201 - Ubatizo wa kujaribiwa kwa Yesu
“Kubali hivi sasa, kwa kuwa ndivyo itapasavyo kuitimiza haki yote”. Baada ya kutimiza umri wa miaka 30, ulikuwa wakati kwa Yesu kuanza kazi ambayo kwayo baba yake wa mbinguni alikuwa amemuandaa. Yohana binamu yake alikuwa tayari akihubiri ukingoni mwa Yordani. Alikuwa ndiye “sauti inayolia jangwani” Yohana alielezea ujilio wa Masihi akimwahutubia watu kumrudia Mungu. Yesu alipokuja Bethasania ambako Yohana alikuwa akibatiza ilidhihirika kwa Yohana kwamba huyu ni Masihi ambaye kuja kwake alikuwa akimhubiria. Mathayo 3: 3:1-11
Ujumbe wa Yohana na mwito wa toba (mathayo 3:1-12)
Katika siku ambapo Yohana mbatizaji alianza utumishi ake taifa la
Wasadukayo, Wafarisayo, Waandishi na wanasheria walionyesha kana kwamba walikuwa wanadini wazito, lakini klwa ujumla, ilikuwa yote muonekana wa nje. Yohana alisema waziwazi juu ya msimamo wao. Maneno yake ya nguvu yaliamsha hisia za watu wengi nao wakenda ukingoni mwa Yordani kumsikiliza.aliwaita wote kutubu na kujitoa wenyewe kwa Mungu wakati muda ulikuwepo bado, kwani, alionya siku ya hukumu ilikaribia . Luka 3:9; Malaki 3:2.
Yohana alikuwa ndiye mtangulizi wa Masihi, kwa kuwa hivyo ndivyo, kiini cha mahubiri yake ikimhusu aliye mkuu mwenye nguvu kuliko yeye mwenyewe. Ujumbe wake ulitoka kwa Isaya 40:3-8. alikuwa “sauti aliaye jangwani, tengenezeni njia ya Bwana”(Mathayo 3:3). Aliwaita wau kuona ya kwamba “mwili wote ni manyasi na uzuri wote uliopo ni kama
Ubatizo wa Yesu (Mathayo 3:3-15)
Siku moja wakati Yohana akibatiza Yodani Yesu alitembea katikati ya makundi na kujitokeza mbele yake. Ingawaje ahielekei kuwa Yohana alimfahamu binamu yake kwa uso Yesu aliishi Nazarethi na Yohana alitumia maisha yake nyikani (Luka 1:80), alielewa ya kwamba hapa palikuwa na mtu asiye wa kawaida akisimama mbele yake. Yohana alipotazama usowa mwana wa Mungu akaanza kujihisi uhitaji wake mwenyewe “mimi nahitaji kubatizwa na wewe, unakujaje kwangu?” Jibu la Yesu linaonyesha jinsi ilivyo muhimu ya kwamba matakwa ya Mungu yatiiwe “Kubali hivi sasa, ya kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote” akajibu Yesu. Ingawa yeye binafsi hakuwa na dhambi, katka kubatizwa Yesu alionyesha kibali chake kwa utaratibu wa kwamba Mungu pekee ndiye mwenye haki na kwamba “mwili wote ni manyasi”
Sis, pia inatupasa kutambua utaratibu huu wa toka na kuwa peke yetu wenyewe hatuwezi kutenda lolote litakalotufanya tuwe wenye haki. Inatupasa tutoe usikivu kamili kwa neno la Mungu na
Jibu kutoka mbinguni (Mathayo 3;16-17)
Mara pakafuata, Yesus alipobatizwa dalili kuthibitisha ngzai yake kuwa ni Masihi. Roho wa Mungu akashuka juu yake (mst 16). Yohana alikuwa ameshaambiwa na Mungu ya kwamba hii ndiyo itakavyokuwa ishara ya kumtambulisha Masihi (yohana 1: 32-33). Hua hakuwa oeke ishara iliyotolewa, sauti kutokja mbinguni, pia ilitamka maneno “huyu ni mwanangu, ninayependezwa naye” (mst17) ndivyo ilivyoanza huduma ya mwana wa Mungu. Alijilishwa kwahivo kw aishara sisi zoweza kukosewa na maneno yaliyofuata hayakuachia shaka yoyote kuwa hapa alikuwepo Masihi wa Israeli.
Kujaribiwa jangwani (mathayo 4:1-11)
Yesu “alijaribiw akama sisi katika kilajambo, lakini bila dhambi” (Ebrania 4:15). Yesu alijalribiwa katika njia tatu ambazo huchipusha shambi, “tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima” (1Yohana 2:16). Alivishinda vishawishi hvi vyote vya mjaribu na hivyo alimheshimu Mungu katika bustani ya Edeni tamaa hizi hizi zilileta aguko la Adamu na Hawa.. hivyo Adamu wa pili alifanikiwa ambapo yule wa kwanza alishindwa. Kielelzo kifuatacho kinalinganisha matukio haya.
Majibu ya Yesu yote yalitokea kwenye kitabu cha Kumbukumbu la torati. Hili linatokeza ya kwamba Yesu alikuwa akifikiria mwana wa Mungu kitaifa, Israeli, na maonyo na mafundisho Musa aliyewapatia kwasababu walishindwa. Yesu alisikiliza masomo haya na kutokana na nguvu alizopata kwa Baba yake, alishinda madhaifu haya tuliyonayo sisi sote.
|
Yote yaliyomo duniani |
Anguko la Edeni |
Kujaribiwa kwa Yesu |
Jibu la Yesu kwa mjaribu |
|
Mwanzo 2 mst 16 “tamaa ya mwili” |
Mwanzo 3 mst 6 “mti ulikuwa mzuri kwa chakula” |
Mathayo 4 mst 2 “amrisha wawe haya yawe mkate” |
Mathayo 4 (mst 4) “mtu hataishi kwa makate pekee” |
|
“tamaa ya macho” |
“ukipendeza kwa macho” |
Mst 8 “akamwonyesha falme zote za dunia” |
Mst 10 “ utamwabudu bwana Mungu wako” |
|
“kiburi cha uzima” |
“mti unaotam,anisha kumpa mtu hekima” |
Mst 6 “ukiwa mwana wa Mungu jitupe chini” |
Mst 7 “usimjaribu Bwana Mungu wako” |
Yesu alikuwa katika mawasiliano ya karibu na Baba yeka anaye alikuwa amefunga siku arobaini usiku na mchana, hesabu hiii arobaini umaarufu wake, kwani inaweza kulinganishwa na muda wa kujaribu na kuangaliza (linganisha Hesabu 14:33 -34; Yoha 3:4 – 10).
Mjaribu alitaka Yesu konyesha ya kwamba kweli alikuwa mwana wa Mungu na kwamba angaliweza kuridhisha haja za mwili kwa kuyageuza mawe kuwa mikate. Lakini Yesu akakumbuka kuwa Mungu aliwafanya Israeli “kuteeka na njaa” (Kumbukumbu ya Torati 8:3) ili waweke tumaini lao kwa Yahwe na wala wasitegemee nguvu zao wenyewe. Zawadi ya Mungu ya nguvu ya roho kwa Yesu haikuwa ya makusudi ya kuridhisha tama binafsi. Akili ya Yesu ilijikita katika maneno ya Musa alipokumbuka ya kwamba Mungu aliwaongoza Israeli kule nyikani ili “awathibitishe kuona walichokuwa nacho moyoni mwao, iwapo wangalizitunza mari zake au la” kumbukumbu la Torati 8:2). Jibu
Mvuto wa kiburi cha maisha, jitupe chini kutokea juu ya hekalu (Mathayo 4:5-7)
Ndipo mjaribu alipojaribu mwelekeo tofauti, akamvuta Yesu kuonyesha ya kwamba alikuwa ndiye mwana wa Mungu kwa kuruka kutoka kwenye kilele cha hekalu na kuokulewa na malaika. Akinukuu Zaburi, mjaribu alisema “malaika wangalikuchukuwa ili usikwae mguu wako kwenye jiwe” (Zaburi 91:11-12). Mjaribu kwa kweli alipindisha Zaburi hii ili kukidhi wazo lake.
Yesu hakudanganyika.alifahamu ya kwamba Zaburi iliwekwa mipaka namna Mungu angalivyomlinda. Mwandishi wa Zaburi alisema ya kuwa ulinzi wa Mungu ulitolewa kwa sababu alikuwa maeweka imani kwa Mungu siyo katika njia ya uovu (Zaburi 91:2-4; 8-10) kutumia ulinzi huu kudhihirisha kiburi cha uzima ilikuwa kinyume na maana ya Zaburi hii.
Tena akili ya Yesu ilielekea kwa Israeli huko nyikani. Pale Musa na Meriba Israeli walikuwa na kiu ya maji na kuanza kunung’unika na kutia shaka kuhusu uwepo wa Yahwe. “Je Bwana yupo kati yetu au la?”(Kutoka 17:7)
Katika jibu
Mvuto wa tamaa ya macho. Utukufu wa falme(Mathayo 4:7-10)
Hatimaye mjaribu alisheheneza kwa macho ya Bwana utukufu wa tawala za ulimwengu akimuahidia kumpatia iwapo Yesu angelijitoa kwake. “Hizi zote nitakupa ikiwa utanipigia goti na kuniabudu” (mst 9). Yesu alikuwa na utukufu mbele yake lakini alijua ya kwamba msalaba ni budi uje kwanza, tenda hapakuwa na kusitasita katika uamuzi wake. Akakumbuka maneno yake Musa kwa Israeli ya kwamba Yahwe alikuwa amewapatia ushindi na kuwaleta katika nchi ya ahadi. Katika maana ya maneno ya Musa alijibu “Utamwabudu Bwana Mungu wako naye ndiyr pekee utakayemtumikia” (Mathayo 4:10, Kumbukumbu la Torati 6:13).
Sasa mjaribu akamwacha Yesu “kwa kipindi” na malaika wa Mungu wakaja “wakamtumikia”(mst 11), kwa matayarisho ya siku zilizokuwa bado hazijawadia.
Kushinda jaribu
Kumbukumbu ya jaribu la Yesu inaweza kutusaidia sisi katika juhudi zetu kushinda majaribu yetu wenyewe, yakobo anatukumbusha ya kwamba “kila mtu hujaribiwa anapovutwa mbali na tamaa yake mwenywe na kushawishika”(Yakobo 1:14-15). Mjaribu wakati alipokuja kwa Yesu, Bwana mara moja alifanya akili ya kujikita juu ya mafundisho ya Musa alikazia kwa Israeli kabla ya kufa kwake. Kutokana na kumbukumbu hii alipata nguvu na jibu kw aushawishi wa mjaribu. Pana masomo ya maana kwetu hapa. Njia ya kushinda jaribu ni kufikiria neno
Somo kwa ajili yetu
Ujumbe wa Yohana Mbatizaji ni kweli leo kama lilivyokuwa wakati ule watu leo wanaonyesha kiburi aina ile ile ya kimwili na kukataa kumgeukia Mungu kama watu walivyofanya muda wa Yohana. Katika hili tunaweza kuona kwa hakika ya kwamba “miili yote ni
Maktaba ya rejea
“Story of the Bible” (Dr. P. Mansfied) Vol 8, pages 69-89
“A life of Jesus” (M. Purkis) book 2, chapter 3, 4
“Nazareti Revisited” (R. Roberts) chapter 11
Maswali ya fungu
- Ni nini ilikuwa kazi ya Yohana Mbatizaji?
- a) Yesu alikuwa akionyesha nini kwa kupendelea kubatizwa?
b) Ni ishara gani zilionyeshwa na Mungu wakati wa ubatizwa wa Yesu?
- a) Eleza ile hali ya utatu wa majaribu ambayo yesu alikabili nyikani?
b) TUnashindaje majaribu? (Tunalishindaje jaribu?
Maswali ya insha
- Ni nini ilikuwa ujumbe wa Yohana Mbatizaji na waweza kutumika siku zetu?
- Ni kwa jinsi gani Yesu aliweza kushinda majaribu?
- Ni masomo gani twaweza kujifunza kutokana na mfano wake?