CSSA 2-3-11 - ELIJAH AND ELISHA

Swahili

186. ELIYA NA ELISHA

"Roho ya Eliya inakaa juu ya Elisha"

 

Wakati wa enzi ya utawala wa Ahabu, matendo ya Israeli yalistahili hukumu ya Mungu, naye nabii Eliya ndiye aliyekuwa kusudi la huduma kwa mfalme mwovu na taifa lililoasi. Hata hivyo Eliya alihitaji kufundishwa kuwa kazi ya Mungu haihitaji tu kuhukumu waovu na kuharibu ibada ya sanamu, bali pia elimu ilitakiwa ili kuwaimarisha wanaume na wanawake katika njia ya Mungu. Ilikuwani kwa ajili ya hali hii ya kuwatia moyo na kuwajenga mabaki ya waaminifu waliokuwa wamesalia ambao ndiyo uliokuwa msingi wa huduma ya rehema ya Elisha.Tukiziangalia kwa pamoja, kazi za hawa manabii wawili wakubwa wenye nguvu zionatupatia picha ya kupendeza ya tabia kamilifu ya BWANA. Na sisi kazi zetu zinatakiwe zidhihirishe tabia ya aina hii.

1 Wafalme 19 na 2 Wafalme 20

 

ELIYA NA SAUTI NDOGO YA UTULIVU

Juu ya Mlima Karmeli mbele ya kusanyiko la wa Israeli ambao walikuwa watazamaji, mfalme na kundi la manabii waongo wamwaduo Baari, Eliya aliweza kuwashinda kwa kuwathibitishia kuwa BWANA pekee ndiye alikuwa Mungu aliye hai na wa kweli. Lakini Eliya aliikimbia hasira kuu ya Yezebeli (1 Wafalme 19:1-3), wakati Ahabu, mfalme akitazama tu bila kujali. Katika hali ya namna hii Elihuzunika kiasi cha kumkatisha tamaa, alitambua kuwa maisha yake yalikuwa hatarini kwa ajili ya kusimama katika Kweli, na hata aliamini kuwa yeye peke yake ndiye mtumishi wa BWANA aliyekuwa amebakia katika Israeli (1 Wafalme 19:9-10). Uthibitisho wa Mungu ulimhakikishia kuwa Mungu hutenda kazi na watu wale waliotayari kuzifuata njia zake (linganisha 1 Wafalme 19 :10-12; Ayubu 4 :16), kwa maana walikuwepo pia watu 7000 katika Israeli waliokuwa wamejitenga na hawakumwabudu Baari (mstari 18). Eliya alinyenyekezwa na yale ambayo Mungu alimwonyesha kule juu ya Mlima Horebu. Na kisha Mungu alimwamuru Eliya arudi na afanye kazi 3:

 

1. Alitakiwa ampake mafuta Hazaeli ili awe mfalme wa Syria.

2. Alitakiwa ampake mafuta Yehu ili awe mfalme wa Israeli.

3. Alitakiwa ampake mafuta Elisha ili awe nabii badala yake (mstari 7-18 ).

 

ELISHA ANAMBADILI ELIYA – 1 Wafalme 19:19-21

Ni amri ya tatu peke yake iliyotekelezwa na Eliya,zile mbili zingine zilitekelezwa na Elisha. Eliya akarudi kutoka Mlima Horebu na kumkuta Elisha mwana wa Shafati akilima shamba. Eliya akalitupa vazi lake juu ya Elisha, ikionyesha kuwa Mungu alitaka awe nabii badala yake. Elisha "Naye akawaacha ng`ombe, akamfuata Eliya mbio, akasema nipe ruhusa, nakuomba, nikambusu baba yangu na mama yangu na kisha nitakufuata" (mstari 20). Kwa hiyo Elisha kwa hiari akajitenga na njia ya maisha yake ya zamani na "akainuka akamfuata Eliya, na akamhudumia" (mstari 21).

 

Na wakati wa miaka miachache iliyofuata Eliya na Elisha walitumia muda wao mwingi wakitengeneza tena shule ya manabii ambayo Yezebeli alijaribu kuiangamiza. Watu walikusanyika pamoja na kujifunza mapenzi ya Mungu chini ya Eliya. Ile sauti ndogo ya utulivu ya neno la Mungu ilikuwa ikijenga pole pole kundi la wanaume na wanawake ili waweze kuwa kituo cha nguvu katika taifa. Katika madarasa yetu, sisi pia tunaweza kukusanyika pamoja na wengine wenye imani ya thamani ili kuendelea kuisikia ile sauti ndogo ya utulivu ya Neno la Mungu.Tunaweza kwa jinsi hiyo kumtukuza Mungu katika mafundisho yetu na katika kutafakari na hivyo kuwa mfano mzuri wa waumini wanaolipenda neno la Mungu na kuzitii amri zake.

 

ELIYA ANACHUKULIWA MBINGUNI - 2 Wafalme 2

Wakati walipokuwa wakisafiri pamoja kutoka Gilgali, Eliya akamwambia Elisha abaki mahali fulani kwa sababu Mungu alimwagiza yeye kwenda Betheli. Elisha akakataa kumwacha Eliya, kwa hiyo wakaenda pamoja wote wawili. Na kule Betheli, wana wana manabii wakaja kwa Elisha wakamwuliza iwapo alifahamu kuwa Mungu atamchukua Eliya siku ile. Na baada ya tukio hili, tukio kama hili lilitokea mara mbili, mara moja walipokuwa wanasafiri kuelekea Yeriko na tena likatokea walipokuwa wakisafiri kuelekea Yordani lakini ikawa kabla Elisha hajakataa kuachana na bwana wake. Walipofika kwenye ukingo wa mto Yordani, Eliya akayapiga maji kwa shuka lake, ambalo lilisababisha maji ya mto kugawanyika. Walipovuka mto, Eliya akamwambia Elisha amwombe kitu kimoja ambacho angependa yeye amfunyie kabla hajaondoka, naye Elisha akasema " Nakuomba, sehemu mara dufu ya roho yako na iwe juu yangu". Hakuwa na maana kuwa alitaka nguvu ya Eliya mara mbili, bali alikuwa akiomba kuwa ndiye awe mrithi wa huduma ya Eliya (kutokana na inaonekana katika lugha ya asili ya Kiebrania). Ingawa Elisha alikuwa ameomba "neno gumu" (kwa sababu ni Mungu ambaye angeweza kumkubalia ombi la aina hiyo) alihakikishiwa na Eliya kuwa anepokea kwa sharti ikiwa kama atamwona wakati akiondoka. Na baada ya muda mfupi watu hawa wawili wakatenganisha na gari lililokuwa likiwaka moto mkali, na Eliya akachukuliwa juu katika mawingu kwa upepo wa kusulisuli asiweze kuonekana. Nabii mkubwa Eliya akawa amemaliza kazi yake - na sasa ilikuwa ni zamu ya Elisha, "mtu wa Mungu", akianza kazi kuanzia pale bwana wake alipoishia.

 

KAZI YA BAADAYE YA ELIYA - Malaki 4:5-6; Marko 9:11-12

Eliya alichukuliwa wakati alipokuwa katikati ya kazi yake-lakini ataianza tena kazi yake mara nyingine katika siku zinazokuja. Mungu anatuambia sisi katika Malaki 4:5 Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii kabla haijaja siku ile ya BWANA iliyokuu na kuogofya. Wakati wa kuja Kristo mara ya pili, Mungu atamtuma Eliya kwa watu wa Israeli waliotawanyika ulimwenguni kote ili kuwashauri ya kuwa Masihi wao amerudi.

 

YULE MTU ELISHA NA KAZI YAKE

Elisha akaliokota vazi la Eliya lililoanguka na akairudia njia ile ile alikizifuata nyanyo zake, akitafakari kwa mshangao mambo yale aliyoyaona. Je, atakuwa amempokea "sehemu mara dufu" ya roho ya Eliya? Akararua vazi lake mwenyewe katika vipande viwili na kuichukua ile nguo ya Eliya ambayo ilianguka ardhini wakati Eliya alipokuwa akichukuliwa kwenda juu. Wakati akirudi mto Yordani, akachukua ile nguo na kuyapiga maji ya mto kama vile Eliya alivyofanya, akasema "Yuko wapi BWANA, Mungu wa Eliya?" Akijibu kilio chake hiki, Mungu akayagawanya maji ya mto, siyo kwamba vazi lilikuwa na nguvu yoyote, bali ni kwa sababu Elisha alikuwa ameomba mwujiza. Kwa hiyo, kwa ishara hii kubwa ikawa uthibitisho kuwa roho ya Mungu ilikuwa pamoja naye. Elisha akarudi akitembea sehemu iliyokavu mpaka upande wa pili wa mto. Ndipo wana wa manabii waliokuwa wakiangalia, wakasema, "Roho ya Eliya inakaa juu ya Elisha" (2 Wafalme 2:15).

 

Sauti ya Eliya isiyotetemeka, iliyo imara, sauti iliyo makini ambayo iliamuru uamsho, iliyokemea dhambi, iliyotamka hukumu itakayokuja iliwatisha watu wote wa Israeli. Ilifanya kazi na mafundisho ya upole sana, na ilisababisha Elisha kuwa mpole zaidi na mwenye bidii sana. Eliya alifanya miujiza minane katika hudumu yake, ambayo miujiza yake mingi ilizungumzia hukumu, kwa mfano ukame na moto kutoka mbinguni. Na kwa upande mwingine miujiza ya Elisha kumi na sita kimsingi hasa ilizungumzia rehema, uponyaji, wema wa Mungu, kuimarishana katika maisha ya imani na nia ya Mungu ya kuokoa watu wanaomwamini Yeye. Hata hivyo, pale ilipokuwa ni muhimu Elisha hakushindwa kumdhihirisha BWANA kuwa ni Mungu wa hukumu. Katika tukio moja maalumu, mapema katika huduma yake, alipokuwa njia akienda Betheli wakati kundi la vijana (anaglia matumizi ya neno hilo hilo kwa Lugha ya Kiebrania katika Mwanzo 21:12; 41 :12; 1 Wafalme 20 :14) walianza kumdhihaki wakisema, "paa juu, ewe mwenye upara!" Elisha akageuka na kuwaalani kwa jina la BWANA ambapo dubu jike wawili walitokea porini na kuua vijana 42 kati yao. Hapa pana fundisho muhimu sana kwa ajili yetu kwa ajili ya kuwaheshimu wazee; na hasa hasa watumishi wa Mungu katika eklesia. Mungu kamwe hadhihakiwi, na wala neno lake lisifikiriwe kuwa ni jambo dogo sana. Huduma ya Eliya na Elisha ilikuwa ikionyesha hivyo. Mungu atawaonyesha rehema watu wote waliotayari kuegeza mioyo yao imwelekee Yeye, lakini ataleta hukumu kwa watu wote wanaomwacha kwa kuyaacha mapenzi yake na kutomheshimu Mungu.

 

Hakuna mtu yeyote leo aliye na karama ya Mungu ya nguvu za roho mtakatifu kwa ajili ya kutenda miujiza, lakini sisi wote sote tunalo Neno la Mungu tulilopewa kwa uvuvio wa roho ya Mungu (2 Timotheo 3 :16). Yesu alisema mara nyingi kwamba maneno aliyokuwa akiyasema yalikuwa si maneno yake bali yalikuwa maneno ya Mungu (Yohana 12:49,50 ), na katika Yohana 6: 63, alisema, "maneno hayo niliyowaambia, ni roho, tena ni uzima". Hivyo tunaweza, kwa kuliamini neno la Mungu, tunapata katika maandiko miujiza hii na mfano wa watu wengi walio waaminifu, uthibitisho ule ule kwamba Mungu tunayemwabudu ndiye aliye hai na wa Kweli.

 

FUNDISHO KWETU

Mungu alitoa uangalifu na kwa wema maagizo kwa watu wake. Hata siku hizi pia Mungu huwapatia maagizo watu kwa uangalifu kwa ajili yetu; kwa maana amelihifadhi lake kwa ajili yetu sisi wote ili tulitumie. Tumchukue Elisha awe mfano kwetu na wale wana wa manabii ambao walimfuata kwa bidii badala ya Eliya na kujifunza kutoka kwa mtu huyu aliyelisema Neno la Mungu (2 Timotheo 3:14-17). Elisha ingawa alikuwa kijana tu alipoitwa kumfuata Eliya, alifanya hivyo kwa hiari na akajifunza Kweli kwa bidii. Akifikia kuwa mtumishi mwaminifu na akachaguliwa na Mungu kufanya kazi za Eliya. Ingawa sisi pia ni vijana, tunaweza pia kushirikiana kwa hiari na kwa kujifunza kwa bidii Kweli na kutenda kazi kwa ajili ya Kristo (1 Timotheo 4:12-16).

 

MAKTABA REJEA

Mkono wa Mungu usioonekana.

 

MASWALI YA VIFUNGU

1. Je, ni jinsi gani Eliya alivyolitumia fundisho la "sauti ndogo ya utulivu" kwa mafunzo katika Neno la Mungu?

2. Eliya ana kazi ya kufanya siku zinazokuja - ni kazi gani hiyo?

3. Ni ombi gani ambalo Elisha alimwomba Eliya kabla hajachukuliwa katika upepo wa kisulisuli?

4. Je, ni kwa jinsi gani kazi za Eliya na Elisha zilitofautiana?

 

MASWALI YA INSHA

Eleza jinsi Eliya alivyochukuliwa juu na namna "roho ya Eliya ilivyokaa juu ya Elisha".

 

MIUJIZA MINANE YA ELIYA

Na. Mwujiza Rejea Maana yake kiroho

1. Kufunnga mbingu 1 Wafalme 17:1 Ukame wa kiroho (Amosi 8:11).

2. Kuongezeka kwa mafuta 1 Wafalme 17:14 Chakula kwa wacha Mungu wakati wa ukame

3. Kufufuliwa kwa mwana wa mjane 1 Wafalme 17:22,23 Ufufuo.

4. Moto kutoka mbinguni 1 Wafalme 18:38 Uthibitisho wa kuwepo kwa hukumu

5. Mvua 1 Wafalme 18:45 Kumwagwa kwa roho (Yoeli 2:23).

6. Kuangamizwa kwa watu hamsini 2 Wafalme 1: 10. Kukataliwa katika hukumu.

7. Kuangamizwa kwa watu hamsini 2 Wafalme 1:12. Kukataliwa katika hukumu.

8. Maji kugawanyika 2 Wafalme 2: 8 Mamlaka juu ya maji ambayo ni mfano (linganisha ufufuo 17:15).

 

MIUJIZA KUMI NA SITA YA ELISHA

Na.Mwujiza Rejea Maana yake kiroho

1. Maji kugawanyika 2 Wafalme 2:14 Nguo ya Eliya kuwa juu ya Elisha.

2. Kuponywa kwa maji 2 Wafalme 2:21 Uponyaji kwa njia ya "agano la chumvi" (Mambo ya Walawi 2:13; Hesabu 18:19).

3. Wenye mzaha kuangamizwa na dubu 2 Wafalme 2:24 Adhabu kwa watu wote wafanyao mzaha na kumkataa

Mungu.

  1. Maji katika nchi kame 2 Wafalme 3:20 Mungu anatosheleza mahitaji katika dunia kame.

  2. Mafuta kwa ajili ya mjane 2 Wafalme 4:1 Neno la Mungu hutolewa bila kipimo ili kuwalisha wote wanaomwamini Mungu.

  3. Zawadi ya mwana wa kiume 2 Wafalme 4:16 Utumishi wa upendo huzaa mzao atokaye kwa Mungu.

  4. Kufufuka kwa mwana 2 Wafalme 4:35 Kufufuka kwa uzao uliotoka kwa Mungu.

  5. Kuponya chakula 2 Wafalme 4:41 Kuongezeka kwa chakula kilicholetwa na Mungu husababisha "kifo sufuriani", lakini huridhika kwa "mkate wa kila siku" uletao afya.

  6. Mkate kuongezeka 2 Wafalme 4 :43 Hata katikati ya ukame Mungu, Mungu ataleta "mkate wa uzima" kwa watu wote wanaomwendea Yeye.

10. Kuponyw kwa Naamani 2 Wafalme 5:10 Kuamini na kuzikwa katika maji kusafisha dhambi na huongoza katika maisha mapya.

11. Kupigwa kwa Gehazi 2 Wafalme 5:27 Kutamani mali ya dunia ni kujiletea hukumu ya Mungu.

12. Shoka kuelea 2 Wafalme 6:6 Wale wanaopotea (chuma) wanaweza kupatikana kwa kuamini msalaba (mti uliokatwa na kutupwa majini).

13. Kuona kwa kipofu 2 Wafalme 6:17 Imani huwawezesha watu kuona jinsi Mungu anaavyowapatia mahitaji yao.

14. Waashuru kupigwa upofu 2 Wafalme 6:18 Ulinzi ule ule wa Mungu hufanya kazi ya kuwalinda watu wa Mungu dhidi ya wale ambao wangewadhuru.

15. Kurejeshewa kuona tena 2 Wafalme 6:20 ni pale ambapo tunakuwa mateka wa Mungu ndipo vita vinapokwisha nasi tunapata amani ya kweli.

16. Uzima kupitia kifo 2 Wafalme 13:21 Yesu Kristo "kwa njia ya kifo, alimharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti" (Waebrania 2:14) na kwa kukutana naye husababisha ufufuo.

 

Swahili Title
186 ELIYA NA ELISHA
English files
Swahili file
Literature type
Sub type
Sub sub type