wa nchi kwa miaka 38 zaidi.

Hesabu 13 & 14; Kumbukumbu la Torati 1:19-46

NCHI ILIYOPELELEZWA

Wale wapelelezi kumi na wawili walitumia siku 40 kuipeleleza Nchi. Waliikuta kama vile Mungu alivyokuwa ameielezea, “ikitiririka maziwa na asali” (Kutoka 3:8). Kwa hiyo, Nchi ilikuwa na neema sana jambo lililosababisha watu wawili kubeba kishada cha zabibu kutoka katika kijito (Bonde) cha Eshkoli. Hili lilikuwa ni eneo karibu na Hebroni ambapo, katika miaka ya awali, Abrahamu aliishi (Mwanzo 13:18; 14:13). Matunda mengine pia yaliletwa ili kuonyesha rutuba ya nchi.

TAARIFA YA UOVU WA MAJASUSI.

Wapelelezi walirudi baada ya siku 40 na kusema, “nchi inatiririka maziwa na asali... LAKINI”. Kisha wakaendelea kutoa taarifa ambayo iliwazuia watu wasiingie kuimiliki. Ilikuwa ni “habari mbaya” ambayo “waliizua” (Hesabu 13:32) kwa maana ilipuuza hali nzuri ya nchi na ilisisitiza matatizo ya “miji yenye kuta”, “majitu”, “watu wenye nguvu” kwa namnaambayo iliwakatisha tamaa Israeli. Kulikuwa na wapelelezi 10 ambao walidumisha msimamo huu kwa nguvu. Hawakuwa na imani kabisa na hawakujali shughuli za Mungu na watu wake na walikuwa wamesahau upendo wake kwao.

MAJASUSI WAWILI WAAMINIFU.

Ni Kalebu na Yoshua pekee ndiyo waliokuwa tayari kusimama dhidi ya taarifa hii mbaya na kuwatia moyo watuwainuke. Walikuwa wamevutiwa na kile walichokiona na kutambua thamani halisi ya ardhi hiyo. Walikuwa na shauku ya kuimiliki na walitiwa moyo sana na kujua kwamba kulikuwa na hofu ya Israeli katika mioyo ya wakazi. Waliwaambia watu kwamba, Wakanani “ni mkate wetu; ulinzi wao umewaacha na Yahwe yu pamoja nasi.” Kalebu na Yoshua walionyesha imani kwaMungu; hiyo ni? Waliamini ahadi za Mungu kwamba angewapa nchi, na walitaka watu wairithi. Imani ni nini basi? Ni kutazamia kwa ujasiri mambo yatarajiwayo: kukubalika kwa mambo yasiyoonekana (cf. Waebrania 11:1): na usadikisho kamili kwamba kile Mungu anachoahidi ana uwezo wa kufanya (Warumi 4:21).

 

 

MUSA APATANISHA WATU.

Mwitikio wa watu kwa ujumbe wa Kalebu na Yoshua ulikuwa ni kuchukua mawe ili kuwaua. Walitafuta kutetea ukosefu wao wa imani kwa kusema kwamba walikuwa wakiwafikiria wake na watoto wao tu. Huu ulikuwa ni uongo lakini walikuwa wamejidanganya kwa kudhani ni kweli.

Ghafla Mungu aliwatuliza watu kwa kufunua utukufu wake juu na ndani ya Hema. Alimwambia Musa kwamba alikuwa akifikiria kuwaangamiza wanung’unikaji wote na kuunda taifa jipya kutoka kwake.

Mwitikio wa Musa ulikuwa wa haraka. Alikuwa na wasiwasi kwa sababu mbili:

  1. Jina la Mungu lingeweza kushushwa mbele ya macho ya mataifa yaliyozunguka;
  2. Hakutaka watu waangamizwe. Ingawa walikuwa wadhambi, alikuwa na hisia ya kuwajibika kwao.

Hakujitafutia umaarufu bali alifikiria tu wengine na hasa kuhusu Mungu. Akiwa amejawa na huruma kwa watu wake aliomba kwa ajili ya maisha yao (Hesabu 14:17-19). Msingi wa ombi lake ni kuheshimiwa kwa jina la Mungu mwenyewe (mst. 18). Je, Yahwe hangekuwa mwenye rehema na mvumilivu kama vile alivyojibainisha (Kutoka 34:6-8)?

Bila shaka alijawa na furaha na amani alipomsikia Mungu akisema, “Nimewasamehe...” (Hesabu 14:20). Lakini, kabla Mungu hajamaliza kile alichokuwa akisema, Musa alitambua kwamba Mungu “hatawaondolea hatia hata kidogo” (m. 18) “Kwa maana” Mungu alikiambia kizazi kile, “mizoga yenu itaanguka jangwani” (Mst. 28 na 29).

VIAPO VIWILI.

Hesabu 14 inarekodi viapo viwili vilivyoapishwa na Mungu. Kiapo cha Mungu ni cha kudumu: hakuna kinachoweza kukibadilisha. Kwa hiyo, Mungu alipoapa kwa uwepo wake mwenyewe, kwamba ataijaza dunia utukufu wake (Hesabu 14:21) Musa angefurahi kwa maana alijua kwamba utukufu wa Mungu uliohusishakujifunua tabia yake ya haki ndani ya watu. Hatimaye jamii ya watu ingeishi duniani, ambao wote wangeakisi tabia ya kimungu, jina na utukufu katika kila namna:

kiakili—katika kumjua Mungu;

kimaadili—katika ushirika wao na Mungu;

kimwili—katika asili yao—ya kimungu na isiyoweza kuharibika kama ya Mungu.

Musa aliona katika msamaha wa Mungu (mst. 20) kwamba kusudi la Mungu la kuendeleza jamii hii ya watu kupitia taifa la Israeli lingebaki bila kubadilika. Lakini, Mungu aliweka wazi kabisa kwamba ingawa alikuwa amelisamehe taifa hilo, watu wenye hatia ndani yake wangeadhibiwa.

Kwa hiyo, aliapa kwa kiapo cha pili kwamba wale wote wenye umri wa zaidi ya miaka 20 wangefia nyikani. Katika ghadhabu yake kizazi kizima zaidi ya miaka 20 hakingeingia katika nchi ya ahadi (Zab. 95:8-11; Ebr. 3:16-18).

Musa angehuzunishwa sana na jambo hili, lakini aliona ndani yake haki ya Mungu. Pia, kwa sababu ilithibitishwa kwa kiapo hakuwahi tena kuwaombea watu wake kwa maana neno la Mungu lingesimama.

 

TAIFA LILIADHIBIWA.

Walihukumiwa na Mungu kutangatanga miaka 40 nyikani (miaka 2 ilikuwa tayari imeshapita) hadi wale wote wenye umri wa zaidi ya miaka 20 walipokufa - mwaka kwa kila siku wapelelezi walikuwa katika nchi. Hiyo ni picha ya kuhuzunisha kama nini—hebu fikiri marudio ya watu hao wote kufa, siku baada ya siku, mpaka kizazi kizima kiangamie!

Watoto wao, waliosema “watakuwa mateka” (Hesabu 14:3), ndio wangerithi nchi. Mwitikio wao kwa hili ulikuwa mbaya kama vile mwenendo wa wengine ulivyokuwa.

Walipuuza kauli ya Mungu ya “geuka, nenda jangwani kwa njia ya Bahari ya Shamu” (Hesabu 14:25). Badala yake, walichukua mapanga yao na kujaribu kuteka nchi (Hesabu 14:40; Kumb. 1:41). Licha ya maonyo ya Musa, walipanda dhidi ya Waamori waliokuwa kusini mwa nchi na wakashindwa, na wengi wakafa.

Ni watu wawili tu wa kundi hilo kubwa la watu (wenye umri wa zaidi ya miaka 20) wangeingia nchini—Kalebu na Yoshua. Wangelipwa kwa imani yao. Adhabu ya papo hapo ilitolewa kwa wale wapelelezi 10 wasio waaminifu ambao “walikufa kwa tauni mbele za Bwana” (Hesabu 14:37).

FUNZOKWETU:

Ni lazima tuamini bila shaka ahadi za Mungu kuhusu Ufalme na tusivunjwe moyo na matatizo tunayokabiliana nayo siku baada ya siku. Tazamio la Utukufu wa Mungu kuijaza dunia linapaswa kutufurahisha na linapaswa kututia moyo kutazamia siku ya ujiowa Kristo. Tunapaswa pia kufikiria kwa makini kuhusu ukali wa hukumu za Mungu juu ya watu wake walipoasi au kutotii kama inavyoonekana katika kutengwa kwao na Nchi ya Ahadi.

Linganisha Somo la Mkufunzi Na. 14.

MAKTABA YA MAREJEO:

“Mkono wa Mungu Unaoonekana” (R. Roberts) Sura ya 17

“Mahali ilipotokea” (Islip Collyer) Sura ya 6

“Hadithi ya Biblia” (H. P. Mansfield) — Kitabu 2 Kurasa 71-80

“Musa Mtumishi Wangu” (H. Tennant) — Kurasa. 115-125

AYA ZA MASWALI:

  1.  
    1. Ni ripoti gani “mbaya” ya wale wapelelezi 10 wasio na imani?
    2. Ripoti nzuri ya Yoshua na Kalebu ni ipi?
  2. Imani ni nini?
  3. Eleza jinsi Musa alivyosihi kwa ajili ya watu wa Israeli Mungu aliposema angewaangamiza kwa sababu ya kusitasita kuingia katika Nchi ya Ahadi.
  4. Eleza viapo viwili vya Yahwe kama vilivyoandikwa katika Hesabu 14 na uonyeshe jinsi viapo hivyo vitatimizwa au vitakavyotimizwa.

 

MASWALI YA INSHA:

  1. Yoshua na Kalebu waliripoti kwa uaminifu wema wa nchi ya ahadi. Tofauti na wapelelezi wengine na watu, onyesha jinsi na kwa nini walikuwa waaminifu.
  2. Kwa nini Mungu aliwahukumu Israeli kutangatanga kwa miaka arobaini jangwani? Katika jibu lako eleza viapo viwili ambavyo Yahwe alivitoa wakati huo.

 

Swahili Title
152. WAJASUSI 12 KATIKA NCHI
African text
CSSA
Translator 1
Carl Hinton
Translator 2
Jacob Haule
Literature type
Sub type
Sub sub type