208. KUWAFUNDISHA WANAFUNZI WAKE
(iii) Namna ya kusali “salini namna hii…..”
Katika kuwafundisha wanafunzi wake kusali Yesu alionyesha kwa mfano wake yeye mwenyewe thamani ya kusali. Katika huduma yake nzito, Yesu wakati wote aligeukia kwa babaye wa mbinguni kwa nguvu wa uongozi. Wakipokea mfano huu bora wanafunzi walimwomba awafundishe jinsi ya kusali, ndiyo maana tunayo sala rahisi lakini yenye kina “sala ya Bwana” pia alionyesha katika mfano haja ya kusali buila kukoma, na tupangiliemarisha yesu katika mfano ukamilifu wa mtu was ala – Bwana Yesu mwenyewe.
Mathayo 6:5-15; luka 11:1-13; 18:9-14
Mfano wa yesu
Mwanzoni kabisa mwa huduma yake, Yesu anaonekana katika sala kwa baba yake,. Luka anaandika”ikatokea ya kwa Yesu naye baada ya ubatizo wakem akiomba, mbingu zilifunguka” (Luka 3:21). Hii ni ya kwanza ya nyakati nyingi za mwana wa Mungu akiwa katika sala. Shughuli yake isiyokoma ilipata nguvu katika nguvu ya sala. Kw ahiyo tutategemea ya kwmaba Yesu alichagua wanfunzi wake (mitume) na kazi yao ya sasa na siku za mbele akilini, aliomba kwa baba kwa mwongozo katika chaguo hili la maana. Hatuna budi kuguswa na ukweli kwamba “akaenda milimani kusali na akaendelea usiku kucha katika sala kwa Mungu”(Luka 6:12). Tena tunamuona Yesu akienda kwenye ukimya (utulivu) wa mlima kwa ajili ya sala ya tafakari baada ya kusikia juu ya kifo cha ukatili cha binamu yake Yohana Mbatizaji, na baada ya kuwalisha wale 5,0000.
Halafu palukuwapo matukio ambapo utulivu haukupatikana kwake. Lakini kuwepo kwa wanfunzi wake “hakukuzuia sala….. naye alipokuwa peke yake akiomba wanfunzi wake walikuwa naye” (Luka 9:18) wala hakushindwa kusali wakti akiponya wagonjwa, kama alivyoonekana kwa mfano wakati wa kumfufua Lazaro (Yohana 11:41-42). Kwa hiyo ni sawa ya kwamba nyakati za furaha kuuu kama alipogeuka (Alipobadilika) (Luka 9:39) na nyakati za huzuni kama ya binafsi,, kama katika bustani ya Gestemane (Luka 22:39-40), ya kwamba tunmwona mwana wa Adamu katika sala. Tafakari mateso yake ayle ambaye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu, yake ilikuwa kafara kamilifu lakini iliyotolewa kwa gharama kuu kwake mwenyewe, kama ilivyoelezwa kwa maneno ambaye katika siku zake za mwili, baada ya kutoa sala na maombezi kwa kulia na machozi mengi kw ayeye ambaye alikuwa na uwezo kumwokoakutoka kifo na akasikiwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu, ingawa alikuw amwana kasha alijifunza utiifu kw avile vitu alivyoteseka navyo” (Waebrabia 5:7-9)
Je vipi kwa wanafunzi? Mtume Paulo anawahamasisha kila mwanafunzi wa Kristo….” Katika kila kitu kwa sana na maombezi pamoja na shukurani haja zenu zijulikana na Mungu (Wafilipi 4:6)
SALA YA MANAFIKI (Mathayo 6:5-8)
Viongozi wa dini Wayahidi walikuwa wanafiki, ibada yao ya hadharani na mavazi yao walihamasishwa, siyo kwa kumpendeza Mungu, ila kwa hamu ya kusifiwa na wanadamu wenzao. Walikwenda hatua mbali sana kujionyesha kuwa wenye kuabudu. Ilikuwa ni gharama waliyokuw tayari kuilipa. Yesu alisema “wamepata thawabu yao” walipata sifa ya watu bali siyo sifa ya Mungu, ilikuwa tendo la bandia lenye unafiki bayana.
Yesu alionyesha kwa mfano wake yeye mwenyewe ya kwamba sala ilikuwa tendo la utegemezi kama mtoto, hisia ya upendo na tegemea lake kw ababaye wa mbinguni. Kwa hivyo wafuasi wake wangeelewa thamani ya kusali katika siri (faragha) wakifunga mlango nyuma yao katika ithbati ya binafsi wakimwaga mioyo yao kwa Mungu “aliye sirini, na baba yako aonaye sirini atawazawadia wazi wazi”. Kurudiarudia bila faida haikuwa muhimu kwa sana “baba yenu anajua yale ninayoyahitaji kabla hamjamuomba” moyo mwanifu unajua shukrnai na maombi rahisini tofauti kabisa kw awatu wanaojikiri watsikiwa kw akusema mengi kwao (linganisha Mhubiri 5:2)
SALA YA BWANA (Mathayo 6:9-13).
Luka anatuambia sisi kwamba Yesu alikuwa akisali wakati mmoja wa wanfunzi wake alivuviwa kusema “Bwamna tufundishe kusali….”(luka 11:11). Yesu alijibu kwa kuwapa mtindo was ala inayokubalika “kwa mtindo huu basi salini”mpango wake ni kama ifuatavyo:-
Upendo wetu kwa Mungu mst 9,10
Upendo wa Mungu kwetu mst 11-13
Uweza wa Mungu kutoa vitu uombavyo mst 13. Kwa kifupi hebu tufikirie sala hii, kifungu kwa kifungu,
“Baba yetu uliye mbinguni” ndicho kifungu cha kuanzia cha upendo kwa Mungu kwa imani ya kwamba anatuona sisi kuwa watoto wake, kupitia ubatizzo uhusiano huo ni wa uhakika na wa binafsi. Ni heshima iliaje basi kumsema muumba “Yahwe” Élohim” kuwa baba aliye mbinguni anaywaita watoto wke kumuabudu yeye katika utakatifu.
“Jina lako litukuzwe” ndiye msemo wa kumsifu unaokumbusha suala tufuku la wokovu uliomo ndnai ya jina Yahwe. Kulikutuza jina hilo ni kuzaheshimu zile karama za rehema na haki ambazo ndiyo msingi wa wito wa Mungu kuelekea ufalme wake.
“Ufalme wake uje” ndiyo tama yetu kuu ya moyo kuliko zote akili zetu zinarudi nymba kwneye ahadi iliyofanyika katika Edeni kwa Abrahamu, kwa Daudi na kw ategemeo na imani tunaomba utekelezaji wake, maana ndipo “mapenzi yako yatimie hapa duniani kam huko mbinguni” yatatimizwa. Ndipo utukufu wa Mungu utajaa dnianii, watu wtaabudu katika nyumba ya ibada (sala) kwa ajili ya mataifa yote na duniani amani na salama kwa watu wote. Iwapo tunataka kushiriki katika ufalme ule basi mapenzi yetu ni lazima yawe katika mstari mmoja na mapenzi yake Mungu, kwa mfano w aYesu mwenywe aliyesali (aliyeomba) “mapenzi yako yatimizwe”
“Utupe leo mkate wetu wa kila siku” inaonyesha kutegemea kwetu juu ya Mungu kutupatia mahitaji yetu hata katika dunia hii ambamo mwandamu anafikiri najitosheleza mwenyewe. Lakini Yesu anafundisha ya kuwa inatupasa kutosahahu cha kula cha kiroho , kusooma neno la Mungu kila siku.
“Utusamehe makosa / madeni yetu kama tunavyowasamehe wadeni wanaotukosea sisi” inamwoonyesha mwanfunzi kuwa iwapo ungesamehewa basi inapasa nawe tayri kusamehe wengine. Msamaha, kupitia ubatizo katika jina la Yesu kristo linalofunika dhambi,basi una uwajibikaji na masharti yake.
“Usitutie majaribuni bali tuokoe na maovu” ndicho kilio cha wmwanfunzi akitafuta ukombozi kutoka hatarini siyo kwmaba anaweza kutazamiwa kuw ahuru kutokana na majaribu kwnai yamewekwa kwa ajili ya kutakasa imani yake. Hii ni sala ya kufunguliwa na kulindwa. Ni wazi pia ya kwamba tahadhari inapasa ichjukuliwe kutokuangukia katika majaribu kwa uzembe wetu.
“kwa kuwa ufalme ni wako na nguvu, na utukufu, milele..”sala inamalizika (inafungwa na mkazo wa sifa, kama vile wa ufunguzu wafuga kwa makzo wa ushindi, ya kwamba hali na iwe vipi kwa mwanfunzi anaamini kw anguvu juu ya utukufu wake Mungu anayetawala katika utawala wa wandamu na hivi karibuni atafunua nguvu yake na utukufu. Kwa iamnai hiuo manafunzi wa Kristo atasema kwa nguvu “amina” au “na iwe hivyo” akikubali mapenzi ya mUngu katika kujisalimisha kwa mitihani na kushangilia juu ya mibaraka.
RAFIKI KATIKATI YA USIKU (Luka 1:5-13)
Katiak kifungu hiki Yesu anaongeza elekezo kubw asana la kusisimua juu ya sala. Anamuelezea mtu alikuwa na mgeni asiyetazamiwa saa sita usiku. Hakuwa na mkate (chakula) cha kumpatia na kulazimika kumwendea rafiki akimwomba msaada. Jibu lilikuwa kali “usinusumbue mlango sana umefungwa, na watoto wangu wamo kitandani na mimi siwezi kuamka na kukupatia” hilo halikumkatisha tamaa mgeni. Aliendelea kumwomba rafiki yake na mwishowe kukazana kwake kukamfaidisha.
Yesu aliueleza mfano kua somo katika majibu kwa sala. Anasema ya kwamba kwa hakika mUngu atatujibu “kuomba” Kwetu “kutafuta” kwetu na “kubisha” kwetu. Vile baba asingalifikiria kumpatia mwanawe jiwe wakati mkate unaombwa, wala nyoka badala ya samaki, au nge badala ya yai, hivyo hivyo baba yetu wa mbinguni atajibu na kuwapatia “vitu vizuri”(Mathayo 7:11) wao wamwombao.
Mfano huu hauna maana ya kuhusika katika kila kipengele kama Mungu, asionekana kama “rafiki” mlalamishi, avutaye miguu habari hii inalenga katika hali mbili halisi.
Haja ya ahraka yawatu kwa ajili ya msaada, na uwezo wa Mungu kukidhi haja ile.
Unaakzia uvumilia (subira) katika sala lakini tungaliweza kuongeza ya kwamba nyakati Fulani sala zetu hazijillaiwi kwa sababu sala zingine “zinaomba vibaya” (ona 1 Petro 3:12; Yakaobo 4:3, Zaburi 66:18: Isaya 59:1,2)
Somo kwetu
Mfano wa Yesu katika sala ntilie mkazo kwetu tegemeo lake kamili kwa baba yake kwa ajili ya nguvu na mwongozo. Alionya juu ya ibada ya unafiki na kuwafundisha wanafunzi wake kusali katika siri kwa Mungu ambaye atawapatia fadhila peupe. Kurudia rudia kwa ubatili siyo muhimu nayo ni dalili (ishara) ya “wapagani”. Baadaye inabainisha Mfarisayo na mtoza ushuru ambao wanatofautiana juu ya msimamo katika sala. Sala ya unyenyekevu unayotamkwa kimya kimya kwa imani itakubaliwa na Mngu nayo ndiyo inayopendeza zaidi kuliko Mungu kutusikia sisi na kutuongoza kwenye ufalme.
Kutuhamasisha sisi kushiriki katika imani ile ile ya sala, Yesu anatupatia “Sala ya Bwana” sala ya mfano kwa wanafunzi wote. Inaanza na kuisha kwa kumsifu Mungu na kuwemo maombi mafupi machache kw aajili ya msaada. Mungu anaahidi kusikia maombi ya watoto wake, akiwapatia “vitu vizuri” mibaraka sasa na katika enzi ijayo.
Maktaba ya rejea
“Making Prayer Powerful” (H.P.Mansfield)
“A life of Jesus” (M.Purkis) pages 102, 125, 144, 250
“Prayer”(M.Purkis and C. TENNANT) chapters 8 and 9
“The teaching of the master” (L. G. Sargent) pages 190 – 229
Maswali ya fungu
Tofautisha njia waliyotumia viongozi na kujahudi katika kusali na ile ya mfuasi wa kweli wa Kristo.
Ni masomo gani tujifunga kutokana na mfano wa Bwana yesu Kristo akiwa katika sala?
Kwa nini tunasali “ufalme wako uje” katika sala zetu?
Mfano wa rafiki saa sita usiku unatufundisha nini juu ya sala?
Maswali ya Insha
Onyesha namna “sala ya Bwana” ni kielelezo cha sala kwetu?
Eleza mfano wa rafiki ambaye mwanzoni hakutoa mkate alioombwa usiku saa sita, na unavyohusika na sala