How to use this Bible course - Lesson 01

Swahili

                                                                                    SOMO LA 1                                             

MASOMO YA BIBLIA YA KIKRISTADELFIA KWA NJIA YA POSTA

 

NAMNA YA KUITUMIA KOZI HII YA BIBLIA

                          

 

 

SOMO: Zaburi 19

 

Kozi hii imeandaliwa ili kukusaidia uweze kuielewa Biblia, ambayo ni Neno la Mungu. Biblia, ambayo pia huitwa “Maandiko”, ndio kitabu pekee kinachoweza kuaminika, kutuambia juu ya Mungu na mpango wake kwa dunia, na kwa watu wanaoishi juu yake. Inatoa ahadi ya mbaraka kwa kila mtu anayeisoma, akiwa na nia ya dhati ya kuielewa.

 

Utahitaji kuwa na Biblia yako mwenyewe

Ni fursa ya bahati kuwa na nakala ya Neno la Mungu. Ili kuifuatilia vizuri kozi hii, utahitaji kuwa na nakala yako mwenyewe ya Biblia yote (na sio Agano Jipya tu). Kama bado hujawa nayo, unaweza kupata moja kwa bei ambayo sio kubwa, kutoka kwenye tawi la karibu la Chama cha Biblia, au katika maduka ya vitabu. Karibu kila nchi ina tawi la Chama hicho. Lakini, kama hili haliko chini ya uwezo wako, tafadhali mwambie mkufunzi wako haraka; anaweza kukusaidia pengine kupata hata iliyotumika.

 

Masomo haya kwa njia ya Posta yana mada 60, moja kwa kila juma. Kama mkufunzi wako (mtu anayekutumia masomo haya) anaishi mbali na wewe, inawezekana kuwa utapata masomo kadhaa pamoja, pamoja na karatasi za maswali, pengine mara moja kwa mwezi. Mkufunzi wako ni:

 

 

 

 

 

 

 

Kumbukumbu yako itakuwa namba: ______________

Tafadhali utumie namba yako hii kwa mawasiliano yote, kwenye karatasi za majibu, n.k.

 

Tunakuomba utume majibu yako yote (na maswali uliyonayo) kwa mkufunzi wako. Ingekuwa vizuri zaidi umwandikie mkufunzi wako tu, hata kama unaona kuna anwani zingine kwenye machapisho yetu.

 

Kama utapenda pia kutumia Biblia ya Kiingereza, nukulu zilizowekwa  zipo katika Biblia ya Kiingereza ya  ‘Authorized Version’. Yapo machapisho mengine ya kisasa zaidi, kama ‘Revised Standard Version’ na ‘New International Version’, lakini yanaweza yasiwepo katika baadhi ya nchi. Hata hivyo yoyote ile utakayoitumia, utaona haitabadilisha maana au kuathiri kujifunza kwako Biblia.

 

Mafundisho haya tunayatoa bure. Gharama pekee utakayoingia ni kulipia gharama ya kutuma barua yako kwa mkufunzi wako, mara moja kwa mwezi. Lengo letu ni kukusaidia wewe kufurahia kuyasoma Maandiko, na tunatamani uweze kuugundua ujumbe wa maana sana na wokovu ulioko ndani yake, kupitia kwa Yesu Kristo. Hatutoi vyeti au hati yoyote kwa kuichukua kozi hii, ila mwishoni mwa masomo haya 60 tungependa bado tuendelee kukusaidia kuendelea kujifunza Biblia yako.

 

Rejea za Biblia

‘Rejea’ kutoka kwenye Biblia itakapokuwa imetolewa, itakuwa imeandikwa ifuatavyo:

 

Mwanzo 1 – hii ina maana ya Kitabu cha Mwanzo, Sura ya 1.

Mwanzo 1:1-7 ina maana ya Kitabu cha Mwanzo, Sura ya 1,  

                      mstari wa 1 mpaka wa 7 (mstari wa 7 unahusika).

 

Namna ya kujifunza masomo haya

Jizoeze kufanya mada moja kila juma. Tungeonelea uhakikishe unaielewa kila mada, kabla hujaendelea na nyingine inayofuata. Unaweza ukaona ni kitu cha manufaa kupitia kila mada mara tatu. Mara ya kwanza kwa kutaka kupata wazo la jumla la kile kinachosemwa, mara ya pili kwa kuifungua Biblia yako kwenye rejea zilizotolewa, na kuandika kwa kifupi kwenye kipande cha karatasi tatizo unaloliona au swali, na mara ya tatu kuisoma tena mada yote. Ni vizuri katika hatua hii kulisoma SOMO la Biblia lilitolewa mwanzoni mwa mada hiyo.

 

Mwishoni mwa kila mada utaona mistari ya manufaa ya kutazama kwenye Biblia yako, na Andiko moja tunalokutaka hasa kuliweka moyoni. Utaona kuwa, mistari hii itabakia kwenye kumbukumbu yako na itakusaidia katika maisha yako yote.

 

Pamoja na karatasi zako za mada za kwanza utakazopewa, utapewa pia na ‘Mpango wa Kujisomea Biblia wa Kila Siku’, tunaouita BIBLE READING PLANNER (kwa Kingereza). Kijitabu hiki kitakupa mfumo wa namna ya kusoma Biblia, kwa kusoma kifungu kimoja kila siku. Kama utakuwa na utayari wa kufanya hivyo, utapata ufahamu mzuri wa sehemu zote za Biblia baada ya muda.

 

Unaweza kupenda kuweka Mpango wako huo ndani ya Biblia yako, kwa ajili ya kuutumia wakati wa kusoma kila siku. Hili ni jambo jema. Kijitabu hiki kina maoni kinayokupa juu ya vifungu hivyo unavyosoma kila siku; na hasa ni muhtasari wa kile ulichosoma. Kina rejea za mistari mingine ya kwenye Maandiko, na ramani ndogo ndogo na michoro, inayoweza kukusaidia katika kujifunza kwako.

 

Kujibu maswali

Tunakutaka utume majibu yako kwa mkufunzi wako kila mwezi. Unatakiwa ujibu kwa kutumia maneno yako, usinakili tu kile masomo yalichosema. Jaribu kusema kile unachoamini mwenyewe kuwa kweli. Kama hukubaliani na chochote unachosoma, au una maswali yoyote, tafadhali sema hivyo; hili ni jambo la muhimu sana. Kumbuka, tunaweza kukusaidia zaidi kama tukiwa tunajua unachofikiri. Kama kwa sababu yoyote huwezi kutuma majibu yako, basi mwandikie tu mkufunzi wako   kumwambia unapenda kuendelea na masomo.

 

Matumizi ya muda

Kwa vyovyote, kujifunza huku kutakuchukulia sehemu ya muda wako, pengine dakika 15 au 20 kila siku kwa kusoma somo lako la Biblia, na kama nusu saa kwa kujifunza mada uliyopewa. Utahitaji pia muda wa kujibu karatasi za maswali. Hata hivyo utagundua kuwa, Maandiko yanavutia kiasi kwamba utahitaji kutumia muda wa zaidi na zaidi kuyapitia.

 

Soma Biblia yako kwa kuomba. Anza kipindi cha kusoma Biblia au kujifunza kwa kumwomba Mungu, ukiomba msaada wake uweze kuelewa. Hapa  kuna ombi fupi kutoka katika Kitabu cha Zaburi:

 

“Uyafumbue macho yangu niyatazame maajabu yatokayo katika sheria yako” (Zaburi 119:18).

 

Kama tukimwomba Mungu kwa dhati, atayafungua macho yetu na kutusaidia kukielewa kitabu chake hiki cha muhimu sana kwetu.

 

Kama hatutasikia kutoka kwako

Tuna hakika utakuwa unaelewa kuwa, kuna watu wengi duniani humu  wanaotamani kuipata kozi hii ya Biblia. Kama hatupati mwitikio wowote kutoka kwako, kwa wewe kututumia majibu ya karatasi za maswali ulizopata, tutachukulia kuwa huhitaji tena kuendelea kupata masomo haya na tutaacha kuendelea kuyatuma kwako.

 

Kama una matatizo yoyote katika kujibu, au katika kutuma karatasi zilizojibiwa, tafadhali wasiliana na mkufunzi wako umweleze. Itakuwa ni furaha kwetu kuendelea kukutumia masomo. Tunachohitaji tu ni kujua kama yanakufikia, na umekuwa ukiyatumia kukusaidia katika kujifunza kwako Neno la Mungu.

 

 

 

 

Kozi kamili ya Biblia:

Ifuatayo ni orodha ya mada ya kila somo, katika kozi hii ya masomo 60

 

  1. Namna ya Kuitumia Kozi Hii ya Biblia
  2. Wakristadelfia ni Watu Gani?
  3. Mwongozo Wetu Biblia
  4. Injili

 

Karatasi ya Maswali Na. 1

 

  1. Mungu na Uumbaji
  2. Mungu Aliupenda Ulimwengu
  3. Kurudi kwa Bwana Yesu Duniani
  4. Ishara za Kurudi kwa Yesu

 

Karatasi ya Maswali Na. 2

 

  1. ‘Ufalme Wako Uje’
  2. Mungu anavyoiona Historia
  3. Ufalme wa Mungu – Amani Duniani

 

Karatasi ya Maswali Na. 3

 

  1. Ahadi za Mungu  kwa Ibrahimu
  2. Wayahudi katika Historia (Sehemu ya 1)
  3. Wayahudi katika Historia (Sehemu ya 2)
  4. Ahadi za Mungu kwa Daudi

 

Karatasi ya Maswali Na. 4

 

  1. Baba na Mwana
  2. Maisha ya Yesu
  3. Kifo cha Yesu
  4. Ufufuo na Kupaa kwa Yesu Kristo

 

Karatasi ya Maswali Na. 5

 

  1. Roho Mtakatifu wa Mungu
  2. Karama za Roho Mtakatifu
  3. Dhambi na Matokeo yake (Sehemu ya 1)
  4. Dhambi  na Matokeo yake (sehemu ya 2)

 

Karatasi ya Maswali Na. 6

 

  1. Kwa Neema Mmeokolewa
  2. Ufufuo wa Wafu
  3. Hukumu
  4. Uzima wa Milele

 

Karatasi ya Maswali Na. 7

 

  1. Malaika
  2. Ibilisi, Mapepo, Shetani
  3. Ibilisi na Dhambi
  4. Ubatizo

 

Karatasi ya Maswali Na. 8

 

  1. Ndoa ya Kikristo
  2. Matatizo katika Ndoa
  3. Wajibu Wetu kwa Taifa
  4. Maombi
  5. Kutembea Katika Njia ya Uzima

 

Karatasi ya Maswali Na. 9

 

  1. Usomaji wa Biblia wa Kila Siku
  2. Ushirika na Walio wa Imani moja
  3. Uwezo wa Ulimi
  4. Kumega Mkate

 

Karatasi ya Maswali Na. 10

 

  1. Maisha ya Kifamilia katika Huduma ya  Yesu
  2. Tatizo la Dhambi
  3. Neno la Mungu katika Maisha yetu ya Kila Siku
  4. Kanisa la Mungu

 

Karatasi ya Maswali Na. 11

 

  1. Tunavyowafikiria Wengine ni Muhimu kwa Mungu
  2. Kumpenda Jirani Yako
  3. Biblia Inavyosema Juu ya Mateso
  4. Kuishi kwa Hofu

 

Karatasi ya Maswali Na. 12

 

  1. Ni Sahihi Kupenda Makuu?
  2. Uaminifu kwa Mungu na Mwanawe, Yesu Kristo
  3. Matumizi na Udhibiti wa Hasira
  4. Mfuasi na Nchi

 

Karatasi ya Maswali Na. 13

 

  1. Kufanya Mapenzi: zawadi kutoka kwa Mungu
  2. Kuchagua Mchumba
  3. Vipengere kuhusu Hukumu na Ufalme wa Mungu
  4. Zawadi ya Thamani Kubwa ya Tumaini katika Maisha yako

 

Karatasi ya Maswali Na. 14

 

  1. Imani na Kuufanyia Kazi Ukristo
  2. Neema ya Mungu
  3. Muhtasari wa Mafundisho ya Biblia
  4. Hatua Inayofuata

 

Karatasi ya Maswali ya Mwisho

 

 

 

 

Swahili Title
Namna ya kuitumia kozi hii ya Biblia - Somo la 01
Swahili file
PDF file
Arabic file
Status
Second Translation
African text
Christadelphian Bible Mission